Quantcast
Channel: SUFIANIMAFOTO
Viewing all 13053 articles
Browse latest View live

MBIO ZA MBEYA TULIA MARATHON ZAFANA JIJINI MBEYA

$
0
0
Mwenyekiti wa Taasisi ya Tulia Trust, na Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Tulia Ackson, akizindua mbio za Kilometa 45, wakati wa Mbio za Mbeya Tulia Marathon (MTM) zilizofanyika kwenye Uwanja wa Sokoine jijini Mbeya jana na kushirikisha wageni mbalimbali kutoka mikoa tofauti na Makampuni.  Picha Zote na Muhidin Sufiani (MAFOTO)
Mwenyekiti wa Taasisi ya Tulia Trust, na Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Tulia Ackson, akiongoza mbio za Kilometa Tano, wakati wa Mbio za Mbeya Tulia Marathon (MTM) zilizofanyika kwenye Uwanja wa Sokoine jijini Mbeya leo na kushirikisha wageni mbalimbali kutoka mikoa tofauti na Makampuni. 
Wadau wakishiriki mbio hizo
Mshindi wa kwanza wa mbio za Kilometa 100 kwa upande wa wanawake, Nasra Abdallah, akimalizia mbio za Mbeya Tulia Marathon (MTM) zilizofanyika kwenye Uwanja wa Sokoine jijini Mbeya leo na kushirikisha wageni mbalimbali kutoka mikoa tofauti na Makampuni. 
Mshindi wa Marathoni ni Abraham Too alikimbia 2:42:02:08, Francis Bowen wote wa Kenya 2:42:02:73 na Nestory Steven aliyekimbia saa 2:45:39, Ambapo wa kwanza alipata Sh milioni 3, wa pili milioni 2 na watatu milioni 1.
Wanawake  ni:- 
Nusu marathoni ni Failuna Abdi, Christina Kambua wa Kenya na Adelina Trazias wa Tanzania, kwa wanaume ni Bernard Musau wa Kenya, Paschal Mombo wa Tanzania na George Olihaki wa Kenya. Ambapo mshindi alipata sh milioni 2  wa pili wa pili 700,000 na watatu 500,000.
Kwa upande wa mbio za Baiskeli bingwa ni Richard Laizer, Hamis Hussein na Masunga Duba, kwa wanawake ni Sophia Khatimu, Lawlence Luzuba na Habibu Mathias
Mita 1500 ambao walivikwa medali na Nanai ni James  John, Geofrey Edison, Yeli Adam kwa wanawake ni Sarah Ariko, Omega Elia na Silvana Elias
Mwenyekiti wa Taasisi ya Tulia Trust, na Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Tulia Ackson, akizindua mbio za Kilometa 45, wakati wa Mbio za Mbeya Tulia Marathon (MTM) zilizofanyika kwenye Uwanja wa Sokoine jijini Mbeya na kushirikisha wageni mbalimbali kutoka mikoa tofauti na Makampuni. 
Mwenyekiti wa Taasisi ya Tulia Trust, na Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Tulia Ackson, akizindua mbio za Kilometa 21, wakati wa Mbio za Mbeya Tulia Marathon (MTM) zilizofanyika kwenye Uwanja wa Sokoine jijini Mbeya na kushirikisha wageni mbalimbali kutoka mikoa tofauti na Makampuni. 
Mwenyekiti wa Taasisi ya Tulia Trust, na Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Tulia Ackson, akiwaongoza washiriki mbio za Kilometa Tano, kufanya mazoezi ya kujiandaa kushiriki Mbio za Mbeya Tulia Marathon (MTM) zilizofanyika kwenye Uwanja wa Sokoine jijini Mbeya leo na kushirikisha wageni mbalimbali kutoka mikoa tofauti na Makampuni. 
Wadau wakipozi kwa picha
Mshindi wa tatu Kilometa 45 kwa wanawake kutoka Kenya akimalizia mbio
Wazee wakijifua kabla ya kuanza kutimua mbio za Kilometa mbili
Washiriki wa mbio za wazee za Kilometa mbili wakianza kutimua mbio
Baadhi ya washiriki wakifanya mazoezi ya kujiandaa na mbio
Mpigapicha wa Azam Tv, akiwa kazini kupata matukio ya mbio hizo kwa kutumia usafiri wa Bodaboda
Mwakilishi wa Kampuni ya Derm Electrics, Irene na Mtangazaji wa Redio ya Mbeya Fm, Gwamaka Mwankota, wakishiriki mbio hizo.
Wawakilishi kutoka DSTV wakishiriki mbio za Kilometa tano
Mhes Dkt. Tulia akiwaongoza washiriki wa mbio za Kilometa tano kumaliza mbio hizo.
Kutoka (kushoto) ni msanii wa muziki wa kizazi kipya, Farid Kubanda Fid Q, Sebastian na Barbara kutoka Clouds pamoja na mwakilishi wa Tatu Mzuka, wakiwa katika Uwanja wa Sokoine kushuhudia mbio hizo.

Mshindi wa pili wa mbio za Kilometa 45 kwa upande wa wanawake, Sarah Ramadhan, akimalizia mbio hizo 
Mshindi wa pili wa mbio za Kilometa 45 kwa upande wa wanawake, Sarah Ramadhan, akibebwa na wasaidizi baada ya kuzidiwa na kuishiwa nguvu wakati akimalizia mbio hizo za Mbeya Tulia Marathon (MTM) zilizofanyika kwenye Uwanja wa Sokoine jijini Mbeya leo na kushirikisha wageni mbalimbali kutoka mikoa tofauti na Makampuni.
Mshindi wa pili Kilometa 21 akimalizia mbio
Mshindi wa kwanza wa mbio za Kilometa 100 kwa upande wa wanaume, akimalizia mbio za Mbeya Tulia Marathon (MTM) zilizofanyika kwenye Uwanja wa Sokoine jijini Mbeya leo na kushirikisha wageni mbalimbali kutoka mikoa tofauti na Makampuni. 

Wakimbiaji wa Kilometa 500 wakianza kutimua mbio
Marry Naali akimalizia mbio za Kilometa 800 na kushika nafasi ya kwanza
 Wadau katika pozi la picha
 Washiriki kutoka CRDB wakipiga picha ya kumbukumbu na Naibu Spika
 Mafoto naye hakuwa nyuma kushiriki mbio hizo za kilometa tano
  Naibu Spika, Dkt. Tulia akijadili jambo na Mkuu wa Mkoa wa Mbeya,Amosi Makala.

UFUNGUZI WA MICHUANO YA SIRRO CUP KIBITI 2018

$
0
0
 Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini IGP Simon Sirro akimkabidhi mpira mmoja wa Viongozi wa timu zinazoshiriki mashindano ya Sirro Kibiti mwaka 2018 katika uwanja wa Samora Kibiti wakati wa uzinduzi wa michezo hiyo uliofanyika jana. Mashindano hayo yanashirikisha timu 16 kutoka Wilaya za Mkuranga, Kibiti na Rufiji
Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini IGP Simon Sirro akisalimiana na wachezaji wa timu ya mpira wa miguu ya Migomba kutoka Wilayani Rufiji wakati wa ufunguzi wa  mashindano ya Sirro Kibiti mwaka 2018 katika uwanja wa Samora Kibiti. Mashindano hayo yanashirikisha timu 16 kutoka Wilaya za Mkuranga, Kibiti na Rufiji
 Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini IGP Simon Sirro, akipunga mkoni kuwasalimu wakazi wa Kibiti wakati wa Sherehe za ufunguzi wa  mashindano ya Sirro Kibiti mwaka 2018 katika uwanja wa Samora Kibiti. Mashindano yanayoshirikisha timu 16 kutoka Wilaya za Mkuranga, Kibiti na Rufiji.
 Msanii Malima Ndolela (Mzee wa Ndolela) akitumbuiza  wakati wa Sherehe za ufunguzi wa  mashindano ya Sirro Kibiti mwaka 2018 katika uwanja wa Samora Kibiti. Mashindano yanayoshirikisha timu 16 kutoka Wilaya za Mkuranga, Kibiti na Rufiji. 

 Msanii Man Prince, akitumbuiza  wakati wa Sherehe za ufunguzi wa  mashindano ya Sirro Kibiti mwaka 2018 katika uwanja wa Samora Kibiti. Mashindano yanayoshirikisha timu 16 kutoka Wilaya za Mkuranga, Kibiti na Rufiji. Picha na Jeshi la Polisi.

RAIS DKT MAGUFULI ALIPOTEMBELEA CHUO KIKUU CHA KILIMO CHA SOKOINE MOROGORO

$
0
0
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Mkuu wa Magezera mkoa wa Morogoro Kamishna Msaidizi wa magereza Mwandamizi (SACP) Mzee ramadhani Nyamka alipowasili Chuo Kikuu cha Kilimo cha Sokoine (SUA) mkoani Morogoro kukutana na wafanyakazi na wanafunzi pamoja na wadau wa chuo jana Mei 7, 2018.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Mkuu wa Magezera mkoa wa Morogoro Kamishna Msaidizi wa magereza Mwandamizi (SACP) Mzee ramadhani Nyamka alipowasili Chuo Kikuu cha Kilimo cha Sokoine (SUA) mkoani Morogoro kukutana na wafanyakazi na wanafunzi pamoja na wadau wa chuo.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akihutubia jumuiya ya Chuo Kikuu cha Kilimo cha Sokoine (SUA) mkoani Morogoro alipofika na kukutana na wafanyakazi na wanafunzi pamoja na wadau wa chuo hicho.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akikaribisha maswali, maoni na ushauri toka kwa jumuiya ya Chuo Kikuu cha Kilimo cha Sokoine (SUA) mkoani Morogoro alipofika na kukutana na wafanyakazi na wanafunzi pamoja na wadau wa chuo hicho leo. Wengine toka kulia ni Mama Janeth Magufuli, Makamu Mkuu wa SUA Profesa Raphael Tihelwa Chibunda, Waziri wa elimu,sayansi,na teknolojia na ufundi Profesa Joyce Ndalichako na Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Dkt. Kebwe Stephen Kebwe.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimpongeza kwa taarifa nzuri Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Kilimo cha Sokoine (SUA) Profesa Raphael Tihelwa Chibunda alipofika na kukutana na wafanyakazi na wanafunzi pamoja na wadau wa chuo hicho.
Sehemu ya wanafunzi, wahadhiri, wafanyakazi na wadau wa Chuo Kikuu cha Kilimo cha Sokoine mkoani Mrorogoro wakimsilikiza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli alipofika na kukutana nao chuo hapo.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiongea jambo na Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Kilimo cha Sokoine (SUA) Profesa Raphael Tihelwa Chibunda alipofika na kukutana na wafanyakazi na wanafunzi pamoja na wadau wa chuo hicho.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akipungiana mikono na wanafunzi, wahadhiri, wafanyakazi na wadau wa Chuo Kikuu cha Kilimo cha Sokoine (SUA) baada ya kukutana nao.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli katika picha ya pamoja na baadhi ya wanafunzi, wahadhiri, wafanyakazi na wadau wa Chuo Kikuu cha Kilimo cha Sokoine (SUA) baada ya kukutana nao
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli katika picha ya pamoja na Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Mkoa alipotembelea Chuo Kikuu cha Kilimo cha Sokoine (SUA) na kukutana na wanafunzi, wahadhiri, wafanyakazi na wadau wa chuo hicho leo.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akipeana mikono na Katibu Tawala wa Mkoa wa Morogoro Bw. Tandari baada ya kukutana na kuongea na wanafunzi, wahadhiri, wafanyakazi na wadau wa Chuo Kikuu cha Kilimo cha Sokoine (SUA). Wengine ni Waziri wa elimu,sayansi,na teknolojia na ufundi Profesa Joyce Ndalichako na Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Dkt. Kebwe Stephen Kebwe. Picha na IKULU

RAIS KARIA AIAGA TIMU YA WATOTO WA KITUO CHA WATOTO WENYE MAZINGIRA MAGUMU CHA TANZANIA STREET ACADEMY (TSC)

$
0
0
Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania TFF Wallace Karia leo ameiaga timu ya Watoto wa Kituo cha Watoto wenye mazingira magumu kutoka kituo cha Tanzania Street Academy (TSC) cha jijini Mwanza waliokwenda nchini Russia kwenye Kombe la dunia kwa Watoto wanaoishi kwenye mazingira magumu.
Timu hiyo imeondoka leo kwa ndege ya Shirika la Ndege la Qatar wakiwa na wachezaji 9 na viongozi 4 kutimiza jumla ya watu 13 kwenye msafara wao.
Rais wa TFF Ndugu Karia ameitakia heri katika safari yao hiyo ya Russia akiwataka kufahamu wanabeba bendera ya Tanzania ambayo ina heshima kubwa hivyo wahakikishe wanafanya vizuri.
Amesema TFF inaamini timu hiyo itafanya vizuri kama ilivyokuwa mwaka 2014 waliporudi na kombe kutoka nchini Brazil kwenye mashindano kama hayo.
Naye Rais wa Taasisi hiyo ya TSC Altaf Mansoor ambaye pia ni mkurugenzi wa kampuni ya Moil ameshukuru ushirikiano mkubwa kutoka kwa TFF ambao wametekeleza kila kilichoombwa pamoja na serikali na sehemu iliyobaki ni kwa vijana hao kwenda kufanya vizuri na kurudi na kikombe.
Katika hatua nyingine Rais wa TFF Ndugu Karia amesema ili kuhakikisha TFF inajikita katika maendeleo ya mpira wa miguu TFF imewaachia Bodi ya Ligi kuwa huru kusimamia Ligi Kuu na Daraja la Kwanza na TFF inaingia pale tu wanapoona mambo hayaendi sawa.
Amesema TFF inasimamia zaidi sera,timu za Taifa na Ligi za chini ikiwemo Ligi ya Mabingwa wa Mikoa (RCL) inayoendelea kwenye vituo vinne vya Geita,Rukwa,Singida na Kilimanjaro.
“Uongozi wangu umepunguza mzigo na kuacha huru vitu vingine vifanywe na Bodi ya Ligi kwa kuwaacha huru na sisi tunasimamia sera na timu za Taifa na mafanikio mnayaona na yatakuja mengi zaidi” amesema Karia.
Ameongeza kuwa ni vizuri watu kuwa na mtazamo chanya kuondokana na mtazamo hasi ambao siku zote hukimbiza wadhamini wanaotaka kuingia kwenye mpira wa miguu akiwataka wadau kubadilika katika mtazamo wao kwakuwa hata TFF iliyopo madarakani tayari imebadilika.

LIGI KUU BARA KUMALIZIKA MEI 31

$
0
0
Msimu wa Ligi wa 2017/2018 kwa mujibu wa Kalenda ya Mashindano ya Shirikisho la Mpira wa Tanzania (TFF) unamalizika Mei 31, 2018.
Bodi ya Ligi Kuu Tanzania (TPLB) ambao ndiyo waendeshaji wa Ligi Kuu ya Vodacom (VPL), Ligi Daraja la Kwanza (FDL) na Ligi Daraja la Pili (SDL) tunatoa pongezi kwa timu ambazo zimefanikiwa kupanda daraja.
Kwa upande wa FDL zilizopanda kwenda VPL msimu wa 2018/2019 kulingana na msimamo wa mwisho wa Ligi hiyo ni; Kundi A ni JKT Tanzania FC ya Dar es Salaam na African Lyon ya Dar es Salaam.
Kundi B ni Kinondoni Municipal Council FC ya Dar es Salaam na Coastal Union ya Tanga wakati Kundi C ni Biashara United FC ya Musoma na Alliance Schools FC ya Mwanza.
Kwa upande wa SDL zilizopanda kwenda FDL msimu wa 2018/2019 ni timu nne zilizoongoza makundi pamoja na washindwa bora (best looser) watatu. Kundi A ni Reha FC ya Dar es Salaam, Kundi B ni Arusha FC ya Arusha, Green Warriors ya Dar es Salaam, na Mashujaa FC ya Kigoma.
Washindwa bora ni Namungo FC ya Lindi,  Pepsi FC ya Dar es Salaam, na Boma FC ya Kyela, Mbeya.

IMETOLEWA NA BODI YA LIGI KUU TANZANIA   

RAIS DKT. MAGUFULI AWAAPISHA BALOZI WA TANZANIA NCHINI CANADA NA KATIBU TAWALA WA MKOA WA TABORA LEO

$
0
0
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimuapisha Mhe. Alphayo Kidata kuwa balozi wa Tanzania nchini Canada kwenye hafla ndogo iliyofanyika Ikulu jijini Dar es salaam leo Mei 10, 2018
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimuapisha Mhe. Alphayo Kidata kuwa balozi wa Tanzania nchini Canada kwenye hafla ndogo iliyofanyika Ikulu jijini Dar es salaam leo Mei 10, 2018
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimuapisha Mhe. Msalika Robert Makungu kuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Tabora  kwenye hafla ndogo iliyofanyika Ikulu jijini Dar es salaam leo 

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimuapisha Mhe. Msalika Robert Makungu kuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Tabora  kwenye hafla ndogo iliyofanyika Ikulu jijini Dar es salaam leo 
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akishuhudia Mhe. Alphayo Kidata  aliyemuapisha kuwa balozi wa Tanzania nchini Canada  na Mhe. Msalika Robert Makungu kuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Tabora   wakila kiapo cha ahadi na uadilifu kwa viongozi wa umma kwenye hafla ndogo iliyofanyika Ikulu jijini Dar es salaam leo
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiongea baada ya kuwaapisha Mhe. Alphayo Kidata kuwa balozi wa Tanzania nchini Canada  na Mhe. Msalika Robert Makungu kuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Tabora kwenye hafla ndogo iliyofanyika Ikulu jijini Dar es salaam leo
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwapongeza  baada ya kuwaapisha  Mhe. Alphayo Kidata kuwa balozi wa Tanzania nchini Canada  na Mhe. Msalika Robert Makungu kuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Tabora kwenye hafla ndogo iliyofanyika Ikulu jijini Dar es salaam leo
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akipata picha ya pamoja baada ya kuwaapisha Mhe. Alphayo Kidata kuwa balozi wa Tanzania nchini Canada  na Mhe. Msalika Robert Makungu kuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Tabora kwenye hafla ndogo iliyofanyika Ikulu jijini Dar es salaam leo Mei 10, 2018. Kulia ni  Waziri Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za mitaa (TAMISEMI) Mhe.  Selemani Jaffo na kushoto ni Naibu Waziri wa Mambo ya nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Suzan Kolimba akifuatiwa na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akipata picha ya pamoja na wakuu wa Vyombo vya Ulinzi na Usalama baada ya kuwaapisha Mhe. Alphayo Kidata kuwa balozi wa Tanzania nchini Canada  na Mhe. Msalika Robert Makungu kuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Tabora kwenye hafla ndogo iliyofanyika Ikulu jijini Dar es salaam leo Mei 10, 2018.Wengine mbele Kulia ni  Waziri Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za mitaa (TAMISEMI) Mhe.  Selemani Jaffo na kushoto ni Naibu Waziri wa Mambo ya nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Suzan Kolimba akifuatiwa na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi. Picha na Ikulu

USAJILI WA VITAMBULISHO VYA TAIFA KWA WANANCHI NI BURE-NIDA

BILIONI 50/- ZATOLEWA KUANZA UJENZI WA STENDI MPYA YA MABASI INAYOJENGWA MBEZI LUIS JIJINI DAR

$
0
0
Muonekano wa standi hiyo ya kisasa inayotarajiwa kujengwa ambayo itakuwa na sehemu za kupumzikia abiria,itakuwa na sehemu za kupaki magari madogo takribani 300,pamoja na Mabasi makubwa 200,na sehemu za biashara.
Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam, Paul Makonda (katikati) akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es salaam kuhusu ujenzi wa Stendi ya mabasi ya kwenda mkoani kinatachotarajiwa kujengwa eneo la Mbezi Luis jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya watendaji wa Manispaa wakisikiliza mjadala uliokuwa ukiongozwa na mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda. 
******************************************
MKUU wa Mkoa wa Dar es salaam Paul Makonda amezungumza na viongozi mbalimbali kuanzia ngazi ya watendaji hadi wakurugenzi wa Manispaa kuhusu miradi mbalimbali ya kichumi katika kujenga nchi.
Makonda ameeleza hayo leo wakati anzungumzia ujenzi wa Stendi ya mabasi ya abiria yaendayo mikoani Ubungo ambao tayari Sh.bilioni 50 imetolewa kwa ajili ya kuanza kujengwa kituo hicho kitakachokuwa cha kisasa kikiwa na huduma mbalimbali za jamii ikiwemo hoteli, supermarketi na huduma za kibenki.
Makonda ameeleza kituo hicho kinatarajiwa kujengwa eneo la Mbezi Luis ambapo amebainisha Manispaa za Jiji hilo imetengewa bajeti ya Sh. bilioni 250 kutoka Mfuko wa Rais kwa ajili ya kuendeleza miradi mbalimbali.
Pia amesema miradi inayosimamiwa na Manispaa ambayo Serikali inaifanyia kazi kama fukwe ya Coco beach ambayo ni mali ya wananchi na itatengenezwa ili wananchi wafurahi kutembelea na kushiriki kula keki ya taifa.
Aidha ameongeza kuwa mapato yameongezeka kutoka Sh.milioni 87 hadi Sh.bilioni moja na kuwasisitiza watendaji kuwa wakali kuhusu matumizi ya fedha.
Makonda amesema lazima manispaa zote ziwe na uchumi madhubuti na kuwahudumia wananchi na kuiacha Serikali kuu kujenga miradi mikubwa kama Standard gauge, miradi ya umeme sambamba na kuangalia usalama nchini.
Pia amewataka wananchi wa Mkoa huo kuunga mkono juhudi za Rais Magufuli kwa kazi kubwa ya kuleta mabadiliko nchini na ameahidi kama watendaji watashirikiana katika kuifikisha Tanzania katika maendeleo na kueleza kuwa haina haja ya kumbeza Rais Magufuli kwani kazi anayoifanya ni kwa faida ya wananchi kama vile miradi ya maji, barabara na umeme hivyo lazima tutambue mchango huu na tuunge mkono juhudi zake.

TANZANIA YATAJWA KUWA BUSTANI YA EDEN NA CHIMBUKO LA MWANADAMU WA KALE DUNIANI

$
0
0

Hatimaye utata uliokuwa ukiendelea duniani kwa watafiti wa mambo ya kale kuhusiana na mahali mwanadamu wa kwanza alipotokea umemalizika baada ya jopo la wataalam liloundwa na Wizara ya Maliasili na Utalii kufuatia ushahidi wa vinasaba kubaini kuwa binadamu huyo alitokea barani Afrika huku ikidaiwa kuwa ni Tanzania eneo la Olduvai Gorge.
Hayo yameelezwa na Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Japhet Hasunga wakati wa mkutano wa wadau wa sekta ya ufugaji nyuki aloiutisha kujadili maendeleo ya sekta hiyo Jijini Dodoma mwishoni mwa wiki.
Amesema utafiti huo umeshirikisha wataalamu kutoka mataifa mbalimbali duniani na kuwa kumalizika kwake kutaiwezesha sekta ya utalii nchini kukua kwa kasi sambamba na kuongeza pato la taifa.

TUME YA TAIFA YA UCHAGUZI YAKUTANA NA UJUMBE WA EU

$
0
0
 Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) Jaji Semistocles Kaijage (katikati) akieleza jambo wakati alipokutana na ujumbe kutoka Ubalozi wa Jumuiya ya Ulaya kujadiliana Taarifa ya Utazamaji wa Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2015 iliyotolewa na jumuiya hiyo.Kushoto ni Makamu Mwenyekiti wa NEC Jaji Mkuu Mst. (Znz) Hamid Mahmoud Hamid na kulia ni Kaimu Mkurugenzi wa Uchaguzi na Mkuu wa Idara ya Habari na Elimu ya Mpiga Kura Giveness Aswile.
Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) Jaji Semistocles Kaijage (wa nne kushoto) akifafanua jambo kwa Balozi wa Jumuiya ya Ulaya (EU) Roeland Van de Geer (wa pili kushoto) na Mtaalau wa Masuala ya Siasa wa EU, Anna Costantin.Ujumbe huo ulifika ofisi za Tume jijini Dar es Salaam kujadili Taarifa ya Utazamaji wa Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2015 ilyotolewa na jumuiya hiyo.
Mjumbe wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) Asina Omari (wa pili kulia) akiwasilisha taarifa fup kuhusu Tume na majukumu yake kwa ujumbe kutoka Ubalozi wa Jumuiya ya Ulaya (EU) (kushoto) uliofika ofisi za NEC kujadili Taarifa ya Utazamaji wa Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2015 iliyotolewa na jumuiya hiyo.Katikati ni Mwenyekiti wa NEC Jaji Semistocles Kaijage.Picha na Hussein Makame-NEC

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

MWENYEKITI WA CHAMA CHA MAPINDUZI CCM RAIS DKT. MAGUFULI AKIWA KATIKA OFISI NDOGO ZA CCM LUMUMBA JIJINI DAR ES SALAAM

$
0
0
 Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi CCM Rais Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Makamu Mwenyekiti wa CCM (Bara) Philip Mangula katika Ofisi ndogo za CCM Lumumba jijini Dar es Salaam.
 Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi CCM Rais Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na Makamu Mwenyekiti wa CCM kwa upande wa Tanzania Bara Philip Mangula katika Ofisi ndogo za CCM Lumumba jijini Dar es Salaam.
  Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi CCM Rais Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika Ofisi ndogo za CCM Lumumba jijini Dar es Salaam.
 Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi CCM Rais Dkt. John Pombe Magufuli akitoka katika Ofisi ndogo za CCM Lumumba jijini Dar es Salaam na Makamu Mwenyekiti wa CCM (Bara) Philip Mangula pamoja na Katibu Mkuu wa CCM Abrahman Kinana
  Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi CCM Rais Dkt. John Pombe Magufuli akitoka katika Ofisi ndogo za CCM Lumumba jijini Dar es Salaam na Makamu Mwenyekiti wa CCM (Bara) Philip Mangula pamoja na Katibu Mkuu wa CCM Abrahman Kinana
Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi CCM Rais Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na Katibu Mkuu wa CCM Abrahman Kinana wakati akiondoka akiwa katika Ofisi ndogo za CCM Lumumba jijini Dar es Salaam. PICHA NA IKULU

MAONESHO YA NISHATI MBADALA WA MKAA KATIKA WIKI YA MAADHIMISHO YA SIKU YA MAZINGIRA DUNIANI

$
0
0

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
OFISI YA MAKAMU WA RAIS
TANGAZO
MWALIKO WA KUSHIRIKI MAONESHO YA NISHATI MBADALA WA MKAA KATIKA WIKI YA MAADHIMISHO YA SIKU YA MAZINGIRA DUNIANI,
31 MEI -  5 JUNI, 2018, VIWANJA VYA MNAZI MMOJA, DAR ES SALAAM
Ofisi ya Makamu wa Rais inawaalika wadau kutoka taasisi za serikali, zisizo za serikali, sekta binafsi, taasisi za utafiti na vyuo vikuu kuonesha bidhaa, ubunifu na uvumbuzi wao katika teknolojia mbalimbali za nishati za kupikia ambazo ni mbadala wa mkaa. Vile vile katika eneo la maonesho wajasiriamali waliowekeza au wenye nia ya kuwekeza katika teknolojia ya nishati mbadala wa mkaa watapewa elimu ya ujasiriamali kuhusu masuala na fursa mbalimbali katika biashara ya uendelezaji wa nishati mbadala. Pia taasisi za fedha zitatoa taarifa za mikopo kwenye ujasiriamali wa nishati.
Maonesho haya yatafanyika kuanzia tarehe 31 Mei hadi 5 Juni, 2018 katika Viwanja vya Mnazi Mmoja, Dar es Salaam.
Maonesho haya ni sehemu ya Maadhimisho ya Siku ya Mazingira Duniani ambayo kitaifa maadhimisho haya yatafanyika Jijini Dar es Salaam. Aidha kwa sehemu kubwa maonesho haya  yatalenga kuchochea ujasiriamali na biashara na nishati mbadala wa mkaa na kuelimisha na kuhamasisha wananchi wote kuondokana na matumizi ya mkaa ili kuokoa misitu yetu na kuhifadhi mazingira.
Wadau wote wenye teknolojia mbalimbali zinazohusu hifadhi ya mazingira ikiwemo kurejereza (recycling) plastiki pia wanakaribishwa kushiriki.
Kwa kuwa fursa hii ni adhimu na adimu ni vema wadau wanaohitaji kushiriki kujiandikisha mapema iwezekanavyo hadi ifikapo tarehe 20 Mei, 2018. Aidha, kila mshiriki wa maonesho haya atatakiwa kulipia gharama za ushiriki ili kuwezesha ushiriki wake, ikiwemo kusafirisha vifaa vyake. Maombi ya ushiriki yaambatane na maelezo mafupi ya teknolojia ya nishati mbadala itakayooneshwa.
Kwa maelezo na mawasiliano zaidi tafadhali wasiliana na Maafisa wafuatao Ofisi ya Makamu wa Rais:
Ndg.Deogratius Paul, 0769257570;
Ndg. Timotheo Mande, 0745 819 197
Wasilisha maombi ya ushiriki kwa:
Katibu Mkuu,
Ofisi ya Makamu wa Rais,
Barabara ya Makole,Jengo la LAPF, Ghorofa ya 7,
S. L. P 2502,
40406 DODOMA,
Barua Pepe: km@vpo.go.tz; Simu: +255 026 235 203 8/0769257570

MSANII LULU MICHAEL SASA KUTUMIKIA KIFUNGO CHA NJE

$
0
0
Muigizaji Elizabeth Michael, maarufu Lulu leo Jumatatu Mei 14, 2018 amebadilishiwa adhabu na sasa anatumikia kifungo cha nje kwa amri ya Mahakama Kuu ya Tanzani, ambapo Magereza imethibitisha kuhusu uamuzi huo.
Lulu alihukumiwa kifungo cha miaka miwili gerezani baada ya kupatikana na hatia ya kuua bila kukusudia.
Hukumu ya kesi hiyo ilisomwa na Jaji wa Mahakama Kuu, Sam Rumanyika, ambaye baada ya kusikiliza utetezi kutoka kwa mawakili wa upande wa mshtakiwa alitoa hukumu.
Lulu, alishtakiwa kwa kesi ya kumuua bila kukusudia, aliyekuwa muigizaji maarufu wa filamu nchini na nje ya nchi, Steven Kanumba ambaye pia alikuwa mpenzi wake.

BENKI YA NMB YAKUTANA NA WAKANDARASI WA DAR KUJADILI CHANGAMOTO ZA KAZI

$
0
0
Mkuu wa Manispaa ya Temeke, Nasib Mbaga, (wa pili kushoto) Mkuu wa Kanda ya Dar es Salaam, Benki ya NMB, Badru Iddi (kushoto) mku wa Dhamana za Serikali wa Benki ya NMB, Vick Bishubo (katikati kulia) Meneja wa Benki ya NMb tawi la Tandika, Faraja Raphael na Meneja wa Benki hiyo tawi la Temeke, Christin, wakifuatilia Semina ya majadiliano na Wakandarasi wa jijini Dar es Salaam, kuhusu changamoto za kazi iliyofanyika kwenye Ukumbi wa Iddi Nyundo Manispaa ya Temeke jijini.
 Mkuu wa Dhamana za Serikali wa Benki ya NMB, Vick Bishubo, akizungumza wakati wa Semina ya majadiliano na Wakandarasi wa jijini Dar es Salaam, kuhusu changamoto za kazi iliyofanyika kwenye Ukumbi wa Iddi Nyundo Manispaa ya Temeke jijini, leo.
 Mkuu wa Kitengo cha Biashara na Fedha Benki ya NMB, Adelin Mloso, akifafanua jambo wakati wa Semina ya majadiliano na Wakandarasi wa jijini Dar es Salaam, kuhusu changamoto za kazi iliyofanyika kwenye Ukumbi wa Iddi Nyundo Manispaa ya Temeke jijini
Umakini wa kufuatilia semina...

KAMERA YA MAFOTO BLOG MITAANI LEO

$
0
0
Magari yakipita kwa taabu katika barabara ya Machinjioni Vingunguti kutokana na barabara hiyo kuharibika kutokana na mvua zinazoendelea kunyesha jijini Dar es Salaam, kama yalivyokutwa na mpigapicha wetu. 

KAMERA YA MAFOTO BLOG MITAANI LEO

$
0
0
Wakazi wa Vingunguti Dar es Salaam, wakivuka kwa taabu katika eneo lililojaa maji kama walivyonaswa na Kamera ya Mafoto Blog Vingunguti 
 Wanafunzi wa Shule ya Msingi Miembeni wakicheza na mbuzi kama walivyonaswa na Kamera ya Mafoto Blog
 Wanafunzi wakivuka eneo lililojaa maji katika mitaa ya Vingunguti Dar es Salaam,

YANGA WAJIFUA KUJIANDAA KUKIPIGA NA RAYON SPORTS YA RWANDA KESHO

$
0
0

Wachezaji wa Yanga wakiwa mazoezini kujiandaa na mchezo wa kesho
Wachezaji wa Yanga wakiwa mazoezini kujiandaa na mchezo wa kesho
Nahodha wa Yanga Nadir Haroub 'Canavaro' akizungumzia mchezo wa kesho
Kocha wa timu ya Rayon Ivan Minnert (kushoto) akizungumza na waandishi wa habari katika mkutano uliofanyika jijini Dar es Salaam, leo kuhusu mchezo wa Kombe la Shirikisho unaopigwa leo kwenye Uwanja wa Taifa. Kulia ni Kocha Msaidizi wa Yanga, Noel Mwandila.
Kiungo wa Yanga, Thaban Kamusoko, akimiliki mpira wakati wa mazoezi hayo.

RAIS MAGUFULI KUNOGESHA UBINGWA WA SIMBA KUWAKABIDHI KOMBE UWANJA WA TAIFA

$
0
0

 Rais wa Shirikisho la mpira wa miguu Tanzania, TFF, Wallace Karia, akizungumza na waandishi wa habari kwenye Ofisi za TFF, jijini Dar es Salaam, leo mchana, wakati akitangaza mgeni rasmi katika mechi ya Ligi Kuu Bara kati ya Simba na Kagera Sugar, ambapo alimtangaza Rais Dkt Magufuli ambaye atawakabidhi Kombe la mshindi wa Ligi Kuu Simba kwa msimu wa 2017-18.

RAIS wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Wallace Karia, leo amemtangaza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli, kuwa anatarajia kuwa mgeni rasmi katika mchezo wa Ligi Kuu Bara kati ya Simba na Kagera Sugar unaotarajia kupigwa Mei 19 mwaka huu.
Aidha amesema kuwa Shirikisho limemuomba, Dk. Magufuli kuwa mgeni rasmi katika mchezo huo ili kuwakabidhi Kombe la ubingwa wa Ligi Kuu, Simba SC siku hiyo katika Uwanja wa Taifa jijin Dar es Salaam.Akizungumza na Waandishi wa Habari leo makao makuu ya ofisi za TFF, Dar es Salaam, Karia amesema mpaka sasa wanasubiri majibu kuhusu ombi hilo.
Pamoja na hayo, Rais Karia amesema kwamba siku hiyo kama Rais Magufuli atakubali mwaliko huo, ataanza kwa kukabidhiwa Kombe la ubingwa wa michuano ya Mataifa ya Afrika Mashariki na Kati kwa vijana chini ya umri wa miaka 17 (CECAFA U17), ambalo Tanzania ilitwaa mapema mwezi huu nchini Burundi.

MAKALA MAALUMU YA SIR ALEX FERGUSON

$
0
0
 Sir Alex Feguson | Wiki chache zinazokuja ni muhimu sana
Kutokwa Damu kwenye/ndani ya Ubongo ║Maswali  na Majibu
Nini maana ya kutokwa damu kwenye/ndani ya Ubongo?
Maana yake ni kuvuja damu kwenye/ndani ya ubongo(A brain haemorrhage is bleeding in or around the brain).  Inasababisha kuvimba kwa ubongo kwa sababu ya mkusanyiko wa damu (hematoma) hii itapelekea kupanda kwa presha ndani ya ubongo na kupunguza mzunguko wa damu ndani ya ubongo.  Dalili zake zitakuwa sawa na mtu aliyepata kiarusi (Stroke) yaani upungufu wa nguvu/kupooza upande mmoja wa mwili. Mara zingine wagonjwa watasikia kichwa kuuma sana, kutoo weza kusema/kuzungumza vizuri na kutoona vizuri pia.
Nini kinasababisha kutokwa damu kwenye/ndani ya Ubongo?
Kuna sababu nyingi ya kutokwa damu kwenye/ndani ya Ubongo.  Inaweza damu kutoka yenyewe (spontaneous) kwa kupasuka mishipa ya damu  (ruptured aneurysm), inajulikana kama Kiarusi/stroke.  Sababu zingine ni shinikizo la damu, ambalo husababisha mishipa kuwa dhaifu na kupasuka.
Upasuaji wa ubongo nini kinafanywa na je unasaidia?
Baadhi ya wagonjwa wa hili tatizo wanahitaji upasuaji kupunguza pressure ndani ya ubongo. Upasuaji huu unapunguza/unatoa damu iliyovuja ndani ya ubongo wakati huohuo madaktari wanarekebisha mishipa iliopasuka (repair).  Kuna njia kadha za upasuaji ili kupunguza/kutoa damu ndani ya ubongo 1. Kupasua kichwa na kuitoa damu 2. Kutoboa tundu dogo na kuivuta damu iliyovuja ndani ya ubongo.
Nini matokeo ya upasuaji huu wa ubongo?
Matokeo ya upasuaji huu unategemea vitu vingi k.m. sehemu gani ya ubongo umetoka damu, kiasi gani cha damu kimetoka n.k. Wagonjwa wengi hawatakufa kwa tatizo hili lakini kupona kunaweza kuchukua muda mrefu wiki/miezi kadha  mpaka miaka au kutopona kabisa (yaani kuweza kuzungumza sawa sawa, kutembea sawa sawa , au kutumia kikamilifu upande wa mwili uliopooza.
Sir Alex Ferguson
Ni sahihi familia ya Sir Feguson kutopenda kuzungumzia hali ya mgonjwa wao (Sir Alex) baada ya kukimbizwa hospitali na kufanyiwa upasuaji wa ubongo.  Lakini kwa mtu wa umri wake na historia ya tatizo la moyo alilo nalo mwaka 2003 Sir Alex aliwekewa betri ya moyo (Pacemaker). Sababu kubwa itakuwa kuvuja damu ndani ya ubongo ambayo husababisha adhari zisizoweza tibika( irreparable damage to those cells).
Kwa ugonjwa wa Sir Alex, madaktari walifanya maamuzi ya kufanya upasuaji kwa sababu walihisi uvujaji wa damu ndani ya ubongo ulikuwa unaharibu sehemu zingine za ubongo.  Hii huwa inahatarisha uhai wa mgonjwa.  Upasuaji huu husaidia kupunguza adhari za muda mrefu kwa Sir Alex ambazo anaweza kuzipata (kutoweza kuzungumza sawa sawa, kupooza upande mmoja n.k) kifupi alichopata ni kiarusi/stroke).
Sir Alex ugonjwa wake asilimia 100% ni mishipa kupasuka ndio maana maamuzi yalikuwa kupasua ingekuwa ni mishapa kuziba mara nyingi upasuaji huwa haufanywi. 
Nini kilicho sababisha? sababu ni nyingi kwa mfano:
1. Udhaifu wa mishipa ya damu ndani ya ubongo, 2. Ugonjwa ndani ya ubongo, 3. Hitilafu katika  ugandaji wa damu (clotting disorders au damu kuwa nyepesi ) labda kwa dawa alizo kuwa anatumia k.m Asprin, clopidogrel nk. Kwa hiyo kila mgojwa anakuwa na sababu tofauti na mwingine.


Siku au wiki chache baada ya upasuaji huu ni muhimu sana kwa mgonjwa kuangaliwa kwa ukaribu kwa mfano damu inaweza toka tena (rebleed)
Kama mgojwa hajapoteza maisha lakini kapooza au hasemi vizuri hakuja rekebishika kwa wiki au miezi kadha uwezekano wa mgonjwa kurudia shughuli zake za kawaida mara nyingi ni vigumu sana.  Kubwa kama madaktari kuna sababu zote za kuendelea kupigania maisha ya mgonjwa husika.
Kila la kheri Sir Alex Ferguson
Mohamed Janabi MD., PhD., FACC
Mpenzi wa mpira wa miguu (Soccer)
Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete

Imetayarishwa na Profesa M Janabi
Viewing all 13053 articles
Browse latest View live


<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>