Mabondia Francis Miyeyusho wa Tanzania (kulia) akitunishiana misuli na bondia Fidelis Ipupa wa Zambia, wakati wa zoezi la kupima uzito kwa ajili ya pambano lao la Kimataifa litakalofanyika kesho kwenye Ukumbi wa Dar Live, jijini Dar es Salaam.
Mabondia hao, wamewaongoza mabondia wengine waTanzania watakaopanda ulingoni kesho katika mapambano ya utangulizi
Zoezi zima la upimaji liliongozwa na Katibu Mkuu wa ngumi za kulipwa, Ibrahim Kamwe, akisaidiwa na Dkt. Madono.
''Mabondia wote waliopima wapo vizuri kwa mapambano yao ambapo Francis Miyeyusho, amepata Kg 55.5 na mpinzani wake Fidelis Ipupa, amepata Kg 56 na Ramadhan Kido wa Dare s salaam amepata Kg 89.7 na mpinzani wake Kg 90.2.
Aidha kutakuwepo na mapambano mengine manne ya utangulizi na mabondia wameuwiana vema na wale kina dada esther na lulu watazichapa kama kawaida''. alisema Kamwe.
Bondia Ramadhan Kido, akipima afya.