Mfungaji mahiri wa magoli wa timu ya mpira wa pete Ikulu aliyecheza nafasi ya (G.S) Monica Kassy akiwania mpira dhidi ya wapinzani wao RAS Morogoro wakati wa mechi ya ufunguzi ambapo Ikulu walishinda kwa magoli 62 kwa11 dhidi ya wapinzani wao.
1. Baadhi ya wachezaji wa Timu ya Ikulu wakimsikiliza Mgeni Rasmi (hayupo pichani) wakati wa ufunguzi wa mashindano ya SHIMIWI taifa yanayoendelea mjini Morogoro.
1. Baadhi ya wachezaji wa timu ya Ikulu wakifuatilia mchezo wa mpira wa pete wanawake kati ya timu yao na wa wapinzani wao RAS Morogoro.
1. Baadhi ya watumishi wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo wakiwa kwenye maandamano siku ya ufunguzi wa mashindano ya SHIMIWI taifa yanayoendelea mjini Morogoro.
**********************************************
Na Eleuteri Mangi- MAELEZO
Timu za Ikulu zimeanza vema mashindano ya Shirikisho la Michezo ya watumishi Wizara na Idara za Serikali (SHIMIWI) kwa kuendeleza ushindi na kung’ara katika mashindano hayo yanayoendelea mjini Morogoro.
Timu hizo zimeanza mashidano hayo kwa ushindi wa kishindo siku ya ufunguzi katika mchezo wa mpira wa pete kwa wanawake na timu ya kuvuta kamba wanaume.
Ikulu imeanza kwa ushindi katika michezo hiyo waliyoanza dhidi ya wapinzani wao ambao ni Timu ya watumishi kutoka Ofisi ya RAS Morogoro kwa mpira wa pete na timu ya Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa kwa mchezo wa kuvuta kamba.
Ushindi huo walioupata Ikulu katika mpira wa pete wanawake wa magoli 62 waliongozwa na mfungaji wao mahiri Monica Kassy aliyecheza nafasi ya ufungaji (G.S) kwa magoli 11dhidi ya wapinzani wao.
Kwa upande wa timu ya kuvuta kamba wanaume ilishinda wapinzani wao kwa kuwavuta mizunguko yote miwili.
Kwa kudhihirisha ubora wa timu yake Mwalimu wa Mpira wa pete kwa timu ya Ikulu Bi. Mary Protas alisema kuwa kwao ushindi ni wa lazima maana wao ndio mabingwa watetezi.
“Ni lazima kutetea ubingwa wetu na ushindi ni lazima kwetu kwa mechi zote tunapocheza na timu pinzani dhidi yetu” alisema mwalimu Mary.
Aidha, mwalimu huyo hakubeza timu pinzani watakaocheza nao na kuwataka wajiandae vizuri kwani kwao ushindi kwao ni muhimu na kuwapelekea kutetea ubingwa wao na kurudi na kombe kazini mara baada ya mashindano.
Kwa upande wake mwalimu wa mpira wa pete timu ya Ofisi ya RAS Morogoro Bw. Oliver Nambunga amesema kuwa timu yake imejitahidi kadiri ya uwezo wao licha ya kuwa ni changa na ni wageni katika mashindano hayo ya kitaifa na kuahidi watajitahidi kufanya vizuri katika mechi zinazofuata.
Mashindano ya SHIMIWI kitaifa mwaka huu yanajumla ya timu 54 zinazoshirikisha ambapo zimeongezeka timu tatu washiriki tofauti na mwaka jana wakati zilishiriki timu 51 katika mashindano hayo yalipofanyika mjini Dodoma.