Mpiga drams maarufu nchini, aliyepata kupiga kazi na bendi Extra Bongo, Martine Kibosho, ambaye ni ndugu moja na mpiga drams wa bendi ya African Stars 'Twanga Pepeta', James Kibosho, anazidi kung'ara huko umangani, ambapo kwa sasa yupo jijini Paris Ufaransa akipiga kazi na kundi la Vipaji Band kwa mkataba wa miezi mitatu.
sehemu ya steji anayopiga kazi Kibosho.
Mpiga bass mahiri ambaye pia ameungana na kibosho katika bendi hiyo, aliyewahi pia kupiga kazi katika bendi ya African Stars, Tanga Pepeta, Kado Bass akiwajibika katika shoo hiyo inayopigwa mara tatubkwa siku, ambapo mashabiki hulipa na kuingia kushuhudia shoo ikiisha wanatoka na kuingia wengine kwa kiingilio kipya. Shoo hiyo hupigwa kwa masaa matatu matatu.
Sehemu ya mashabiki waliohudhuria moja ya shoo.
Martine Kibosho akiwajibika.....kuzikaanga chips.