Quantcast
Channel: SUFIANIMAFOTO
Viewing all articles
Browse latest Browse all 13053

*KAMUHANDA AMFAGILIA JAKAYA KIKWETE KWA UTEUZI WA VIONGOZI WA WIZARA YA HABARI 'MAJEMBE'

$
0
0
NA MAGRETH KINABO – MAELEZO
ALIYEKUWA Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Seith Kamuhanda  amempongeza Rais  Jakaya Kikwete kwa kuwateua viongozi ambao ni majembe (wachapakazi) kuiongoza wizara hiyo  huku akisema  ni watendaji wenye uwezo wa  hali ya juu.

Viongozi walioteuliwa kuongoza wizara hiyo ni Sihaba Nkinga ambaye ni Katibu Mkuu wa sasa na Naibu Katibu Mkuu wake ni Profesa  Elisante  ole Gabriel  Laizer. 

Kauli hiyo imetolewa leo na  Kamuhanda wakati akiwaga viongozi wa wizara hiyo ambapo  pia aliwasisitiza kuendelea kufanya kazi kwa ushirikiano ili kuhakikisha huduma wanazozitoa  kupitia  sekta za habari, vijana, utamaduni na michezo  zinawafikia wananchi.

“Leo ni siku ya furaha kwangu kwa sababu ninaacha majembe mawili ya uhakika.  Ninawaomba mwuwape ushirikiano ili walime vizuri. Ni wizara ngumu kwa sababu inagusa Watanzania  wote   ,”alisema. 

Kwa upande wake Katibu Mkuu wa sasa Sihaba alisema   anamshukuru Kamuhanda kwa kumfundisha kazi katika maeneo mbalimbali ya sekta za wizara hiyo.

  “Nimekaa katika kiti hiki bila ya yeye nisingeweza kukaa katika kiti hiki  bado ataendelea kuwa msaada kwangu kwa kuwa wizara inagusa jamii ,” alisema  Katibu Mkuu Sihaba huku akimwomba aendelee kutoa msaada katika wizara hiyo.

 Aidha  Katibu Mkuu huyo alisema atajitahidi kuongoza wizara ili iendelee kuwa watoto wa familia moja kama ilivyoachwa na Kamuhanda. 

Naye Naibu Katibu Mkuu  Profesa Laizer  alisema   anamshukuru Kamuhanda kwa ushirikiano aliowapo ,pia aliongeza kuwa kufanya kazi kwake vizuri kutokana na ushirikiano huo ukiwemo wa wakurugenzi ,viongozi wa taasisi na watumishi wa wizara hiyo. 

“Kazi kubwa  niliyonayo ni kumsaidia Katibu Mkuu. Nitawasaidia ili tupate Matokeo Makubwa Sasa. Tutajitahidi tusikuangushe,” alisisitiza Profesa Laizer huku akisema wao ni majembe lakini yeye ni shoka na ametoka katika wizara hiyo kwa heshima.

Akitoa neno la shukurani kwa niaba ya menejimenti ya wizara hiyo Profesa, Hermans Mwansoko  alimpongeza Kamuhanda kutokana na utendaji kazi wake wakati akiiongoza,ambapo alisema ameiacha katika hali ya umoja na mshikamano huku akiwajali watumishi hususan wa ngazi za chini.

Viewing all articles
Browse latest Browse all 13053

Trending Articles



<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>