Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana, akihutumia maelfu ya wananchi katika Uwanja wa Shule ya Msingi Mwaka, mjini Tunduma, leo jioni, akiwa katika ziara ya kukagua utekelezaji wa ilani ya CCM, kusikiliza kero za wananchi na kuzungumza nao njia ya kuzitatua, katika mkoa wa Mbeya. Picha na Bashir Nkoromo.
Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akipita katika daraja la mto Songwe, kutoka upande wa Isongole, Ileja mkoani Mbeya, kwenda Ibilima, Wilaya ya Chitipa upande wa Malawi, alipofika wilayani humo jana akiwa katika ziara ya kukagua utekelezaji wa ilani ya CCM, kusikiliza kero za wananchi na kujadiliana nao namna ya kuzipatia ufumbuzi kero hizo, mkoani Mbeya. Kulia ni Mkuu wa Wilaya ya Ileje, Rosemary Senyamule akimweleza changamoto kuhusu mpaka huo.
Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana na Katibu wa NEC, Siasa na Uhusiano wa Kimataifa, Dk. Asha-Rose Migiro wakitoka katika ofisi ya Uhamiaji, Isongole wilayani Ileje mkoani Mbeya jana.
Eneo la Malawi, linalopakana na Tanzania wilayani Ileje mkoani Mbeya
Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana na Katibu wa NEC, Siasa na Uhisiano wa Kimataifa,Dk. Asha-Rose Migiro wakiwasalimia wananchi wa Kata ya Isongole, Ileje mkoa wa Mbeya, jana baada ya kukagua mpaka wa Tanzania na Malawi.