Quantcast
Channel: SUFIANIMAFOTO
Viewing all 13053 articles
Browse latest View live

SHINDANO LA UTUNZI WA HADITHI LA ANDIKA CHALLENGE LAZINDULIWA

$
0
0
Mkurugenzi wa Taasisi ya Dr Ntuyabaliwe, Bi. Jacqueline Mengi akipewa kitabu cha wageni mara baada ya kuwasili ofisini kwa Mwalimu Mkuu wa shule ya msingi Kinondoni, Bw Emmanuel Ntenga kwa ajili ya uzinduzi wa shindano la Andika Challenge kwa watoto wa shule za msingi manispaa ya Kinondoni katika hafla iliyofanyika mwishoni mwa wiki shuleni hapo jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi wa Taasisi ya Dr Ntuyabaliwe, Bi. Jacqueline Mengi akisaini kitabu cha wageni ofisini kwa Mwalimu Mkuu wa shule ya msingi Kinondoni, Bw Emmanuel Ntenga (hayupo pichani) mara baada ya kuwasili shuleni hapo kwa ajili ya uzinduzi wa shindano la Andika Challenge kwa watoto wa shule za msingi manispaa ya Kinondoni katika hafla iliyofanyika mwishoni mwa wiki shuleni hapo jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi wa Taasisi ya Dr Ntuyabaliwe, Bi. Jacqueline Mengi (kulia) akiongozana na mgeni rasmi Kaimu Afisa Elimu Manispaa ya Kinondoni, Esther Kaaya (wa pili kulia), kwa Mwalimu Mkuu wa shule ya msingi Kinondoni, Bw Emmanuel Ntenga (wa pili kushoto), Mwandishi wa Habari wa IPP Ltd. Abdulhamid Njovu (kushoto) wakielekea kwenye ukumbi wa maktaba ya shule ya msingi Kinondoni kwa ajili ya kuzindua shindano la Andika Challenge kwa watoto wa shule za msingi manispaa ya Kinondoni katika hafla iliyofanyika mwishoni mwa wiki shuleni hapo jijini Dar es Salaam.
Mwalimu Mkuu wa shule ya msingi Kinondoni, Bw Emmanuel Ntenga akizungumza machache na kuitambulisha meza kuu wakati wa hafla ya uzinduzi wa shindano la Andika Challenge kwa watoto wa shule za msingi manispaa ya Kinondoni iliyofanyika mwishoni mwa wiki shuleni hapo jijini Dar es Salaam. Kutoka kushoto ni Mtendaji wa Kata ya Mwananyamala, Mickidadi Ngatumbura, Mgeni rasmi Kaimu Afisa Elimu Manispaa ya Kinondoni, Esther Kaaya, Mkurugenzi wa Taasisi ya Dr Ntuyabaliwe, Bi. Jacqueline Mengi pamoja na Afisa Elimu kata ya Mwananyamala, Joshua Biswalo wakiwa meza kuu.
Mgeni rasmi Kaimu Afisa Elimu Manispaa ya Kinondoni, Esther Kaaya akizungumza na wanafunzi pamoja na walimu wa shule ya msingi Kinondoni wakati wa hafla ya uzinduzi wa shindano la Andika Challenge kwa watoto wa shule za msingi manispaa ya Kinondoni iliyofanyika mwishoni mwa wiki shuleni hapo jijini Dar es Salaam. Kulia ni Mkurugenzi wa Taasisi ya Dr Ntuyabaliwe, Bi. Jacqueline Mengi pamoja na Mtendaji wa Kata ya Mwananyamala, Mickidadi Ngatumbura (kushoto).
Mgeni rasmi Kaimu Afisa Elimu Manispaa ya Kinondoni, Esther Kaaya akitoa mkono wa pongezi kwa Mkurugenzi wa Taasisi ya Dr Ntuyabaliwe, Bi. Jacqueline Mengi wakati wa hafla ya uzinduzi wa shindano la Andika Challenge kwa watoto wa shule za msingi manispaa ya Kinondoni iliyofanyika mwishoni mwa wiki shuleni hapo jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi wa Taasisi ya Dr Ntuyabaliwe, Bi. Jacqueline Mengi akizungumza kuhusu vigezo vya kushiriki na zawadi kwa tano bora kwa wanafunzi wa shule za msingi manispaa ya Kinondoni watakaoshiriki shindano la Andika Challengekatika hafla fupi ya uzinduzi huo iliyofanyika kwenye ukumbi wa maktaba ya shule ya msingi Kinondoni mwishoni mwa wiki jijini Dar es Salaam.
Mwanafunzi Brian Jackson wa darasa la saba shule ya msingi Kinondoni akitoa neno loa shukrani kwa Taasisi ya Dr. Ntuyabaliwe kwa kuzindua shindano hilo la andika challenge wakati hafla fupi iliyofanyika kwenye ukumbi wa maktaba shuleni hapo mwishoni mwa wiki jijini Dar es Salaam. Kulia ni Mwanafunzi Blessing Elianoki wa darasa la sita.
Mkurugenzi wa Taasisi ya Dr Ntuyabaliwe, Bi. Jacqueline Mengi akifurahi jambo wakati wanafunzi Brian Jackson na Blessing Elianoki walipokua wakitoa neno la shukrani kwa Taasisi hiyo wakati wa hafla fupi ya uzinduzi wa shindano la Andika Challenge kwa watoto wa shule za msingi manispaa ya Kinondoni uliofanyika mwishoni mwa wiki shuleni hapo jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi wa Taasisi ya Dr Ntuyabaliwe, Bi. Jacqueline Mengi akiwapongeza wanafunzi Brian Jackson na Blessing Elianoki waliotoa neno la shukrani wakati wa hafla fupi ya uzinduzi wa shindano la Andika Challenge kwa watoto wa shule za msingi manispaa ya Kinondoni uliofanyika mwishoni mwa wiki shuleni hapo jijini Dar es Salaam.
Mgeni rasmi Kaimu Afisa Elimu Manispaa ya Kinondoni, Esther Kaaya (wa pili kushoto) akikata utepe kuashiria uzinduzi rasmi wa shindano la andika challenge kwa watoto wa shule za msingi manispaa ya Kinondoni wakati hafla fupi iliyofanyika kwenye ukumbi wa maktaba shuleni hapo mwishoni mwa wiki jijini Dar es Salaam. Wanaoshudia tukio hilo Mkurugenzi wa Taasisi ya Dr Ntuyabaliwe, Bi. Jacqueline Mengi (wa tatu kulia), Mwalimu Mkuu wa shule ya msingi Kinondoni, Bw Emmanuel Ntenga (wa pili kulia), Mtendaji wa Kata ya Mwananyamala, Mickidadi Ngatumbura (kulia) pamoja na Afisa Elimu kata ya Mwananyamala, Joshua Biswalo (kushoto).
Mgeni rasmi Kaimu Afisa Elimu Manispaa ya Kinondoni, Esther Kaaya pamoja na Mkurugenzi wa Taasisi ya Dr Ntuyabaliwe, Bi. Jacqueline Mengi wakizundua shindano la andika challenge kwa watoto wa shule za msingi manispaa ya Kinondoni katika hafla fupi iliyofanyika kwenye ukumbi wa maktaba shuleni hapo mwishoni mwa wiki jijini Dar es Salaam.
Mgeni rasmi Kaimu Afisa Elimu Manispaa ya Kinondoni, Esther Kaaya akimpongeza Mkurugenzi wa Taasisi ya Dr Ntuyabaliwe, Bi. Jacqueline Mengi mara baada ya kuzindua rasmi shindano la andika challenge kwa watoto wa shule za msingi manispaa ya Kinondoni katika hafla fupi iliyofanyika kwenye ukumbi wa maktaba shuleni hapo mwishoni mwa wiki jijini Dar es Salaam.
Sehemu ya waandishi wa habari na baadhi ya walimu wa shule ya msingi Kinondoni waliohudhuria uzinduzi wa shindano la andika challenge kwa watoto wa shule za msingi manispaa ya Kinondoni katika hafla fupi iliyofanyika kwenye ukumbi wa maktaba shuleni hapo mwishoni mwa wiki jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya wanafunzi wa shule ya msingi Kinondoni waliowakilisha wenzao katika hafla fupi ya uzinduzi wa shindano la andika challenge kwa watoto wa shule za msingi manispaa ya Kinondoni iliyofanyika kwenye ukumbi wa maktaba shuleni hapo mwishoni mwa wiki jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi wa Taasisi ya Dr Ntuyabaliwe, Bi. Jacqueline Mengi katika picha ya pamoja na baadhi ya walimu wa shule ya msingi Kinondoni mara baada ya kumalizika kwa hafla ya uzinduzi wa shindano la andika challenge kwa watoto wa shule za msingi manispaa ya Kinondoni uliofanyika kwenye ukumbi wa maktaba shuleni hapo mwishoni mwa wiki jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi wa Taasisi ya Dr Ntuyabaliwe, Bi. Jacqueline Mengi katika picha ya pamoja na baadhi ya wanafunzi na baadhi ya walimu wa shule ya msingi Kinondoni mara baada ya kumalizika kwa hafla ya uzinduzi wa shindano la andika challenge kwa watoto wa shule za msingi manispaa ya Kinondoni uliofanyika kwenye ukumbi wa maktaba shuleni hapo mwishoni mwa wiki jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi wa Taasisi ya Dr Ntuyabaliwe, Bi. Jacqueline Mengi katika picha ya pamoja na mgeni rasmi Kaimu Afisa Elimu Manispaa ya Kinondoni, Esther Kaaya, Mwalimu Mkuu wa shule ya msingi Kinondoni, Bw Emmanuel Ntenga pamoja na baadhi ya wanafunzi wa shule hiyo waliowakilisha wenzao katika hafla fupi ya uzinduzi wa shindano la andika challenge kwa watoto wa shule za msingi manispaa ya Kinondoni uliofanyika kwenye ukumbi wa maktaba shuleni hapo mwishoni mwa wiki jijini Dar es Salaam.
********************************************
Na Mwandishi wetu
TAASISI ya Dr Ntuyabaliwe imezindua shindano la Andika Challenge kwa watoto wa shule za msingi manispaa ya Kinondoni wenye lengo la kuibua vipaji vya watoto katika kubuni na kutunga hadithi.
Shindano hilo linatarajiwa katika siku za usoni kufika Tanzania nzima.
Uzinduzi huo umefanywa katika shule ya msingi Kinondoni wilayani Kinondoni.
Akizindua shindano hilo Kaimu Afisa Elimu Manispaa ya Kinondoni, Esther Kaaya alisema shindano hilo ni muhimu kwa nchi hii hasa katika kukuza uwezo wa kusoma na kuandika na kuibua vipaji vya wanafunzi katika kukuza lugha ya Kiswahili na ubunifu.
Alisema kwamba serikali inafurahishwa na jinsi taasisi hiyo inavyofanywa ya kuibua vipaji vya watoto na kukuza lugha ya Kiswahili kwa kuangalia usomaji wa vitabu na shindano la andika challenge.
Alisema anajua kwamba Taasisi hiyo ilianza na maktaba katika shule za msingi na kuhamasisha usomaji wa vitabu na sasa wanakuja na shindano hilo litakalosambaa nchi nzima.
Alisema andika challenge ni muhimu kwa watoto.
“Tunaamini kuwa tunaenda kukuza vipaji vya watoto…katika kutunga hadithi kwa kuongoza watoto katika kuhakikisha kwamba uchaguzi wa mada zinakuwa na maana zikizingatia fani na maudhui, moja ya tanzu au kipera cha simulizi “ alisema.
Alisema hali hiyo iliyoletwa na taasisi hiyo inahamasisha watoto kufikiri na kutaka walezi walimu na wazazi kuona na kuendeleza uibuaji vipaji vya watoto.
Alisema kwa kuwa na mashindano taasisi hiyo inafanya watoto kuwania tuzo na hivyo kuleta hamasa na changamoto katika utunzi na usambazaji wa maudhui.
Alisema kuna faida nyingi na shindano hilo kwa kuwa inakuza lugha kwa kukuza msamiati pia baadhi ya hadithi zitahifadhi utamaduni wetu.
Kuna wazazi watawaelekeza watoto hadithi na hivyo kuhifadhi mila na desturi
Shindano hilo linagusa wanafunzi wa darasa la nne hadi la 7.
Akitoa neno la shukurani mwanafunzi Brian Jackson ambaye anasoma darasa la saba shule ya Kinondoni alimshukuru mama Mengi kwa kuzindua andika challenge .
Alisema anaamini kuwa kwa mashindano hayo ya utunzi wa hadithi utaibua vipaji na fikira na maarifa na itawapelekea kutundika tunzi mbalimbali za hadithi.
Naye Mkurugenzi wa Taasisi ya Dr Ntuyabaliwe Jacqueline Mengi amesema licha ya Taasisi yake kuhusika na ukarabati wa vyumba vya maktaba na kutoa vitabu kwa shule za msingi, imeamua kuanzisha shindano la ANDIKA CHALLENGE kwa ajili ya wanafunzi wa manispaa za Kinondoni na kabla ya kulipeleka nchi nzima katika awamu tofauti, ikiwa ni kuunga mkono wa jitihada za serikali za kuboresha elimu nchini.
Amesema shindano hilo kwa wilaya ya Kinondoni litafikia kilele Mei 30 mwaka huu, na washindi watano wa kwanza watatangazwa na kuzawadiwa tarehe 16 Juni mwaka huu, wakati wa maadhimisho ya siku ya mtoto wa Afrika kwa mwaka huu.
Mwalimu Mkuu wa shule ya msingi Kinondoni, Bw Emmanuel Ntenga amesema atahakikisha kuwa wanafunzi wengi wa shule yake wanashiriki katika shindano hilo na kutoa wito kwa watoto wengine wilayani humo kuonesha umahiri wao.

MADHIMISHO YA KIMONDO CHA MBOZI KUFANYIKA MWEZI JUNI MKOANI SONGWE

$
0
0
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Japhet Hasunga akiangalia Kimondo cha Mbozi alipotembelea kijiji cha Ndolezi, wilaya ya Mbozi mkoani Songwe jana kwa ajili ya kuangalia maandalizi ya maadhimisho ya siku ya kimondo duniani yatakayofanyika Juni 28 hadi 30 mwaka huu. Kimondo cha Mbozi ni cha pili kwa ukubwa barani Afrika na kinakadiriwa kuwa na tani 12 na mchanganyiko wa madini ya Chuma 90%, Nickel 8.69%, Copper 0.66%, Sulphur 0.01% na Phosphorus 0.11.
**********************************************
Na Hamza Temba-WMU-Songwe
Mkoa wa Songwe kwa kushirikiana na Wizara ya Maliasili na Utalii na wadau wengine wa uhifadhi na maendeleo utafanya maadhimisho ya siku ya Kimondo cha Mbozi kwa mara ya kwanza katika historia kwenye Kijiji cha Ndolezi Kata ya Mlangali, wilayani Mbozi kuanzia Juni 28 hadi 30 mwaka huu .
Maadhimisho hayo yataenda sambamba na maadhimisho ya siku ya Vimondo duniani ambayo yaliazimiwa kufanyika Juni 30 kila mwaka na kikao cha Umoja wa Mataifa cha tarehe 6 Desemba, 2016.
Pamoja na mambo mengine, kikao hicho pia kiliazimia tarehe hiyo kuwa siku ya kuelimisha umma kuhusu elimu ya anga na mafanikio ya tafiti mbalimbali yaliyopatikana kuhusu elimu hiyo, kutambua juhudi zilizofanyika, kuweka sheria za kimataifa na kutoa tahadhari juu ya athari zinazoweza kutokea endapo dunia itafanya uharibifu juu ya anga.
Taarifa hiyo imetolewa jana katika Kijiji cha Ndolezi wilayani Mbozi na Kaimu Katibu Tawala Mkoa wa Songwe, Herman Tesha wakati akiwasilisha taarifa ya maandalizi ya maadhimisho hayo kwa Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Japhet Hasunga ambaye alitembelea kituo hicho kwa ajili ya kukagua shughuli za maandalizi.
Amesema lengo la maadhimisho hayo ni kutangaza Kimondo kama kivutio muhimu cha utalii mkoani Songwe pamoja na vivutio vingine vya mkoa huo kwa ujumla ili kutoa fursa ya uwekezaji kwenye sekta ya utalii mkoani humo. 
Amesema maadhimisho hayo yataenda sambamba na kongamano la uwekezaji na sayansi ya vimondo, maonesho ya malikale, maonesho ya kiutamaduni, mashindano ya riadha (Kimondo Marathon), mashindano ya netiboli na mpira wa miguu (Kimondo Ligi).
Kwa upande wake, Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Japhet Hasunga amesema Serikali kupitia Wizara yake itashiriki kikamilifu katika maadhimisho hayo kwa kushirikiana na mkoa wa Songwe na wadau wengine ili kuhakikisha kivutio hicho cha Kimondo kinajulikana zaidi ndani na nje ya nchi na hatimaye kiongeze idadi ya watalii na mapato.
Amesema wizara yake ina mkakati maalum wa kuimarisha kituo hicho cha utalii ambapo hivi sasa imeshajenga kituo maalum cha taarifa ambacho kimegharimu zaidi ya Shilingi milioni 400 za Kitanzania. 
Aidha, amesema kupitia mkakati mpya wa wizara wa kuimarisha na kuvijengea uwezo vituo vya malikale nchini kwa kuzishirikisha taasisi za uhifadhi wa wanyamapori na misitu, Shirika la Hifadhi za Taifa Tanapa litashirikiana na kituo hicho kwa kuimarisha miundombinu pamoja na utangazaji. 
Nao wananchi wa kijiji cha Ndolezi wakizungumza kwa nyakati tofauti hawakusita kuonyesha furaha zao kuhusu maendeleo ya eneo hilo na kuahidi kutoa ushirikiano kwa Serikali katika mipango na miradi mbalimbali itakayoanzishwa katika eneo hilo kwa faida ya pande zote mbili.
Katika hatua nyingine, baada ya kuhitimishwa kwa ratiba za Mwenge wa Uhuru wilayani Mbozi, wakimbiza Mwenge Kitaifa walilazimika kutumia fursa ya uwepo wao wilayani humo kwenda kutalii kwenye kivutio cha Kimondo wakati wa usiku wakiongozwa na Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Japhet Hasunga. 
Kimondo cha Mbozi kilianguka mwaka 1840 kutoka kwenye obiti yake huko angani huku kikikadiriwa kuwa na tani 12 na mchanganyiko wa madini ya Chuma 90%, Nickel 8.69%, Copper 0.66%, Sulphur 0.01% na Phosphorus 0.11. Kimomdo hicho ni cha pili kwa ukubwa barani Afrika na cha nane duniani kati ya vimondo 600 vilivyodondoka maeneo mbalimbali ulimwenguni, sifa yake kubwa ni kuwa na ubaridi wakati wote hata mchana wa jua kali.
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Japhet Hasunga akikagua mpaka wa eneo la kituo cha kimondo na vijiji jirani alipotembelea kituo hicho cha utalii katika kijiji cha Ndolezi, wilaya ya Mbozi mkoani Songwe jana kwa ajili ya kuangalia maandalizi ya maadhimisho ya siku ya kimondo duniani yatakayofanyika Juni 28 hadi 30 mwaka huu. Kimondo cha Mbozi ni cha pili kwa ukubwa barani Afrika na kinakadiriwa kuwa na tani 12 na mchanganyiko wa madini ya Chuma 90%, Nickel 8.69%, Copper 0.66%, Sulphur 0.01% na Phosphorus 0.11.
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Japhet Hasunga akikagua kituo cha taarifa cha Kimondo cha Mbozi alipotembelea kituo hicho cha utalii katika kijiji cha Ndolezi, wilaya ya Mbozi mkoani Songwe jana kwa ajili ya kuangalia maandalizi ya maadhimisho ya siku ya kimondo duniani yatakayofanyika Juni 28 hadi 30 mwaka huu. Kimondo cha Mbozi ni cha pili kwa ukubwa barani Afrika na kinakadiriwa kuwa na tani 12 na mchanganyiko wa madini ya Chuma 90%, Nickel 8.69%, Copper 0.66%, Sulphur 0.01% na Phosphorus 0.11.
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Japhet Hasunga akizungumza na baadhi ya watalii wa ndani waliotembelea kituo cha utalii cha kimondo katika kijiji cha Ndolezi, wilaya ya Mbozi mkoani Songwe jana. Nyuma yao ni jengo jipya la kituo cha taarifa ambalo ujenzi wake umekamilika.
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Japhet Hasunga akiwa kwenye picha ya pamoja na baadhi ya watalii wa ndani waliotembelea kituo cha utalii cha kimondo katika kijiji cha Ndolezi, wilaya ya Mbozi mkoani Songwe jana. Nyuma yao ni jengo jipya la kituo cha taarifa ambalo ujenzi wake umekamilika. Kimondo cha Mbozi ni cha pili kwa ukubwa barani Afrika na kinakadiriwa kuwa na tani 12 na mchanganyiko wa madini ya Chuma 90%, Nickel 8.69%, Copper 0.66%, Sulphur 0.01% na Phosphorus 0.11.
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Japhet Hasunga (nyuma kulia) akiwa kwenye picha ya pamoja na Wakimbiza Mwenge kitaifa, Mkuu wa Wilaya ya Mbozi, Ernest Palingo (kushoto) na waratibu wa Mwenge mkoa wa Songwe mbele ya Kimondo cha Mbozi katika kijiji cha Ndolezi, wilaya ya Mbozi mkoani Songwe jana usiku baada ya shughuli za Mwenge. Kimondo hicho ni cha pili kwa ukubwa barani Afrika na kinakadiriwa kuwa na tani 12 na mchanganyiko wa madini ya Chuma 90%, Nickel 8.69%, Copper 0.66%, Sulphur 0.01% na Phosphorus 0.11.

VIDEO: RAIS MAGUFULI KUNOGESHA, KUWAKABIDHI SIMBA KOMBE LA UBINGWA

RAIS DKT MAGUFULI AFANYA ZIARA YA GHAFLA BANDARINI DAR ES SALAAM KUKAGUA MATANKI YA MAFUTA YA KULA

$
0
0
ais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akinunua mapapai na ndizi nje ya eneo lenye matanki ya kuhifadhia mafuta ya kula baada ya kushushwa melini alipofanya safari ya ghafla kukagua uingizwaji na ugawaji wa ulipiaji wa ushuru bidhaa hiyo kwenye bandari ya Dar es salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akigawa mapapai na ndizi kwa wananchi nje ya eneo lenye matanki ya kuhifadhia mafuta ya kula baada ya kushushwa melini alipofanya safari ya ghafla kukagua uingizwaji na ugawaji wa ulipiaji wa ushuru bidhaa hiyo kwenye bandari Dar
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akiwasili eneo lenye matanki ya kuhifadhia mafuta ya kula baada ya kushushwa melini alipofanya safari ya ghafla kukagua uingizwaji na ugawaji wa ulipiaji wa ushuru bidhaa hiyo kwenye bandari ya Dar es salaam
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akitoa maelekezo na kuulia maswali alipowasili eneo lenye matanki ya kuhifadhia mafuta ya kula baada ya kushushwa melini alipofanya safari ya ghafla kukagua uingizwaji na ugawaji wa ulipiaji wa ushuru bidhaa hiyo kwenye bandari ya Dar es salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akitoa maelekezo na kuulia maswali alipowasili eneo lenye matanki ya kuhifadhia mafuta ya kula baada ya kushushwa melini alipofanya safari ya ghafla kukagua uingizwaji na ugawaji wa ulipiaji wa ushuru bidhaa hiyo kwenye bandari ya Dar es salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akitoa maelekezo na kuulia maswali alipowasili eneo lenye matanki ya kuhifadhia mafuta ya kula baada ya kushushwa melini alipofanya safari ya ghafla kukagua uingizwaji na ugawaji wa ulipiaji wa ushuru bidhaa hiyo kwenye bandari ya Dar es salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akitoa maelekezo na kuulia maswali alipowasili eneo lenye matanki ya kuhifadhia mafuta ya kula baada ya kushushwa melini alipofanya safari ya ghafla kukagua uingizwaji na ugawaji wa ulipiaji wa ushuru bidhaa hiyo kwenye bandari ya Dar es salaam. 
Wa pili kushoto ni Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji Mhe. Charles Mwijage, kushoto ni Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango Mhe. Doto James, mwenye kofia ngumu ya njano ni Mkurugenzi wa kampuni ya uingizaji mafuta nchini TLS & VOT Bw. Claudio Ghirardi, Kulia ni Katibu Mkuu Wizara ya Viwanda na Biashara Profesa Olesante ole Gabriel anayefuatiwa na Mwenyekiti wa Kamati ya Rais ya Kuchunguza mafuta ya Kula na Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji Profesa Joseph R. Buchweishaija.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akitoa maelekezo na kuulia maswali alipowasili eneo lenye matanki ya kuhifadhia mafuta ya kula baada ya kushushwa melini alipofanya safari ya ghafla kukagua uingizwaji na ugawaji wa ulipiaji wa ushuru bidhaa hiyo kwenye bandari ya Dar es salaam, Nyuma yake ni Mkurugenzi wa kampuni ya uingizaji mafuta nchini TLS & VOT Bw. Claudio Ghirardi,
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akitoa pongezi kwa Bw. Ben Usage Asubisye baada ya kumpandisha cheo kuwa kamishna kamili kutoka Kaimu Kamishna wa Forodha na Bidhaa za Ndani katika Mamlaka ya Mapato (TRA) alipotembelea eneo lenye matanki ya kuhifadhia mafuta ya kula baada ya kushushwa melini alipofanya safari ya ghafla kukagua uingizwaji na ugawaji wa ulipiaji wa ushuru bidhaa hiyo kwenye bandari ya Dar es salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akiondoka eneo lenye matanki ya kuhifadhia mafuta ya kula baada ya kushushwa melini alipofanya safari ya ghafla kukagua uingizwaji na ugawaji wa ulipiaji wa ushuru bidhaa hiyo kwenye bandari ya Dar es salaam
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akisalimiana na wananchi eneo lenye matanki ya kuhifadhia mafuta ya kula baada ya kushushwa melini alipofanya safari ya ghafla kukagua uingizwaji na ugawaji wa ulipiaji wa ushuru bidhaa hiyo kwenye bandari ya Dar es salaam
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akiondoka eneo lenye matanki ya kuhifadhia mafuta ya kula baada ya kushushwa melini alipofanya safari ya ghafla kukagua uingizwaji na ugawaji wa ulipiaji wa ushuru bidhaa hiyo kwenye bandari ya Dar es salaam. Hapa akiagana na Katibu Mkuu Wizara ya Viwanda na Biashara Profesa Olesante ole Gabriel na Mwenyekiti wa Kamati ya Rais ya Kuchunguza mafuta ya Kula na Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji Profesa Joseph R. Buchweishaija.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akiongea na wananchi nje ya eneo lenye matanki ya kuhifadhia mafuta ya kula baada ya kushushwa melini alipofanya safari ya ghafla kukagua uingizwaji na ugawaji wa ulipiaji wa ushuru bidhaa hiyo kwenye bandari ya Dar es salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akiongea na wananchi nje ya eneo lenye matanki ya kuhifadhia mafuta ya kula baada ya kushushwa melini alipofanya safari ya ghafla kukagua uingizwaji na ugawaji wa ulipiaji wa ushuru bidhaa hiyo kwenye bandari ya Dar es salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akiongea na wananchi nje ya eneo lenye matanki ya kuhifadhia mafuta ya kula baada ya kushushwa melini alipofanya safari ya ghafla kukagua uingizwaji na ugawaji wa ulipiaji wa ushuru bidhaa hiyo kwenye bandari ya Dar es salaam. Picha na Ikulu

WAKUU WA MIKOA KANDA YA ZIWA VICTORIA WAKOSOA VIKALI TABIA YA WANASIASA KUIPAKA MATOPE DHAMIRA NJEMA YA SERIKALI KUPAMBANA NA UVUVU HARAMU

$
0
0
Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Luhaga Mpina akihutubia hadhara ya kikosi kazi cha watu 260 alichokiunda kwa ajili ya operesheni Sangara 2018 na Wakuu wa Mikoa mitano inayozunguka Ziwa vicktoria wakati wa mkutano wa kufanya tathimini ya Operesheni hiyo.
Viongozi wakuu wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi waliokaa wakiwa katika picha ya pamoja na makamanda wakuu wa Operesheni Sangara 2018 (waliosimama) wakati wa mkutano wa kufanya tathimini ya Operesheni hiyo. 
Viongozi wakuu wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi waliokaa wakiwa katika picha ya pamoja na sekretarieti ya Operesheni Sangara 2018 (waliosimama) wakati wa mkutano wa kufanya tathimini ya Operesheni hiyo. Picha na John Mapepele
*************************************************
NA JOHN MAPEPELE, MWANZA 
WAKUU wa mikoa inayozunguka Ziwa Victoria wamekosoa vikali tabia ya baadhi ya wanasiasa kuipaka matope dhamira njema ya Serikali ya kupambana na uvuvi haramu ulioshamiri katika ziwa hilo na kutaka viongozi wa aina hiyo kutangaza masilahi yao kwenye eneo la uvuvi kabla ya kuwashambulia viongozi wanaosimamia zoezi hilo kwa misingi ya kisheria. KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA
Wakizungumza kwenye kikao cha tathmini ya operesheni sangara awamu ya pili iliyowahusisha Wakuu wa Mikoa,Wakuu wa Wilaya, Makatibu Tawala wa Mikoa, Wakurugenzi wa Halmashauri za Wilaya, Makamanda wa Polisi wa mikoa na Wakuu wa Idara ya Usalama wa Taifa wa mikoa yote inayozunguka Ziwa Victoria jijini Mwanza jana viongozi hao wametaka hatua zaidi zichukuliwe ili kunusuru rasilimali hizo muhimu kwa maendeleo ya Taifa. 
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Antony Mtaka alielezea kuchukizwa na tabia inayoanza kuota mizizi ya baadhi ya viongozi wa kisiasa kuipaka matope dhamira nzuri ya Serikali ya kukabiliana na uvuvi haramu na kutaka viongozi wa aina hiyo watangaze masilahi yao kabla ya kuanza kuwashambulia viongozi wanaosimamia operesheni hiyo inayotekelezwa kwa mujibu wa sheria . 
“Viongozi wanaopinga operesheni ya kupambana na uvuvi haramu ni muhimu watangaze kwanza masilahi yao kuhusu eneo la uvuvi ili wasiendelee kuchafua taswira za viongozi wanaosimamia wizara hii”alisema Mtaka. 
Naye Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, John Mongela alisema kumekuwepo na dhana zinazojengeka kwamba viongozi wa mikoa inayozunguka Ziwa Victoria hawaungi mkono mapambano ya kukabiliana na uvuvi haramu operesheni jambo ambalo alisema ni upotoshaji mkubwa na kwamba Serikali ya mkoa iko mstari wa mbele na kuwabana watendaji wa ngazi zote watakaobanika kufadhili uvuvi haramu. 
Alisema ni muhimu operesheni hiyo iwe endelevu na kubainisha kuwa suala la uvuvi haramu haliwezi kumalizika kama hakuna dhamira ya dhati miongoni mwa wasimamizi wa sheria na kwamba uongozi wa mkoa huo hautakubali kuendelea kuwa na watumishi wazembe wataoshindwa kusimamia suala hilo. 
Kwa upande wake Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Luhaga Mpina alitangaza kuanza kwa awamu ya tatu ya Operesheni Sangara yenye lengo la kupambana na uvuvi haramu katika Ziwa Victoria sambamba na kutangaza operesheni katika maziwa yote na kuagiza viongozi wakuu wa mikoa na wilaya kuwachukulia hatua kali viongozi wa chini wanaobanika kujihusisha na kufadhili uvuvi haramu. 
Pia alitangaza kuunda kanda mpya ya udhibiti na usimamizi rasilimali za uvuvi katika wilaya za Ukerewe na Sengerema huku akiunda ofisi mpya ya Kanda jijini Mwanza itakayokuwa inaratibu shughuli zote katika kanda hizo saba ili kuongeza usimamizi madhubuti wa rasilimali hizo. 
Aidha Mpina aliongeza kuwa katika awamu ya tatu ya operesheni hiyo itahusisha pia Mahakama zinazotembea ili kuweza kutoa hukumu huko huko ziwani hali itayowezesha kuondokana kabisa na uvuvi haramu. 
Aidha aliwataka watu wote wanaopinga operesheni ya uvuvi haramu wasome takwimu ili kujua ukubwa wa tatizo katika Ziwa Victoria ambapo jumla ya watuhumiwa 3,284 wamekamatwa kujihusisha na uvuvi haramu huku samaki wasioruhusiwa kilo 326,751 , mabondo kilo 5,142 zilikamatwa zikitoroshwa kwenda nje ya nchi na nyavu haramu 566,497 nazo zilikamatwa na kuteketezwa. Pia magari 257, mitumbwi 1278 , pikipiki 269 na injini za mitumbwi 564 vilikamatwa vikihusishwa na makosa ya uvuvi haramu. 
Alisema katika baadhi ya maeneo ya Bushengere wilayani Ukerewe wazazi wamewaonya watoto wao kutotumika na mafisadi kwenye uvuvi haramu kwani wakikamatwa wao ndio wanaopata tabu na kutelekezwa ambapo wameweka azimio la kukataa kutumika tena kwenye jambo hilo. 
Alisema kutokana na operesheni hizo zinazoendelea za kupambana na uvuvi haramu hadi kufikia mwezi Disemba mwaka huu watu wote wanaopinga na hata kuwaombea mabaya viongozi wa operesheni watapata aibu kubwa kwani idadi ya samaki itaongezeka huku akitoa wito kwa viongozi wa ngazi zote wenye mapenzi mema na nchi kuunga mkono vita hiyo kwa manufaa ya Taifa. 
Katibu Mkuu Uvuvi, Dk. Yohana Budeba alisema wizara hiyo imejipanga kikamilifu kuhakikisha sekta ya uvuvi inatoa mchango mkubwa katika pato la Taifa na kwamba operesheni hiyo itaendelea hadi pale uvuvi haramu utakapokoma. 
Mkuu wa Wilaya ya Busega, Tano Mwera alisema wamekuwa wakipokea malalamiko mengi kuhusu operesheni hiyo lakini kila walipofuatilia kupata ushahidi wa malalamiko hayo waliukosa jambo ambalo wamebaini kuwa ni njama za makusudi za kutaka kuhujumu nia njema ya Serikali ya kupambana na kutokomeza uvuvi haramu. 
Kamanda Mkuu wa operesheni hiyo kutoka Ofisi ya Rais (TAMISEMI), Hassan Shelukindo alisema katika operesheni hiyo jumla ya watuhumiwa 22 wakiwemo wenyeviti wa vijiji na vitongoji na viongozi wa BMU wamefungwa jela huku wengine 17 mashauri yao yakiwa yanaendelea Mahakamani kwa makosa ya kujihusisha na uvuvi haramu. 
Shelukindo alisema pia watumishi 6 walikuwa kwenye operesheni hiyo waliondolewa kwa makosa mbalimbali ikiwemo ukiukwaji wa maadili ya kazi ambapo watumishi hao watachukuliwa hatua za kinidhamu na taasisi zao huku jumla ya sh. bilioni 7.5 zikikusanywa kutokana na faini pamoja mauzo ya mabondo,samaki na kayabo.

KAMERA YA MAFOTO BLOG MITAANI LEO

$
0
0
Wanafunzi wa Shule ya Msingi Miembeni, wakitoka shule huku wakiwa wamebeba miwa, kama walivyonaswa na Kamera ya Mafoto Blog Vingunguti, Dar es Salaam.

KAMERA YA MAFOTO BLOG MITAANI LEO

$
0
0
Mjasiriamali akichoma nyama kuwasubiri wateja wake kama alivyonaswa na kamera ya Mafoto Blog nje ya Soko la Machinjio la Vingunguti Dar es Salaam

YANGA YASHINDWA KUTUMIA NAFASI UWANJA WA NYUMBANI YASULUHU 0-0

$
0
0
 Mshambuliaji wa Yanga, Yusuph Mhilu (kushoto) akiwania mpira na beki wa Rayon Sports ya Rwanda, Mutsinzi Ange, wakati wa mchezo wa hatua ya makundi kombe la Shirikisho wa Kundi D, uliochezwa kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam. Katika mchezo huo timu hizo zilitosa suluhu 0-0 na kuifanya Yanga kuendelea kuburuza mkia katika kundi hilo ikiwa na pointi 1 huku Rayon wakijiongezea pointi 1 na kufikisha pointi 2.
***************************************
Na Ripota wa Mafoto Blog, Dar.
Wawakilishi pekee wa Tanzania katika Kombe la Shirikisho Barani Afrika hatua ya makundi Dar Young Africans, wameshindwa kuutumia vyema uwanja wa nyumbani dhidi ya Rayon Sports ya Rwanda baada ya kulazimishwa suluhu ya 0-0.
Yanga waliokuwa dimba la nyumbani Uwanja wa Taifa walikubali matokeo hayo baada ya kushindwa kupata goli la ushindi na wazi kupitia kwa mshambuliaji wake Obrey Chirwa aliyebaki na nyavu na kugongesha mwamba wa juu katika kipindi cha pili.
Mchezo huo ulioanza majira ya saa 1 usiku Yanga waliweza kucheza vizuri katika kipindi cha kwanza wakionekana kutawala sehemu ya kiungo kupitia na Thaban Kamusoko na Pius Buswita.
Akizungumza na waandishi wa habari baada ya mchezo huo, Kocha msaidizi wa Yanga Noel Mwandila amesema kuwa hajaridhishwa na matokeo ya leo dhidi ya Rayon Sports kwani walihitaji ushindi ili kuweza kujiweka katika nafasi nzuri ya kufuzu kwenda hatua inayofuata.
"Sijaridhishwa na matokeo ya leo, katika mchezo huu tulihitaji ushindi ili kuweza kujiweka kwenye nafasi nzuri ya kwenda hatua inayofuata ila wachezaji walikosa umakini na kushindwa kutumia nafasi walizozopata,"amesema Mwandila.
Aidha Mwandila amesema kwa sasa mashindano hayo yanasimama kwa muda mpaka mwezi wa saba ambapo wao sasa wanatumia muda huo kwa ajili ya kukiunda kikosi na kukifanya marekebisho katika nafasi zinazohitajika ili waweze kufanya vizuri kwenye michezo inayofuata.
Baada ya mechi hii Yanga wanakuwa na alama 1 baada ya mchezo wa kwanza kufungwa huku Rayon wakiwa na alama 2.
 Mwashiuya akijikunja kupiga shuti
 Nyota wa mchezo Hassan Kessy akiambaa na mpira

TRA YAKAMATA BIDHAA MBALIMBALI KUPITIA NJIA ZA MAGENDO ZIKIWA NA THAMANI YA ZAIDI YA SHILINGI MILIONI 20

$
0
0
Na Veronica Kazimoto, Arusha
Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), imekamata malori mawili yenye bidhaa mbalimbali eneo la Loliondo Wilaya ya Ngorongoro mkoani Arusha kupitia njia ya magendo yakitokea nchini Kenya zenye thamani ya zaidi ya shilingi milioni 20.
Akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Arusha, Kamishna Mkuu wa TRA Bw. Charles Kichere amesema kuwa, malori hayo yenye namba T 985 AJP na T 840 ABF yalikamatwa usiku wa tarehe 10 Mei, 2018 na kusisitiza kuwa wafanyabiashara wenye bidhaa hizo wamevunja sheria kwa kuwa hawakulipa kodi stahiki kama inavyotakiwa.
Kichere amefafanua kuwa, wafanyabiashara wenye bidhaa hizi zilizokamatwa, wamevunja kifungu cha sheria namba 82 na 200  cha Sheria ya Usimamizi wa Kodi ya Mwaka 2015 na Sheria ya Forodha ya Afrika Mashariki ya Mwaka 2004. Hivyo kwa Sheria hizi, wafanyabiashara hawa wanatakiwa kulipa kodi pamoja na faini ya shilingi milioni 39 na magari yao kutaifishwa.
"Kwa ujumla bidhaa hizi zote zina thamani ya shilingi 20,037,330.15 ambayo kodi ya bidhaa hizi ni shillingi 28,524,758.11 na adhabu au faini ya bidhaa hizi ni shilingi 10,768,665.08. Hivyo jumla ya mapato yanayotakiwa kulipwa Serikalini ni shilingi 39,293,423.19," alieleza Kichere.
Amezitaja bidhaa zilizokamatwa kuwa ni pamoja na mifuko 362 ya sukari yenye uzito wa kilo 50 kila mmoja, maboksi 40 ya mafuta ya kula yanayoitwa Karibu, maboksi matatu ya mafuta ya kula yanayoitwa Daria, magaloni 100 ya mafuta ya kula yanayoitwa Nyata na maboksi matatu ya viungo vya mboga  
Kufuatia tukio hilo, Kamishna Mkuu Kichere amewakumbusha wafanyabiashara wote kuzingatia taratibu za uingizaji bidhaa nchini ili kuepuka hasara kwenye biashara zao na kuongeza kuwa, TRA haitavumilia ukiukwaji wowote utakaofanywa na wafanyabiashara kwa kutozingatia sheria na taratibu hizo.

KAMPUNI YA UCHIMBAJI MADINI YA TANZANITE ONE YAKUBALI KUILIPA SERIKALI FIDIA MARA BAADA YA KUFIKIA MAKUBALIANO

$
0
0
Kiongozi wa Kamati ya Majadiliano kwa upande wa Serikali, Waziri wa Katiba na Sheria Profesa Palamagamba Kabudi akitia saini pamoja na Mkurugenzi wa Tanzanite One Faisal Juma mara baada ya kufikia makubaliano na Kampuni hiyo ya Uchimbaji wa Madini ambayo imekubali kulipa fidia kwa Serikali pamoja na mambo mengine ya Kimkataba. 
Kiongozi wa Kamati ya Majadiliano kwa upande wa Serikali Waziri wa Katiba na Sheria Profesa Palamagamba Kabudi akibadilishana hati za Makubaliano na Mkurugenzi wa Tanzanite One Faisal Juma mara baada ya Kampuni hiyo ya Uchimbaji wa Madini kukubali kulipa fidia kwa Serikali. 
Kiongozi wa Kamati ya Majadiliano kwa upande wa Serikali Waziri wa Katiba na Sheria Profesa Palamagamba Kabudi akiwa na watendaji wa Kampuni ya Uchimbaji madini ya Tanzanite One wakati akielekea kusaini hati za makubaliano baina ya kampuni hiyo na Serikali.
Kiongozi wa Kamati ya Majadiliano kwa upande wa Serikali Waziri wa Katiba na Sheria Profesa Palamagamba Kabudi akizungumza mara baada ya kuhitimisha mazungumzo na kusaini hati ya Makubaliano yatakayoiwezesha Serikali kulipwa fidia na Kampuni ya uchimbaji madini ya Tanzaniate.
Kiongozi wa Kamati ya Majadiliano kwa upande Kampuni ya Tanzanite One Faisal Juma akizungumza mara baada ya kuhitimisha mazungumzo na kusaini hati ya Makubaliano yatakayoiwezesha Serikali kulipwa fidia na Kampuni ya uchimbaji madini ya Tanzaniate.
Kiongozi wa Kamati ya Majadiliano kwa upande wa Serikali Waziri wa Katiba na Sheria Profesa Palamagamba Kabudi akiagana na Mkurugenzi wa Tanzanite One Faisal Juma mara baada ya Kampuni hiyo ya Uchimbaji wa Madini kukubali kulipa fidia kwa Serikali pamoja na mambo mengine ya Kimkataba kama walivyokubaliana. PICHA NA IKULU
********************************************
Kampuni ya uchimbaji madini ya Tanzanite One imekubali kuilipa Serikali fidia pamoja na kodi watakayokubaliana kutokana na dosari zilizokuwepo hapo awali.
Makubaliano hayo yametiwa saini Jijini Dar es Salaam na Mwenyekiti wa Kamati iliyoundwa na Mhe. Rais Dkt. John Pombe Magufuli Profesa Palamagamba Kabuni na Mkurugenzi wa Tanzanite One Bw.Faisal Juma.
Akizungumza mara baada ya kutia saini makubaliano hayo, Mwenyekiti wa kamati ya majadiliano kwa upande wa Serikali, Prof. Palamagamba Kabudi amesema Tanzanite One imekubali kulipa fidia Serikali kutokana na mambo iliyofanya ambayo yalikuwa kinyume na utaratibu ulioleta hasara kwa Serikali.
Amesema fidia hiyo inatakiwa kulipwa kwa awamu ambapo awamu ya kwanza italipwa ndani ya wiki mbili kuanzia leo na haitahusisha Kodi. Pia Kampuni hiyo Tanzanite One italazimika kulipa kodi kama kawaida inazodaiwa na Serikali na tozo nyingine zote zinazodaiwa na Serikali.
Pia Serikali imekubaliana na Kampuni ya Tanzanite One kuwa itafuata masharti yote ya sheria ya madini ya mwaka 2010 ambayo inaeleza kuwa ni Watanzania tu ndio wanaoruhusiwa kuchimba madini ya Vito na pale ambapo watanzania hawana uwezo huo ndipo wanapoweza kuingia ubia na wageni.
Aidha Prof. Kabudi amesema kuhusu wachimbaji wadogo wadogo wa Tanzanite katika eneo la Mirerani utaratibu mpya unawekwa lengo kubwa ikiwa ni kutekeleza sheria ya madini ya mwaka 2010 ambayo inalenga madini ya vito kuwa mikononi mwa Watanzania.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa Kampuni ya Tanzanite One Faisal Juma amemshukuru Mhe. Rais Magufuli kwa kuunda kamati hiyo ya kizalendo katika kufuatilia rasilimali za madini nchini ambapo wameweza kujadiliana na kufikia muafaka wa kulipa fidia ikiwa ni mbali na malipo yote yaliyotakiwa kulipwa serikali ikiwemo kodi.
Amesema Tanzanite One itahakikisha inafuata taratibu zote za Sheria ya Madini ya mwaka 2010 kwa lengo la kuhakikisha rasilimali ya madini inawanufaisha Watanzania na kwamba uvunjifu wa sheria uliofanywa na kampuni hiyo hautajirudia tena.
“Sisi kama Tanzanite One tunaihakikishia Serikali kuwa uaminifu uliotuonyesha na sisi pia kama Kampuni tutahakikisha tunakuwa waaminifu na kuwa zao hili linanufaisha taifa kutokana na imani aliyotuonyesha Mhe. Rais kama wananchi wake kutupa nafasi na fursa ya kusikilizwa ili kurekebisha makosa tuliyoyatenda” amesema Faisal.
Faisal amesema Tanzanite One itahakikisha haitafanya makosa iliyofanya mara ya kwanza na hivyo kuwa mfano wa kampuni nyingine za madini kuhakikisha rasilimali za madini zinawanufaisha Watanzania.
Jaffar Haniu
Naibu Mkurugenzi Mawasiliano ya Rais, IKULU.
Dar es Salaam
16 Mei, 2018

RAIS DKT MAGUFULI AZINDUA KITUO CHA UWEKEZAJI CHA JWTZ NA VIWANDA VYA MAJI NA USHONAJI

$
0
0
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu Dkt. John Pombe Magufuli akijadiliana jambo na Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa Mhe. Dkt Hussein Mwinyi, Mkuu wa Majeshi Jenerali Venance Mabeyo, Mkuu wa JKT Meja Jenerali Martin Busungu alipowasili kuzindua kituo cha uwekezaji cha JWTZ kupitia SUMA-JKT kilichopo Mgulani jijini Dar es salaam leo Mei 17, 2018. Kituo kicho kina viwanda vya ushonaji na maji ya kunywa pamoja na Shule ya Sekondari ya Jitegemee na Ukumbi wa kisasa wa Mikutano.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa Mhe. Dkt Hussein Mwinyi, Mkuu wa Majeshi Jenerali Venance Mabeyo, Mkuu wa JKT Meja Jenerali Martin Busungu wakifunua pazia kuashiria kuzinduliwa rasmi kwa kituo cha uwekezaji cha JWTZ kupitia SUMA-JKT kilichopo Mgulani jijini Dar es salaam leo Mei 17, 2018. Kituo kicho kina viwanda vya ushonaji na maji ya kunywa pamoja na Shule ya Sekondari ya Jitegemee na Ukumbi wa kisasa wa Mikutano.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu Dkt. John Pombe Magufuli akitembela kwainda cha ushonaji nguo baada ya kuzindua rasmi kituo cha uwekezaji cha JWTZ kupitia SUMA-JKT kilichopo Mgulani jijini Dar es salaam leo Mei 17, 2018. Kituo kicho kina viwanda vya ushonaji na maji ya kunywa pamoja na Shule ya Sekondari ya Jitegemee na Ukumbi wa kisasa wa Mikutano.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu Dkt. John Pombe Magufuli akifurahia sare za kijeshi zinazoshinwa na kiwanda cha ushonaji nguo baada ya kuzindua rasmi kituo cha uwekezaji cha JWTZ kupitia SUMA-JKT kilichopo Mgulani jijini Dar es salaam leo Mei 17, 2018. Kituo kicho kina viwanda vya ushonaji na maji ya kunywa pamoja na Shule ya Sekondari ya Jitegemee na Ukumbi wa kisasa wa Mikutano.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu Dkt. John Pombe Magufuli akikagua kiwanda cha kutengeneza maji ya kunywa ya UHURU PEAK baada ya kuzindua rasmi kituo cha uwekezaji cha JWTZ kupitia SUMA-JKT kilichopo Mgulani jijini Dar es salaam leo Mei 17, 2018. Kituo kicho kina viwanda vya ushonaji na maji ya kunywa pamoja na Shule ya Sekondari ya Jitegemee na Ukumbi wa kisasa wa Mikutano.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu Dkt. John Pombe Magufuli akinywa maji yaliyotengenezwa na kiwanda cha kutengeneza maji ya kunywa ya UHURU PEAK baada ya kuzindua rasmi kituo cha uwekezaji cha JWTZ kupitia SUMA-JKT kilichopo Mgulani jijini Dar es salaam leo Mei 17, 2018. Kituo kicho kina viwanda vya ushonaji na maji ya kunywa pamoja na Shule ya Sekondari ya Jitegemee na Ukumbi wa kisasa wa Mikutano. 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu Dkt. John Pombe Magufuli akimpa maji ya UHURU PEAK Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa Mhe. Dkt Hussein Mwinyi,wakati wa sherehe za kuzindua kituo cha uwekezaji cha JWTZ kupitia SUMA-JKT kilichopo Mgulani jijini Dar es salaam leo Mei 17, 2018. Kituo kicho kina viwanda vya ushonaji na kutengeneza maji ya kunywa pamoja na Shule ya Sekondari ya Jitegemee na Ukumbi wa kisasa wa Mikutano. 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu Dkt. John Pombe Magufuli, Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa Mhe. Dkt Hussein Mwinyi, Mkuu wa Majeshi Jenerali Venance Mabeyo, Mkuu wa JKT Meja Jenerali Martin Busungu na Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam wakipata picha ya kumbukumbu na watendaji wa kituo cha uwekezaji cha JWTZ kupitia SUMA-JKT kilichopo Mgulani jijini Dar es salaam leo Mei 17, 2018. Kituo kicho kina viwanda vya ushonaji na maji ya kunywa pamoja na Shule ya Sekondari ya Jitegemee na Ukumbi wa kisasa wa Mikutano.
Picha na IKULU

PENTECOSTAL REVIVAL WEEKEND WITH REV. DR HURUMA NKONE MAY 18-20, 2018 MBEZI BEACH, DAR

NAIBU WAZIRI WA AFYA AZINDUA PROGRAMU YA 'UNI LIFE CAMPUS' MUHAS

$
0
0
Mgeni Rasmi, Mheshimiwa Dkt. Faustine Ndugulile, Naibu Waziri Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto akitoa hotuba wakati wa uzinduzi wa Uni Life Campus Program kwenye Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili, MUHAS. 
Wafanyakazi na wanafunzi wa MUHAS wakifuatilia hotuba za uzinduzi wa Uni Life Campus Program kwenye Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili, MUHAS 
Kaimu Makamu Mkuu wa Chuo, Prof. Appolinary Kamuhabwa akizungumza katika sherehe za uzinduzi wa Uni Life Campus Program kwenye Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili, MUHAS. 
Mbunge anaewakilisha Vyuo Vikuu katika Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambaye pia ni Mwanzilishi wa Uni Life Campus Program, Mheshimiwa Esther Mmasi akielezea maono ya program hii wakati wa uzinduzi wa Uni Life Campus Program kwenye Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili, MUHAS
Dkt. Faustine Ndugulile, Naibu Waziri Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto akitoa ufafanuzi wa maswali yaliyoulizwa na wanafunzi wakati uzinduzi wa Uni Life Campus Program kwenye Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili, MUHAS. 
Mgeni Rasmi, Mheshimiwa Dkt. Faustine Ndugulile, Naibu Waziri Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto (ameketi katikati), Mbunge anaewakilisha Vyuo Vikuu katika Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mwanzilishi wa Uni Life Campus Program, Mheshimiwa Esther Mmasi (wa pili kushoto), Kaimu Makamu Mkuu wa Chuo, Prof. Appolinary Kamuhabwa (wa pili kulia), msemaji wa jeshi la polisi (kulia) na mwakilishi wa kutoka bodi ya mikopo (kushoto), wakiwa katika picha ya pamoja na viongozi wa serikali ya wanafunzi wa MUHAS 
Naibu Waziri Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. Faustine Ndugulile akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kuzindua Uni Life Campus Program kwenye Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili, MUHAS 
********************************************
Na Mwandishi Wetu. 
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. Faustine Ndugulile amezindua programu ya Uni Life Campus kwa wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi, MUHAS. 
Akizungumza katika uzinduzi wa programu hiyo, Dkt. Ndugulile amewahimiza wanafunzi wa MUHAS kuzingatia masomo pamoja na kupenda kujihusisha na mambo mengine kwenye jamii. 
Amesisitiza kuwa kama wanafunzi wa fani za afya wanao uwezo wa kujihusisha na programu mbalimbali zinazofikia jamii zenye uhitaji na kushiriki katika kutoa huduma za afya. 
Akitoa mifano ya maisha yake kama mwanafunzi wa miaka ya nyuma wa Chuo hiki, Dkt. Ndugulile amesema katika maisha ni muhimu sana kuwa na malengo pamoja na mipango ya kuweza kufikia malengo hayo.
 Amesema nafasi mbalimbali zipo ila zinahitaji kujibidiisha hasa kwenye vikundi mbalimbali vya kitaaluma ili uweze kuzitambua nafasi hizo na kuziomba. 
Naibu Waziri pia amewaasa wanafunzi kuwa makina na jinsi wanavyotumia mitandao ya jamii maana ina uwezo mkubwa wa kuwajenga kama wakitumia vizuri na kuwabomoa endapo ikitumika vibaya.
 "Watu wa afya ni kioo cha jamii hivyo basi ni muhimu kuzingatia maadili ya sekta hii na kuhakikisha tabia zenu zinaendana na mienendo yenu", aliongeza. Akielezea maono ya programu hii, Mwanzilishi wa Uni Life Campus Program ambaye pia ni Mbunge anaewakilisha Vyuo Vikuu katika Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Bi Esther Mmasi amesema mojawapo ya malengo la programu hii ni kuongeza kiwango cha kujitambua kwa wanafunzi ili kupunguza changamoto wanazokabiliana nazo wakiwa vyuoni. 
Amesema programu hii pia imelenga kuongeza uelewa wa wanafunzi wa vyuo wa namna nzuri wa kutumia technolojia ya mawasiliano na pia kusisitizia matumizi mazuri ya mitandao ya kijamii. 
Naye Kaimu Makamu Mkuu wa Chuo, Prof. Appolinary Kamuhabwa amesema Chuo kinatambua umuhimu wa wanafunzi kupata maarifa yatakayo wawezesha kujitambua na kutambua nafasi walizo nazo ili waweze kuzitumia kikamilifu. 
Kutokana na hilo, Prof. Kamuhabwa alisema Chuo kinatoa kipaumbele cha kutosha katika kuhakikisha wanafunzi hasa wa jinsia ya kike ambao mara nyingi ndio wahanga wakubwa wa changamoto mbalimbali za kimfumo, wanapatiwa semina za kuwajengea ujasiri na kuwa na mtazamo chanya katika maisha.
 "Lengo kuu la kuwa na semina mbalimbali ni katika kuhakikisha wanafunzi wanafanya vizuri katika masomo yao bila kuwa na vizuizi vya masuala mengine ya kijamii ambayo yanaweza kuwakwamisha" aliongeza.

JUMUIYA YA KIHINDU TANZANIA (BAPS) YATOA SH MILIONI 68 KWA AJILI YA KULIPIA MATIBABU YA UPASUAJI WA MOYOKWA WATOTO WENYE MATATIZO YA MOYO NCHINI

$
0
0
 Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Prof. Mohamed Janabi akiwa katika picha ya pamoja na kaimu kiongozi wa Jumuia ya Kihindu  Duniani (BAPS) Mtukufu Bhaktipriyadas  Swami  pamoja na viongozi wengine wa jumuia hiyo wa hapa nchini wakati kiongozi huyo alipotembelea Tanzania  hivi karibuni. BAPS imetoa kiasi cha shilingi milioni 68 fedha ambazo zitatumika kwa ajili ya kulipia gharama za upasuaji wa moyo kwa watoto 30. 
Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Prof. Mohamed Janabi akisalimiana na  kaimu kiongozi wa Jumuia ya Kihindu  Duniani (BAPS) Mtukufu Bhaktipriyadas  Swami  alipotembelea Tanzania  hivi karibuni. BAPS imetoa kiasi cha shilingi milioni 68 fedha ambazo zitatumika kwaajili ya kulipia gharama za  upasuaji wa moyo kwa watoto 30.
Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Prof. Mohamed Janabi na  Viongozi wa Jumuia ya Kihindu  (BAPS) wakijadili jambo wakati  Kaimu kiongozi wa Dunia wa Jumuia hiyo Mtukufu Bhaktipriyadas  Swami  alipotembelea Tanzania  hivi karibuni. BAPS imetoa kiasi cha shilingi milioni 68 fedha ambazo zitatumika kwaajili ya kulipia gharama za  upasuaji wa moyo kwa watoto 30.
Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Prof. Mohamed Janabi akiwa katika picha ya pamoja na  kaimu kiongozi wa Jumuia ya Kihindu  Duniani (BAPS) Mtukufu Bhaktipriyadas  Swami  alipotembelea Tanzania  hivi karibuni. Tangu mwaka 2016 BAPS wamekuwa wakitoa fedha kwa ajili ya upasuaji wa moyo kwa watoto ambapo hadi sasa jumla ya watoto 290 wameshafanyiwa upasuaji.
Kaimu kiongozi wa Jumuia ya Kihindu  Duniani (BAPS) Mtukufu Bhaktipriyadas  Swami  akimpa zawadi  Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Prof. Mohamed Janabi wakati kiongozi huyo alipotembelea nchini  hivi karibuni. Tangu mwaka 2016 BAPS wamekuwa wakitoa fedha kwa ajili ya upasuaji wa moyo kwa watoto ambapo hadi sasa jumla ya watoto 290 wameshafanyiwa upasuaji na hali zao zinaendelea vizuri. Picha na JKCI
***************************************************
Na Mwandishi  Maalum
Jumuia ya Kihindu Tanzania (BAPS) imetoa kiasi cha shilingi milioni 68 fedha ambazo ziatumika kwaajili ya kulipia gharama za matibabu ya upasuaji wa moyo kwa watoto wenye matatizo hayo hapa nchini.
Fedha hizo ambazo zitatumika kwaajili ya upasuaji wa moyo kwa watoto 30 wanaotibiwa katika Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) zimetolewa hivi karibuni na kaimu kiongozi wa Dunia wa jumuia hiyo. 
Akizungumza kuhusu msaada huo Kaimu kiongozi wa Jumuia ya Kihindu Duniani Mtukutu Bhaktipriyadas Swami alisema wametoa fedha hizo kwa ajili ya kusaidia jamii yenye uhitaji hasa watoto wanaosumbuliwa na maradhi ya moyo. 
Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete Prof. Mohamed Janabi alishukuru kwa msaada huo na kusema kuwa fedha zilizotolewa zitatumika kwa walengwa ambao ni watoto wanaotakiwa kufanyiwa upasuaji wa moyo. 
Prof. Janabi alisema kuwa Taasisi hiyo imekuwa na uhusiano mzuri na Jumuia ya BAPS ambao kila mwaka wamekuwa wakichangia fedha kwaajili ya matibabu ya moyo kwa watoto ambao baada ya matibabu wamepona na wengine wamerudi shuleni kuendelea na masomo yao. 
Tangu mwaka 2016 BAPS wamekuwa wakitoa fedha kwa ajili ya upasuaji wa moyo kwa watoto ambapo hadi sasa jumla ya watoto 290 wameshafanyiwa upasuaji.

KATIBU MKUU SIHABA NKINGA AKUTANA NA KIKUNDI CHA KITAIFA CHA MASUALA YA JINSIA KATIKA SERA, MIPANGO, MIKAKATI, PROGRAMU NA BAJETI.

$
0
0

 Mshauri Mwandamizi wa Masuala ya Kisera UN Women nchini Bi. Usu Mallya akielezea Mipango ya masuala mbalimbali ya kuwawezesha wanawake kiuchumi katika kikao baina ya Katibu Mkuu Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Bi. Sihaba Nkinga na kikundi cha uingizaji wa masuala ya jinsia katika Sera, Mipango, Mikakati, Programu na Bajeti za kitaifa jijini Dar es Salaam kujadili utekelezaji wa malengo endelevu ya Umoja wa Mataifa katika sekta mbalimbali. Kulia ni Katibu Mkuu Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Bi. Sihaba Nkinga.
 Mkurugenzi Msaidizi  Idara ya Maendeleo ya Jinsia  Bi. Mwajuma Magwiza (kulia) akielezea jinsi maadhimisho ya Siku ya Kimataifa ya Wanawake kwa mwaka 2018 yalivyofanyika na kuwashuruku wadau kwa kuwezesha kufanikisha maadhimisho hayo katika kikao kilichowakutanisha Katibu Mkuu Maendeleo ya Jamii, Jinsia,  Wazee na Watoto Bi. Sihaba Nkinga alipokutana na kikundi cha uingizaji wa masuala ya jinsia katika Sera, Mipango, Mikakati, Programu na Bajeti za kitaifa jijini Dar es Salaam.
 Mwezeshaji wa Masuala ya Jinsia Dkt. Linda Mhando(kulia) akielezea masuala mbalimbali aliyoyapata katika utafiti alioufanya kuhusu utekelezaji wa Sera ya Maendeleo ya Jinsia ya Mwaka (2000) na ushauri wake kuhusu maboresho ya Sera hiyo wakati wa kikao kati ya Katibu Mkuu Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Bi. Sihaba Nkinga na kikundi cha uingizaji wa masuala ya jinsia katika Sera, Mipango, Mikakati, Programu na Bajeti za kitaifa jijini Dar es Salaam.
Baadhi wajumbe wa kikundi cha uingizaji wa masuala ya jinsia katika Sera, Mipango, Mikakati, Programu na Bajeti za kitaifa wakifuatilia mada mbalimbali zilizokuwa zikiwasiliwa katika kikao kati yao na Katibu Mkuu Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Bi. Sihaba Nkinga Jijini Dar es Salaam. Picha na Kitengo cha Mawasiliano WAMJW

SERIKALI YAANDAA MWONGOZO WA KITAIFA WA MAFUNZO KWA VITENDO KWA WAHITIMU WA VYUO

$
0
0
Na Lilian Lundo - MAELEZO, Dodoma.
Serikali imeandaa mwongozo wa Kitaifa wa mafunzo kwa vitendo kwa wahitimu wa vyuo ili kuondoa pengo la ujuzi linalohitajika katika soko la ajira hapa nchini.
Hayo yamesemwa leo Bungeni Jijini Dodoma na Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu Sera Bunge Kazi Vijana Ajira na Watu Wenye Ulemavu Mhe. Antony Mavunde alipokuwa akijibu swali la Mbunge wa Viti Maalum Mhe. Zainab Athuman Katimba juu ya Serikali haioni haja ya kutungwa sera ya mafunzo kwa vitendo kazini kwa wahitimu wa Elimu ya Juu na Vyuo vya Ufundi (Internship Policy for Higher Learning Institutions and Technical Colleges Graduates) ili vijana waweze kupata ujuzi utakaoendana na mahitaji ya soko la ajira.
"Katika kuhakikisha pengo la ujuzi (skills gap/skills mismatch) kati ya ujuzi walionao wahitimu na ule unaohitajika katika soko la ajira, ni kweli Serikali imeona kuna haja ya kuwa na miongozo ya kisera ambapo kupitia Ofisi yangu tumeandaa mwongozo wa Kitaifa wa mafunzo kwa vitendo kwa wahitimu (National Internship Guideline)," amesema Mhe. Mavunde.
Ameendelea kusema kuwa mwongozo huo ulizinduliwa rasmi Septemba, 2017 na kuanza kutumika rasmi ambapo katika mwaka wa fedha 2017/2018 zaidi ya nafasi 750 zimetolewa na waajiri mbalimbali kuwezesha wahitimu kufanya mafunzo.
Aidha amesema, Serikali inafanya marekebisho ya Sera ya Taifa ya Ajira ya mwaka 2008 ili kuendana na mahitaji ya sasa ambapo sera mpya pamoja na mkakati wa utekelezaji wake iko katika hatua za mwisho na inatarajiwa kukamilika ifikapo Juni mwaka huu.
"Miongoni mwa matamko mahususi ya sera hii ni pamoja na kusisitiza kuwepo kwa mafunzo kwa vitendo kazini kwa wahitimu wa vyuo. Baada ya kupitishwa sera hii, suala la mafunzo ya vitendo kazini kwa wahitimu litawekwa katika Sheria ya Ajira na Mahusiano Kazini Na. 6 ya mwaka 2004.
Hata hivyo, Mhe. Mavunde ametoa wito kwa waajiri wote nchini kuendelea kushirikiana na Serikali katika utekelezaji wa programu ya mafunzo kazini kwa wahitimu kwa kutoa fursa kwa vijana wahitimu kujifunza katika maeneo yao ya kazi.

USHAHIDI KESI MATUMIZI MABAYA YA MADARAKA INAYOMKABILI TIDO MHANDO KUSIKILIZWA JUNI 8

$
0
0
USHAHIDI dhidi ya kesi ya matumizi mabaya ya madaraka inayomkabili Mkurugenzi Mkuu wa zamani wa Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC), Tido Mhando utaendelea kusikikizwa Juni 8,mwaka huu.
Kesi hiyo ambayo ilikuwa iendelee kusikilizwa kwa shahidi wa nne wa upande wa mashtaka kutoa ushahidi wao, imeahirishwa sababu shahidi waliyemtarajia kutoa ushahidi Katika kesi hiyo anaudhuru.
Hayo yameelezwa na Wakili wa Takukuru, Leonard Swai, mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu , Huruma Shaidi wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu.
Baada ya kutolewa kwa maelezo hayo, Hakimu Shaidi ameahirisha kesi hiyo hadi Juni 8 mwaka huu ambao mashahidi wa upande wa mashtaka wataendelea kutoa ushahidi.
Katika kesi hiyo tayari mashahidi watatu wamekwishatoa ushahidi wao ambao ni Afisa uchunguzi wa Takukuru, Victor Lesuya, Mwanasheria wa TBC, Gwakisa Mlawa na aliyekuwa Mkurugenzi Mkuu wa TBC, Clement Mshana.
Tido anakabiliwa na mashtaka manne ya kutumia madaraka vibaya na moja la kuisababishia Serikali hasara ya Sh.milioni 887. 
Katika kesi hiyo inadaiwa kuwa Juni 16, 2008, akiwa Dubai, Umoja wa Falme za Kiarabu (UAE), Tido aliyekuwa mkurugenzi wa TBC, kwa makusudi alitumia madaraka yake vibaya kwa kusaini mkataba wa kuendesha na utangazaji wa vipindi vya televisheni kati ya TBC na Channel 2 Group Corporation (BV1) bila ya kupitisha zabuni, kitu ambacho ni kinyume na Sheria ya Manunuzi na kuinufaisha BVl.
Katika shtaka la pili, Tido anadaiwa kutumia vibaya madaraka yake Juni 20, 2008 aliposaini makubaliano kwa utangazaji wa digitali duniani kati ya TBC na BVl.
Katika shtaka la tatu, anadaiwa Agosti 11, 2008 na Septemba 2008 akiwa Dubai, Tido alitumia vibaya madaraka yake kusaini mkataba wa makubaliano kwa ununuzi, usambazaji kufunga vifaa vya usambazaji na mnara wa utangazaji kati ya TBC na BVI na kuifaidisha BVI.
Katika shtaka la nne, anadaiwa kuwa Novemba 16, 2008 akiwa Dubai, Tido alitumia vibaya madaraka yake kusaini mkataba wa makubaliano kwa kuendesha miundombinu ya utangazaji (DTT Broadcast Infrastructure) kati ya TBC na BVI na kuinufaisha BVI.
Katika shtaka la mwisho, anadaiwa kuwa kati ya Juni 16 na Novemba 16, 2008 akiwa UAE, Tido aliisababishia TBCli hasara ya Sh.887,122,219.19.

SETHI AIBUKA, APINGA KUNG'OLEWA IPTL

$
0
0
Na Mwandishi Wetu
Mkurugenzi na Mmilikiwa kampuni ya PAP/IPTL ,Harbinder Sing Sethi Amekanusha taarifa zinazosambzwa mitandao kuwa amefutwa kuwa Mwenyekiti na Mtendaji Mkuu wa kampuni hiyo.
Hayo yameelezwa leo na Mwanasheria wa mmiliki wa Kampuni ya PAP/IPTL, Harbinder Sing Sethi, Hajra Mungula, mara baada ya kupokea taarifa kutoka kwa mteja wake na kusema Sethi bado Mwenyekiti na Mtendaji Mkuu wa kampuni hiyo.
Wakili Mungula amesema kuwa watanzania kupuuza kwa taarifa zilizotolewa awali na watu wanaojiita kuwa Mwenyekiti na Ofisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni hiyo.
Katika taarifa kwa vyombo vya habari iliyotolewa na Wakili Hajra Mungula imesema kuwa yeye kama mwanasheria wa Sethi, amewasiliana na mteja wake, ambaye yuko rumande na kushangazwa na taarifa hizo.
Ilisema hivi karibuni kumeripotiwa taarifa kwenye vyombo vya habari kwamba kampuni inayomilikiwa na Harbinder Sing Sethi imebadilisha uongozi katika ngazi za Mwenyekiti wa bodi ya wakurugenzi na Mkurugenzi mtendaji wake.
"Taarifa iliyosambazwa na anayejiita mwenyekiti wa bodi mpya, Ambroce Brixio imemtaja yeye kuwa na cheo hicho na Joseph Makandege kuwa Mkurugenzi wake ambaye kwa miezi kadhaa sasa hajawahi kuonana nae ikiwemo hata kutofika mahakamani siku ambazo kesi imekuwa ikitajwa" imesema sehemeu ya taarifa hiyo.
Wakili Hajra, aliandika katika taarifa hiyo kuwa taarifa hizo zimemfikia kwa masikitiko makubwa Mwenyekiti halali na mmiliki wa kampuni hii ya kuzalisha umeme ya IPTL ambayo kimsingi inamilikiwa na kampuni anayoimiliki ya Pan Africa Power Solutions(PAP).
Kwa mujibu wa taarifa ya mwanasheria huyo, pamoja na kuagiza wanasheria wake kuchukua hatua za haraka za kisheria mwenyekiti Sethi pia hana taarifa zozote juu ya mabadiliko hayo.
"Mwenyekiti Seth anapenda kuutaarifu umma kupitia sisi kwamba wazipuuze taarifa hizo kwa kuwa hazitokani na mamlaka halali za kisheria za kampuni hiyo," ilisema mwanasheria huyo.
Ilisema pamoja na kwamba Mwenyekiti Sethi bado yuko mahabusu akituhumiwa mashtaka kadhaa ya jinai, hiyo haiondoi ukweli kuwa IPTL ni kampuni binafsi yenye wamiliki halali wenye hisa halali na wala sio NGO ambayo mtu yeyote anaweza kutangaza mapinduzi ya kiuongozi wakati wowote.
"Mwenyekiti anapenda kuwahakikishia watanzania wote kuwa licha ya uwepo wa mashtaka yanayomkabili bado kampuni hiyo ipo chini ya usimamizi salama wa PAP na kwamba madeni yote, madai, mali na stahiki zote zizohusiana na kampuni hiyo zipo katika mikono salama mpaka sasa" ilisema sehemu ya taarifa.
Aidha, ilisema taarifa hiyo, Mwenyekiti anawahakikishia watanzania kuwa ataendelea kutoa ushirikiano mahsusi kuhakikisha nchi inajiepusha na hasara zinazotokana na matendo ya aina ya kina Makandege na wenzake ya kukurupuka bila kufuata sheria na taratibu

DENI LA TAIFA HALIJAONGEZEKA: BENKI KUU

$
0
0

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

DENI LA TAIFA HALIJAONGEZEKA KWA SH. TRILIONI 12
Benki Kuu ya Tanzania (BoT) imeshitushwa na taarifa potofu zilizochapishwa na gazeti la Mwananchi toleo Na. 6499 la tarehe 17 Mei 2018 kuhusu Deni la Taifa na kusema taarifa hizo sio sahihi na zinapaswa kupuuzwa. Katika toleo hilo, gazeti hilo lilidai kwamba kulikuwa na ongezeko la sh. trilioni 12 katika deni la taifa kati ya Desemba 2017 na Machi 2018, takwimu ambazo sio sahihi.
Takwimu sahihi ni kwamba Deni la Serikali pekee liliongezeka kwa sh. trilioni 2 kutoka sh. trilioni 47 hadi sh. trilioni 49. Deni hilo linajumuisha mikopo kutoka nchi wahisani, mashirika ya fedha ya kimataifa pamoja na mabenki ya kibiashara ya kimataifa wakati deni la ndani la Serikali linajumuisha dhamana za Serikali za muda mfupi na hati fungani za Serikali pamoja na madeni mengineyo. 
Aidha, Deni la nje la sekta binafsi kati ya mwezi Desemba 2017 na Machi 2018 liliongezeka kwa sh. trilioni 1.0 tu, kutoka sh. trilioni 9 hadi sh. trilioni 10. Hivyo, Deni la Taifa, ambalo linajumuisha Deni la Serikali la ndani na nje na deni la nje la sekta binafsi, liliongezeka kwa sh. trilioni 3 kutoka sh. trilioni 56 mwezi Desemba 2017 hadi sh. trilioni 59 mwezi Machi 2018.
Ongezeko la Deni la Taifa linatokana na mikopo mipya kwa ajili ya miradi mbalimbali ya maendeleo na malimbikizo ya riba, hasa kutoka nchi za kundi lisilo la wanachama wa Paris, ambazo hazijatoa misamaha ya madeni kulingana na makubaliano.  Pamoja na ongezeko hilo, Deni la Taifa bado ni himilivu. Aidha, kuongezeka kwa Deni la Taifa kunatokana na jitihada za Serikali kujenga mazingira bora zaidi ya kuongeza uzalishaji katika sekta mbalimbali za uchumi ili kufikia azma ya Tanzania ya viwanda na yenye uchumi wa kati ifikapo mwaka 2025.
Badala ya kulinganisha takwimu zinazofanana, gazeti la Mwananchi limelinganisha takwimu za Deni la Serikali la Desemba 2017 na Deni la Taifa la Machi, 2018 ambazo zinajumuisha vitu tofauti.
Hivyo, Benki Kuu ya Tanzania inalitaka gazeti hilo kuchapisha taarifa ya takwimu sahihi kwa uzito ule ule kama lilivyopotosha. Aidha, tunatoa wito kwa vyombo vya habari kuomba ufafanuzi wa masuala yanayohusu taasisi hii ili kuepusha matatizo yanayoweza kujitokeza kwa kuchapisha taarifa zisizo sahihi.
BENKI KUU YA TANZANIA
Idara ya Uhusiano wa Umma na Itifaki
19 Mei 2018

KAMERA YA MAFOTO BLOG MITAANI LEO

$
0
0
 Vijana wachuuzi wa nyama wakiandaa eneo la kuuzia nyama kama walivyonaswa na kamera ya mafoto Blog,nje ya machinjio ya Vingunguti Dar es Salaam. Vijana hawa huuza kila pande moja la nyma kwa Sh. 1500
Viewing all 13053 articles
Browse latest View live


<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>