Mkuu wa Kanda ya Dodoma, ya Mradi wa Health Promotion and System Strengthening (HPSS) ambao pia unajulikana kama‘Tuimarishe Afya Project’, Prof. Manoris Meshack, akimkabodhi Ofisa Tawala Mkoa wa Dodoma, Rehema Madenge, Kabrasha la usimamizi wa Mfumo wa Uboreshaji Upatikanaji wa Dawa na Vifaa Tiba kupitia Mzabuni mmoja kwa Mkoa wa Dodoma. Wanaoshuhudia ni Naibu Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Mhe. Dkt. Steven Kebwe na Balozi wa Uswisi nchini Tanzania, Mhe. Balozi Olivier Chave. Hafla hiyo imefanyika hivi Karibuni katika hoteli ya New Dodoma, mjini Dodoma.
Naibu Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Mhe. Dkt. Steven Kebwe akizindua na Mfumo wa Uboreshaji Upatikanaji wa Dawa na Vifaa Tiba kupitia Mzabuni mmoja kwa Mkoa wa Dodoma, uliofanyika katika hoteli ya New Dodoma, mjini Dodoma hivi karibuni. Kushoto kwake ni Balozi wa Uswisi nchini Tanzania, Mhe. Balozi Olivier Chave, na Naibu Mtendaji Mkuu wa HPSS ya Uswisi, Dr. Karin Wieden Mayer, Wa kwanza kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Dr. Rehema Nchimbi.
Mkurugenzi wa Duka la Dawa la Bahari, akionyesha mkataba wa kuwa msambazaji pekee wa madawa kwa Mkoa wa Dodoma baada ya kushinda zabuni ya usambazaji wa madawa. Wanaoshuhudia ni Naibu Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Mhe. Dkt. Steven Kebwe na Balozi wa Uswisi nchini Tanzania, Mhe. Balozi Olivier Chave. Hafla hiyo imefanyika hivi Karibuni katika hoteli ya New Dodoma, mjini Dodoma.
Naibu Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Mhe. Dkt. Steven Kebwe akimpongeza Kaimu Mganga Mkuu Mkoa wa Dodoma, Dr. Zainab Chaula, mara baada ya Uzinduzi wa Mfumo wa Uboreshaji Upatikanaji wa Dawa na Vifaa Tiba kupitia Mzabuni mmoja kwa Mkoa wa Dodoma, uliofanyika katika hoteli ya New Dodoma, mjini Dodoma hivi karibuni. Kushoto kwake ni Balozi wa Uswisi nchini Tanzania, Mhe. Balozi Olivier Chave, na Naibu Mtendaji Mkuu wa HPSS ya Uswisi, Dr. Karin Wieden Mayer, Wa kwanza kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Dr. Rehema Nchimbi na Afisa Tawala Mkoa wa Dodoma, Rehema Madenge.
Naibu Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Mhe. Dkt. Kebwe Steven Kebwe akihutubia kwenye uzinduzi wa Mfumo wa Uboreshaji Upatikanaji wa Dawa na Vifaa Tiba kupitia Mzabuni mmoja kwa Mkoa wa Dodoma, uliofanyika katika hoteli ya New Dodoma, mjini Dodoma hivi karibuni.
Naibu Mtendaji Mkuu wa Mradi wa Health Promotion and System Strengthening (HPSS) ambao pia unajulikana kama‘Tuimarishe Afya Project’ Dr. Karin Wieden Mayer, akihutubia kwenye uzinduzi wa Mfumo wa Uboreshaji Upatikanaji wa Dawa na Vifaa Tiba kupitia Mzabuni mmoja kwa Mkoa wa Dodoma, uliofanyika katika hoteli ya New Dodoma, mjini Dodoma hivi karibuni.
Mkuu wa Kanda ya Dodoma, ya Mradi wa Health Promotion and System Strengthening (HPSS) ambao pia unajulikana kama‘Tuimarishe Afya Project’, Prof. Manoris Meshack, akihutubia kwenye uzinduzi wa Mfumo wa Uboreshaji Upatikanaji wa Dawa na Vifaa Tiba kupitia Mzabuni mmoja kwa Mkoa wa Dodoma, uliofanyika katika hoteli ya New Dodoma, mjini Dodoma hivi karibuni.
***************************************
By Pascal Mayalla
Tanzania imeipongezwa Uswisi, kwa mradi wa Health Promotion and System Strengthening (HPSS) ambao pia unajulikana kama ‘Tuimarishe Afya Project’unaofadhiliwa na serikali ya Uswisi, umepongezwa kwa kuwa ni moja ya miradi saidizi sana katika kuimarisha Afya kwa wananchi wa wilaya 7 za mkoa wa Dodoma.
Pongezi hizo zimetolewa na Naibu Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Dr. Kebwe Stephen Kebwe, wakati wa Uzinduzi wa Mfumo wa uboreshaji upatikanaji wa Dawa na Vifaa Tiba kupitia Mzabuni mmoja kwa Mkoa wa Dodoma hivi karibuni.
Naibu Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Mhe. Dkt. Steven Kebwe alisema HPSS, ambao wanasimamia mradi wa CHF iliyoboreshwa kwa mafanikio makubwa, wanaleta matumaini mapya katika usimamizi wa mfumo huu mpya ambao ni mzuri na utakuwa shirikishi kwani utahakikisha kuwa jamii inapata mahitaji sahihi ya dawa na pia watumishi wa sekta ya afya wanafanya kazi kwa bidii kwa lengo la kupambana na magonjwa nchini.
Waziri Kebwe, ameipongeza Mradi huu ambao ni sehemu ya ushirikiano kati ya Serikali ya Uswisi na Tanzania katika kuleta maendeleo na kuboresha afya za wananchi ambao umelenga kukabiliana na upungufu na dawa na vifaa tiba katika Hospitali mbalimbali ili kuboresha afya za wananchi kwa kuwahakikishia upatikanaji wa huduma za tiba zilizobora na za uhakika.
Kiongozi wa kikosikazi cha mradi huo HPSS kwa hapa nchini, , Profesa Manoris Meshack amesema kuwa tayari Kampuni binafsi ya Bahari Limited imeshachaguliwa kwa njia ya mchakato wa zabuni ambapo kampuni hiyo ndiyo itakayokuwa muuzaji mkuu, hivyo oda za dawa kutoka vituo vyote vya afya vya kila wilaya katika mkoa wa Dodoma zitanunuliwa kutoka kwa muuzaji mmoja yaani kutoka kwa muuzaji mkuu.
Naye Balozi wa Uswisi nchini Tanzania, Mhe. Balozi Olivier Chave aliupongeza ushirikiano uliopo kati ya Serikali ya Tanzania na Uswisi katika Nyanja mbalimbali za maendeleo. Amesema kusudio la mradi huu ni kuweza kuchangia katika jitihada za kuweza kufikia Malengo ya Maendeleo ya Milenia (MDGs) hasa malengo ya kupunguza idadi ya vifo vya watoto wachanga, afya ya uzazi, mapambano dhidi ya Ukimwi/VVU, Malaria, magonjwa mengine, afya ya mazingira, maji safi ya kunywa na kuboresha usafi wa mazingira.
Naibu Mtendaji Mkuu wa HPSS ya Uswisi, Dr. Karin Wieden Mayer, amepongeza jitihada za serikali ya Tanzania na uongozi wa mkoa wa Dodoma pamoja na uongozi wa serikali za mtaa wakishirikiana na mradi wa HPSS kwa kuanzisha mfumo wa kuwa na Muuzaji Mkuu (Prime Vendor) ni jambo la kujivunia na uwe mfano wa kuigwa kwa mikoa mengine nchini.
Mradi wa HPSS ulizinduliwa mwaka 2011 ukilenga kuusaidia mkoa wa Dodoma kwa kipindi cha miaka Kumi katika sekta ya Bima ya Afya, uboreshaji wa afya ya jamii, usimamiaji wa dawa na usimamiaji wa matengenezo ya vifaa vya afya, mradi huu umefadhiliwa na Ubalozi wa Uswisi nchini Tanzania na unatekelezwa na Shirika la The Swiss Tropical and Public Health Institute (Swiss TPH) likishirikiana na Shirika la Ujerumani la The Micro Insurance Academy (MIA) pamoja na Shirika la The Ifakara Health Institute la Tanzania.