Quantcast
Channel: SUFIANIMAFOTO
Viewing all 13053 articles
Browse latest View live

WAZIRI MKUU MAJALIWA AIPONGEZA KAMPUNI YA PREMIUM AGRO CHEM LTD KWA KUSAMBAZA MBOLEA KIASI KIKUBWA NCHINI

$
0
0
Na Dotto Mwaibale
WAZIRI Mkuu Majaliwa Kassim Majaliwa, ameipongeza Kampuni ya Premium Agro Chem Limited inayojihusisha na mbolea, kutokana na kazi nzuri na kutia ya kusambza kiasi kikubwa cha mbolea kwa wakulima nchini na hivyo kusaidia kupunguza adha iliyokuwa ikiwasumbua baadhi ya wadau wa sekta hiyo.
Waziri Mkuu alitoa kauli hiyo ya pongezi jana alipokuwa akikagua zoezi la upakiaji wa mbolea na usafirishaji ili kufikia malengo ya kutekeleza agizo la hivi karibuni lililotolewa na Rais Dkt.John Pombe Magufuli, Ikulu Jijini Dar es Salaam.
Rais Magufuli, alimuagiza Waziri Mkuu kusimamia zoezi hilo kwa ajili ya kumaliza malalamiko ya wakulima wa mazao ya chakula na biashara kwa mikoa yenye uzalishaji mkubwa wa chakula.
Mikoa maarufu kwa uzalishaji huo inafahamika kama The Big ni Katavi, Rukwa, Songwe, Mbeya, Iringa, Njombe na Ruvuma.
Akizungumza na watendaji wa kampuni hiyo, Waziri Mkuu aliipongeza kutokana na uamuzi wao wa kukubali kufanya kazi hiyo usiku na mchana na kusaidia kupunguza malalamiko ya wakulima.
"Kwa kweli ninawapongeza kwa kazi nzuri, mmetusaidia kwa kiwango cha juu, tunawashuru kwa kazi mliyoifanya na mnayoendelea kuifanya kwa nia njema, huu ni uzalendo mkubwa na unaostahili kupongezwa na kuungwa mkono na kila mpenda maendeleo," alisema Waziri Mkuu Majaliwa.
Alisema wakulima wa mazao ya chakula wanahitaji huduma ya kufikishiwa mbolea kwa wakati, lakini kwa taarifa nilizozipata, kazi kubwa imefanywa na kampuni yenu ndani ya siku mbili hizi, yamesaidia kwa kiasi kikubwa kupunguza kama sio kumaliza kabisa malalamiko ya wadau wenu.
Kwa upande wake Waziri wa Kilimo Dkt. Charles Tizeba, alitumia muda huo kumweleza Waziri Mkuu, kwamba kampuni hiyo imefanyakazi kubwa usiku na mchana kupakia mbolea kwa ajili ya mikoa iliyokuwa na changamoto nyingi.
Alisema mpaka jana usiku, magari makubwa ya kubeba migizo mali ya Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ), yalipakiwa kwa ajili ya kusambaza mbolea zaidi ya tani 600 kwa mikoa ya Rukwa na Katavi.
Lakini pia Mheshimiwa Waziri Mkuu, mawakala wa kampuni hii ya Premium wameendelea kuja hapa na kuchukua mbolea kwa ajili ya kukabilia na hali ya mahitaji makubwa yanayowakabili wakulima vijijini," alisema Waziri Tizeba na kuongeza kwamba kampuni hiyo imeendelea kushirikiana bila masharti na Kampuni ya Taifa ya Mbolea kusambaza mbolea hizo katika maeneo ambayo wao hawana mawakala ama hawana matawi ya kuuzia.

MKUU WA MKOA WA RUVUMA AIPA TANO KAMPUNI YA PREMIUM AGRO CHEM LTD

$
0
0
Na Dotto Mwaibale
MKUU wa Mkoa wa Ruvuma Chritina Mndeme, ameipongeza kampuni ya Premium Agro Chem Limited, kutokana na kazi nzuri iliyofanya ya kuharakisha upatikanaji wa mbolea za kupandia aina ya Urea kwa wakulima wa mkoa wake na wilaya zake kwa ujumla.
Mkuu huyo wa mkoa alisema mazingira ya mkoa huo na mahitaji yaliwafanya viongozi kuwa katika changamoto kubwa, lakini kampuni hiyo imefanyakazi kubwa ya kuwafikishia wakulima hao mbolea. 
Alisema mahitaji ya mkoa wake kwa sasa ni zaidi ya tani 52,700, lakini wamepokea kiasi cha tani 15,200, na kutaka juhudi zaidi zifanyike kwani mbolea ya kupandia inahitajika kwa wakulima hao kabla ya Januari 15 mwaka huu.
"Ninawashukuru sana wadau wa mbolea na kilimo kwenye mkoa wetu, lakini kipekee naomba niwashukuru sana Kampuni ya Premium Agro Chem Ltd, kutokana na kazi nnzuri ya kutusambazia kupitia mawakala wao na hata matawi yao hapa Songea na Mbinga, ninawashukuru na kuwapongeza sana kwa kazi nzuri, wameonyesha uzalendo mkubwa," alisema RC Mndeme.
Mkuu huyo wa mkoa aliwaagiza wakuu wa wilaya na wakurugenzi wa Halmashauri ndani ya mkoa wake, kufuatilia suala la upatikanaji wa mbolea kwa wakulima kwenye maeneo yao na kazi hiyo inatakiwa kufanyika masaa 24 bila kuchoka.
Kwa upande wake Meneja Biashara na Masoko wa kampuni hiyo ya Premium Agro Chem Ltd, Brijesh Barot, alisema kwamba wamesambaza zaidi ya tani 8,200 kwa mkoa wa Ruvuma na bado wanaendelea kusambaza kupitia kwa mawakala wengi zaidi.
"Tunaendelea kusambaza mbolea kwa mikoa yote, Njombe, Ruvuma, Mbeya, Iringa, Rukwa, Songwe na Katavi, kupitia kwa mawakala pamoja na kuwatumia maafisa wetu walio katika vituo vya matawi yetu huko kwa ajili ya kuharakisha upatikanaji wa mbolea kwa wakulima vijijini," alisema Barot.
Alisema kampuni yao inafanyakazi kazi hizo kizalendo na ndio maana wamekubali kuuza kwa bei elekezi mbolea ambayo wao walikuwa wameinunua muda mrefu kabla ya kutolewa kwa maagizo ya kununua kwa mfumo maalum wa serikali, na hili linafanywa kwa kumuunga mkono Rais Dkt Magufuli na Waziri Mkuu Majaliwa Kassim Majaliwa.

NAIBU WAZIRI KWANDIKWA AWATAKA TEMESA KUPELEKA KIVUKO LINDI

$
0
0
 Mkuu wa Mkoa wa Lindi, Godfrey Zambi, akitoa taarifa kwa Naibu Waziri wa Ujenzi, Elias Kwandika, kuhusu hali ya miundombinu ya barabara, madaraja, vivuko, pamoja na viwanja vya ndege katika mkoa huo. Naibu Waziri huyo yupo katika ziara ya kikazi ya siku 3 mkoani humo.
Naibu Waziri wa Ujenzi, Elias Kwandikwa, akizungumza na uongozi wa mkoa wa Lindi katika kikao kazi, kuhusu umuhimu wa wataalamu wote kushirikiana katika masuala ya ujenzi wa miundombinu ya barabara katika mkoa huo. Kulia ni Meneja wa Wakala wa Barabara (TANROADS), mkoa wa Lindi, Mhandisi Isaack Mwanawima akisikiliza.
Meneja wa Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA), mkoa wa Lindi, Mhandisi Grayson Maleko, akitoa maelezo kwa Naibu Waziri wa Ujenzi, Elias Kwandikwa, kuhusu ujenzi wa maegesho ya kivuko kitakachotoa huduma kati ya Lindi Mjini na Kitunda, alipokuwa akikagua ujenzi wake mkoani humo.
Muonekano wa ujenzi wa maegesho ya kivuko kitakachotoa huduma kati ya Lindi Mjini na Kitunda, ambapo mkataba wa kukikokota Kivuko hiko kutoka Pangani mkoani Tanga kuja Lindi upo katika hatua za mwisho.
**************************************
Naibu Waziri wa Ujenzi, Elias Kwandikwa, ameuagiza Uongozi wa Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA) makao makuu kusaini haraka mkataba kwa mkandarasi atakayebeba kivuko kipya  kutoka eneo kinapotengenezwa wilayani Pangani mkoani Tanga hadi mkoani Lindi.
Akizungumza mara baada ya kukagua maegesho ya kivuko hicho ambacho kinatarajiwa kutoa huduma za usafiri kutoka Lindi Mjini - Kitunda mkoani humo, Naibu Waziri huyo amewahakikishia wananchi kutegemea kupata huduma nzuri za usafiri kwani ujenzi wa kivuko na  maegesho  yake  kwa sasa umefika katika hatua nzuri.
"Naagiza Mamlaka husika kusaini haraka mkataba kwa mkandarasi atakayebeba kivuko hiki kutoka Tanga hadi hapa ili wananchi waone kwamba kivuko kimefika na kipo tayari kwa ajili ya kutoa huduma", amesema Naibu Waziri Kwandikwa.
Aidha, Naibu Waziri huyo ameridhishwa na ujenzi wa maegesho hayo ambayo kwa sasa ujenzi wake umebakia asilimia 10 na hivyo kutarajiwa kukamilika muda wowote.
Katika hatua nyingine Naibu Waziri Kwandikwa, ametembelea na kukagua uwanja wa ndege wa Lindi ambapo amesema Serikali inaendelea na mpango wake wa kuboresha viwanja vya ndege nchini ili kuimarisha huduma katika usafiri wa anga.

Amefafanua kuwa Serikali kupitia mwaka wa fedha 2018/19 licha ya kuwa na mpango wa kuboresha uwanja huo pia itaboresha Uwanja wa ndege wa Kilwa Masoko lengo ni kuleta maendeleo kwa wananchi.
Kwa upande wake Meneja wa TEMESA mkoani Lindi, Mhandisi Greyson Maleko, amemhakikishia Naibu Waziri huyo kujipanga katika kuhakikisha wananchi wa Lindi wanapata huduma bora za kivuko.
Naye, Mbunge wa Viti Maalum kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), mkoani humo Mheshimiwa Hamida Abdallah, ameipongeza na kuishukuru Serikali ya Awamu ya Tano kwa kusogeza maendeleo kwa wananchi na kutatua changamoto mbalimbali zinazowakabili.
Naibu Waziri Kwandikwa amemaliza ziara ya kikazi ya siku Tatu mkoani humo ambapo ametembelea na kukagua Miradi mbalimbali inayotekelezwa na Wizara yake ili kujionea maendeleo na changamoto zake.

DKT FAUSTINE AWAHASA WANANCHI KUSHIRIKI KIKAMILIFU SHUGHULI ZA MAENDELEO.

$
0
0
 Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na watoto Dkt. Faustine Ndugulile akikagua mashine ya  Utla Sound wakati akiwa katika ziara yake Mkoani Katavi ya kukagua shughuli za utoaji wa huduma za Afya na kutathimini shughuli za maendeleo zinazofanywa na wananchi wenyewe kwa kushirikiana na Serikali.
 Naibu Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na watoto Dkt. Faustine Ndugulile akiwaonesha nembo ya MSD GOT inayotambulisha kuwa Dawa hiyo inatolewa na Serikali kwa wananchi. KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

 Naibu Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na watoto Dkt. Faustine Ndugulile akikagua moja kati ya Friji ya kuhifadhi Dawa za chanjo
Naibu Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na watoto Dkt. Faustine Ndugulile akiwa ndani ya duka la Dawa la MSD kufanya ukaguzi juu ya upatikanaji wa Dawa zote, Kulia ni Mfamasia wa duka hilo Bahati Kazimili
Naibu Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na watoto Dkt. Faustine Ndugulile akiongea na mgonjwa katika wodi ya Wazazi katika Hospitali ya Manispaa Mpanda wakati akiwa katika ziara yake Mkoani Katavi ya kukagua shughuli za utoaji wa huduma za Afya, Kulia ni Mganga Mkuu Manispaa ya Mpanda Dkt. Mahenge

Naibu Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na watoto Dkt. Faustine Ndugulile akifuatilia taarifa ya dawa katika Bin card kwenye chumba cha uhifadhi dawa kituo cha Afya Kanoge.
*********************************************
Na WAMJW. KATAVI.
Naibu Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsioa,Wazee na Watoto Dkt.Faustine Ndugulile amewataka wananchi kutumia nguvu  kazi yao katika ujenzi na uboreshaji wa Zahanati katika Wilaya zao kuliko kupeleka pesa nyingi kwa wakandarasi.
Dkt.Ndugulile ameyasema hao wilayani hapa wakati wa ziara ya kikazi ya  kukagua shughuli za utoaji huduma za afya na kutathimini  shughuli za maendeleo ikiwemo ya upanuzi wa miundombinu zikiwemo ya Zahanati
Alisema kutumia nguvu kazi zao itasaidia  kwa kiasi kikubwa kupunguza gharama ambazo zingeweza kujitokeza kama wangetoa tenda hiyo kwa wakandarasi.”Nyinyi ndio wasimamizi wakuu wa shughuli hizi na mkiharibu tutakuja kuwalaumu nyinyi
Aidha,alisema Serikali imetoa shilingi milioni 400 kwa ajili ya kuboresha miundombinu  ya huduma za afya  nchini  kwa upande wa uzazi wa dharura ikiwemo upasuaji, wodi ya wazazi,maabara ,wodi ya watoto pamoja na nyumba ya mtumishi kwenye vituo vya afya ambapo ujenzi huo unaanza mara moja
Kwa upande mwingine Dkt. Ndugulile ameendele kuwatoa hofu wananchi juu ya hali ya upatikanaji wa dawa, huku akiwasisitiza wananchi wasiuziwe dawa zozote muhimu kwani hali ya upatikanaji wa Dawa ni nzuri maeneo yote na sasa ni wastani wa asilimia 80.

“Katika kituo cha Afya Kanoge, bajeti ya dawa imeongezeka kutoka Milioni 300 mpaka Bilioni 2.5, kwahiyo dawa tunazo za kutosha, hivyo hatutarajii kuona mtu aje hapa aambiwe akanunue dawa sehemu nyingine, wamenithibitishia waganga wangu asilimia 90 ya dawa muhimu zipo” aliendelea Dkt. Ndugulile

Wakati huo huo Dkt. Ndugulile amesisitiza watumishi wa afya juu ya utunzaji wa kumbukumbu za dawa katika stoo ya madawa ikiwemo kuweka za kujua idadi za dawa zilizoingia na kutoka pamoja na utunzaji wa takwimu za mahudhurio ya wagonjwa wa kila siku, jambo linalopunguza ufanisi katika kazi.

Hata hivyo Dkt. Ndugulile amemtaka Mganga Mkuu wa Manispaa ya Mpanda Dkt. Mahenge kuanzisha ofisi ya kushughulikia malalamiko ya watu pindi wanapokutana na changamoto wakati wakipata huduma katika Kituo hicho cha Afya.

Naye Mganga Mkuu wa Mkoa wa Katavi Dkt. Yahaya Hussein wakati akiwasilisha taarifa ya Mkoa alisema kuwa Mkoa wa Katavi unakabiriwa na uhaba mkubwa wa watumishi wa kada ya Afya hali inayopelekea changamoto kubwa katika utoaji wa huduma kwa wananchi.
“Hadi kufikia Septemba 2017 Mkoa wa Katavi una jumla ya watumishi 693 sawa na asilimia 28 kati ya watumishi 2,437 wanaohitajika, kati ya hao 19 ni watumishi ngazi ya Mkoa na 674 ngazi ya Serikali za mitaa, kwa ujumla Mkoa wa Katavi una jumla ya upungufu wa watumishi 1,744” Alisema Dkt.  Hussein.
Dkt. Yahaya Hussein aliongeza kuwa Mkoa unaendelea kuzisimamia Halmashauri kuhakikisha zinatenga bajeti kwa ajili ya kuwakatia kadi za Afya ya Jamii (CHF) wazee ili kuendelea kupata Huduma za Afya kwa urahisi katika maeneo yao.
Mpaka kufikia Mwezi Septemba 2017 jumla ya wazee 19,248 wametambuliwa, na kati ya hao jumla ya wazee 1,807 sawa na asilimia 9.4 wameshapatiwa kadi za CHF katika Halmashauri zote za Mkoa wa Katavi.

KATIBU MKUU KIONGOZI BALOZI JOHN KIJAZI APOKEA KWA NIABA YA RAIS KANUNI ZA SHERIA YA MADINI NAMBA 7 YA MWAKA 2017

$
0
0
Waziri wa Sheria na Katiba Profesa Palamagamba Kabudi akimpa muhtasari Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi kabla ya kumkabidhi vitabu vya Kanuni za sheria ya Madini namba 7 ya mwaka 2017 ambaye anapokea kwa niaba ya Rais Dkt John Pombe Magufuli aliyeagiza kuandaliwa kwa kanuni hizo ndani haraka ili sheria iweze kufanya kazi. Hafla hiyo ndogo, iliyohudhuriwa pia na Manaibu Waziri wa Madini Mhe. Doto Biteko na pamoja na Katibu Mkuu wa Wizara ya Madini, Profesa Simon Msanjila, imefanyika Ikulu jijini Dar es salaam leo Alhamisi 11, 2018
Waziri wa Sheria na Katiba Profesa Palamagamba Kabudi akimsikiliza Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi baada ya ya kumkabidhi vitabu vya Kanuni za sheria ya Madini namba 7 ya mwaka 2017 ambaye anapokea kwa niaba ya Rais Dkt John Pombe Magufuli aliyeagiza kuandaliwa kwa kanuni hizo ndani haraka ili sheria iweze kufanya kazi. Hafla hiyo ndogo, iliyohudhuriwa pia na Manaibu Waziri wa Madini Mhe. stanslaus Nyongo na Mhe. Doto Biteko na pamoja na Katibu Mkuu wa Wizara ya Madini, Profesa Simon Msanjila, imefanyika Ikulu jijini Dar es salaam leo Alhamisi 11, 2018
Waziri wa Sheria na Katiba Profesa Palamagamba Kabudi akimkabidhi Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi vitabu vya Kanuni za sheria ya Madini namba 7 ya mwaka 2017 ambaye anapokea kwa niaba ya Rais Dkt John Pombe Magufuli aliyeagiza kuandaliwa kwa kanuni hizo ndani haraka ili sheria iweze kufanya kazi. Hafla hiyo ndogo, iliyohudhuriwa pia na Manaibu Waziri wa Madini Mhe. Doto Biteko na pamoja na Katibu Mkuu wa Wizara ya Madini, Profesa Simon Msanjila, imefanyika Ikulu jijini Dar es salaam leo Alhamisi 11, 2018
Waziri wa Sheria na Katiba Profesa Palamagamba Kabudi akimkabidhi Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Philip Mpango kitabu cha Kanuni za sheria ya Madini namba 7 ya mwaka 2017 baada ya Balozi Kijazi kuvipokea kwa niaba ya Rais Ikulu jijini Dar es salaam leo Alhamisi 11, 2018. Wengine ni Manaibu Waziri wa Madini Mhe. Stanslaus Nyongo na Mhe. Doto Biteko, pamoja na Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango Bw. Dotto James na Katibu Mkuu wa Wizara ya Madini, Profesa Simon Msanjila.
Waziri wa Sheria na Katiba Profesa Palamagamba Kabudi, Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Philip Mpango, Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi na Manaibu Waziri wa Madini Mhe. Stanslaus Nyongo na Mhe. Doto Biteko, Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango Bw. Dotto James pamoja na Katibu Mkuu wa Wizara ya Madini, Profesa Simon Msanjila, wakiwa na vitabu vya Kanuni za sheria ya Madini namba 7 ya mwaka 2017 baada ya Balozi Kijazi kuvipokea kwa niaba ya Rais Ikulu jijini Dar es salaam leo Alhamisi 11, 2018. Picha na Ikulu

KIGWANGALA ASISITIZA KUWEPO KAULI MBIU YA KUTANGAZA UTALII

$
0
0

Waziri wa Maliasili na Utalii Dkt. Khamis Kigwangalla akisisistiza jambo wakati wa hafla ya uzinduzi wa Kamati ya Kitaifa ya Utambulisho wa Utalii wa Tanzania leo hafla iliyofanyika katika ukumbi wa Chuo cha Taifa cha Utalii Jijini Dar es Salaam leo. Kamati hiyo yenye wajumbe 22 imeundwa na Mhe. Waziri kwa lengo la kupitia na kubuni mkakati mbadala wa namna ya kutangaza utalii wa Tanzania ndani na nje ya nchi.
**************************************
WAZIRI wa Maliasili na Utalii Dkt.Hamis Kigwangala amesema ipo haja ya kuwa na kauli mbiu ambayo itatumika kuutangaza utalii wa Tanzania katika mataifa mbalimbali duniani.

Amesema Tanzania imejaaliwa kuwa na maeneo mengi ya utalii lakini hayajafahamika kutokana na nguvu ndogo ya kuyatangaza kwake, hivyo kusababisha watalii wengi kufanya utalii katika maeneo machache ya utalii ukiwamo Mlima Kilimanjaro. KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA
Dk.Kigwangala ametoa kauli hiyo jijini Dar es Salaam leo wakati anazindua Kamati ya Utambulisho wa Utalii Tanzania na kufafanua kuna vivutio vingi na sasa ipo haja kuendelea kuvitangaza kwa nguvu zote.
Amesema wajumbe wa kamati watakuwa na jukumu la kuweka mikakati sahihi ya kuhakikisha utalii wa Tanzania unaendelea kutangazwa kwa lengo la kuongeza watalii wa ndani na nje ya nchi.
"Tunayo maeneo mengi ya utalii lakini yanayofahamika ni machache, kuna watalii wanakuja kwa ajili ya kwenda Mlima Klimanjaro na wengine Mbuga ya Serengeti wakati yapo maeneo mengi ya utalii.Lazima tutangaze utalii wetu na hii kamati itatusaidia kutuongoza,"amesema Dk.Kigwangala.
Amewataka wajumbe wa kamati hiyo kutafuta kauli mbiu ambayo itautangaza utalii wa Tanzania nchi mbalimbali duniani.
"Iwe kauli mbiu ambayo itatutofautisha Tanzania na nchi nyingine kwenye mambo ya utalii na lazima tuwe na kauli mbiu ya kipekee katika kuutangaza utalii wetu,"amesema Dk.Kigwangala.
Amefafanua kuna mbuga za wanyama 16 lakini zinazotambulika chache,hivyo juhudi zinahitaji kutangaza vivuto vya utalii vilivyopo.
Mwenyekiti Mwenza wa Kamati ya Kitaifa ya Utambulisho wa Utalii Tanzania Richard Lugimbana amemhakikishia Dk.Kigwangala kuwa wanatambua jukumu ambalo wamepewa na hivyo ni wajibu wao kuweka mikakati ambayo itasaidia kuutambulisha utalii wetu. 
Mkurugenzi Mtendaji wa Bodi ya Utalii Devotha Mdachi amefafanua kamati hiyo ina jumla ya wajumbe 21 ambao wengi wao ni watalaamu wa masoko.
Ameongeza utambulisho mpya kwa ajili ya kutangaza utalii wa Tanzania utaifanya nchi kuwa katika ramani nzuri ya kutambulika kwa vivutio vyake vya utalii.
Mwenyekiti wa Kamati ya Kitaifa ya Utambulisho wa Utalii wa Tanzania Bibi. Devotha Mdachi akielezea jambo mbele ya wajumbe wa kamati hiyo (hawapo pichani) mara baada ya kuzinduliwa rasmi kwa Kamati hiyo leo Jijini Dar es Salaam. Kulia ni Mwenyekiti Mwenza wa Kamati hiyo Richard Rugimbana. Kamati hiyo yenye wajumbe 21imeundwa na Mhe. Waziri kwa lengo la kupitia na kubuni mkakati mbadala wa namna ya kutangaza utalii wa Tanzania ndani na nje ya nchi.
Baadhi ya wajumbe wa Kamati ya Kitaifa ya Utambulisho wa Utalii wa Tanzania wakifuatilia hotuba ya Waziri wa Maliasili na Utalii Dkt. Khamis Kigwangalla wakati wa hafla ya uzinduzi wa kamati hiyo leo Jijini Dar es Salaam. Kamati hiyo yenye wajumbe 21 imeundwa na Mhe. Waziri kwa lengo la kupitia na kubuni mkakati mbadala wa namna ya kutangaza utalii wa Tanzania ndani na nje ya nchi.
Waziri wa Maliasili na Utalii Dkt. Khamis Kigwangalla (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na wajumbe wa Kamati ya Kitaifa ya Utambulisho wa Utalii wa Tanzania lmara baada ya uzinduzi wa kamati hiyo leo Jijini Dar es Salaam. Kamati hiyo yenye wajumbe 21 imeundwa na Mhe. Waziri kwa lengo la kupitia na kubuni mkakati mbadala wa namna ya kutangaza utalii wa Tanzania ndani na nje ya nchi. Picha na Frank Shija – MAELEZO

TANESCO YATOA SIKU NNE (4) KWA WADAIWA SUGU WA BILI ZA UMEME

$
0
0
Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) tunautaarifu Umma na Wateja wetu wote kuwa, tumetoa muda wa siku nne (4) kuanzia Januari 12, 2018 hadi siku ya Jumatatu Januari 15, 2018 kwa wadaiwa sugu wawe wamelipa madeni yao.
Baada ya muda huo kuisha Shirika litasitisha Huduma ya umeme dhidi ya Wateja watakaoshindwa kulipa madeni ikiwa ni pamoja na kuchukua hatua zingine za kisheria.
Ofisi za TANESCO zitakuwa wazi siku ya Jumamosi Saa 3:00 Asubuhi hadi Saa 9:00 Mchana.

mawasiliano
Kituo cha miito ya simu Makao Makuu +255 222 194 400 na +255 768 985 100
Tovuti: www.tanesco.co.tz, mitandao ya kijamii:
Mitandao ya kijamii
Twitter, www.twitter.com/tanescoyetu,
Facebook https://www.facebook.com/tanescoyetultd/
IMETOLEWA NA: OFISI YA UHUSIANO
TANESCO MAKAO MAKUU
JANUARI 11, 2018

NAIBU SPIKA TULIA ACKSON AWAJULIA HALI MAPACHA WALIOUNGANA WALIOLAZWA TAASISI YA JKCI

$
0
0
 Kaimu Mkurugenzi wa Tiba Shirikishi wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) ambaye pia ni Daktari Bingwa wa Magonjwa ya Moyo Delila Kimambo akimweleza  Naibu Spika wa Bunge Mhe. Dkt.  Tulia Ackson maendeleo ya afya za pacha walioungana Maria na Consolata waliolazwa  Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) kwa ajili ya Matibabu.
*******************************
Naibu Spika wa Bunge Mhe. Dkt. Tulia Ackson kupitia Taasisi ya Tulia (Tulia Trust Fund) akabidhi TV sita (6) kwa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) ambazo zimefungwa katika wodi na kliniki za watoto. Awajulia hali pacha walioungana Maria na Consolata waliolazwa katika Taasisi hiyo kwa ajili ya Matibabu.
 Picha no. 2 Naibu Spika wa Bunge Mhe. Dkt.  Tulia Ackson akiwajulia hali pacha walioungana Maria na Consolata waliolazwa  katika Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI)kwa ajili ya Matibabu.
Naibu Spika wa Bunge Mhe.  Dkt.  Tulia Ackson akimkabidhi Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Utawala na Fedha Agnes Kuhenga Televisheni moja kati ya nne zilizotolewa na Taasisi ya Tulia (Tulia Trust Fund) kwa ajili ya watoto wanaotibiwa katika Taasisi hiyo. Jumla ya TV sita zimetolewa na Tulia Trust ambazo zimefungwa  katika wodi na kliniki za watoto.
  Naibu Spika wa Bunge Mhe. Dkt. Tulia Ackson akimjulia hali mtoto aliyelazwa katika Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) kwa ajili ya matibabu.  Mhe. Dkt. Tulia kupitia Taasisi ya Tulia (Tulia Trust Fund) ametoa TV sita kwa JKCI ambazo zimefungwa  katika wodi na kliniki za watoto.
 Naibu Spika wa Bunge Mhe. Dkt. Tulia Ackson akimjulia hali mtoto aliyelazwa katika Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) kwa ajili ya matibabu.  Mhe. Dkt. Tulia kupitia Taasisi ya Tulia (Tulia Trust Fund) ametoa TV sita kwa JKCI ambazo zimefungwa  katika wodi na kliniki za watoto. Picha na JKCI

KIYOMBO MCHEZAJI BORA DISEMBA

$
0
0
Mshambuliaji wa Mbao FC ya Mwanza, Habibu Kiyombo amechaguliwa Mchezaji Bora wa mwezi Disemba wa Ligi Kuu ya Vodacom (VPL) msimu wa 2017/2018.
Kiyombo ameibuka mchezaji bora baada ya kuwashinda wachezaji wenzake wawili alioingia nao fainali kutokana na tathmini iliyofanywa na kikao cha Kamati ya Tuzo wiki hii.
Kwa mwezi Disemba ambao timu 12 kati ya 16 zinazoshiriki ligi hiyo kila moja ilicheza mechi moja, Kiyombo aliisaidia timu yake kufunga mabao mawili katika mchezo dhidi ya Yanga ambao Mbao ilishinda mabao 2-0.
Kutokana na matokeo hayo, Mbao ilipanda kutoka nafasi ya nane hadi ya saba katika msimamo wa ligi, huku Kiyombo akifikisha mabao saba ya kufunga kwake msimu huu, akiwa nyuma ya Emmanuel Okwi wa Simba anayeongoza akiwa na mabao nane.
Kiyombo aliwashinda mshambuliaji wa Simba, John Bocco aliyefunga mabao mawili katika ushindi wa 2-0 wa Simba dhidi ya Ndanda na beki Bruce Kangwa aliyeisaidia Azam katika ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya Stand United.
Katika mchezo huo wa Azam, beki huyo alifunga bao moja na kutoa pasi ya usaidizi wa bao lingine. Wachezaji wote hao hakuna aliyepata kadi.
Kutokana na ushindi huo, Kiyombo atazawadiwa tuzo, kisimbusi cha Azam na fedha taslimu sh. 1,000,000 (milioni moja) kutoka kwa wadhamini wakuu wa Ligi hiyo, Kampuni ya Vodacom.
Wachezaji wengine ambao tayari wametwaa tuzo ya mwezi kwa msimu huu ni Emmanuel Okwi (Agosti), Shafiq Batambuze (Septemba), Obrey Chirwa (Oktoba) na Mudathir Yahya( Novemba).

WIZARA YA MALIASILI NA UTALII YATANGAZA RASMI VIWANGO VIPYA VYA ADA KWA MAWAKALA WA KUSAFIRISHA WATALII NCHINI

$
0
0
Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla (kulia) na Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Maj. Gen. Gaudence Milanzi (kushoto).
************************************
Na Hamza Temba-WMU-Dar 
Wizara ya Maliasili na Utalii imetangaza rasmi viwango vipya vya malipo ya ada kwa Mawakala wa kusafirisha watalii nchini baada ya kukamilika kwa marekebisho ya kanuni ya ada na tozo za biashara ya utalii yaliyofanyika mwezi Desemba mwaka jana, 2017.
Taarifa iliyotolewa jana na Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Maj. Gen. Gaudence Milanzi, imeeleza kuwa baada ya kukamilika kwa marekebisho hayo ya kanuni, Tangazo la Serikali namba 506 la tarehe 29 Desemba, 2017, limeweka viwango vipya vya ada kwa mawakala wa kusafirisha watalii (Tour Operators na Safari Outfitters).
Taarifa hiyo imeeleza viwango hivyo kuwa ni shilingi sawa na dola za Kimarekani 500 kwa kampuni za wazawa zenye umiliki mkubwa wa raia wa Tanzania na zinazomiliki gari 1 hadi 3.
"Shilingi sawa na dola za Kimarekani 2,000 kwa kampuni zenye gari 4 hadi 10, shilingi sawa na dola za Kimarekani 3,000 kwa kampuni zenye gari 11 hadi 50 na shilingi sawa na dola za Kimarekani 5,000 kwa kampuni zenye kumiliki gari 51 na kuendelea", imeeleza taarifa hiyo.
Kwa upande wa kampuni za kigeni zenye umiliki mkubwa wa raia wa kigeni na zinazomiliki gari 10 hadi 30 zitalipa ada ya shilingi sawa na dola za Kimarekani 5,000, kampuni zenye gari 31 hadi 50 zitalipa shilingi sawa na dola za kimarekani 7,500 na na kampuni zenye gari 51 na kuendelea zitalipa shilingi sawa na dola za Kimarekani 10,000.
Kufuatia marekebisho hayo, muda wa kutumika kwa leseni za mwaka 2017 za Wakala wa kusafirisha watalii (Tour Operators na Safari Outfitters) umesogezwa mbele hadi tarehe 31 Januari, 2018 ili kuwezesha maandalizi ya kuingia kwenye mabadiliko ya viwango hivyo vipya.
Aidha, taarifa hiyo imeeleza kuwa maombi ya usajili na leseni za biashara ya utalii na leseni za waongoza watalii kwa mwaka 2018 kwa wafanyabiashara wapya na wanaoendelea na biashara yanaendelea kupokelewa.
Waombaji wote wametakiwa kufuata masharti ya uombaji wa leseni hizo ikiwemo kuwasilisha nakala za hati za usajili wa magari zilizothibitishwa kisheria kwa Wakala wa kusafirisha watalii (wapya na wanaoendelea na biashara) na kivuli cha leseni ya mwaka 2017 kwa wafanyabiasbara wote. 
"Ni kosa kisheria kuwasilisha taarifa za uongo na adhabu yake ni pamoja na kufutiwa leseni", imeeleza sehemu ya taarifa hiyo.
Desemba 10 na 11 mwaka 2017, Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla alikutana na wadau wa sekta ya utalii jijini Arusha kwa lengo la kuwashirikisha katika mapendekezo ya viwango vipya vya ada kwa Wakala wa kusafirisha watalii ambavyo vilivyotolewa na Wizara yake. Mapendekezo ya viwango hivyo yalilenga kuongeza mapato na kuwawezesha wafanyabiashara wadogo wenye gari kuanzia moja kuingia katika biashara hiyo.

RAIS WA ZANZIBAR DKT. SHEIN ATUNUKU NISHANI YA MAPINDUZI NA UTUMISHI ULIOTUKUKA LEO

$
0
0
 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein, akitunuku Nishani ya Mapinduzi yaviongozi na Wananchi Wenye Sifa Maalum Bi. Fatma Said Ali, wakati wa hafla hiyo iiliyofanyika katika viwanja vya Ikulu Zanzibar kuadhimisha miaka 54 ya Mapinduzi ya Zanzibar, leo mchana.
 Dkt Shein akimtunuku Nishani,  Salum Nassor Said (MKWECHE)  
Dkt. Shein  akimtunuki Nishani, Msanii Maarufu wa Taarab Zanzibar Mwanacha Hassan Kijore.
 Dkt. Shein, akimtunuku Nishani ya Utumishi wa Serikali Saleh Sadik Osman,
 Dkt. Shein, akisalimiana na Viongozi wa Vyombo vya Ulinzi na Usalama, wakati wa hafla hiyo 
 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Ali Mohamed Shein, akiwa katika picha ya pamoja na watunukiwa wa Nishani za Mapinduzi na Utumishi wa Serikali baada ya hafla hiyo ya kukabidhi iliyofanyika katika viwanja vya Ikulu Zanzibar. 
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein, akiwa katika picha na Wawakilishi na Ndugu na Jamaa wa Viongozi marehemu waliofika mbele ya haki wakipokea kwa niaba ya Wazee wao,Nishani za Mapinduzi na Utumishi wa Serikali baada ya hafla hiyo ya kukabidhi iliofanyika katika viwanja vya Ikulu Zanzibar. Picha na Ikulu     

TAN COMMUNICATION MEDIA WAMLILIA ZUBERI MSABAHA

MAKAMU WA RAIS AHUDHURIA MSIBA WA SAID NATEPE

$
0
0
  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa amekaa pamoja na Mama Siti Mwinyi mke wa Rais Mstaafu wa Awamu ya Pili (kushoto) pamoja na Huda Karume mke wa Balozi Ali Karume kwenye msiba wa Bw. Said Abdallah Natepe aliwahi kuwa Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais na Utawala Bora. 
Makamu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania leo alijumuika na Viongozi pamoja na wananchi Mazizini kwenye msiba wa Marehemu Said Abdallah Natepe
   Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa amekaa pamoja na Mama Siti Mwinyi mke wa Rais Mstaafu wa Awamu ya Pili (kushoto) pamoja na Huda Karume mke wa Balozi Ali Karume kwenye msiba wa Bw. Said Abdallah Natepe aliwahi kuwa Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais na Utawala Bora. 
Rais Mstaafu wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar akiwasili Mazizini kuhudhuria msiba wa Said Abdallah Natepe
 Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe. Balozi Seif Idd akiwasili Mazizini kuhudhuria msiba wa Said Abdallah Natepe.
 Mwili wa marehemu Said Natepe ukibebwa tayari kwenda kupumzishwa kwenye makaburi ya Mwache. 
Mwili wa marehemu Said Natepe ukibebwa tayari kwenda kupumzishwa kwenye makaburi ya Mwache.  Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais

CAF YAMTEUA RAIS KARIA KUSIMAMIA CHAN

$
0
0
Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania(TFF) Ndugu Wallace Karia ameteuliwa na Shirikisho la Mpira wa Miguu Barani Africa CAF kuwa kamishna wa mechi ya kwanza ya ufunguzi wa Fainali za Africa kwa wachezaji wa ndani CHAN kati ya Morocco na Mauritania itakayochezwa Januari 13, 2018.
Mchezo huo ambao Rais Karia atausimamia akiwa Kamishna utachezwa kwenye Uwanja wa nyasi asilia wa Mohamed V huko Casablanca.
Waamuzi watakaochezesha mchezo huo ni Janny Sikazwe kutoka Zambia atakuwa muamuzi wa katikati akisaidiwa na muamuzi msaidizi namba moja kutoka Kenya Marwa Aden Range na muamuzi msaidizi namba mbili akitokea Msumbiji Arsenio Chandreque Maringula wakati muamuzi wa mezani Louis Hakizimana akitokea Rwanda.
Mchezo huo unaohusisha timu mwenyeji unatarajiwa kufuatiliwa na mashabiki wengi zaidi.
Rais Karia hivi karibuni pia aliteuliwa na CAF kuwa mmoja wa wajumbe wa kamati ya maandalizi ya michuano hiyo ya CHAN itakayoanza Januari 13 mpaka Februari 4, 2018.
Mashindano hayo yanayofanyika kwa mara ya tano(5) bingwa mtetezi akiwa DR Congo.

DKT. NDUGULILE AING’ARISHA PROGRAMU YA KIKUNDI MLEZI KWA WANAWAKE WAJASIRIAMALI MKOANI KATAVI.

$
0
0
  Naibu Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Dkt. Faustine Ndugulile (Mb) akiangalia moja ya bidhaa ya mvinyo inayotengenezwa na Kikundi cha Wanawake wajasiriamali cha Humbaji kilichopo katika Manispaa ya Mpanda alipofanya ziara ya siku mbili ya kuamsaha ari ya wananchi kufanya shughuli za maendeleo ili kuchangia azma ya kufikia uchumi wa kati na wa viwanda.
Naibu Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto he. Dkt. Faustine Ndugulile (Mb) akishona sweta kwa kutumia mashine maalum wakati alipotembelea Kikundi cha wanawake wajasiriamali kilichopo katika Manispaa ya Mpanda mkoani Katavi alipofanya ziara ya siku mbili ya kuamsha ari ya wananchi kuanzisha shughuli za maendeleo. KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

    Naibu Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Dkt. Faustine Ndugulile (Mb) akiangalia sweta lililotengenezwa na moja ya kikundi cha wanawake wajasiliamali  wakati alipotembelea Kikundi cha wanawake wajasiriamali kilichopo katika Halmashauri ya Wilaya ya Mpanda katika ziara yake ya  siku mbili ya kuamsha ari ya wananchi kufanya shughuli za maendeleo.
Naibu Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Dkt. Faustine Ndugulile(Mb) akizungumza na vikundi vya wanawake wajasilimali wa Wilaya ya Mpanda mkoani Katavi alipofanya ziara ya siku mbili ya kuamsha ari ya wananchi kufanya shughuli za maendeleo.
 Mkuu wa Wilaya ya Mpanda akiwahamasisha wanawake wa Manispaa ya Mpanda na Mkoa wa Katavi kujiunga na vikundi vya ujasiriamali ili kuweza kuunganisha nguvu ya kufanya biashara zao wakati wa ziara ya siku mbili ya Naibu Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Dkt. Faustine Ndugulile(Mb.) ya kuamsaha ari ya wananchi kushiriki shughuli za maendeleo.
Mratibu wa Dawati la Maendeleo ya Jamii kutoka Ofisi ya Rais TAMISEMI Bi. Mwajina Lipinga akielezea umuhimu wa Maafisa maendeleo ya Jamii katika kuwakusanya na kuwaunganisha wananwake katika vikundi vya wajasiriamali ili waweze kujikwamua kiuchumi wakati wa ziara ya siku mbili ya Naibu Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Dkt. Faustine Ndugulile(Mb) ya kuamsha ari ya wananchi kufanya shughuli za maendeleo.
Naibu Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Dkt. Faustine Ndugulile (Mb.) akitoa motisha kwa mwakilishi  wa kikundi kitakaocholelewa na Kikundi kingine ikiwa ni utekelezaji wa programu ya ‘Kikundi Mlezi’ yenye lengo la kuwawezesha wanawake wajasilimali kuwezeshana  wenyewe katika kuanzisha na kuendeleza miradi ya kibiashara.
Naibu Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Dkt. Faustine Ndugulile (Mb) akiwa katika picha ya pamoja na moja ya kikundi cha wanawake wajasiliamali kilichopo katika Manispaa ya Mpanda mara baada ya kuhitimisha ziara ya siku mbili ya kuamsha ari ya wananchi kufanya shughuli za maendeleo. Picha na Kitengo cha Mawasiliano WAMJW
*******************************************
Naibu Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Dkt. Faustine Ndugulile (Mb) ameing’arisha programu ya ‘Kikundi Mlezi’ katika Manispaa ya Mpanda mkoani Katavi yenye lengo la kuwawezesha wanawake wajasirimali kuwezeshana  wenyewe katika kuanzisha na kuendeleza miradi ya biashara zao.
Dkt. Ndugulile ameitambulisha  programu hiyo wakati alipofanya ziara ya siku mbili katika manispaa ya Mpanda mkoani Katavi katika zoezi la kuamsha ari ya wananchi kuibua miradi na kuanzisha shughiuli za uzalishaji kawa kuzingatia fursa, mazingira na soko.
Dkt.Ndugulile amesema kuwa  ili kufanikisha kufikiwa kwa Tanzania ya viwanda Serikali itaendelea kuwasaidia wajasiriamali wadogo wadogo hasa wanawake katika kuwawezesha kuanzisha vikundi vitakayoanzisha viwanda vidogo vidogo na vya kati.
Ameongeza kuwa lengo la kuzindua Programu ya ‘Kikundi Mlezi’ ni kuwashirikisha wanawake wajasirimali waliokomaa katika biashara kuwasaidia wanawake wajasiriamali wanaoanza shughuli hizo kwa kuwapatia uelewa wa soko, mbinu za biashara, upatikanaji wa mikopo na mahitaji ya kiufundi.
“Niseme programu hii itasaidia kwa asilimia kubwa kuibua wanawake ambao hawakuwa na uwezo katika kuanzisha biashara zao na kufanya wanawake kujiunga na vikundi na hatimaye kuanzisha viwanda vidogo na vya kati”alisisitiza Mhe. Dkt. Ndugulile.
Kwa upande wake Mkuu wa  Wilaya ya Mpanda Mhe. Lilian Matinga amesema kuwa program ya ‘Kikundi Mlezi’ itasaidia kuwainua wanawake na kujitokeza kwa wingi kujishughulisha na shughuli za uzalishaji.
Naye Mwakilishi wa Katibu Mkuu Maendeleo ya Jamii, Jinsia,Wazee na Watoto Bw. Julius Mbilinyi  amesema kuwa Wizara itaendelea kuhamasisha wanawake kujitokeza na kujiunga na vikundi na kusaidiana katika kuendesha biashara ambazo zitawasaidia kujikwamua kiuchumi.
Mmoja wa Wanawake wajasiliamali Wilayani Mpanda Bi.Nuru Saimon ameishukuru Serikali kwa kuzindua Mpango huo utakaowawezesha wanawake kusaidiana  katika kuanzisha na kuinuka katika biashara ambazo zitawasaidia kujikwamua kiuchumi.
Naibu Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Dkt. Faustine Ndugulile (Mb) amefanya ziara ya siku mbili mkoani Katavi na kuwatembelea wanawake wajasiliamali katika kuhamasisha wanawake kujishughulisha ili kusaidia kufikia lengo la kuwa na Tanzania ya Viwanda. Msisitizo umetolewa kwa wananchi kupenda bidhaa zetu kwa kununua bidhaa zetu wenyewe ili kufikia lengo la uanzishaji wa viwanda 100 kwa kila mkoa.

MWILI WA MAMA PERAS NGOMBALE MWIRU, WAZIKWA LEO MAKABURI YA KINONDONI JIJINI DAR

$
0
0
Jeneza lenye mwili wa Marehemu Mama Peras Ngombale Mwiru (Mama Kinje), Mke wa Mmoja waasisi wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Mzee Kingunge Ngomale Mwiru ukiwasili kwenye makaburi ya Kinondoni jijini Dar es salaam, alikopumzishwa kwenye nyumba yake ya milele. Mama Peras (Mama Kinje) amezikwa jioni ya leo kwenye makaburi Kinondoni, huku viongozi mbalimbali wa Kitaifa na Vyama vya siasa wakishiriki mazishi hayo.
Rais Mstaafu, Dkt. Jakaya Kikwete akiwa na familia ya Marehemu, wakishuhudia Jeneza lenye mwili wa Mama Peras Ngombale Mwiru likishushwa kaburini, wakati wa mazishi yake yaliyofanyika jioni ya leo kwenye makaburi ya Kinondoni jijini Dar es salaam. Kushoto kwake ni Mtoto wa Marehemu Mama Peras, Kinje Ngombale Mwiru aliyeambatana na mkewe.
Mume wa Marehemu Mama Peras Ngombale Mwiru, Mzee Kingunge Ngombale Mwiru akiweka udongo kwenye kaburi ya Mke wake mpendwa, wakati wa mazishi yake yaliyofanyika jioni ya leo kwenye makaburi ya Kinondoni jijini Dar es salaam.
Mtoto wa Marehemu Mama Peras, Kinje Ngombale Mwiru na Mkewe Anitha wakiweka udongo kwenye kaburi la Mama yao. 
Rais Mstaafu, Dkt. Jakaya Kikwete akiweka udongo kaburini.
Askofu akiweka msalaba kaburini.
Waziri Mkuu Mstaafu, Edward Lowassa na Mkewe Mama Regina wakiweka shada ya maua kwenye kaburi la Mama Peras Ngombale Mwiru (Mama Kinje), Mke wa Mmoja waasisi wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Mzee Kingunge Ngomale Mwiru
Waziri Mkuu Mstaafu, Jaji Joseph Warioba na Mkewe wakiweka shada ya maua kwenye kaburi la Mama Peras Ngombale Mwiru (Mama Kinje), Mke wa Mmoja waasisi wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Mzee Kingunge Ngomale Mwiru
Mama Anna Mkapa akiweka shada ya maua kwenye kaburi la Mama Peras Ngombale Mwiru (Mama Kinje), Mke wa Mmoja waasisi wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Mzee Kingunge Ngomale Mwiru.

MATUKIO KATIKA PICHA SHEREHE ZA MIAKA 54 YA MAPINDUZI YA ZANZIBAR

$
0
0
Amiri Jeshi Mkuu na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akifurahia jambo na Rais Mstaafu wa awamu ya pili Mzee Ali Hassan Mwinyi pamoja na Rais Mstaafu wa Awamu ya nne Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete mara baada ya kuwasili katika uwanja wa Amani kwa ajili ya kuhudhuria sherehe za sherehe za miaka 54 ya Mapinduzi ya Zanzibar.
Rais wa Zanzibar Mhe. Dkt. Ali Mohamed Shein akipungia mkono wakati akiwasili katika uwanja wa Amani.

Amiri Jeshi Mkuu na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza jambo na Rais wa Zanzibar Mhe. Dkt. Ali Mohamed Shein katika sherehe za miaka 54 ya Mapinduzi ya Zanzibar zilizofanyika katika uwanja wa Abeid Amani Karume kisiwani humo.
Amiri Jeshi Mkuu na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na Rais wa Zanzibar Mhe. Dkt. Ali Mohamed Shein pamoja na viongozi wengine wa kitaifa wakiwa wamesimama wakati gwaride la heshma(halionekani pichani) lilipokuwa likipita katika sherehe za miaka 54 ya Mapinduzi ya Zanzibar zilizofanyika katika uwanja wa Abeid Amani Karume kisiwani humo. 
Amiri Jeshi Mkuu na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Mama Fatma Karume mara baada ya kuwasili katika uwanja wa Amani kisiwani Zanzibar.

Baadhi ya Mabalozi wa Nchini mbalimbali wanaowakilisha nchi zao Tanzania wakifuatilia sherehe za Maadhimisho ya Miaka 54 ya Mapinduzi ya Zanzibar katika viwanja vya Amaan Zanzibar.
Rais wa Zanzibar Mhe. Dkt. Ali Mohamed Shein akihutubia mamia ya wananchi waliohudhuria katika sherehe za miaka 54 ya Mapinduzi ya Zanzibar zilizofanyika katika uwanja wa Abeid Amani Karume kisiwani Zanzibar.
Rais mstaafu wa awamu ya Tatu Benjamini Mkapa akifurahia jambo wakati alipokuwa akizungumza na Rais mstaafu wa Zanzibar Amani Abeid Karume katika sherehe za miaka 54 ya Mapinduzi ya Zanzibar zilizofanyika katika uwanja wa Abeid Amani Karume kisiwani Zanzibar.
Amiri Jeshi Mkuu na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akipokea Saluti kutoka kwa Mkuu wa Majeshi Jenerali Venance Mabeyo pamoja na Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini (IGP) Simon Sirro mara baada ya kuhudhuria sherehe za miaka 54 ya Mapinduzi ya Zanzibar zilizofanyika katika uwanja wa Abeid Amani Karume kisiwani Zanzibar.
Wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Taifa cha Zanzibar SUZA wakipita mbele ya jukwaa kuu katika maandamano ya sherehe za sherehe za miaka 54 ya Mapinduzi ya Zanzibar
Rais wa Zanzibar Mhe. Dkt. Ali Mohamed Shein akikagua gwaride la Heshma katika sherehe za miaka 54 ya Mapinduzi ya Zanzibar zolizofanyika katika uwanja wa Amani.
Amiri Jeshi Mkuu na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na Rais Mstaafu wa awamu ya Tatu Benjamin Mkapa mara baada ya sherehe za miaka 54 ya Mapinduzi ya Zanzibar zolizofanyika katika uwanja wa Amani. 
Amiri Jeshi Mkuu na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiondoka katika uwanja wa Amani mara baada ya kuhudhuria sherehe za miaka 54 ya Mapinduzi ya Zanzibar.

Amiri Jeshi Mkuu na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na wanachi mara baada ya sherehe za miaka 54 ya Mapinduzi ya Zanzibar zilizofanyika katika uwanja wa Abeid Amani Karume kisiwani Zanzibar.
PICHA NA IKULU

WAWILI WATUPWA JELA MIAKA MITANO KWA KUSAFIRISHA DHAHABU

$
0
0
WAFANYABIASHARA wawili maarufu Naushad Mohammed Suleiman (63) na Ali Makame Juma (36) wakazi wa Zanzibar, wamehukumiwa kwenda jela miaka mitano au kulipa faini ya jumla ya sh.milioni sita baada ya kukiri mashtaka ya kusafirisha madini ya dhahabu vipande saba vyenye thamani ya Sh milioni 989.7 bila kuwa na leseni. 
Hukumu hiyo imesomwa jana jioni na Hakimu Mkazi Mkuu Wilbard Mashauri wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu.
Akisoma hukumu hiyo, Hakimu Mashauri amesema washtakiwa wametiwa hatiani kwa kukiri makosa waliyoshitakiwa nayo ya uhujumu uchumi ambayo ni kula njama na kusafirisha dhahabu bila kuwa na kibali.
Aidha mahakama imeamuru kuwa, miche saba ya dhahabu pamoja na fedha za nchi 25 ambazo washtakiwa walikamatwa nazo zimetaifishwa na serikali.
Kabla ya kusomwa kwa adhabu, upande wa mashtaka ulitoa niche saba ya dhahabu, fedha za nchi 25 za kigeni zikiwa kwenye mabegi mawili.
Kabla ya kusomewa adhabu mahakama iliuliza upande wa mashtaka kama wanalolote la kusema ambapo, Wakili Faraja Nchimbi aliiomba mahakama itoe adhabu Kali kwa washtakiwa ili iwe fundisho kwao na kwa wengine wenye mawazo ya kutenda kosa kama hilo.
Alisema vitendo vilivyofanywa na washtakiwa vinaleta hasara kubwa kwa nchi ya Tanzania na pia vinachangia kwa asilimia kubwa kurudisha nyuma uchumi wa Tainzania.
"Mheshimiwa ni rai yetu, washtakiwa wanastahili kupata adhabu Kali kwa mujibu wa sheria ili pia kulinda rasilimali za nchi yetu, amesema Nchimbi".
Katika utetezi wao washtakiwa wakiwakilishwa na Wakili wao Emmanuel Safari aliomba mahakama kutowapa washtakiwa adhabu Kali kwa kuwa ni wakosaji wa mara ya kwanza na pia wamekiri wenyewe kutenda makosa na wameondoa usumbufu wa kuita mashahidi kwani wamejutia makosa waliyotenda.
Aliongeza kuwa kitendo cha washtakiwa kuachia mali waliyokamatwa nayo ambayo ni mali halali inaonyesha kuwa wameishajiadhibu. " Tunaomba mahakama izingatie kutokuwa na leseni ni suala ambalo wengi hawalijui hivyo wameishajiadhibu wenyewe" amedai Safari.
Ameongeza, mshtakiwa Mohammed ni mgonjwa hawezi kusimama vizuri pia anasumbuliwa na ugonjwa wa moyo.
"Nimezingatia maombi ya upande wa mashtaka na uteezi wenu kuwa ni wakosaji wa mara ya kwanza lakini kitendo mlichofanya ni kosa na kinafanya uchumi wa nchi hii udidimie"
" Mahakama inawahukumu katika shtaka la kula njama kulipa faini ya sh.milioni mbili au kwenda jela miaka miwili na katika shtaka la pili la kusafirisha dhahabu mnatakiwa kulipa faini ya sh.milioni nne na mkishindwa mtatumikia kifungo cha miaka mitatu jela, na ikiwa mtaenda gerezani adhabu zote zitaenda pamoja", alisema Hakimu Mashauri.
Mapema jana asubuhi, wakati kesi hiyo ilipokuja kutajwa, upande wa mashtaka ukiwakilishwa na Wakili wa Serikali, Jehovaness Zacharia ulidai mahakani hapo kuwa Mkurugenzi wa Mashitaka nchini (DPP), ametoa kibali cha kuipa mamlaka mahakama hiyo kusikiliza shauri hilo.
Baada ya kueleza hayo, Hakimu Mashauri aliutaka upande wa mashitaka kuwasomea makosa upya ambapo wakili Zacharia alidai kuwa washitakiwa wanakabiliwa na makosa mawili, ambapo inadaiwa kati ya November Mosi na 29, 2017 katika siku isiyofahamika kati ya Dar es Salaam na Mkoa wa Geita, walikula njama kufanya kosa la kusafirisha madini nje ya nchi isivyohalali.
Pia wanadaiwa November 29, 2017 katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Aman Karume, walikutwa wakisafirisha madini kwenda Dubai katika Falme za Kiarabu ambavyo in vipande saba vya dhahabu vyenye uzito wa kilogramu 18.354 vyenye thamani ya Sh. milioni 989.7 bila kuwa na leseni.

VIKAO VYA KAMATI ZA BUNGE KUANZA JUMATATU

MAFURIKO YA CHEMBA DODOMA YAUA MTU MMOJA

$
0
0
Askari wa zimamoto wakiendelea na zoezi la kuokoa watu waliozingirwa na maji.
Mkuu wa wilaya ya Chemba Simon Odunga akizungumza na maafisa wa jeshi la zimamoto katika zoezi la kuhamisha wananchi waliozingirwa na maji.
Wananchi wakihamisha mali zao kutokana na nyumba zao kuzingirwa na maji.
Wananchi wakihamisha mali zao kutokana na nyumba zao kuzingirwa na maji.
Wananchi wakihamisha mali zao kutokana na nyumba zao kuzingirwa na maji.
**********************************
Mtu mmoja mkazi wa kijiji cha Mwakisebe kata ya Kimaha wilayani chemba mkoani Dodoma amefariki dunia, huku watu wengine zaidi ya 2000 wakiwa hawana mahali pa kuishi baada ya nyumba zao kubomoka na nyingine kuzingirwa na maji, kufuatia mvua kubwa zinazoendelea kunyesha wilayani humo.
Wilaya ya Chemba ni miongoni mwa wilaya mpya zinazopatikana makao makuu ya nchi Dodoma ambapo katika msimu wa mvua hizi za masika maeneo mbalimbali ya mkoa wa Dodoma yamekuwa yakipata mvua nyingi zinazosababisha mafuriko na adhari mbalimbali kujitokeza ikiwemo kuharibika kwa miundombinu ya barabara.
Athari za mvua hizo zimejitokeza katika vijiji vya Olboloti,Kaloleni na Mrijo Chini ambavyo ndivyo vinavyodaiwa kuwa ndio vimeathiriwa zaidi na mafuriko hayo.
Kwa upande wake, Mwenyekiti wa kijiji cha Olboloti Abdalah Suti amesema kuwa mvua iliyonyesha katika maeneo yao ni kubwa na kwamba haijawahi kutokea tangu miaka ya 1960.
Amiry Issa ni Mkuu wa zimamoto kituo cha Dodoma amesema kuwa kikosi kinaendelea na shughuli za uokozi kuzunguka vijiji hivyo huku akiwataka wananchi kutosogelea maeneo hatarishi.
Akizungumzia hilo,Mkuu wa wilaya ya Chemba ambaye pia ni mwenyekiti wa kamati ya ulinzi na usalama wilaya hiyo, Simon Odunga amesema kuwa eneo wanaloishi wananchi hao ni eneo hatarishi kwani wanazungukwa na milima huku akiwataka wananchi waliojenga katika maeneo ya mabondeni kuhama mara moja.
Viewing all 13053 articles
Browse latest View live


<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>