Quantcast
Channel: SUFIANIMAFOTO
Viewing all 13053 articles
Browse latest View live

*MAMA SALMA KIKWETE MGENI RASMI MAADHIMISHO YA SIKU YA WAKUNGA DUNIANI

$
0
0
MKE wa Rais, Mama Salma Kikwete, anatarajia kuwa mgeni rasmi katika Sherehe za maadhimisho ya Siku ya Wakunga Duniani, zinazotarajia kufanyika Mei 5, jijini Dar es Salaam. 

 Chama cha Wakunga Tanzania (TAMA) kitaadhimisha   siku ya Wakunga Duniani   (International Day of Midwives hapa nchini kwa siku mbili kuanzia tarehe 4hadi 5/2015.  

      Siku ya Wakunga Duniani huadhimishwa duniani kote tarehe tano mwezi wa tano ya  kila mwaka. 

Madhumuni ya Maadhimisho hayo ni kuhamasisha  Wadau mbalimbali  pamoja na Jamii kwa ujumla  kuhusu umuhimu wa wakunga na shughuli  wanazozifanya katika kupunguza vifo vya  akina mama vinavyotokana na uzazi pamoja na vifo  vya  watoto wachanga na wenye umri chini ya miaka mitano.  

Kauli Mbiu ya Mwaka huu (2014) ni “Wakunga Wataalam Wanahitajika Duniani kwa wingi sasa kuliko siku zote.” (The World Needs Midwives Today Than Ever)   

Hii inalenga katika  kuhakikisha kuwa huduma za Afya ya Uzazi na Mtoto zinatolewa na Wakunga wenye utalaam kwa kufuata  miongozo na viwango vilivyowekwa   ili  kuchangia katika   kufikia Malengo ya Maendeleo ya Milenia  namba  3,4, 5 na 6.  

Tanzania ni mmojawapo ya  nchi   zenye uhaba  wa  watao  huduma wenye ujuzi hususani Wakunga  katika ngazi ya  zahanati na vituo vya afya ambako ndiko wakinana  mama wengi wanapata huduma ya  wakiwa wajawazito, kujifungua na baada ya kujifungua.  

TANZANIA MIDWIVES ASSOCIATION  (TAMA)  
Address: HQ Dar Es Salaam   
P.O. Box 65524 Dar Es  Salaam Tanzania E-Mail: seolesh@yahoo.com  
  
Katika kuadhimisha siku hiyo, Wakunga kwa kushirikiana na wadau mbalimbali   watafanya shughili tatu ambazo ni:  
1. Kongamano la kisayansi kwa   siku moja tarehe 4/5/2014   ambapo watajadili   mada  na shughuli mbalimbali zinazofanywa na Wakunga.  
Mahali :   Hospitali ya Taifa ya Muhimhili  Jengo la  New  OPD  Chumba                 no 60,   linaloangaliana na Wadi ya Wazazi  
Mgeni Rasmi: Mheshimiwa Dkt. Seif S Rashidi (MB)  Waziri wa Afya na                           Ustawi Wa Jamii  
2 Kutoa huduma  za afya ya uzazi na mtoto katika viwanja vya Mnazimmoja kwa akina mama, watoto , vijana na wanaume kwa siku mbili 4/hadi 5/2014. Huduma zitakazotolewa ni:  
* Uzazi wa mpango,  
* Chanjo kwa watoto  
* Ushauri na upimaji  wa hiari  wa virus vya UKIMWI, 
 * Uchunguzi wa saratani ya  matiti na kizazi kwa akina mama  
* Utoaji  wa hiari wa damu.  
* Elimu na   ushauri kuhusu hudma ya Afya ya Uzazi na Mtoto 
* Wanaume watapata sindano ya Pepopunda ( tetanus)  
Huduma zitakazotolewa ni bure hakuna malipo.   
3 Kufanya mandamano kutoka makao makuu ya Wizara ya Afya  hadi Viwanja vya Mnazimmoja siku ya kilele tarehe 5/5/2014. Maandamano yataongozwa na Brass band ya JKT Mgulani. 
         Mgeni Rasmi ni:  Mheshimiwa Mama Salma Kikwete, Mke wa Mh. Dkt. Jakaya                                     Mrisho  Kikwete Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania  
Kwa heshima na taadhima Chama kinaomba vyombo vya habari kutusaidia  kutoa taarifa kwa  Wananchi.  
Tunatanguliza shukurani zetu.
    
Dr Sebalda Leshabari KATIBU MKUU TAMA 

*MFUMO MPYA WA KIELEKTRONIKI WAONGEZA UKUSANYAJI WA MAPATO MANISPAA YA KINONDONI

$
0
0
 Afisa Uhusiano wa Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni Bw. Sebastian Mhowera akieleza kwa waandishi wa Habari (hawapo pichani) kuhusu mfumo mpya wa kielektroniki wa ukusanyaji  mapato unatumiwa na manispaa hiyo,wakati wa mkutano uliofanyika katika ukumbi wa Idara ya Habari (MAELEZO) Leo Jijini Dar es Salaam. Kulia ni Afisa Habari wa Idara ya Habari(MAELEZO) Fatma Salum.
Mchambuzi wa Mifumo ya Komputa Bw. Jackson Kiema akiwaonyesha waandishi wa habari(hawapo pichani) mashine ya kielektroniki inayotumika katika ukusanyaji wa mapato na kuhifadhi taarifa za mapato, wakati wa mkutano uliofanyika katika ukumbi wa Idara ya Habari (MAELEZO) Leo Jijini Dar es Salaam.Kulia ni Afisa Uhusiano wa Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni Bw. Sebastian Mhowera. PICHA NA HASSAN SILAYO-MAELEZO
***************************************
MFUMO MPYA WA UKUSANYAJI WA MAPATO
 Kutokana na kukua kwa sekta ya mawasiliano nchini, Manispaa ya Kinondoni imeanzisha utaratibu wa ulipaji wa kodi kwa kutumia huduma ya simu za mkononi na Max-malipo.
Huduma hiyo mpya inayotolewa kupitia mfumo unaojulikana kama “e–payment system”,humwezesha mwananchi kulipa kodi yake muda wowote, kwa haraka na urahisi na mahali popote.
Huduma hii inatolewa na Manispaa kwa kushirikiana na wakala anayetambulika kama “Max-malipo” ambaye kupitia huduma zake mitaa 171 iliyopo katika Kata 34 imeunganishwa katika mifumo hiyo ya ulipaji kodi.
Mfumo huu wa ukusanyaji wa kodi ndani ya Manispaa ni hatua ya utekelezaji unaozingatia maelekezo ya waraka wa Serikali Na. 5 wa mwaka 2009 unaohamasisha matumizi ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA) kwa lengo la kurahisisha utoaji wa huduma kwa Umma, kwa ufanisi na kwa wakati.
Kimsingi hatua hii inahamasisha ushirikishwaji wa wananchi katika utoaji wa maamuzi yanayohusu mambo yao na kuwezesha uwepo wa Serikali iliyo wazi, inayowajibika na makini katika kutekeleza majukumu yake kwa Taifa.
Hivyo basi kutokana na malengo na umuhimu wa kuwarahisishia wananchi, Manispaa iliona ni vema ikaingia haraka ndani ya utaratibu huu ili Mwananchi aweze kulipia kodi popote kwa kutumia Max-malipo au wakala wa simu za mkononi yaani Tigo pesa Na. 212888 na M-Pesa Na. 212888.

MAFANIKIO YALIYOPATIKANA.
Katika kipindi kifupi cha muda wa miezi 3, tangu mfumo huu mpya ulipoanzishwa rasmi kumekuwa na mafanikio makubwa kama ifuatavyo:-

Mapato yameongezeka kwa kiwango kikubwa mfano; ada ·        ya kuchangia huduma za Afya (Cost sharing) imeongezeka kutoka Tshs. 45,000,000/= kwa wiki hadi kufikia Tshs. 65,000,000/= kwa wiki, sawa na ongezeko LA 69%

·        Chanzo cha kodi ya majengo hadi mwishoni mwa Machi tulikusanya Tshs. 339,000,000/= tofauti na awali ambapo hadi kipindi kama mwaka 2013 tulikusanya sawa na ongezeko la asilimia 269 hiki Tshs. 126,000,000/=

Maeneo mengine ongezeko la mapato limezidi bajeti ya mwaka iliyotakiwa kukusanywa. Kwa mfano katika ushuru wa huduma za jiji (City Service Kavy) ambapo tumezidi kwa 18% ·        Ushuru wa Masoko umeongezeka kwa wastani wa asilimia 20 ya lengo la kila mwezi.

·        Lesseni za biashara hadi Machi tumekusanya Tshs. 2.4 Bilioni sawa na 93% ya bajeti ya Manispaa ya chanzo hiki ya Tshs. 2.6 Bilioni kwa mwaka.

Napenda kuwahakikishia wananchi wa Kinondoni kuwa Manispaa ya Kinondoni itazidi kuboresha huduma zake ili kuweza kufikia malengo yaliyokusudiwa na kuwawezesha kuwa na maisha bora kutokana na mafanikio haya, lipa.

Lipa kodi kwa maendeleo ya Manispaa yako.

IMETOLEWA NA
SEBASTIAN MODESTUS MHOWERA
AFISA UHUSIANO WA MANISPAA
HALMASHAURI YA MANISPAA YA KINONDONI 
SIMU NA: 0754-227024

*SERIKALI YAZUNGUMZIA MAADHIMISHO YA WIKI YA ELIMU

$
0
0
Msemaji wa Serikali Bw. Assah Mwambene akiongea na waandishi wa habari(hawapo pichani) kuhusu maadhimisho ya Wiki ya Elimu yatakayo fanyika kitaifa mkoani Dodoma. Kulia ni Afisa Habari wa Idara ya Habari Magreth Kinabo
*****************************************
HASSAN SILAYO- MAELEZO
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mizengo Pinda kesho atazindua maadhimisho wa Wiki ya Elimu Mjini Dodoma.
Akizungumza na waandishi wa Habari Msemaji wa Serikali Bw. Assah Mwambene alisema kuwa Maadhimisho hayo yatakwenda sambamba na Maafisa elimu wa Mikoa kutoa taarifa kwa wananchi kupitia vyombo vya habari kuhusu maendeleo ya sekta ya elimu katika mikoa yao.

“Maadhimisho ya wiki ya elimu yatakwenda sambamba kwa taarifa mbalimbali kuhusu mafanikio katika sekta ya elimu kutolewa na maafisa elimu wa mikoa ili kuwapa fursa wananchi kujua nini kimefanyika katika sekta ya elimu”. Alisema Mwambene.
Pia Bw. Mwambene aliongeza kuwa katika maadhimisho hayo shule mbalimbali za msingi na sekondari zilizofanya vizuri katika mitihani ya kitaifa zitapewa zawadi.
Aidha Mwambene aliongeza kuwa wanafunzi walioandika insha kuhusu Afrika Mashariki na SADC watapewa zawadi.
Maadhimisho hayo yatafungwa Tarehe kumi na Rais Jakaya Kikwete  mkoani Dodoma

RATIBA YA MIKUTANO YA WAANDISHI WA HABARI NA MAAFISA ELIMU WA MIKOA
S/N
TAREHE
MKOA
MHUSIKA
NAMBA YA SIMU
1
2/5/2014
DODOMA
BW.JUMA KAPONDA

0784 584863
MOROGORO
BIBI W. NKAYA

2
3/5/2014
DSM
BW. R. MAPUNDA
0754 744536
PWANI
BW. YUSUPH KIPENGELE

TANGA
BW. R. CHOMOLA

3
4/5/2014
KILIMANJARO
BIBI. LUCY MALISA

TABORA
BW. J. MABEYO

RUVUMA
BIBI. MAYASA HASHIM

4
5/5/2014
KATAVI
BW. ERNEST HINJU

RUKWA
BW. S. MGINA

LINDI
BW. GIFT ENOCK

MTWARA
BW. HIPSON KIPENYA

5
6/5/2014
MANYARA
BW. IBRAHIM MBANGO

NJOMBE
BW. SAID NYANSILO

MBEYA
BW. R. NTYAMA

ARUSHA
BW. NESTORY MLOKA

6
7/5/2014
MWANZA
BW. H. MAULID
0754 432691
MARA
BW. E. MPALILE

GEITA
BIBI. E. BUCHUMA

SIMIYU
BW. A. KAMAMBA
0764856644
7
8/5/2014
KIGOMA
BW. SALVATORY SHAURI
0754 361266
KAGERA


SHINYANGA
BIBI. EVA MLOPA

8
9/5/2014
IRINGA
BW. J. MNYIKAMBI

SINGIDA
BIBI. FATUMA KILIMIA


9

10/5/2014



*WANAHABARI 'MATESTER' WASHINDA UONJAJI BIA ZA TBL

$
0
0
 Meneja Uhusiano wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), Editha Mushi (kushoto), akiwapongeza waandishi wa habari washindi wa uonjaji bia za kampuni hiyo katika mashindano yaliyofanyika baada ya kutembelea kiwanda hicho, Dar es Salaam juzi. Wa pili kushoto ni mshindi wa kwanza, Richard Makore wa gazeti la Nipashe, mshindi wa pili, Mnaku Mbani wa gazeti la Business Times na Denis Fusi wa gazeti la Habari Leo aliyeshika nafasi ya tatu.
Mpishi Mkuu wa Bia wa Kiwanda cha Kampuni ya Bia Tanzania  (TBL) Dar es Salaam, Calvin Nkya (kulia) akimkabidhi zawad ya bia mshindi wa kwanza wa kuonja bia Richard Makore wa gazeti la Nipashe
Meneja Uhusiano wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), Editha Mushi (kulia) akimkabidhi zawadi ya bia Mwandishi wa habari wa gazeti la Business Times, Mnaku Mbani baada ya kuwa mshindi wa pili wa uonjaji bia.
Mpishi Mkuu wa Kiwanda cha Bia cha Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), Dar es Salaam, Calvin Nkya (aliyenyoosha mkono), akitoa maelezo ya jinsi bia zinavyotengenezwa kisasa wakati  wa ziara ya waandishi wa habari kiwandani hapo juzi, ambapo pia walishiriki katika shindano la kuonja bia
Mpishi Mkuu wa Kiwanda cha Bia cha Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), Dar es Salaam, Calvin Nkya (aliyenyoosha mkono), akitoa maelezo ya jinsi bia zinavyotengenezwa kisasa wakati  wa ziara ya waandishi wa habari kiwandani hapo juzi, ambapo pia walishiriki katika shindano la kuonja bia
Mpishi Mkuu wa Kiwanda cha Bia cha Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), Dar es Salaam, Calvin Nkya (aliyenyoosha mkono), akitoa maelezo ya jinsi bia zinavyotengenezwa kwa kutumia kompyuta wakati  wa ziara ya waandishi wa habari kiwandani hapo juzi, ambapo pia walishiriki katika shindano la kuonja bia
Wanahabari wakipata maelezo jinsi bia inavyochachuliwa
Wanahabari wakitembelea eneo la matanki ya kuchachulia bia
Baadhi ya waandishi wa habari wakiangalia vifaa maalumu vya kuhifadhia kimiminika cha bia kinachouzwa bila kuwekwa kwenye chupa katika hoteli mbalimbali, walipotembelea Kiwanda cha Bia Tanzania (TBL), Dar es Salaam juzi. Waandishi hao walishiriki katika mashindano ya kuonja bia za TBL.

*MAKAMU WA RAIS DKT. BILAL AHUDHURIA IABADA MAALUM YA KUSIMIKWA ASKOFU MTEULE ALEN SISO WA KANISA LA METHODIST TANZANIA- JIMBO TEULE LA MASHARIKI NA PWANI, DAR ES SALAAM

$
0
0
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akimpongeza Askofu Mteule, Alen Legeza Siso, baada ya kumkabidhi Katiba na Kanuni za Kanisa la Methodist Tanzania, wakati wa Ibada Maalum ya Kuwekwa Wakfu (kusimikwa) askofu huyo, iliyofanyika kwenye Kanisa la Imanueli dhehebu la Methodox, Jimbo teule la Pwani na Mashariki lililopo Bunju Jijini Dar es Salaam, leo.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiwahutubia Waumini wa dini ya Kikristo wa Kanisa la Methodist Tanzania, wakati wa Ibada Maalum ya Kusimikwa Askofu Mteule Alen Legeza Siso, iliyofanyika kwenye Kanisa la Imanueli, Jimbo teule la Pwani na Mashariki lililopo Bunju Jijini Dar es Salaam, leo.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiagana na Askofu Mkuu wa Kanisa la Methidist Tanzania, Dkt. Mathew Byamungu, baada ya Ibada maalum ya kusimikwa Askofu Mteule, Alen Legeza Siso, (kulia) kuwa Askofu wa Jimbo la Mashariki na Pwani iliyofanyika kwenye Kanisa la Imanueli, Jimbo hilo lililopo Bunju Jijini Dar es Salaam, leo.
  Askofu Mkuu wa Kanisa la Methidist Tanzania, Mathew Byamungu, akimsimika Askofu Alen Legeza Siso, kuwa Askofu Mkuu wa Jimbo la Mashariki na Pwani, Makanisa ya Methodist Tanzania, wakati wa Ibada Maalum ya kuwekwa Wakfu Askofu huyo iliyofanyika leo Mei 3, 2014, kwenye Kanisa la Emanueli lililopo Bunju jijini Dar es Salaam. 
  Baadhi ya Waumini wa Kanisa hilo waliohudhuria Ibada hiyo maalum ya kumsimika Askofu Mteule, Alen Siso.
  Baadhi ya Waumini wa Kanisa hilo waliohudhuria Ibada hiyo maalum ya kumsimika Askofu Mteule, Alen Siso.
Askofu Mkuu wa Kanisa la  Methodist  Tanzania, Dkt. Mathew Byamungu, akimvisha pete Askofu Alen Legeza Siso, ya kuashiria kuwa Askofo wa Kanisa hilo, baada ya kusimikwa rasmi wakati wa Ibada maalum iliyofanyika Kanisa la Emanueli lililopo Bunju jijini Dar Es Salaam, leo.
 Makamu wa Rais wa Jamhiri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiwa katika picha ya pamoja na Askofu Mkuu wa Kanisa la  Methodist  Tanzania, Dkt. Mathew Byamungu, Askofu Mteule wa Jimbo la Mashariki na Pwani, aliyesimikwa, Alen Siso na baadhi ya wachungaji wa Kanisa la Emanuel, baada ya ibada maalum ya kusimikwa Askofu, Alen, leo.
 Makamu wa Rais wa Jamhiri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiwa katika picha ya pamoja na Askofu Mkuu wa Kanisa la  Methodist  Tanzania, Dkt. Mathew Byamungu, Askofu Mteule wa Jimbo la Mashariki na Pwani, aliyesimikwa, Alen Siso na baadhi ya wachungaji wa Kanisa la Emanuel, baada ya ibada maalum ya kusimikwa Askofu, Alen, leo.
 Kikundi cha Kwaya cha Msasani, kikitoa burudani wakati wa Ibada hiyo.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisalimina na baadhi ya wachungaji wa Kanisa la Emanueli, Jimbo la Mashariki na Pwani, wakati alipowasili jimboni hapo kwa ajili ya kuhudhuria Ibada maalum ya Kusimikwa, Askofu Mteule, Alen Legeza Siso, jijini Dar es Salaam, leo.
**************************************
HOTUBA YA  MHESHIMIWA  DKT. MOHAMMED GHARIB BILAL, KUSOMA ZAIDI BOFYA READ MORE MAKAMU WA RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA, KATIKA IBADA YA KUSIMIKWA ASKOFU  MTEULE ALEN SISO WA KANISA LA METHODIST TANZANIA- JIMBO TEULE LA MASHARIKI NA PWANI, DAR ES SALAAM, TAREHE 3.5.2014
Mhe. Said Meck Sadiki, Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam;
Baba Dkt. Mathew Byamungu , Askofu Mkuu wa Kanisa la  Methodist  Tanzania:
Alen Siso, Askofu wa Jimbo Teule la Mashariki na Pwani;
Mhe. Jordan Rugimbana, Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni;
Maaskofu na Wakuu wa Madhehebu mbalimbali  mliopo;
Viongozi wa Serikali na Vyama vya Siasa mliopo hapa;
Wawakilishi wa Mashirika na Wahisani mbalimbali;
Ndugu Waandishi wa Habari;
Waumini  wote mliohudhuria;
Wageni Waalikwa;
Mabibi na Mabwana;

Bwana Yesu asifiwe! 
Aawali ya yote, tuna kila sababu kumshukuru Mwenyezi Mungu, mwingi wa rehema , kwa kutupa uzima na kutuwezesha kukusanyika hapa siku  leo. Tuliopata kibali hiki, ni upendeleo wa aina yake, wapo  wenzetu wengi, wameshindwa kuiona siku ya leo, wengine wamelala hospitalini wakipigania uhai. Sisi tuliopata nafasi hii, tuna kila sababu, kumrudishia Mungu sifa na utukufu.
Baba Askofu Mkuu;
Ndugu  Waumini;
Kabla sijaendelea, napenda niseme neno moja; Nimekuwa na bahati kubwa kusimama chini ya dari ya Kanisa la Methodist Tanzania. Nakumbuka ni mwaka jana, Aprili 27, mlinialika  katika Harambe na Ibada  Maalumu ya kumshukuru Mungu, kwenye  Kanisa la Methodist Tanzania, pale Msasani. Leo hii mmenialika tena  katika tukio hili la kihistoria, la kusimikwa Askofu Mteule Alen Siso. Nawashukuru sana, kwa moyo wa upendo na heshima kubwa mnayonipa.  Sina maneno mazito ya kushukuru, zaidi ya kusema ; Bwana azidi kuwatunza na kuwapigania !
Nichukue fursa hii  kipekee, kukushukuru wewe binafsi Baba Askofu Mkuu Dkt. Byamungu, Watendaji wa Jimbo  Teule la Mashariki na Pwani, na Uongozi mzima wa  Kanisa la Methodist Tanzania,  kwa  mwaliko wenu wa leo. Nimeupokea kwa moyo mweupe, na  mikono miwili. Asanteni sana.
Baba Askofu Mkuu;
Ndugu waumini;
Napenda nitumie nafasi hii, kulipongeza Kanisa la Methodist Tanzania, chini ya uongozi wako Baba Askofu Mkuu, Dkt. Byamungu , kwa namna mnavyoendelea kupanuka, sambamba na kuunga mkono juhudi za Serikali, kuwaletea wananchi wake maendeleo.
Kwa mujibu wa maelezo, Kanisa la Methodist Tanzania, lilianza kutoa huduma ya kiroho hapa nchini, Juni 12 mwaka 1991. Leo hii  lina miaka 23 tu, lakini tumeona namna lilivyopiga hatua kubwa, kuchangia nyanja mbalimbali za maendeleo ya jamii.
Ujenzi wa hospitali tano mkoani Geita, shule mkoani Arusha, uchimbaji visima virefu kwa shule na magereza  katika mikoa ya Dar es Salaam na Pwani, na ujenzi wa Chuo cha Theolojia  huko Dodoma na Arusha, ni baadhi tu ya mambo mengi mema, yanayofanywa na kanisa hili. Kwa niaba ya Serikali, nawapongeza  kwa kazi kubwa mnayofanya. Tutaendelea kuwa karibu nanyi,   kwa kila jambo mtakaloona tunapaswa kushirikiana.
Wageni Waalikwa;
Mabibi na Mabwana;
Napenda nipongeze pia, mchango mkubwa unaotolewa na mashirika na taasisi mbalimbali za dini hapa nchini, kusaidia juhudi za Serikali kuwaletea wananchi wake maendeleo. Taasisi na mashirika ya dini, yamekuwa mstari wa  mbele kujenga  shule, vyuo, hospitali na huduma zingine mbalimbali za jamii. Serikali peke yake haiwezi kufanya miujiza.Tunathamini na kutambua  mchango mkubwa  unaotolewa na mashirika na taasisi zote za dini .  Nawahakikishia kwamba, Serikali itaendelea kushirikiana kwa karibu na mashirika haya, kwa maslahi ya maendeleo ya nchi yetu.
Wito wangu kwa mashirika na taasisi za dini; Fanyeni kila linalowezekana, kuboresha  zaidi huduma zenu,  ili ziendane na ushindani  wa zama hizi. Hakikisheni mnakuwa na shule bora za kisasa zenye vifaa vya kutosha kufundishia, kadhalika hospitali zenu ziwe za kisasa , hata visima mnavyochimba, viwe na ubora wa unaotakiwa. Nawatia shime;  Kazi mnayofanya ni nzuri, endeleeni na moyo huo,  na Bwana atazidi kubariki kazi za mikono yenu.
Baba Askofu Mkuu;
Ndugu Waumini;
Mabibi na Mabwana;
Napenda kutumia nafasi hii kuwaasa Watanzania kudumisha amani na mshikamano wetu, ambao umekuwa tunu kubwa tangu tulipopata Uhuru. Ni juzi tu tumeadhimisha Miaka 50 ya Muungano wetu huku nchi yetu ikiendelea kuwa kisiwa cha amani na utulivu.  Katika hili, nawakumbusha watu wa Mungu kukesha na kuliombea  Taifa  letu. Si  watu wote wanafurahia mafanikio haya. Wapo wanaotuombea mabaya usiku na mchana, wanataka waone  siku moja tumefarakana na kupoteza mwelekeo. Naamini watu wa Mungu mkisugua goti katika hili, kamwe Shetani hatapata nafasi ya kujiinua katika Taifa letu. 
Sisi katika Serikali, tutaendelea kusimamia kwa nguvu zote,  dhamana kubwa mliyotupa, ya kudumisha  Umoja na Mshikamano wa nchi yetu. Naamini kwa kuwa hata  Mungu wetu hafurahii mafarakano na utengano, ataendelea kusimama upande wa haki kutupigania. Tutaendelea kusimamia misingi ya utawala wa bora  bila kujali rangi ya mtu kabila, dini, jinsia  wala eneo analotoka.
Baba Askofu Mkuu;
Ndugu Waumini;
Upendo ni sharti  muhimu sana katika maisha ya kila siku ndani ya jamii. Nilipozungumza nanyi mwaka jana huko Msasani, nilizungumzia hili, Napenda kurudia tena katika hadhara hii. Nazungumzia hili kutokana na mazingira ya mpito ambayo Taifa letu,  linapita kwa sasa. 
Baba Askofu Mkuu, ni vigumu nchi yetu kuendelea kuwa na amani kama watu wetu hawapendani. Ni vigumu watu wetu kuendelea kukaa  pamoja  kama hawavumiliani. Ni vigumu nchi yetu kuendelea kuwa ya amani  na utulivu, kama watu wetu hawaheshimiani.  Bila Upendo na Kuvumiliana, Taifa letu litasambaratika.
Tupo katika mchakato wa kuandika Katiba Mpya. Tulianzisha mchakato huu kwa nia njema ya kuwawezesha Watanzania kupata Katiba, inayoendana na  mazingira ya sasa. Tofauti na ilivyotarajiwa, mchakato huu umeanza kugubikwa na malumbano huku baadhi ya Wabunge wa Bunge Maalumu la Katiba, wakitangaza  kususa vikao. Kukosekana Upendo, ni moja ya sababu  kuu ya kushindwa kuvumiliana, hata katika mijadala ya Bunge la Katiba.  
Ndani ya Biblia takatifu,  Kitabu cha Wakorintho wa Kwanza, mlango wa 13, mstari wa 4  hadi 8, kimezungumza  vizuri sana kuhusu Upendo; nitanukuu:-“Upendo huvumilia, hufadhili, upendo hauhusudu, upendo hautakabari, haujivuni, haukosi kuwa na adabu, hautafuti mambo yake, hauoni uchungu,hauhesababu mabaya, haufurahii udhalimu bali hufurahi pamoja na kweli, huvumilia yote, hustahimili yote,  upendo haupungui neno wakati wowote… Ukiendelea mstari wa 13, unahitimisha kwa kusema:-  “Basi sasa inadumu imani, tumaini , upendo  haya matatu;  na katika hayo,  lililo kuu ni  UPENDO.”
Pia Maandiko matakatifu katika Waraka wa Kwanza wa Petro Mtume, mlango wa 4, mstari wa 8  hadi 10, yanasema hivi; nitanukuu:-” Zaidi ya yote iweni na juhudi nyingi katika kupendana kwasababu upendano husitiri wingi wa dhambi. Mkaribishane ninyi kwa ninyi pasipo kunung’unika  kila mmoja kwa kadri alivyoipokea karama, itumieni kwa kuhudumiana kama mawakili wema wa neema mbalimbali za Mungu.”
Nawasihi waumini wa dini zote nchini, kuzidi kuombea jambo  hili , ili mchato huo, ufikie hatma njema kama ilivyokusudiwa. Nawakumbusha pia  Wabunge wa Bunge Maalumu la Katiba, watakaporejea Agosti mwaka huu, kujenga upendo miongoni mwao , wakumbuke kwamba wanawakilisha mamilioni ya Watanzania. Biblia imetuambia kuwa wakijenga upendo, Watavumiliana, hawatahesabiana mabaya,  hawatapenda udhalimu na wala hawatakoseana adabu.
Baba Askofu Mkuu;
Viongozi wa dini mbalimbali mliopo;
Ndugu Waumini;
Jukumu mlilotupa la kuongoza Watanzania,  haliwezi kuwa na tija, kama wananchi tunaowaongoza, hawatamjua  Mungu na kufuata mafundisho yake.  Watu wetu wakimjua Mungu hawatatoa wala kupokea rushwa, hawatauza wala kutumia dawa za kuleva, hawatajichukulia sheria mikononi, hawataiba wala kudhulumu, hawatajilimbikizia mali,  hawatatega kazini, watakaa mbali na uasherati  na maovu mengine yote. Taifa la wacha Mungu lina  amani , upendo, umoja na mshikamano. Hivyo lina nafasi  kubwa ya kusonga mbele. Lakini ni kazi ngumu sana kuongoza Taifa la watu waliotekwa na ibilisi.
Natoa changamoto kwa viongozi wa dini zote nchini, kuhakikisha  mnawajengea waumini  wenu, misingi ya madili mema. Waumini wenu wakifuata mafundisho ya Mungu, Taifa litakuwa na raia wema, wachapakazi, maovu ndani ya jamii yatapungua sana kama si kumalizika kabisa.
Vilevile nitumie nafasi hii, kuwakumbusha waumini wa dini zote nchini, kuendelea kuvumiliana, kuheshimiana na kupendana. Ni wajibu wa kila mmoja wetu, kuheshimu dini ya  mwenzake. Hakuna dini bora kuliko nyingine, dini zote ni sawa, tofauti yake, ni taratibu za namna ya kuabudu. Tofauti hizi haziondoi haki yetu ya kuwa watoto wa Baba mmoja Mungu,  walio katika nyumba moja ambayo ni Tanzania. Pendaneni, kwani maandiko matakatifu, yanatufundisha kuwapenda hata maadui wanaotuudhi.
Kitabu cha Mathayo, mlango wa 5, mstari wa 43 hadi 45  unasema hivi,nanukuu;  “Mmesikia kwamba imenenwa umpende jirani yako, na umchukie adui yako, lakini mimi nawaambia, wapendeni adui zenu , waombeeni wanaowaudhi, ili mpate kuwa wana wa Baba yenu aliye mbinguni, maana yeye huwaangazia jua lake waovu na wema , huwanyeshea mvua wenye haki na wasio na haki.”
Baba Askofu Mkuu;
Ndugu Waumini;
Mabibi na Mabwana;
Nitumie nafasi hii kukupongeza Baba Askofu Alen Siso, kwa namna Mungu alivyokuinua, hatimaye leo umesimikwa rasmi kuwa Askofu wa Jimbo Teule la Mashariki na Pwani. Naamini kuchaguliwa kwako, hakukuja kwa bahati bali “BWANA AMEKUCHAGUA, NA  ANA HAJA NAWE.”
Baba Askofu Siso, tukio hili kwako, ni ile  sauti iliyoandikwa katika Kitabu cha nabiiIsaya mlango  6 mstari wa 8, ikisema kwamba, nanukuu; “ Kisha nikasikia sauti ya Bwana akisema, Nimtume nani, naye ni nani atakayekwenda kwa ajili yenu? Ndipo niliposema. Mimi hapa, nitume mimi.” 
Ujumbe huu umeelezwa pia katika Injili ya  Luka , mlango wa 12,  mstari wa 42 hadi wa 43,  nanukuu; Bwana akasema, ni nani basi aliye  wakili mwaminifu, mwenye busara, ambaye Bwana wake atamweka juu ya utumishi wake wote, awape watu posho kwa wakati wake?
Baba Askofu Siso, mistari niliyoisoma hapo juu ni ushahidi kwamba umepokea utumishi huu kwa Kuitwa na Kuitika. Sisi sote tuliokusanyika hapa leo, ni mashahidi.  Ifanye kazi ya Mungu kwa moyo mmoja. Naamini utakuwa mchungaji mwema, utakaowachunga kondoo wa Mungu, na kuwarudisha zizini wale waliopotea.
Ndugu Waumini;
Mabibi na Mabwana;
Niwaombe viongozi wote wa kanisa hili, kuanzia wewe Baba Askofu Mkuu, Dkt. Byamungu, kuzidisha mshikamano miongoni mwenu, na kumsaidia Askofu wetu mpya, kufanya kazi hii takatifu kwa ufanisi.  Zingatieni  maneno ya Mungu kutoka Waraka wa Kwanza wa Petro Mtume, mlango wa 5, mstari  wa 2 hadi wa 4, nanukuu ;“Lichungeni kundi la Mungu lililo kwenu, na kulisimamia, si kwa kulazimishwa bali kwa hiyari, kama Mungu atakavyo,si kwa kutaka fedha ya aibu bali kwa moyo, wala si kama wajifanyao mabwana juu ya mitaa yao, bali kwa kujifanya vielelezo kwa lile kundi.”

Baba Askofu Mkuu Byamungu;
Askofu Siso;
Ndugu Waumini;
Mabibi na Mabwana;
Kabla ya kuhitimisha hotuba yangu, napenda kuwahakikishia kuwa,  nimepokea changamoto zenu mbalimbali mlizosoma  kwenye risala yenu. Nimesikia matatizo yenu ya maeneo ya kujenga miradi. Serikali kupitia mamlaka zake, itafuatilia kwa karibu masuala hayo, kuangalia namna bora ya kuyapatia ufumbuzi.
Baada ya kusema hayo, kwa mara nyingine, napenda kukushukuruni kwa kunialika mahali hapa siku ya leo. Nazidi kuwasihi sana watu wa Mungu, msichoke kuliombea Taifa letu, kwani kuna nguvu kubwa ndani  ya maombi. Kemeeni  njama zote zenye nia mbaya ya kuvuruga Amani, Umoja na Mshikamano wetu.  Daima, pendeni kusikiliza mema, msivutike kusikiliza maovu . Nawaachia ujumbe kutoka Kitabu cha Mithali,  mlango wa 11, mstari wa 31 hadi 32, unasema hivi; “ Kinywa cha mwenye haki hutoa hekima, bali ulimi wa ukaidi utakatiliwa mbali. Midomo ya mwenye haki huyajua yatakayokubaliwa, bali kinywa chao wasio haki hunena ukaidi.”
 Mungu awabariki sana.  Ahsanteni sana kwa kunisikiliza.

*RAIS JAKAYA KIKWETE AONGOZA KAMPENI DHIDI YA UKIMW KILIMANJARO

$
0
0
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akikabidhi hundi ya jumla ya Shilingi Milioni miamoja na Hamsini 150m/- kwa wawakilishi wa kituo cha kulea watoto yatima cha Moyo wa Huruma kilichopo mkoa wa Geita.

Fedha hizo si sehemu ya shilingi milioni mia saba (700m/-) alizokabidhi Rais Kikwete jana usiku kwa taasisi mbalimbali zinazojishughulisha na mapambano dhidi ya ukimwi Tanzania.Fedha hizo zinatokana na kampeni ya kukusanya fedha kwa njia ya kupanda mlima Kilimanjaro kila mwaka ambapo wafadhili mbalimbali huchangia watoto na watu wengine.Pichani watoto wawili watakaopanda mlima Kilimanjaro Jacob Musa (watatu kushoto) na Julitha Sylvester (wapili kulia) wanaofadhiliwa na kituo cha Moyo wa huruma wakipokea hundi ya kituo chao.

Wengine katika picha kutoka kushoto ni Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu Dr.Florence Turuka,Mkurugenzi Mkuu wa TACAIDS Bi Fatma Mrisho,Mkurugenzi Mtendaji wa Geita Gold Mines Bwana Michael Van Anen (watano kushoto)  Naibu Waziri wa Afya Dr.Steven Kebwe, na kulia ni msimamizi wa kituo cha kulelea watot yatima cha Moyo wa Huruma Sista Adalbera Mukure.
Katika hafla ya jana ya kuchangia kampeni hiyo iliyofanyika katika hoteli ya Hyatt Regency Kilimanjaro jijini Dar es Salaam zaidi ya shilingi milioni mia tisa 900m/- zilikusanywa .Picha na Freddy Maro

*MALKIA NA RAIS MPYA WA KIJIJI CHA MAISHA PLUS WAPATIKANA

$
0
0
Ndani ya Kijiji cha Maisha Plus/ Mama Shujaa wa chakula kila siku ya Alhamisi huwa panafanyika uchaguzi wa kumpata Rais mpya ambaye anachaguliwa na Washiriki wenyewe wa Kijiji cha Maisha Plus ambapo kati ya hao mmoja hupatikana na  Marais  waliopita hawapatiwi nafasi ya kugombea tena, na kwamba mama yake na Rais huteuliwa moja kwa moja kuwa Malkia wa Kijiji hicho.
Malkia Mpya wa Kijiji cha Maisha Plus Elizabeth Masha kutoka Morogoro Tanzania.
Rais Mpya wa Kijiji cha Maisha Plus Mary Masha, kutoka Nchini Kenya.

Kazi ya uchaguzi ilianza Kijijini hapo ambapo idadi ya washiriki 36 wakiwemo vijana 16 na kinamama 20 Kila siku ya Alhamisi ni siku ya uchaguzi wa Rais wa kijiji cha Maisha Plus  ambaye husimamia shughuli zote zinazofanyika katika kijji hicho.

Wiki hii washiriki 10 waliteuliwa kugombea nafasi ya urais ambapo 7 ndiyo waliopigiwa kura ya siri na kupata mshindi. Washiriki wawili kati yao hawakuweza kugombea nafasi ya hiyo kutokana na utaratibu uliopo kwamba aliyewahi kushika wadhifa huo kwa muhula uliopita hataweza kugombea tena.

Marais hao wa mihula uliyopita ni Bonifas Mang’anyi na Bakari Khalid wote watanzania. Abdul Karim kutoka Burundi alijitoa kwa kuwa hakuwa tayari kushika wadhifa huo kwa sasa.
 Kwa kawaida kila kijana huwa na mama katika kijiji cha Maisha Plus na endapo kijana atachaguliwa kuwa Rais mama yake huwa Malkia ambaye humshauri Rais na kufanya maamuzi katika kijiji hicho.

Uchaguzi ulifanyika kwa wagombea 7 akiwemo Shida Mganga, Seif Mohamed, Ally Thabiti, Mbonimpaye Nkoronko na Hyasinta Hokororo kutoka Tanzania, Ngabozinza Daniel kutoka Rwanda na Mary Masha kutoka Kenya. Uchaguzi wa Rais ulifanyika mara mbili kwa kuwa washindi walipata kura sawa iliyopelekea kurudia kupiga kura ili kupata mshindi mmoja. 

Washindi waliopata kura sawa ni Mary Masha kutoka Kenya na Ally Thabit kutoka Tanzania ambapo Mary Masha aliibuka mshindi kwa kura 21 kwa 15. Hivyo Rais wa wiki hii ni Mary Masha na malkia Elizabeth Simon.
Utaratibu wa kuchagua wagombea: Kila mshiriki hujaza fomu kuteua jina la atakayekuwa kuwa Rais wa wiki hiyo. Walioteuliwa hujinadi ili wapate kupigiwa kura na hatimaye kupata mshindi.

*SHIME WAANDISHI WA HABARI MSIKUBALI KUTUMIWA KAMA MADARAJA, UNGANENI

$
0
0
DSC_0017
Baadhi ya waandishi wa habari na wadau kutoka asasi mbalimbali nchini wakifanya usajili kwenye kongamano la siku moja lilioandiliwa kuadhimisha Uhuru wa vyombo vya Habari Duniani 2014 lililofanyika jijini Arusha. 
Picha na Zainul Mzige.
**************************************
Na Waandishi Wetu, Arusha
Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri (TEF), Absalom Kibanda ametoa wito kwa waandishi wa habari nchini kuyapa uzito matukio yanayowatokea waandishi wa habari na kuyapigia kelele kwa nguvu zote ili kuyakomesha.
Kibanda aliyasema hayo jana mjini Arusha katika kongamano lililoandaliwa kama sehemu ya maadhimisho ya siku ya uhuru wa vyombo vya habari duniani na kuongeza kwamba wakati umefika kwa waandishi wa habari kuondoa tofauti zao na kuungana pamoja kuongeza nguvu waliyonayo kukabiliana na ukatili unaoendelea dhidi ya waandishi wa habari katika miaka ya hivi karibuni.
“Baadhi ya wahariri huwa hawayaandiki madhila yanayowasibu waandishi wa habari na kuyapa uzito unaostahili aidha kwa huyapuuzia au kudharau kwa kuwa hayawahusu moja kwa moja,” alisema Kibanda.
Aliongeza kwa kusema kuwa vyombo vya habari mara nyingi vimekuwa vikinyooshewa vidole na kulaumiwa kwa kutokufanya kazi kwa uadilifu jambo ambalo linatafsiriwa kuwa ni la uonevu, vinatumiwa vibaya na hakuna anayesimama kuvitetea kutokana na mchango wake mkubwa katika jamii.
DSC_0053
Afisa Mipango Kitengo cha Mawasiliano, Habari na Tehama UNESCO, Bw. Al Amin Yusuph, akiwasilisha mada kuhusu mchango wa uhuru wa vyombo vya habari katika utawala bora, kukuza uwezo na kupunguza umaskini kongamano la waandishi wa habari lilioandaliwa kama sehemu ya maadhimisho ya siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari Duniani yanayofanyika jijini Arusha.

“Kwa sasa tasnia hii iko kwenye wakati mgumu sana kwani hata marais wa nchi mbalimbali mfano Uganda, Kenya hata Marekani wanakinzana na vyombo vya habari kwa madai kuwa kauli zao zinapotoshwa, laikini ukweli ni kwamba ni vyema kauli hizo za viongozi zikachunguzwa kwa undani zaidi ili kuelewa iwapo zina uwajibikaji ndani yake,” alisema Kibanda.

Kibanda aliongeza kuwa wakati umefika sasa kwa waandishi kutambua kuwa kuna ajenda za siri zilizojificha dhidi ya uteswaji wa waandhishi wa habari hivyo yasidharauliwe, yafanyiwe kazi kwa kina ili kuelewa kiini cha tatizo kwa kupata ufumbuzi.
Kwa upande wake mwandishi mkongwe na aliyetunukiwa tuzo ya maisha mwaka 2012 na Baraza la Habari Hamza Kasongo alisema vyombo vya habari vina nguvu kubwa katika kushawishi hivyo vitumie nguvu hiyo kama muhimili wa nne wa nchi katika kuzikabili changamoto zilizopo.

“Kuwe na mtandao unaoeleweka wa mawasaliano kati ya waandishi wa habari nchini ili kuhakikisha kuwa matatizo yaliyopo yanatatuliwa bila woga na kwa ujasiri kwa lengo la kufanya kazi kwa ufanisi mkubwa,” alisema Kasongo.
DSC_0060
Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam Kitivo cha Sheria , Bw. James Jesse, akitoa mada kuhusu umuhimu wa sheria katika kulinda haki ya uhuru wa kujieleza kwa kila mtu wakati wa kongamano la waandishi wa habari lilioandaliwa kama sehemu ya maadhimisho ya siku ya uhuru wa vyombo vya habari duniani yanayofikia kilele leo jijini Arusha.

Mwanahabari mwingine mkongwe Dokta Samwilu Mwaffisi aliyetoa mada ya Maadili ya Uandishi wa Habari alisema kuwa kuna haja ya waandishi kuzingatia uhuru wa habari walionao kwa kuzingatia maadili yanayowaongoza ili kuboresha heshima waliyonayo katika jamii kwa kuandika ukweli na uhakika, bila upendeleo, kutoa fursa ya kujitetea na kukubali kuomba radhi pale unapokosea.
“Kuandika habari zenye kuzingatia maadili kunapunguza manung’uniko, mashauri na kuongeza heshima ya chombo cha habari na mwanahabari mwenyewe,”
Akizungumzia suala la ufanisi, Rais wa Vilabu vya Waandishi wa Habari, Kenneth Simbaya, aliwaasa waandishi wa habari kusimamia ukweli katika kazi zao na kuacha kufanya kazi kwa mazoea jambo ambalo litakawaweka huru zaidi katika utekelezaji wa shughuli zao za uandishi wa habari.
Maadhimisho hayo yaliyoandaliwa na umoja wa asasi mbalimbali chini ya uenyekiti wa MISA TANZANIA unafikia kilele chake tarehe 3 Mei kwa kuzindua majarida mbalimbali, matamko kutoka asasi mbalimbali na kuhitimishwa kwa tafrija ya chakula cha jioni chini ya mgeni rasmi Jaji Mstaafu Mheshimiwa Mark Bomani.
DSC_0341
Mwanahabari Mkongwe kutoka Chuo Kikuu Huria, Dokta Samwilu Mwaffisi (kulia) akiwasilisha mada ya Maadili ya Uandishi wa Habari kwenye kongamano la siku moja lilioandiliwa kuadhimisha Uhuru wa vyombo vya Habari Duniani 2014 lililofanyika jijini Arusha. Kushoto ni Mhadhiri kutoka Chuo Kikuu cha Iringa, Bw. Simon Berege.
DSC_0311
Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri (TEF), Absalom Kibanda, akitoa maoni yake wakati wa kongamano la siku moja lilioandiliwa kuadhimisha Uhuru wa vyombo vya Habari Duniani 2014 lililofanyika jijini Arusha.
DSC_0079
Pichani juu na chini ni baadhi ya waandishi wa habari wakongwe, mabalozi na wanahabari washiriki katika kongamano la siku moja lilioandiliwa kuadhimisha Uhuru wa vyombo vya Habari Duniani 2014 lililofanyika jijini Arusha.
DSC_0028
DSC_0283
DSC_0371
Mwandishi wa Habari Chokonozi, Bw. Fredrick Katulanda, akielezea madhila mbalimbali yaliyomsibu katika utekelezaji wake wa kuandika habari za uchambuzi.
DSC_0119
Mwanahabari Mkongwe Bi. Leila Sheikh akichangia mada ya Mchango wa Uhuru Wa Vyombo Vya Habari Katika Utawala Bora, Kukuza Uwezo Na Kupunguza Umaskini wakati wa kongamano la siku moja lilioandiliwa kuadhimisha Uhuru wa vyombo vya Habari Duniani 2014 lililofanyika jijini Arusha.
DSC_0348
Mmiliki wa Gazeti tando la Mjengwa na Kituo cha Redio Kwanza Jamii, Bw. Maggid Mjengwa akielezea jinsi Intaneti inavyoweza kuunganisha mtandao wa Redio.
DSC_0339
Makamu Mwenyekiti wa Mtandao wa Vyombo vya Habari Jamii Tanzania (COMNETA) na Mkurugenzi wa kituo cha mawasiliano Sengerema, Bw. Felician Ncheye akichangia mada.
DSC_0386
Mkufunzi wa Redio Jamii kutoka UNESCO, Mama Rose Haji Mwalimu, (kushoto) akiwa na baadhi ya washiriki wa Kongamamo hilo.
DSC_0310
Rais wa Umoja wa Vilabu vya Waandishi wa habari Tanzania (UTPC) Bw. Kenneth Simbaya, akishiriki kwenye kongamano la siku moja lilioandiliwa kuadhimisha Uhuru wa vyombo vya Habari Duniani 2014 lililofanyika jijini Arusha.
DSC_0281
Picha juu na chini Baadhi ya washiriki wakichangia maoni yao kwenye kongamano la siku moja lilioandiliwa kuadhimisha Uhuru wa vyombo vya Habari Duniani 2014 lililofanyika jijini Arusha.
DSC_0322
DSC_0214
Kongamano la siku moja lilioandiliwa kuadhimisha Uhuru wa vyombo vya Habari Duniani 2014 likiendelea.
DSC_0164
Mwanakamati wa maandilizi ya maadhimisho ya Kongamano la Uhuru wa Vyombo vya Habari Duniani 2014, Usia Nkhoma Ledama wa Kitengo cha Habari cha Umoja wa Mataifa (UNIC), akibadilishana mawazo na Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri (TEF), Absalom Kibanda nje ya ukumbi wa Kimataifa wa mikutano wa AICC jijini Arusha.

*BREAKING NEEEEZZZ!!!! MILIPULO KADHAA YAUA NA KUJERUHI MJINI MOMBASA

$
0
0
 Mlipuko kadhaa imetokea mjini Mombasa nchini Kenya, ambapo imedaiwa walipuaji wamelipua sehemu tatu tofauti.
Akizungumza kutoa taarifa za tukio hilo Kamishna wa kaunti ya mombasa Nelson Marwa, amesema kuwa waliotekeleza shambulizi hilo huenda wametoroka wakitumia piki piki.

Aidha amesema kuwa watu 3 wamefariki kutokana shambulizi hilo la guruneti, huku mlipuko mwingine ukishuhudiwa katika eneo la Nyali Reef, lakini hakuna majeruhi.

Ikumbukwe kuwa shambulizi hili linajiri siku chache tu baada ya mlipuko mwingine kushuhudiwa jijini Nairobi katika kituo cha polisi cha Pangani ambapo watu 4 wakiwemo maafisa 2 wa polisi walifariki.

Msemaji huyo amesema kuwa maafisa wa polisi  tayari wameanza kuwasaka washukiwa wa matukio hayo.
Repoti kutoka Shirika la Msalaba mwekundu, inasema kuwa waliofariki ni watu watstu akiwamo mwanamke mmoja na wanaume wawili.

Wwalijeruhiwa 25,kwa sasa waliojeruhiwa wanaendelea na matibabu ikiwa ni pamoja na xray na ukaguzi mwengne.vioñgozi wa kaunti wa msa wamefika.
Majeruhi wakipatiwa matibabu.
Baadhi ya mashuhuda wa tukio hilo wakiwa eneo la tukio.
Majeruhi.....akihudumiwa.
Majeruhi....
Majeruhi...
Mmoja kati ya watu waliopoteza maisha katika tukio hilo.

*MLIPUKO MWINGINE JIJINI NAIROBI

$
0
0
Baada ya milipuko iliyotokea jana mjini Mombasa mwingine umetokea jijini Nairobi jana na kujeruhi watu kadhaa.

*NAPE ALIPOHUTUBIA WAKAZI WA GOMBANI PEMBA, KINANA AWASAMBARATISHA UKAWA

$
0
0

Kinana akiwahutubia wananchi wa mjini Zanzibar jana, 
Wananchi wakishangilia na kuonesha vidole kuunga mkono serikali mbili za Muungano wakati wa mkutano wa hadhara wa CCM leo kwenye viwanja vya Kibandamaiti mjini Zanzibar.Mkutano huo uliudhuriwa na viongozi mbalimbali  akiwemo Katibu Mkuu Abdulrahman Kinana.
 Mama Fatma Karume akihutubia katika mkutano huo na kukemea Ukawa wanaotaka kuuvunja Muungano kwa kutaka Serikali Tatu katika mabadiliko ya Katiba mpya.
 Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrhman Kinana akimpongeza Mjane wa Hayati Abeid Amani Karume, kwa hotuba yake nzuri katika mkutano huo.
 Wananchi wakishangilia katika mkutano huo hasa baada ya Mjumbe wa NEC, Mohamed Seif Khatib kumuelezea Katibu Mkuu wa CUF, Seif Sharif Hamad kuwa na tabia ya kinyonga  kuhusu suala la Muungano, ambapo awali alikuwa muuminji Muungano wa Serikali tatu, mara wa mkataba na sasa anataka Serikali tau
 Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Nape Nnauye akimpongeza Mohamed Seif Khatibu kwa hotuba yake nzuri/
 Mjumbe wa Bunge la Katiba, Hamza Hassan Juma akielezea kwenye mkutano huo kuhusu mambo mbalimbali yaliyokubaliwa kuwekwa kwenye Katiba  Mpya ili kupunguza kero mbalimbali za wazanzibari kwenye Muungano.
 Mjumbe wa Bunge la Katiba, Steven Wassira akiwaeleza wana Ukawa kuwa hawawezi kutenganisha Muungano na Mapinduzi ya Zanzibar kama ilivyo uhusiano wa Uhuru wa Tanganyika na Muungano
 Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar,  Balozi Ali Seif Idd akihutubia katika mkutano huo na kupendekeza UKAWA kufutwa kwa vile haina uhalali wowote akidai kuwa si chama kwani haina usajili. Alisema kuwa Ukawa imeundwa kwa lengo la kuuvunja Muungano uliodumu kwa miaka 50 na kudumisha amani na umoja kwa Tanzania.
 Kinana akihutubia katika mkutano huo na kutamka kuwa CCMitasimia kidete kuhakikiasha uchumi wa Zanzibar unaimarika.
 Kinana na viongozi wengine wakiuombea dua muungano wa Tanzania pamoja viongozi waanzilishi wa muungano huo ambao ni Julius Nyerere na Abeid Karume
 Mbunge wa Mtera, Livingstone Lusinde  akikemea kitendo cha viongozi wa UKAWA kungea uongo na tabia ya kuwakejeli waasisi wa Muungano wa Tanzania.
 Mjumbe wa Bunge la Katiba,Asha Bakari Makame akimchana chana Katibu Mkuu wa CUF, Seif Sharif Hamad kwa tabia yake ya kinyonga kuhusu muundo wa Muungano.

 Mamboo poa/
 Mjumbe wa Bunge la Katiba, Ummy Mwalimu akielezea jambo kuhusu mwenendo usi faa wa UKAWA  kukimbia vikao vya bunge hilo
 Mjumbe wa Bunge la Katiba Emmanuel Nchimbi akinukuuu kwenye kitabu kilichotungwa na Maalim Seif Sharif Hamad kinachopinga Muungano

*VIWANJA VYA NYAMAGANA MWANZA NA KAITABA BUKOBA KUWEKWA VYASI BANDIA

$
0
0
Uwanja wa Nyamagana Mwanza unavyoonekana kwa sasa, ambao ni mmoja kati ya viwanja viwili vinavyotarajia kuwekwa nyasi bandia.
*****************************************
Mtaalamu wa nyasi bandia kutoka Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu (FIFA), Ian McClemen amewasili nchini leo alfajiri (Mei 4 mwaka huu) ambapo atakuwepo kwa siku tatu.

McClemen ameondoka leo (Mei 4 mwak huu) kwenda Bukoba ambapo atakagua Uwanja wa Kaitaba, na kesho (Mei 5 mwaka huu) atakwenda jijini Mwanza kukagua Uwanja wa Nyamagana.

Viwanja hivyo vinawekwa nyasi bandia kwa ufadhili wa FIFA chini ya mpango wa misaada wa Goal Projects. Baada ya ukaguzi huo, McClemen atatuma ripoti yake FIFA ili shirikisho hilo liweze kuteua mkandarasi wa kufanya kazi hiyo.

Kwa Tanzania viwanja vilivyowekwa nyasi bandia hadi sasa kupitia Goal Project ni Uwanja wa Uhuru uliopo Dar es Salaam, Uwanja wa Karume (Dar es Salaam) na Uwanja wa Gombani uliopo Pemba.

*MYWEATHER ALIPOSHUHUDIWA NA KINA MATUMLA,CHEKA, KALAMA AKISHINDA KWA POINTI

$
0
0
Marcos Maidana punches as Floyd Mayweather Jr. defends during their fight at MGM Grand.
Bondia Floyd Myweathe (kushoto) akipangua ngumi ya Marcos Maidana,
wakati wa pambano lao lililochezwa alfajili ya kuamkia jana. PointI za majaji, Judge Michael Pernick Scored  114-114, ambazo ni droo. Bert Clements alitoa pointi 117-111 na Dave Moretti, alitoa 116-112.
Floyd Mayweather Jr. punches Marcos Maidana during their fight at MGM Grand.
Bondia Floyd Myweather kushoto akioneshana umwamba wa kumshambulia, Marcos Maidana wakati wa pambano lao.
Marcos Maidana defends against Floyd Mayweather Jr. during their fight at MGM Grand.
Bondia Floyd Myweather (kushoto) akidundana na Marcos Maidana.
Mabondia Rashid Matumla kushoto,Fransic Cheka na Kalama Nyilawila wakifuatilia pambano la Myweather na Maidana kupitia luninga katika ukumbi wa Igo Lounge Sinza, usiku wa kuamkia jana.

*SHINDANO LA MISS DAR CITY CENTER KUFANYIKA MEI 24

$
0
0
Na Mwandishi Wetu
SHINDANO la Miss Dar City Center limezinduliwa rasmi jana na linatarajiwa kufanyika mei 24 kwaka huu katika ukumbi ambao utatangazwa baade, huku likishirikisha warembo 15.

Akizungumza katika uzinduzi huo jana, mratibu wa shindano hilo, Judith Charles alisema kuwa, mwaka huu shindano hilo litambapwa na vionjo tofauti tofauti ili kulifanya kuwa la aina yake.

Judith alisema kwamba, wameangalia changamoto zilizotokea kwa waandaaji wa waliopita wa shindano hilo, ili kuweza kulifanya kuwa na ubora wa hali ya juu zaidi kuliko ilivyowahi kutokea.

“Tumetumia changamoto ya waandaaji waliopita wa shindano hili na sisi tumeamua kuliboresha zaidi na hivyo tunaamini kabisa kwamba litakuwa katika kiwango cha juu zaidi tofauti na uilivyokuwa hapo mwanzo,” alisema Judith.

Aidha aliongeza kusema kwamba, ana aimani kubwa kwamba Miss Dar City Center ndiko atakakotokea Miss Tanzania 2014, kwani wamejiandaa kwa ukamilifu wa hali ya juu.

Judith alisema kwamba ana imani kubwa na matron ambaye pia ndie mwalimu wa warembo wa shindano hilo, Eshe Rashid kuwa atawapa mafunzo mazuri zaidi yatakayowezesha kuwa bora zaidi jukwaani.

Pia aliongeza kusema kwamba, zawadi kwa washindi wa shindano hilo zitakuwa zimeboreshwa zaidi na hivyo ana imani zitavutiwa zaidi na warembo hao.

Aidha Judith alisema, shindano hilo kwa kiasi kikubwa linafadhiliwa na  Prima, Zanzi, Sky light band, Clouds FM, Dimond Bureu De Change LTD, gazeti la Jambo leo, Klabu Maisha ambako warembo wanafanyia mazoezi, blog ya Sufianimafoto, blog ya Father Kidevu, Hoteli ya JB Belmont na Machapta Production.

*MSAJILI WA VYAMA VYA SIASA ATAKIWA KULIANGALIA KWA JICHO LA TATU KUNDI LA UKAWA

$
0
0
Mjumbe wa Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Taifa ya Chama Cha Mapinduzi Balozi Seif Ali Iddi akizungumza katika mkutano wa hadhara wa uwanja wa Demokrasia uliopo Kibanda maiti Mjini Zanzibar.
Picha na Hassan Issa wa – OMPR – ZNZ.
*****************************************************
Msajili wa Vyama vya Siasa Nchni Tanzania ameombwa kuliangalia kwa umakini kundi linalojiita Umoja wa Katiba ya Watanzania { UKAWA } lilioamua kuenesha mikutano ya hadhara inayoashiria mfumo wa kisiasa bila ya kuzingatia taratibu za kisheria zinazofuata usajili rasmi.
Ombi hilo limetolewa na Mjumbe wa Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Taifa ya Chama cha Mapinduzi Balozi Seif Ali Iddi wakati akisalimia kwenye mkutano wa hadhara wa CCM uliofanyika katika Uwanja wa Demokrasia Kiband Maiti Mjini Zanzibar.
Balozi Seif ambae pia ni Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar alisema kundi hilo lililoundwa na baadhi ya Viongozi wa juu wa vyama vyasKisiasa vya Upinzani limeshindwa kutekeleza kazi waliyotumwa na Wananchi ya kutengeneza mfumo wa kupata Katiba mpya kupitia Bunge Maalum la Katiba.
Alisema kitendo cha Viongozi hao ambacho kinawakosesha wananchi lile wanalolihitaji kinafaa kiangaliwe kwa umakini na msajili wa vyama vya siasa kwa vile kinaweza kuwakosesha wananchi hao muda wao wa kushughulikia mahitaji yao ya Kimaendeleo na kujikita zaidi katika mikutano hiyo yenye ushawishi zaidi wa kisiasa.
Balozi vSeif aliwatahadharisha wana CCM na Wananchi wote kujiepusha na kundi hilo ambalo limekuwa likichukuwa kodi zao bila ya kutekeleza majukumu waliyo wakabidhi.
“ Kama kweli wana uchungu na nyinyi wananchi mbona walisubiri kwanza kutia mfukoni mkwanja { posho } halafu ndio wakaingia mitini kuvikimbia vikao vya Bunge Maalum kwa kujenga hoja “. Alisema Balozi Seif.
Mjumbe huyo wa Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM aliwaonya wale viongozi wa siasa wenye tabia ya kumsakama katika majukwaa ya kisiasa kuachana na tabia hiyo mara moja kwa vile wengi kati yao anawaelewa udhaifu wao wa Kisiasa.
Alisema endapo kama viongoz hao wataendelea na hulka hiyo waelewe kwamba muda si mrefu atalazimika kufichua maovu na aibu zao.

*WANAKIJIJI WA MASANGANYA KISARAWE WAMTIMUA MWENYEKITI WAO WA KIJIJI

$
0
0
Askari Polisi akiwatuliza wanakijiji wa kijiji cha Masanganya Wilaya ya Kisarawe Mkoa wa Pwani, jana baada ya hatua walizozichukua za Kumfukuza Mwenyekiti wa Kijiji hicho, Rajabu Iddi  juzi kutokana na ubadhilifu wa matumizi mabaya na kutumia vibaya madaraka yake wakati wa Mkutano na Viongozi wa Wilaya ya Kisarawe. Picha na Jumanne Juma.

* AFRICA IS CALLING - TUBINGEN INTERNATIONAL AFRICAN FESTIVAL-GERMANY 2014 - OUT NOW!

$
0
0
Dear  Africans, friends, lovers and well-wishers of Africa,

The Lord Major of Tübingen University community –Boris Palmer and its community, the president of chamber of commerce and industry and its investors in Africa, join the African Diaspora in Germany, to welcome thousands of visitors with different backgrounds, culture, status and interest  from 17 – 20 July 2014 – friends, lovers and well-wishers of Africa, Business partners, Investors, celebrities, African Ambassadors and Diaspora worldwide - 4days NONSTOP at the African- Village –Festplatz in Tübingen - Thursday 17th to Sunday 20th July 2014

ENOUGH IS ENOUGH - Africa´s image in Germany has been jeopardized, characterising the continent of Africa with catastrophes, hunger, poverty, corruption and diseases ONLY, reducing the integrity of Africa, a limitation for children and youths in our communities to discover and enjoy the benefits that AFRICA has to offer.  Tübingen International African Festival organized and presented by the African Diaspora, share and present to you the true story of their different countries, values, potentials, business opportunities, tourist attractions as well as institutions with experience in dealing with different countries of Africa.

Tübingen International African Festival, powered by AFRIKAKTIV e.V – Founder & Projectmanager – Susan Tatah backed by the African Diaspora and its Ambassadors in Germany, aim at changing and redefining African narratives in Germany.

2014 Tübingen Africa Festival Campaigns & Memorial:  MALARIA NO MORE, STOP RIVERBLINDNESS  &  Kwibuka 20 –WE REMEMBER RWANDA!

This festival gathers African Diaspora in Germany together, irrespective of their countries of origin, religious, status and gender to brand, present and promote the 54 African countries through partnership, networking, contacts and more

Registration open is to all sectors with focused on Africa – Dateline  June 30th 2014

Online register now to participate just a click on this link

VISIT:  www.afrikafestival.net  / CALL + 49 152-106-10374 - 24/7 service line

Susan Tatah – Founder & CEO – be the change you want to see in Germany today!

AFRIKAKTIV e.V- CONNECTING THE FUTURE


*CDA YABOMOA ZAIDI YA NYUMBA 65 MANISPAA YA DODOMA

$
0
0
 Tingatinga la Mamraka ya ustawishaji makao makuu [CDA] likibomoa moja ya nyumba zilizopo katika hifadhi ya Barabara inayotarajiwa kuanza kujengwa havi karibuni, ambapo zaidi ya nyumba 65 zilibomolewa katika eneo hilo la mlamwa kusini.
 Wanawake wa mtaa wa Mlimwa wakimsaidia Mwenzao aiyezilai baada ya Tingatinga la CDA kufika kwa ajili ya kubomoa nyumba yake kwa ajili ya kupisha ujenzi wa Barabara, zoezi hilo lilifanyika Jana ambapo nyumba zaidi ya 65 zilibomolewa na kuacha familia zaidi ya 150 zikikosa makazi.
 Mwenyekiti wa mtaa huo Zubeda Haji akielekeza jambo wakati wa ubomoaji huo.
 Wananchi wa Mlimwa waking'oa mabati muda mfupi kabla ya Tinga tinga la CDA kufika na kuibomoa nyumba hiyo ili kupisha hifadhi ya Barabara
  Bibi huyu mkazi wa Mlimwa Kusini ambaye hakufahamika jina lake akiwa hajui la kufanya baada ya nyumba yake aliyokuwa akiishi iliyojengwa kwa mtindo wa Tembe huku akiachwa na vyombo vyake alivyoweka kwenye shamba la mahindi baada ya CDA kufanya uvunjaji huo kwa nyumba zote zilizopo katika hifadhi ya Barabara.
Wananchi wa Mlimwa kusini wakiwa katika hekaheka ya kuhamisha mizigo yao na kukimbia nyumba zao baada ya kupata taarifa za ujio wa Tinga tinga la CDA kwa ajili ya kubomoa nyumba zao ili kupisha ujenzi wa barabara.PICHA NA JOHN BANDA 

*MKE ALALAMIKA KUVURUGIWA NDOA YAKE NA ANAYEDHANIWA NI LULU, ANGALIZO: WAREMBO WANAOTUMIA MAJINA NA PICHA ZA MASTAA KATIKA PFOFILE ZAO NA KUSAJILI KATIKA HUDUMA ZA TIGO PESA

$
0
0
 "Ni  muda  mrefu  nimekuwa  nikifuatilia  mienendo  ya  mume  wangu  kutokana  na  tabia  yake  kubadilika  sana  siku  za  hivi  karibuni, nikabaini  kuwa  kuna  msichana  anawasiliana  naye  kwa  kutumiana meseji  za  mapenzi, sikuwa  na  haraka  nikaamua  kufanya  uchunguzi  wangu  kimyakimya"
"Wiki  iliyopita  mume  wangu  akiwa  amekwenda  kuoga  akasahau  kuzima  simu  yake,na  siyo  kawaida  yake  kuacha  simu  yake  bila  kuizima,mara  meseji  ikaingia,nikaangalia  nikaona  jina  la  mtumaji amesevu  Lulu, moyo  ukalipuka"
Ndivyo  alivyoanza  kuongea  mama  mmoja  wa  makamo  anayefanyakazi  katika  ofisi  moja  nyeti  katikati  ya  jiji  la  Dar  alipokuja  kuongea  na  mwandishi  wetu  wiki  iliyopita  baada  ya  ndoa  yake  kuingiliwa  na  mdudu  mbaya....
Akiongea  kwa  masikitiko  makubwa, mama  huyo  ambaye  hakupenda  kutaja  jina  lake  kutokana  na  unyeti  wa  kazi  anayoifanya, alidai  kuwa  msichana  huyo  anayetaka  kuiharibu  ndoa  yake  yenye  miaka  25  jina  lake  ni  Elizabeth  Michael....
Mama  huyo  alidai  kuwa  jina  hilo  alilibaini  baada  ya  kukuta  meseji  za  mapenzi  kwenye  simu  ya  mume  wake  na  yeye  kuamua  kuifuatilia  namba  hiyo  kwa  kufanya  kama  anataka  kumtumia  pesa  msichana  huyo  na  kukugundua  jina  hilo....
Akiongea  kwa  upole, mama  huyo  alidai  kuwa katika  simu  ya  mume  wake, jina  la  mtumaji  lilikuwa  Lulu, lakini  alipofanya  uchunguzi  wake  wa  kujifanya  kama anatuma  pesa  kwa  namba  ya  msichana  huyo  ndipo  alipobaini  kuwa  mmiliki  wa  namba  hiyo  ni  Elizabeth  Michael...
Mwandishi  alimuuliza  mama  huyo  kama  anadhani  kuwa  msichana  huyo  anayetaka  kuiharibu  ndoa  yake  ni  muigizaji  maarufu  wa  filamu  hapa  nchini Elizabeth  Michael  "Lulu", lakini  alikataa  kuthibitisha  hilo  kwa  madai  kuwa  tangu  siku  hiyo  namba  ya  binti  huyo  imekuwa  haipatikani....
"Baada  ya  kugundua  siku  ile ,  nilichukua  simu  yake  na  kutaka  kuwasiliana  naye  ili  niweze  kumuonya  mwenyewe  kimyakimya  kwa  wakati  wangu, wala  sikuwa  na  lengo  la  kuja  kwenye  vyombi  vya  habari , lakini  sikuwahi  kumpata  hewani  tena  kila  nilipojaribu  kumpigia"Alisema  na  kuongeza:
"Huenda  mume  wangu  alishtikia  kuwa  nimeona  ujumbe  ule, kwa  sababu  mimi  nilipoisoma  meseji  ile  sikuifuta, ili  akiona  meseji  imesomwa  aelewe  nimeshajua  kila  kitu, pengine  ndiye  aliyemwambia  binti  huyo  abadili  namba  yake"
Mwandishi  alimuomba  mama  huyo  ampatie  namba  ya  huyo  msichana  ili  kuweza  kujua  kama  ni  Lulu  muigizaji  ama  siyo ( mwandishi  anazijua  namba  zote  za  Lulu ), lakini  namba  hiyo  ni  tofauti  na  anazotumia  Lulu  Mwenyewe....
Mwandishi  alipojaribu  kama  kumtumia  pesa  msichana  huyo, jina  lililotokeza  ni  Elizabeth Michael, na  alipojaribu  kuipiga  namba  hiyo  ilikuwa  haipatikani  hewani....
Juhudi  za  kumsaka  Lulu   ili  kuona  kama  anaitambua  namba  hiyo  hazikuzaa  matunda  kutokana  na  namba  zake  mbili  kutopatikana  na  nyingine  ikiita  bila  kupokelewa....

ANGALIZO:
Baadhi  ya  wasichana  wa  mjini  wamekuwa  wakitumia  majina  ya  wasanii  maarufu  katika  nyendo  zao  ili  kuwatapeli  watu. Miongoni  mwa  njia  wanazotumia  ni  pamoja  na   kujisajili  kwenye  mitandao  ya  kijamii  kwa  majina  ya  watu  maarufu  ili  kuwatapeli  watu.

*NAPE NNAUYE ALIPOHUTUBIA VIWANJA VYA KIANDA MAITI ZANZIBAR

Viewing all 13053 articles
Browse latest View live


<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>