*****************************************************
Na Mwandishi Wetu, Dar
MABONDIA Ibrahimu Class 'King Class Mawe' na Simba Watunduru wametambiana kiasi cha kutaka kukiuka miiko ya mchezo wa masumbwi walipotaka kuchapana makonde kavu kavu mbele ya Rais wa TPBO Yassini Abdallah 'Ostadhi' wakati wa zoezi la utiaji saini mkataba wa makubaliano wa kupambana katika pambano lao la kirafiki litakalochezwa kwenye Ukumbi wa Diamond Jubilee Agost 30, mwaka huu.
Mabondia King Class (kushoto) na Simba wa Tunduru, wakitunishiana misuli wakati wa zoezi hilo.
Rais wa TPBO LIMITED Yassini Abdallah 'Ostadhi' akimkabidhi, mkataba wa makubaliano bondia Ibrahimu Class 'King Class Mawe' baada ya kutia saini katika ofisi za TPBO LTD Dar es salaam. |
Rais wa TPBO Ltd, Yassini Abdallah 'Ostadhi' akimkabidhi mkataba wa makubaliano bondia Simba Watunduru baada ya kutia saini katika ofisi za TPBO LTD Dar es salaam. |