Wananchi waliokuwepo eneo la Ubungo leo mchana wamemshambulia askari wa usalama barabarani kwa kile walichodai kuwa amesababisha ajali. Watu hao walianza kumshambulia askari huyo huku wakimtwanga mangumi na kumchania sare yake ya kazi kama anavyoonekana pichani.