Quantcast
Channel: SUFIANIMAFOTO
Viewing all 13053 articles
Browse latest View live

*KAMPUNI YA PR PROMOTION YATAMBULISHA MISS REDDS MBAGALA 2014.

$
0
0
 Afisa Habari Kampuni ya PR Promotion Bw. Victor Mkumbo (kushoto) akitoa maelezo mbele ya waandishi wa Habari (hawapo pichani) kuhusu utambulisho wa Miss Redds kwa Kitongoji cha Mbagala kwa mwaka 2014. Katikati ni Mratibu wa Kampuni hiyo Bw. Tesha Japhet na kulia ni Meneja wa Kampuni ya PR Promotion Bw. Gervas Sinsakala.
 Baadhi ya warembo watakaoshirki kinyang’anyiro hiko wakiwa wamepozi wakati wa utambulisho wao katika Mkutano na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya Waandishi wa Habari walioshiriki katika Mkutano wakisikiliza na kupiga picha mbalimbali kuhusu utambulisho wa Miss Redds kwa Kitongoji cha Mbagala kwa mwaka 2014.
****************************************************
Na Benedict Liwenga-Maelezo.
KAMPUNI ya PR Promotion inatarajia kuleta kitongoji kipya katika mashindano ya Urembo Tanzania kupitia Wilaya ya Temeke ambayo ni Miss Mbagala kwa mwaka 2014.
Hayo yamesemwa leo na Mratibu wa Kampuni hiyo Bw. Tesha Japhet wakati wa Mkutano na Waandishi wa Habari katika Ukumbi wa Habari Maelezo leo jijini Dar es Salaam uliohusu tambulisho wa Miss Redds Mbagala kwa mwaka 2014.
“Hii ni mara ya kwanza kitongoji cha Mbagala kuandaa mashindano ya Miss Tanzania baada ya kuongezwa na Kamati ya Redds Miss Tanzania mwaka huu, hivyo wilaya ya Temeke itakuwa na vitongoji vine ambavyo ni Chango’mbe, Kurasini, Kigamboni na Mbagala”. Alisema Japhet.
Bw. Japhet ameongeza kuwa washindi watatu wa mwanzo katika mashindano hayo watashiriki moja kwa moja katika mashindano ya Miss Redds Temeke 2014.

Mashindano hayo ya Miss Mbagala 2014 yatajumuisha jumla ya washiriki 16 kutoka maeneo mbalimbali ya Mbagala na majina yao ni Amina Salim (20), Aquilina Paul (22), Restuta Charles (21), Suzan Paul (19), Natalia Rohath (22), Grace John (20), Neema Roman (19), Lucrecia Mushi (20), Subira Ally (23), Lucy Lyombo (20), Joyce Mkandila (20), Lulu Baraka (22), Macklina Robert (21), Sylivia Robert (24), Esther Mnahi (20) na Maureen Msangi (20).

Aidha, Warembo wote watatambulishwa rasmi siku ya Ijumaa ya tarehe 9 Mei, 2014 sambamba na uzinduzi rasmi wa Miss Mbagala 2014 utafanyika katika Ukumbi wa Dar Live uliopo Mbagala jijini Dar es Salaam kuanzia majira ya saa 2 usiku.
PR Promotion ni Kampuni ya burudani iliyosajiriwa na BASATA tangu mwaka 2009 imekuwa ikifanya maonesho mbalimbali ya sanaa ikiwemo urembo pamoja na kuendesha mikutano na waandishi wa habari na inajihusisha na upigaji picha za mnato na video katika matukio mbalimbali.

*BALOZI LIBERATA MULAMULA AHUDHURIA ONESHO LA PICHA ZA KUCHORA LA JAMBO, TANZANIA

$
0
0

Mariam Osher Mmarekani mchoraji aliyetembelea mbuga za wanyama Tanzania na kubuni uchoraji wa wanyama aliowaona huko Tanzania na kutumia michoro hiyo kuitangaza Tanzania kwa Wamarekani na raia wengine ambao wajawahifika Tanzania kwenye maonesho ya picha zake yaliyofanyika leo Silver Spring, Maryland kwenye ukumbi wa WPG uliopo 8230 Georgia Ave.

Mhe. Liberata Mulamula , Balozi wa Tanzania nchini Marekani (wapili toka kulia) akiwa pamoja na Afisa wa Ubalozi kitengo cha Utalii Bi. Immaculata Diyamett wakifuatilia maelezo ya Marian Osher.

Balozi Liberata Mulamula pamoja na Afisa Immaculata Diyamett wakifuatilia maelezo ya Marian Osher
Juu na chini ni watu mbalimbali waliofika kwenye onesho hilo la Marian Osher.


Mhe. Balozi Liberata Mulamula akitoa shukurani zake kwa Marian Osher huku akiongea na watu waliofika kwenye onesho hilo kuwaelezea vivutio vilivyopo kwenye mbuga zetu za wanyama.

*MAMA SALMA KIKWETE AHUDHURIA SHEREHE ZA KILELE CHA SIKU YA WAKUNGA DUNIANI, JIJINI DAR

$
0
0
 Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akisalimiana na Ndugu Clavery Mpagama mara baada ya kuwasili Mnazi Mmoja kuhudhuria kilele cha siku ya wakunga duniani leo tarehe 5.5.2014.
 Maandamano ya wakunga yakipita mbele ya mgeni rasmi mke wa rais Mama Salma Kikwete, wakati wa kilele cha siku ya wakunga duniani yaliyofanyika katika viwanja vya Mnazi Mmoja, jijini Dar es Salaam, leo. 
 Maandamano yakipita mbele ya jukwaa kuu.
 Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akipokea maandamano ya wakunga wakati wa kilele cha siku ya wakunga duniani yaliyofanyika katika viwanja vya Mnazi Mmoja.
 Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akimsalimi mtoto Rahim mwenye umri wa miezi 2 akiwa na baba yake ndugu Amir Adam, 35, na mama yake Hamida (kushoto) walipompeleka kupata chanjo wakati wa sherehe za kilele cha siku ya wakunga duniani iliyoadhimishwa kitaifa katika viwanja vya Mnazi Mmoja.
 Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akitembelea mabanda mbalimbali yaliyokuwa yakitoa huduma ya afya ya mama na mtoto wakati wa kilele cha cha sherehe za siku ya wakunga duniani iliyoadhimishwa kitaifa mkoani Dar es Salaam.
 Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akitembelea mabanda mbalimbali yaliyokuwa yakitoa huduma ya afya ya mama na mtoto wakati wa kilele cha cha sherehe za siku ya wakunga duniani iliyoadhimishwa kitaifa mkoani Dar es Salaam.
  Wakunga mbalimbali na wananchi wakifurahia wakati wa maadhimisho hayo. 
Mke wa Rais akiwa katika picha ya pamoja na viongozi wa Chama cha Wakunga Tanzania na baadhi ya wakunga waliohudhuria sharehe za kilele cha siku ya wakunga duniani. Picha na John Lukuwi

*DART KUANZA KUTOA HUDUMA MAPEMA MWAKANI

$
0
0
 Meneja usimamizi wa Barabara toka Wakala wa mabasi yaendayo haraka (DART) Mhandisi Mohamedi Kaganda (kulia) akielezea kwa waandishi wa Habar (hawapo pichani) leo  Jijini Dar Es Salaam namna mabasi hayo yatakavyofanya safari zake mara  awamu ya kwanza ya mradi huo itakapoanza mapema mwakani , Kushoto ni Afisa Habari wa Idara ya Habari Maelezo Frank Mvungi.
 Meneja Uhusiano Mradi wa mabasi yaendayo haraka (DART) Bw. William Gatambi (kushoto) akiwaeleza  waandishi wa habari leo Jijini Dar es Salaam katika ukumbi wa Idara ya Habari Maelezo kuhusu  maendeleo ya mradi huo ambao awamu ya kwanza itakamilika mwishoni wa mwaka huu. Kulia ni Afisa Habari wa Idara ya Habari Maelezo Frank Mvungi.
 Meneja uendeshaji wa DART  Bw.Peter Munuo  akieleza kwa waandishi wa habari kuhusu faida za mradi  huo ikiwemo kuondoa tatizo la foleni katika jiji la Dar es salaam na viunga vyake.mara  mradi huo  utakapoanza mapema mwakani.Picha na Georgina Misama
 ***********************************************
Na Frank Mvungi- Maelezo
Serikali inatarajia kuanza kutoa huduma za awali (interim services) katika mradi wa Mabasi yaendayo Haraka (DART) Kutoka Kimara mwisho hadi Kivukoni jijini Dar es salaam mwaka 2015 baada ya miundombinu kukamilika.
Hayo yamesemwa na Meneja Uhusiano wa Wakala wa mabasi yaendayo haraka (DART) Bw.William Gatambi  wakati wa mkutano na waandishi wa habari leo jijini Dar es salaam.
Gatambi alisema kuwa mara baada ya kukamilika kwa miundo mbinu ya mradi huo awamu ya kwanza mwishoni mwa mwaka 2014 itasadia kufanikisha usafiri wenye tija kwa wakazi wa jiji la Dar es salaam na vitongoji vyake.
Miundombinu hiyo, inajumuisha barabara ya kilomita 20.9 kuanzia Kimara Mwisho hadi Kivukoni,Barabara ya Kawawa kutoka Morocco hadi Magomeni na Barabara ya Msimbazi hadi eneo la Gerezani Kariakoo.
 Aliongeza kuwa ina vituo vidogo 27,vituo vikuu vitano, vituo mlisho vine na karakana mbili. Pia inajumuisha njia za waenda kwa miguu na baiskeli.
Akifafanua Gatambi alisema mradi wa majaribio utaanza na mabasi 20 yatakayokuwa na uwezo wa kuchukua abiria kati ya 145 hadi 160 kwa wakati mmoja hali itakayosaidia kuondoa kabisa kadhia ya usafiri kwa wakazi wa jiji la Dar es salaam.
Aidha, katika mradi huo wa majaribio Gatambi amesema kutakuwa na mabasi mengine 10 yenye uwezo wa kuchukua abiria kati ya 50 na 60 ambayo yatatumika kuchukua abiria kutoka pembezoni mwa jiji la Dar es salaam kuja katika vituo vikuu vya mabasi yaendayo Haraka.
Kwa upande wakeMeneja Usimamizi wa Barabara wa DART Mhandisi Mohamed Kuganda amesema mradi huo utasaidia kuondoa tatizo la foleni Jijini Dar es salaam na kuwafanya wananchi kupata huduma ya usafiri yenye kukidhi viwango vya Kimataifa.
Pia Kuganda alisema DART kwa kushirikiana na Halmashauri za Jiji la Dar es salaam inafanya maandalizi ya kuboresha barabara mlisho (feeder roads) katika maeneo yatakayotumiwa na mabasi mlisho.

Katika mradi wa mabasi yaendayo haraka kutakuwa na Vituo Vikuu (terminals) vitano 5 katika, maeneo ya Kimara, Ubungo, Morocco, Kariakoo na Kivukoni ambapo vituo hivi ndiko mabasi yatakapokuwa yanaanzia na kumalizia safari kubadilishana abiria kati ya njia kuu na njia mlisho (feeder roads) ambapo vituo hivyo vikubwa vinatoa nafasi ya kuweza kuanzishwa kwa huduma muhimu kwenye vituo hivyo kama maeneo ya kukatia tiketi na vyoo.

*TAARIFA KWA UMMA JUU YA UPOTOSHWAJI WA TAARIFA YA HALI YA HEWA

$
0
0
JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA WIZARA YA UCHUKUZI
       MAMLAKA YA HALI YA HEWA

                             TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

 YAH : UPOTOSHWAJI WA TAHADHARI YA HALI YA HEWA KUHUSIANA NA MVUA ZINAZOENDELEA KUNYESHA
Mamlaka ya Hali ya Hewa nchini inapenda kukanusha kuhusiana na taarifa ya ujumbe mfupi wa simu na katika mitandao ya kijamii wenye maneno yafuatayo : ‘TMA warning heavy rains of strong easterly winds 100km an hour expected to hit Dar coast from Somalia, Heavy rains 120mm above sea level expected today and tommorrow. People must avoid Sea and areas near to Sea should be alert cautioned. Tanzania Meteorological Agency  www.tma.gov.tz’   Mamlaka inapenda kuutaarifu umma kuwa taarifa hiyo siyo ya kweli  na ina  lengo la kupotosha umma na wala haijatolewa na Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania.
Mamlaka ina kuwakumbusha wananchi wote kuendelea kufuatilia taarifa zetu kupitia vyanzo husika vya Mamlaka vikiwemo utabiri wa kila siku utolewao kupitia radio, televisheni na tovuti ya Mamlaka (www.meteo.go.tz).

Taarifa sahihi za mwenendo wa mvua na tahadhari za hali mbaya ya hewa zinatolewa  na zinapatikana kupitia njia rasmi za utoaji taarifa maalum za kiofisi (official weather statement). Hivyo taarifa kuhusiana na mvua zinazoendelea imekuwa ikitolewa katika utabiri wa kila siku kupitia vyombo vya habari, mtandao wa kijamii  wa Mamlaka na tovuti ya Mamlaka.
Tunawatakia shughuli njema katika ujenzi wa Taifa letu.
Simu: +255 22 2460706-8

Telefax: +255 22 2460735, 2460700                                                                                             S.L.P.   3056,
Barua pepe: met@meteo.go.tz                                                                                         DAR  ES SALAAM
Tovuti: www.meteo.go.tz
                                                                                                                                05/05/2014

IMETOLEWA NA MAMLAKA YA HALI YA HEWA TANZANIA

*WABUNGE WAPYA RIDHIWANI KIKWETE NA GODFREY MGIMWA WAAPISHWA NDANI YA BUNGE LA BAJETI MJINI DODOMA

$
0
0
Mbunge Mpya wa Jimbo la Chalinze,Mh. Ridhiwani Kikwete akila kiapo Bungeni Mjini Dodoma,leo Mei 6, 2014.
Mbunge Mpya wa Jimbo la Kalenga,Mh. Godfrey Mgimwa akila kiapo 
Bungeni mjini Dodoma leo Mei 6, 2014.
Waziri Mkuu,Mh. Mizengo Pinda akimpongeza Mbunge Mpya wa Chalinze,Ridhiwani Kikwete baada ya kuapishwa, Bungeni Mjini Dodoma 
leo Mei 6, 2014.
Waziri wa Nchi,Sera na Uratibu wa Bunge,Mh. William Lukuvi akimpongeza Mbunge Mpya wa Chalinze,Ridhiwani Kikwete baada ya kuapishwa, Bungeni Mjini Dodoma leo Mei 6, 2014.
Spika wa Bunge,Mh. Anne Makinda na watendaji wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Wakiimba wimbo wa Taifa kabla ya shughuli za Bunge kuanza leo mei 6, 2014.
Mbunge Mpya wa Jimbo la Kalenga,Mh. Godfrey Mgimwa akisindikizwa na wabunge wa CCM kuingia Bungeni mjini Dodoma leo Mei 2014.
Mbunge Mpya wa Jimbo la Chalinze,Mh. Ridhiwani Kikwete akisindikizwa na wabunge wa CCM kuingia kwenye Ukumbu wa Bunge Mjini Dodoma, leo Mei 6, 2014.
Mke wa Rais,Mama Salma Kikwete akiwa Bungeni Mjini Dodoma Mei 6,2014 wakati mwanae,Ridhiwani Kikwete alipoapishwa. Kulia kwake ni Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Dkt. Rehema nchimbi.
Mke wa Rais,Mama Salma Kikwete na familia wakiwa Bungeni Mjini Dodoma leo Mei 6,2014 wakati mwanae,Ridhiwani Kikwete alipoapishwa . Kulia kwake ni Mkuu wa Mkoa wa Dodoma , Dkt. Rehema Nchimbi.Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu

*MAKAMU WA RAIS DKT. BILAL AFUNGUA MKUTANO WA MAZUNGUMZO BAINA YA VIONGOZI WA DINI MBALIMBALI NA WANASIASA KUHUSU UJENZI WA DEMOKRASIA, MAENDELEO UIMARISHWAJI WA AMANI, JIJINI DAR ES SALAAM.

$
0
0
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akihutubia wakati akifungua rasmi Mkutano wa siku mbili wa Mazungumzo baina ya Viongozi wa Dini mbalimbali na Wanasiasa kuhusu ujenzi wa Demokrasia, Maendeleo na uimarishwaji wa Amani ulioshirikisha nchi za Afrika na kufanyika kwenye Hoteli ya White Sands, jijini Dar es Salaam, leo.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisalimiana na Kadhi Mkuu wa Zanzibar, Sheikh Khamis haji, na baadhi ya viongozi wa dini wakati alipowasili kwenye Hoteli ya White Sands, jijini Dar es Salaam, leo Meo 6, 2014 kwa ajili ya kufungua rasmi Mkutano wa siku mbili wa Mazungumzo baina ya Viongozi wa Dini mbalimbali na Wanasiasa kuhusu ujenzi wa Demokrasia, Maendeleo na uimarishwaji wa Amani ulioshirikisha nchi za Afrika jijini Dar es Salaam.
 Baadhi ya wadau wa mkutano huo waliohudhuria, kutoka (kushoto) ni Wilfred Mlay, Dkt. Willibrod Slaa, Hellen Kijo-Bisimba na wengineo wakishiriki dua ya pamoja.
 Baadhi ya wadau wa mkutano huo waliohudhuria, kutoka (kushoto) ni Wilfred Mlay, Dkt. Willibrod Slaa, Hellen Kijo-Bisimba na wengineo wakishiriki dua ya pamoja.
 Baadhi ya wadau waliohudhuria mkutano huo, wakimsikiliza Makamu wa Rais wakati akifungua ramsi mkutano huo wa mazungumzo Mazungumzo baina ya Viongozi wa Dini mbalimbali na Wanasiasa kuhusu ujenzi wa Demokrasia, Maendeleo na uimarishwaji wa Amani ulioshirikisha nchi za Afrika na kufanyika kwenye Hoteli ya White Sands, jijini Dar es Salaam, leo.

 Baadhi ya wadau waliohudhuria mkutano huo, wakimsikiliza Makamu wa Rais wakati akifungua ramsi mkutano huo wa mazungumzo Mazungumzo baina ya Viongozi wa Dini mbalimbali na Wanasiasa kuhusu ujenzi wa Demokrasia, Maendeleo na uimarishwaji wa Amani ulioshirikisha nchi za Afrika na kufanyika kwenye Hoteli ya White Sands, jijini Dar es Salaam, leo.

 Askofu Dkt. Alex Malasusa, akizungumza wakati wa Mkutano huo.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiagana na baadhi ya washiriki wa mkutano huo baada ya kufungua mkutano huo katika Hoteli ya White Sands.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiagana na mmoja kati ya washiriki wa mkutano huo, Mwalimu wa Chuo Kikuu cha Kiislamu cha Morogoro, Prof. Juma Mikidadi, wakati akiondoka baada ya kufungua rasmi mkutano huo. leo jijini Dar es Salaam.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisalimiana na Katibu wa Chadema, Dkt. Willibrod Slaa, wakati wa kupiga picha ya pamoja baada ya kufungua rasmi Mkutano wa siku mbili wa Mazungumzo baina ya Viongozi wa Dini mbalimbali na Wanasiasa kuhusu ujenzi wa Demokrasia, Maendeleo na uimarishwaji wa Amani ulioshirikisha nchi za Afrika na kufanyika kwenye Hoteli ya White Sands, jijini Dar es Salaam, leo.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya washiriki wa mkutano huo.

Makamu wa Rais, Dkt. Bilal, akiongozana na baadhi ya viongozi wa dini, wakati akiondoka kwenye Hoteli ya White Sands baada ya kufungua mkutano huo.

*SIKILIZA CLIP HII YA NAPE KUNGURU HAFUGIKI NA BI AISHA BAKARI ZANZIBAR


*ANDIKENI HABARI ZA KUMKOMBOA MWANANCHI : JAJI BOMANI

$
0
0
DSC_0083
Mshehereshaji ambaye ni Mwanakamati ya maandilizi ya maadhimisho ya Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari Duniani 2014, Usia Nkhoma Ledama akiwatambulisha baadhi ya waandishi wa habari wakongwe (hawapo pichani) kwa mgeni rasmi Jaji Mstaafu Mark Bomani. Picha zote na Zainul Mzige.
***********************************
Na Mwandishi wetu
Jaji Mstaafu Mark Bomani amesema lengo la mchakato wa Katiba ni kuhakikisha kwamba Tanzania inapata Katiba ambayo ni bora zaidi kuliko zote itakayoshughulikia changamoto na kuweka mazingira ambayo yatamrahisishia maendeleo mwananchi kwa haraka.
Akitoa risala katika maadhimisho ya Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari Duniani leo katika ukumbi wa Kimataifa wa Mikutano wa AICC jijini Arusha, Jaji Mstaafu Mark Bomani, amesema jukumu la mwanahabari ni kuwaelimisha baadhi ya wabunge wa Bunge Maalum la Katiba ambao hawana uelewa mkubwa na mchakato wa Katiba hawajui maana halisi ya Katiba mambo ambayo yanasababisha kujadili Katiba hiyo kwa maneno mabaya, kutishiana, matusi na kejeli.
DSC_0171
Baadhi ya waandishi wa habari wakongwe (Ma-veterans) wakimsalimia mgeni rasmi.
“Zoezi la mchakato wa Katiba ni kubwa na wabunge wengi wa Bunge Maalum la Katiba hawaelewi wajibu wao katika kuijadili Katiba hiyo matokeo yake ndio hayo wanayoshuhudia Watanzania”.
Mara nyingi Watanzania wameshuhudia mijadala ya kejeli, malumbano, matusi, kudharauliana pale hoja zinapojengwa na upande ambao haukubaliki na upande mwingine jambo ambalo limewavunja moyo Watanzania na kutokuwa na imani ya kupata Katiba inayolenga kumlinda mwananchi.
Jukumu la wanahabari ni kutoa elimu ya kutosha kuhusu yaliyomo katika Katiba Mpya na kuandika habari za maendeleo ili majadiliano yatokanayo yawe endelevu yamtendee haki mwananchi wa kawaida kwa lengo la kuboresha maisha yao.
DSC_0077
Meza Kuu, kutoka kushoto ni Kaimu Mkurugenzi wa Shirika la Elimu, Sayansi na Mawasiliano ya Umoja wa Mataifa (UNESCO) Bw. Abdul Wahab Coulibaly, Mkurugenzi wa Mfuko wa Vyombo vya Habari Tanzania (TMF) Bw. Ernest Sungura, Mkuu wa Wilaya ya Arusha, Bw. John Mongela, Mgeni rasmi Jaji Mstaafu Mark Bomani, Mwenyekiti wa Taasisi ya Vyombo vya Habari Kusini mwa Afrika, Tawi la Tanzania (MISA-TAN), Bw. Mohamed Tibanyendera, Rais wa Umoja wa Vilabu vya Waandishi wa habari Tanzania (UTPC) Bw. Kenneth Simbaya na Meneja Utafiti na Ushapishaji wa Baraza la Habari Tanzania (MCT), Bw. John Mirenyi.
“Inasikitisha kuona kuwa hali ya Mtanzania inazidi kudidimia au kubaki pale pale katika sehemu nyingi hasa vijijini katika kipindi cha miaka 40 iliyopita kwa kukosa fursa muhimu za maendeleo na viongozi hawalioni hilo”, amesema Jaji Mstaafu Mark Bomani.
Wakati huo huo mgeni huyo rasmi amekemea tabia ya kuandika habari za kuwasifu viongozi na kupokea Rushwa hali iliyojitokeza katika miaka ya hivi karibuni na kusema kwamba ni fedhea kwa tasnia ya habari kutofuata maadili ya uandishi.
Amesema kwamba nchi itaendeshwa kwa kusimamia haki na ukweli na kuwataka wanahabari wasichoke kuisimamia haki na uhuru wa nchi yao bila woga kwani bila kufanya hivyo nchi itaongozwa kiimla.
DSC_0348
Mgeni rasmi Jaji Mstaafu Mark Bomani, akitoa risala wakati wa maadhimisho ya Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari Duniani 2014 yaliyofanyika kwenye ukumbi wa mikutano wa kimataifa wa AICC jijini Arusha mwishoni mwa juma.
“Kuna tabia ya vyombo vya habari ya vyombo vya habari kununuliwa ili visiandike au kufichua maovu ni fedhea kwani vyombo vya habari ni kioo cha jamii”.
Akizungumzia kuhusu sheria za habari za mwaka 2007 na 2008, Jaji Mstaafu amesema ni aibu kuona mswaada wa sheria ya habari umekwama kwa zaidi ya miaka 10 kwa sababu ambazo hadi leo hazijaeleweka.
Amewataka waandishi wa habari wasikate tamaa na badala yake waendelea na kupambana kuhakikisha kwamba harakati za kupata Sheria ya Haki ya Kujua inafanikiwa ili kupunguza matukio ya manyanyaso, kupigwa, kuteswa, kufungwa kwa vyombo vya habari na kuuwawa.
“Haki haiyombwi simamieni Haki zenu na songeni mbele”, ameongeza Jaji Bomani.
DSC_0429
Sehemu ya wadau wa tasnia ya Habari wakisikiliza risala ya mgeni rasmi.
DSC_0329
Mkuu wa Wilaya ya Arusha, Bw. John Mongela akizungumza kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa wa Arusha kwenye maadhimisho ya Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari Duniani yaliyofanyika jijini Arusha kenye ukumbi wa mikutano wa Kimataifa wa AICC.
DSC_0112
Mwenyekiti wa Taasisi ya Vyombo vya Habari Kusini mwa Afrika, Tawi la Tanzania (MISA-TAN), Bw. Mohamed Tibanyendera, akizungumza kwenye maadhimisho ya Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari Duniani 2014 yaliyofanyika kwenye ukumbi wamikutano wa Kimataifa wa AICC jijini Arusha.
DSC_0163
Wageni waalikwa na wadau wa tasnia ya habari wakiwa kwenye ukimya kumkumbuka Mwandishi aliyeuwawa mkoani Iringa Daudi Mwangosi.
DSC_0188
Mkurugenzi wa Shirika la Elimu, Sayansi na Mawasiliano ya Umoja wa Mataifa (UNESCO) Bw. Abdul Wahab Coulibaly, akitoa Ujumbe wa Pamoja wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa na Mkurugenzi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Maendeleo ya Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) Irina Bokovas kuhusiana na Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari Duniani 2014.
DSC_0217
Meneja Machapisho, Utafiti na Uhifadhi Hati wa Baraza la Habari Tanzania (MCT), Bw. John Mirenyi, akitoa maelezo ya machapisho mbalimbali yaliyoandaliwa na baraza hilo yakiwemo yenye madhila mbalimbali yaliwahi kuwakumba baadhi ya waandishi wa habari ndani na nje ya nchi.
DSC_0241
Mkurugenzi wa Mfuko wa Vyombo vya Habari Tanzania (TMF) Bw. Ernest Sungura, akizungumzia mchango wa mfuko huo unaowawezesha waandishi wa habari kutafuta habari za uchunguzi na zinazoigusa jamii.
DSC_0247
Wasanii wa Bendi ya Mrisho Mpoto (Mjomba Band) wakitoa burudani kwa wageni waalikwa wakati wa maadhimisho ya siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari Duniani 2014 yaliyofanyika jijini Arusha mwishoni mwa juma.
DSC_0156
Sehemu ya wadau wa tasnia ya habari wakifuatilia yaliyokuwa yakijiri ukumbini hapo.
DSC_0259
Katibu wa Chama cha Wamiliki wa Vyombo vya Habari nchini (MOAT), Henry Muhanika, akisoma hotuba kwa niaba ya Dr. Reginald Mengi kwenye maadhisho hayo.
DSC_0269
Rais wa Umoja wa Vilabu vya Waandishi wa habari Tanzania (UTPC) Bw. Kenneth Simbaya, akizungumzia wakati wa maadhimisho hayo.
DSC_0286
Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri (TEF), Absalom Kibanda, akizungumzia changamoto mbalimbali zinazowakumba waandishi wa habari wakati maadhimisho ya Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari Duniani 2014 yaliyofanyika jijini Arusha.
DSC_0288
Mkurugenzi wa TAMWA, Bi. Valerie Msoka, akizungumzia changamoto za usawa wa Kijinsia katika uongozi kwenye Vyombo vya Habari nchini.
DSC_0304
Meneja Uhusiano wa TANAPA, Pascal Shelutete, akizungumzia ushiriki wao kwenye Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari Duniani 2014 ambapo aliwataka waandishi wahabari kutumia kalamu zao vizuri katika kukuza Utalii wa Tanzania ndani na nje ya nchi.
DSC_0312
Meneja Uhusiano wa Hifadhi ya Taifa ya Ngorongoro, Bw. Adam Akyoo, akifafanua jambo wakati wa maadhimisho ya Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari Duniani 2014 ambapo amewataka waandishi wa habari kutumia nafasi yao katika kupambana na suala la Ujangili linaloendelea nchini.
DSC_0382
Mrisho Mpoto akiwafungua vitambaa wasaani wa Mjomba Bendi kama ishara ya kuwapa Uhuru waandishi wa Habari kuzungumza kilio chao mbele ya mgeni rasmi kama ujumbe wa Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari Duniani 2014.
DSC_0398
Mrisho Mpoto na Bendi yake akighani mashairi na kuelezea madhila wayapatayo waandishi wa habari wawapo kazini ikiwemo usalama wao katika kazi zao za kila siku.
DSC_0405
Makamu wa Rais wa Umoja wa Vilabu vya Waandishi wa habari Tanzania (UTPC), Jane Mihanji akimkaribisha mgeni rasmi Jaji Mstaafu Mark Bomani kuzindua Video mpya ya wimbo "Uhuru Wangu" wa Mrisho Mpoto uliokuwa kwenye Albamu yake mpya inayoitwa WAITE.
DSC_0414
Mgeni rasmi Jaji Mstaafu Mark Bomani, akibonyeza kitufe kuzindua rasmi wimbo huo wakati maadhimisho ya Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari Duniani 2014.
DSC_0422
Wageni waalikwa wakitiza wimbo huo.
DSC_0466
DSC_0497
DSC_0052
DSC_0547
Mkurugenzi wa Mbeya Highlands FM, Bi. Jacqueline Mwakyambiki, akishiriki kwenye maadhimisho ya Siku ya Uhuru wa Vyombo Vya Habari Duniani 2014 yaliyofanyika jijini Arusha.
DSC_0445
Mgeni rasmi Jaji Mark Bomani akizindua Album mpya ya Mrisho Mpoto inayoitwa "WAITE".
DSC_0476
Mgeni rasmi kwenye maadhimisho ya Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari Duniani Jaji Mstaafu Mark Bomani akizindua na kuonyesha moja ya Ripoti ya Unyanyasaji dhidi ya Uhuru wa Habari iliyoandaliwa na Baraza la Habari Tanzania (MCT). Kulia ni Mwenyekiti wa Taasisi ya Vyombo vya Habari Kusini mwa Afrika - Taiw la Tanzania (Misa - Tan), Bw. Mohamed Tibanyendera.
DSC_0493
DSC_0518
MKUU wa Wilaya ya Bagamoyo, mkoani Pwani, Ahmed Kipozi akiteta jambo na mmoja wa Waandishi wa Habari wakongwe Bw. Salim Salim kutoka visiwani Zanzibar.
DSC_0562
Waandishi wa Habari wakongwe (Ma-Veterans) kutoka kushoto Mama Eda Sanga, Fatuma Aloo na Leila Sheikh wakifurahi jambo wakati wa maadhimisho ya Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari yaliyofanyika jijini Arusha .
DSC_0359
Mshauri na Mkufunzi wa Redio Jamii kutoka UNESCO, Mama Rose Haji Mwalimu, akisalimiana na Meneja Uhusiano wa Hifadhi ya Taifa ya Ngorongoro, Bw. Adam Akyoo wakati maadhimisho ya Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari Duniani 2014 yaliyofanyika jijini Arusha.
DSC_0579
Wadau wa tasnia ya habari wakinunua Album ya msaanii Mrisho Mpoto.
DSC_0572
Baadhi ya wasanii wa Mjomba Band wakiwa kwenye picha ya pamoja na Mwandishi wa habari mkongwe Leila Sheikh.

*HABARI KUTOKA TFF LEO, TFF KUANZISHA MFUKO WA MAENDELEO, MWINYI KAZIMOTO ATUA TAIFA STARS

$
0
0
*TFF KUANZISHA MFUKO WA MAENDELEO
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) limeazimia kuanzisha Mfuko wa Maendeleo ya Mpira wa Miguu Tanzania (TFF Development Trust Fund).

Uamuzi wa kuanzisha mfuko huo umepitishwa katika kikao cha Kamati ya Utendaji ya TFF iliyokutana Mei 3 mwaka huu jijini Dar es Salaam ambapo madhumuni yake ni kutafuta vyanzo vya rasilimali za kuendeleza programu za mpira wa miguu Tanzania.

Mfuko huo utakaokuwa chini ya uenyekiti wa Rais aliyepita wa TFF, Leodegar Tenga utatafuta rasilimali za kuendeshea michuano ya Taifa na kimataifa ya wavulana na wasichana kwa vijana wenye umri chini ya miaka 13, 15, 17 na 19.

Pia kuendeleza maeneo ya ardhi kote Tanzania ambayo ni mali ya TFF kwa kujenga vituo vya michezo (sports centres), kutafuta rasilimali za kutoa mafunzo kwa makocha, marefa, madaktari wa tiba ya michezo na viongozi (administrators).

Majukumu mengine ya mfuko huo ni kuagiza na kusambaza vifaa vya michezo hasa kwa watoto wadogo (grassroots) na vijana.

Mfuko huo utazinduliwa Oktoba 8 mwaka huu ambayo ni siku ya kilele cha Tanzania kutimiza miaka 50 ya uanachama wake katika Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu (FIFA).

Mbali ya Tenga, wajumbe wengine wanaounda bodi ya mfuko huo ni Mwenyekiti wa zamani wa Simba, Ayoub Chamshama, Katibu Mkuu wa zamani wa TFF, Fredrick Mwakalebela, Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya Michezo ya Kubahatisha, Tarimba Abbas na Mbunge wa Viti Maalum, Zarina Madabida.

*MWINYI KAZIMOTO ATUA TAIFA STARS
Kiungo mshambuliaji wa timu ya Al Markhiya ya Qatar, Mwinyi Kazimoto amewasili nchini kujiunga na kikosi cha Taifa Stars kinachojiandaa na mechi ya michuano ya Afrika dhidi ya Zimbabwe.

Kazimoto ambaye amewasili nchini jana (Mei 5 mwaka huu) anatarajia kusafiri leo (Mei 6 mwaka huu) kwenda Tukuyu mkoani Mbeya ambapo Taifa Stars imeweka kambi yake chini ya Kocha Mart Nooij kujiandaa kwa mechi hiyo.

Taifa Stars inayodhaminiwa na Kilimanjaro Premium Lager juzi (Mei 4 mwaka huu) ilicheza mechi ya kirafiki na Malawi (Flames) ikiwa ni sehemu ya maandalizi kabla ya kuikabili Zimbabwe (Mighty Warriors). Mechi hiyo dhidi ya Flames ilichezwa Uwanja wa Kumbukumbu ya Sokoine na kumalizika kwa suluhu.

*WACONGO KUCHEZESHA MECHI YA NGORONGORO HEROES
Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF) limeteua waamuzi kutoka Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo (DRC) kuchezesha mechi kati ya Tanzania (Ngorongoro Heroes) na Nigeria.

Mechi ya mchujo kusaka tiketi ya kucheza Fainali za 19 za Afrika kwa vijana wenye umri chini ya miaka 20 zitakazofanyika mwakani nchini Senegal itachezwa wikiendi hii jijini Dar es Salaam.


Waamuzi hao wataongozwa na Jean-Jacques Ndala Ngambo atakayesaidiwa na Oliver Safari Kabene, Nabina Blaise Sebutu na Mupemba Ignace Nkongolo. Kamishna wa mechi hiyo namba 37 ni Poiret Antoine Ralph Danny kutoka Shelisheli.

*BONANZA LA KWANZA LA MICHEZO KUFANYIKA GYMKHANA CLUB DAR ES SALAAM, MEI 24

$
0
0
Bonanza la kwanza kushirikisha michezo tofauti katika klabu ya Dar es Salaam Gymkhana limepangwa kufanyika Mei 24 kwenye viwanja hivyo.
Bonanza hilo limeandaliwa na klabu ya Gumkhana kwa kushirikiana na kampuni ya Golden Waves Limited (GWL) na litashirikisha michezo ya golf, kriketi, squashi, tennis, riadha, snuka, chesi na mpira wa miguu.

Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya Golden Waves Limited, Kevin Luande alisema jana kuwa ushriki kwa timu katika bonanza hilo upo wazi na wanakaribisha makampuni mbali mbali na watu binafsi kuomba kushriki.

Luande alisema kuwa sababu kubwa ya kuandaa bonanza hilo ni kuwakutanisha pamoja wadau mbali mbali wa michezo na wafanyabiashara kubadilishana mawazo baada ya kazi ngumu ya ujenzi wa taifa.

“Tumekaa na klabu ya Gymkhana na kukubaliana kuandaa tukio hili la aina yake, pamoja na kuwa michezo ni afya, bonanza hili litatumika kama jukwaa la kuwakutanisha wadau katika sekta tofauti ambao wamekuwa ‘busy’ katika sughuli mbali mbali na kutumia siku hiyo kubadilishana mawazo,” alisema Luande.
Aliongeza kuwa fomu za kuomba kushiriki zinapatikana kupitia njia ya mtandao wa klabu ya Gymkhana ambao ni; gm@gymkhana.co.tz au kwa kutuma moja kwa moja kupitia email;kevin@goldenwaves.co.tz.

*MAGARI ZAIDI YA MIA YAKWAMA ENEO LA MANZESE BARABARA YA DAR ES SALAAM MTWARA

$
0
0
 Malori na Mabasi yakiwa kwenye msongamano baada ya kushindwa kuendelea na safari kwa takribani masaa zaidi ya nane katika eneo la Manzese lililopo Kilwa barabara ya Dar Es salaam kuelekea Mtwara, jana kutokana na eneo hilo kuharibiwa vibaya na mvua zinazoendelea kunyesha na kupelekea magari zaidi ya mia kukwama katika eneo hilo.
 Baadhi ya wasafiri kwenye mabasi yaendayo Dar Es Salaam kutoka Mtwara, Lindi na Kilwa na yale yatokayo Jijini Dar Es Salaam kuekelea mikoa ya Kusini wakiwa wamesimama kushuhudia juhudi zinazofanya na vijana wa eneo la Manzese na baadhi ya madereva wa malori na mabasi pamoja na abiria kuhakikisha wanasaidia magari kuvuka ili kuweza kuendelea na safari zao.
 Wasafiri na wakazi wa Eneo la Manzese wakishuhudia greda lililofika kwaajili ya kusaidia kusawazisha eneo hilo na kutoa magari yaliyonasa kutokana na eneo hilo kujaa maji na tope zito yaliyosababisha magari kukwama kwa takribani masaa zaidi ya nane hapo jana.
 Mabasi yatokeayo Mikoa ya Kusini kuelekea Bara yakiwa yamekwama katika eneo la Manzese - Kilwa kutokana na barabara kuwa mbovu katika eneo hilo kutokana na mvua zinazoendelea kunyesha na kupelekea kusababisha magari zaidi ya mia kunasa na kutoendelea na safari zao kwa zaidi ya masaa nane.
Greda likiondoa tope na kusawazisha eneo hilo ambalo lilileta usumbufu mkubwa sana kwa watumiaji wa barabara ya Dar Mtwara na kupelekea magari zaidi ya mia kukwama katika eneo hilo lililoaharibiwa na mvua zinazoendelea kunyesha. Picha zote na Josephat Lukaza wa Lukaza Blog.
 Malori yakiwa kwenye msururu.

*MKUTANO WA WIZARA YA AFYA WAFANYIKA JIJINI DAR ES SALAAM LEO, MPANGO WA KUTOA HUDUMA PAMOJA NA MAGONJWA YASIYOAMBUKIZWA WAJA

$
0
0
 Kaimu Mkurugenzi wa Huduma  za Kinga,kutoka Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii Dk,Neema Rusibamayila akifungua mkutano wa tatu wa   wa siku tatu wa magonjwa yasiyopewa  kipaumbele leo unaoendelea kwenye hoteli ya Bahari Beach jijini Dares Salaam.
 Afisa  wa Program  wa Magonjwa  yasiyopewa  kipaumbele Kitaifa  kutoka Shirika  la  Afya la Dunia(WHO) Alphonsina  Nanai akizungumza jambo leo wakati wa ufunguzi wa mkutano wa tatu wa siku tatu  wa magonjwa hayo unaoendelea   kwenye hoteli ya Bahari Beach jijini Dares Salaam.
 Meneja Mpango  wa Taifa wa Magonjwa yasiyopewa kipaumbele,Dk, Upendo Mwingira (kushoto), Kaimu Mkurugenzi wa Huduma za Kinga, kutoka Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii Dk,Neema Rusibamayila(katikati) na kulia  ni Afisa  wa Program  wa Magonjwa  yasiyopewa  kipaumbele Kitaifa  kutoka Shirika  la  Afya la Dunia(WHO) Alphonsina  Nanai wakifuatilia mkutano wa tatu wa  siku tatu  wa magonjwa hayo unaoendelea   kwenye hoteli ya Bahari Beach jijini Dares Salaam.
 Mmoja  wadau  wa  mkutano wa tatu wa   wa siku tatu wa magonjwa yasiyopewa  kipaumbele, Tesome  Kanno kutoka (ITI) akijadili jambo  leo wakati wa mkutano huo , unaoendelea  kwenye hoteli ya Bahari Beach jijini Dares Salaam.
 Kaimu Mkurugenzi wa Huduma  za Kinga,kutoka Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii Dk,Neema Rusibamayila  (wa pili kushoto) akiwa  katika picha ya pamoja  baada ya kufungua mkutano wa tatu wa   wa siku tatu wa magonjwa yasiyopewa  kipaumbele leo unaoendelea  kwenye hoteli ya Bahari Beach jijini Dares Salaam.
 Baadhi wa wadau wakifuatilia mkutano wa tatu wa   wa siku tatu wa magonjwa yasiyopewa kipaumbele, Tesome  Kanno, unaoendelea  kwenye hoteli ya Bahari Beach jijini Dares Salaam.
Baadhi wa wadau wakifuatilia mkutano wa tatu wa   wa siku tatu wa magonjwa yasiyopewa kipaumbele, Tesome  Kanno, unaoendelea  kwenye hoteli ya Bahari Beach jijini Dares Salaam. Picha na Magreth Kinabo - Maelezo
*******************************************
Serikali inaandaa mpango wa kutoa huduma za magonjwa yasiyopewa kipaumbele(NTD,s) kwa pamoja ili kuweza kufikia watu wengi kwa kupunguza gharama.
Hayo yamasemwa leo na Kaimu Mkurugenzi wa Huduma  za Kinga,kutoka Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii Dk,Neema Rusibamayila wakati akifungua mkutano wa tatu wa   wa siku tatu wa magonjwa yasiyopewa  kipaumbele leo unaoendelea  kwenye hoteli ya Bahari Beach jijini Dares Salaam.

“ Tumekutana na wadau mbalimbali katika mkutano huu lengo ni  tunataka kuandaa mpango wa  kutoa huduma na dawa kwa magonjwa yasiyopewa kiupaumbele kwa pamoja badala ya ugonjwa mmoja pekee.Tunaweza kupata matokeo zaidi na kusaidia  kuwafikia  watu wengi  kwa kuwa utarahisisha utendaji kazi, utoaji elimu na dawa,” alisema Dk. Neema.
Dk. Neema aliyataja magonjwa hayo kuwa ni Usubi, Trakoma, Kichocho, Minyoo, Mabusha na Matende.
Aliongeza kuwa  hivi sasa huduma hiyo imeweza kufikia  wilaya 108  kati ya 160.Hivyo  changamoto iliyopo ni kufikia mikoa saba.
Alisema mpango huo ulianza mwaka 2012 na unaendelea hadi mwaka 2017, ambapo mafanikio yameonekana mfano katika kupambana na ugonjwa wa usubi utafiti ulifanyika umeonesha kuwa kati ya wilaya tisa ni wilaya mbili ndizo zitaendelea kupatiwa dawa.  
Naye Meneja Mpango  wa Taifa wa Magonjwa yasiyopewa kipaumbele(NTD,s),Dk, Upendo Mwingira alisema changamoto nyingine iliyopo katika kubabiliana na magonjwa hayo ni baadhi ya jamii kuwa na uelewa mdogo juu ya magonjwa hayo ambayo dalili zake si rahisi kuonekana kwa macho  kwani huonekana baada ya muda mrefu mfano Matende na Mabusha.
Alisema  baadhi ya jamii   huwa mwitiko mdogo  wakati wa utoaji wa huduma, hivyo Dk. Upendo aliitaka jamii kujitokeza kwa wingi wakati wa utoaji wa huduma hizo.
 Alizitaja  baadhi ya athari ya magonjwa hayo kuwa ni ulemavu wa kudumu na miongoni mwa sababu zinazochangia kuwepo kwa matataizo hayo ni umasikini.
 Dk. Upendo

*RAIS KIKWETE AWASILI ABUJA, NIGERIA, KUHUDHURIA MKUTANO WA UCHUMI DUNIANI

$
0
0
 Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akipokea shada la maua mara baada ya kutua katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Nnamdi Azikiwe jijini Abuja, Nigeria, usiku wa Mei 6, 2014 ambako atahudhuria  Mkutano wa siku 3 wa Uchumi Duniani kuhusu Afrika (World Economic Forum for Africa).
 Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akilakiwa na maafisa mbalimbali wa Tanzania na Nigeria jijini Abuja, Nigeria, usiku wa Mei 6, 2014 ambako atahudhuria Mkutano wa siku 3 wa Uchumi Duniani kuhusu Afrika (World Economic Forum for Africa).
 Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akilakiwa na maafisa mbalimbali wa Tanzania na Nigeria jijini Abuja, Nigeria, usiku wa Mei 6, 2014 ambako atahudhuria Mkutano wa siku 3 wa Uchumi Duniani kuhusu Afrika (World Economic Forum for Africa).
 Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akilakiwa na maafisa mbalimbali wa Tanzania na Nigeria jijini Abuja, Nigeria, usiku wa Mei 6, 2014 ambako atahudhuria Mkutano wa siku 3 wa Uchumi Duniani kuhusu Afrika (World Economic Forum for Africa).
 Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akilakiwa na maafisa mbalimbali wa Tanzania na Nigeria jijini Abuja, Nigeria, usiku wa Mei 6, 2014 ambako atahudhuria Mkutano wa siku 3 wa Uchumi Duniani kuhusu Afrika (World Economic Forum for Africa).
 Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akiongozana na  Waziri wa Nishati wa Nigeria Profesa Chinedu Ositadinma Nebo na Balozi wa Tanzania nchini Nigeria Mhe Daniel Ole Njoolay baada ya kupokewa katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Nnamdi Azikiwe jijini Abuja, Nigeria, usiku wa Mei 6, 2014 ambako atahudhuria Mkutano wa siku 3 wa Uchumi Duniani kuhusu Afrika (World Economic Forum for Africa).
 Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akiongozana na  Waziri wa Nishati wa Nigeria Profesa Chinedu Ositadinma Nebo na Balozi wa Tanzania nchini Nigeria Mhe Daniel Ole Njoolay baada ya kupokewa katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Nnamdi Azikiwe jijini Abuja, Nigeria, usiku wa Mei 6, 2014 ambako atahudhuria Mkutano wa siku 3 wa Uchumi Duniani kuhusu Afrika (World Economic Forum for Africa).

Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akiwa Balozi wa Tanzania nchini Nigeria Mhe. Daniel Ole Njoolay, Waziri wa Viwanda na Biashara Dkt Abdallah Kigoda na Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar,Mhe. Mohammed Aboud Mohammed  baada ya kuwasili jijini Abuja, Nigeria, usiku wa Mei 6, 2014 ambako atahudhuria Mkutano wa siku 3 wa Uchumi Duniani kuhusu Afrika (World Economic Forum for Africa).  PICHA NA IKULU

*A GENOCIDE WE CAN STOP: JOIN US AS WE FIGHT TO SERVE LIVES IN AFRICA THROUGH PEACE & STABILITY BOXING TOURNAMENT IN AFRICA AT ADDIS ABABA, ETHIOPIA

$
0
0
JUBA, REPUBLIC OF SOUTH SUDAN, MAY 6, 2914: ​Women and children pulled from schools and hospitals and killed by the roadside, hate propaganda filling the airwaves - Rwanda 20 years ago? This is happening right now in South Sudan, and we have the power to help stop it. 

Two men are to blame: President Salva Kiir and his former deputy Riek Machar. Locked in a bitter power struggle, both are cynically stoking tensions between ethnic groups that have lived peacefully together for decades. Both men have assets and family abroad. If we hit Kiir and Machar where it hurts -- their wallets -- we can stop this nightmare from spiraling into genocide.

With peace talks slowly resuming, the US and France are calling on the UN Security Council to impose sanctions and deploy more peacekeepers to protect civilians. Russia may try to block action, but even China doesn't want to see this oil-rich nation slide into chaos. So it's winnable - if we act fast. Let's flood key leaders with 1 million voices urging them to pass sanctions and deploy a stronger mission to protect the people of South Sudan:


It’s heartbreaking - and outrageous. More than one million of South Sudan’s eleven million people have fled their homes, tens of thousands have died, the country is facing widespread famine. Yet for months large delegations from both sides have been staying in plush hotels in neighbouring Ethiopia, making little effort and less progress in negotiating for peace.

We can stop this insanity. Sanctions, including asset freezes and travel bans, will directly affect Kiir and Machar's abilities to access their assets and visit friends and family living abroad. Even if we lose at the Security Council, unilateral sanctions by several countries will have a serious effect. 

Bolstering the UN protection force is also key. The UN has, unprecedentedly, opened its own bases to shelter 85,000 civilians fleeing from massacres. But there are less than 9,000 UN troops to cover a country the size of France. One UN base has already been brazenly attacked, and the government is ominously threatening to kick the UN out of the country. We urgently need a much larger, stronger UN mission. 

We failed to stop the spiral of violence in Syria 3 years ago, but this conflict is new, and can still be contained. Let's not fail South Sudan. Sign and share with everyone:


South Sudan is the world's newest nation, and it was born out of decades of resistance to the genocidal brutality of Sudan's regime. But like many of our countries that have been around for a long time, there's a big gap between the leadership and the people. The gap is tragic, because President Salva Kiir was widely thought to be sincerely motivated, but he and Riek Machar seem to have become gripped by escalating anger, fear, and thirst for power. Let's stand with the South Sudanese people and help them rein in their leaders, to recover the peace that they have suffered so long for.
To Members of the UN Security Council and concerned regional countries:
As citizens from around the world deeply concerned with the situation in South Sudan, we call on you to take all measures to stop the spiral of hatred and violence. These include imposing a robust sanctions regime on the government, rebel leaders and top commanders responsible for the violence, and reinforcing the UNMISS peacekeepers with sufficient troops and capacity to better protect civilians. We also call on you to ensure immediate humanitarian assistance is delivered to tackle the threat of famine, and that the perpetrators of atrocities are tried by an international court. 20 years ago the world said "never again" after the Rwanda genocide - it’s time to live up to that promise.

Boko Haram Abducts 103 Girls From High School In Chibok, Borno State

Secondary school girls in northern Nigeria. Photo Credit: Pius Utomi Ekpei/AFP/Getty Images
By Saharareporters, New York
SaharaReporters has just learned that suspected members of the Islamist militant group, Boko Haram, have abducted 103 students in a daring raid at the Girls Secondary School in Chibok, a town on the border between Borno and Adamawa States. 
The group’s assault on the all-female high school took place on Monday night. A security source disclosed that members of the extremist Islamist group killed a soldier guarding the school and inflicted injuries on several villagers before abducting the students. 
The police commissioner in Borno State, Lawan Tanko, confirmed the kidnapping of the students to reporters in the state. 
A source who lives near the school told a correspondent of SaharaReporters that there was complete chaos during the attack, adding that the students could put up no resistance to the heavily armed attackers.
 
The mass abduction lasted between 9PM -3 AM as sect members made several trips picking and choosing their victims out of the 250 students enrolled in the school. 
Residents of the area also told Saharareporters that  the militants  razed 100 homes because some of the residents initially resisted the militants.

​Boxers Across African continent have joined hands fighting to keep Peace & Stability in Africa​ in the Part -I of the "IBF Peace & Stability Boxing Tournament in Africa" scheduled at the African Capital City of Addis Ababa, Federal Democratic Republic of Ethiopia, May 31, 2014.
 

Join hands as we serve lives by fighting for Peace & Stability in Africa.
Visit our website for more exciting news on IBF Africa, Middle East & Persian Gulf Pro Boxing activities:

They call it AFRICA...................We call it HOME

*MAKAMU WA RAIS DKT. BILAL AKUTANA NA KUZUNGUMZA NA VIONGOZI WA CCM NA WAFANYAKAZI WA KIWANDA CHA MGOLOLO (W) MUFINDI, IKULU DAR.

$
0
0
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akizungumza na Viongozi wa CCM Wilaya na Mufindi wlioongazana na baadhi ya Wafanyakazi wa Kiwanda cha Mgololo, wakati walipofika Ofisini kwa Makamu Ikulu Jijini Dar es Salaam, leo Mei7, 2014.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akizungumza na Viongozi wa CCM Wilaya na Mufindi wlioongazana na baadhi ya Wafanyakazi wa Kiwanda cha Mgololo, wakati walipofika Ofisini kwa Makamu Ikulu Jijini Dar es Salaam, leo.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiwa katika picha ya pamoja na Viongozi wa CCM Wilaya ya Mufindi na baadhi ya wafanyakazi wa Kiwanda cha Mgololo, waliofika Ofosini kwake Ikulu jijini Dar es Salaam, leo kwa mazungumzo. 

*KINANA KUANZA ZIARA YA SIKU 26 TABORA, SINGIDA NA MANYARA

$
0
0

*NI YA KUKAGUA UTEKELEZAJI WA ILANI YA CCM
*KUSIKILIZA KERO ZA WANANCHI
* KUKAGUA MAANDALIZI YA CHAMA YA UCHAGUZI WA SERIKALI ZA MITAA


Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye  akiwa na baadhi ya waandishi wa habari watakaoungana na Katibu Mkuu wa CCM, Andulrahman Kinana, katika ziara ya siku 26 katika mikoa ya Tabora, Singida na Manyara itakayoanza kesho katika jimbo la Igunga mkoani Tabora. Nape alipigapicha na na waandishi hao leo baada ya kuzungumza nao kuhusu ziara hiyo, katika Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya CCM, Mtaa wa Lumumba , Dar eSalaam. Kulia na kushoto ni baadhi ya magari maalum yatakayotumiwa na waandishi hao.

*MKUTANO MKUU WA CHAMA CHA WAANDISHI WA HABARI ZA MICHEZO CHA KIMATAIFA (AIPS) WAMALIZIKA JIJINI BAKU

$
0
0
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
A; MKUTANO MKUU AIPS
WIKI iliyopita kulifanyika Mkutano Mkuu wa Chama cha Kimataifa cha Waandishi wa Habari za Michezo (AIPS) jijini Baku, Azerbaijan.
Mkutano huo ulishirikisha viongozi wa vyama 116 vya waandishi wa habari za michezo duniani, ambapo Chama cha Waandishi wa Habari za Michezo Tanzania (TASWA), kiliwakilishwa na Katibu Mkuu, Amir Mhando.
Katika mkutano huo msisitizo mkubwa umewekwa kwa nchi wanachama kutilia mkazo program za kuwaendeleza waandishi chipukizi wa habari za michezo, lakini pia AIPS yenyewe nayo pamoja na Chama cha Waandishi wa Habari za Michezo Afrika (AIPS-Afrika) vimechukua jukumu la kusaidia kwa wale watakaokidhi vigezo wanavyohitaji.
Hivyo kila nchi mwanachama itatuma wasifu wa majina ya wanahabari chipukizi wasiozidi watano, ambao AIPS yenyewe itaangalia wale watakaofaa na kuwaandalia mafunzo baadaye mwaka huu.
Kwa upande wa AIPS Afrika yenyewe itaendesha mafunzo kwa wanahabari chipukizi 25, ambayo yatafanyika Morocco, lakini kipaumbele cha kwanza kitakuwa kwa nchi 16 zitakazocheza fainali za mataifa ya Afrika mwakani nchini humo na nafasi zingine zitabaki kwa nchi ambazo hazitaenda Morocco.
 Mafunzo ni ya wazi kwa waandishi wowote chipukizi wasiozidi umri wa miaka 25, hata wale waliopo kwenye vyuo vya uandishi wa habari wataruhusiwa kuomba. Tanzania imewahi kupata nafasi moja mwaka 2011, ambapo Mwita Mwaikenda wakati huo akiwa mwanafunzo wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, alishiriki mafunzo hayo yaliyoandaliwa na AIPS akiwa miongoni mwa Waafrika watatu tu waliopata nafasi hiyo.
 Utaratibu kuhusiana na suala hili utaelezwa vizuri baada ya kikao cha Kamati ya Utendaji ya TASWA kitakachofanyika Jumatatu wiki ijayo kujadili masuala mbalimbali.
 B: Ziara Uganda
Kulifanyika kikao cha viongozi wa nchi wanachama wa AIPS ambao wanatoka Afrika Mashariki, ambapo nchi za Burundi, Kenya, Tanzania na Uganda zilishiriki na kukubaliana kufanyike ziara ya kimafunzo itakayohusisha waaandishi wa habari za michezo Septemba 25-29 mwaka huu Kampala, Uganda. Rwanda licha ya kutoshiriki mkutano wa AIPS, lakini tulikubaliana nayo ialikwe.
Katika makubaliano hayo kila nchi itakuwa na washiriki wasiopungua 20 na wasiozidi 35, ambapo pia litafanyika kongamano kuhusiana na masuala mbalimbali ya waandishi wa habari za michezo kwa ukanda huo na siku ya mwisho litafanyika bonanza la michezo mbalimbali. Taarifa zaidi za ziara hiyo itatolewa siku za usoni.
C; Ushirikiano wa kimafunzo
 Baadhi ya nchi zilizoshiriki mkutano huo wa 77 wa AIPS, zilikubaliana kuanzisha utaratibu wa kubadilishana utaalamu wa kitaaluma kwa nchi mbalimbali, kwa kuwatoa baadhi ya wanahabari kwenda nchi zilizo katika makubaliano hayo kujifunza kwa gharama za nchi mwenyeji. 
Hata hivyo makubaliano hayo, yataanza kufanya kazi baada ya kila nchi kupata baraka za Kamati ya Utendaji na kutuma majibu kwa waratibu kwamba wanaafiki. Kamati ya Utendaji ya TASWA katika kikao chake kijacho hilo litakuwa moja ya ajenda.

Nawasilisha
Amir Mhando
Katibu Mkuu TASWA
07/05/2014

*RAIS WA ZANZIBAR DKT. SHEIN AZUNGUMZA NA UONGOZI IDARA MAALUM ZA SMZ

$
0
0
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe,Dkt.Ali Mohamed Shein (katikati) akizungumza na Uongozi wa Idara Maalum za SMZ katika mkutano wa utekelezaji mpango kazi wa robo tatu ya mwaka  Machi-Julai 2013/2014,katika ukumbi wa mikutano Ikulu Mjini Unguja leo asubuhi.
 Baadhi ya makamanda wa Idara maalum za SMZ wakimsikiliza  Waziri wa Ofisi ya Rais,Tawala za Mikoa na Idara Maalum za SMZ,Mhe,Haji Omar Kheri (hayupo pichani) alipokuwa akiwasilisha taarifa ya utekelezaji mpango kazi wa robo tatu ya mwaka  Julai-Machi 2013/2014,mbele ya  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe,Dkt.Ali Mohamed Shein,katika ukumbi wa mikutano Ikulu Mjini Unguja leo asubuhi. Picha na Ramadhan Othman,Ikulu.

*PRESIDENT KIKWETE MEETS FORMER BRITISH PM GORDON BROWN AND MARK SUZMAN OF THE GATES FOUNDATION IN ABUJA, NIGERIA, TODAY

$
0
0
President Dr. Jakaya Mrisho Kikwete shakes hands with Rt. Hon. Gordon Brown (MP), UN Special Envoy for Global Education and Former British Prime Minister in the sidelines of the World Economic Forum on Africa in Abuja, Nigeria, May 7, 2014.
President Dr. Jakaya Mrisho Kikwete in a bilateral meeting with Rt. Hon. Gordon Brown (MP), UN Special Envoy for Global Education and Former British Prime Minister in the sidelines of the World Economic Forum on Africa in Abuja, Nigeria, May 7, 2014.
President Dr. Jakaya Mrisho Kikwete shakes hands with Mr Mark Suzman, President of Global Policy and Advocacy and Country Programmes of the Gates Foundation after holding bilateral talks in the sidelines of the World economic Forum on Africa in Abuja, Nigeria, today May 7, 2014. Photos by State House.
Viewing all 13053 articles
Browse latest View live