↧
NJIA YA RELI YASOMBWA NA MAJI KOLOSA HUDUMA YA USAFIRI YASITISHWA
↧
JAFO, SHAKA WAMPIGIA DEBE KUNIKUNI KISARAWE
Kaimu Katibu Mkuu wa Umoja wa Vijana Chama Cha Mapinduzi(CCM) Shaka Hamdu Shaka akiwa na Mbunge wa Kisarawe Selemani Jafo katika ufungaji wa kampeni za uchaguzi mdogo wa udiwani Kata ya Kurui.
Kaimu Katibu Mkuu wa Umoja wa Vijana Chama Cha Mapinduzi(CCM) Shaka Hamdu Shaka akivishwa skafu wakati alipofika katika kata ya Kurui kufunga kampeni za uchaguzi mdogo wa udiwani wa kata hiyo.
Kaimu Katibu Mkuu wa Umoja wa Vijana Chama Cha Mapinduzi(CCM) Shaka Hamdu Shaka akimnadi mgombea wa udiwani wa kata ya Kurui Mussa Kunikuni
Kaimu Katibu Mkuu wa Umoja wa Vijana Chama Cha Mapinduzi(CCM) Shaka Hamdu Shaka akipokea mmoja wa wanachama kutoka vyama vya upinzani
Mbunge wa Kisarawe Selemani Jafo akizungumza katika ufungaji wa kampeni za udiwani kata ya Kurui
*******************************************
Kaimu Katibu Mkuu wa Umoja wa Vijana Chama Cha Mapinduzi(CCM) Shaka Hamdu Shaka amemwagia sifa Mbunge wa Jimbo la Kisarawe Mhe. Selemani Jafo kwa uchapakazi wake uliotukuka na hivyo amewataka wananchi wa kata ya Kurui wilayani Kisarawe wasifanye makosa kabisa wahakikishe wanamchagua Mussa Kunikuni kuwa diwani wa kata hiyo katika uchaguzi utakaofanyika kesho Januari 13, mwaka huu.
Akifunga kampeni za uchaguzi mdogo wa udiwani wa Kata ya Kurui Shaka amesema wananchi watakapomchagua Mussa Kunikuni hapo kesho itasaidia kuleta maendeleo makubwa katika kata hiyo kwa kuwa atakuwa anaunganisha juhudi kubwa inayofanywa na Rais John Pombe Magufuli pamoja na Mbunge Jafo katika suala zima la utekelezaji wa Ilani ya CCM ndani ya kata hiyo na wilaya nzima kwa ujumla.
Naye,Mwenyeki wa mkoa wa Pwani ndugu Ramadhani Maneno amewataka wananchi wa kata hiyo kutofanya makosa katika uchaguzi wa kesho kwani mkoa mzima wa Pwani umeelekeza jicho lake katika kata hiyo ile kuleta heshima kwa mkoa wa Pwani.
↧
↧
DC ALI HAPI AZIPONGEZA DAWASA NA DAWASCO KWA USIMAMIZI MZURI UTEKELEZAJI WA UJENZI WA MIRADI YA UBORESHAJI MAJI
Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni jijini Dar es Salaam, Mhe., Ali Hapi, (katikati), akiteremka kutoka juu ya tenki kubwa la kuhifadhia maji linalojengwa huko Mabwepande nje kidogo ya jiji, wakati wa ziara yake ya kukagua maendeleo ya utekelezaji wa mradi wa ujenzi wa miundombinu ya maji wilayani kwake Januari 13, 2018.![]()
NA K-VIS BLOG/Khalfan Said
MKUU wa wilaya ya Kinondoni Mhe. Ali Hapi, amewataka wakandarasi wanaotekeleza ujenzi wa mradi wa uboreshaji wa huduma za ugawaji na usambazaji maji wilayani kwake kuongeza kasi ya kukamilisha mradi huo kama ambavyo mkataba unaelekeza.
Mhe. Hapi aliyasema hayo leo Januari 13, 2018 mwishoni mwa ziara yake ya kukagua maendeleo ya ujenzi wa miundomnbinu hiyo inayohusisha matenki makubwa manne na vituo vinne vya kusukuma maji (Booster Stations) ikiwa ni pamoja na utandikaji wa mabomba ya kusafirisha maji.
“Mradi huu ulipaswa kuwa umekamilika Novemba mwaka jana, lakini hatua waliyofikia baadhi ya maeneo wako asilimia 80, mengine asilimia 75 na mengine asilimia 50, ahadi yao ni kwamba ndani ya kipindi kifupi kijacho wataweza kukamilisha mradi huu.” Alisema
Hata hivyo Mheshimiwa Hapi amepongeza usimamizi na ufuatiliaji wa karibu unaofanywa na mamlaka husika zinzosim amia mradi huo. “Niwapongeze DAWASA na DAWASCO kwa kazi nzuri ya kuhakikisha wanasimamia na kufuatilia utekelezaji wa mradi huu.” Alisema Mhe. Hapi.
Alitaja maeneo yatakayofaidika na mradi huu kuwa ni pamoja na wakazi wa Makongo, Changanyikeni, Salasala, Bunju, Mabwepande na Wazo.
“Mradi ukikamilika utaondoa kero ya maji katika wilaya yetu kwa asilimia 95, kwa hivyo, hii nifaraja kubwa kwa wananchi wa Kinondonbi hususan katika maeneo nilkiyoyataja.” Alifafanua.
Mhe. Hapi, akimsikiliza Mkandarasi, Mhandisi P.G. Rajani(kulia) wa kampuni ya WAPCOS limited ya India, alipotembelea sehemu ya ujenzi wa tenki kubwa la kuhifadhia maji huko Salasala jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Modester Mushi kaimu mkurugenzi wa ufundi DAWASA.
Mhe. Hapi na msafara wake wakipanda juu ya tanki linalojengwa.
Mhe. Hapi akipokelewa na Meneja Uhusiano wa Jamii, DAWASA, Bi. Neli Msuya, wakati akiwasili huko Makongo Juu, kuanza ziara ya kukagua miradi hiyo.
Meneja Uhusiano wa Jamii, Bi. Neli Msuya, (wapilia kushoto) na Afisa Uhusiano wa Jamii wa DAWASA, Bi. Mecky Mdaku, wakimsubiri Mkuu wa wilaya Mhe. Hapi, alipozuru eneo la Makongo Juu kukagua ujenzi wa kituo cha kusukuma maji.
Mhe. Hapi, (kulia), akifurahia jambo na afisa kutoka DAWASCO, Bi.Judith Singinika(katikati), baada ya kutembelea eneo la ujenzi Bunju.
Tenki kubwa likifunikwa huko Salasala.
Mhe. Hapi, (kushoto), akiwa na Bi.Modester Mushi kaimu mkurugenzi wa ufundi DAWASA, (kulia) na Bi. Neli Msuya, Meneja Uhusiano wa Jamii, DAWASA, walipotembelea ujenzi wa kituo cha kusukuma maji Bunju.
Mkuu wa Wilaya Mhe. Hapi, akizungumza na waandishi wa habari mwishoni mwa ziara hiyo, huko Mabwepande.
Bi.Mecky Mdaku, Afisa Uhusiano wa Jamii, DAWASA, akipanda juu ya tenki la Makongo Juu lililofikia asilimia 80 kukamilika
↧
MWENYEKITI WA CHAMA CHA MAPINDUZI (CCM) RAIS MHE. DKT. MAGUFULI AKUTANA NA KUFANYA MAZUNGUMZO NA KATIBU WA ITIKADI NA UENEZI WA (CCM) HUMPHREY POLEPOLE IKULU JIJINI DAR
Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Rais Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Katibu wa Itikadi na Uenezi wa (CCM) Humphrey Polepole kabla ya kuanza mazungumzo yao Ikulu jijini Dar es Salaam.
Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi CCM Rais Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika mazungumzo na Katibu wa Itikadi na Uenezi wa (CCM) Humphrey Polepole Ikulu jijini Dar es Salaam.
Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Rais Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi CCM Rais Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli mara baada ya mazungumzo yao Ikulu jijini Dar es Salaam.
Katibu wa Itikadi na Uenezi wa (CCM) Humphrey Polepole akizungumza mara bada ya kikao chake na Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi CCM Rais Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli Ikulu jijini Dar es Salaam. PICHA NA IKULU
↧
AZAM FC MABINGWA WA KOMBE LA MAPINDUZI TENA 2018
AZAM FC imetwaa tena Kombe la Mapinduzi kwa mara ya pili mfululizo baada ya ushindi wa penalti 4-3 dhidi ya URA ya Uganda kufatia sare ya 0-0 ndani ya dakika 90 usiku wa leo Uwanja wa Amaan, Zanzibar.
Katika mchezo huo uliohudhuriwa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Ali Mohammed Shein, shujaa wa Azam FC alikuwa ni mlinda mlango, Mghana Razack Abalora aliyecheza penalti mbili za wachezaji wa URA.
Abalora aliye katika msimu wake wa kwanza Azam FC tangu asajiliwe kutoka West African Football Academy (WAFA FC) ya Ghana alipangua penati ya kwanza ya URA iliyopigwa na Parrick Mbowa nay a mwisho iliyopigwa na Brian Majwega.
Waliofunga penalti za Azam FC ni Nahodha Himid Mao, Yakubu Mohammed, Enock Atta Agyei na Aggrey Morris wakati Bruce Kangwa alimpelekea mikononi mpira kipa wa URA, Alionzi Nafian na penalti za URA zimefungwa na Charles Ssempa, Shafiq Kagimu na Jimmy Kulaba.
Katika mchezo huo uliochezeshwa na refa mkongwe visiwani hapa, Mfaume Nassor aliyesaidiwa na Mbaraka Haule na Dalila Jaffar, dakika 90 zilikuwa ngumu timu zote zikishambuliana kwa zamu na ziwaendee makipa wa timu zote, Abalora na Alionzi Nafian kwa kuokoa vizuri.
Ushindi huu unamaanisha Azam FC wanatwaa Kombe la Mapinduzi kwa mara ya nne ya rekodi, baada ya awali kulibeba pia katika miaka ya 2012, 2013 na 2017 wakiipiku Simba SC ya Dar es Salaam iliyotwaa mara tatu 2008, 2011 na 2015.
Yanga SC ndiye bingwa wa kwanza wa Kombe la Mapinduzi mwaka 2007 wakati timu nyingine zilizotwaa taji hilo ni Miembeni mwaka 2009, Mtibwa Sugar mwaka 2010 na KCCA ya Uganda mwaka 2014.
Jumla ya timu 11 zilishiriki michuano ya mwaka huu ambazo ni URA, Jamhuri, Mwenge, Azam na Simba zilizokuwa Kundi A na Zimamoto, Mlandege, Yanga, JKU, Taifa Jan’gombe na Singida United zilizokuwa Kundi B.
Kikosi cha Azam FC kilikuwa; Razack Abalora, Himid Mao, Bruce Kangwa, Aggrey Morris, Yakubu Mohammed, Abdallah Kheri/Joseph Mahundi dk59, Stephan Kingue, Frank Domayo/Iddi Kipagwile dk58, Salmin Hoza, Bernard Arthur/Shaaban Iddi dk58 na Yahya Zayed/Enock Atta-Agyei dk64.
URA;Alionzi Nafian, Enock Kibumba, Brian Majwega, Allan Munaaba, Patrick Mbowa, Julius Mutyaba, Nicholas Kagaba, Kalama Deboss/Charles Ssempa dk66, Moses Sseruyide/Peter Lwasa dk81, Hudu Mulikyi na Shafiq Kagimu/Jimmy Kulaba dk82.
↧
↧
BREAKING NEEEEEWZZZZ!!!!! WATU 11 WAFARIKI DUNIA KWA AJALI YA GARI
↧
WAGONJWA 64,093 WATIBIWA KATIKA TAASISI YA MOYO JAKAYA KIKWETE KWA MWAKA 2017

Wagonjwa 225 walifanyiwa upasuaji wa moyo wa kufungua kifua ambapo wagonjwa 200 waliruhusiwa na wagonjwa 25 walifariki Dunia hii ikiwa ni sawa na asilimia 11 (wastani wa kimataifa ni asilimia 13). Kati ya wagonjwa 225 waliofanyiwa upasuaji wa kufungua kifua wagonjwa 105 walifanyiwa upasuaji na madaktari wetu bingwa wa magonjwa ya moyo watoto wakiwa ni 60 na watu wazima 45.
Upasuaji wa moyo wa bila kufungua kifua (Catheterization) kwa kutumia mtambo wa Cathlab ulifanyika kwa wagonjwa 800 kati ya hao 798 wanaendelea vizuri na wagonjwa wawili (2)walifariki hii ikiwa ni chini ya asilimia 1.6. Kati ya wagonjwa 800 waliotibiwa wagonjwa watu wazima 631 walifanyiwa upasuaji na madaktari wetu wa ndani.
Tulikuwa na jumla ya kambi za matibabu 15. Tumefanya matibabu ya pamoja na washirika wetu kutoka mabara ya Asia, Australia, Ulaya na Amerika. Katika kambi zote hizo kambi za watoto ni tano na kambi za watu wazima 10. Jumla ya wagonjwa 120 walifanyiwa upasuaji wa kufungua kifua kati ya hao watoto 80 na watu wazima ni 40. Wagonjwa 169 walifanyiwa upasuaji wa bila kufungua kifua kati ya hao watoto 92 na watu wazima 77.
Kwa wagonjwa wote hao 1025 kufanyiwa upasuaji wa kufungua kifua na bila kufungua kifua hapa nchini Taasisi imeweza kuokoa zaidi ya bilioni 29 (Tshs. 29,725,000,000/=) ambazo Serikali ingezilipa kama wagonjwa hawa wangefanyiwa upasuaji wa moyo nje ya nchi. Gharama za mgonjwa mmoja anayetibiwa nje ya nchi ugonjwa wa moyo ni zaidi ya milioni 29.
ulifanya upasuaji wa kuunganisha mishipa ya damu (AVF- Arterio Venous Fistula) kwa ajili ya kusafishia damu kwa wagonjwa wenye matatizo ya figo (Hemodialysis) 52.
Wakati huo huo Taasisi ilishiriki katika utoaji wa huduma ya upimaji afya bila malipo na kutoa elimu ya afya bora ya moyo kwa wananchi katika mikoa ya Dar es Salaam, Dodoma, Lindi na Katavi. Katika mikoa hiyo tuliweza kuwaona na kuwapatia huduma wananchi 8000.
Malengo tuliyokuwa nayo kwa mwaka huu wa 2018 ni kuona wagonjwa wengi zaidi ya hawa tuliowaona mwaka 2017 katika kliniki zetu za kila siku na kufanya upasuaji. Taasisi imejipanga kufanya upasuaji wa kufungua kifua kwa wagonjwa 400 na bila kufungua kifua kwa wagonjwa 1000.Tunatarajia kuwa na kambi maalum za upasuaji wa moyo zisizozidi 15.Aidha tunawaahidi wananchi kwa mwaka 2018 tutaendelea kutoa huduma katika kiwango cha kimataifa, kuendelea kupunguza kupeleka wagonjwa nje ya nchi, kupunguza gharama za tiba katika Taasisi yetu, kuongeza idadi ya huduma, kuboresha usafi zaidi katika Hospitali yetu na kuzidi kushirikiana na Serikali na wananchi. Changamoto kubwa tunayokabiliana nayo katika kazi zetu za kila siku ni ufinyu wa chumba cha uangalizi maalum (ICU) kwa wagonjwa wanaotoka katika chumba cha upasuaji. Hii inatokea wakati ambao tunafanya upasuaji kwa wagonjwa wengi kwa wakati mmoja hasa kipindi cha kambi za matibabu. Pamoja na ufinyu wa wodi ya watoto. Asilimia 70 ya wagonjwa tunaowafanyia upasuaji wa kufungua kifua ni watoto, tunajumla ya vitanda 123 kati ya hivi vitanda vya watoto ni 24 tu.
Wagonjwa wengi tunaowapokea mioyo yao kutokuwa katika hali nzuri hii ni changamoto nyingine tunayokabiliana nayo katika matibabu ya wagonjwa wetu.
Kwa upande wa wazazi na walezi tunawaomba wasisahau kupima afya za watoto wao pale watakapoona kuna hali ya tofauti katika ukuaji wa mtoto kwani magonjwa mengi ya moyo yanaanzia utotoni. Mtoto akianza kuuguwa magonjwa ya moyo wazazi wengi wanadhani ni matatizo ya kifua baada ya kumfikisha Hospitali na kufanyiwa vipimo ndipo inagundulika mtoto anasumbuliwa na magonjwa ya moyo. Kwa wamama wajawazito wafanye uchunguzi (Fetal Echocardiography) wa kuangalia kama mtoto aliyeko tumboni anamatatizo ya moyo.awashauri watu wazima kujenga tabia ya kupima afya zao mara kwa mara hii itawasaidia kujuwa kama wana matatizo ya moyo au la na hivyo kupata tiba kwa wakati.
Katika Bara la Afrika Taasisi yetu iko katika nafasi ya tatu katika utoaji wa huduma bora za magonjwa ya moyo hasa katika upasuaji wa moyo kwa watoto.
↧
TRL YATANGAZA MABADILIKO YA RATIBA ZA USAFIRI TRENI YA BARA
Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Reli Tanzania (TRL) ambaye ni Mkurugenzi Mkuu Msaidizi (Uendeshaji) Focus Sahani, akizungumza na waandishi wa habari.
*********************************************
Na Ripota wa Mafoto Blog, Dar
KAMPUNI ya Reli Tanzania (TRL) imesema imeamua kuhamishia huduma ya usafiri wa treni kutokea mkoani Dodoma kuanzia kesho badala ya Dar es salaam kama ilivyozoeleka.
Uamuzi huo unakuja kipindi ambacho TRL imesitisha huduma za usafiri huo kutokea Dar es Salaam baada ya miundombinu ya reli kuharibika kati ya stesheni za Kilosa na Gulwe kutokana na mafuriko ya mvua zinazonyesha maeneo hayo na kuharibu miundombinu.

Sehemu ya miundombinu ya reli iliyoharibika
******************************
Akizungunza na waandishi wa habari kutoa ratiba za usafiri huo jijini Dar es Salaam leo, Mkurugenzi Mkuu Msaidizi (uendeshaji) kwa niaba ya Mkurugenzi Mkuuu wa kampuni hiyo, Focus Sahani amesema wakati wanaendelea na matengenezo ya miundombinu iliyohariviwa na mafuriko eneo hilo wameona ni vema usafiri huo ukaendelea kwa kuanzia Mkoa wa Dodoma.
Amesema uongozi baada ya kutathimini hali ya miundombinu ya maeneo mengine yaliyo salama imeamua kuhamishia huduma ya usafiri huo wa treni kutokea Dodoma.
Aidha Sahani amesema ratiba ya huduma ya muda wa kuanzia Dodoma ni kwamba treni ya abiria itaondoka saa moja usiku kesho Jumanne na Ijumaa kwenda Kigoma, Mwanza na Mpanda ambako inatarajiwa kuwasili Mwanza saa 12 jioni siku ya Jumatano na Mpanda saa 12 jioni na Kigoma saa 12 jioni.
"Treni kutoka Mpanda, Mwanza na Kigoma zitatoka huko siku za Jumapili na Alhamis tu. Mpanda inatoka saa moja asubuhi, Mwanza inatoka saa mbili asubuhi na Kigoma inatoka saa1:30 asubuhi.Treni hizo zinafika Dodoma siku ya Jumatatu na Ijumaa saa 1:00 asubuhi, "amesema.
Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Reli Tanzania (TRL) ambaye ni Mkurugenzi Mkuu Msaidizi (Uendeshaji) Focus Sahani, akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) wakati akitangaza mabadiliko ya muda ya Ratiba za usafiri wa Treni na kuharibika kwa miundombinu ya Reli eneo la Kilosa kutokana na mvua zinazoendelea kunyesha nchini, ambapo usafiri huo kwa sasa utaanzia mkoani Dodoma. Kulia ni Mkuu wa Usafirishaji, Shaaban Kiko.
*****************************************
Wakati huohuo Sahani amesema treni pekee ya kutoka Tabora kwenda Mpanda itafanya safari zake siku za Jumanne, Alhamisi na Jumapili na itatoka Mpanda kurejea Tabora katika siku za Jumatatu, Jumatano na Jumamosi.
"Itakuwa inaondoka Tabora saa 12 asubuhi na kuwasili Mpanda saa 12:32 na itaondoka Mpanda kurejea Tabora saa 1:00 asubuhi na kuwasili saa 12:32 jioni. Uongozi WA TRL bado unaendelea kusimamia kazi ya ukarabati wa eneo lililoharibika kati ya Kilosa na Gulwe, "amesema Sahani.
Pia uongozi wa TRL umesema moja ya sababu inayochangia reli kuharibika kwa maji ya mvua inatokana baadhi ya wakulima kulima katika maeneo ya reli,hivyo wamehimiza walnaolima pembezoni kwa reli kuacha kwani madhara yake ni pamoja na kuharibu miundombinu ya reli.
Meneja wa Usalama wa Njia za reli Tanzania, Gukwi Michael (katikati) akifafanua jambo wakati wa mkutano huo na waandishi wa habari.
Kaimu Meneja Masoko wa TRL, Iddi Mzugu, akifafanua jambo kuhusu uharibifu huo.
↧
MAKAMU WA RAIS AKUTANA NA MKUU WA JESHI LA POLISI NCHINI
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan leo amekutana na kufanya mazungumzo na Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini (IGP) Simon Sirro ofisini kwake, Ikulu jijini Dar es Salaam.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan, akiwa katika picha ya pamoja na IGP Sirro baada ya mazungumzo yao.
Wakiagana baada ya mazungumzo. Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais
↧
↧
SERIKALI YATOA UFAFANUZI WA MATUMIZI YA FEDHA ZA KIGENI
Naibu Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji (Mb) akifafanua kuhusu matumizi ya fedha za kigeni ambapo alieleza kuwa Serikali imedhibiti matumizi ya fedha hizo ili kulinda thamani ya shilingi wakati wa Mkutano wa Naibu Waziri huyo na Wafanyabiashara wa Mkoa wa Arusha.
Naibu Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji (kulia) pamoja na meza kuu wakimsikiliza kwa makini mmoja wa wafanyabiashara (hayupo pichani) aliyekuwa akiuliza kuhusu matumizi ya fedha za kigeni wakati wa Mkutano kati ya Naibu Waziri huyo na Wafanyabiashara wa Mkoa wa Arusha.
Baadhi ya Wafanyabiashara wa Mkoa wa Arusha wakiwa katika mkutano na Naibu Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji (Mb) (hayupo pichani) kuhusu ukuzaji wa Sekta ya Biashara Jijini Arusha
********************************************
Na: WFM
Serikali haijazuia matumizi ya fedha za kigeni nchini bali imechukua hatua ya kudhibiti matumizi ya fedha hizo ili kulinda thamani ya Shilingi ya Tanzania.
Hayo yalielezwa na Naibu Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji (MB) alipokutana na wawakilishi wa wafanyabiashara mkoani Arusha kujadiliana mambo mbalimbali kwa ajili ya kukuza sekta ya biashara nchini.
Amesema kuwa sheria haijazuia matumizi ya fedha za kigeni nchini lakini inasisitiza kuwa watu wanapaswa kutambua kuwa sarafu ndiyo fedha halali kwa malipo ndani ya nchi.
“Tatizo kubwa tunalokumbana nalo ni uhuru ulioachiwa ambao unasababisha kushuka kwa thamani ya Shilingi yetu kwani kila mmoja anaweza kutumia fedha za kigeni pia watumiaji wa fedha za kigeni hawafuati thamani ya fedha iliyoko sokoni kila mmoja anakuwa na kiwango tofauti cha thamani ya kubadili fedha za kigeni”. alifafanua Dkt. Kijaji.
Ili kuondoa changamoto hizo Serikali imeamua kurekebisha sheria ya matumizi ya fedha za kigeni na sheria ya Benki Kuu huku ambayo inazitaka bei zote hapa nchini zitangazwe kwa Shilingi ya Tanzania. Bei hizi zinajumuisha kodi za nyumba za kuishi na ofisi, bei za ardhi, gharama za elimu na afya, bei za vyombo vya usafiri na vifaa vya kielektroniki.
“Bei ambazo walengwa wake wakuu ni watalii au wateja ambao sio wakazi zinaweza kutangazwa kwa fedha za kigeni na malipo yake yanaweza kufanyika kwa fedha za kigeni. Hata hivyo kama mlengwa akitaka kulipa kwa Shilingi ya Tanzania asilazimishwe kulipa kwa fedha za kigeni” alieleza Dkt. Kijaji.
Aidha, viwango vya kubadilishia fedha vitakavyotumika katika kuweka hizo bei katika sarafu nyingine vimetakiwa kuwekwa wazi na visizidi vile vya sokoni.
Mkazi yeyote wa Tanzania au mtu wa nje anayeishi Tanzania asilazimishwe kufanya malipo yoyote kwa kutumia fedha za kigeni kama ana Shilingi ya Tanzania mkononi mfano gharama za shule na hoteli.
Aidha Serikali imeagiza vyombo vya dola kuchukua hatua za kisheria kwa wote watakaokiuka maagizo hayo yaliyotolewa na Serikali.
Naibu Waziri Dkt. Kijaji alitoa rai kwa wafanyabiashara nchini kuhimiza matumizi ya sarafu ili kuweza kukuza thamani ya Shilingi hivyo kusaidia kuinua uchumi wa nchi.
↧
BAADHI YA MADAKTARI BINGWA KUTOKA MUHIMBILI WANATAKIWA KUHAMIA HOSPITALI YA TEMEKE KUONGEZA NGUVU.
Waziri wa Afya ,Maendeleo ya jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Ummy Mwalimu mwenye kilemba cheupe akiongea na baadhi ya wananchi wanaosubiri kupata huduma katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa Temeke wakati alipotembelea Hospitali hiyo ili kuona hali ya utoaji huduma kwa wagonjwa hospitalini hapo leo jijini Dar es salaam. PICHA NA WIZARA YA AFYA
Waziri wa Afya ,Maendeleo ya jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Ummy Mwalimu mwenye kilemba cheupe akiongea na baadhi ya wananchi wanaosubiri kupata huduma katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa Temeke wakati alipotembelea Hospitali hiyo ili kuona hali ya utoaji huduma kwa wagonjwa hospitalini hapo leo jijini Dar es salaam.
Waziri wa Afya ,Maendeleo ya jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Ummy Mwalimu akiwajulia hali baadhi ya wagonjwa wakati alipotembelea Hospitali ya Rufaa ya Mkoa Temeke ili kuona hali ya utoaji hudfuma kwa wagonjwa katika hospitali hiyo leo jijini Dar es salaam.
Waziri wa Afya ,Maendeleo ya jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Ummy Mwalimu akiwajulia hali baadhi ya wagonjwa wakati alipotembelea Hospitali ya Rufaa ya Mkoa Temeke ili kuona hali ya utoaji hudfuma kwa wagonjwa katika hospitali hiyo leo jijini Dar es salaam.
Waziri wa Afya ,Maendeleo ya jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Ummy Mwalimu katikati akiongea na watumishi wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa Temeke awapo pichani alipotembelea hospitali hiyo ili kuona hali ya utoaji huduma kwa wagonjwa katika hospitali hiyo leo jijini Dar es salaam, wa kwanza kulia ni Kaimu Mganga Mkuu wa Serikali Dkt. Mohammed Mohammed na wa kwanza kulia ni Mganga Mfawidhi wa Hospitali hiyo Dkt. Amani Malima.
Waziri wa Afya ,Maendeleo ya jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Ummy Mwalimu katikati akipata maelezo kutoka kwa Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa Temeke Dkt. Amani Malima kushoto wakati alipotembelea Hospitali hiyo ili kuona hali ya utoaji huduma kwa wagonjwa katika hospitali hiyo leo jijini Dar es salaam. PICHA NA WIZARA YA AFYA
*****************************************
NA WAMJW-DAR ES SALAAM
BAADHI ya Madaktari bingwa kutoka Hospitali ya Taifa Muhimbili wanatakiwa kuhamia Hospitali ya Rufaa ya Mkoa Temeke ili kuongeza rasilimali watu kwa ajili ya kumudu hali ya ongezeko la wanaotaka huduma bora za afya hospitalini hapo.
Hayo yamezungumzwa na Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu alipotembelea Hospitali hiyo ili kuangalis hali ya utoaji wa huduma za afya kwa wananchi hospitalini hapo.
"Kubwa nliloligundua hapa ni kuna mlundikano wa idadi kubwa ya wanaohitaji huduma hivyo wale madaktari tunaowatoa Muhimbili hasa madaktari bingwa baadhi tutawahamishia hapa ili kusaidiana na madaktari wa Temeke katika kutoa huduma bora kwa watu wengi zaidi" alisema Waziri Ummy.
Aidha Waziri Ummy amesema kuwa Serikali ipo mbioni kutafuta rasilimali fedha kwa ajili ya kujenga jengo la ghorofa nne ambalo litachangia katika kuondoa tatizo la mlundikano wa wagonjwa hospitalini hapo mapema mwaka huu.
Mbali na hayo Waziri Ummy ametoa rai kwa wananchi wore kujiunga na mfuko wa Bima ya Afya ili kupata huduma za matibabu kwa wakati sahihi na kwa bei nafuu hasa kwa watoto wadogo wenye kadi inayoitwa Afya toto Kadi kwa bei ya shilingi 50, 400 tu.
Kwa upande wake Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa Temeke Dkt. Amani Malima amesema kuwa wapo mbioni kuagiza vifaa na vifaa tiba pamoja na kuomba kuongezwa watumishi kwa ajili ya kuhudumia wagonjwa wengi zaidi kama ilivyoelekezwa na Mhe. Waziri Ummy.
"Tunakabiliwa na upungufu wa watumishi na ndo mana kuna mlundikano wengi wa wanaohitaji huduma lakini tunamshukuru Mheshimiwa Waziri kwa kuja na kuona changamoto zetu na kutuhaidi mazuri zaidi katika jitihada za kutoa hufuma bora za afya kwa wananchi" alisema Dkt. Malima.
↧
MPINA ATEKETEZA ZANA HARAMU ZA UVUVI ZA SH. BILIONI 2 WILAYANI UKEREWE
Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Mhe. Luhaga Mpina (mwenye miwani) baada ya kuwasili kwenye kambi ya Uvuvi ya Kisiwa cha Galinzila leo na kuongea na wavuvi. Kulia ni Mkuu wa Wilaya ya Ukerewe Estomiah Chang’a (mwenye kofia) na kulia zaidi ni Mkurugenzi Mtendaji wa Wilaya ya Ukerewe Frank Bahati leo. Mhe. Mpina alichoma moto nyavu haramu za uvuvi zenye thamani ya shilingi bilioni mbili.
Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Mhe. Luhaga Mpina (mwenye miwani) akiwahutubia wavuvi kwenye kambi ya wavuvi katika kisiwa cha Galinzila Wilayani Ukerewe ambapo baadaye alichoma moto nyavu haramu za uvuvi zenye thamani ya shilingi bilioni mbili katika kijiji Kakukuru. KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA
Umati wa wavuvi kwenye kambi ya wavuvi ya Kisiwa cha Galinzila wilayani Ukerewe wakimsikiliza Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Mhe. Luhaga Mpina (hayupo pichani) ambapo baadaye alichoma moto nyavu haramu za uvuvi zenye thamani ya shilingi bilioni mbili katika kijiji cha Kakukuru zilizokamatwa katika operesheni maalum ya siku tano ya kutokomeza uvuvi haramu katika Wilaya ya Ukerewe leo
Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Mhe. Luhaga Mpina akiwa katika picha ya pamoja na kikosi kazi kilichofanya operesheni ya kutokomeza uvuvi haramu katika Wilaya ya Magu na Busega mara baada ya kuteketeza kwa kuchoma moto zana haramu za uvuvi zenye thamani ya Tsh 457,075,000/= katika kijiji cha Kageye wilayani Magu leo
******************************************************
WAZIRI wa Mifugo na Uvuvi, Mhe Luhaga Mpina ametaifisha na kuteketeza zana haramu za uvuvi zenye thamani ya shilingi bilioni 2 zilizokamatwa wakati zikitumika kwa shughuli za uvuvi katika visiwa vidogo vilivyopo ndani ya Wilaya ya Ukerewe mkoani Mwanza huku Shilingi milioni 120 zikikusanywa kama sehemu ya adhabu kwa wavuvi na wafanyabiashara waliokutwa na zana haramu pamoja na makosa ya utoroshaji samaki na mazao yake nje ya nchi.
Waziri Mpina aliwaonya watu wanaotumia majina ya wavuvi kutishia kufanya migomo isiyoisha na kuandamana baada ya uamuzi wa Serikali kuanza kuchukua hatua stahiki za kudhibiti uvuvi haramu, na kwamba msimamo uliowekwa na Serikali ni thabiti na usiyoyumba hivyo migomo na maandamano ya watu wenye lengo la kukwamisha vita dhidi ya uvuvi haramu haitasaidia chochote na badala yake operesheni kali isiyo na mwisho itaendelea hadi pale uvuvi haramu utakapokoma ndani ya Ziwa Victoria.
“Rasilimali zilizopo ndani ya ziwa hili ni mali ya wananchi sisi viongozi mliotupa dhamana ya kuongoza kazi yetu ni ulinzi tu na endapo tutakomesha uvuvi haramu nyie ndio mtakaonufaika hivyo ni itashangaza tajiri aliyempa kibarua cha ulinzi, na mlinzi huyo akafanya kazi vizuri ya kulinda mali za bosi wake alafu tajiri akamlalamikia kibarua wake sisi na watendaji wa Serikali ni vibarua tu wenye mali ni ninyi hatua tunazochukua zitaleta manufaa makubwa kwenu”alisema.
Pamoja na kuteketeza zana haramu, Waziri Mpina alieleza hali ya upatikanaji wa samaki aina ya sangara katika Ziwa Victoria ambapo alisema kwa mujibu wa utafiti uliofanywa na Taasisi ya Utafiti wa Samaki Tanzania (TAFIRI) 2017 unaonesha kuwa samaki waliochini ya sentimita 50 ni asilimia 96.6 hivyo samaki hawa ni wachanga na hawarusiwi kuvuliwa ambapo samaki walio zaidi ya sentimita 85 ni asilimia 0.4 tu ambao ni wazazi na hawarusiwi kuvuliwa pia. Samaki wa sentimita 50 mpaka 85 ambao ndio wanafaa kuvuliwa ni asilimia 3 tu.
“Tafsiri yake ni kwamba ziwa halina samaki wanaostahili kuvuliwa kulingana na kasi ya uvuvi na pia samaki wazazi ni kidogo ambapo inatishia kumalizika kwa samaki na shughuli za uvuvi kukoma katika Ziwa Victoria’alisema .
Akizungumza kwa nyakati tofauti na maelfu ya wavuvi katika Visiwa vya Gagalini na Kakukuru wilayani Ukerewe Waziri Mpina amesema hatua kali zinazochukuliwa na Serikali dhidi ya uvuvi haramu hazilengi kuwaonea wananchi wanyonge bali kuwatengenezea maisha bora ya kizazi cha sasa na baadae ili kiweze kunufaika na rasilimali zilizoko ziwani.
Akiwa katika eneo la Kakukuru Waziri Mpina alishiriki kuteketeza zana haramu zikiwemo vyavu za Makila 14,103, Kokoro 188 , Nyavu za dagaa 211, Nyavu za timba 450, Kamba za Kokoro 10,700 na ndoano 18,450 na Mitumbwi 109 zenye thamani ya sh. Bilioni 2.
Kaimu Mkurugenzi wa Maendeleo ya Uvuvi wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi, Mwaidi Mlolwa amesema Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kifungu cha 26 (i) (ii) kinamtaka kila mtanzania kulinda rasilimali za nchi yetu ikiwemo samaki na mazao yake huku Sheria ya Uvuvi namba 22 ya mwaka 2003 na Kanuni zake za mwaka 2009 zikikataza vitendo vya kutumia zana zisizoruhisiwa kwa mujibu wa sheria.
Mkuu wa Wilaya ya Ukerewe, Estomihn Chang'a alisema Serikali ya wilaya hiyo itaendelea kuunga mkono juhudi za kupambana na uvuvi haramu na kuwachukulia hatua stahiki kuwataka wananchi kuendelea kuwafichua wavuvi haramu ili kulinda rasimali hiyo muhimu waliyopewa na Mungu.
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Ukerewe , Frank Bahati alisema halmashauri imewasimamisha kazi watumishi watatu kwa tuhuma za kujihusisha na uvuvi haramu.
Kwa upande wao baadhi ya wavuvi walimuomba Waziri Mpina kuwasiliana na Waziri wa Viwanda na Biashara, Charles Mwijage ili kuona namna ya kudhibiti nyavu zisizoruhusiwa kutengenezwa na kisha kuuziwa wavuvi.
↧
WIZARA YA MALIASILI NA UTALII YATANGAZA RASMI VIWANGO VIPYA VYA ADA KWA MAWAKALA WA KUSAFIRISHA WATALII NCHINI
Na Hamza Temba-Dar es Salaam
SERIKALI kupitia wizara zake nne tofauti imedhamiria kukabiliana na changamoto mbalimbali za utoaji wa huduma kwa wageni wanaiongia na kutoka nchini kupitia Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius K. Nyerere (JNIA) jijijini Dar es Salaam.
Waziri wa Maliasili na Utalii Dkt. Hamisi Kigwangalla akiteta jambo na Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Dk. Mwigulu Nchemba wakati wa ziara ya pamoja ya kukagua Changamoto mbalimbali wanazokumbana nazo wageni hususan watalii wanaoingia nchini kupitia uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Dar es Salaam JNIA jana kwa ajili ya kukabiliana nazo. KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA
Waziri wa Maliasili na Utalii Dkt. Hamisi Kigwangalla akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es salaam jana wakati wa ziara ya pamoja ya kukagua Changamoto mbalimbali wanazokumbana nazo wageni hususan watalii wanaoingia nchini kupitia uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Dar es Salaam JNIA kwa ajili ya kukabiliana nazo. Wengine walioshiriki ziara hiyo ni Waziri wa Mambo ya Ndani, Dk. Mwigulu Nchemba (wa pili kulia), Naibu Waziri wa Ujenzi na Mawasiliano, Mhandisi Atashasta Nditiye (wa tatu kulia) na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje, Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa, Dk. Susan Kolimba (wa nne kulia).
*******************************************
Mawaziri wa Wizara hizo ambao wamefanya ziara ya pamoja katika uwanja huo jana na kukagua shughuli za utoaji huduma ni Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla, Waziri wa Mambo ya Ndani, Dk.Mwigulu Nchemba, Naibu Waziri wa Mambo ya Nje Dk.Susan Kolimba na Naibu Waziri wa Ujenzi na Mawasiliano, Mhandisi Atashasta Nditiye.
Akizungumza uwanjani hapo, Dk. Kigwangalla alisema wamefikia hatua ya kukutana mawaziri hao baada ya wageni hasa watalii wanaiongia nchini kulalamika kuwa wanatumia muda mwingi kuhudumiwa katika eneo la uwanja huo kiasi cha kuwapotezea muda.
Dk.Kigwangala amesema kutokana na malalamiko hayo ya muda mrefu na mengine kadhaa hatua mbalimbali zimechukuliwa tangu Agosti 8 mwaka 2017 manaibu waziri wa wizara hizo nne walipofanya ziara uwanjani hapo kwa ajili ya kutafuta ufumbuzi changamoto hizo na kwamba kukutana kwao jana ni muelendezo wa kushughulikia kero hizo ambapo mafanikio yameanza kuonekana.
Dk.Kigwangala amesema ipo haja ya kuweka mikakati ya kuboresha huduma katika viwanja vya ndege nchini ukiwamo JNIA huku akisisitiza umuhimu wa watendaji na watoa huduma katika nafasi mbalimbali kuwa wakarimu kwa wageni.
Amesema ni vema hata Polisi walioko uwanjani hapo wakimkamata mgeni basi badala ya kutumia nguvu wawe na ukarimu kwani ni muhimu kumdhibiti mgeni bila kutumia nguvu ili ikibainika hana kosa aachiwe na asiwe na malalamiko ya kunyanyaswa.
Dk.Kigwangala amesema kuna haja kwa wageni wanapokuja Tanzania wakirudi makwao wasimulie ukarimu na uzuri wa nchini yetu.
Ameongeza anatamani kuona kuanzia uwanjani hapo hadi hotelini ambako mgeni anakwenda anatumia muda mchache, anapata nafasi ya kuona picha za viongozi mbalimbali ambazo zitakuwa uwanjani, picha za wanyama na video ambazo zinaonesha utalii wa Tanzania.
Amesema kumpokea mgeni jambo moja lakini namna ya kumhudumia ni jambo jingine na ndilo muhimu zaidi na akafafanua hata teksi ambayo mgeni ataitumia kusafiri dereva awe na ukarimu hata wa kumsalimia na wakati mwingine kutabasamu.
Kwa upande wake, Waziri wa Mambo ya ndani Ndani Dk. Mwigulu Nchemba akizungumza baada ya ziara hiyo alisema jitihada mbalimbali zinafanywa kutatua changamoto hizo.
Ametaja hatua ambazo wizara yake inachukua ni kuharakisha utoaji huduma wa hati za kusafiria kwa njia ya kieletroniki.
Pia wameamua kuongeza idadi ya madawati ya kutolea huduma kwa wageni ikiwa sambamba na kuongeza watoaji huduma ili kurahisisha utoaji huduma wa muda mfupi.
“Taarifa zinaonesha kuwa kwa sasa kuna unafuu mkubwa wa kutoa huduma kwani badala ya saa tatu ambazo zilikuwa zinatumia awali hivi sasa muda wa utoaji huduma umeshuka hadi saa moja, lengo letu ni kushuka zaidi.
“Mbali ya kuboresha huduma tutahakikisha pia tunaongeza ulinzi na usalama katika viwanja vyetu vyote nchini ili kudhibiti wageni wenye nia ovu na nchi yetu.
“Tunafahamu mataifa mengi yameitikia mwito wa uwekezaji nchini hasa katika mikakati ya kufikia Serikali ya Viwanda na uchumi wa kati.
“Hivyo wageni wanakuja kwa nia njema ya kuwekeza lakini hatutaki wale wenye nia mbaya kutumia mwanya huo.Hivyo tutaendelea kuimarisha ulinzi na usalama katika viwanja vyetu,”amesema.
Kwa upande wa Naibu Waziri wa Mambo ya Nje, Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa, Dk. Susan Kolimba amesema wanaridhishwa na hatua ambazo zinachukuliwa katika kuondoa changamoto zinazoelezwa kuwapo uwanjani hapo.
Amesema wizara yao inatamani kuona idadi ya wageni inaongezeka zaidi na wakati huo huo wakifurahia huduma ambazo wanazipata wakifika nchini kwetu. Alisema Wizara yake itaendelea kuitangaza Tanzania na vitutio vyake ili idadi ya watalii iweze kuongezeka.
“Tumefanya ziara na binafsi niseme tu nimeridhishwa na hatua ambazo zinachukuliwa katika kuondoa changamoto hizo,”amesema Dk.Kolimba.
Naye, Naibu Waziri wa Ujenzi na Mawasiliano, Mhandisi Atashasta Nditiye amesema wizara yao tayari imechukua hatua mbalimbali za kuondoa changamoto zilizopo ikiwamo ya kufunga viyoyozi (AC) kwa ajili ya kuondoa hali ya joto.
“AC zilizopo ni za muda mrefu kwani ziliwekwa tangu majengo ya uwanja huo yalipojengwa. Hivyo tayari zimeanza kufungwa AC mpya na ndio maana joto limepungua” amesema.
Pia amesema wamepata kampuni ambayo itakayofanya ukarabati kwa kuongeza eneo la kukaa wageni wanaosubiri huduma mbalimbali kabla ya kutoka uwanjani.
Amesema kuna jitihada mbalimbali Serikali inafanya jitihada za kuondoa msongamano wa wageni ikiwamo ya kuharakisha ujenzi wa jengo jipya la kusafiria wageni la Terminal III ambalo litahudumia watu milioni sita badala ya jengo la sasa ambalo wakati linajengwa lengo lake lilikuwa kuhudumia watu milioni moja.
“Ujenzi wa jengo jipya umekamilika kwa asilimia 70 na litakapokuwa tayari kwa asilimia 100 litaanza kutumika kwa kuwa kasi ya ujenzi inakwenda vizuri,’amesema.
Waziri wa Maliasili na Utalii Dkt. Hamisi Kigwangalla (wa pili kulia) akiteta jambo na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje, Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa, Dk. Susan Kolimba jijini Dar es salaam jana wakati wa ziara ya pamoja ya kukagua Changamoto mbalimbali wanazokumbana nazo wageni hususan watalii wanaoingia nchini kupitia uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Dar es Salaam JNIA kwa ajili ya kukabiliana nazo. Wengine walioshiriki ziara hiyo ni Waziri wa Mambo ya Ndani, Dk. Mwigulu Nchemba (wa tatu kushoto) na Naibu Waziri wa Ujenzi na Mawasiliano, Mhandisi Atashasta Nditiye (wa pili kushoto) .
Waziri wa Maliasili na Utalii Dkt. Hamisi Kigwangalla (wa tatu kulia) akiteta jambo na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje, Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa, Dk. Susan Kolimba jijini Dar es salaam jana wakati wa ziara ya pamoja ya kukagua Changamoto mbalimbali wanazokumbana nazo wageni hususan watalii wanaoingia nchini kupitia uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Dar es Salaam JNIA kwa ajili ya kukabiliana nazo. Wengine walioshiriki ziara hiyo ni Waziri wa Mambo ya Ndani, Dk. Mwigulu Nchemba (kulia) na Naibu Waziri wa Ujenzi na Mawasiliano, Mhandisi Atashasta Nditiye (wa pili kulia).

Naibu Waziri wa Mambo ya Nje, Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa Dkt. Susan Kolimba kulia akitoa maelezo kwa Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Dk. Mwigulu Nchemba kushoto, Naibu Waziri wa Ujenzi, Mhandisi Atashasta Nditiye (wa pili kushoto) na Waziri wa Maliasili na Utalii Dkt. Hamisi Kigwangalla (wa pili kulia) wakati wa ziara hiyo.
↧
↧
CHIRWA NJE MECHI TATU
Kamati ya nidhamu iliyokutana Jumapili Januari 14, 2018 imepitia kesi ya mshambuliaji wa Yanga Obrey Chirwa iliyowasilishwa na Bodi ya Ligi iliyohusu mchezo namba 83 kati ya Yanga na Tanzania Prisons iliyochezwa Novemba 25, 2017 Uwanja wa Azam Complex.
Chirwa alishtakiwa kwa kosa la kumpiga mchezaji wa Tanzania Prisons kwenye mchezo huo uliomalizika kwa sare ya kufungana bao 1-1.
Chirwa ambaye alifika kusikiliza kesi hiyo akiwa na muwakilishi wake alikiri kutenda kosa hilo.
Kamati baada ya kumsikiliza Chirwa na kupitia Video za mchezo huo pamoja na taarifa ya kamishna na Muamuzi imetoa adhabu kwa mchezaji huyo kupitia Kanuni za Ligi Kuu kanuni ya 37(7b) na kanuni za nidhamu za TFF kifungu cha 48(1d) na 48(2).
Chirwa amefungiwa mechi tatu(3) na kutozwa faini ya shilingi laki tano(500,000)
↧
RAIS KARIA AMPONGEZA DAMAS NDUMBARO UBUNGE SONGEA MJINI
Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) Ndugu Wallace Karia kwa niaba ya Shirikisho anatoa pongezi kwa mwanamichezo daktari wa Sheria Dr.Damas Ndumbaro kwa kushinda kiti cha Ubunge Jimbo la Songea Mjini.
Rais Karia amesema ushindi wa Dr.Ndumbaro unaongeza wanamichezo zaidi katika bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambao wanaweza kuwa chachu ya maendeleo ya michezo ikiwemo mpira wa miguu.
Amesema uzoefu wa Dr.Ndumbaro katika mpira wa miguu utasaidia katika nyanja hiyo na itasaidia kupaza sauti kupitia bunge katika harakati za kushirikiana kuusogeza mbele mchezo wa soka.
“Tunaamini uwezo wa Dr.Ndumbaro katika uongozi tumemuona katika mpira wa miguu akiongoza katika sehemu mbalimbali hakika uwezo wake wa uongozi ni mkubwa na atasaidia sana kukua kwa sekta hii ya michezo,sisi TFF tunamtakia kila la kheri kwenye majukumu yake mapya na tutampa ushirikiano wote kuhakikisha tunafikia mafanikio,kwetu ni faraja kubwa kuona wana familia wa mpira wa miguu wakishinda nafasi mbalimbali za uongozi ikiwemo Ubunge”.Alisema Rais Karia.
Rais Karia ameongeza kuwa anaamini Dr.Ndumbaro jimbo lake la Songea Mjini litakuwa moja ya majimbo yenye mfano wa kuigwa katika maendeleo ya mpira wa miguu.
Dr.Ndumbaro amewahi kushika nafasi mbalimbali za uongozi kwenye mpira wa miguu na hivi karibuni Rais Karia alimteuwa kuwa mwenyekiti wa kamati ya rufaa ya leseni za klabu.
Akigombea kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi(CCM) Dr.Ndumbaro amejizolea kura 45762 akiwazidi wagombea wengine 7 kutoka vyama mbalimbali.
↧
SERENGETI BOYS KUINGIA KAMBINI HADI JANUARI 28
Timu Ya Taifa chini ya miaka 17 Serengeti Boys itaendelea kuwepo kambini mpaka Januari 28, 2018.
Maandalizi hayo ya Serengeti Boys yatakwenda sambamba na kucheza mechi za kirafiki kabla ya kuhairisha kambi hiyo itakayokuwa ikifanyika mara kwa mara na mpango uliopo ni kila mwezi timu hiyo kuingia kambini.
Katika hatua nyingine kikosi hicho kimepunguzwa kutoka wachezaji 43 walioitwa mpaka kufikia 34 watakaoendelea na kambi hiyo.
Orodha hiyo inajumuisha wachezaji 30 wa ndani na 4 magolikipa.
↧
CAF YATEUA WANNE TFF KUSIMAMIA MECHI
Shirikisho la Mpira wa Miguu Barani Africa CAF limepitisha majina manne ya wajumbe wa Kamati ya Utendaji ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania TFF kuwa makamishna wa michezo mbalimbali inayoandaliwa na CAF.
Tanzania imekuwa miongoni mwa nchi zilizotoa Makamishna wanne ambayo ni idadi ya juu hakuna nchi iliyozidisha idadi hiyo ambayo ni kwa kipindi cha kutokea mwaka 2018 mpaka 2020.
Wajumbe wa Kamati ya Utendaji ya TFF waliopata nafasi hiyo ni Makamu wa Rais Michael Wambura,Ahmed Mgoyi,Amina Karuma na Sarah Tchao.
Wambura kwa upande wake amechaguliwa kutokana na kufanya vizuri katika aiku za nyuma wakati Mgoyi amepata nafasi hiyo kwa kufanya vizuri kama mechi kamishna wa michezo ya CECAFA nao Karuma na Tchao wameipata nafasi hiyo kutokana na mkakati wa CAF kuanza kuwajengea uwezo viongozi wanawake vijana.
↧
↧
RAIS MAGUFULI AOMBOLEZA VIFO VYA WATU 11 AJALI YA KAGERA
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli amemtumia salamu za rambirambi Mkuu wa Mkoa wa Kagera Meja Jenerali Mstaafu Salum Kijuu kufuatia watu 11 kupoteza maisha katika ajali ya gari iliyotokea katika Kijiji cha Nyangozi, Wilaya ya Biharamulo Mkoani Kagera.
Ajali hii imetokea jana tarehe 14 Januari, 2018 majira ya saa 11 jioni baada ya basi dogo la abiria aina ya Nissan Caravan lililokuwa likitoka Kakonko Mkoani Kigoma kuelekea Kahama Mkoani Shinyanga kuligonga ubavuni lori la mizigo kisha kugongana uso kwa uso na lori jingine na kusababisha vifo vya watu 11 na wengine 6 kujeruhiwa.
Mhe. Rais Magufuli amepokea kwa huzuni na masikitiko makubwa taarifa za vifo vya Watanzania hao na amemtaka Mkuu wa Mkoa wa Kagera Meja Jenerali Mstaafu Salum Kijuu kumfikishia pole kwa familia za Marehemu wote, ndugu, jamaa, marafiki na wote walioguswa na vifo hivyo.
“Nimehuzunishwa na kusikitishwa sana na vifo hivi, nawapa pole wafiwa wote, ninawaombea marehemu wapumzike mahali pema na majeruhi wapone haraka ili waweze kuungana na familia zao na kuendelea na shughuli zao za kila siku” amesema Mhe. Rais Magufuli.
Aidha, Mhe. Rais Magufuli amewakumbusha watumiaji wa barabara hasa madereva kuwa makini na kuzingatia sheria za usalama barabarani na ameviagiza vyombo vinavyohusika kuongeza jitihada za kukabiliana na ajali za barabarani ili kuokoa maisha ya watu na mali zinazopotea kutokana na ajali.
Gerson Msigwa
Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, IKULU
Dar es Salaam
15 Januari, 2018
↧
WANNE WFIKISHWA KIKAANGONI SEKRETARIETI YA MAADILI
Sekretarieti ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania TFF imewapeleka kwenye kamati ya Maadili viongozi wanne kwa kughushi na udanganyifu.
Viongozi walioshtakiwa kwenye Kamati ya Maadili ni msimamizi wa Kituo cha Mtwara Dunstan Mkundi, Katibu wa Chama cha soka mkoa wa Mtwara Kizito Mbano, Muhasibu msaidizi wa klabu ya Simba Suleiman Kahumbu na Katibu msaidizi wa Klabu ya Ndanda FC ya Mtwara Selemani Kachele.
Sekretarieti inawashtaki viongozi hao kwa makosa ya kughushi pamoja na udanganyifu wa mapato kwenye mchezo namba 94 kati ya Ndanda FC ya Mtwara dhidi ya Simba ya Dar es Salaam iliyochezwa Disemba 30, 2017 kwenye Uwanja wa Nangwanda Sijaona, Mtwara.
Kwa tuhuma hizo viongozi hao watatakiwa kufika mbele ya kamati Januari 18, 2018.
Kamati ya maadili iko chini ya mwenyekiti Wakili Hamidu Mbwezeleni, Makamu Mwenyekiti Wakili Steven Zangira, Wajumbe ni Glorious Luoga, Walter Lungu na Amin Bakhresa
↧
SERIKALI KUPITIA DAWASA KUJENGA MITAMBO MITATU YA KISASA YA KUCHAKATA MAJI TAKA JIJINI DAR
Kaimu Mkurugenzi wa Ufundi wa Mamlaka ya Maji Safi na Maji Taka Dar es Salaam, (DAWASA), Bi. Modester Mushi(kushoto), akifafanua jambo leo Januari 15, 2018 kwa kutumia ramani ya mradi wa ujenzi wa mitambo mitatu ya kuchakata maji taka jijini Dar es Salaam, kwa Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, jijini, Mhe. Ali Hapi, wakati alipotembelea eneo la Kilongawima, Mbezi Beach jijini ambako patajengwa moja kati ya mitambo hiyo. Katikati ni Meneja Uhusiano wa Umma wa DAWASA, Bi. Neli Msuya.
***********************************************
NA K-VIS BLOG/Khalfan Said
WIZARA ya Maji na Umwagiliaji, kupitia Mamlaka ya Maji Safi na Maji Taka, Dar es Salaam (DAWASA), inajiandaa kujenga mitambo mitatu ya kisasa ya kuchakata maji taka, ikiwa ni sehemu ya juhudi za serikali za kuboresha hali ya mazingira jijini.
Hayo yamesemwa leo Januari 15, 2018 na Kaimu Mkurugenzi wa Ufundi wa DAWASA, Bi. Modester Mushi wakati akitoa taarifa ya ujenzi wa mitambo hiyo kwa Mkuu wa Wilaya ya Kinodnoni jijini Dar es Salaam, Mhe. Ali Hapi, wakati alipotembelea moja ya maeneo ya mradi huo huko Kilongawima, Mbezi Beach.
“Ujenzi wa mitambo hii utakwenda sambamba na ujenzi wa mfumo wa ukusanyaji maji taka katika jiji la Dar es Salaam ambapo lengo ni kulaza jumla ya kilomita 563 za mabomba ya ukubwa mbalimbali ya ukusanyaji na usafirisha maji taka kutoka sehemu mbalimbali za jiji na kuyamwaga kwenye mitambo mikubwa mitatu itakayojengwa hapa Kilongawima,(Mbezi Beach), Jangwani na Kurasini.” Kaimu Mkurugenzi huyo amemueleza Mkuu wa Wilaya Mhe. Hapi. KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA
Kuhusu ukubwa wa mitambo hiyo, Bi. Modester alisema, Mtambo wa Kilongawima (Mbezi Beach) utakapokamilika, utakuwa na uwezo wa kuchakata maji taka yenye mita za ujazo 16,000 kwa siku, wakati ule wa Jangwani utakuwa na uwezo wa kusafisha (kuchakata) maji taka yenye lita za ujazo 200,000 kwa siku na ule wa Kurasini utakuwa na uwezo wa kuchakata maji taka yenye lita za ujazo 11,000 kwa siku.
“Ujenzi wa mitambo hii utaanza muda wowote mwaka huu wa 2018 na utagharimu kiasi cha dola za Kimarekani Milioini 65.” Alisema.
Akifafanua zaidi jinsi mitambo hiyo ya kisasa itakavyofanya kazi, Bi.Modester Mushi alisema, mitambo hiyo pia itazalisha gesi asilia na umeme kwa ajili ya kujiendesha, na hivyo kupunguza matumizi na gharama za umeme.
“Lakini pia maji yatakayokuwa yamesafishwa yatauzwa na kutumika katika shughuli mbalimbali kama vile kupoozea mitambo na umwagiliaji wa bustani wakati tope litakalobaki baada ya mchakato huo wa usafishaji maji taka litaweza kutumika kama mbolea kwa ajili ya kilimo lakini pia kuendesha bustani za miti ya kivuli na hivyo kulipendezesha jiji.” Alifafanua Bi. Modester na kuongeza,
Katika eneo la Jangwani , bustani ya kisasa itakayokuwa na miti ya kivuli, maua na viti vya kupumzikia itajengwa ili kuboresha taswira ya eneo hilo la Jangwani na hiyo itakuwa ni mchango wa DAWASA katika kuunga mkono harakati za Serikali za kuboresha usafi wa mazingira.
Kwa upande wake, Mkuu wa Wilaya Mhe. Ali Hapi, aliwapongeza DAWASA kwa hatua wanazochukua hususan kazi ya kuanza mradi huo na kuwataka waharakishe utekelezaji wa mradi. “Changamoto kubwa ambayo tubnakabiliana nayo sisi viongozi wa serikali hatuelewi sana ni ucheleweshwaji wa mradi,tunatamani kuona vitu vinatokea na hasa mnapotuhakikishia kuwa fedha zipo, kama mnachangamoto zozote ni vizuri kuzifikisha kwenye mamlaka zinazohusika ili ziwasaidie kutatua changamoto hizo ili kwa pamoja tuweze kuwaletea wananchi maendeleo.” Alisema Mhe. Hapi.
Mheshimiwa Hapi pia alitembelea kituo cha kusukuma maji taka cha Shoppers Plaza, Mikocheni pamoja na kutembeelea maeneo korofi yanayovuja maji taka kwenye eneo la Mikocheni na Mwenge na kuitaka Kampuni inayosimamia uendeshaji wa kuondoa maji taka DAWASCO kuhakikisha wahandisi wake wanatoka maofisini na kukagua maeneo korofi ili kuchukua hatua za kuyarekebisha.
“Nasisitiza tena Wahandisi watembelee maeneo ambayo kazi zao zipo, watembelee barabara zetu, Halmashauri zinatumia fedha nyingi kurekebiusha barabara zetu, zikirekebisha baada ya mwezi mmoja chemba zinapasuka na kuharibu barabara, hatuwezi kuendelea na utaratibu huu, ni lazima tutafute suluhu.” Alisema.
Hapi akizungumza kwenye moja ya maeneo korofi ya chemba ya maji taka Mikocheni jijini Dar es Salaam, wakati wa ziara hiyo.
Mhe. Hapi akizunghumza kwenye eneo korofi la chemba ya maji Taka Mikocheni jijini Dar es Salaam, wakati wa ziara hiyo.
Mkuu wa Wilaya Mhe. Ali Hapi, (kulia), akifafanua jambo wakati alipotembelea eneo lililopangwa kujengwa mtambo wa kuchakata maji taka huko Kilongawima, Mbezi Beach jijini Dar es Salaam, leo Januari 15, 2018. Kulia ni Meneja Uhusiano wa Umma wa DAWASA, Bi. Neli Msuya.
Bi. Modester akimsikilkiza kwa makini Mkuu wa Wilaya Mhe. Ali Hapi (hayupo pichani).
Mkuu wa Wilaya Mhe. Hapi, (kulia), akibadilishana mawazo na Kaimu Mkurugenzi wa Ufundi wa DAWASA, Bi. Modester Mushi, (kushoto) na Meneja Uhusiano wa Umma, Bi., Neli Msuya.
Hapi akizungumza mbele ya Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa Mwenge jijini Dar es Salaam, Bw.Bashiri Hoza, (kulia) na Mkuu wa Kituo cha Polisi Mwenge, alipotembelea kuona maeneo korofi ambayo chemba za mitaro ya maji taka hufumuka mara kwa mara kwenye eneo hilo jirani na soko la Mwenge.![]()
Hapi akizungumza mbele ya wananchi alipotembelea maeneo korofi ambayo chemba za maji taka hufumuka mara kwa mara eneo la Mwenge jijini Dar es Salaam.
Mheshimiwa Hapi, akitoa maelekezo alipotembelea eneo la Mikocheni jijini Dar es Salaam kuona miundombinu ya maji taka.
↧