Mwamuzi wa maonesho ya Wanasayansi Vijana wa Tanzania kutoka Kitengo cha Masuala ya Teknolojia wa ESB International Edwina O’ Callaghan (kushoto) akisikiliza maelezo juu ya matumizi ya umeme wa mwanga wa jua kwa matumizi ya kupikia kwa kutumia jiko lililotengenezwa kwa ajili ya kupikia (Oven) kutoka kwa mwanafunzi Deogratius Daudi wa shule ya Sekondari Mwembeni kutoka mkoani Mara (kulia), katikati ni mwanafunzi Yusuph Tito.
Mbilimbi ni tunda linalotumika kama chachandu (kiungo cha mboga) kwa ajili ya kuongeza ladha ya chakula, lina uwingi wa asidi (citric acid) ambayo ni muhimu kwa binadam mahususi kwa ajili ya mmeng’enyo wa chakula mwilini. Linatumiwa hasa mikoa ya ukanda wa Pwani ikiwemo Dar es Salaam, Morogoro,Pwani, Lindi na Tanga. Shule ya Sekondari ya Wasichana Kilakala kutoka mkoani Morogoro (imewakilishwa na Irene Maigwa na Betha Shao wote kidato cha sita) kwenye banda lao la maonesho ya Wanasayansi Vijana wa Tanzania yaliyofanyika katika ukumbi wa Diamond Jubilee leo jijini Dar es Salaam.
Mwanafunzi wa shule ya sekondari ya wasichana Jangwani Liberata Kasekwa (kushoto) akimulezea mwl. Salome Mbago kutoka shule ya sekondari Morogoro (katikati) aliyeshikilia chupa nyenye dawa ya kuulia wadudu iliyotengenezwa kwa kutumia limao kwenye maonesho ya Wanasayansi Vijana wa Tanzania yaliyofanyika katika ukumbi wa Diamond Jubilee leo jijini Dar es Salaam. Picha na Eleuteri Mangi - MAELEZO