MSANII wa Filamu nchini Elizabeth Michael 'Lulu' ameonyesha kipaji chake kwa kuimba vyema wimbo wa YAHAYA wa Nguli wa muziki wa Kizaki kipya Lady Jay Dee, na kutunzwa mijihela wakati akiimba wimbo huo na Jide kwenye uzinduzi wa Video yake mpya na ya kwanza kusimama peke yake ya FOOLISH AGE.
Baada ya move hiyo kali ya dakika 120 iliyoonyesha ukali wa staa huyo kuoneshwa kwa dakika 20 tu na kubakisha zingine 100 kusubiri wateja kuziona majumbani kwao alipanda jukwaani kujitambulisha na kutoa shukrani kwa wapenzi na mashabiki wa tasnia ya filamu nchini Tanzania kwa muitikio wao ambapo alipanda na kuimba wimbo huo wa Yahaya.
Lulu alianza kwa kuimba kiitikio cha wimbo huo akiwa Back Stage, na kuwashangaza watu pale alipomudu vyema wimbo huo kiasi cha mashabiki ‘Mapedeshee’ wakiongozwa na Pedeshee Rich Rich, kupanda jukwaani na kumtunza fedha kibao ambazo hakika zilimpagawisha msanii huyo na mwisho wa wimbo huo alitamka kuwa kweli muziki unalipa.
“Jamanieee kumbe muziki unalipa ile mbaya yaani nimeimba ubeti mmoja tu hapa ona mijihela kibao, kuanzia sasa na mimi nitaanza kuimba muziki”, alisema Lulu, huku akishangiliwa na mashabiki wake.
Uzinduzi wa filamu hiyo ya kiswahili ambayo ina sub title ya Kiingereza na ambayo haipaswi kuangaliwa na watoto chini ya miaka 16, huku ikiwa imechezwa na wasanii maarufu na wakongwe kama Elizabeth Michael mwenyewe, Diana Kimaro, Hashim Kambi, Ombeni Phiri na Mzee Jengua ulifanyika usiku huu kwenye ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es Salaam. KWA MATUKIA ZAIDI BOFYA HAPO CHINI
Wasanii mbalimbali walihudhuria show hiyo usiku huu pale Mlimani City. Picha kwa hisani ya Father Kidevu Blog.
Lulu akizungumza machache mara baada ya Move yake hiyo kuoneshwa kwa mashabiki na wapenzi wa filamu Tanzania ndani ya Ukumbi wa Mlimani City.
Wadau walifuatilia burudani...
Jide akikamua jukwaani...
Mama na mwanao ni kama chanda na Pete... huyo ni Natasha (kulia) na Bintiye Monalisa.
.... Walitunzana tu kivyao vyao...
noti alizo tuzwa Jide...
Rich Rich akimwaga noti
Wadau wakifuatilia uzinduzi huo wa Filamu.
Furaha ilitawala
Mwogozaji wa Filamu za Kibongo, Leah Mwendamseke nae alikuwepo kuangalia kazi hiyo ya Lulu.
Waongoza Shughuli hiyo watangazaji wa Redio na TV Double G na mwana dada kutoka Times FM walikuwepo.