Dereva wa basi la wachezaji wa timu ya Yanga ya Jijini Dar es Salaam, Maulid Kiula, (pichani) amefariki dunia leo alfajiri huko maeneo ya Ilala.
Taratibu za maziko zinaendelea kufanyika nyumbani kwa marehemu huko mtaa wa Chunya Ilala, Dar es Salaam.
Mungu iweke roho ya marehemu Maulid mahala pema peponi, Amen