Quantcast
Channel: SUFIANIMAFOTO
Viewing all articles
Browse latest Browse all 13053

*CHANZO CHA MAJI IKORONGO NDIYO MKOMBOZI WA MJI WA MPANDA

$
0
0
 Wakaguzi wa miradi ya maendeleo kutoka Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango wakiangalia chanzo cha chemichemi ya maji cha Ikorongo kilichoko kilometa 13.2 kutoka Mpanda mjini. Chanzo hicho kina uwezo wa kutoa maji ya kutosha mji wote wa Mpanda.
************************************
Na Mwandishi wetu, Katavi
Chanzo cha maji cha chemichemi ya Ikorongo ambacho ni cha asili kipo kilometa 13.2 kutoka Mpanda mjini, mkoani Katavi. Chanzo hiki cha maji kinazungukwa na miti na uoto wa asili unaolinda maji hayo yawe safi na salama kwa matumizi ya binadamu.
Mhandisi wa Maji wa Mkoa wa Katavi Magdalena Mkeremi anasema chanzo hiki cha maji ni chemichemi yenye maji masafi yasiyokauka hata wakati wa kiangazi.
Chanzo hiki kina uwezo wa kuzalisha zaidi ya lita milioni sita kwa siku.
Mradi wa maji wa Mji wa Mpanda ni wa gharama nafuu kwa sababu hautumii pampu ya aina yoyote bali maji husambazwa kwa njia ya mserereko (gravity).

Bomba kubwa la maji la inchi kumi limelazwa kutoka kwenye chanzo na kupelekwa Kazima kwenye tanki kubwa la ujazo wa lita milioni moja ambalo limejengwa eneo la kilometa 13 kutoka kwenye chanzo cha maji.  Vile vile  maji kutoka kwenye tanki hilo na kwenda mjini na katika mitaa au vijiji pia hutumia mserereko hivyo, kurahisisha gharama zake.

Mradi huo wa maji wa vijiji kumi au mitaa kumi ya mji wa Mpanda unagharamiwa na Serikali ya Tanzania kwa kushirikiana na Benki ya Dunia chini ya mfumo wa Matokeo Makubwa Sasa.
“Maji yalikuwa tatizo kubwa hapa kwetu lakini ujio wa mradi huu umerahisisha upatikanaji wa maji mjini na kwenye mitaa ya mji wa Mpanda,” anasema Mhandisi.

Tayari vimejengwa vituo vya kuchotea maji 41 katika mitaa kumi na watu binafsi wapatao 300 wameunganishiwa maji kupitia chanzo hicho cha maji.
Amesema mradi huo umetekelezwa kwa muda wa miaka mitatu tangu 2012/13 -2014/15 ambapo umekamilika mwezi Septemba 2014.

Amesema ili kuufanya mradi huo kuwa endelevu wamejenga nyumba ya mlinzi ili kulinda chanzo hicho cha maji kisiharibiwe kwa namna yoyote ile ikiwa ni pamoja na kulinda mazingira yanayozunguka eneo hilo.

Viewing all articles
Browse latest Browse all 13053

Trending Articles