Quantcast
Channel: SUFIANIMAFOTO
Viewing all articles
Browse latest Browse all 13053

*BALOZI IDD AYAONYA MATAIFA KUTOUPOTOSHA UMMA KUHUSU ZANZIBAR

$
0
0


Wananchi wakiwa katika shughuli zao za kujitafutia kipato cha kila siku, maeneo ya Soko Kuu la Zanzibar almaarufu kama Malkiti ya Darajani.

Makamu wa pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Iddi, ameyataka mataifa kuacha kupotosha ukweli wa hali ya usalama wa Zanzibar na vitongoji vyake.
Akizungumza katika Mahojiano maalum ofisini kwake kuhusu mustakabali wa hali ya Kisiasa ilivyo Visiwani humo, alisema kuwa watu wengi wamekuwa wakiongea uongo na kuupotosha Umma, jambo ambalo si zuri,  wakati hali ya Zanzibar na wananchi wake wametulia na wananendelea na shughuli zao za kila siku.
Aliongeza kuwa hakuna machafuko yeyote ndani ya Visiwa hivyo, na watu wanaendelea kuchapa kazi wakisubiri siku itakayotangazwa ili kurudiwa kwa uchaguzi ili Viongozi pia waanze kufanya kazi ya kuwatumiakia wananchi wao.

Katika mitaa ya mji wa Zanzibar wananchi wanaendelea na maisha yao ya kawaida ya kujitafutia ridhiki na kuchapa kazi kama kawaida jambo ambalo limeoneka ni jema tofauti na watu wengi wanavyoizungumzia Zanzibar.

Akiongea Bwana Juma Ally ambae ni Mkazi wa Zanzibar alisema wanamshukuru Mungu kwa kila linaloendelea na wao wapo tayari kurudia uchaguzi pindi utakapotangazwa na Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar (ZEC).

Viewing all articles
Browse latest Browse all 13053

Trending Articles



<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>