![]() |
DUNIA MZOBORA |
DAR ES SALAAM, Tanzania
MHARIRI Mwandamizi wa magazeti ya Uhuru na Mzalendo, Dunia Mzobora, ambaye amefariki dunia jana, anazikwa leo katika makaburi ya Kisutu jijini Dar es Salaam.
Habari zimesema Mzobora (49), ambaye alifariki dunia ghafla jana saa 12 asubuhi katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH), alikokuwa amepelekwa kwa matibabu zaidi, akitokea Hospitali ya Aga Khan pia ya Dar es Salaam, anazikwa leo saa 7 mchana katika makaburi hayo.