Wakati Rais wa Marekani Barack Obama, akitarajia kutua kesho nchini Tanzania kwa ajili ya ziara ya siku mbili, Wasanii Masanja Mkandamizaji kutoka kundi la Ze Comedy na msanii wa muziki wa kizazi kipya, Shilole, wao wametua kwenye ardhi ya Obama, kama wanavyoonekana pichani na mwenyekiti wa kamati ya maandalizi wa sherehe ya miaka 3 ya Vijimambo na tamasha la Utamaduni wa Kiswahili, Bw. Baraka Daudi,wakati akiwapokea kwenye Uwanja wa Ndege wa kimataifa wa Dulles uliopo Sterling, Virginia, tayari wasanii hao kufanya makamuzi katika Tamasha hilo la Vijimambo.
Asha Riz mjumbe aliyewawakilisha Tano Ladies kwenye mapokezi hayo akipata picha ya pamoja na wasanii Masanja Mkandamizaji na Shilole mara tu walipowasili uwanja wa ndege wa kimataifa wa Dulles uliopo Sterling, Virginia.
Asha Riz katika picha ya pamoja na Shilole.
Wasanii Masanja Mkandamizaji na Shilole wakielekea kuchukua usafiri kuelekea Washington, DC kwa Obama
Shilole katika ukodak moment alipokua uwanja wa ndege wa kimataifa wa Dulles uliopo Sterling, Virginia.
Masanja Mkandamizaji kwenye Ukondak Moment uwanja wa ndege wa kimataifa wa Dulles uliopo Sterling, Virginia.
Masanja na Shilole katika picha ya pamoja.
Msanja akionyesha uwanja wa Julius Nyerere wa Marekani " NIMETUA KWA OBAMA UNABISHA???"