Quantcast
Channel: SUFIANIMAFOTO
Viewing all articles
Browse latest Browse all 13053

*BENKI YA NBC YAFURAHI NA NA WATEJA WAKE KWENYE UZINDUZI KITENGO CHA PRIVATE BANKING SUITE

$
0
0
  Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya  NBC Tanzania, Mizinga Melu akizungumza katika hafla iliyoandaliwa na benki hiyo baada ya uzinduzi wa kitengo cha Huduma Binafsi za Kibenki kwa Wateja Wakubwa cha NBC jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki. Kitengo hicho kipo katika Jengo la Coco Plaza karibu ya ufukwe  wa Coco Beach.
 Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Harry Kitillya (kulia) akisalimiana na Meneja wa Tawi la NBC Sea Cliff, Mariam Kombo katika hafla hiyo jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki. Katikati  ni Mkurugenzi Mtendaji wa NBC, Mizinga Melu. KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPO CHINI

 Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Harry Kitillya (kulia) akisalimiana na Mkuu wa Idara Huduma za Kibenki kwa Wateja Wakubwa na Uwekezaji  wa Benki ya NBC, Andre Potgieter katika hafla iliyoandaliwa na benki hiyo baada ya uzinduzi wa kitengo cha Huduma Binafsi za Kibenki kwa Wateja Wakubwa jijini Dar es salaam mwishoni mwa wiki. Kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa NBC, Mizinga Melu na wa  pili (kulia) ni mteja wa benki hiyo, Paul Chizi.
 Mkuu wa Kitengo cha Huduma Binafsi za Kibenki kwa Wateja Wakubwa cha NBC, Andrew Massawe akizungumza katika hafla hiyo. Pamoja naye ni baadhi ya maofisa katika kitengo hicho cha wateja binafsi wakubwa.
 Ofisa Mwendeshaji  Mkuu wa Benki ya NBC, Maharage Chande (kushoto) akisalimiana na mmoja wa wateja wa benki hiyo, Paul Chizi katika hafla hiyo. Wengine katikati ni  Mkuu wa Idara Huduma za Kibenki kwa Wateja Wakubwa na Uwekezaji  wa Benki ya NBC, Andre Potgieter na Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Harry Kitillya.
 Mmoja wa wateja wa NBC, Paul Chizi akiipongeza Benki ya NBC kwa jitihada za kuanzisha kitengo maalumu cha kuhudumia wateja wakubwa  (Private Banking).
Wasanii wa kikundi cha sarakasi cha  Mama Afrika wakitoa burudani katika hafla hiyo.

Viewing all articles
Browse latest Browse all 13053

Trending Articles



<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>