Mtandao huu wa www.sufianimafoto.com, unawatakia Sikukuu njema ya Eid El Fitri, wadau wote wa mtandao huu. Tusherehekee kwa amani na utulivu na kuyafuate yote yaliyoamrishwa na Mwenyezi Mungu na kuendelea kuyakataa yale yote yaliyokatazwa, Inshaallah. Na pia tuuenzi mwezi huu kama mwalimu mzuri kwa kuendelea kutenda mema na kuyaacha yote tuliyoyaacha ndani ya huu mtukufu wa Ramadhan na kesho ni Mwezi Mosi Shawwal 1434, Sikukuu iliyotukuka kwa Waumin wote wa Kiislam. MUNGU ATUJAALIE KUYAACHA MABAYA YOTE TULIYOYAACHA KIPINDI CHA MWEZI MTUKUFU WA RAMADHAN, NA ATUONGOZE KUENDELEA NA MEMA, AMINA INSHAALLAH
↧