Kutokana na mambo kutokaa sawa kuhusu mjadala unaoendele mjini Dodoma kuhusu sakata la fedha za Escrow, kikao hicho cha Bunge kimehairishwa kwa mara ya pili leo.
Baada ya kuahirishwa kikao hicho sasa kinatarajia kukaa tena saa kumi jioni ili kutoa muda kwa kamati kuendelea kusaka maridhiano, ili Bunge litakapokutana jioni liweze kufikia muafaka bila kuwepo na mivutano.
Mh Spika Anne Makinda amefikia uamuzi huo baada ya kuombwa bunge kuahirishwa kwa saa moja na Waziri wa Nchi, Mh William Lukuvi ili wabunge wa CCM waweze kukutana na kuafikiana ili bunge likapokaa tena waweze kuwa na maamuzi.
Hata hivyo Mh Zitto Kabwe yeye aliomba masaa mawili, Mh Mbatia akaomba wapewe muda zaidi, na katika kuhitimisha, Mh Spika akatoa maamuzi na kusema bunge litakutana saa kumi jioni.
ZITO ATAJA MAJINA YA WANAOTAKIWA KUINGIA KAMATI YA KUANDIKA MAAZIMIO YA KUWAWAJIBISHA WATUHUMIWA WA TEGETA ESCROW.
![]()
ZITO ATAJA MAJINA YA WANAOTAKIWA KUINGIA KAMATI YA KUANDIKA MAAZIMIO YA KUWAWAJIBISHA WATUHUMIWA WA TEGETA ESCROW.
