Quantcast
Channel: SUFIANIMAFOTO
Viewing all articles
Browse latest Browse all 13053

*KILIMANJARO STARS YATINGA NUSU FAINALI CHALENJI BAADA YA KUICHAPA UGANDA

$
0
0
Wachezaji wa Kilimanjaro Stars na viongozi, wakimpongeza kipa Ivo Mapunda, baada ya kuokoa penati mbili na zaidi ya mwisho iliyowawezesha kutinga hatua ya nusu fainali baada ya mchezo wa na Uganda kwenye Uwanja wa Agakhan jijini Mombasa leo.
****************************************
Timu ya Kilimanjaro Stars imetinga hatua ya nusu fainali ya michuano ya chalenji, baada ya kuifungashia virago Uganda kwa mikwaju ya penati. 

Katika mchezo huo timu hizo zilitoka sare kwa kufungana mabao 2-2 ndani ya dakika 90, huku Uganda wakianza kuongoza na baadae Mrisho Ngasa kuisawazishia Kilimanjaro na kuongeza bao la pili lililodumu hadi mapumziko. 

Uganda walipata bao la kusawazisha na kufanya mchezo huo kumalizika kwa sare na timu hizo kwenda katka hatua ya mikwaju. 
Kilimanjaro walikosa penati mbili zilizopigwa na Erasto Nyoni na Mbwana Samatta, huku Uganda nao wakikosa penati mbili. 

Waliopata penati kwa upande wa Kilimanjaro ni Amri Kiemba, Athuman Iddi chuji na Kelvin Yondani. Penati hizo ziliingia hatua ya pili huku Kipa wa Kilimanjaro Ivo Mapunda akiibeba Tanzania kwa kudaka penati ya hatua pili na kuifanya Tanzania kutinga katika hatua hiyo ya nusu fainali.

Viewing all articles
Browse latest Browse all 13053

Trending Articles



<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>