↧
KAMERA YA MAFOTO BLOG MITAANI LEO
↧
KILELE CHA MAADHIMISHO YA JUMA LA ELIMU KITAIFA WILAYANI MKALAMA, MKOA WA SINGIDA
Mkuu wa Mkoa wa Singida. Dk Rehema Nchimbi akizungumza na wadau wa elimu, walimu pamoja na wanafunzi wakati wa kufunga maadhimisho ya Juma la Elimu kitaifa iliyofanyika katika wilaya ya Mkalama mkoani Singida.
Mwenyekiti Wa Bodi ya Mtandao wa Elimu Tanzania Dk John Kallage akitoa risala ya majumuisho ya uhamasishaji ya Juma la Elimu Kitaifa yaliyofanyika katika wilayani Mkalama mkoani Singida.
Mkuu wa Mkoa wa Singida Mh Dk Rehema Nchimbi akigawa mipira ya Miguu kwa baadhi ya wakuu wa shule za Msingi na Sekondari katika wilaya ya Mkalama ambayo iliyotolewa na Mtandao wa Elimu Tanzania wakati wa kilele cha Maadhimisho ya juma la elimu Kitaifa.
Mkuu wa Mkoa wa Singida. Dk Rehema Nchimbi akiendesha harambee ya kuchangia maboresho ya Elimu wilayani Mkalama wakati wa kilele cha juma la elimu yaliyofanyika wilayani humo.
Baadhi ya wanafunzi wakimuonyesha mabango yenye ujumbe wa Kuhamasisha Uwajibikaji wa Pamoja kwa Elimu Bora wakati wa kilele cha juma la maadhimisho ya Elimu yaliyofanyika Wilayani Mkalama.
Wanafunzi wakiwa kwenye maandamano wakati wa kilele cha juma la elimu kitaifa
**********************************************************
Kampeni ya Juma ya Elimu Duniani huadhimishwa duniani kote kati ya mwezi wa nne na wa tano. Nchini Tanzania Maadhimisho haya huratibiwa na Mtandao wa Elimu Tanzania (TENMET) Ikishirikiana na wadau mbalimbali wa elimu, serikali na taasisi binafsi.
Kwa Mwaka 2018 maadhimisho ya Juma la Elimu Kitaifa yamefanyika Wilaya ya Mkalama, Mkoa wa Singida kuanzia tarehe Mei 14 hadi Mei 18 2018 ambapo Mgeni rasmi katika sherehe za Kilele cha Maadhimisho ya Juma la Elimu Kitaifa alikua Mkuu wa Mkoa wa Singida Mh. Dk Rehema Nchimbi.
Akisoma majumuisho ya uhamasishaji wa juma la Elimu wilayani Mkalama Mwenyekiti wa Bodi ya Mtandao wa Elimu Tanzania Dk. John Kallage alielezea mada ya Mwaka huu Kitaifa ni “Uwajibikaji wa pamoja kwa Elimu Bora kwa wote” na kwa wilaya ya Mkalama uhamasishaji ulifanyika katika Shule za Msingi sita na Shule za Sekondari tatu ambapo ni katika vijiji sita ambavyo ni Mbigigi, Kikhonda, Ikolo, Mwangeza, Malaja na Nyahaa.
Wadau wa elimu walifanikiwa kufanya mikutano ya kijamii ikijumuisha wazazi, wanajamii na viongozi wa serikali ya kijiji, dini na watu mashuhuri ili kubaini na kuzitafutia ufumbuzi changamoto za Elimu kwa pamoja.
Wadau wa Elimu katika Ziara ya uhamasishaji wa Juma la Elimu katika wilaya ya Mkalama walibaini Changamoto mbalimbali ikiwemo Bajeti finyu ya Serikali isiyokidhi mahitaji ya Sekta ya Elimu, Upungufu Mkubwa wa walimu na hasa waalimu wa masomo ya Sayansi na walimu wa Kike, Upungufu wa madawati, Upungufu wa vitabu vya kiada na ziada, Miundombinu isiyokidhi mahitaji mfano Vyumba vya madarasa, Vyoo, Maji na Nyumba za walimu pamoja na uhaba wa miundombinu rafiki kwa watu wenye mahitaji maalumu.
Katika Risala ya Majumuisho ya uhamasishaji wa Juma la Elimu Kitaifa wilayani Mkalama Mwenyekiti wa Mtandao wa Elimu Tanzania Dk John Kallage alisema “Mtandao wa Elimu Tanzania unatambua na kupongeza juhudi mbalimbali za Serikali katika kuboresha Kiwango cha Elimu nchini ikiwa ni pamoja na utoaji wa elimu bila malipo ya ada”
Mtandao wa Elimu Tanzania na waadau wa Elimu waliishauri Serikali kuongeza jitihada za kuinua ubora wa Elimu nchini ili kufikia malengo ya Kitaifa na Kimataifa kwa Kuongeza Bajeti ya elimu, kuajiri walimu wa kutosha na kuboresha mazingira yao ya kufanyia kazi, kuimarisha miundombinu ikiwemo vyumba vya madarasa, vyoo, upatikanaji wa maji na nyumba za walimu, Kuboresha mitaala ili iweze kuendana na wakati pamoja na kuongeza mapambano ya kupinga mila kandamizi zinarudisha nyuma jitihada za maendeleo ya elimu.
Mtandao wa Elimu Tanzania katika kuunga mkono juhudi za serikali katika kuboresha Elimu imechangia vifaa mbalimbali ikiwemo Mabati na milango kwa ajili ya kuisaidia Shule ya Msingi Mbigigi vyenye Thamani ya Tshs 12,000,000/= pamoja na Mipira ya miguu katika shule zote zilizptembelewa na wadau wa Elimu.
Mkuu wa Mkoa wa Singida Mh. Dk Rehema Nchimbi akifunga Maadhimisho wa Juma la Elimu Kitaifa, Alipongeza juhudi na jitihada mbalimbali zinazofanywa na Mtandao wa Elimu Tanzania pamoja na wanachama wake katika kuinua na kuboresha Elimu Nchini. Akiongea katika Sherehe hizo Mh. Dk Rehema Nchimbi alisema “Elimu ni kipaumbele cha serikali ya awamu ya Tano na Utoaji wa elimu bure kuanzia shule ya msingi hadi sekondari ni kiashiria tosha na hivi karibuni tu Serikali imetangaza Ajira mpya kwa waalimu wa masomo ya Sayansi na natumai hata wilaya ya Mkalama itafaidika”.
Katika Sherehe hizo pia Mkuu wa Singida aliendesha harambee kwa ajili ya Kuchangia maboresho ya Elimu na inakadiriwa kiasi cha Milioni Tatu zitakusanywa.
↧
↧
REMA FC YAICHAPA AIRPORT FC 8-4 NA KUTINGA FAINALI ZA KURUGENZI CUP
Aziz Rashid wa timu ya Rema 1000 FC ya Haydom wilayani Mbulu akimiliki mpira huku Elihuruma Daniel wa timu ya Airport FC akijaribu kunyanga'anya wakati wa mchezo wao wa nusu Fainali ya Michuano ya Kombe la Kurugenzi Cup 2018 yanayoendelea mjini Haydom, Timu ya Rema 1000 FC imeifunga timu ya Airport Magoli 8-4 na kutinga fainali ambapo sasa itakutana na timu ya Dongobesh FC ambayo nayo imeshinda mchezo wake wa leo wa Nusu Fainali baada ya kuifunga timu ya Young Boys FC magoli 2-0.
Mashindano hayo yanaandaliwa na Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Mbulu Bw. Hudson Kamoga na yanafanyika kwenye uwanja wa Shule ya Msingi ya Haydom kwa udhamini mkubwa wa Kiwanda cha maziwa cha ASAS cha mkoani Iringa na Benki ya CRDB.
Mchezo wa Fainali utafanyika kesho kwenye uwanja wa huohuo kwa kuzikutanisha timu za Dongobesh FC na Rema 1000 FC ambapo pia kutakuwa na burudani mbalimbali za ngoma za asili wakiwemo pia wachekeshaji MC Pilipili na Katarina wa Karatu.
Aziz Rashid wa Rema 1000 FC ya Haydom Mbulu akimiliki mpira huku Elihuruma Daniel wa timu ya Airport FC akijaribu kunyanga'anya huku kiatu kikiwa kimechomoka mguuni wakati wa mchezo wao wa nusu Fainali ya Michuano ya Kombe la Kurugenzi Cup 2018 yanayoendelea mjini Haydom
Kocha wa timu ya Rema 1000 FC Bw. Jared Ochieng akiwaelekeza wachezaji wa timu yake kwa kuchora chini kutokana na makosa waliyokuwa wakisababisha katika mchezo huo wakati wa mapumziko.
Samson Madawabora ambaye ni Daktari katika Hospitali ya Haydom na mmiliki wa timu hiyo akiwapongeza wachezaji wake mara baada ya kutinga fainali ya michuano hiyo leo.
Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Mbulu Bw. Hudson Kamoga pamoja na baadhi ya viongozi wa halmashauri hiyo wakifuatilia mchezo huo.
Wachezaji wa timu ya Dongobesh FC na Young Boys FC wakisalimiana kabla ya kuanza kwa mchezo wao wa pili wa nusu fainali uliochezwa leo kwenye uwanja wa shule ya Msingi Haydom.
Kikosi cha timu ya Young Boys FC kikiwa katika picha ya pamoja.
Kikosi cha timu ya Dongobesh FC kikiwa katika picha ya pamoja kabla ya kuanza kwa mchezo huo.
Wachezaji wa timu ya Dongobesh FC na Young Boys FC wakichuana vikali katika mchezo wao wa nusu fainali uliofanyika kwenye uwanja wa Shule ya Msingi Haydom leo.
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbulu Bw. Hudson Kamoga kulia akiwa na Mchekeshaji MC Pilipili wakifuatilia mchezo wa Nusu fainali kati ya timu ya Dongobesh FC na Young Boys FC.![]()

Mchekeshaji MC Pilipili akitangaza mchezo wa nusu fainali kati ya timu ya Dongobesh FC na Young Boys FC wakati ulipokuwa ukiendelea kwenye uwanja wa shule ya Msingi Haydom.![]()

Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbulu Bw. Hudson Kamoga akiwa na mtangazaji wa Radio Clouds Jacob Mbuya wakishuhudia mchezo huo.
Mashabiki wa timu ya Dongobesh FC wakimbeba juu juu golikipa wao anayejulikana kwa jina la Mapilau mara baada ya kuibuka washindi wa mchezo huo na kutinga fainali.
Mashabiki mbalimbali wakiwemo akina mama wakiwa wamefurika uwanjani kushuhudia mchezo huo.
↧
RAIS DKT MAGUFULI APOKEA MAKOMBE YA UBINGWA WA SERENGETI BOYS NA TSC, AKABIDHI LA UBINGWA WA LIGI KUU KWA SIMBA

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akikabidhi kombe la Ubingwa wa Ligi kuu ya Soka ya Vodacom kwa nahodha wa Simba SC John Bocco baada ya mchezo wa kutimiza ratiba klabu hiyo ya Msimbazi na Kagera sugar ambapo walifungwa bao 1-0 katika Uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam leo








↧
KATIBU MKUU (W) HABARI SUZAN MLAWI KATIKA MAANDALIZI YA TAMASHA LA SABA LA 4CCP MKOANI MANYARA
Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Bi. Suzan Mlawi akimsikiliza Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbulu Bw. Hudson Kamoga mara baada ya kuwasili kwenye kituo cha Utamaduni cha Haydom cha 4CCP kilichopo mjini Haydom kwa ajili ya kuzindua maandalizi ya Tamasha la Saba la 4CCP linalotarajiwa kufanyika kuanzia Tarehe 3-6 mwezi Oktoba mwaka huu mjini Haydom wilaya ya Mbulu Mkoani Manyara.
Katibu Mkuu Bi Suzan Mlawi pia ametembelea jamii za makabila manne makuu ya Afrika yanayopatikana katika kituo hicho na kujionea nyumba na tamaduni mbalimbali kutoka kwa wananchi wa Jamii za Wahzabe, Watatoga, Wabantu na jamii ya Wakhosain , Kulia ni Nelson Faustine Afisa Miradi wa Kituo cha 4CCP Haydom.
Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Bi. Suzan Mlawi akimsikiliza Bw. Nelson Faustine Afisa Miradi wa Kituo cha Utamaduni cha 4CCP Haydom wakati alipokuwa akiangalia ngoma ya kabila la Wahadzabe wakati alipotembelea katika kituo hicho leo.
Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Bi. Suzan Mlawi akimsikiliza Bw. Nelson Faustine Afisa Miradi wa Kituo cha Utamaduni cha 4CCP Haydom wakati alipokuwa akiangalia ngoma ya kabila la Wahadzabe wakati alipotembelea katika kituo hicho leo kutoka kulia ni Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Mbulu Bw. Hudson Kamoga na Eliminata Awet Mratibu wa kituo cha Utamaduni Haydom.
Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Bi. Suzan Mlawi akimsikiliza Bw. Bi Eliminata Awet Mratibu wa Kituo Cha Utamaduni Haydom cha 4CCP wakati akimpa maelezo kuhusu tamaduni zinazopatikana kituoni hapo kutoka kushoto ni Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Mbulu Bw. Hudson Kamoga na Nelson Faustine Afisa Miradi wa Kituo cha 4CCP Haydom
Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Bi. Suzan Mlawi akimsikiliza Bw. Nelson Faustine Afisa Miradi wa Kituo cha Utamaduni cha 4CCP Haydom wakati alipokuwa akiangalia ngoma ya kabila la Watatoga alipotembelea katika kituo hicho leo.
Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Bi. Suzan Mlawi akiongozana na Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mbulu Bw. Hudson Kamoga na Eliminata Awet Mratibu wa Kituo cha Utamaduni 4CCP cha Haydom alipokuwa akielekea kuangalia nyumba za makabila hayo kulia ni Mkurugenzi wa Hospitali ya Haydom Dk. Emanuel Nuwass.
Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Bi. Suzan Mlawi Bi Eliminata Awet Mratibu wa Kituo cha Utamaduni cha 4CCP Haydom wakiangalia nyumba ya wanyilamba wakati alipotembelea katika kituo hicho leo.
Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Bi. Suzan Mlawi na Mkurugenzi wa halmashauri ya Wilaya ya Mbulu wakitoka nje ya nyumba ya kabila ya Wanyiramba huku wakiongozwa na mzee Salum Shaban Mwakilishi wa wabantu na aliyekuwa akitoa maelezo kuhusu tamaduni za kabila hilo alipokuwa akiangalia nyumba ya kabila la Wanyiramba wakati alipotembelea katika kituo hicho leo.![]()

Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Bi. Suzan Mlawi akiakiondoka mara baada ya kutembelea nyumba ya Wanyiramba na Wanyisanzu inazopatikana katika Kituo cha utamaduni cha 4CCP Haydom alipotembelea katika kituo hicho leo.![]()

Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Bi. Suzan Mlawi akionyeshwa picha mbalimbali zinazoonyesha matukio ya Kituo cha Utamaduni cha 4CCP Haydom wakati alipotembelea katika kituo hicho leo.
Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Bi. Suzan Mlawi akimsikiliza Bw. Edward Mashimba Mwenyekiti wa Kabila la Wahdzabe wakati akitoa maelezo kuhusu nyumba ya kabila hilo inayopatikana katika Kituo cha Utamaduni cha 4CCP Haydom wakati alipotembelea katika kituo hicho leo.
Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Bi. Suzan Mlawi akipiga picha ya pamoja na Bw. Edward Mashimba Mwenyekiti wa Kabila la Wahdzabe pamoja na Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Mbulu Bw. Hudson Kamoga, kulia ni Mratibu wa Kituo hicho Bi. Eliminata Awet.
Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Mbulu Bw. Hudson Kamoga akizungumza katika hafla ya uzinduzi wa tamasha hilo uliofanyika leo kwenye kituo cha Utamaduni cha 4CCP mjini Haydom.
Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Bi. Suzan Mlawi na Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Mbulu Bw. Hudson Kamoga wakifurahia jambo wakati MC Pilipili alipokuwa akizungumza katika uzinduzi huo.
Baadhi ya wananchi wa Jamii za Watatoga, Wahadzabe Wakhosain na wabantu wakiwa katika hafla hiyo.
Jamii ya watatoga wakifuatilia hafla hiyo
Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Bi. Suzan Mlawi akizindua rasmi maandalizi ya tamasha hilo.
Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Bi. Suzan Mlawi , Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Mbulu na Mratibu wa kituo cha Utamaduni cha 4CCP cha haydom wakipiga makofi mara baada ya uzinduzi huo.![]()

Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Bi. Suzan Mlawi akiwa katika picha ya pamoja na jamii hizo pamoja na viongozi wa kituo hicho na Halmashauri ya Mbulu.
Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Bi. Suzan Mlawi akivishwa mgorole na wazee wa kimila.
Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Bi. Suzan Mlawi akizungumza na jamii hizo wakati wa uzinduzi huo
↧
↧
TULIA TRUST YAWAPELEKA BUJORA DANCE GROUP KUWAKILISHA NCHI MASHINDANO YA NGOMA NCHINI INDIA
Mwanakikundi wa Bujora Deogratius Willium akizungumza kabla ya kuanza safari ya kuelekea nchini India kwa ajili ya kuiwakilisha nchi kwenye mashindano ya kucheza baada ya kuibuka washindi katika mashindano ya Tulia Traditional Dance Festival mwaka jana yaliyo chini ya Naibu Spika Dkt Tulia Ackson.
*********************
Na Leandra Gabriel, Dar.
WASHINDI wa Tulia Traditiona Dance Festistal 2017 chini ya Taaisisi ya Tulia Trust Bujora Dance Group la Mkoa Mwanza leo wameelekea nchini India kushiriki mashindano ya ngoma ya asili yatakayofanyika tarehe 25 na 26 wiki hii.
Akizungumza na vyombo vya habari mmoja wa wanakikundi hao Deogratius Willium ameeleza kuwa walishinda katika mashindano ya Tulia dance mwaka jana na kwa sasa wanaelekea India katika mashindano hayo ya ngoma za asili.
Aidha ameeleza kuwa wana uzoefu na wamejiandaa na wanajiamini, na kuwaomba watanzania wawaombee ili waweze kurudi na ushindi.
Pia Veronika Sombi mshiriki wa kikundi hicho ameeleza kuwa ameeleza kuwa walishinda kwa kishindo Mbeya kwa kuibuka nafasi ya kwanza kati ya vikundi 81, hivyo ushindi lazima urudi nyumbani.
Pia wamemshukuru Dk. Tulia kwa kuanzisha mashindano hayo kwani kama vijana wamepata fursa ya kutangaza utamaduni wa mtanzania sambamba na kutembea katika nchi nyingi duniani kama Sweden na Korea.
Mashindano haya ya kulinda utamaduni yalianza mapema mwaka 2016 huko Tukuyu Mkoani Mbeya chini ya Dkt. Tulia Ackson ambaye ni naibu spika wa Bunge la Jamuhuri wa muungano wa Tanzania, pia ni muasisi wa mashindano hayo.
Washindi wa mashindano hayo hunufaika kwa namna mbalimbali kama vile kueneza utamaduni nje ya nchi na kupata mafunzo katika vyuo vya sanaa hasa Bagamoyo ambapo washindi wa mwaka 2016 waliendeleza ujuzi katika chuo hicho cha sanaa.
↧
RAIS NA MWENYEKITI WA CCM DKT MAGUFULI AONGONZA MKUTANO WA HALMASHAURI KUU YA TAIFA (NEC) YA CCM JIJINI DAR ES SALAAM LEO
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mwenyekiti wa CCM Dkt. John Pombe Magufuli na meza kuu wakishangilia baada ya kuwaita Ndg. Mizengo Pinda na Ndg. Makongoro Nyerere waingie ukumbini baada ya kukubaliwa kuwa wajumbe wa Mkutano wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) wa Chama cha Mapinduzi (CCM) katika ukumbi wa Kikwete jijini Dar es salaam leo Jumatatu Mei 28, 2018
Wajumbe wakishangilia baada ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mwenyekiti wa CCM Dkt. John Pombe Magufuli kuwaita Ndg. Mizengo Pinda na Ndg. Makongoro Nyerere waingie ukumbini baada ya kukubaliwa kuwa wajumbe wa Mkutano wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) wa Chama cha Mapinduzi (CCM) katika ukumbi wa Kikwete jijini Dar es salaam leo Jumatatu Mei 28, 2018
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mwenyekiti wa CCM Dkt. John Pombe Magufuli akiongoza Mkutano wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Katika ukumbi wa Kikwete jijini Dar es salaam leo Jumatatu Mei 28, 2018
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa baraza la Mapinduzi ambaye pia ni Makamu Mwenyekiti wa CCM (Visiwani) Dkt. Ali Mohamed Shein akipendekeza majina ya wanachama wa CCM kutoka visiwani wataopigiwa kura kuwa wajumbe Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) wa Chama cha Mapinduzi (CCM) ukumbi wa Kikwete leo Jumatatu Mei 28, 2018
Picha na IKULU.
↧
NAIBU SPIKA AONGOZA WABUNGE KUSAINI KITABU CHA MAOMBOLEZO YA ALIYEKUWA MBUNGE WA BUYUMBU LEO BUNGENI JIJINI DODOMA
Naibu Spika wa Bunge Dkt. Tulia Ackson, akisaini kitabu cha Maombolezo kufuatia kifo cha aliyekuwa Mbunge wa Buyungu Marehemu Mwl. Kasuku Samson Bilago. Mwili wa Marehemu unatarajiwa kuletwa Bungeni kesho Jumanne tarehe 29 Mei, 2018 kwa ajili ya Waheshimiwa Wabunge kutoa heshima za mwisho kabla ya kusafirishwa kwenda kuzikwa kijijini kwake Kasuga, Wilayani Kakonko, Mkoani Kigoma. Awali mapema leo, Naibu Spika Dkt. Tulia Ackson aliahirisha Bunge kutokana na Msiba huo.
Waziri wa Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Walemavu Mhe. Jenista Mhagama akisaini kitabu cha Maombolezo kufuatia kifo cha aliyekuwa Mbunge wa Buyungu Marehemu Mwl. Kasuku Samson Bilago.
Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Philip Mpango akisaini kitabu cha Maombolezo kufuatia kifo cha aliyekuwa Mbunge wa Buyungu Marehemu Mwl. Kasuku Samson Bilago.
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Dkt. Harrison Mwakyembe akisaini kitabu cha Maombolezo kufuatia kifo cha aliyekuwa Mbunge wa Buyungu Marehemu Mwl. Kasuku Samson Bilago.
Waziri wa Utumishi na Utawala Bora Capt. George akisaini kitabu cha Maombolezo kufuatia kifo cha aliyekuwa Mbunge wa Buyungu Marehemu Mwl. Kasuku Samson Bilago.
Mbunge wa kuteuliwa na Rais Mhe. Salma Kikwete akisaini kitabu cha Maombolezo kufuatia kifo cha aliyekuwa Mbunge wa Buyungu Marehemu Mwl. Kasuku Samson Bilago.
Mbunge wa Tarime Mjini , Mhe. Esther Matiko akisaini kitabu cha Maombolezo kufuatia kifo cha aliyekuwa Mbunge wa Buyungu Marehemu Mwl. Kasuku Samson Bilago.
Waheshimiwa Wabunge wakijipanga kusaini kitabu cha Maombolezo kufuatia kifo cha aliyekuwa Mbunge wa Buyungu Marehemu Mwl. Kasuku Samson Bilago. Aliyeketi kusaini ni Mbunge wa Mufindi Kaskazini Mhe. Mahmoud Mgimwa.
Waheshimiwa Wabunge wakijipanga kusaini kitabu cha Maombolezo kufuatia kifo cha aliyekuwa Mbunge wa Buyungu Marehemu Mwl. Kasuku Samson Bilago.
PICHA NA BUNGE
↧
Waziri Jafo awaagiza Makatibu Tawala wa Mikoa kutoa Takwimu za Wazee ifikapo 30 Juni, 2018
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Seleman Jafo, akizungumza wakati wa Hafla ya kuwapatia Vitambulisho Wazee wa Jiji la Dodoma.
*******************
Na. Atley Kuni-OR TAMISEMI
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. Selemani Jafo (Mb), amewaagiza Makatibu Tawala wa Mikoa Tanzania Bara kuwasilisha taarifa za takwimu za wazee ifikapo 30, Juni 2018.
Waziri Jafo, alitoa kauli hiyo mapema leo alipokuwa akizindua zoezi la kuwapatia vitambulisho maalum wazee wapatao 1,118 wa Jiji la Dodoma kutoka kata za Mkonze, Mnadani, Uhuru, Madukani, Makole na Majengo. Vitambulisho hivyo, pamoja na mambo mengine vitawawezesha wazee hao kupata huduma za afya bure na kwa wakati.
“Ifikapo tarehe 15 Juni, 2018 kila kata iwe imetambua wazee na ifikapo tarehe 22 Juni, 2018 kila Halmashauri iwe imeunganisha taarifa za wazee kutoka katika kata zake zote” alisema Waziri. Aidha Waziri Jafo aliagiza kuwa, “ifikapo Juni, 26, 2018 kila Mkoa uwe umeunganisha taarifa zote na kuzituma kwa Katibu Mkuu Ofisi ya Rais TAMISEMI”. Aliwaonyawale wote watakaoshindwa kutimiza agizo hilo kuchukuliwa hatua kulingana na miongozo, kwasababu watakuwa wameshindwa kutekeleza wajibu wao.
Mkurugenzi wa Jiji la Dodoma akitoa salam za jiji muda mfupi kabla ya zoezi la ugawaji wa Vitambulisho kwa wazee halifanyika.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa Jiji la Dodoma Ndugu Godwin Kunambi akizungumza katika hafla hiyo alisema shabaha ni kuwafikia wazee wote kwenye Jiji hilo, na kubainisha kwamba, vitambulisho wanavyo vitoa kwa wazee hao vitatumika pia kuwapa kipaumbele wazee sehemu zote za kutolea huduma hususan ofisi za serikali.
“Mhe. Waziri tunataka vitambulisho hivi tunavyo wapatia wazee wetu leo viwasaidie pia kupata huduma kwa haraka na kwa wakati pindi wanapofika kwenye ofisi zingine za Serikali” alisema Kunambi.
Mbali na kutolea ufafanuzi wa matumizi ya vitambulisho hivyo, Mkurugenzi Kunambi alisema juu ya Jiji hilo lilivyo jipanga katika suala zima la makusanyo ya mapato ya ndani, ambayo ndio yamekuwa chachu ya kuboresha huduma za afya kwa makundi maalum hususan wazee.
Mmoja ya Wazee akipokea kitambulisho mara baada yakuzinduliwa kwa zoezi lakuwapatia vitambulisho wazee Jiji la Dodoma.
“Mhe. Waziri, Jiji limepanga kukusanya Bil. 68 katika mwaka wa fedha ujao ikilinganishwa na mwaka huu wa fedha ambapo tulijiwekea lengo la kukusanya Bil. 20 nahadi kufikia mwezi Februari tulikuwa tumekusanya Bil. 14”. Kunambi ameongeza kuwa, katika mwaka ujao wa fedha wametenga kiasi cha Mil. 58 kwaajili yakuwezesha huduma za wazee kwenye Jiji hilo.
Naye Kaimu Mkuu wa Wilaya ya Dodoma Mjini ambaye pia ni Mkuu wa Wilaya ya Kongwa Mhe. Deo Ndejembi, ametumia fursa hiyo kuwaonya baadhi ya watendaji wanao waambia wazee kwamba hakuna dawa.
“Kumekuwepo na malalamiko mengi siku za nyuma kutoka kwa wazee kuwa, baadhi ya watendaji wa afya wanawanyanyapaa wazee na kuwaambia hakuna dawa wafikapo vituoni, sasa Mhe Waziri, mimi niliseme kwa uwazi kabisa hatuta mvumilia mtu yeyote atakaye onekana ni kikwazo kwa wazee hawa kadi zimetoka wazee wahudumiwe, sio mnajiwekea vijiduka karibu na vituo halafu mnawaambia waende waka nunue” alionya Ndejembi
Picha ya pamoja kati ya Mhe. Waziri Viongozi wa Halmashauri na wazee waliopatiwa vitambulisho.
Awali akitoa taarifa ya uandaji wa vitambulisho Mganga Mkuu wa Jiji la Dodoma, Dkt. Mohamed Nyembea, alisema utekelezaji wa zoezi hilo ulianza kwa hatua za awali kwa kuwatambua wazee katika Kata 41 za Jiji la Dodoma, ambapo jumla ya wazee 15,885 kutoka kata 33 miongoni mwa 41 wamekwisha tambuliwa na miongoni mwao wanawake ni 9,132 na wanaume ni 6,753 ambapo ni sawa na asilimia 80.5 ya kata zote 41 za Jiji la hilo.
Utoaji wa vitambulisho kwa wazee ni utekelezaji wa sera ya Taifa ya wazee ya mwaka 2003 ambapo inazungumzia mambo muhimu ya wazee ikiwepo kutenga dirisha maalum katika vituo vya kutolea huduma za afya.
Diwani wa Kata ya Mkonze akishukuru kwaniaba ya wananchi wa Mkonze.
↧
↧
MWILI WA MBUNGE KASUKU BILAGO WAAGWA LEO JIJINI DAR
Na Said Mwishehe, Globu ya jamii
MWILI wa aliyekuwa Mbunge wa Buyungu wilayani Kakonko mkoani Kigoma Kasuku Samson Bilago(Chadema), aliyefariki duniani juzi katika Hospitali ya Taifa Muhimbili umeagwa leo jijini Dar es Salaam ambapo Mwenyekiti wa Chadema Freeman Mbowe ameongoza mamia ya waombolezaji wakati wa kuaga mwili wa mbunge huyo.
Akizungumza leo jijini Dar es Salaam wakati wa kuaga mwili wa mbunge huyo, Mbowe amesema mwili wa Bilago utapumzishwa kwenye nyumba yeke ya milele Alhamisi wiki hii mkoani Kigoma na kesho wabunge watapata nafasi ya kutoa heshima zao za mwisho mkoani Dodoma.
Kuhusu ratiba ya mazishi Mbowe amesema wamekaa kikao na familia na kukubaliana mwili wa marehemu Bilago upumzishwe Almasi ili kutoa nafasi ya wananchi wa jimbo lake kumuaga na kutoa heshima zao za mwisho.Amefafanua wamekubaliana na ombi la Paroko wa Kakonko la kutaka marehemu Bilago ibada ya kumuaga ifanyike Kanisani lakini akaeleza Chadema imeamua Jumatano aagwe katika viwanja vya wazi na kisha siku inayoafuata(Alhamisi) ndio itakuwa kanisani.
Akizungumzia taarifa za kifo cha mbunge huyo amesema alifariki dunia Jumamosi mchana siku ya Jumamosi wakati akipatiwa matibabu Hospitali ya Taifa Muhimbili na taarifa za kuumwa kwake alizipata akiwa nchini Afrika Kusini.Hivyo aliagiza wabunge na viongozi wengine wa Chadema kufanya jitihada za kuhakikisha anapata matibabu.
"Akiwa hospitali ya Muhimbili alinitumia ujumbe kupitia simu yangu ya mkononi akinieleza kuwa anaumwa sana na akahitaji nije kumuona.Lakini wakati ananitumia ujumbe huo sikuwepo nchini."Hivyo niliporudi nikaenda kumuona hospitali na tukawa na mpango wa kumpeleka nje kwa matibabu lakini ilipofika Jumamosi akafariki dunia,"amesema Mbowe na kuongeza Chadema imepata pigo kubwa kwa kuondokewa na Mbunge wao makini na ni pigo kwa familia.
Awali akizungumza mbele ya waombolezaji waliofika kuaga mwili wa marehemu Bilago, Paroko wa Parokia ya Magomeni jijini Dar es Salaam Christan Nyumayo amesema enzi za uhai wake kiongozi huyo alikuwa ameweka maisha yake kwenye imani ya dini yake na hata Parokia ya Kakonko imethibitisha hilo na ndio maana inataka lazima ibada yake ikafanyike ndani ya Kanisa.
Pia amesema maisha yake aliyandaa akiwa hai na ndio maana leo hii anaagwa kwa heshima kubwa ,hivyo ametoa rai kwa walio hai kuhakikusha wanatenda mema na kuandaa maisha yao ya baadae."Ukiwa kibaka katika uhai wao kuna uwezekano mkubwa wa kuzikwa na vibaka wenzako na ukiwa mcha Mungu basi utazikwa na wacha Mungu.Hivyo tunachoshuhudia leo hii ndugu yetu amepata heshima ya kuagwa katika mazingira ya utulivu na unyenyekevu kwasababu aliishi maisha ya kumpendeza Mungu.Nilipopata taarifa za kutakiwa kuja hapa sikuwa na shaka ya aina yoyote,"amesema Paroko Nyumayo.
Mwili wa aliyekuwa Mbunge wa Buyungu wilayani Kakonko mkoani Kigoma Kasuku Samson Bilago(Chadema), aliyefariki duniani juzi katika Hospitali ya Taifa Muhimbili ,ukiwasili katika viwanja vya Karimjee kwa ajili ya kuagwa mapema leo mchana jijini Dar.
Mwili wa aliyekuwa Mbunge wa Buyungu wilayani Kakonko mkoani Kigoma Kasuku Samson Bilago(Chadema),ukiingizwa ndani ya ukumi wa Karimjee,mapema leo mchana tayari kwa kuagwa na waombolezaji mbalimbali wakiwemo viongozi waandamizi wa chama cha CHADEMA.
Baadhi ya viongozi waandamizi wa chama cha CHADEMA,wakiwa ndanni ya ukumbi wa Karimjee tayari kutoa heshima zao za mwisho kwa aliyekuwa bunge wa Buyungu wilayani Kakonko mkoani Kigoma Kasuku Samson Bilago(Chadema), aliyefariki duniani juzi katika Hospitali ya Taifa Muhimbili .
Sanduku lenye mwili wa aliyekuwa Mbunge wa Buyungu wilayani Kakonko mkoani Kigoma Kasuku Samson Bilago (Chadema), aliyefariki duniani juzi katika Hospitali ya Taifa Muhimbili,tayari kwa kutokewa heshima za mwisho na baadhi ya viongozi waandamizi wa chama hicho pamoja na waombolezaji wengine.
Baadhi ya waombolezaji wakishiri sala ya kuaga mwili wa aliyekuwa Mbunge wa Buyungu wilayani Kakonko mkoani Kigoma Kasuku Samson Bilago (Chadema), aliyefariki duniani juzi katika Hospitali ya Taifa Muhimbili .
Baadhi ya viongozi waandamizi wa CHADEMA na baadhi ya waombolezaji wakishiriki sala ya kuaga mwili wa aliyekuwa Mbunge wa Buyungu wilayani Kakonko mkoani Kigoma Kasuku Samson Bilago (Chadema), aliyefariki duniani juzi katika Hospitali ya Taifa Muhimbili .
Baadhi ya Waandishi wa habari wakirekodi tukio la kuwasili mwili wa aliyekuwa Mbunge wa Buyungu wilayani Kakonko mkoani Kigoma Kasuku Samson Bilago(Chadema), aliyefariki duniani juzi katika Hospitali ya Taifa Muhimbili .PICHA NA MICHUZIJR.
↧
Makala aweka wazi mahusiano yake na Odama
Mtayarishaji na muigizaji wa filamu hapa nchini Laurent Matiholo maarufu kama “Makala” amefunguka na kuweka wazi juu ya ukaribu wake wa kimahusiano na msanii mwenzake Jeniffer Kyaka maarufu kama ”Odama”.
Makala ambaye alijipatia umaarufu mkubwa sana tasnia hii ya filamu,baada ya kupokelewa vema na mashabiki katika kazi zake zilizomtambulisha vema kwenye ulimwengu huo zikiwemo filamu ya Kiss Me, Hot Love, Shella, Surprise na nyingine kibao alizocheza katika kiwango cha hali ya juu na kujipatia umaarufu mkubwa na ndani na nje ya nchi akiwa chini ya Mtunzi na Mtayarishaji nguli Mussa Banzi.
Makala amesema hayo baada ya kuwepo kwa taarifa kwenye baadhi ya mitandao ya kijamii, zikimuhusisha kuwa na ukaribu ambayo ukifananishwa na kuwa na mahusiano ya kimapenzi na msanii mwenzake kitu ambacho akina ukweli wowote.
“Unajua Bongo kumekuwa na mambo mengi sana na watu hata hawajui tumetoka wapi na Odama wanaanza kusambaza uzushi wa mimi kutoka kimahusiano nae, taarifa hizo wanazosambaza hawana uhakika nazo na laiti Wangejua navyomchukulia huyo dada kama nimezaliwa naye tumbo mmoja wala waingethubutu kunipakazia najisikia vibaya,"amesema Makala.
Amesema kuwa katika mafanikio yake Odama amekuwa na mchango mkubwa sana kama dada yake na amempiga tafu sana na anatamani siku moja aje kufikia alipokuwa yeye kwa sasa.
Makala ni mmiliki wa kampuni ya Usambazaji inayofahamika kama Wa Ukweli na kwa sasa anatamba na filamu ya Big SURPRISE inayokimbiza kwenye tasnia ya filamu akicheza na wakali wenzake wakiwemo Gabo,Odama,Mzee Jengua na wengine kibao,yupo njiani kuachia kazi mpya nyingine.
↧
RAIS DKT. MAGUFULI ALIPOWAANDALIA FUTARI WAGENI MBALIMBALI IKULU JIJINI DAR ES SALAAM

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimkaribisha kufuturu Waziri wa masuala ya Dini wa Saudia Arabia Dkt. Saleh Abdulaziz Alashek Ikulu jijini Dar es salaam Jumatatu Mei 28, 2018

Mufti Mkuu wa Tanzania Sheikh Aboubakary Zubeiry Ally akiswalisha viongozi na waalikwa mbalimbali swala ya Magharibi kabla ya futari iliyoandaliwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli Ikulu jijini Dar es salaam Jumatatu Mei 28, 2018.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimkaribisha kufuturu Waziri wa masuala ya Dini wa Saudia Arabia Dkt. Saleh Abdulaziz Alashek Ikulu jijini Dar es salaam Jumatatu Mei 28, 2018

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimkaribisha kufuturu Waziri wa masuala ya Dini wa Saudia Arabia Dkt. Saleh Abdulaziz Alashek Ikulu jijini Dar es salaam Jumatatu Mei 28, 2018

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimkaribisha kufuturu Mufti Mkuu wa Tanzania Sheik Aboubakary Zubeiry Ally Ikulu jijini Dar es salaam Jumatatu Mei 28, 2018

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli na wageni wake wakiingia ukumbinini kufuturu Ikulu jijini Dar es salaam Jumatatu Mei 28, 2018

Waziri wa masuala ya Dini wa Saudia Arabia Dkt. Saleh Abdulaziz Alashek akipakua futari akiwa ameongozana na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa na Balozi wa Saudi Arabia nchini Mhe. Mohamed bin Mansour al Malik Ikulu jijini Dar es salaam Jumatatu Mei 28, 2018

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli na akikaribisah wageni wake kuchukua futari na kufuturu Ikulu jijini Dar es salaam Jumatatu Mei 28, 2018

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli na akikaribisah wageni wake kuchukua futari na kufuturu Ikulu jijini Dar es salaam Jumatatu Mei 28, 2018

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli na akikaribisah wageni wake kuchukua futari na kufuturu Ikulu jijini Dar es salaam Jumatatu Mei 28, 2018

Mawaziri Wakuu Wastaafu Dkt. Salim Ahmed Salim, Jaji Joseph Sinde Warioba na waalikwa wengine wakichukua futari Ikulu jijini Dar es salaam Jumatatu Mei 28, 2018

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akijiunga na wageni mbalimbali kuchukua futari aliyowaandalia
Ikulu jijini Dar es salaam Jumatatu Mei 28, 2018
Waziri wa Sheria na Katiba Profesa Palamagamba Kabudi akiwa na Jaji Mkuu Profesa Inbrahim Juma na Kaimu Mkurugenzi wa Mashariki ya Kati kutoka Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikianowa Afrika Mashariki, Bw. Suleiman Salehe wakichukua futari
Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Jenerali Venance Mabeyo (kushoto) akifuatiwa na Inspekta Jenerali wa Polisi Simon Sirro, Inspekta Jenerali wa Magereza Dkt. Juma Malewa (wa pili kulia) na wageni wengine wakichukua futari iliyoandaliwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli Ikulu jijini Dar es salaam Jumatatu Mei 28, 2018
Makamu wa Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa na Mama Janeth Magufuri, Mama Mary Majaliwa, Mama Anna Mkapa na Mama Khadija Mwinyi wakiongea baada ya kupata futari iliyoandaliwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli Ikulu jijini Dar es salaam Jumatatu Mei 28, 2018
Kamishna Jenerali wa Uhamiaji Dkt. Anna Makakala (kulia) akiwa na Mama Evelyn Warioba wakiwa katika futari hiyo
Waalikwa wakibadilishana mawazo baada ya kufuturu Ikulu jijini Dar es salaam Jumatatu Mei 28, 2018
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa meza kuu na Rais wa Zanzibar Dkt. Ali Mohamed Shein pamoja na Mufti wa Tanzania Sheikh Aboubakary Zubery mara baada ya kufuturu Ikulu jijini Dar es Salaam. Kulia kwake ni Waziri wa masuala ya Dini kutoka Saudia Arabia Dkt. Saleh Abdulaziz Alashek na Makamu Mwenyekiti wa CCM (Bara) Ndg. Philip Mangula
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akifurahia jambo na Waziri wa masuala ya Dini wa Saudia Arabia Dkt. Saleh Abdulaziz Alashek na Makamu Mwenyekiti wa CCM (Bara) Ndg. Philip Mangula kwenye futari aliyoandaa
Ikulu jijini Dar es salaam Jumatatu Mei 28, 2018
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akiwa amekaa na Rais mstaafu wa awamu ya Tatu Benjamin Mkapa wa pili kutoka kulia, Rais mstaafu wa awamu ya pili Ali Hassan Mwinyi, Waziri Mkuu Mstaafu Mzee John Malecela, Makamu wa Rais Mstaafu Dkt. Mohamed Gharib Bilal, Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi pamoja na viongozi na wageni mbalimbali walioshiriki Futari iliyoandaliwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli Ikulu jijini Dar es Salaam.
Waalikwa wakimsikiliza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufulibaada ya futari aliyowaandalia Ikulu jijini Dar es Salaam.
Waalikwa wakimsikiliza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufulibaada ya futari aliyowaandalia Ikulu jijini Dar es Salaam.
Waalikwa wakimsikiliza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufulibaada ya futari aliyowaandalia Ikulu jijini Dar es Salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na wageni mbalimbali kutoka ndani na nje ya nchi walioshiriki katika futari aliyowaandalia Ikulu jijini Dar es Salaam.
Waalikwa wakimsikiliza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufulibaada ya futari aliyowaandalia Ikulu jijini Dar es Salaam.
Waalikwa wakimsikiliza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufulibaada ya futari aliyowaandalia Ikulu jijini Dar es Salaam.
Waalikwa wakimsikiliza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufulibaada ya futari aliyowaandalia Ikulu jijini Dar es Salaam.
Waalikwa wakimsikiliza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufulibaada ya futari aliyowaandalia Ikulu jijini Dar es Salaam.
Makamu wa Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa na Mama Janeth Magufuri, Mama Mary Majaliwa, Mama Anna Mkapa na Mama Khadija Mwinyi wakati wa futari iliyoandaliwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli Ikulu jijini Dar es salaam Jumatatu Mei 28, 2018
Waalikwa wakimsikiliza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufulibaada ya futari aliyowaandalia Ikulu jijini Dar es Salaam.
Waalikwa wakimsikiliza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufulibaada ya futari aliyowaandalia Ikulu jijini Dar es Salaam.
Waalikwa wakimsikiliza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufulibaada ya futari aliyowaandalia Ikulu jijini Dar es Salaam.
Waalikwa na viongozi mbalimbali wakimsikiliza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli baada ya futari aliyowaandalia Ikulu jijini Dar es Salaam.
Waalikwa na viongozi mbalimbali wakimsikiliza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli baada ya futari aliyowaandalia Ikulu jijini Dar es Salaam.
Waziri Mkuu Mhe Kassim Majaliwa na Rais Mstaafu Mhe. Benjamin Mkapa na waalikwa wengine wakimsikiliza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufulibaada ya futari aliyowaandalia Ikulu jijini Dar es Salaam.
Waalikwa wakimsikiliza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufulibaada ya futari aliyowaandalia Ikulu jijini Dar es Salaam.
Waziri wa masuala ya Dini wa Saudia Arabia Dkt. Saleh Abdulaziz Alashek akiongea baada ya futari Ikulu jijini Dar es salaam Jumatatu Mei 28, 2018
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimpongeza kwa hotuba Waziri wa masuala ya Dini wa Saudia Arabia Dkt. Saleh Abdulaziz Alashek bada ya futari Ikulu jijini Dar es salaam Jumatatu Mei 28, 2018
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimpongeza kwa hotuba Waziri wa masuala ya Dini wa Saudia Arabia Dkt. Saleh Abdulaziz Alashek bada ya futari Ikulu jijini Dar es salaam Jumatatu Mei 28, 2018
Mufti Mkuu wa Tanzania akiongea baada ya futari Ikulu jijini Dar es Salaam.
Waalikwa na viongozi mbalimbali wakimsikiliza Mufti Mkuu wa Tanzania akiongea baada ya futari Ikulu jijini Dar es Salaam.
Waalikwa na viongozi mbalimbali wakimsikiliza Mufti Mkuu wa Tanzania akiongea baada ya futari Ikulu jijini Dar es Salaam.
Waalikwa na viongozi mbalimbali wakimsikiliza Mufti Mkuu wa Tanzania akiongea baada ya futari Ikulu jijini Dar es Salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na wageni wake baada ya futari aliyowaandalia Ikulu jijini Dar es Salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na wageni wake baada ya futari aliyowaandalia Ikulu jijini Dar es Salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na wageni wake baada ya futari aliyowaandalia Ikulu jijini Dar es Salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiongea na Rais wa Zanzibar Dkt. Ali Mohamed Shein na Rais Mstaafu Mhe. Benjamin Mkapa baada ya kufuru Ikulu jijini Dar es Salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na Makamu wa Rais Mstaafu Dkt Mohamed Ghalib Bilali baada ya kufuru Ikulu jijini Dar es Salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na Rais mstaafu wa awamu ya pili Ali Hassan Mwinyi mara baada ya kufuru Ikulu jijini Dar es Salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiagana ujumbe kutoka Saudi Arabia mara baada ya kufuru Ikulu jijini Dar es Salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na Jaji Mkuu Profesa Ibrahim Juma baada ya kufuru Ikulu jijini Dar es Salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano Mhe. Job Ndugai baada ya kufuru Ikulu jijini Dar es Salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na Spika wa Baraza la Wawakilishi la Zanzibar Mhe. Zuberi Ali Maulid baada ya kufuru Ikulu jijini Dar es Salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na Shehe Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Alhad Mussa Salum baada ya kufuru Ikulu jijini Dar es Salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na Waziri wa Maliasili na Utalii Dkt. Hamisi Kigwangwalla baada ya kufuru Ikulu jijini Dar es Salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na IGP Simon Sirro baada ya kufuru Ikulu jijini Dar es Salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Jenerali Venance Mabeyo baada ya kufuru Ikulu jijini Dar es Salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na Inspekta Jenerali wa Magereza Dkt. Juma Malewa baada ya kufuru Ikulu jijini Dar es Salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na vingozi mbalimbali baada ya kufuru Ikulu jijini Dar es Salaam.
Rais mstaafu wa awamu ya Tatu Mhe. Benjamin Mkapa, Rais mstaafu wa awamu ya pili Ali Hassan Mwinyi, Waziri Mkuu Mstaafu Mzee John Malecela na Katibu Mkuu Mstaafu wa CCM Ndg. Abdulrahman Kinana wakitoka ukumbini baada ya futari.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiongea na Waziri wa masuala ya Dini wa Saudia Arabia Dkt. Saleh Abdulaziz Alashek na Balozi wa Saudi Arabia nchini Mhe. Mohamed bin Mansour al Malik baada ya kufuturu Ikulu jijini Dar es salaam Jumatatu Mei 28, 2018
Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa akisalimiana na Mkuu wa Majeshi ya Ulinsi Jenerali Venance Mabeyo baada ya futari
Waziri wa Maliasili na Utalii Dkt. Hamisi Kigwangwalla akiongea na wakuu wa wilaya za Kinondoni, Mhe. Ally Hapi, Temeke Mhe. Fekix Lyaniva na wa Kigamboni Mhe. Hashim Mgandilwa baada ya kufuturu
Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Jenerali Venance Mabeyo akizungumza na Mufti Mkuu wa Tanzania Sheikh Aboubakary Zubeiry Ally na Shehe Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Alhad Mussa Salum baada ya futari
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akisalimiana na Waziri Mkuu Mstaafu Dkt. Salim Ahmed Salim. Nyuma yake ni Waziri Mkuu Mstaafu Jaji Joseph Sinde Warioba baada ya kufuturu
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akisalimiana na IGP Simon Sirro baada ya kufuturu
Katibu Mkuu wa CCM mstaafu Ndg. Abdulrahman Kinana akiongea na Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Jenerali Venance Mabeyo, Inspekta Jenerali wa Magereza Dkt. Juma Malewa na IGP Simon Sirro
Mawaziri wakuu wastaafu Dkt. Salim Ahmed Salim na Jaji Joseph Sinde Warioba na wake zao Mama Evelyn Warioba na Mama Amne Salim
Makamu wa Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa ameongozana na Mama Janeth Magufuli na Kamishna Jenerali wa Uhamiaji Dkt. Anna Peter Makakala
Makamu wa Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan akisalimiana na IGP Simon Sirro
Makamu wa Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan akisalimiana na Katibu Mkuu wa CCM mstaafu Ndg. Abdulrahman Kinana
Makamu wa Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan akisalimiana na Makamu wa Rais Mstaafu Dkt. Mohamed Ghalib Bilali
Mama Janeth Magufuli akiwa na Mama Mary Majaliwa na Mama Asha Bilali na Mama Zakia Bilali
Mama Janeth Magufuli akisalimiana na Makamu Mwenyekiti wa CCM (Bara) Ndg. Philip Mangula
Mama Janeth Magufuli akisalimiana na Makamu wa Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan
Mama Janeth Magufuli akisalimiana na Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa
Mama Janeth Magufuli akiongea na Katibu Mkuu wa CCM Mstaafu Ndg. Abdulrahman Kinana
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na Waziri wa masuala ya Dini wa Saudia Arabia Dkt. Saleh Abdulaziz Alashek, Mufti Mkuu wa Tanzania Sheikh Aboubakary Zubeiry Ally na Shehe Mkuu wa Dar es salaam Alhad Mussa Salum baada ya kufuturu Ikulu jijini Dar es salaam Jumatatu Mei 28, 2018
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Mama Amne Salim
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimtambulsiha Jaji Mkuu wa Tanzania Profesa Ibrahim Juma kwa Waziri wa masuala ya Dini wa Saudia Arabia Dkt. Saleh Abdulaziz Alashek baada ya futari Ikulu jijini Dar es salaam Jumatatu Mei 28, 2018
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiongea na viongozi mbalimbali baada ya futari Ikulu jijini Dar es salaam Jumatatu Mei 28, 2018
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na Spika wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar Mhe. Zuberi Ali Maulid baada ya futari Ikulu jijini Dar es salaam Jumatatu Mei 28, 2018.Picha na IKULU
↧
MASHINDANO YA UMISETA KUANZA WIKI IJAYO JIJINI MWANZA
Waziri wa Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo Dk.Harrison Mwakyembe akimrushia mpira Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(TAMISEMI) Selemani Jafo
**********************
Mashindano ya michezo ya Umoja wa Michezo wa Shule za Msingi Tanzania (UMITASHUMTA) na Umoja wa Michezo ya Shule za Sekondari Tanzania (UMISETA) yanatarajiwa kufunguliwa rasmi tarehe 4 juni, 2018 jijini Mwanza.
Mashindano ya michezo ya UMISSETA ngazi ya Taifa yataanza tarehe 04 juni 2018 hadi tarehe 15 juni 2018 katika viwanja vya chuo cha ualimu cha butimba jijini Mwanza na kufuatiwa na mashindano ya UMITASHUMTA ambayo yatafanyika katika viwanja hivyo hivyo kuanzia tarehe 17 juni 2018 hadi tarehe 29 juni 2018.
Mashindano hayo ya UMISSETA na UMITASHUMTA yanatarajiwa kuonyeshwa moja kwa moja na Kituo cha Televisheni cha AZAM kutoka jijini Dar es salaam
Akizungumza kwenye ufunguzi wa matangazo ya moja kwa moja ya Televisheni ya AZAM uliofanyika katika uwanja wa Jamhuri jijini Dodoma, Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mheshimiwa Selemani Jafo alikipongeza kituo cha AZAM TV kwa kukubali kuyatangaza mashindano hayo ambayo ndiyo chimbuko la michezo nchini.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mheshimiwa Selemani Jafo akipiga mpira kuashiria ufunguzi wa matangazo mubashara ya mashindano ya UMITASHUMTA na UMISETA yatakayofanyika jijini Mwanza
Waziri Jafo alisema kuwa kwa namna ya pekee mwaka huu mashindano ya UMISSETA na UMITASHUMTA yataonyeshwa moja kwa moja na kwenye Televisheni na hivyo kuwawezesha watanzania kujionea vipaji mbalimbali vya watoto wao.
Pia Waziri Jafo aliwaagiza Maafisa Elimu wa Mikoa hasa wanaosimamia michezo nchini kuhakikisha wanawapeleka walimu wa michezo waliofundishwa katika shule za michezo ili wafundishe shule maalum zilizotengwa kuandaa vijana kimichezo.
“Waziri Ndalichako unasimamia sera na umetoa maelekezo kwa mujibu wa sera na hivi sasa kila mkoa tuna shule zipatazo mbili za michezo,na bahati nzuri kwa taarifa za wataalam wangu shule zile zimeanza kusimamiwa vizuri kwa kuinua vipaji vya vijana wetu ndani ya nchi yetu,naomba mlisimamie,”alisisitiza waziri Jafo.
Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof.Joyce Ndalichako akicheza mpira wa pete na mmoja wa wanafunzi.
Kwa upande wake Waziri wa Elimu, Sayansi, Teknolojia na Mafunzo ya Ufundi Profesa Joyce Ndalichako pamoja na kupongeza hatua hiyo ya AZAM TV pia aliagiza Mikoa kuhakikisha kuwa inatekeleza agizo la kutenga shule mbili maalum kwa ajili ya michezo na kuhakikisha kuwa mamlaka husika zinapeleka walimu waliosomea fani ya michezo
Naye Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Dkt. Harrison Mwakyembe aliipongeza hatua hiyo ya AZAM Televisheni kwani kuonekana kwa mashindano hayo kutachochea ari ya vijana wengi nchini kupenda michezo.
Mapema Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais TAMISEMI Bwana Tixon Nzunda alisema kuwa katika mashindano ya mwaka huu jumla ya wanamichezo 3,360 kutoka mikoa 28 ikiwemo miwili kutoka Zanzibar watashiriki kwenye UMISSETA ambapo michezo 10 itashindanishwa.
Bwana Nzunda aliongeza kuwa kwa upande wa UMITASHUMTA jumla ya wanamichezo 3120 kutoka mikoa 26 ya Tanzania bara watashiriki ikiwa ni wachezaji 120 kila mkoa.
Jumla ya michezo 9 ikiwemo mpira wa miguu wavulana na wasichana, mpira wa miguu maalum (wavulana viziwi), Netibali kwa wasichana, mpira wa wavu, mikono, kengele kwa wasioona, riadha maalum, riadha kawaida na sanaa za maonyesho.
Kikundi cha ngoma
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mheshimiwa Selemani Jafo akizungumza katika ufunguzi wa matangazo mubashara ya mashindano ya UMITASHUMTA na UMISETA yatakayofanyika jijini Mwanza.
Wanafunzi wa shule wakimsikiliza Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mheshimiwa Selemani Jafo.
↧
↧
TPA TANGA YAJIVUNIA KASI YA UTOAJI HUDUMA
MENEJA wa Bandari ya Tanga (TPA) Percival Salama kulia akimueleza Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji Charles Mwijage mipango ya bandari hiyo na namna walivyoboresha huduma zao kwa wafanyabiashara wanayoitumia
Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji Charles Mwijage akisalimia na Meneja wa Bandari ya Tanga Percival Salama mara baada ya kuwasili kwenye viwanja vya Mwahako Jijini Tanga alipokwenda kufungua maonyesho ya sita ya biashara ya kimataifa.
********************
MENEJA wa Bandari ya Tanga (TPA) Percival Salama amesema wanajivunia kuboreshwa huduma zao kwa kiwango kikubwa ikiwemo uandaaji wa nyaraka kwa kasi na usalama wa kutosha kwa wateja na hivyo kutumia muda mfupi kutokana na taasisi zinazohusika kuwepo sehemu moja hivyo kuwawia rahisi kuweza kufanya shughuli zao kwa wakati mmoja.
Salama aliyasema hayo wakati akizungumza na waandishi wa habari kwenye viwanja vya Mwahako Jijini Tanga kunakoendelea maonyesho ya kimataifa ya sita ya biashara ambapo alisema kutokana na hali hiyo hakuna sehemu ambayo mteja anaweza kupita akikwama bila wao kujua mara kila hatua wanazokuwa wakipitia wanatambua mara moja.
Alisema kuwa sehemu ambazo mteja anaingia kwenye bandari hiyo anapata taarifa moja kwa moja hiyo ikiwa wanakumbana na vikwazo vya namna yoyote zikijitokeza inawawia rahisi kuweza kuona na kuvishughulia kwa muda mfupi ili kuweza kuondoa usumbufu ambazo unaweza kuwakabili wafanyabiashara.
“Kwa kweli huduma za bandari ya Tanga tumeziboresha kwa kiasi kikubwa kutokana na kasi ya uandaaji wa nyaraka lakini hata usalama wa kutosha kwa wateja ambao wamekuwa wakiitumia hali iliyofanya kutumia muda mfupi kutokana na taasisi zinazohusika kuwepo sehemu moja hivyo kuwawia rahisi kuweza kufanya shughuli zao kwa wakati mmoja “Alisema.
Akizungumzia ujenzi wa gati,Meneja Salama alisema gati hilo litakalokuwa la usafirishaji wa mafuta ghafi kutoka Hoima nchini Uganda hadi Bandari ya Tanga hakutakuwa na uchimbaji eneo hilo kwani lina kina zaidi ya mita 20 linajisholeza na meli zinazotarajiwa kubeba tani laki moja hadi laki mbili na nusu kuingia na kufanya upakuaji.
“Sehemu ambayo serikali na TPA inataka kuchimba eneo ambalo kuna gati ya sasa kwa muda wa miaka 129 wanahudumia meli nangani kwani wanaona msingi wake uwezo wa Bandari ya Tanga ni shehena 750,000 lakini mwaka 2016 Bandari hiyo ilizidi kiwango cha uhudumiaji na kufikia tani 843,000 hivyo kutokana na matokeo hayo wakaona ipo haja ya kuboresha Bandari hii”Alisema.
Alisema mwaka Agosti 8 mwaka jana Rais Dkt John Magufuli akiwa mkoani Tanga alitoa maagizo kuwa anataka bandari ya Tanga inayohudumia mizigo sasa ichimbwe na meli zifike kwenye gati ambapo wao tayari wamekwisha kuanza utekelezaji wa agizo hilo.
Meneja huyo alisema wameanza kutekeleza maagizo hayo tayari mkandarasi wa BICO ameingia kazini na amesaini mkataba wa miezi minne kuanza kufanya kazi ya utafiti kwenye eneo la sasa la Bandari ili kujua chini ya bahari kuna udongo wa namna gani ili hatua nyengine ya kumpata mkandarasi kwa ajili ya ujenzi na ushauri zifanyike.
Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji Charles Mwijage kushoto akisisitiza jambo kwa Meneja wa Bandari ya Tanga Percival Salama mara baada ya kufungua maonyesho ya sita ya Kimataifa ya Biashara yanayoendelea kwenye viwanja vya Mwahako Jijini Tanga katikati ni Mkuu wa Mkoa wa Tanga,Martine Shigella.
↧
VIJANA 966 WAHITIMU MAFUNZO YA KIJESHI MLALE JKT
Mwakilishi wa mkuu wa Jeshi la kujenga Taifa(Jkt)Kanal Hassan Mabena kulia akisalimiana na Mkuu wa mkoa wa Ruvuma Christina Mndeme katika kikosi cha 842 Kj Mlale jana wakati mkuu wa mkoa alipkwenda kwa ajili ya kufunga mafunzo ya kijeshi na ujasiriamali kwa vijana 966 Operesheni Mererani.
Mkuu wa mkoa wa Ruvuma Christina Mndeme akiangalia Tikiti maji katika Bustani ya kikosi cha 842 Kj Mlale JKT mkoani Ruvuma alipokwenda kwa ajili ya kufunga mafunzo ya vijana Operesheni Mererani jana.
Mkuu wa kikosi cha 842 Kj Mlale Jkt Luteni Kanali Absolomon Shausi akimuonesha Mkuu wa mkoa wa Ruvuma sehemu ya Shamba la Mahindi ya chakula yanayolimwa na vijana wa jeshi la kujenga Taifa katika kikosi hicho.
Mkuu wa mkoa wa Ruvuma Christina Mndeme akitoa kitambaa kama Ishara ya kuweka jiwe la msingi la ujenzi wa jengo la mradi wa ufugaji Kuku katika kikosi cha 842 Kj Mlale mkoani Ruvuma,anayemsaidia kuondoa kitambaa ni mkuu wa kikosi hicho Lutewn Kanali Absolomon Shausi.
Baadhi ya vijana wa Jeshi la kujenga Taifa Operesheni Mererani 2018 waliopo katika kikosi cha 842 Kj Mlale wakionesha umahiri wa kuvuka vikwazo.
Mkuu wa mkoa wa Ruvuma Christina Mndeme akikagua Gwaride maalum la vijana wa kujitolea waliomaliza mafunzo ya miezi minne ya kijeshi katika kikosi cha 842 Kj Mlale wilayani Songea ambapo jumla ya vijana 966 walimaliza mafunzo ya kijeshi na ujasiriamali katika kikosi hicho.
Baadhi ya vijana waliohitimu mafunzo ya kijeshi na ujasiriamali katika kikosi cha 842 Kj Mlale Operesheni Mererani wakipita kwa mwendo wa haraka mbele ya mkuu wa mkoa wa Ruvuma Christina Mndeme(hayupo pichani)wakati wa kuhitimu mafunzo yao ya miezi minne katika kikosi hicho.
Mkuu wa mkoa wa Ruvuma Christina Mndeme akiongea na vijana,wazazi,Askari na maafisa mbalimbali wa jeshi la kujenga Taifa na Jeshi la Wananchi wa Tanzania katika kikosi cha 842 wakati wa kufunga mafunzo ya miezi minne ya kijeshi na Ujasiriamali kwa vijana 966 waliohitimu mafunzo yao jana,kushoto kwake ni mkuu wa kikosi cha 842 Kj Mlale Luten Kanal Absomlomon Shausi.
Picha na Muhidin Amri
↧
WIZARA YA ARDHI YAOMBA BILIONI 73 KWA MWAKA 2018/2019
WAZIRI wa Ardhi, Nyumba na Maedeleo ya Makazi, Willium Lukuvi akiwasilisha Bungeni hotuba ya makadirio ya mapato na matumizi kwa wizara yake kwa mwaka wa fedha 2018/2019 ambapo ameliomba Bunge kujadili na kuopitisha kiasi cha shilingi 73,071,273,632 iloi wizara iweze kutumiza majukumu yake.
Waziri, Lukuvi ameliambia Bunge kuwa katika mwaka wa fedha wa 2018/19 wizara inataraji kukusanya kiasi cha Shilingi Bilioni 120 kutokana na kodi, tozo, na ada mbalimbali za zinazotokana na shughuli za sekta ya ardhi kwa kutekeleza mikakati ambayo wamejiwekea.
Msemaji wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ardhi na Maliasili na Utalii, Halima Bulembo akisoma taarifa ya Kamati Bungeni leo.
Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Willium Lukuvi akijadili jambo na Naibu Waziri wake, Dk. Angelina Mabula Bungeni leo.
Wabunge wakiwa Bungeni jijini Dodoma leo
Wageni wakiwa Bungeni jijini Dodoma
Wabunge Munira Mustapha akijadili jambo na Hussein Bashe Bungeni jijini Dodoma.
Wageni wakiwa Bungeni wakifuatulia kikao cha Bunge leo. BOFYA HAPA KUONA ZAIDI.
Wabunge wakiwa Bungeni jijini Dodoma leo
Wabunge wakiwa Bungeni jijini Dodoma leo
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dk. Faustine Ndugulile akiwa Bungeni.
↧
TaESA WAKANUSHA TAARIFA YA TANGAZO LA AJIRA LINALOSAMBAA MTANDAONIl
WAKALA wa Huduma za Ajira Tanzania(TaEsa) umesema umesikitishwa na taarifa potofu ambazo zinasambazwa kupitia tangazo la ajira
Imefahamika taarifa hiyo inayosambaa kupitia tangazo hilo inasomeka ‘’CHINI YA MH:RAIS WETU DKT JOHN POMBE MAGUFULI KUPITIA SHERIA YA UANDIKISHAJI VIZAZI NA VIFO SURA 108 YA MWAKA 2000’’ kwamba tunatangaza ajira kwa vijana wote waliomaliza mafunzo ya uwalimu ngazi ya cheti,stashahada na waliosoma vyuo vya utumishi wa umma ngazi ya cheti.
Taarifa hiyo ya upotoshaji inaendelea kueleza mchakato wa usajili ajira linaratibiwa na RITA kwa kushirikiana na TaESA na kwamba maombi yameanza kupokelewa Mei 5 mwaka 2018 hadi Julai 7 mwaka 2018 na hivyo waombaji wote watume maombi yao kupitia barua pepe, taesa.ritarecruitment.go.tz@outlook.com.
Taarifa ya TaESA imesema leo jijini Dar es Salaam imefafanua tangazo hilo ni uzushi na utapeli wa wazi kwani RITA haina utaratibu wa kutangaza ajira kupitia utaratibu huo ulioainishwa hapo juu.
Imefafanuliwa badala yake ajira zote zinatangazwa kwa kufuata taratibu zilizowekwa na kusimamiwa na Sekretarieti ya Ajira na siyo TaESA.Aidha wamesena wanachukua fursa hiyo kuwatahadharisha wananchi kuhusu watu wanaojifanya kuwa ni Mawakala wa RITA chini ya Kampuni yao ya Mtema Brokers Limited ambao wanafanya kazi za usajili wa vizazi na vifo katika Mikoa mbalimbali Tanzania Bara.
TaESA imeelezwa watu hao ni matapeli hivyo yeyote mwenye taarifa sahihi afike kituo cha Polisi kilichopo karibu naye au awapigie kwa namba za simu hapo juu.Kampuni hiyo imeshawatapeli wananchi katika maeneo ya Kipunguni B,Temeke,Kinondoni,Kigamboni Sinza Jijini Dar es salaam na Mlandizi mkoani Pwani ambapo zaidi ya wananchi 1000 wametapeliwa fedha zao.
Afisa habari wa TaESA, Jamila Mbarouk akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) leo jijini Dar es Salaam , kuhusu kukanusha na kuwaomba wananchi wasitume fedha katika Kampuni ya Mtema Brokers Limited watatapeliwa pesa zao.
Afisa habari wa Wakala wa Usajili, Ufilisi na Udhamini (RITA),Jafari Hamadi akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) kuhusu kukanusha taarifa zilizo enea katika mitandao ya kijamii na kubandikwa katika semu mbalimbali unaosema kwamba wametangaza ajira, Tangazo hilo ni uzushi na utapeli wa wazi kwani RITA haina utaratibu wa kutangaza ajira kupitia utaratibu huo.(Picha na Emmanuel Massaka Globu ya jamii)
Mkutano ukiendelea.
↧
↧
BREAKING NEWS: DKT. BASHIRU ALLY APITISHWA NA NEC KUWA KATIBU MKUU WA CHAMA CHA MAPINDUZI (CCM)
Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi CCM Rais Dkt. John Pombe Magufuli akimpongeza Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi CCM Dkt. Bashiru Ally mara baada ya kumpendekeza na kupitishwa na wajumbe wote waliohudhuria kikao cha Halmashauri Kuu ya Taifa NEC Ikulu jijini Dar es Salaam.
Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi CCM Rais Dkt. John Pombe Magufuli akimkaribisha Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi CCM Dkt. Bashiru Ally kwenye meza kuu mara baada ya kumpendekeza na kupitishwa na wajumbe wote waliohudhuria kikao cha Halmashauri Kuu ya Taifa NEC Ikulu jijini Dar es Salaam.
Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi CCM Rais Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza mara baada ya Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi CCM Dkt. Bashiru Ally wapili kutoka kulia kwenye meza kuu kupitishwa na wajumbe wote waliohudhuria kikao cha Halmashauri Kuu ya Taifa NEC Ikulu jijini Dar es Salaam.
Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi CCM Rais Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na wajumbe wa NEC hawaonekani pichani, kushoto ni Makamu Mwenyekiti wa CCM-Zanzibar, Rais wa Zanzibar Dkt. Ali Mohamed Shein pamoja na Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi CCM Dkt. Bashiru Ally.
Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi CCM Dkt. Bashiru Ally akiwa meza kuu mara baada ya kupitishwa na wajumbe wote waliohudhuria kikao cha Halmashauri Kuu ya Taifa NEC Ikulu jijini Dar es Salaam.
Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi CCM Dkt. Bashiru Ally akiwashukuru Wajumbe wa NEC kwa kumpitisha kuwa Katibu Mkuu wa Chama Ikulu jijini Dar es Salaam.
Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi CCM Rais Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na wajumbe mara baada ya kikao cha NEC Ikulu jijini Dar es Salaam. PICHA NA IKULU.
↧
Watanzania watakiwa kujenga utamaduni wa kunywa maziwa kila siku kujenga afya,kuongeza pato la taifa.
Mkuu wa Wilaya ya Arusha Mheshimiwa Daniel Daqarro akiwa na wenyekiti wa bodi ya maziwa bwana Charles Malunde na Kaimu Mkurugenzi wa alaza la Kilimo Tanzania bwana Timothy Mbaga wakizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) katika maadhimisho ya wiki ya mifigo na maziwa,Jijini Arusha.
******************
Akizungumza na waandishi wa habari,Mkuu wa Wilaya ya Arusha Daniel Daqarro kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mrisho Gambo,amesema katika kuadhimisha wiki ya maziwa Mkoani Arusha, wananchi wanapaswa kujitokeza kwa wingi katika viwanja vya Themi Njiro maalufu kama viwanja vya nanenane.
Amesema maonyesho hayo ya wiki ya maziwa yanatija kubwa sana kwa wafugaji,wasindikaji na wananchi kwa ujumla kwani wataweza kujifunza juu ya umuhimu wa unywaji maziwa na ufugaji wa kisasa.Aidha,amewataka maafisa mifigo wote kuhakikisha wanasambaza elimu hiyo mpaka ngazi za chini kwenye jamii hususani namna ya ufugaji wa Ngo’mbe wachache na wenye tija.
Mwenyekiti wa bodi ya maziwa bwana Charles Malunde, amesema unywaji wa maziwa kwa Mtanzania mmoja ni wastani wa lita 47 kwa mwaka ukilinganisha na nchi nyingine za Afrika Mashariki ambapo wastani upo juu,hasa nchi ya Kenya ni lita 63 kwa Mwaka.
Amesema maziwa ni mlo kamili kwani yamebeba virutubisho vya aina zote vinavyoitajika katika mwili wa binadamu.Akisisitiza zaidi,amesema Tanzania ina takribani Ng’ombe milioni 30.5 ambapo Ngo’mbe milioni 27 niwakienyeji na wanatoa lita 1 hadi 1.5 ya maziwa kwa siku na milioni 1 ndio Ngo’mbe wa kisasa.
Tanzania ina idadi kubwa ya Ngo’mbe na hawana tija katika uzalishaji wa maziwa kwani Ngo’mbe wa kisasa wanauwezo wakutoa lita 30 hadi 40 za maziwa kwa siku.Kaimu Mkurugenzi wa balaza la Kilimo Tanzania bwana Timothy Mbaga,amesema maonyesho hayo ya 21 hayatakuwa na kiingilio chochote ili kutoa fursa zaidi kwa wafugaji kushiriki kwa wingi.
Pia maonyesho hayo yatawasaidia wafugaji kupata maarifa mbalimbali kutoka ndani na nje ya nchi na takribani makapuni 40 yameshathibitisha ushiriki.Maonyesho ya mifugo na wiki ya maziwa Kitaifa yatafanyika jijini Arusha kuanzia Mei 30 hadi Juni 1, 2018 katika viwanja vya Themi Njiro na yatafunguliwa na Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mheshimiwa Luhanga Mpina na kufungwa na Waziri wa Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mheshimiwa Selemani Jafo.
↧
Tanzania itaendelea kushiriki katika ulinzi wa amani duniani, Balozi Mahiga
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Balozi Dkt. Augustine Mahiga akihutubia katika maadhimisho ya miaka 70 ya Siku ya Walinda Amani Duniani yaliyofanyika katika viwanja vya Mashujaa vya Mnanzi Mmoja Jijini Dar es Salaam tarehe 29 Mei 2018.
********************
Siku ya Walinda Amani Duniani huadhimishwa tarehe 29 Mei ya kila mwaka ambapo kaulimbiu ya maadhimisho hayo kwa mwaka huu ni "Ulinzi wa Amani wa Umoja wa Mataifa: Miaka 70 ya huduma na kujitoa (UN Peacekeeping: 70 Years of Service and Sacrifice).
Katika hotuba yake, Mhe. Waziri Mahiga alieleza kuwa yapata miaka 12 tangu Tanzania ianze kushiriki katika ulinzi wa amani chini ya bendera ya Umoja wa Mataifa.
Pia akasisitiza Tanzania itaendelea kuwa mstari wa mbele katika kuhakikisha inasaidia kupatikana kwa amani katika mataifa mengine kwakuwa hakuna taifa linaloweza kufanikiwa katika maendeleo pasipo kuwepo na amani ya uhakika. " Sio jambo rahisi kukubali kutoa uhai wako kwa ajili ya mtu mwingine lakini Tanzania itaendelea kuungana na mataifa mengine duniani katika kusaidia kupatikana kwa amani ya mataifa hayo" alisema Mhe. Mahiga.
Aidha, Katika kuwakumbuka Walinda Amani wote Duniani waliopoteza maisha wakati wakitekeleza majukumu yao, pamoja na kutoa heshima kwa wale ambao bado wanaendelea na jukumu la kulinda amani, Tanzania imepoteza jumla ya askari wapatao 30 ndani ya miaka 10, pia dunia imepoteza zaidi ya askari 3500 na kwa sasa Tanzania inajivunia kuwa na jumla ya askari wapatao 2,600 wanaohudumu katika misheni sita (6) za ulinzi wa Amani za Umoja wa Mataifa.
Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) nchini, Bw. Alvaro Rodriguez akihutubia katika maadhimisho ya siku ya Walinda Amani Duniani ambapo alieleza pamoja na kuendelea kusimamia utekelezaji wa shughuli za maendeleo, Umoja wa Mataifa utaendelea kuhakikisha Dunia inakuwa mahali salama pa kuishi ili kuweza kuyafikia malengo ya maendeleo endelevu.
Mhe. Waziri Mahiga akiweka shada la maua katika Mnara wa Mashujaa uliopo Viwanja vya Mnazi Mmoja ikiwa ni sehemu ya kuenzi mchango wa Walinda Amani Duniani.
Wakitoa heshima kwa ajili ya kuwakumbuka Walinda Amani, waliosimama mbele kutoka kushoto ni Mhe. Waziri Mahiga akiwa na Mwakilishi kutoka Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ), Maj. Gen. Henry Kamunde, Bw. Alvaro Rodriguez na Mwakilishi kutoka Jeshi la Polisi Tanzania, Kamishna Nsato Marijani.
Mhe.Waziri Mahiga akisalimiana na Askari walioshiriki katika Misheni za Ulinzi wa Amani za Umoja wa Mataifa.
Mhe. Waziri Mahiga akisalimiana na sehemu nyingine ya Askari walioshiriki katika Misheni za Ulinzi wa Amani za Umoja wa Mataifa.
Kulia ni Kaimu Mkurugenzi Idara ya Ushirikiano wa Kimataifa, Bw. Deusdedit Kaganda pamoja na askari kutoka Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ) na Jeshi la Polisi Tanzania wakifuatilia hotuba ya Mgeni Rasmi.
Sehemu nyingine ya Askari na wageni waalikwa wakifuatilia hotuba ya Mgeni Rasmi.
Waheshimiwa Mabalozi na Wawakilishi wa Mashirika ya Kimataifa nchini wakifuatilia matukio mbalimbali katika maadhimisho hayo.
Sehemu nyingine ya Waheshimiwa Mabalozi, Wawakilishi wa Mashirika ya Kimataifa nchini na wageni waalikwa wakifuatilia matukio mbalimbali katika maadhimisho hayo.
Waheshimiwa Mabalozi na Wageni waalikwa wakifuatilia maadhimisho ya Siku ya Walinda Amani Duniani.
Gwaride la heshima kwa Mgeni Rasmi.
Askari wa JWTZ wakiingia viwanja vya Mnazi Mmoja.
↧