Manahodha wa timu za Taifa za Ureno, Christiano Ronaldo (kushoto) akipongezana na kupeana Fair Play na Ibrahimovic, baada ya mchezo wao marudiano wa kufuzu kucheza Fainali za Kombe la Dunia 2014, uliochezwa usiku huu nchini Sweden. Katika mchezo huo Ureno imeichapa Sweden mabao 3-2 ambayo yote yamefungwa na Ronaldo na kufanya Sweden kutolewa kwa jumla ya mabao 4-2 baada ya mchezo wa kwanza Sweden kupigwabao 1-0. Mabao mawili yote ya Sweden yamefungwa na Ibrahimovic.
↧