NA ELEUTERI MANGI- MAELEZO
BENKI ya Barclays Tanzania imechezesha droo yake ya tatu na ya mwisho kwa kampeni ya “Maisha bomba na Barclays Golden Briefcase” kwa wateja wake ambapo wateja 13 wamepata fursa ya kujishindia masanduku 13 ya dhahabu ya kila mwezi kwa muda wa miezi mitatu.
Hayo yamesemwa na Kaimu Mkurugenzi wa banki ya Barclays, Kitengo cha wateja binafsi Bw. Musa Kitoi alipokuwa akiongea na waandishi wa habari leo jijini Dar es salaam Kaimu Mkurugenzi Kitoi alisema “Fursa ya ushindi ilikuwa wazi kwa kila mteja waliopo na watarajiwa wenye akaunti na banki ya Barclays Tanzania,”
“Leo tumekamilisha droo yetu ya tatu na tumepata washindi kumi na watatu,”alisema.
Miongoni mwa washindi waliopoatikana katika droo hiyo ni Holline Hemedi Membi, Walter Julius Mushi, Mozer I. Mohamed, Robert Donart Magesa, Hemed Rashid Hemed.
Wengine ni Bi Azida Bakari, Freda Temba, Bi Sultan Manji, Salum Abdala Nassoro, Bi Azah Sultan, Abdalah Mohamed Hamisi na Hilary Samwel Kwayu.
Aidha Banki ya Barclays imetoa zawadi kwa washindi wa droo ya pili iliyofanyika Juni 18, 2013 ambapo kulikuwa na masanduku 13 ya dhahabu. Kila mteja mshindi alichagua na kufungua sanduku na kujua zawadi yake.
Washindi wa droo ya pili waliokuwepo na kukabidhiwa zawadi zao ni Nabila Khan aliyejishindia i- Pad, Martha Hewison amejishindia mashine ya kufulia, Dkt. Kunda John na Darvish Bhatt kila moja alijishindia vocha ya ya thamani ya shilingi 200,000.
Kwa upande wake mshindi wa i- Pad alisema kuwa amefurahi sana kupata zawadi hiyo kwani ilikuwa ni ndoto yake aliyotamani kujishindia na amemshukuru Mungu kwa ndoto yake kutimia.
Naibu Mkurugenzi Kitoi aiongeza kuwa mmoja kati ya washindi waliochaguliwa leo atakuwa mshindi wa jumla na atajishindia kitita cha shilingi za Kitanzania milioni kumi tasilimu.
ha
Kampeni hii ilizinduliwa rasmi Aprili 11, 2013 na Banki ya Barclays Tanzania itaend3elea kuwa na kampeni nyingine inayotarjiwa kuanza hivi karibuni ambayo itawawezesha wateja wetu kujishindia zawadi mbalimbali.