Quantcast
Channel: SUFIANIMAFOTO
Viewing all articles
Browse latest Browse all 13053

*TANZANIA KUWA MWENYEJI WA TAMASHA LA SANAA NA UTAMADUNI

$
0
0
Na Anitha Jonas -  Maelezo, Dar es Salaam
TANZANIA inatarajia kuwa mwenyeji wa tamasha la sanaa na utamaduni litakaloandaliwa na Taasisi   ya (TaSUBa) iliyopo Wilayani Bagamoyo Mkoani Pwani kuanzia tarehe 22 hadi 28 Septemba mwaka huu.
Aidha Jumla ya vikundi 143 vya Tanzania vinatarajia kuonyesha kazi zao mbalimbali za sanaa katika tamasha hilo ambalo linatarajia kushirikisha jumla ya mataifa 8 kutoka Mabara ya Asia, Ulaya na Afrika.
Akizungumza na waandishi wa habari leo Ijumaa (Septemba 19, 2014) Jijini Dar es Salaam Kaimu Mtendaji wa TaSUBa Bw. Michael Kadinde aliyataja mataifa yanayoshiriki tamasha hilo kuwa ni Norway,Ujerumani, Korea, Uganda, Zambia, Burundi, New Zealand pamoja na Kenya.
Kalinde alizitaja kazi za sanaa zinazotarajiwa kuonyeshwa katika tamasha hilo kuwa ni pamoja na ngoma, muziki na vichekesho.
Naye Afisa Mkuu Idara ya Taaluma Bw. Gabriel Kiiza alisema kuwa Tamasha hilo linatarajia kukusanya watazamaji 10,000 kutoka katika nchi washiriki kwa malengo ya kutazama sanaa mbalimbali zilizoandaliwa kitaalamu kutoka kwa wanafunzi na wakufunzi wa mataifa husika.
“Nawaomba Watanzania wajitokeze kwa wingi ili waweze kuja kuona sanaa hizi zitakazowakilishwa na wasanii kutoka sehemu mbalimbali za dunia ili waweze kujifunza kupitia sanaa hizo”alisema Kadinde.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Tamasha na Mkufunzi wa Sanaa kutoka TaSUBa Bw. Abrahaman Bafadhili Bura ,aliongeza kuwa taasisi hiyo kwa sasa inapitia changamoto mbalimbali kama ikiwemo ukosefu wa fedha hivyo ametoa wito kwa Taasisi binafsi na umma kwa ujumla kuwapa ushirikiano katika kufanikisha tamasha hilo nchini.

Viewing all articles
Browse latest Browse all 13053


<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>