Quantcast
Channel: SUFIANIMAFOTO
Viewing all articles
Browse latest Browse all 13053

*BAKWATA YATAKA TUKIO LA KYELA LIFANYIWE UCHUNGUZI

$
0
0
NA JENNIFER CHAMILA – MAELEZO

BARAZA   Kuu la Waislam Tanzania (BAKWATA) limeviomba vyombo vya dola kuendelea kufanya uchunguzi  kuhusu tukio la kuvamiwa,kupigwa na kujeruhiwa kwa Imamu na waumini wa Kiislamu wakiwa msikitini wakati wa swala ya Idd-el-Fitri iliyofanyika katika Msikiti Mkuu wa Wilaya ya Kyela mkoani Mbeya na  kuhakikisha.

Aidha  baraza  hilo limesikitishwa   na kitendo  hicho, na kuvitaka vyombo hivyo kuhakikisha kwamba wahalifu wote wanafikishwa mbele ya sheria.

Kwa mujibu wa   taarifa iliyotolewa leo kwa  vyombo vya habari  na Mufti wa Tanzania Sheikh Issa Simba, imelaani kitendo hicho na kusema watu waliofanya kitendo hicho wamegeuka maagizo ya ya Qur’an Tukufu pamoja na Sheria za Nchi.

 “BAKWATA imewataka wananchi wote kufuata taratibu sahihi jambo lolote linapo tokea.”Kama yupo mtu yoyote ana manung’uniko au hoja yoyote dhidi ya mwenzake au taasisi yoyote,ni lazima watumie taratibu sahihi za kidini au za kisheria na sio kuchukua sheria mkononi”alisema Sheikh Issa.

 Alisema baraza hilo   linamuomba Mwenyezi Mungu awaponye  watu wote waliathirika  na tukio hilo.

Viewing all articles
Browse latest Browse all 13053

Trending Articles



<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>