Quantcast
Channel: SUFIANIMAFOTO
Viewing all 13053 articles
Browse latest View live

*LOWASSA ALIPOKUWA KATIKA ZIARA YA KAMPENI MKOANI SHINYANGA JANA

$
0
0
Mgombea Urais wa Tanzania wa UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh. Edward Lowassa akiongozana na aliekuwa Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Shinyanga, Ndg. Hamis Mngeja wakiwapungia wananchi wa Mji wa Kahama, wakati wakiwasili kwenye Uwanja wa Stendi mpya, Nyasubi, Kahama Mjini kulikofanyika Mkutano wa Kampeni za Mgombea huyo.
Mgombea Urais wa Tanzania wa UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh. Edward Lowassa, akipokelewa na Mwenyeji wake, Mgombea Ubunge wa Ukawa kupitia CHADEMA, Mh. James Lembeli, wakati akiwasili kwenye Uwanja wa Stendi mpya, Nyasubi, Kahama Mjini , kulikofanyika Mkutano wa Kampeni za Mgombea huyo.
Mgombea Urais wa Tanzania wa UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh. Edward Lowassa, akiwasalimia wananchi wa Mji wa Kahama.
Mgombea Urais wa Tanzania wa UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh. Edward Lowassa, akiwa ameinua juu mfano wa funguo.


*MAGUFULI ALIVYOTIKISA MJINI TABORA, AFUNIKA BOVU UWANJA WA ALI HASSAN MWINYI

$
0
0
 Mgombea Urais wa CCM Dkt Magufuli,akiwahutubia Wananchi wa Tabora jioni ya leo kwenye mkutano wa hadhara wa kampeni uliofanyika katika uwanja wa  Ali Hassan Mwinyi.Dkt Magufuli alisema kuwa Serikali yake kwa sehemu kubwa itakuwa upande wa wananchi wanyonge ili hatimaye wawe na maisha yenye neema na kwenye hilo ana uhakika atafanya kazi nzuri maana kwake yeye ni kazi tu na hakuomba kuwa Rais ili awe mwanasiasa bali anaomba nafasi hiyo kwa kujua anajua namna ambavyo amejipanga kufanya kazi kwa ajili ya maendeleo ya Watanzania wote. 
PICHA NA MICHUZI JR-TABORA

 Sehemu ya umati wa watu waliokuwa katika uwanja wa Ali Hassan Mwinyi jioni ya leo walipokuwa wakimsikiliza Mgombea Urais wa CCM Dkt Magufuli.
  Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akihutubia wakazi wa tabora mjini na kuwaambia kuwa Dk. Magufuli ni kiongozi sahihi anayehitajika Tanzania kwa sasa na kuwataka wananchi kumpigia kura zote ifikapo Oktoba 25 mwaka huu.
  Mgombea wa Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Chama Cha Mapinduzi Dk. John Pombe Magufuli akihutubia wakazi wa mji wa Tabora waliofurika kwenye mkutano wa kampeni za CCM ambapo aliwaambia anataka kujenga Tanzania mpya yenye kuleta maendeleo kwa wananchi wote.
 Mmoja wa Makada walioko kwenye timu ya uhamasishaji wa kampeni za CCM,Mh.Samweli Sitta akiwahutubia wananchi wa Tabora kwenye mkutano wa kampeni za Urais ndani ya uwanja wa Ali Hassan Mwinyi jioni ya leo.


 Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,kupitia chama cha Mapinduzi (CCM),Dkt John Magufuli akiwapungia mkono wananchi wa mji wa Tabora waliokuwa wamefurika kwenye uwanja wa Ali Hassa Mwinyi mapema leo jioni,alipokuwa akiwasili kwenye mkutano wa hadhara wa kampeni.
  Mgombea wa Urais kupitia CCM Dk. John Pombe Magufuli akihutubia umati wa wananchi wa mji wa Tabora waliojazana kusikiliza Sera na Mipango ya Chama Cha Mapinduzi itakayotumika kuongoza kwa miaka 10 ijayo.

 Wananchi wakishangilia .
  Sehemu ya umati wa wananchi wakimsikiliza Mgombea Urais wa CCM Dkt John Pombe Magufuli alipokuwa akiwahutubia jioni ya leo kwenye mkutano wa hadhara wa kampeni ndani ya uwanja wa Ali Hassa Mwinyi,mjini Tabora.
 Baadhi ya Wakazi wa mji wa Simiyu wakisubiri kumsikiliza mgombea Urais wa CCM,Dkt Magufuli kuwahutubia akitokea wilayani Nzega mapema leo mchana
 Wafuasi wa chama cha CCM sambamba na wananchi wa Uyui wakimsikiliza Mgombea Urais wa CCM Dkt John Pombe Magufuli alipokuwa akiwahutubia kwenye mkutano wa kampeni mapema leo mchana.
 Wafuasi wa chama cha CCM wakiwa na Mabango yao ndani ya uwanja wa Ali Hassan Mwinyi,wakimpokea Mgombea Urais wa CCM Dkt John Pombe Magufuli
 Sehemu ya umati wa wananchi wakimsikiliza Mgombea Urais wa CCM Dkt John Pombe Magufuli alipokuwa akiwahutubia jioni ya leo kwenye mkutano wa hadhara wa kampeni ndani ya uwanja wa Ali Hassa Mwinyi,mjini Tabora
 Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Tabora Ndugu Hassani Wakasubi akitoa ufafanuzi mfupi kwenye mkutano wa kampeni wa hadhara uliofanyika jioni ya leo kwenye uwanja wa Ali Hassa Mwinyi,mjini Tabora
  Sehemu ya umati wa wananchi wakimsikiliza Mgombea Urais wa CCM Dkt John Pombe Magufuli alipokuwa akiwahutubia jioni ya leo kwenye mkutano wa hadhara wa kampeni ndani ya uwanja wa Ali Hassa Mwinyi,mjini Tabora
 Wananchi wakishangilia wakati Dkt Magufuli alipokuwa akiwahutubia.

*MAKAMU WA RAIS AADHIMISHA KILELE CHA SIKU YA MARA (MARA DAY) BUTIAMA MKOANI MARA

$
0
0
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muugano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiwasha Mshumaa katika Kaburi ya Hayati Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere, kama ishara ya Kumbukumbu wakati alipofika katika Jumba la makumbusho Butiama mkoani Mara leo Sept 15, 2015 baadda ya kuadhimisha Kilele cha Siku ya Mara (Mara Day) iliyofanyika Butiama.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muugano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiweka Shada la Maua katika Kaburi ya Hayati Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere, kama ishara ya Kumbukumbu wakati alipofika katika Jumba la makumbusho Butiama mkoani Mara leo Sept 15, 2015 baadda ya kuadhimisha Kilele cha Siku ya Mara (Mara Day) iliyofanyika Butiama. Kushoto ni Waziri wa Maji na Umwagiliaji wa Kenya, Eugene Wamalwa.
Makamu wa Rais waJamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akihutubia wakati wa sherehe za maadhimisho ya Kilele cha Siku ya Mara (Mara Day) zilizofanyika  kwenye Uwanja wa Mwenge, Butiama mkoani Mara leo.

KWA PICHA ZA SHEREHE HIZI NA HABARI KAMILI ZITAWAJIA HAPO BAADAYE

*MKUTANO WA MAZINGIRA LEO

$
0
0
Waziri wa Nchi,Ofisi ya Makamu wa Rais(Mazingira) Dkt. Binilith Mahenge akizungumza na waandishi wa habari leo  katika ukumbi wa mikutano wa ofisi jijini Dar es Salaam kuhusu maadhimisho ya siku ya kimataifa ya hifadhi ya tabaka la ozone yakayofanyika kesho Septemba 16, mwaka huu.Kulia ni Kaimu Katibu Mkuu wa Ofisi hiyo, Injia Adelina Madete. Picha na Maelezo

*MASK YA ASALI, NDIZI MBIVU NA NDIMU KWA WALE WENYE USO WA MAFUTA

$
0
0
Kama mlivyoomba wadau kwa wale wenye USO wenye MAFUTA mengi hii ni MASK unayoweza kutumia ukiwa nyumbani na ikakuaaidia.
Nini cha kufanya:-
1. Ponda ponda NDIZI MBIVU MOJA mpaka iwe laini kabisa
2. Chukua KIJIKO KIMOJA CHA ASALI
3. Chukua KIJIKO KIMOJA CHA NDIMU
4. Changanya kwa pamoja vitu hivyo vizuri.
5. Paka mchanganyiko huo kwenye uso msafi kama inavyoonekana kwenye picha na kaa nao kuanzia dakika 15 hadi 30 kisha osha na maji ya uvuguvugu.
Unaweza tumia mask hii mara moja kwa siku.

*MAGUFULI ALIPOPOKELEWA KAMA MFALME KIGOMA,WANANCHI WAKIRI WAZI ATOSHA KUWA RAIS

$
0
0
Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,kupitia chama cha Mapinduzi Dkt John Pombe Magufuli akiwahutubia  maelfu ya wananchi waliofurika kwenye mkutano wa hadhara wa kampeni za Urais,uliofanyika katika uwanja wa Kawawa,mkoani Kigoma jioni ya leo. PICHA NA MICHUZI JR-KIGOMA.
 Dkt Mafuli amewaabia wananchi wa Kigoma kwenye mkutano wa kampeni leo jioni kwenye uwanja wa kawawa kuwa Serikali yake kwa sehemu kubwa itakuwa upande wa wananchi wanyonge ili hatimaye wawe na maisha yenye neema,amesema kuwa Serikali yake haitakuwa ya kunyanyasa mama ntile na kudaiwa kodi za hovyo hovyo,amesema kuwa ataimarisha ukusanyaji wa kodi kwenye serikali yake, lakini pia atawabana wafayabiashara  wakubwa ambapo baadhi yao hawalipi kodi

Magufuli amewataka Wananchi kumuamini kwa yale ambayo amekuwa akiyasema kwenye mikutano yake ya kampeni na kuongeza anachoahidi ndicho ambacho atakitekeleza kwenye serikali yake na kwenye maisha yake huwa hataki kutoa ahadi za uongo.
Maelfu ya wananchi waliofurika kwenye mkutano wa hadhara wa kampeni za Urais,uliofanyika katika uwanja wa Kawawa,mkoani Kigoma jioni ya leo wakimsikiliza Mgombea Urais wa CCM Dkt John Pombe Magufuli alipokuwa akiwahutubia.
Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,kupitia chama cha Mapinduzi Dkt John Pombe Magufuli akiwahutubia  maelfu ya wananchi waliofurika kwenye mkutano wa hadhara wa kampeni za Urais,uliofanyika katika uwanja wa Kawawa,mkoani Kigoma jioni ya leo.

Aidha hadi jana, tarehe 16 September 2015, Mgombea Urais wa CCM, Dkt. John Pombe Magufuli, alikuwa amekwishafanya kampeni katika mikoa 12 na Majimbo 94. Amekwishafanya mikutano mikubwa ya hadhara 76 na mikutano ya barabarani 381. Amekwishatembea, kwa gari, jumla ya kilomita 13,720. Kwa ujumla amekwishakutana, moja kwa moja, na asilimia zaidi ya 30 ya wapiga kura.
Wananchi na Mabango yao
Mgombea Urais wa CCM Dkt John Pombe Magufuli akiwahutubia wakazi wa Nguruka kwenye mkutano wa kampeni wa hadhara mapema leo mchana.
Wakazi wa Nguruka waifuatilia Mkutano.
Mgombea Urais wa CCM Dkt Magufuli akimkabidhi Ilani ya chama cha CCM kwa Mgombea Ubunge wa Kigoma Kusini,Hasna Mwilima na pia kummwombea kura kwa wananchi mapema leo kwenye mkutano wa hadhara wa kampeni uliofanyika Nguruka mkoani Kigoma.
Wananchi wakisikiliza sera za Mgombea Urais wa CCM Dkt John Pombe Magufuli
Baadhi ya Wananchi wa Uvinza wakiwa wamefunga barabara wakitaka wasikilizwe kero zao na Mgombea Urais wa CCM,Dkt Magufuli alipokuwa akipita mjni humo akielekea Kigoma mjini kwenye mkutano wa hadhara.
Baadhi ya akina mama wakishangilia jambo
Mgombea Ubunge wa jimbo la Kigoma Kaskazini Peter Selukamba akiwahutubia wananchi wa Kalinzi,mkoani Kigoma kweny mkutano wa kampeni za Uraisi jioni ya leo.
Baadhi ya wafuasi wa chama cha CCM wakifuatilia mkutano wa hadhara katika kijiji cha Kalinzi,ambapo mgombea Urais wa CCM Dkt Magufulia aliwahutubia wananchi.
Wakazi wa mji wa Nguruka,mkoani Kigoma wakifuatilia mkutano wa hadhara
Wananchi na mabango yao
Kada maarufu na aliyewahi kuwa Katibu MKuu wa CCM,Mh Yusuph Makamba akisalimiana na Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,kupitia chama cha CCM Dkt John Pombe Magufuli kabla ya kupanda jukwaani na kuwaomba ridhaa wakazi wa kigoma ya kuwaongoza katika awamu ya tano.
Wananchi wakishangilia jambo kweye mkutano wa kampeni za Urais

Wananchi wakifuatilia mkutano wa kampeni
Kada maarufu na aliyewahi kuwa Katibu MKuu wa CCM,Mh Yusuph Makamba akiwahutubia wananchi wa Kigoma na vitongoji vyake jioni ya leo kwenye mkutano wa hadhara wa kampeni za Urais,uliofanyka katika uwanja wa Kawawa mkoani Kigoma

*WAWEKEZAJI UTURUKI WAALIKWA KUWEKEZA HIFADHI ZA TAIFA

$
0
0
Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Hifadhi za Taifa(Tanapa)Allan Kijazi  akiwa kwenye mazungumzo na Balozi wa Uturuki nchini, Yasemin Eralp(katikati)aliyefika makao makuu ya Shirika hilo leo,kulia ni Katibu Msaidizi wa Ubalozi wa Uturuki,Berat Colak.
Balozi wa Uturuki nchini, Yasemin Eralp(kushoto) akipokea zawadi kutoka kwa Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Tanapa,Allan Kijazi alipotembelea Makao Makuu ya shirika hilo  jijini Arusha.
Katibu Msaidizi wa Ubalozi wa Uturuki,Berat Colak(kushoto) akipokea zawadi kutoka kwa Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Hifadhi za Taifa(Tanapa),Allan Kijazi alipotembelea Makao Makuu ya shirika hilo  jijini Arusha.  
***********************************************************
Balozi wa Uturuki nchini Mhe. Yasemine Eralp amesema atawaalika wawekezaji kutoka Uturuki ili waweze kutumia fursa za uwekezaji zilizopo katika Hifadhi za Taifa nchini. Balozi Eralp alitoa ahadi hiyo alipotembelea Makao Makuu ya TANAPA jijini Arusha na kukutana na viongozi wa shirika.
Balozi Eralp amesema kuwa sekta ya utalii ni miongoni mwa vipaumbele vyake na kwamba atatumia muda wake mwingi kuhakikisha kuwa sekta hiyo inastawi na kuvutia watalii wengi nchini kutoka Uturuki.

Katika mazungumzo yake na viongozi wa TANAPA, Balozi Eralp alitoa nafasi kwa TANAPA kutangaza katika Jarida la Shirika la Ndege la Uturuki Skyline Magazine, na kwamba  fursa hii itasaidia  kuvutia wageni wengi zaidi nchini kutoka nchi zaidi ya 60 zinazofikiwa na shirika hilo la ndege ulimwenguni.

Balozi Eralp alikubaliana na TANAPA kuwa atafanya mazungumzo na Turkish Airline ili waweze kuandaa safari za kutembelea vivutio vya utalii katika hifadhi kwa waandishi wa habari na mawakala wa wageni kutoka Uturuki ili waweze kuzitangaza Hifadhi za Taifa katika Bara la Ulaya.

Kwa upande wake, Mkurugenzi Mkuu wa TANAPA Allan Kijazi aliahidi kuwa TANAPA itatoa ushirikiano wa dhati katika kuhakikisha kuwa malengo ya Mhe. Balozi Eralp yanatimizwa ikiwa ni pamoja na  shirika kutumia fursa ya kupata watalii kutoka Uturuki ambayo ni miongoni mwa nchi ambazo uchumi wake unakua kwa kasi kubwa na kuwa fursa za kupata wageni wengi zaidi  kutoka Uturuki zinaonekana dhahiri.

Imetolewa na Idara ya Mawasiliano
Hifadhi za Taifa Tanzania

*TAARIFA YA TATHIMINI YA KAMPENI ZA UCHAGUZI KWA WAGOMBEA KWA TIKETI YA CCM.

$
0
0
*MWENENDO WA KAMPENI ZA CCM
Hadi jana, tarehe 16 September 2015, Mgombea Urais wa CCM, Dr. John Pombe Magufuli, alikuwa amekwishafanya kampeni katika mikoa 12 na Majimbo 94. Amekwishafanya mikutano mikubwa ya hadhara 76 na mikutano ya barabarani 381. Amekwishatembea, kwa gari, jumla ya kilomita 13,720. Kwa ujumla amekwishakutana, moja kwa moja, na asilimia zaidi ya 30 ya wapiga kura. Kwa kuwa baadhi ya mikutano yetu inatangazwa moja kwa moja na redio za kijamii na luninga, wapiga kura waliopata nafasi ya kumsikia wanakadiriwa kufikia asilimia 70.
Tunafarijika na idadi kubwa ya watu wanaokuja kwenye mikutano ya kampeni zetu. Tunafarijika pia kwamba karibu Watanzania wote wanaopata fursa ya kumuona na kumsikia wamemuelewa na wamepata matumaini ya Tanzania Mpya kupitia kwake. Utafiti wetu wa ndani, tulioufanya kwa kipindi cha siku kumi zilizopita katika majimbo 246 kati ya majimbo 269, unaonyesha kwamba Dr. Magufuli atapata ushindi wa asilimia 69.3 Tunaamini kwamba asilimia hizi zitaongezek kadri Watanzania wengi zaidi wanavyopata fursa ya kumsikiliza Dr. Magufuli na kusikiliza Ilani na sera za CCM.

Kwa upande wa kampeni zetu za Ubunge,  zaidi ya robo tatu ya wagombea Ubunge wa CCM wamekwishazindua kampeni zao na wanaendelea vizuri. Sekretarieti ya Kampeni ya CCM inaanda program maalum ya kampeni
katika majimbo yenye changamoto mahsusi.
Napenda kuchukua fursa hii kuwajulisha wana-CCM kwamba viongozi na makada wengine wa CCM, waliopo madarakani na wastaafu watapita tena, jimbo kwa jimbo, nchi nzima katika siku 30 za mwisho katika jitihada za kuongeza ushindi wa CCM na Dr. Magufuli.

*MIDAHALO YA WAGOMBEA
Wiki tatu zilizopita, CCM, na kwa hakika vyama vingine pia, ilipokea mwaliko wa Mgombea Urais wa CCM, Dr. John Pombe Magufuli, kushiriki kwenye mdahalo wa wagombea Urais uliondaliwa na Baraza la Habari Tanzania (Media Council of Tanzania) kwa kushirikiana na taasisi nyingine kadhaa, ikiwemo Twaweza. Dr. Magufuli amekubali kushiriki katika mdahalo huo. 

Kwa msingi huo, kauli ya UKAWA iliyotolewa jana na Mwenyekiti wa NCCR-Mageuzi, Ndugu James Mbatia, kwamba UKAWA inaomba mdahalo ni njia ya kuwahadaa Watanzania tu kwa kuwa mwaliko wa mdahalo ulikwishatolewa mapema kwa vyama vyote na wanaotakiwa kushiriki ni wagombea Urais wa vyama.

CCM inafurahishwa na utamaduni wa midahalo ambao unaanza kujitokeza
katika chaguzi zetu. Na inaamini kwamba midahalo ya Wagombea Urais ni
sehemu muhimu ya kuwashirikisha wapiga kura katika mchakato wa uchaguzi na kuwasaidia waamue nani wamchague kwa misingi ya hoja na sera na sio kwa ushabiki, kwa mihemko, na kwa propaganda. Mdahalo unatoa fursa ya wagombea kuulizwa maswali ya moja kwa moja na kutoa ufafanuzi wa kina kuhusu sera na ahadi zao, fursa ambayo hawaipati kwenye mikutano ya hadhara kampeni.

Hatukubaliani na kauli ya UKAWA kwamba mdahalo usiwe baina ya wagombea
bali uwe baina ya Wenyeviti wa Vyama. Tunaamini hoja hii ni kichekesho. Haijawahi kutokea popote duniani kwenye utamaduni wa midahalo, kwamba wagombea wasishiriki bali watu wengine ndio wafanye midahalo kwa niaba yao.  Tunaamini mdahalo huu unapaswa kuwa baina ya wagombea. Wao ndio wanaoomba dhamana. Wao ndio wanaopaswa kujibu maswali na kufafanua kuhusu ahadi zao.

CCM inaamini kwamba ili mdahalo huu uwe na tija, wagombea Urais wote,
hasa wa vyama vikuu, wawepo na washiriki. Mdahalo hautakuwa na maana
kama mgombea mmojawapo wa vyama vikuu atatengeneza kisingizio ili asishiriki.
*UCHAGUZI WA AMANI
CCM inasikitishwa na kauli zinatolewa na baadhi ya viongozi wa UKAWA zenye kuashiria fujo na vurugu. Kauli kwamba kura zitaibiwa hazina msingi wowote. Kauli hizi zinaashiria maandalizi ya kushindwa na maandalizi ya kufanya vurugu baada ya matokeo ya kushindwa.

Utaratibu wa uchaguzi wetu unajulikana na umekubalika na vyama vyote. Kura zinapigwa kituoni na kuhesabiwa kituoni mbele ya mawakala wa vyama vyote, wasimamizi wa uchaguzi na waangalizi wa uchaguzi wa ndani na nje ya nchi. Baada ya kura kuhesabiwa, matokeo yanajazwa katika fomu ambayo kila wakala anasaini na kupewa nakala. 
Nakala ya matokeo hayo pia inabandikwa nje ya kituo cha kupiga kura. Kila Chama, na kila Mtanzania, kina fursa ya kujumlisha matokeo yake kwenye kila kituo na kupata jumla kuu. 

Matokeo ya nchi nzima yanajumlishwa mahala pamoja huku kukiwa na waangalizi wa uchaguzi wa ndani na nje ya nchi, pamoja na wawakilishi wa vyama vyote na wao wakiwa na fomu zao za kila kituo nchi nzima.

Tunapenda kuwasihi Watanzania wasikubali vishawishi vya kufanya vurugu. Mara nyingi, viongozi wanaohamasisha vurugu wanakuwa na ulinzi au walinzi au uwezo wa kukimbilia pahala penye utulivu zaidi huku wakiwaacha wafuasi wao katika wakihangaika.

*UCHAGUZI NA UMOJA WA KITAIFA
CCM pia inapenda kusisitiza imani yake kwamba uchaguzi haupaswi kutugawa kama taifa. Uchaguzi ni tukio la kupita. Kuna maisha baada ya uchaguzi. Kuna taifa baada ya uchaguzi. Lazima taifa liendelee kubaki moja, tuendelee kubaki wamoja. Tusitoe kauli za kupitiliza zenye mrengo wa kujenga chuki katika jamii na kuhatarisha umoja na amani ya nchi yetu.

Kama Chama kilichoasisi umoja wa taifa letu, tunaendelea kuasa kwamba
wanasiasa wasijinadi kwa misingi ya udini, ukabila wala ukanda. CCM haina mpango kuendeleza mjadala wa kauli ya Mgombea wa UKAWA Ndugu Edward Lowassa aliyoitoa kanisani Tabora tarehe 6 September 2015kwamba nchi ilishapata viongozi Wakatoliki na kwamba sasa ni zamu ya Walutheri kuchukua nafasi hiyo. Tunaamini mjadala huo hauna tija. 

Tunaamini kwamba Watanzania wengi, wa dini na madhehebu yote, hawaamini katika siasa za namna hii. Tuliamini kwamba UKAWA ingetumia fursa ya mkutano wao na waandishi wa habari jana kuomba radhi kwa Watanzania. Kwakuwa hawakufanya hivyo, tunapendekeza mjadala wa jambo hili ufungwe. Itoshe tu kwamba Ndugu Lowassa amesema hivyo, Tume ya Uchaguzi imemuonya, na yeye hajajitokeza kuomba radhi wala kufafanua. Watanzania wamemjua ni kiongozi wa aina gani na watatoa hukumu yao Tarehe 25 Oktoba 2015.

Imetolewa na:-

January Y. Makamba,
MJUMBE WA HALMASHAURI KUU YA TAIFA YA CCM
MJUMBE WA KAMATI YA KAMPENI YA CCM
16/9/2015

*HUDUMA YA SIMBA NEWS SASA KUPATIKANA KWA WATEJA WA VODACOM PIA

*MABADILIKO YA KAMATI NDOGO ZA TFF

$
0
0
Kikao cha Kamati ya Utendaji cha Shirikisho la Mpira wa Miguu nchini (TFF) kilichofanyika Septemba 06, mwaka huu kilifanya mabadiliko madogo ya kamati zake ndogo ndogo.
Mjumbe wa Kamati ya Utendaji, Blassy Kiondo aliyekua Mwenyekiti wa Kamati ya Soka la Wanawake ameteuliwa kuwa Mwenyekiti wa Kamati ya Soka la Ufukweni na Sakafuni (Beach Soccer and Futsal).
Amina Karuma ambaye ni Mwenyekiti wa Chama cha Mpira wa Miguu cha Wanawake nchini (TWFA) na Mjumbe wa Kamati ya Utendaji aliteuliwa kuwa Mwenyekiti wa Kamati ya Soka la Wanawake.
*COPA COCA COLA KUFANYIKA MWAKANI
Mashindano ya Copa Coca Cola yanayodhaminiwa na Kampuni ya Vinywaji ya Coca Cola yaliyokuwa yafanyike katikati ya mwaka huu, sasa yatafanyika mapema mwakani mwezi Februari kuanzia ngazi ya Wilaya na fainali zake kufanyika mwezi Juni na Julai 2016. KUSOMA ZAIDI BOFYA LINK HIYO CHINI

*RAIS KIKWETE AKAGUA MAENDELEO YA KITUO CHA MICHEZO KWA VIJANA CHA KIDONGO CHEKUNDU DAR ES SALAAM

$
0
0
 Kituo cha Michezo kwa vija na cha Kidongo Chekundu jijini Dar es salaam kinavyoonekana kutoka angani
 Rais Jakaya Mrisho kikwete akitembezwa na Mkurugenzi Mkuu wa kampuni ya umeme ya Symbion Bw. Paul Hicks wakati akikagua maendeleo ya ujenzi wa kituo cha kisasa cha Michezo kwa vijana cha Kidongo Chekundu jijini Dar es salaam. Kituo hicho kinajengwa kwa msaada wa Klabu ya Sunderland ya Uingereza na kampuni ya symbion
 Rais Jakaya Mrisho kikwete akitembezwa na Mkurugenzi Mkuu wa kampuni ya umeme ya Symbion Bw. Paul Hicks kwa mmoja wa wasimamizi wa mradi huo wakati akikagua maendeleo ya ujenzi wa kituo cha kisasa cha Michezo kwa vijana cha Kidongo Chekundu jijini Dar es salaam. Kituo hicho kinajengwa kwa msaada wa Klabu ya Sunderland  ya Uingereza na kampuni ya symbion
Rais Jakaya Mrisho kikwete akitembezwa na Mkurugenzi Mkuu wa kampuni ya umeme ya Symbion Bw. Paul Hicks kwa kocha wa vijana wa kandanda mwenye kutambulika na FIFA kutoka Uingereza  wa mradi huo wakati akikagua maendeleo ya ujenzi wa kituo cha kisasa cha Michezo kwa vijana cha Kidongo Chekundu jijini Dar es salaam. Kituo hicho kinajengwa kwa msaada wa Klabu ya Sunderland ya Uingereza na kampuni ya symbion. PICHA NA MICHUZI

*WENGI WAJITOKEZA UZINDUZI WA AWAMU YA PILI KUPINGA UKATILI WA KIJINSIA DHIDI YA WANAWAKE MASOKONI

$
0
0
 Ofisa Mtendaji Kata ya Temeke, Elias Wawa akizungumza katika uzinduzi wa awamu ya pili kupinga ukatili wa kijinsia dhidi ya wanawake masokoni uliofanyika soko la Temeke Sterio Dar es Salaam jana. Uzinduzi huo  upo chini ya mradi wa Mpe Riziki si Matusi 'Acha Lugha Chafu na Udhalilishaji Sokoni' Unaendeshwa na Shirika Equality for Growth (EfG). 
 Mwenyekiti wa Mtaa wa Matumbi uliopo katika wilaya ya Temeke, Khatibu Lindi, akizungumza katika mkutano huo.
 Mwenyekiti wa Soko la Temeke Sterio, Hamad Juma Mtemi, akizungumza katika mkutano huo.
 Ofisa Maendeleo ya Jamii Kata ya Temeke, Agnes Soso, akizungumza katika uzinduzi huo. KUSOMA ZAIDI BOFYA READ MORE
 Ofisa Ufuatiliaji na Tathimini wa Shirika la Equality for Growth (EfG), Samora Julius (kulia), akitoa mada mbalimbali kuhusu ukatili wa jinsia masokoni wakati wa uzinduzi huo.
 Ofisa Mradi wa EfG, Susan Sitta, akielezea historia fupi ya 
shirika hilo.
 Wananchi wakiwa kwenye Uzinduzi huo.
 Mkazi wa Chamanzi, Husna Abdallah akielezea udhalilishaji wa jinsia katika masoko.
 Wasanii wa kundi la Machozi wakiigiza igizo la ukatili wa jinsia 
 Maofisa wa EfG wa ndani na nje ya nchi na wadau mbalimbali wakiwa kwenye uzinduzi huo.
 Mkutano ukiendelea.
 Wananchi wakifuatila matukio mbalimbali kwenye uzinduzi huo.
 Soko la Temeke Sterio ulipofanyika uzinduzi huo.
 Taswira katika uzinduzi huo.
 Msanii wa Kundi la Utamaduni la Machozi, akitoa burudani.
Burudani zikiendelea kutoka kundi la Machozi.
*******************************
Na Dotto Mwaibale, Dar
 OFISA Mtendaji wa Kata ya Temeke, Elias Wawa amelipongeza Shirika la Equality for Growth (EfG), kwa jitihada zake na kupunguza ukatili wa kijinsia dhidi ya wanawake masokoni.

Wawa alitoa pongezi hizo Dar es Salaam jana, wakati akizungumza na wanahabari katika  uzinduzi wa awamu ya pili ya kupinga vitendo vya ukatili wa jinsia dhidi ya wanawake katika Soko la Temeke Sterio.

"Nalipongeza shirika la EfG kwa jitihada zao za kutoa elimu kwa wananchi katika masoko mbalimbali kwani imesaidia kupunguza vitendo vya udhalilishaji na ukatili wa jinsia masokoni" alisema Wawa.

Akizungumza katika uzinduzi huo, Ofisa Mradi wa Shirika la EfG, Susan Sitta alisema shirika hilo lililosajiriwa Septemba 6, 2015 dhima yake ni kuinua maendeleo ya sekta isiyo rasmi Tanzania, hususani wanawake, kwa kupunguza umaskini kwa njia ya kutoa mafunzo ya sheria na haki za binadamu, kutoa msaada wa kisheria, kuwezesha kuwepo kwa fursa za biashara kwa wanawake na wanaume pamoja na kushawishi utungaji wa sera zinazoinua wanawake na kujenga uwezo sawa kwa wanawake na wanaume.

Sitta alisema shirika hilo linatekeleza mradi unaoitwa Mpe Riziki si Matusi katika masoko sita Wilayani Ilala ambayo ameyataja kuwa ni Feri, Kisutu, Mchikichini, Gezaulole, Tabata Muslimu na Temeke Sterio.

Alisema mradi huo umelenga kuwalinda wanawake katika sekta isiyo rasmi hususani wafanyabiashara masokoni dhidi ya ukatili wa kijinsia.

Aliongeza kuwa mradi huo pia unaangalia wanawake wafanyabiashara katika masoko ya ya Wilaya ya Ilala na Temeke na kuhakikisha wanafanyabiashara zao katika mazingira huru yasiyo na ukatili wa matusi, kingono, kimwili, kiuchumi na kisiasa.

"Mradi huu zaidi unaangalia na kuhakikisha wanawake wanaheshiwa na kufurahi haki yao ya kiuchumi" alisema Sitta.

Sitta alisema utafiti uliofanywa na shirika hilo juu ya ukatili dhidi ya wanawake masokoni unaonesha asilimia 90.32 ya wanawake katika sekta isiyo rasmi wanafanyiwa ukatili mara kwa mara wa kingono, kimwili na matusi katika maeneo yao ya kazi.  

Mkazi wa Chamanzi, Husna Abdallah alisema kufanyiwa viendo vya ukatili wa jinsia kwa wanawake wafanyabiashara masokono kwa upande mwingine kunachangiwa na wanawake wenyewe pale wateja wanapowashika katika miili yao na wao kufurahi jambo hilo bila kuchukua hatua ya kuwakalipia au kuwapeleka kwa uongozi wa soko husika.

*TASWA YAPATA MDHAMINI MPYA KUWAPA ZAWADI WANAMICHEZO BORA KATIKA UONGOZI WA RAIS JAKAYA

$
0
0
TAASISI ya GSM Foundation ya Dar es Salaam imetoa Sh milioni 50 kwa ajili ya kudhamini tuzo za wanamichezo  waliofanya vizuri zaidi katika miaka 10 ya uongozi wa Rais Jakaya Kikwete.
Utoaji wa tuzo hizo utafanyika Oktoba 8, mwaka huu ukumbi wa Mlimani City, Dar es Salaam, ambapo wanamichezo pia watatumia tuzo hizo zilizoandaliwa na Chama cha Waandishi wa Habari za Michezo Tanzania (TASWA) kumuaga Rais Kikwete anayemaliza muda wake kikatiba.
Kwa mujibu wa TASWA licha ya kumuaga Rais Kikwete na kutoa tuzo kwa wanamichezo 10 waliofanya vizuri zaidi, pia chama hicho kitatoa Tuzo ya Heshima  Rais Kikwete ikiwa ni kuthamini mchango wake kwa michezo katika utawala wake. 
Akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari kutambulisha udhamini huo Dar es Salaam jana, mwakilishi wa GSM Foundation, Elibariki Lukumay, alisema wameguswa na tukio hilo na kuona kuna umuhimu wa kuiunga mkono TASWA. 
“Taasisi yetu ambayo ina kampuni mbalimbali imeguswa na kitendo ambacho TASWA inakiandaa na kwa kuanzia tunatoa kiasi hicho cha fedha kufanikisha jambo hilo na tunawaomba wengine pia waunge mkono.
“Rais Kikwete amefanya mambo makubwa katika michezo nchi hii, hivyo tukiwa pia wadau wakubwa wa michezo tumeona ni vyema tuungane na wenzetu wa TASWA katika kumuaga na kumshukuru kwa mchango mkubwa alioufanya kwa michezo,” alisema Lukumay.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa TASWA, Juma Pinto aliishukuru taasisi hiyo na kusema kuwa bajeti ya tukio hilo ni Sh milioni 130 na kwamba wadhamini hao wamefungua milango kwa wengine ili kulifanikisha jambo hilo.

Tunaamini mchango wa Rais Kikwete katika medani ya michezo hauna mfano na kila mdau wa michezo atakubali amefanya mambo makubwa kwa michezo.
“Tunafahamu Rais alivyosimamia serikali yake kulipia  makocha wa michezo ya soka, netiboli na ngumi. Pia chini ya utawala wake serikali ilipeleka wanariadha wetu China, Ethiopia na New Zealand kwa maandalizi ya mashindano ya kimataifa,” alisema.
Alifafanua kuwa karibu vyama vyote vya michezo nchini vitashikirikishwa katika tukio hilo ikiwa ni pamoja kuwa karibu kwa kila hatua na Wizara Ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo pamoja na Baraza la Michezo la Taifa (BMT).

*TANGAZO LA MSIBA

$
0
0

Mpigapicha Mkuu wa Kampuni ya Tanzania Standard Newsapapers (TSN) Limited, wachapishaji wa magazeti ya Dailynews, Sundaynews, Habarileo, Habarileo Jumapili na Spotileo, Mohamed Mambo anasikitika kutangaza kifo cha mke wake Margaret Amon Mwaisaga (pichani) kilichotokea Hospitali ya TMJ  15.09.2015. 

Msiba upo nyumbani kwa familia ya marehemu Mikocheni nyumba namba 87 barabara itokayo Clouds FM kwenda Kanisa la Mchungaji Rwakatare na mazishi yatafanyika leo Ijumaa makaburi ya Kinondoni jijini Dar es Salaam kunzia saa sita. 

*TATIZO LA UHABA WA MAJI WILAYANI MKURANGA SASA KUBAKI KUWA HISTORIA.

$
0
0
 Mtaalam wa mitambo wa Kampuni ya ZENTAS Sahtn Topal ( katikati) akifafanua teknolojia na vifaa vilivyotumika kuchimba kisima hicho.
 Maji kutoka katika kisima hicho yakitiririka kufuatia kufanyika kwa majaribio ya kuyatoa maji kutoka ardhini.
 Kiongozi wa waendesha mitambo ya uchimbaji visima wa kampuni ya ZENTAS Bw. Sima Teodor ( kushoto) akitoa maelezo kwa wandishi wa habari kuhusu kazi ya uchimbaji wa kisima hicho katika eneo la mradi wilayani Mkuranga. Picha na Aron Msigwa/ MAELEZO.
Mwakilishi wa Kampuni ya Uchimbaji wa Visima ya ZENTAS kutoka Uturuki nchini Tanzania Dkt, Mohammed Akbar Akitoa taarifa za kukamilika kwa kazi ya uchimbaji wa kisima chenye urefu wa mita 541 eneo la Mkwalia, Mkuranga, Pwani leo.Kisima hicho kinauwezo wa kuzalisha maji lita milioni 1.8 kwa siku.
**************************************************************
Na.Aron Msigwa- MAELEZO, Mkuranga,Pwani.
Wananchi wa wilaya ya Mkuranga,mkoa wa Pwani wanatarajia kunufaika na mradi mkubwa wa usambazaji wa maji kufuatia kukamilika kwa zoezi la uchimbaji wa kisima cha maji chenye urefu wa mita 541 ambacho kina uwezo wa kuzalisha lita milioni  1.8  kwa siku.

Akitoa taarifa za kukamilika kwa kazi ya uchimbaji wa kisima hicho  mwakilishi wa kampuni ya kuchimba visima ya ZENTAS  kutoka Uturuki nchini Tanzania, Dkt.Mohammed Akbar amesema wao kama wataalam wanaendelea na kazi ya kuyatoa maji kutoka ardhini  jambo ambalo linaendelea kwa ufanisi makubwa.

 Amesema mtambo wa kuchimba kisima hicho uliwasili eneo la mradi Julai 9 mwaka huu na kuongeza kuwa mara baada ya kuwasili katika eneo la mradi kazi ya uchimbaji ilianza na kubainisha kuwa  sasa kisima hicho kinazalisha kiasi cha lita  76,000 kwa saa na lita milioni  1.8 kwa siku.

Dkt. Akbar amesema endapo maji hayo yataunganishwa kwenye miundombinu ya maji ya mji huo yatakidhi mahitaji ya maji ya mji wa Mkuranga ambayo ni lita laki  Sita na Elfu mbili  kwa siku (602,000).

" Kwetu Haya  ni mafanikio makubwa ukizingatia mradi wenyewe haujaanza kusambaza maji kwani visima hivi vilikuwa ni kwa ajili ya utafiti, kiwango cha maji kilichopatikana ni kikubwa, kilichobakia sasa ni kwa mamlaka husika na Serikali kukamilisha mipango iliyobaki ili maji haya yawafikie wananchi" Amesema.

Ameongeza kuwa chini ya mradi huo wamechimba visima 9 na kati ya hivyo visima 7 vinafanya vizuri na  2 vimeharibika na kueleza kuwa matarajio yao  ni kuona visima vitano ambavyo sasa  vimekamilika vizuri vikizalisha  lita milioni 55.

Meneja wa Mamlaka ya Maji Mkuranga mjini (MKUWASA) Muhandisi Filbert Pius akiuzungumzia mradi huo amesema kuwa utakapokamilika utawasaidia wananchi kupata maji safi na kuondoa tatizo la muda mrefu la ukosefu wa maji katika maeneo mbalimbali ya mji huo.

Amesema mahitaji ya maji katika mji huo ni makubwa kuliko uwezo wa sasa wa kuzalisha maji ambapo vyanzo vilivyopo vina uwezo wa kuzalisha lita 135,000 kwa siku  ikilinganishwa na mahitaji ya sasa ya lita 602,000 kwa siku kwa wakazi wapatao 25,847.

" Wananchi sasa watapata nafuu, tofauti kabisa na mwanzo, maji yanayozalishwa hapa ni mengi  lita 1,800,000 kwa siku hii inakidhi  mara mbili mahitaji yote ya wananchi wa mji wa Mkuranga " Amesisitiza Muhandisi Pius.

Ameiomba Serikali kuendelea kutoa fedha za kufanikisha ujenzi wa miundombinu yenye urefu wa kilometa 2 inayotarajiwa kukamilika ndani ya mwezi huu ili Mkuranga  ambao sasa ni mji wa viwanda upate  huduma ya uhakika ya maji,

Pia amesema kukamilika kwa ujenzi wa matenki makubwa ya kuhifadhia maji eneo la Mkwalia ulipo mradi huo pamoja na eneo la Kurungu kutaiwezesha hospitali ya Wilaya ya Mkuranga kupata huduma ya uhakika ya maji ambayo imekuwa kero ya muda mrefu kwa wagonjwa wanafika kupata huduma.

Meneja Uhusiano wa Jamii wa Mamlaka ya Maji Safi na Maji Taka (DAWASA) Bi.Nelly Msuya akifafanua kuhudsu mradi huo amesema unajengwa unatekelezwa na DAWASA kwa niaba ya Serikali na akifafanua kuwa maeneo yote yenye miundombinu ya maji katika wilaya ya Mkuranga yanatarajiwa kuanza kupata huduma hiyo ifikapo Oktoba mwaka huu.

Amesema mradi huo sasa uko katika hatua za majaribio na unatarajiwa kuwanufaisha wananchi wote mara  kukamilika kwa ujenzi wa miundombinu kwenye maeneo ambayo hayakuwa na mabomba ya kusambazia maji , ujenzi wa matenki makubwa ya kuhifadhia maji na kukamilika kwa  taratibu za kitaalam ili maji hayo yawafikie wananchi.

"Nachoweza kusema kwa upande wa wilayanya Mkuranga tumefika pazuri, sisi kama DAWASA watekelezaji wa miradi mbalimbali ya maji kwa niaba ya Serikali tutahakikisha kero ya maji  katika wilaya hii  na maeneo mengine inapatiwa ufumbuzi,  tumeshatoa mamlaka kwa miji na wilaya  kubuni, kusimamia  na kuendeleza miradi ya maji ili wananchi wengi zaidi wanufaike" Amesisitiza.

Aidha, amebainisha kuwa mradi wa ujenzi wa visima 8 eneo la Mkuranga umegharimu kiasi cha shilingi bilioni 7.4 na kufafanua kuwa awamu inayofuata ni kuyapeleka maji hayo yakaunganishwe na mfumo wa kusambazia maji uliopo, ujenzi, uongezaji wa matenki makubwa ya kuhifadhia maji na ununuzi wa pampu ya kusukuma maji hayo kutoka kwenye chanzo.

*TAARIFA KWA UMMA, SAFARI ZA RAIS JAKAYA KIKWETE NJE YA NCHI

$
0
0
JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
WIZARA YA MAMBO YA NJE NA USHIRIKIANO WA KIMATAIFA
 


Simu:255-22-2114615, 211906-12
Barua pepe: nje@nje.go.tz
Barua pepe: gcu@nje.go.tz

Nukushi: 255-22-2116600

              

 


                20 KIVUKONI FRONT,
                           P.O. BOX 9000,
                  11466 DAR ES SALAAM, 
                                    Tanzania.

 
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Safari za Mhe. Rais Jakaya Mrisho Kikwete Nje ya Nchi
Wizara imesikitishwa na taarifa za uongo zilitolewa katika vyombo vya habari kuwa Mhe. Jakaya Kikwete, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika uongozi wake wa miaka 10 ametumia Shilingi trilioni 4 kwa ajili ya safari za kikazi nje ya nchi, ambazo ni wastani wa bajeti nzima ya wizara kwa miaka mitano (5).
Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa inapenda kutoa ufafanuzi kuwa tangu Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete aingie madarakani mwaka 2005, kiasi kikubwa kabisa cha bajeti kuwahi kutengwa kwa ajili ya safari za Viongozi Wakuu yaani Rais, Makamu wa Rais na Waziri Mkuu ni shilingi bilioni 50 ambazo zilitengwa kwa Mwaka wa Fedha 2014/2015 kwa ajili ya Idara ya Itifaki. Kwa miaka mingine yote wastani umekuwa ni kati ya shilingi bilioni tano hadi 25 kulingana na mahitaji ya idara hiyo.
Ifahamike kuwa kiasi hicho cha shilingi bilioni 50 ni bajeti nzima ya Idara ya Itifaki, ambapo kuna fungu maalum kwa ajili ya ziara za viongozi. Fungu hilo linagharamia makundi makuu matano kama ifuatavyo:
1.     Kundi la Rais wakiwemo Wasaidizi, Mawaziri au Wakuu wa Taasisi na Walinzi;
2.     Kundi la Makamu wa Rais wakiwemo Wasaidizi, Mawaziri au Wakuu wa Taasisi na Walinzi;
3.     Kundi la Waziri Mkuu wakiwemo Wasaidizi, Mawaziri au Wakuu wa Taasisi na Walinzi;
4.     Kundi la Wakuu wa Nchi na Serikali kutoka nje ya nchi wanapotembelea Tanzania; na
5.     Kundi la Wajumbe Maalum wanaokuja nchini kuleta taarifa muhimu kwa Rais.
Makundi yote haya hugaramiwa na Serikali kupitia Wizara ya Mambo ya Nje ndani ya bajeti ya Idara ya Itifaki kifungu cha Ziara za Viongozi.  
Aidha uandaaji wa bajeti ya Wizara chini ya Idara ya Sera na Mipango unahusisha wadau wengine nje ya Wizara kama vile Kamati ya Bunge ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa na hupitishwa kila mwaka na Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Tunapenda kuwaatahadharisha wananchi juu ya watu wanaotoa taarifa za uongo kwa madhumuni ya  kujenga chuki dhidi ya Serikali.  Ikumbukwe kuwa ziara za viongozi zinazoratibiwa na Wizara ya Mambo ya Nje zina mafanikio makubwa kwa nchi na Watanzania kwa ujumla.
Wizara inaandaa taarifa ya ndefu ya utekelezaji wa majukumu ya Wizara, changamoto na mafanikio yaliyopatikana ndani ya kipindi cha miaka kumi ya uongozi wa Rais Jakaya Mrisho Kikwete ambayo itatolewa kwa umma kwa lengo la kutoa elimu zaidi. 
Imetolewa na:
Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali kwa Umma,
Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa,
17 Septemba 2015

*LOWASSA ALIPOHUTUBIA KATIKA ZIARA YAKE YA KAMPENI, BARIADI MKOANI SIMIYU

$
0
0
Mgombea Urais wa Tanzania wa UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh. Edward Lowassa, akiwapungia mkono wananchi wa Mji wa Bariadi (hawapo pichani) wakati alipowasili kwenye Uwanja wa Mpira wa Halmashauri Wilaya ya Bariadi Mkoani Simiyu, kulikofanyika Mkutano wa Kampeni zake, anazoendelea kuzifanya katika Majimbo mbali mbali ya Uchaguzi hapa nchini. Katika ziara hiyo, Mh. Lowassa aliambatana na Waziri Mkuu wa Zamani, Mh. Fredrick Sumaye pamoja na Mwanasheria wa CHADEMA, Mh. Tundu Lissu.
Mgombea Urais wa Tanzania wa UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh. Edward Lowassa, akisalimiana na baadhi ya viongozi wa Vyama vinavyounda UKAWA wa Mkoa wa Simiyu, wakati alipowasili kwenye Uwanja wa Mpira wa Halmashauri Wilaya ya Bariadi Mkoani Simiyu, kulikofanyika Mkutano wa Kampeni zake, anazoendelea kuzifanya katika Majimbo mbali mbali ya Uchaguzi hapa nchini. KUSOMA ZAIDI BOFYA READ MORE
Mgombea Urais wa Tanzania wa UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh. Edward Lowassa, akiagana na Mgombea Ubunge wa Jimbo la Badiadi kupitia CHADEMA, Godwin Simba, mara baada ya Mkutano wa Kampeni, uliofanyika kwenye Uwanja wa Halmashauri ya WIlaya ya Bariadi, Mkoani Mkoani humo, leo Septemba 17, 2015. Katikati yao ni Waziri Mkuu wa Zamani, Mh. Fredrick Sumaye na Kulia ni Mwanasheria wa CHADEMA, Mh. Tundu Lissu.

*TAMKO LA VIONGOZI WA DINI KUHUSU UHURU, HAKI NA AMANI KUELEKEA UCHAGUZI MKUU

$
0
0
Sisi, viongozi wa dini pamoja na taasisi zinazosimamia mchakato wa uchaguzi (NEC, TAKUKURU, Polisi pamoja na Msajili wa vyama vya siasa)  tuliokutana  tarehe 17/9/2015, tumepata nafasi ya kujadili kwa kina suala la uhuru,haki na amani kuelekea uchaguzi mkuu utakaofanyika 25/10/2015 na wajibu wa kila mdau kuhakikisha kuwa uhuru,haki na amani vinalindwa kipindi hiki.

Suala la uhuru haki na amani ni wajibu wetu sisi viongozi wa dini na watanzania wote kwa ujumla na halina mjadala.Kila mmoja achukuwe nafasi yake kulinda uhuru,haki na amani na kuweka uzalendo kwanza kuliko kutanguliza maslahi binafsi ya vyama vya siasa.
Viongozi wa dini wamepata nafasi ya kujadili na vyombo hivi masuala ya msingi kama kuhakikisha kuwa maadili ya uchaguzi yanazingatiwa kwa wote, muda wa kutangaza matokeo ya kura unazingatiwa , haki ya wananchi kupata matokeo haraka ili kuepuka fujo wakati wa kusubiri na kutangazwa kwa matokeo. 
Jeshi la polisi kutokutumia nguvu kupita kiasi, wajibu wa Msajili kuhakikisha vyama vyote vinapata fursa sawa na pia tumejadili suala la kutumia nyumba za ibada kama sehemu ya jukwaa la siasa.
Viongozi wa dini tumekubaliana kwa pamoja kuepuka kutumia nyumba za ibada kuonyesha ushabiki wa aina yoyote kwa chama chochote cha siasa.
Baada ya kujadili kwa kina masuala hayo viongozi wa dini wanatoa wito ufuatao;
1. Vyombo vya habari vifanye kazi kwa ueledi bila upendeleo na pia kuhakikisha kuwa inatoa taarifa ya kutosha kuelimisha umma.
2. Tunaishauri NEC kwenye chaguzi zijazo  iweke utaratibu maalum wa kuruhusu wanafunzi wa vyuo vikuu waliojiandikisha pamoja na watu wote waliojiandikisha/watakaojiandikisha waweze kupiga kura.
3. Tunaishauri  NEC    kwenye chaguzi zijazo  siku ya kupiga kura isiwe siku ya ibada.
4. NEC iendelee kutoa elimu ya uraia  kuhusu haki ya raia kupiga kura na haki yao ya  kukaa mita mia moja kusubiri matokeo yatangazwe kwa utulivu kama ambavyo NEC imehakikishia viongozi wa dini kuwa kila kituo itabandika matokeo yote (Urais,Ubunge na Udiwani)
5.  Pamoja na kutimiza wajibu wake wa msingi wa kulinda raia na mali zao Jeshi la polisi wakati huu wa uchaguzi  liendelee kutimiza wajibu wake wa kusimamia amani na taratibu kwa haki bila upendeleo.

6. Wagombea,wafuasi   na wanaowanadi,  wanaaswa waache mara moja lugha za matusi,vitisho,kejeli na kukashifiana vinavyoweza kuchochea fujo na kuleta uvunjifu wa amani wajikite kunadi sera za vyama vyao.

7.Tunawahimiza wananchi kuwa makini katika kufuatilia kampeni na sera mbalimbali za wagombea, kuzipima kwa hali ya juu sera hizo, kutokuuza kadi zao za kupigia kura, kutokununuliwa na kujitokeza kwa wingi kutumia uhuru na haki yao ya kuchagua viongozi wanao wataka kwa hiari na  amani.

 8. Viongozi wa dini wanawahimiza Watanzania wote kuendelea kuombea nchi hii kuendelea kuwa  taifa lililojengwa   katika misingi ya uhuru , haki na amani.
9. Viongozi wa dini tutabaki kuwa manabii na wahubiri wa uhuru,haki na amani wakati huu , wakati wa uchaguzi na baada ya uchaguzi.
Sisi viongozi wa dini Tunawashukuru Inspekta generali wa polisi, Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi, Msajili wa Vyama vya siasa na Mkurugenzi Mkuu wa TAKUKURU kwa ufafanuzi makini na wa kina juu ya nafasi na utayari wao wa kushirikiana na viongozi wa dini kuhakikisha uhuru, haki na amani vinaendelea nchini.

Maelezo yao na mafafanuzi  yao tumeyasikia  na tutaendeleza kwa kuwa  hiki ni kikao cha mwanzo na tutaendelea kuwa na vikao vingine pamoja nao kuelekea uchaguzi mkuu ili kufuatilia utekelezaji na kuendeleza makubaliano yetu katika kuhakikisha uhuru,haki na amani.

*MAMA SAMIA SULUHU ALIVYOITEKA MIKINDANI NA MAFIA

$
0
0
 Mgombea Mwenza wa Urais kwa tiketi ya CCM, Mama samia Suluhu Hassan akihutubia umati wa wananchi katika mkutano wa kampeni, uliofanyika katika mji mdogo wa Mikindani mkoani Mtwara.
 Wananchi wakimshangilia Mgombea Mwenza wa Urais kwa tiketi ya CCM, Mama Samia Suluhu Hassan katika mkutano wa kampeni uliofanyika leo katika mji mdogo wa Mikindani mkoani Mtwara
  Wananchi wakimshangilia Mgombea Mwenza wa Urais kwa tiketi ya CCM, Mama Samia Suluhu Hassan katika mkutano wa kampeni uliofanyika leo katika mji mdogo wa Mikindani mkoani Mtwara
 Mgombea Ubunge jimbo la Mtwara mjini, Murji Mohammed akiomba kura baada ya kunadiwa na Mgombea Mwenza wa Urais kwa tiketi ya CCM, Mama Samia Suluhu Hassan katika mkutano wa kampeni uliofanyika leo katika mji mdogo wa Mikindani mkoani Mtwara
 Wasanii wakichangamsha kwa muziki katika mkutano wa kampeni uliofanyika leo katika mji mdogo wa Mikindani mkoani Mtwara. KUSOMA ZAIDI BOFYA READ MORE

 Mgombea Mwenza wa Urais kwa tiketi ya CCM, Mama Samia Suluhu Hassan na Mgombea Ubunge jimbo la Mtwara mjini, Murji Mohammed wakiwapongeza wasanii baada ya kutumbuiza muziki uliosisimua wananchi wakati wa mkutano wa kampeni uliofanyika leo katika mji mdogo wa Mikindani mkoani Mtwara
 Kada nguri wa CCM, Kijana Mtera Mwampamba, akimuombea kura Mgombea Urais kwa tiketi ya CCM, Dk. John Magufuli, katika mkutano wa kampeni uliofanyika leo katika mji mdogo wa Mikindani mkoani Mtwara
 Mgombea Mwenza wa Urais kwa tiketi ya CCM, Mama samia Suluhu Hassan akimpongeza Mtela Mwampamba baada ya kuhutubia katika mkutano wa kampeni uliofanyika leo katika mji mdogo wa Mikindani mkoani Mtwara
 Mwanamuziki wa msanii wa Bongo Movie, Snura akichangamsha mkutano kwa kuimba wimbo wa kuifangilia CCM, wakati wa mkutano wa kampeni uliofanyika leo katika mji mdogo wa Mikindani mkoani Mtwara
 Baadhi ya wasanii wa Bongo Movie wakishiriki na wananchi wengine kuselebuka muziki, wakati wa mkutano wa kampeni uliofanyika leo katika mji mdogo wa Mikindani mkani Mtwara
 Wananchi wakishangilia wakati wa mkutano wa kampeni uliofanyika katika mji mdogo wa Mikindani mkoani Mtwara
 Wasanii wa kundi la Hapa ni Kazi Tu, wakionyesha umahiri wao walipotumbuiza katika mkutano wa kampeni uliofanyika leo katika mji mdogo wa Mikindani mkoani Mtwara
 Mratibu wa 'Mama Sema na Mwanao' Steve Nyerere akiwa na kamarade, Ally Choky, wakati wa mkutano wa kampeni uliofanyika katika mji mdogo wa Mikindani mkoani Mtwara
 Mgombea Ubunge jimbo la Mtwara Vijijini, Hawa Ghasia akiwa na mtoto aliyepoteana na mama yake, kutokana na wingi wa watu waliofurika wakati wa mkutano wa kampeni za CCM uliofanyika katika mji mdogo wa Mikindani mkoani Mtwara
 Mgmbea Mwenza wa Urais kwa tiketi ya CCM, Mama Samia Suluhu Hassan akipokea wanachama wapya kutoka vyama vya upinzani, kikiwemo Chadema, katika mkutano wa kampeni uliofanyika katika mji mdogo wa Mikindani mkoani Mtwara
 Mama Samia akiungana na vijana kuishangilia CCM baada ya kuwapokea walipoamua kutangaza kuhamia CCM wakati wa mkutano wa kampeni uliofanyika leo katika mji mdogo wa Kimindani mkoani Mtwara.
"'CCM Hoyeeeee" Kijana Rashid Njechele, akipaza sauti kwa kusema hivyo, baada ya kutangaza kuhamia CCM kutoka CUF, wakati wa mkutano wa kampeni wa Mgombea Mwenza wa Urais kwa tiketi ya CCM Mama Samia (kulia), uliofanyika katika mji mdogo wa Mikindani mkoani Mtwara
 Baadhi ya waandishi wa habari na maofisa wa CCM, wakiwa katika ndege, wakati wa safari ya Mgombea Mwenza wa Urais kwa tiketi ya CCM Mama Samia Suluhu Hassan kutoka Mtwara kwenda Kisiwa cha Mafia kufanya mkutano wa kampeni.
 Mgombea Mwenza wa Urais kwa tiketi ya CCM, Mama Samia Suluhu Hassani akishuka kwenye Ndege kwenye Uwanja wa Ndege wa Mafia, alipowasili kwa ajili ya kufanya mkutano wa kampeni katika kisiwa hicho.
 Mgombea Mwenza wa Urais kwa tiketi ya CCM, Maa Samia Suluhu Hassan akiwa na baadhi ya viongozi waliomlaki kwenye Uwanja wa Ndege wa Mafia, baada ya kuwasili kwa ajili ya kuhutubia mkutano wa kampeni katika kisiwa hicho.
 Mgombea Mwenza wa Urais kwa tiketi ya CCM, Mama samia akisoma baadhi ya mabango yaliyokuwa yamebebwa na wananchi kueleza matumaini yao kwake, wakati wa mapokezi, alipowasili katika Kisiwa cha Mafia kuhutubia mkutano wa kampeni. Kushoto ni Mgombea wa Ubunge katika jimbo hilo, Mbarak Dau
 Aliyekuwa Mbunge wa Mafia ambaye pia aliingia katika kinyan'ganyiro cha kuomba ridhaa ya CCm kuwania tena ubunge wa jimbo hilo, Abdulkarim Shah, akimnadi Mgombea wa Ubunge wa jimbo hilo, Mbarak Dau, katika mkutano wa kampeni uliofanyika katika katika Kisiwa hicho cha Mafia
 Mgombea Mwenza wa Urais kwa tiketi ya CCM, Mama Samia Suluhu Hassan akimpongeza Kada wa CUF, Mohamed Albadawi, baada ya kutangaza kuhamia CCM katika mkutano wa kampeni uliofanyika leo katika jimbo la Mafia mkoa wa Pwani. Albadawi awali alikuwa Mgombea Ubunge katika jimbo hilo kwa tiketi ya CUF baada ya kuongoza katika kura za maoni, lakini baadaye akaenguliwa na chama hicho na kupachikwa, Shomari Kimbau ambaye alihamia CUF baada ya kushindwa katika kura za maoni za CCM
 Mgombea Mwenza wa Urais kwa tiketi ya CCM, Mama samia Suluhu Hassan akihutubia mkutano wa kampeni leo katika Jimbo la mafia mkoa wa Pwani
 Mgombea Mwenza wa Urais kwa tiketi ya CCM, Mama samia Suluhu Hassan akimnadi Mgombea Ubunge jimbo la MafiaMbarak Dau katika mkutano wa kampeni uliofanyika katika jimbo hilo mkoa wa Pwani
Mgombea Mwenza wa Urais kwa tiketi ya CCM Mama Samia suluhu (Kushoto), akishiriki kucheza muziki wa taarab uliokuwa ukitumbuizwa na nguli wa muziki huo, Mzee mwishoni mwa mkutano wa kampeni uliofanyika leo katika jimbo la Mafia mkoa wa Pwani. PICHA ZOTE NA BASHIR NKOROMO

*PRESIDENT KIKWETE LEADS A HIGH LEVEL PANEL IN NEW YORK

$
0
0
The Chairman of the UN High level panel on Global Response to Health Crises President Dr.Jakaya Mrisho Kikwete leads a consultative session in New York shortly after he arrived this morning. On the Left is the UN Deputy Secretary General Mr.Jan Eliason.  
The Secretary-General has asked the Panel to make recommendations to strengthen national and international systems to prevent and manage future health crises, taking into account lessons learned from the response to the outbreak of Ebola virus disease.
In carrying out its work, the Panel will undertake a wide range of consultations, including with representatives from the affected countries and communities, the United Nations system, multilateral and bilateral financial institutions and regional development banks, non-governmental organizations, countries supporting the response effort, other Member States, health-care providers, academic and research institutions, the private sector and other experts.  
The Panel will be supported by a Resource Group of leading experts which is to provide advice to the Panel on technical and other issues.
The Panel held its first meeting in early May 2015 and is expected to submit its final report to the Secretary-General at the end of December 2015.  The Secretary-General will make the report available to the General Assembly and undertake further action as appropriate.
Other panel members include Celso Amorim from Brazil, Micheline Calmy Rey from Switzerland, Marty Natalegawa from Indonesia, Joy Pumaphi from Botswana and Rajiv Shah from the US. Photo by Freddy Maro
Viewing all 13053 articles
Browse latest View live