Quantcast
Channel: SUFIANIMAFOTO
Viewing all articles
Browse latest Browse all 13053

*MKOA WA RUKWA KUJENGWA CHUO KIKUU

$
0
0
Mwenyekiti wa Sekretariati ya  Jukwaa  la Maendeleo  Mkoa wa Rukwa Bw.Joachim Sikulumbwe kushoto ,akiongea na  waandishi wa habari kuhusu mkakati wa kuanzisha chuo kikuu katika mkoa wa Rukwa  kulia ni Mjumbe wa Sekretariati JUMARU Bw.Titus Simsamba.(picha na Lorietha Laurence-Maelezo)



Jennifer Chamila-Maelezo
MKOA wa Rukwa  unatarajia kuanzisha chuo kikuu  ambacho kitasaidia vijana wengi wanaokosa nafasi za kuendelea na elimu ya juu kwa  kupata nafasi ya kujiunga na chuo kikuu.

Mkakati huo unaosimamiwa na  Jukwaa la Maendeleo Mkoa wa Rukwa(JUMARU) ambao ni halali chini ya sheria za nchi ilioanzishwa mwaka 2009 na wakazi wa mkoa wa Rukwa(Wanarukwa) kwa lengo la kuunganisha nguvu za wanarukwa wote  ili kuleta maendeleo katika mkoa huo na wakazi wake.

Akiongea na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam Mwenyekiti wa Sekretariati wa JUMARU Bw.Joachim Sikulumbwe amesema kuwa wameandaa kongamano la wanarukwa wote waishio jijini Dar es Salaam litakalo fanyika Septemba 01  mwaka huu,katika ukumbi wa Ubungo –Urafiki Social hall.

“Kongamano hilo litazungumzia  maliasili na rasilimali  za mkoa wa Rukwa na maendelao yake ,kiuchumi,kisiasa,kijamii na kiutamaduni nawaomba wanarukwa wajitokeze na kuhudhuria kwa wingi”alisema bw. Sikulumbwe,

Naye Makamo mwenyekiti kamati ya wahadhiri mchakato wa chuo kikuu  cha Rukwa bw.Bernard Kasimila amesema sababu ya kuanzisha chuo hicho ni kuwezesha vijana wenye sifa za kuendelea na masomo kupata fursa ya kujiunga na chuo kikuu.

Mkoa wa Rukwa ni sehemu ya Tanzania iliyoko nyanda za juu kusini  yenye wakazi zaidi ya milioni moja kwa sense ya 2012 , una  wilaya  3, halmashauri 4,tarafa 17,kata 64,na vijiji 202,unajishughuli zaidi na  kilimo,uvuvi na utalii.

 


Viewing all articles
Browse latest Browse all 13053

Trending Articles



<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>