Quantcast
Channel: SUFIANIMAFOTO
Viewing all articles
Browse latest Browse all 13053

*YANGA YAANZA KWA KICHAPO LIGI KUU, AZAM FC YACHANUA, MBEYA CITY YABANWA, STENDI YACHEZEA KICHAPO 4-1

$
0
0
TIMU ya Yanga ya jijini Dar es Salaam, leo imeanza vibaya mechi yake ya kufungua dimba la pazia la Ligi Kuu msimu huu wa 2014-2015 kwa kukubari kipigo cha mabao 2-0 dhidi ya Mtibwa Sugar, katika mchezo ulichezwa kwenye uwanja wa Jamhuri mjini Morogoro, leo jioni.

Katika mchezo huo, alikuwa ni Mussa Hassan 'Mgosi' katika dakika ya 15, alipowanyanyua mashabiki wa Mtibwa kwa kuifungia timu yake bao la kwanza kwa mpira wa kichwa akionganisha krosi murua iliyopigwa na Ame Ali.

Hadi timu hizo zinakwenda mapumziko baada ya kumalizika dakika 45 za kipindi cha kwanza Mtibwa Sugar walikuwa mbele kwa bao 1-0.

Aidha katika dakika ya 47, mshambuliaji wa Yanga, Mbrazil, Genilson Jaja, alikosa penati na kuwanyong'onyesha mashabiki wa Yaga.


Baada ya bao hilo, nyuki wakaingia uwanjani jambo lililosababisha wachezaji walale chini kwa dakika mbili, kabla ya wadudu hao kuondoka na mchezo kuendelea kana kwamba na wao walikuwa wakishangilia bao hilo la Mgosi.



Katika dakika ya 32 ‘Jaja’ alikosa bao la kuisawazishia Yanga baada ya kuunganisha mpira wa kichwa kona ya Haruna Niyonzima, lakini Hassan Ramadhani akaokoa ukiwa unaelekea wavuni.



Dakika ya 48, Simon Msuva aliyetokea benchi kuchukua nafasi ya Hamisi Kiiza ‘Diego’aliifungia Yanga SC bao, lakini refa akasema aliotea. Dakika ya 49 tena, Mrisho Ngassa alifunga bao lakini refa akasema aliotea pia.



Dakika ya 67, Simon Msuva alivamia langoni mwa Mtibwa na kutoa vitu vilivyokuwa chini upande wa nyavu kubwa na kukimbia navyo huku akikimbizwa na kipa Said Mohamed Kasarama kabla ya kuvitupa nje.



Dakika ya 82 alikuwa ni mtoa pasi ya bao la kwanza, Ame Ali aliifungia Mtibwa bao la pili baada ya kufanikiwa kuwahadaa mabeki wawili wa kati wa Yanga SC, Nadir Haroub ‘Cannaaro’ na Kevin Yondan kisha kumtungua Dida kufuatia pasi nzuri ya Hassan Ramadhani.



Yanga SC iliathiriwa na mabadiliko iliyoyafanya dakika za mwishoni kumtoa Mbuyu Twite aliyekuwa mhimili wa safu ya ulinzi na kuingiza mshambuliaji, Said Bahanuzi.
Kocha wa Yanga SC, Marcio Maximo ambaye alimfundisha kocha wa Mtibwa Sugar, Mecky Mexime alipokuwa Taifa Stars alikuwa mnyonge baada ya meci hiyo. 
Kikosi cha Mtibwa Sugar kilikuwa; Said Mohammed, Hassan Ramadhani, David Luhende/Majaliwa Shaaban dk64, Salim Mbonde, Andrew Vincent, Shaaban Nditi, Ali Shomary, Muzamil Yassin, Ame Ali, Mussa Mgosi/Vincent Barnabas dk50 na Mussa Nampaka/Dickson Daud dk72. 
Yanga SC; Deo Munishi ‘Dida’, Juma Abdul, Oscar Joshua/Omega Seme, Nadir Haroub ‘Cannavaro’, Kevin Yondan, Mbuyu Twite/Said Bahanuzi dk72, Hassan Dilunga, Haruna Niyonzima, Genilson Santana ‘Jaja’, Mrisho Ngassa na Hamisi Kiiza/Simon Msuva dk46. 


MATOKEO YA HUKO KWINGINEKO YALIKUWA HIVI:-
MTIBWA SUGAR 2- YANGA 0
AZAM FC 3- POLISI 1
MBEYA CITY 0- JKT RUVU 0
MGAMBO JKT 1-KAGERA SUGAR 0
STENDI UNITED 1- NDANDA FC 4
RUVU SHOOTING 0 TANZANIA PRISONS 2

Viewing all articles
Browse latest Browse all 13053

Trending Articles



<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>