Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiwahutubia wananchi wa mji wa Vwawa kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika jioni ya leo katika mji huo ambao ndiyo makao makuu ya wilaya ya Mbozi, mkutano huo umehudhuriwa na wananchi mbalimbali wa mji wa vwawa, Katika ziara hiyo Kinana ameongozana na Katibu wa NEC Itikadi, Siasa na Uenezi Nape Nnauye na Dr. Asha Rose Migiro Katibu wa NEC Siasa na Uhusiani wa Kimataifa, Akizungumza katika mkutano huo Nape Nnauye amesema Injinia Christopher Chiza aache kuzungumza na vyombo vya habari badala yake aandae majibu kwa ajili ya kuhojiwa kwenye kikao cha Kamati Kuu kwa sababu kuitwa kwake kwenye kamati kuu ya CCM hakukwepeki, Kutokana na matatizo na malalamiko ya wakulima kuhusu pembejeo, kukopwa mazao yao na suala zima la wakulima kuikataa mbolea ya Minjingu huku wakilazimishwa kuitumia.
Kutoka kulia ni Mkuu wa mkoa wa Mbeya Mh. Abbas Kandoro, Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana,Dr. Asha Rozi Migiro Katibu wa NEC Siasa na Uhusiano wa Kimataifa, Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Mbeya na Mbunge wa jimbo la Mbozi Mashariki Mh. Godfrey Zambi na Nape Nnauye Katibu wa NEC Siasa Itikadi na Uenezi wakipanda miti katika eneo ambalo zahanati ya kijiji cha Mtunduru kata ya Isansa inajengwa kwa ajili ya kutunza mazingira na kuzuia upepo.![3 - Copy]()


Nape Nnauye akiwahutubia wananchi wa wilaya ya Viwawa. KUSOMA ZAIDI BOFYA READ MORE



