Quantcast
Channel: SUFIANIMAFOTO
Viewing all 13053 articles
Browse latest View live

MUDA WA KUSHUGHULIKIA MIZIGO MPAKANI RUSUMO WAPUNGUA

$
0
0
Na Veronica Kazimoto

Serikali ya Tanzania na Rwanda kupitia Mamlaka zake za Mapato zimefanikiwa kupunguza muda wa kushughulikia mizigo mpakani Rusumo mkoani Kagera kwa asilimia 73.
Hayo yamesemwa leo na Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Bw. Charles Kichere wakati wa Mkutano wa kwanza wa Kamati ya Uratibu wa Pamoja wa Mradi wa Maendeleo wa Kuwezesha Biashara na Udhibiti wa Mipaka Afrika Mashariki uliofanyika katika ukumbi wa Benki Kuu ya Tanzania, Zanzibar.
Kichere amesema kuwa, baadhi ya mafanikio muhimu ya mradi huu ni pamoja na uendeshaji wa Kituo cha Huduma za Pamoja Mpakani kwenye mipaka ya Rusumo na Namanga na maendeleo ya uwezo wa utendaji kazi wa maofisa wa forodha na mawakala.
"Mafanikio ya mradi huu yanaonekana wazi, kwa mfano tukichukulia mpaka wa Tanzania na Rwanda eneo la Rusumo, muda wa kushughulikia mizigo mpakani hapo umepungua kwa asilimia 73% yaani kutoka masaa manane na dakika 42 hadi kufikia masaa mawili na dakika 20 tu," alisema Kichere.
Mradi huu wa Maendeleo wa Kuwezesha Biashara na Udhibiti wa Mipaka Afrika Mashariki ni wa miaka mitatu na nusu ambao unafadhiliwa na Shirika la Kimataifa la Maendeleo la Japan (JICA) na ulizinduliwa rasmi mwezi Desemba, 2017.
Mradi huu unatekelezwa na Mamlaka tano za Mapato za nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki ambazo ni Tanzania, Burundi, Kenya, Rwanda na Uganda.
Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Bw. Charles Kichere (katikati) akizungumza wakati wa Mkutano wa kwanza wa Kamati ya Uratibu wa Pamoja wa Mradi wa Maendeleo wa Kuwezesha Biashara na Udhibiti wa Mipaka Afrika Mashariki uliofanyika leo Zanzibar. Kushoto ni Mhe. Audace Niyonzima wa Mamlaka ya Mapato Burundi na kulia ni Bw. Toshio Nagase Mwakilishi Mkazi wa JICA.
Baadhi ya wajumbe wa Mkutano wa kwanza wa Kamati ya Uratibu wa Pamoja wa Mradi wa Maendeleo wa Kuwezesha Biashara na Udhibiti wa Mipaka Afrika Mashariki ambao umefanyika leo Zanzibar.
Baadhi ya wajumbe wa Mkutano wa kwanza wa Kamati ya Uratibu wa Pamoja wa Mradi wa Maendeleo wa Kuwezesha Biashara na Udhibiti wa Mipaka Afrika Mashariki ambao umefanyika leo Zanzibar.
Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Bw. Charles Kichere (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya Makamishna Wakuu kutoka nchi za Afrika Mashariki na wajumbe wa Mkutano wa kwanza wa Kamati ya Uratibu wa Pamoja wa Mradi wa Maendeleo wa Kuwezesha Biashara na Udhibiti wa Mipaka Afrika Mashariki ambao umefanyika leo Zanzibar.

SEKTA YA FEDHA YATAKIWA KUONGEZA UBUNIFU KATIKA UTOAJI WA MIKOPO

$
0
0
Na Benny Mwaipaja, WFM, Dodoma
******************
SERIKALI imeitaka Sekta ndogo ya Benki kuongeza ubunifu kwa kutoa mikopo ya muda mfupi na mrefu ambayo itawezesha ukuaji wa sekta za viwanda na kilimo pamoja na wajasiriamali wadogo.
Hayo yamebainishwa Jijini Dodoma na Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT) Prof. Florens Luoga, kwa niaba ya Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Philip Mpango, katika Mkutano wa wadau wa Sekta ya Fedha uliowashirikisha wabunge, washirika wa Maendeleo, wakuu wa Taasisi za fedha na Wizara ya Fedha na Mipango.
Prof. Luoga alitoa wito huo kufuatia kuwepo kwa changamoto katika Sekta hiyo ikiwemo ukosefu wa uwekezaji wa miradi mikubwa ya maendeleo katika viwanda, kilimo na miundombinu pia ukosefu wa mikopo kwa wajasiriamali wadogo na wa kati.
“Kuna kiwango cha chini cha upatikanaji wa huduma za bima za kilimo, gharama kubwa za huduma za fedha, mifumo hafifu ya kuwalinda watumiaji wa huduma za fedha, ukosefu wa elimu ya fedha kwa wananchi na wananchi wengi kutofikiwa na huduma za fedha ambapo ni asilimia 8.6 tu ya nguvu kazi ya wananchi waishio vijijini wanapata huduma za benki ikilinganishwa na asilimia 32.1 ya nguvu kazi kwa wanaoishi mijini” alisisitiza Prof Luoga.

Gavana huyo wa Benki Kuu alisema kuwa ili kukabiliana na changamoto hizo, Serikali ilifanya maboresho ya Sekta ya Fedha katika eneo la ubinafsishaji wa benki za Serikali kurekebisha na kutunga sera na sheria mbalimbali hadi kufikia Desemba, 2017 ili kuweka misingi imara ya kuwezesha ukuaji, ushindani na ufanisi katika sekta ya fedha.
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango Dkt. Khatibu Kazungu akisisitiza kuhusu sekta ya fedha kuwa na mikakakati yenye tija katika kukuza uchumi wa viwanda wakati wa mkutano wa wadau wa sekta ya Fedha na Wizara ya Fedha na Mipango Jijini Dodoma.
Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT) Prof. Florens Luoga, akielezea kuwapo kwa changamoto ya kiwango cha chini cha upatikanaji wa huduma za bima za kilimo na gharama kubwa za huduma za fedha wakati wa mkutano wa wadau wa sekta ya Fedha na Wizara ya Fedha na Mipango Jijini Dodoma.
Kaimu Kamishna wa Sera za Fedha wa Wizara ya Fedha na Mipango Bw. Michael Nyagoga akielezea dhana ya Mkutano wa wadau wa sekta ya Fedha na Wizara ya Fedha na Mipango kuwa ni pamoja na kutatua changamoto mbalimbali za kifedha za Sekta ya Viwanda nchini.
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB Dkt. Charles Kimei, akisikiliza kwa makini wito wa Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT) Prof. Florens Luoga (hayupo pichani) kuhusu Sekta ndogo ya Benki kuongeza ubunifu kwa kutoa mikopo ya muda mfupi na mrefu ambayo itawezesha ukuaji wa sekta za viwanda, Jijini Dodoma.
Baadhi ya wakurugenzi wa taasisi za fedha na maafisa waandamizi wa Serikali kutoka Wizara ya Fedha na Mipango wakisikiliza maelezo ya Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango Dkt. Khatibu Kazungu (hayupo pichani) alipokua akieleza wajibu wa sekta ya fedha nchini katika kuwezesha viwanda vidogo vidogo, wakati wa mkutano wa wadau wa sekta ya Fedha na Wizara ya Fedha na Mipango Jijini Dodoma.
Wakuu wa taasisi za fedha wakiwa katika majadiliano na Wizara ya Fedha na Mipango Jijini Dodoma kuhusu mchango wa sekta ya fedha katika ukuaji wa viwanda nchini. 
Wakuu wa taasisi za fedha wakiwa katika picha ya pamoja na meza kuu wakati wa mkutano wa wadau wa sekta ya Fedha na Wizara ya Fedha na Mipango Jijini Dodoma.
Watumishi wa Wizara ya Fedha na Mipango wakiwa katika picha ya pamoja na meza kuu wakati wa mkutano wa wadau wa sekta ya Fedha na Wizara ya Fedha na Mipango Jijini Dodoma ulioangazia mchango wa sekta ya fedha katika ukuaji wa viwanda nchini.
(Picha na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini Wizaya ya Fedha na Mipango).

Mwili wa aliyekuwa Mbunge wa Buyungu Marehemu Mwl. Kasuku Bilago wasafirishwa

$
0
0

Naibu Spika wa Bunge, Mhe. Dkt. Tulia Ackson akizungumza wakati wa tukio la kuaga mwili wa aliyekuwa Mbunge wa Buyungu Marehemu Mwl. Kasuku Bilago katika Viwanja vya Bunge Jijini Dodoma. Mara baada ya tukio hilo mwili huo ulisafirishwa kwenda Wilayani Kakonko, Mkoani Kigoma kwa ajili ya mazishi.
Naibu Spika wa Bunge, Mhe. Dkt. Tulia Ackson akitoa heshima za mwisho wakati wa kuaga mwili wa aliyekuwa Mbunge wa Buyungu Marehemu Mwl. Kasuku Bilago. Mara baada ya tukio hilo mwili huo ulisafirishwa kwenda Wilayani Kakonko, Mkoani Kigoma kwa ajili ya mazishi
Naibu Spika wa Bunge, Mhe. Dkt. Tulia Ackson akiweka shada la maua wakati wa kuaga mwili wa aliyekuwa Mbunge wa Buyungu Marehemu Mwl. Kasuku Bilago. Mara baada ya tukio hilo mwili huo ulisafirishwa kwenda Wilayani Kakonko, Mkoani Kigoma kwa ajili ya mazishi
Naibu Spika wa Bunge, Mhe. Dkt. Tulia Ackson (wa pili kulia) akizungumza na Kiongozi wa Kambi ya Upinzani Bungeni Mhe. Freeman Mbowe (wa pili kushoto), Mbunge wa Vunjo, Mhe. James Mbatia (kushoto) na Mbunge wa Bunda Mjini, Mhe. Esther Bulaya (kulia) wakati wakusafirisha mwili wa aliyekuwa Mbunge wa Buyungu Marehemu Mwl. Kasuku Bilago katika Uwanja wa Ndege wa Jijini Dodoma.

MGANGA MFAWIDHI KAKONKO AJINYONGA KWA TAULO, DC ASHANGAZWA

$
0
0

Na Rhoda Ezeikel Kigoma,

MGANGA Mfawidhi wa Kituo cha Afya Kakonko wilayani Kakonko mkoani kigoma Dk.Mejo Banikila ( 43 ) amekutwa amejinyonga chumbani kwake kwa kutumia taulo.
Hayo yamebainishwa na Mkuu wa Wilaya ya Kanali Hosea Ndagala alipokuwa akizungumzia tukio hilo na kwamba wakati alipofika nyumbani kwa marehemu huyo kuangalia tukio hilo ameelezwa tukio hilo limetokea usiku wa kuamkia jana ambapo Dk.Banikila alikutuwa amejinyonga.
Kanali Ndagalla amesema matukio ya watu kujinyonga katika wilaya ya Kakonko yamekuwa yakiongezeka na wanaendelea na uchunguzi ili kubaini sababu hasa za watu kuchukua maamzi magumu kama hayo.
Aidha Mkuu huyo amewataka wananchi kuhudhuria Kanisani na misikitini ili kusikiliza mahubiri na kupunguza msongo wa mawazo kwa kuwaeleza wenzao ilikwaweze kuwashauri na kuepukana na tatizo hili la Wananchi kujinyonga.
Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Kigoma Martin Otieno alithibitisha kutokea tukio hilo na kuwaomba wananchi kuacha kuchukua maamuzi ya kujinyonga kwa sababu yeyote ile kwakuwa ni matukio ambayo yameendelea kutokea nchini na kwamba wanaendelea na uchunguzi kujua sababu iliyosababisha mganga huyo kuchukua uamuzi huo.
Kwa upande wao baadhi ya wapangaji wenzake wamesema kwa muda wa miezi nane wameyo ishi naye wameishi nae vizuri licha ya kuwa siku mbili kabla ya tukio amekuwa akionekana mnyonge mpaka tukio hilo kutokea .
Walisema Mganga huyo alikuwa akifanya kazi zake vizuri na amekuwa akijitoa sana kuhakikisha wagonjwa wanapata huduma kwa wakati na kwamba watamkumbuka kwa Mambo mengi.

WAZIRI WA AFYA ZANZIBAR AFANYA ZIARA YA KUTEMBELEA KITUO CHA AFYA RAHALEO NA MAKAAZI YA MADAKTARI WA CHINA NA CUBA

$
0
0
MUUGUZI wa Kitu cha Afya Rahaleo Wanu Amour akimuonyesha kichupa cha chanjo ya watoto Waziri wa Afya Hamad Rashid Mohamed (mwenye suti) alipofanya ziara ya kutembelea kituo hicho .
**************************
Na Ramadhani Ali – Maelezo Zanzibar.

Waziri wa Afya Hamad Rashid Mohamed amesisitiza msimamo wake wa kufuatilia na kupambana na Wafanyakazi wakorofi wenye tabia ya kuwatolea lugha chafu wagonjwa wanapofika vituo vya afya kutafuta huduma.
Amesema Wafanyakazi wengi wa vituo vya afya ni wazuri na wanatekeleza wajibu wao kwa uadilifu mkubwa lakini bado wapo wafanyakazi wachache wenye tabia ya kuwanyanyasa wagonjwa na kuwaharibia sifa nzuri wenzao. Waziri Hamad Rashid ameeleza hayo alipokuwa akizungumza na Wafanyakazi wa Kituo cha afya cha Rahaleo baada ya kufanya ziara ya ghafla katika kituo hicho.
Aliwakumbusha wafanyakazi wa sekta ya afya kuwa kilio kikubwa cha Wananchi kilikuwa ni upungufu wa dawa na lugha mbaya kwa wagonjwa lakini tatizo la dawa Serikali imelipatia ufumbuzi. Aliwataka wafanyakazi wa afya kubadilika na kuwafanyia wema na kuwapa upendo wananchi wanapofika katika vituo vyao kwa vile lugha nzuri inawapa nafuu wagonjwa .
WAZIRI wa Afya Hamad Rashid Mohamed akizungumza na Madaktari wa Kichina wanaofanya kazi Zanzibar alipotembelea Makaazi yao Mtaaa wa Vuga Mjini Zanzibar.

Hata hivyo Waziri wa Afya amewataka wagonjwa na jamaa za wagonjwa wanapofika vituo vya afya kufuata taratibu zilizowekwa ili kujenga maelewano mazuri na wafanyakazi. Aidha Waziri Hamad Rashid ameziagiza Manispaa na Mabaraza ya Miji kuimarisha usafi katika vituo vya afya kufuatia uamuzi wa Serikali wa kufanya ugatuzi na vituo hivyo kuwa chini yao.
Mfanyakazi wa Maabara wa Kituo cha Rahaleo Ineneni Fadhil Abdalla alimueleza Waziri Hamad kuwa baadhi ya wananachi wanaopeleka wagonjwa vituo vya afya wamekuwa chanzo kikubwa cha kuvuruga uhusiano mwema baina yao na wagonjwa. Amewashauri wananchi kwa upande wao kuwa wavumilivu na kuwasaidia wanapofika kupatiwa huduma ili kazi zao ziwe nyepesi zaidi.
KIONGOZI wa Madaktari kutoka Cuba Dkt. Katia Duany Baderas akizungumza na Waziri wa Afya Hamad Rashid Mohamed (alievaa suti) alipotembelea katika Makaazi yao Vuga (kulia) Naibu Waziri wa Afya Harusi Said Suleiman na wapili (kushoto) Mkurugenzi Utumishi Wizara ya Afya Ramadhani Khamis Juma .

Wakati huo huo Waziri wa Afya alitembelea makaazi ya Madaktari wa China na Cuba katika mtaa wa Vuga na kuwashukuru kwa kazi nzuri wanayofanya ya kuwahudumia wananchi wa Zanzibar. Alitoa pongezi maalum kwa Serikali ya Cuba kwa msaada mkubwa uliopelekea kuanzishwa shahada ya kwanza katika Chuo cha Taaluma za Sayansi za afya na kukubali kuwapokea wanafunzi wanaochuka shahada hiyo kwa masomo zaidi katika nchi yao.
Amewaomba wahadhiri wa Cuba wanaofundisha Chuo hicho kutoa ushauri kwa Wizara ya afya juu ya kuimarisha huduma ya afya ya msingi na mbinu zitakaosaidia kupunguza idadi ya wagonjwa wa Zanzibar wanaopelekwa nje kwa ajili ya matibabu.
DAKTARI dhamana wa Kituo cha Afya cha Rahaleo Ashura Miraji Mpatani akizungumzia changamoto na mafanikio ya Kituo cha Afya cha Rahaleo wakati wa ziara ya Waziri wa Afya Hamad Rashid (hayupo pichani).
WAZIRI wa Afya Zanzibar Hamad Rashid Mohamed akizungumza na Wafanyakazi wa Kituo cha Afya Rahaleo wakati wa ziara yake katika Kituo hicho. PICHA NA ABDALLA OMAR.

WANAFUNZI ZAIDI YA 600 WA DARASA LA TATU WASOMA KWENYE CHUMBA KIMOJA

$
0
0

Na Rhoda Ezekiel Kigoma, 

WANAFUNZI zaidi ya 600 wa darasa la tatu katika Shule ya Msingi Kumkambati Kata ya Nyamidaho wilayani Kasulu mkoani Kigoma, wanalazimika kusoma katika chumba kimoja kutokana na uhaba wa madarasa na wingi wa wanafunzi.
Hali hiyo imewalazimu wazazi kuanzisha ujenzi wa shule nyingine Katika vijiji jirani vya Kumtundu na Mkuyuni.Hayo yalibainika jana wakati wa ziara ya Mkuu wa Wilaya ya Kasulu Brigedia Jenerali Marco Gaguti wakati akitembelea miradi ya Wilaya hiyo ilioanzishwa na wananchi na inayofadhiliwa na Serikali.
Ambapo alifika katika Shule ya Msingi Kumtundu iliyoanza kujengwa kwa juhudi za wananchi wa kijiji hicho ili kupunguza wingi wa wanafunzi katika shule iliyopo katika Kijiji jirani cha Mvungwe.
Akitoa taarifa ya shule hiyo Mkuu wa Shule ya Msingi Kumkumbati Falesi Lugati amesema hhule hiyo inajumla ya wanafunzi 2024 na jumla ya walimu 14 na darasa la tatu ndilo lina wanafunzi 600, ambapo wanalazimika kuwagawa awamu mbili ya asubuhi na mchana kwa lengo a kuwaweze kuwafundisha na kumpunguzia mzigo mwalimu anaefundisha darasa hilo .
Amesema shule hiyo inahudumia wanafunzi wa vijiji viwili na wameanza kutatua tatizo la mrundikano wa wanafunzi kwa kujenga vyumba viwili vya madarasa, na wananchi wa Kijiji cha Mkumtundu wameanza ujenzi wa shule mpya itakayo saidia kupunguza wanafunzi waliopo katika shule hiyo kuhamia katika shule jirani inayojengwa.
Akisoma taarifa ya ujenzi wa Shule hiyo Katibu wa kamati ya ujenzi wa Shule ya Msingi Kumtundu Raphael Zacharia amesema wameanza ujenzi wa madarasa manne na ofisi moja na ujenzi wa msingi na ukuta pamoja na upauaji umekalika na jumla ya ghalama ni Sh. milioni 14 na Sh.milioni 11 zimechangwa na wananchi na Waziri wa Elimu alichangia Sh. milioni tatu. 
Amesema changamoto ni upungufu wa vifaa vya ujenzi uhaba wa kifungu cha fedha kuwalipa mafundi na kuomba Serikali kuunga mkono kuchangia vifaa vya ujenzi ili kukamilisha ujenzi pamoja na upatikanaji huduma za maji.
Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Kasulu Brigedia Jenerali Marco Gaguti aliwapongeza wananchi kwa hatua hiyo waliyoichukua ya kuona upungufu wa vyumba vya madarasa na kuona wanafunzi wanavyoteseka na kuamua kutafuta shule nyingine ili kutatua tatizo la wanafunzi kutembea umbali mrefu kufuata huduma ya shule.
Amesema ataendelea kuhimiza fedha inayotakiwa kutolewa kwa ajili ya kumalizia shule hiyo ianze, na kuahidi kuchangia Sh.milioni mbili kutoka katika Mfuko wa Mkuu wa Wilaya ili kuiongezea kwenye vifaa ambavyo bado havija nunuluwa.
Aidha Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Kasulu Godfrey Kasekenya amesema wamejipanga shule hiyo inakamilika Januari mwaka 2019 wanafunzi wanaanza kusoma na wao kama halmashauri wamejiandaa kukamilisha matundu 10 ya vyoo kupitia mfuko wa EPFORR kiasi cha Sh. milioni nane zimetengwa kwaajili ya shughuli hiyo.
Brigedia Jenerali Gaguti alitembelea vituo viwili vya Afya vya Nyamidaho na Nyakitonto Vituo vya Afya vinavyo jengwa kwa fedha za Serikali Kuu kwa kutuma uraratibu wa Force Account ambapo aliwapongeza viongozi wa vijiji na wananchi kwa kujitolea kukamilisha ujenzi huo kwa gharama nafuu na kazi inaendelea vizuri na kuwataka Wananchi wote kuendelea kushirikiana na Serikali katika shughuli.

RC Wangabo kutumia nguvu ya dola kukomesha Kipindupindu

$
0
0
Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Mh. Joachim Wangabo (wa pili toka kushoto) akiwa Mkuu wa Wilaya ya Sumbawanga Dkt. Khalfan Haule (wa kwanza kushoto pamoja na timu ya afya ya wilaya na kamati ya ulinzi na usalama ya mkoa wakikagua vyoo katika Kijiji cha Namasinzi, Kata ya kapenta, Wilayani Sumbawanga.
**********************

Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Mh. Joachim Wangabo amesema atalazimika kuwatumia polisi kusimamia zoezi la usafi na ujenzi wa vyoo salama katika Kijiji cha Namasinzi, kata ya Kapenta, bonde la ziwa Rukwa Wilayani Sumbawanga baada ya wananchi hao kushindwa kujenga vyoo hivyo mbali na elimu ya umuhimu wa vyoo waliyopewa kwa muda mrefu.
Amesema kuwa ikifikia hatua hiyo Kijiji hicho kitafungiwa na hakuna atakayetoka wala kuingia na hatimae kusitisha shughuli za kiuchumi za Kijiji hicho ambacho ni maarufu kwa kilimo cha mpunga hali itakayopelekea maisha magumu kwa wananchi hao jambo ambalo asingependa litokee.
Katika kuhakikisha hali hiyo haitokei Mh. Wangabo alimuagiza Mkuu wa Wilaya ya Sumbawanga Dk. Khalfan Haule na timu yake ya usafi ya halmashauri kuhakikisha wanapita kaya kwa kaya ili kuzibaini kaya zisizopenda usafi na zisizokuwa na vyoo na kuzichukulia hatua za kisheria kwani kwa kushindwa kufanya hivyo kipindupindu hakitamalizika katika bonde hilo.
“Sasa tutatumia nguvu ya dola, ili kuhakikisha kwamba kila mtu anaishi katika maisha ya usafi wala sio uchafu, na kila mtu ahakikishe kwamba anakuwa na kiboko Fulani ambacho ni kigumu amuone mtu anachemsha maji, anayaweka maji yake yanapoa akienda shambani anakwenda na maji mbayo yamekwisha poa, lakini mkilea lea hivi, waswahili wanasema ukicheka na nyani unavuna mabua, mabua ambayo tunayavuna ni vifo.” Alisisitiza.
Aliyasema hayo katika Mkutano wa hadhara alioufanya katika kijiji cha Namasinzi, Kata ya Kapenta, Wilayani Sumbawanga, kijiji ambacho wananchi watatu wamefariki kwa ugonjwa wa kipindupindu na wengine wakiendelea kupatiwa huduma. 
Kwa upande wake Mganga Mkuu wa hlamshauri ya Wilaya ya Sumbawanga Dkt. Fani Musa aliendelea kuishukuru serikali kwa kuendelea kupeleka misaada katika bonde hilo ili kuhakikisha wanakabiliana na ugonjwa huo na kusisitiza kuwa wataendelea kutoa elimu bila ya kuchoka akiamini kuwa wananchi hao wataelewa wakiendelea kusimamiwa.
“Serikali imekuwa ikifanya kazi tatu kwa wakati mmoja, tumekuwa tukitoa elimu ya ugonjwa huu kwa lengo la kuzuia haya yasitokee, lakini yakitokea tunatumia nguvu kubwa ya kukabiliana na tatizo hili lakini pia serikali inatoa dawa za kutosha ili kuweza kuponya pia, ugonjwa wa kipindupindu ni kitendo cha kula kinyesi ambacho ni kibichi, hivyo watu ni muhimu kujenga vyoo salama,” Alimalizia.
Tangu kulipuka kwa ugonjwa huo tarehe 6 Mei, 2018 watu 14 wameshafariki na wengine 221 wakiendelea na kupatiwa matibabu katika kambi za wagonjwa hao katika bonde la ziwa Rukwa, Wilayani Sumbawanga.
Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Mh. Joachim Wangabo (kulia) akikabidhi tenki la lita 5000 kwa mwenyekiti wa kitongoji cha Liweliyamvula, Kijiji cha Lumbesa, Kata ya Kapenta, Wilayani Sumbawanga Paulo Maufi, ikiwa ni miongoni mwa juhudi za serikali kuhakikisha wananchi wanapata maji safi na salama na kuhifadhiwa sehemu salama, kuepukana na kipindupindu.
Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Mh. Joachim Wangabo (kulia) akikabidhi dawa za “Water guard” kwa mwenyekiti wa kitongoji cha Liweliyamvula, Kijiji cha Lumbesa, Kata ya Kapenta, Wilayani Sumbawanga Paulo Maufi, ikiwa ni miongoni mwa juhudi za serikali kuhakikisha wananchi wanapata maji safi na salama, kuepukana na kipindupindu.

WATUMISHI WATATU WA HALMASHAURI YA KALIUA MATATANI KWA KUSHINDWA KUONYESHA ZILIPO MILIONI TATU ZA UJENZI WA MADARASA

$
0
0


NA TIGANYA VINCENT, TABORA
MKUU wa Mkoa wa Tabora Aggrey Mwanri ameagiza kuchukuliwa hatua kwa watumishi watatu wa Halmashauri ya Wilaya ya Kaliua kwa tuhuma za kukiuka taratibu za manunuzi wakati wa ujenzi wa vyumba viwili vya madarasa katika Shule ya Msingi Susitila na hivyo kusababisha upotevu wa milioni tatu za nguvu za wananchi. Hatua hiyo ilitokana na taarifa ya Mkaguzi wa Ndani wa Halmashauri hiyo kubaini ukiukwaji wa taratibu mbalimbali zilisababisha shilingi milioni tatu kutokuwa na maelezo juu ya matumizi yake.
Alisema jengo hilo ambalo bado halijakamilika linaoonyesha kutumia milioni 6 ambazo hazilinganisha na hali halisi lilipofikia jengo wakati katika shule za jirani ya Imalampaka imetumia milioni mbili kujenga vyumba viwili vya madarasa hadi kufikia hatua ya kuezekwa. Mkuu huyo wa Mkoa alimwagiza Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Kaliua kuhakikisha anawachukulia hatua ikiwemo kurudisha shilingi milioni tatu ambazo hazionekana matumizi yake, kushushwa vyeo na kuondolewa katika nafasi zao kwa wale ambao watabainika kutenda kosa.
Alisema hatua isipochukuliwa inawakatisha tamaa wananchi ambao wanajitolea nguvu zao katika kuchangia miradi ya maendeleo huku fedha zikiishia mifukoni mwa wachache. Awali Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya hiyo Dkt. John Pima akitoa taarifa ya ukaguzi maalumu alisema Mkaguzi amebaini ukiukaji wa Sheria, taratibu, kanuni na utoaji wa taarifa za uongo kwa viongozi na umma.
Alisema Kaimu Mtendaji wa Kijiji cha Mtakuja Josephine Benjamin alishindwa kutimiza wajibu na hivyo kutozingatia sheria, taratibu na kanuni wakati wa ukusanyaji na matumizi ya fedha zilizotokana na michango ya wananchi.
Dkt. Pima alisema kwa upande naye Kaimu Mkuu wa Shule ya Susitila Juma Kitwama alitoa taarifa za uongo kwa Mkuu wa Mkoa na umma kwa kutoa taarifa ambayo hakuwa na uhakika nayo juu matumizi ya milioni sita zilizotokana na michango ya wananchi.
Dkt. Pima aliongeza mtuhumiwa huyo pia alishindwa kutoa viambatanisho vinavyothibitisha matumizi ya fedha hizo na kusema kuwa hana viambatisho vya matumizi ya fedha hizo kwa kuwa alipewa taarifa hiyo kutoka kwa aliyekuwa Kaimu Mtendaji wa Kijiji cha Susutila Mussa Elias.
Mapema wiki iliyopita Mkuu wa Mkoa wa Tabora akiwa katika ziara ya ukaguzi wa miradi ya ujenzi wa vyumba vya madarasa katika Wilaya mbalimbali alisimamisha ujenzi wa vyumba viwili vya madarasa baada ya kutoridhishwa na taarifa ya matumizi ya fedha katika mradi huo na kuagiza Mkaguzi wa Ndani wa Halmashauri kupitia na kisha kutoa taarifa kwake.
Alichukua uamuzi huo ikiwa ni sehemu ya kutaka kuzuia ubadhirifu ambao ungeweza kutokana na fedha nyingine milioni 24 walizopatiwa na Serikali kupitia Equip T ili kukamilisha mradi huo.

WAZIRI MKUU MAJALIWA AZINDUA MAADHIMISHO YA MIAKA 15 TANGU KUANZISHWA KWA MFUKO WA DHARURA WA RAIS WA MAREKANI WA KUPAMBANA NA MAAMBUKIZI YA VIRUSI VYA UKIMWI (PEPFAR)

$
0
0
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza wakati alipozindua Maadhimisho ya Miaka 15 Tangu Kuanzishwa kwa Mfuko wa Dharura wa Rais wa Marekani wa Kupambana na Kudhibiti Maambukizi ya Virusi vya Ukimwi (PEPFAR) kwenye Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere jijini Dar es salaam, Mei 30, 2018.
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu akizungumza katika Uzinduzi wa Maadhimisho ya Miaka 15 Tangu Kuanzishwa kwa Mfuko wa Dharura wa Rais wa Marekani wa Kupambana na Kudhibiti Maambukizi ya Virusi vya Ukimwi (PEPFAR) kwenye Kituo cha Kimataifa cha Mikutano cha Julius Nyerere jijini Dar es salaam, Mei 30, 2018.Uzinduzi huo ulifanywa na Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu (kulia) na Kaimu Balozi wa Marekani Nchini, Dkt. Inmi Patterson kabla ya Kuzindua Maadhimisho ya Miaka 15 Tangu Kuanzishwa kwa Mfuko wa Dharura wa Rais wa Marekani wa Kupambana na Kudhibiti Maambukizi ya Virusi vya Ukimwi (PEPFAR) kwenye Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere jijini Dar es salaam, Mei 30, 2018.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Kaimu Balozi wa Marekani Nchini, Dkt. Inmi Patterson wakati alipowasili kwenye Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere jijini Dar es salaam kuzindua Maadhimisho ya Miaka 15 Tangu Kuanzishwa kwa Mfuko wa Dharura wa Rais wa Marekani wa Kupambana na Kudhibiti Maambukizi ya Virusi vya Ukimwi (PEPFAR), Mei 30, 2018.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiagana baadhi ya viongozi walioshiriki katika Uzinduzi wa Maadhimisho ya Miaka 15 Tangu Kuanzishwa kwa Mfuko wa Dharura wa Rais wa Marekani wa Kupambana na Kudhibiti Maambukizi ya Virusi vya Ukimwi (PEPFAR) Kwenye Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere jijini Dar es salaam, Mei 30, 2018. Kutoka kulia ni Dkt. Janet Mwambona wa Taasisi HIV/AIDS Treatment Advisor,Walter Reed Army Institute Of Research, Brian Rettmann ambaye ni Mratibu wa PEPFAR nchini, Dkt. Leonard Maboko, Mkurugenzi Mtendaji wa Tume yaTaifa ya Kudhibiti Ukimwi Tanzania na wanne kulia ni Kaimu Balozi wa Marekani nchini, Inmi Patterson.(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu.

Dkt. Abaasi Awataka Wanahabari Kutumia Kalamu Zao Kupunguza ajali.

$
0
0
Mkurugenzi wa Idara ya Habari-MAELEZO na Msemaji Mkuu wa Serikali, Dkt. Hassan Abbasi akiongea wakati wa ufunguzi rasmi wa mafunzo maalum kuhusu uandishi wa habari za usalama barabarani jana jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi wa Idara ya Habari-MAELEZO na Msemaji Mkuu wa Serikali akimkabidhi vitendea kazi mwandishi wa Gazeti la Habarileo, Evance Ng’ingo ambaye anashiriki mafunzo maalum ya miezi sita kuhusu usalama barabarani.

Mkurugenzi wa Idara ya Habari-MAELEZO na Msemaji Mkuu wa Serikali, Dkt. Hassan Abbasi amewataka waandishiwa habari nchini kutumia taaluma ya habari kuielemisha jamii juu ya usalama barabarini ili kupunguza ajali ambazo zimeendelea kusababisha vifo visivyo vya lazima na ulemavu wa maisha.
Dkt. Abbasi ametoa wito huo leo jijini Dar es Salaam wakati akifungua mafunzo maalumu ya miezi sita juu ya uandishi bora wa habari zinazohusu usalama barabarani, kwa waandishi wa habari 17 kutoka vyombo mbalimbali vya habari nchini.
Ameeleza kuwa ajali za barabarani zitapungua kwa kiwango kikubwa endapo waandishi wa habari watatumia taaluma yao kuielemisha jamii juu ya usalama barababrani, kupaza sauti za wananchi pale palipo na changamoto zinazohitaji usimamizi wa Serikali na pia kuwa sehemu ya mageuzi yanayofanywa na Serikali kuwaondolea wananchi changamoto za ajali.
“Zaidi ya watu milioni moja na laki mbili hufariki kila mwaka duniani kutokana na ajali za barabarani na kati ya vifo hivyo asilimia 90 hutokea katika nchi zinazoendelea ikiwemo Tanzania. Wengi wanaofariki kwa ajali ni watu wenye umri wa kati ya miaka 15-29 na hivyo kuwa na atahari kubwa kiuchumi na kijamii,” alieleza Dkt. Abbasi.
Amewataka washiriki wa mafunzo hayo kuzingatia kwa umakini mafunzo watakayopata ili watumie maarifa watakayoyapata kuleta mabadiliko chanya kwa jamii na wadau wa usalama barabarani. Nae Mkurugenzi wa Uhakiki na Ubora kutoka Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. Mohamed Mohamed, amesema kuwa Wizara pamoja na Shirika la Afya Duniani (WHO) wameona ni muhimu waandishi wa habari kuwa na ufahamu wa kutosha juu ya masuala ya usalama barabarani kwa kuwa wao wana nafasi kubwa ya kufikisha elimu hiyo kwa jamii kubwa zaidi.
Dkt. Mohamed ameeleza kuwa watu wengi wamekuwa wakipoteza maisha katika ajali kutokana na sababu nyingi ikiwemo majeruhi kukosa huduma za haraka pindi ajali inapotokea kutokana na hospitali kuwa mbali. Amesema kuwa ili kukabiliana na changamoto ya majeruhi kukosa huduma za haraka wakati wa ajali, Wizara ipo katika hatua za mwisho kuweka vituo vya kutolea huduma za dharua (Emergency Medicine Services Centre) katika barabarani kuu ziendazo mikoani ambapo vitarahisisha kuwapatia huduma za haraka majeruhi wa ajali.
Waandishi wanaoshiriki mafunzo haya ni pamoja na Abadallah Msuya kutoka Daily News, Evance Ng’ingo na Adam Ruta kutoka Habarileo, Agness Mbapu kutoka TBC, Beaty Tesha kutoka TBC Taifa, Aisia Rweyemamu na Chrispin Gerald kutoka The Guardian, Dickson Kanyika kutoka Star Tv na Radio Free Africa, Herrieth Makweta kutoka Mwananchi na Jasmin Shamweku kutoka Redio ABM ya Dodoma.
Waandishi wengine ni Juhudi Felix kutoka FADECO Wilayani Karagwe, Margaret Malisa kutoka Nipashe, Renatus Mutabuzi kutoka ITV, Sylvanus Kayela kutoma Mlimani TV, Veronica Mrema kutoka Mtanzania na Vumilia Kondo kutoka Abood Media ya Morogoro. Mafunzo haya usalama barabarani kwa waandishi wa habari ni ya tangu kuanzishwa kwake mwaka 2016 kwa ushirikiano kati ya Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, na Shirika la Afya Duniani.

DC SANGA ATOA TATHMINI YA AWALI YA MAAFA YA MVUA MKURANGA

$
0
0
Mwenyekiti wa halmashauri ya Mkuranga ,Juma Abeid akizungumza jambo katika kikao cha baraza la madiwani ,wa kulia ni Mkurugenzi wa halmashauri hiyo ,Mshamu Munde.
Na Mwamvua Mwinyi,Mkuranga.

MWENYEKITI wa kamati ya ulinzi na usalama wilayani Mkuranga, Filberto Sanga, ametoa tathmini ya awali ya maafa yaliyotokea katika mvua zilizonyesha hivi karibuni ambapo wanafunzi watano wamepoteza maisha kwenye mvua hizo. Aidha ametoa tahadhari kwa watu na watoto kuacha kukatiza katika mito na maeneo hatarishi ili kuepukana na maafa yanayoweza kujitokeza.
Akitoa tathmini hiyo kwa baraza la madiwani wa halmashauri hiyo, Sanga alitaja kata walizopoteza watoto hao kuwa ni Tambani wanafunzi wawili ambao walizama, kata ya Mianzi, Mwarusembe,Mwandege mwanafunzi mmoja mmoja. Alieleza kuwa, pia ipo miundombinu ya barabara ambayo imeharibika vibaya na haipitiki. Sanga alisema ,wakati mvua ikiwa ni neema lakini mazingira yalishindwa kuhimili ,hivyo wamejipanga kuanza kukarabati baadhi ya miundombinu baada ya mvua kukoma. Alifafanua ,tathmini bado inaendelea na watatoa ukubwa wa maafa yaliyotokea baadae.
Diwani viti maalum Mkuranga, Daima Utanga akizungumza jambo wakati wa kikao cha baraza la madiwani wilayani humo .
WAKATI HUO HUO , Baadhi ya madiwani wa halmashauri ya wilaya ya Mkuranga wamemtaka afisa elimu msingi wa halmashauri hiyo, kuweka wazi idadi ya shule zilizotumika kiasi cha fedha mil.29. Fedha hizo ni kati ya mil.151 iliyopangwa kwa ajili ya ukarabati na ujenzi wa shule mbalimbali wilayani humo ambapo inadaiwa kutumika mil.29 .
Diwani wa kata ya Mwandege ,Kowero Edward na diwani wa viti maalum Daima Utanga waliibua hoja hiyo, katika kikao cha madiwani kilichofanyika wilayani hapo. Walitaka kujua zilizotumika kwenye ukarabati na ujenzi wa madarasa na shule ngapi kwani taarifa inaonyesha gharama bila idadi ya shule husika, zilizotumika fedha hiyo.
"Tunahitaji majibu ya fedha hizi ,na mchanganuo ili tuweze kujiridhisha" alieleza Daima.
Nae Mwenyekiti wa kamati ya elimu, afya na maji ,Shaban Manda alibainisha ,fedha hizo zimetumika kweli lakini kutokana na suala la idadi ya shule zilipoelekezwa fedha hizo ,watarejea kwenye kamati na kikao kijacho kutaletwa majibu ya uhakika ya hoja hiyo.
Alisema ,afisa elimu msingi wa halmashauri ya Mkuranga ni mgeni ,hivyo kutokana na hilo ,hawezi kuwa na majibu ya moja kwa moja. Manda ,alieleza jumla ya Tsh. mil.151 zimetengwa kwa ajili ya kukarabati na ujenzi ambapo hadi sasa mil.29 pekee.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa halmashauri hiyo ,Juma Abeid alisema masuala ya fedha na matumizi yazingatiwe ili kuondoa maswali kwa madiwani. Alisema ,uongozi wowote ni vijiti hivyo hakuna ugeni kwenye ofisi. Abeid aliwataka madiwani wawe na subira ,kuiachia kamati kwenda kukaa ,na kikao kinachofuata watapatiwa majibu ya uhakika.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa halmashauri ya Mkuranga, Mshamu Munde alisema wanajivunia kupata hati safi .
"Hati safi hii tuliyoipata sio sifa ya mtu mmoja ,tunajipongeza wote watendaji,mbunge wetu Abdallah Ulega, madiwani na wilaya ";
",Tusiishie hapa tuendelee na jitihada na kufanya kazi kwa kujituma ili kwenda na kasi ya serikali ya awamu ya tano" alifafanua Munde.
Aliwaomba watendaji kufanya kazi kwa bidii kwa maslahi ya wanaMkuranga. Munde alisema ,ushirikiano ndio nguzo pekee katika utendaji kazi hivyo aliwaomba watendaji hao na madiwani kuwa kitu kimoja ili kuleta maendeleo chanja na kuinua uchumi.

SERIKALI YATOA BILIONI 40 KUSHUGHULIKIA TATIZO LA MAJI MUHEZA

$
0
0
Waziri wa Maji na Umwagiliaji Mhandisi Isack Kamwelwe akiangalia mchanga unazotumika kwenye ujenzi wa tanki la maji eneo la Ngomeni
 Waziri wa Maji na Umwagiliaji Mhandisi Isack Kamwelwe akiangalia kikoto zinazotumika kwenye ujenzi wa tanki la maji eneo la Ngomeni Waziri wa Maji na Umwagiliaji Mhandisi Isaack Kamwele akizungumza na wananchi wa Kijiji cha Mashewa Tarafa ya Amani wilayani wakati alipofanya ziara ya kutembelea maeneo hayo 
MKUU wa mkoa wa Tanga Martine Shigella akizungumza katika ziara hiyo ya Waziri wa Maji na Umwagiliaji Mhandisi Isack Kamwelwe kulia wilayani Muheza
MKUU wa wilaya ya Muheza Mhandisi Mwanasha Tumbo akizungumza 
Kaimu Mkurugenzi wa Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Jijini Tanga Mhandisi Aram Phares akiwapungia mkono wananchi kwenye ziara hiyo 
Waziri wa Maji na Umwagiliaji Mhandisi Isack Kamwelwe kushoto akiwa na Mkuu wa Mkoa wa Tanga Martine Shigella wakitazama namna maji yanavyotoka kwenye Kijiji cha Mashewa Tarafa ya Amani wakati alipofanya ziara kutembelea vyanzo vya maji kushoto ni Mkuu wa wilaya ya Muheza Mhandisi Mwanasha Tumbo kulia ni Katibu Tawala wa Mkoa wa Tanga (RAS) Mhandisi Zena Saidi
Mkuu wa wilaya ya Muheza Mkoani Tanga Mhandisi Mwanasha Tumbo kulia akimueleza jambo Waziri wa Maji na Umwagiliaji Mhandisi Isack Kamwelwe kushoto ni Mkuu wa mkoa wa Tanga Martine Shigella na Katibu Tawala wa Mkoa wa Tanga Mhandisi Zena Saidi
Waziri wa Maji na Umwagiliaji Mhandisi Isack Kamwelwe katika akisisitiza jambo kwa Katibu Tawala wa mkoa wa Tanga Mhandisi Zena Saidi wakati alipotembelea eneo la Ngomeni kwenye na kuangalia tanki kubwa la maji ambalo litakalokuwa la lita milioni saba linalotarajiwa kukamilika mwezi wa tatu mwakani litakuwa limekamilika kwa ajili ya kutoa maji Pongwe Jijini Tanga hadi wilayani Muheza kushoto ni Mkuu wa mkoa wa Tanga Martine Shigella
Mkandarasi anayetekeleza mradi wa maji kutoka Pongwe hadi Jijini Tanga kutoka kampuni ya Koberg Contrustion Co.Limited Stephen Kingili wa pili kulia akimuonyesha jambo Waziri wa Maji na Umwagiliaji Mhandisi Isack Kamwelwe kushoto wakati alipotembelea na kuangalia tanki kubwa la maji eneo la Ngomeni wilayani Muheza ambalo litakalokuwa la lita milioni saba linalotarajiwa kukamilika mwezi wa tatu mwakani litakuwa limekamilika kwa ajili ya kutoa maji Pongwe Jijini Tanga hadi wilayani Muheza
Waziri wa Maji na Umwagiliaji Mhandisi Isack Kamwelwe akisisitiza kulia ni Katibu Tawala wa Mkoa wa Tanga Mhandisi Zena Saidi kushoto ni Mkuu wa mkoa wa Tanga Martine Shigella
Mkandarasi anayetekeleza mradi wa maji kutoka Pongwe hadi Jijini Tanga kutoka kampuni ya Koberg Contrustion Co.Limited Stephen Kingili kulia akizungumza na Waziri wa Maji na Umwagiliaji Mhandisi Isack Kamwelwe wakati alipotembelea na kuangalia tanki kubwa la maji eneo la Ngomeni wilayani Muheza ambalo litakalokuwa la lita milioni saba linalotarajiwa kukamilika mwezi wa tatu mwakani litakuwa limekamilika kwa ajili ya kutoa maji Pongwe Jijini Tanga hadi wilayani Muheza kushoto ni Mkuu wa mkoa wa Tanga Martine Shigella
Mkandarasi anayetekeleza mradi wa maji kutoka Pongwe hadi Jijini Tanga kutoka kampuni ya Koberg Contrustion Co.Limited Stephen Kingili wa pili kulia akimuonyesha jambo Waziri wa Maji na Umwagiliaji Mhandisi Isack Kamwelwe kushoto wakati alipotembelea na kuangalia tanki kubwa la maji eneo la Ngomeni wilayani Muheza ambalo litakalokuwa la lita milioni saba linalotarajiwa kukamilika mwezi wa tatu mwakani litakuwa limekamilika kwa ajili ya kutoa maji Pongwe Jijini Tanga hadi wilayani Muheza
***************************************
SERIKALI imeanza kulishughulikia tatizo la maji wilayani Muheza kwa vitendo baada ya kutoa kiasi cha bilioni 40 kwa ajili ya kutoa maji kwenye chanzo cha mto zigi kupelekwa kwenye vijiji mbalimbali ili kuweza kuondosha kero hizo iliyokuwepo muda mrefu iliyokuwa ikiwafanya wananchi kutumia muda mwingi kusaka huduma hiyo. 
Hayo yalibainishwa na Waziri wa Maji na Umwagiliaji Mhandisi Isaack Kamwele wakati alipofanya ziara wilayani humo kutembelea vyanzo vya maji Amani na kuzungumza na wananchi katika Kijiji cha Mashewa Tarafa ya Amani. 
Alisema kuwa mpango huo wa serikali unakusudia kuhakikisha changamoto za maji ambazo walikuwa wanakabiliana nazo wananchi hao kwa muda mrefu zinamaliza ili waweze kunufaika na huduma hiyo muhimu kwa ustawi wa maisha yao na jamii zinazowazunguka. 
Waziri Kamwelwe alisema hatua hiyo ni juhudi kubwa zinazofanywa na Rais John Magufuli kushughulikia changamoto zinazowakabili wananchi zikiwemo za maji ili kuhakikisha tatizo la kutokupatikana kwa huduma hiyo linaondoka kwa watanzania. 
“Ndugu zangu serikali tumetoa bilioni 40 kwa ajili ya kushughulikia tatizo la maji wilayani Muheza kutoka chanzo cha Mto zigi kupita vijiji vyote hadi Muheza mjini huu ni mpango wa kuhakikisha changamoto ya upatikanaji wa huduma ya maji Muheza tunaipatia ufumbuzi wa kina “Alisema. 
Aidha alisema kutokana na juhudi kubwa zinazofanywa na Rais Dkt John Magufuli zimeweza kuleta mafanikio ambapo juzi tumesaidia mkataba na serikali ya India wa dola Bilioni 500 kwa ajili ya kutatua changamoto za upatikanaji wa maji ambapo katika fedha hizo dola milioni 100 zitakuja wilaya za Muheza na Korogwe kwa lengo la kuhakikisha wanashughulikia tatizo la maji.
“Ndugu zangu mbunge wenu anafanya kazi kubwa na nzuri sana wakati ofisi ipo pale Jijini Dar es Salaam alinifuata ofisini akaniambia kwenye Jimbo lake kuna tatizo kubwa la maji hasa nyakati za kiangazi kwa wananchi kununua maji ndoo hadi kiasi cha sh.2000 nikachukua maamuzi ya haraka kwa lengo la kulishughulikia “Alisema. 
Alisema kuwa sio muda mrefu serikali itawapeleka wataalamu kwenye maeneo yenu hivyo kuwataka kushirikiana nao wakati wakitekeleza shughuli zao ili kuona namna nzuri ya kuweza kuzipatia ufumbuzi changamoto ambazo za kutokupatikana kwa huduma kwa vijiji visivyo na uhakika wa maji.
Waziri huyo alisema kuwa mpango wa serikali ni kuhakikisha mpaka ifikapo mwaka 2020 vijiji vyote vinakuwa na uwezo wa kupata maji ili kuweza kufikia asilimia 85 na mijini kufikia asilimia 95 Hata hivyo alisema kuwa eneo la Ngomeni wilayani humo kutajengwa tanki kubwa la maji litakalokuwa la lita milioni saba ambalo litakamilika mwezi wa tatu mwakani litakuwa limekamilika kwa ajili ya kutoa maji Pongwe Jijini Tanga hadi wilayani Muheza (Habari kwa Hisani ya Blog ya Kijamii ya Tanga Raha)

BUJORA DANCE GROUP WAREJEA NCHINI KWASHANGWE

$
0
0
 Kiongozi wa msafara Hassan Ngoma(katikati) akiwa pamoja na wanakikundi cha Ngoma cha Bujora cha Mkoani  Mwanza wakiwa wamewasili kutoka Nchini India walipokuwa wameenda kwenye tamasha la ngoma za asili kwa mataifa ya Afrika takribani nane yaliyoanza kutimua vumbi Mei 25 hadi Mei 30 katika miji mitatu tofauti.
**********************
Na Agness Francis.

KIKUNDI cha  ngoma cha Bujora Dance  kililokwenda Nchini India katika tamasha la michezo ya asili Afrika kimerejea nchini. 

Kundi hilo lililofanya vizuri zaidi katika mashindano ya Tulia Traditional Dances Festival 2018  ambao waliibuka kuwa ndio washindi limeifanya Tanzania kuwa kivutio huko nchini India.

Ambapo kundi hilo kutokea mwanza Mei 25 mwaka huu ndio lilianza kufanya kazi hiyo ya michezo  asili ya Mtanzania ambapo waliifanya nchi yetu kuwa kivutio katika tamasha la hilo iliyoshirikisha nchi nane  lenye lengo la kuimarisha mahusiano ya kitamaduni.

Kiongozi wa msafara huo Hassan Ngoma amesema kuwa  tamasha hilo lililokonga nyoyo za watu wengi sana  lilifanyika katika miji mitatu  New Delhi, khairagah pamoja na Chandigarh huko nchini India.

Ambapo Usiku wa May 27 heshima nyingine ya Tanzania ilitengenezwa katika mji wa Chandigarh nchini hapo huku kundi  hilo la ngoma za asili  walionyesha tena uwezo wao katika tamasha hilo.

Ngoma amesema usiku wa Mei 30 ndio walihitimisha kufanya maonyesho yao  katika tamasha hilo la wiki ya Afrika ambapo walimalizia kwa kutoa burudani ya uhakika katika mji wa Khairagarh wakiwa ndio waalikwa pekee katika mji huo.

"Imekuwa fursa nzuri kwetu ya kuitangaza tamaduni ya kitanzania kwa nchi mbali mbali lilitoshiriki tamasha la michezo ya asili Afrika" amesema Hassan Ngoma.
Kikundi cha Bujora kikiwa kimewasili Uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Mwl. Julius Nyerere Jijini Dar es Salaam wakitokeaNchini India walipokuwa wameenda kwenye tamasha la ngoma za asili kwa mataifa ya Afrika takribani nane yaliyoanza kutimua vumbi Mei 25 hadi Mei 30 katika miji mitatu tofauti. 

MATUKIO MBALIMBALI YA WAZIRI MKUU BUNGENI JIJINI DODOMA LEO

$
0
0
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na Mbunge wa Bariadi Magharibi, Andrew Chenge Bungeni jijini Dodoma, leo.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na Mbunge wa Kijitoupele Zanzibar, Shamsi Vuai Nahodha Bungeni jijini Dodoma. 
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenyeulemavu Jenista Mhagama, akijadili jambo na Waziri wa Elimu Profesa Joice Ndalichako, Bungeni jijini Dodoma. 
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, akizungumza na Waziri wa Elimu Profesa Joice Ndalichako, Bungeni jijini Dodoma.
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, akisalimiana na Makamu wa Rais wa Bunge la Afrika, Stephen Masele ambaye ni Mbunge wa Shinyanga Mjini, ofisini kwake Bungeni mjini Dodoma. 
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, akizungumza na Makamu wa Rais wa Bunge la Afrika, Stephen Masele ambaye ni Mbunge wa Shinyanga Mjini, ofisini kwake Bungeni mjini Dodoma, kutoka kushoto ni Mbunge wa Mbozi Magharibi Mheshimiwa David Silinde na Mbunge wa Viti Maalum Zanzibar Asha Abdullah Juma. Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu

MSANII SAM WA UKWELI AFARIKI DUNIA

$
0
0
Habari  zilizotufikia hivi pande zinasema kuwa Msanii wa Muziki wa kikazi kipya nchini Sam wa Ukweli amefariki Dunia jana u siku.
Imeelezwa kuwa Sam alikutwa na umauti wakati akiwa njiani kupelekwa hospitali ya Mwananyamala kwa matibabu baada ya kuishiwa ngivu wakati akiwa Studio akirekodi wimbo wake mpya.
Aidha imeelezwa kuwa Sam aliishiwa nguvu ghafla wakati akiingiza vocal katika wimbo wake mpya na kukimbizwa katika hospitali ya Parestina ambako alihamishiwa Mwananyamala na kufariki njiani Kabla ya kufikishwa hospitalinhospitalini hapo.
Taratibu za maziko zinafanyika ambalo anatarajia kuzikwa Bagamoyo.
MUNGU ILAZE ROHO YA MAREHEMU SAM MAHALA PEMA PEPONI, AMEEN 

RATIBA YA LIGI YA VIJANA U20 KWA KLABU ZA LIGU KUU NA MAKUNDI YAKAMILIKA

$
0
0
Upangaji wa ratiba na makundi ya Ligi ya Vijana U20 kwa klabu za Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara umefanyika leo Alhamis Juni 7,2018 Makao Makuu ya Azamtv.
Timu hizo 16 zimepangwa kwenye makundi manne yenye timu nne kila kundi.
Ligi hiyo inatarajia kuanza kutimua vumbi Juni 9,2018 mpaka Juni 21,2018 zikifanyika kwenye Jiji la Dodoma viwanja vya Chuo Kikuu cha Dodoma UDOM.

Kundi A
Young Africans 
Ruvu Shooting 
Mbeya City 
Mbao FC 

Kundi B
Simba 
Singida United 
Stand United
Njombe Mji 

Kundi C 
Azam FC 
Mtibwa Sugar 
Mwadui FC 
Majimaji FC 

Kundi D 
Tanzania Prisons 
Lipuli FC 
Kagera Sugar 
Ndanda FC
Katika kundi A Young Africans watafungua pazia la mashindano hayo dhidi ya Ruvu Shooting saa 8 mchana ikifuatiwa na mchezo wa pili Mbeya City dhidi ya Mbao FC Juni 9,2018 saa 10 jioni.
Mechi nyingine zitakazochezwa katika siku hiyo ya kwanza ni za kundi C ambapo Azam FC watacheza na Mtibwa Sugar saa 8 mchana ikifuatiwa na mchezo wa pili utakaoanza saa 10 kati ya Mwadui na Majimaji 
Kundi B wenyewe wataanza mechi zao Juni 10,2018 ambapo Simba watacheza dhidi ya Singida United nao Stand United watacheza na Njombe Mji saa 10 jioni.
Mechi nyingine za siku hiyo ni za Kundi D Tanzania Prisons dhidi ya Lipuli FC saa 8 mchana ikifuatiwa na mchezo wa Kagera Sugar dhidi ya Ndanda FC saa 10 jioni.

WAZIRI MWIJAGE AIPONGEZA KAMPUNI YA TOTAL KWA KUZINDUA MAFUTA YA MAGARI RAFIKI KWA MAZINGIRA

$
0
0
Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji Charles Mwijage (katikati) akikata utepe kuashiria uzinduzi wa mafuta ya Total Excellium ya petrol na Diesel ambayo yana uwezo wa kusafisha injini na kuiwezesha injini kufanya kazi kwa kipindi kirefu, wengine ni Balozi wa Ufaransa hapa nchini Fredric Clavier (watatu kushoto) Mkurugenzi Mtendaji wa Total nchini Tarik Moufaddal (watatu kutoka kulia). 
Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji Charles Mwijage akitoa huduma ya kujaza mafuta kwenye gari la mmoja wa wateja wa Total wakati wa uzinduzi wa mafuta ya Total Excellium ya petrol na Diesel uliofanyika leo jijini Dar es Salaam, Mafuta hayo yana uwezo wa kusafisha injini na kuiwezesha injini kufanya kazi kwa kipindi kirefu. kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa Total nchini Tarik Moufaddal na ni Balozi wa Ufaransa hapa nchini Fredric Clavier. Na Mwandishi Wetu. Waziri wa Viwanda na Biashara, Charles Mwijage ameipongeza kampuni ya mafuta ya TOTAL kwa kuwa mstari wa mbele kwenye kuhakikisha kuwa watanzania wanapata mafuta bora ya vyombo vya moto. Mwijage alizungumza jijini Dar es Salaam kwenye uzinduzi wa mafuta ya vyombo vya moto aina ya TOTAL Excellium kutoka kampuni ya mafuta ya TOTAL. Mafuta hayo yaliyotengenezwa kwa teknolojia ya ubora wa juu ya kimataifa ya TOTAL EXCELLIUM, kwa bidhaa zinazotumia mafuta ya Petroli na Diesel katika soko la Tanzania. “Uzinduzi wa mafuta haya umekuja wakati muafaka kwani sasa tuko kwenye wiki ya mazingira na mafuta haya yanapunguza uchafuzi wa hali ya hewa utokanao na vyombo vya moto, nawapongeza kampuni ya TOTAL kwa kuwaletea watanzania bidhaa bora, na mimi na utaalamu wangu wa mafuta nafahamu hii ni hatua kubwa sana kwenye teknolojia ya kuboresha mafuta,” alisema Mwijage. Mafuta haya mapya yana uwezo wa kusafisha injini na kuwezesha injini kufanya kazi kwa kipindi kirefu, kuwezesha matumizi kidogo ya mafuta na kupunguza uchafuzi wa hali ya hewa utokanao na moshi wa vyombo vya moto. Mafuta ya TOTAL EXCELLIUM yanapatikana katika vituo vyote vya kuuza mafuta vya kampuni ya TOTAL kwa gharama ya bei ya kawaida ya mafuta kwenye soko. Tarik Moufaddal, Mwenyekiti na Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya TOTAL nchini anasisitiza, “Kuzinduliwa kwa TOTAL EXCELLIUM, katika soko la Tanzania ni hatua mpya na muhimu kwetu nchini hususani katika kufanikisha dhamira yetu ya kuingiza bidhaa bora za nishati. Tunayo dhamira ya kuwapatia wateja wetu bidhaa zenye ubora wa hali ya juu, sambamba na huduma bora kupitia mtandao wetu ambao umeenea nchini kote, uzinduzi wa TOTAL EXCELLIUM, unadhihirisha kuwa tumejipanga kuleta mapinduzi yenye kuleta manufaa katika sekta ya mafuta nchini.” "TOTAL EXCELLIUM imetengenezwa kwa teknolojia ya juu ya kisasa ambayo inawezesha kusafisha injini, kuwezesha injini kufanya kazi kwa kipindi kirefu bila kuchoka, matumizi kidogo ya mafuta kuendesha injini, kupunguza uchafuzi wa mazingira utokanao na moshi na ni mazuri kwa matumzi ya aina zote za magari kuanzia madogo mpaka makubwa,” aliongeza Tarik. “Uzinduzi huu ni moja ya ubunifu mkubwa wa kampuni uliolenga kuhakikisha wateja wetu wanapata bidhaa bora na kuwawezesha matumizi kidogo ya mafuta yaliyotengenezwa kwa teknolojia ya kisasa ya Excellium. TOTAL EXCELLIUM imetengenezwa kwa ubunifu wa teknolojia za kisasa zenye kuleta ubora. Timu yetu ya wataalamu wa utafiti wamefanikisha kutengeneza mafuta haya kukidhi mahitaji ya wateja wetu wanaotumia magari ya kisasa ambayo yanahitaji umakini mkubwa katika matunzo ya injini kwa matumizi yao ya kila siku” Mkurugenzi wa Mtandao wa TOTAL wa Nikesh Mehta. “Zaidi ya watafiti makini na wataalamu wenye uzoefu mbalimbali wanafanyia kazi suala la kuleta bidhaa za mafuta na vilainishi vya injini na mitambo zenye ubora mkubwa zaidi katika kituo chetu cha utafiti cha Solaize,nchini Ufaransa.Wataalamu hao wamekuwa wakifanya kazi hiyo kwa zaidi ya miaka miwili kuboresha mafuta ya TOTAL EXCELLIUM. Zaidi ya kanuni za kisayansi 2,300 zimefanyiwa majaribio katika maabara kwa zaidi ya masaa 6,000 na mafuta haya yamefanyiwa majaribio ya awali barabarani kwa zaidi ya masaa 8,500 sawa na kilometa 300,000. Haya yote yanathibitisha uhakika na ubora wa mafuta ya TOTAL EXCELLIUM na yanasafisha injini za magari na kupunguza uharibifu wa mazingira,” anasema Marsha Msuya, Mkurugenzi wa Masuala ya Ndani ya kampuni ya TOTAL.

WAZIRI MWAKYEMBE AIPA MENO BMT KUSIMAMIA MCHEZO WA KUOGELEA

$
0
0
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Dkt. Harrison Mwakyembe (katikati) akisisitiza jambo wakati wa mkutano wa pamoja baina ya serikali na viongozi wa zamani wa Chama Cha Kuogelea Nchini (TSA) na kuamuru BMT kusimamia shughuli za mchezo huo wakati mchakato wa kuandaa uchaguzi mkuu ukiandaliwa. Kulia ni Katibu Mkuu wa Wizara, Suzan Mlawi na Kaimu Katibu Mkuu wa BMT. Alex Nkeyenge.
********************************************************
Na Mwandishi wetu
Dar es Salaam. Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Dkt. Harrison Mwakyembe ameipa mamlaka Baraza la Michezo la Tanzania (BMT) kusimamia shughuli za mchezo wa kuogelea wakati mchakato wa kuandaa uchaguzi mkuu wa chama hichon (TSA) ukiandaliwa.
Waziri Mwakyembe alisema hayo juzi katika kikao kilicho wakutanisha viongozi wa zamani walioenguliwa madarakani na wanachama wa chama hicho na Kamati ya Muda iliyomaliza muda wake wa miezi mitatu.
Alisema kuwa TSA imekuwa na mvutano wa uongozi kwa muda sasa na kuhatarisha maendeleo ya mchezo huo ambao umeifanya Tanzania kutambulika zaidi kwa nchi za Kanda ya Tatu (Cana zone three) ikiwa ni mabingwa mara mbili mfululizo.
Mwakyembe alisema kuwa mbali ya BMT kusimamia mchezo huo kwa sasa, viongozi wa zamani chini ya mwenyekiti Alex Moshi na Katibu Mkuu, Ramadhani Namkoveka wanatakiwa kuwasilisha ripoti ya utendaji wao ikiwa pamoja na taarifa za fedha (mapatona matumizi) kwa Msajili wa Klabu na Vyama Vya Michezo.
Alifafanua kuwa TSA ilitakiwa kufanya hivyo mwaka jana, lakini kutokana na hali ilivyokuwa, zoezi hilo lilisogezwa mbele mpaka Februari 28 mwaka huu, jambo ambalo halikufanyika.
“Nawaagiza kuwasilisha taarifa za utendaji wenu haraka iwezekanavyo kwa Msajili, kinyume hayo, sheria itachukua mkondo wake, serikali ya Awamu ya Tano haina mchezo mchezo kwa viongozi ambao hawawajibiki na tutafanya haya kwa kila chama cha michezo,” alisema Mwakyembe.
Alisema kuwa hata viongozi ambao walijihudhuru nafasi zao, wanatakiwa kuwasilisha taarifa zao mpaka pale walipoamua kuachana na uongozi.
“Naipongeza Kamati ya Muda kwa kukamilisha kazi zao kwa muda wa miezi mitatu kama walivyopewa na BMT na kwa sasa suala la Katiba litajadiliwa na Kaimu Katibu Mkuu wa BMT, Msajili na viongozi wa zamani na Kamati hiyo siku ya Jumatano (June 13),” alisema.
Kamati ya Muda iliyokuwa chini ya Mwenyekiti, Imani Dominick na Katibu wake, Inviolata Itatiro iliyomaliza muda wake Juni 9 mwaka huu. Wajumbe wengine wa kamati hiyo walikuwa, Alex Mwaipasi, Amina Mfaume na Anna Shanalingigwa.
Kaimu Katibu Mkuu wa BMT, Alex Nkeyenge akizungumzaWanachama wa TSA wakifuatilia mkutano
Mwenyekiti wa zamani wa TSA, Alex Moshi akizungumza
Mwenyekiti wa Kamati ya Muda wa TSA, Imani Dominick akizungumza

SABA WAKAMATWA HIFADHI YA SAADAN KWA TUHUMA ZA UWINDAJI HARAMU WA KUTUMIA SILAHA

$
0
0

Kamanda wa polisi mkoani Pwani ACP Jonathan Shanna akionyesha pembe ya mnyama ajulikanae kama pongo na silaha mbalimbali ambazo zimekamatwa katika misako inayoendelea.
***************************************************
Na Linda Shebby, Chalinze
JESHI la Polisi Mkoa wa Pwani kwa kushirikiana na Shirika la Hifadhi ya Taifa (TANAPA) wamewakamata watu saba katika hifadhi ya Saadan ambao wamekutwa wakimiliki silaha ambazo walikuwa wakizitumia kufanyia uwindaji haramu katika hifadhi hiyo bila ya kuwa na kibali.
Huku wakituhumiwa kumuua myama mmoja adimu anayepatikana kwenye hifadhi hiyo ya Saadan pekee aliyemtaja kwa jina Pongwe 
Akizungumza leo Kamanda wa Polisi Mkoa wa Pwani Jonathan Shanna amewataja watuhumiwa waliokamatwa kuwa ni Hadija Rashid ( 32 )mkazi wa Mkange amekamatwa na Magobore mawili, Amina Athumani (30) mkazi wa Gama amekamatwa na risasi tisa za Short Gun, Mohamed Athuman (65) mkazi wa Manda ambaye amekamatwa magobore mawili Yusuph Salum( 62) ,pamoja na Salum Ramadhan( 96)mkazi wa Manda amekamatwa na magobore mawili. 
Kamanda Shanna amewataja watuhumiwa wengine kuwa ni Athumani Abdully (26), Siwatu Bakari(40) na Mussa Abdully wote wakazi wa Manda na walipokamatwa kila mmoja alikiwa na gobore moja.
Kutokana na tukio hilo Kamanda Shanna ametoa siku moja kwa raia wanaomiliki silaha isivyo halali kuzisalimisha mara moja.
Katika tukio la pili Jeshi la Polisi mkoani hapa wamekamata gari lilikokuwa limeibiwa katika eneo la vigwaza mapema mwaka huu lenye namba za usajili T 265 BZC aina ya Mitsubish Canter tukio hilo lilitokea baada ya kundi la watu sita.
Kamanda wa polisi mkoani Pwani ACP Jonathan Shanna akionyesha gari lililokuwa limeibwa na kubadilishwa namba za usajili (bandia).
***************************************
Huku mmoja wao akijifanya ni Mwalimu wa Shule ya sekondari Vigwaza akiwa na wenzake walimfuata dereva aitwaye Omari Nyange(39) na kumwambia kuwa wanataka kumkodi ili wakahamishe vyombo dereva huyo alikubaliana na watu hao na walipoanza safari ya kwenda eneo la Madafu walimbadilikia na kumkaba kisha kumpora gari hilo na yeye kumtupa nje.
Baada ya taarifa hizo kufika katika Jeshi la Polisi walianza upelelezi na Juni 6 mwaka huu wakalikamata katika Wilaya ya Kilombero mkoani Morogoro baada ya mwizi mmoja kukamatwa aliyetajwa kwa jina la Kasimu Nasoro(40) ambaye amekiri kuhusika na tukio hilo.
Amefafanua amekiri kuwa baada ya kuiba gari hilo walilibadilisha namba na kufunga namba za bandia ambazo ni T 525 ABM na kulisafitisha hadi Mangula.
Ambako walitengeneza kadi bandia na kwenda kuliuza kwa kiasi cha Sh. 8,000,000 kwa Florida Stanslaus mkazi wa Mang'ula Morogoro.
Katika tukio la tatu Jeshi la Polisi katika mzani wa Msata Wilaya ya Kipolisi Chalinze wamekamata madumu matupu yanayodaiwa kukamata gari aina ya fuso lililokuwa linaendeshwa na dereva likiwa limebeba vyuma chakavu ambavyo havikulipiwa ushuru wa serikali ambapo walitozwa faini kiasi cha Sh. milioni 2,000,000 na maofisa wa kuhifadhi na kutunza mazingira kwa kosa la kukwepa ushuru.
Baadhi ya silaha zilizokamatwa na jeshi la polisi mkoani Pwani

KIKAO NA WADAU WA MAENDELEO NA SEKTA YA AFYA KATIBU MKUU

$
0
0
 Katibu Mkuu Wizara ya Afya Dkt. Mpoki Ulisubisya akiwakabidhi vyeti watumishi watatu wa Sekretarieti ya pamoja kwa kutambua michango yao kwa kipindi chote cha utumishi wao wakati wa Mkutano wa robo mwaka wa kitaalam katika sekta ya afya uliofanyika leo jijini Dar es salaam.
 Katibu Mkuu Wizara ya Afya Dkt. Mpoki Ulisubisya akiwakabidhi vyeti watumishi watatu wa Sekretarieti ya pamoja kwa kutambua michango yao kwa kipindi chote cha utumishi wao wakati wa Mkutano wa robo mwaka wa kitaalam katika sekta ya afya uliofanyika leo jijini Dar es salaam.
 Katibu Mkuu Wizara ya Afya Dkt. Mpoki Ulisubisya akiwakabidhi vyeti watumishi watatu wa Sekretarieti ya pamoja kwa kutambua michango yao kwa kipindi chote cha utumishi wao wakati wa Mkutano wa robo mwaka wa kitaalam katika sekta ya afya uliofanyika leo jijini Dar es salaam.
 Katibu Mkuu Wizara ya Afya Dkt. Mpoki Ulisubisya akiongea na baadhi wadau wa maendeleo,wadau wa sekta ya afya wa Serikali na Binafisi na Wakurugenzi wa vitengo mbalimbali kutoka Wizara ya Afya hawapo pichani wakatri wa Mkutano wa robo mwaka wa kitaalam katika sekta ya afya uliofanyika leo jijini Dar es salaam.
 Katibu Mkuu Wizara ya Afya Dkt. Mpoki Ulisubisya katikati akiwa kwenye picha ya pamoja na baadhi wadau wa maendeleo,wadau wa sekta ya afya wa Serikali na Binafisi na Wakurugenzi wa vitengo mbalimbali kutoka Wizara ya Afya hawapo pichani wakatri wa Mkutano wa robo mwaka wa kitaalam katika sekta ya afya uliofanyika leo jijini Dar es salaam.
Baadhi wadau wa maendeleo,wadau wa sekta ya afya wa Serikali na Binafsi na Wakurugenzi wa vitengo mbalimbali kutoka Wizara ya Afya wakifuatilia kwa makini maelekezo kutoka kwa Katibu Mkuu Wizara ya Afya Dkt. Mpoki Ulisubisya hayupo pichani wakati wa Mkutano wa robo mwaka wa kitaalam katika sekta ya afya uliofanyika leo jijini Dar es salaam.
 Baadhi wadau wa maendeleo,wadau wa sekta ya afya wa Serikali na Binafsi na Wakurugenzi wa vitengo mbalimbali kutoka Wizara ya Afya wakifuatilia kwa makini maelekezo kutoka kwa Katibu Mkuu Wizara ya Afya Dkt. Mpoki Ulisubisya hayupo pichani wakati wa Mkutano wa robo mwaka wa kitaalam katika sekta ya afya uliofanyika leo jijini Dar es salaam.
Baadhi wadau wa maendeleo,wadau wa sekta ya afya wa Serikali na Binafsi na Wakurugenzi wa vitengo mbalimbali kutoka Wizara ya Afya wakifuatilia kwa makini maelekezo kutoka kwa Katibu Mkuu Wizara ya Afya Dkt. Mpoki Ulisubisya hayupo pichani wakati wa Mkutano wa robo mwaka wa kitaalam katika sekta ya afya uliofanyika leo jijini Dar es salaam.
********************************************************
Katibu Mkuu Wizara ya Afya Dkt. Mpoki Ulisubisya ameongoza mkutano wa robo mwaka wa kitaalam katika sekta ya Afya unaowaleta pamoja Serikali ,wadau wa maendeleo,Sekta binafsi na Asasi za kiraia.
Leongo la mkutano huo ni kuangalia utekelezaji wa maazimio ya pamoja na kuandaa mipango mipya ya utekelezaji wa mpango mkakati wa sekta ya afya wan ne kupitia vikundi kazi 11 vya kilaam.
Pia watumishi watatu wa Sekretarieti ya pamoja wametunukiwa vyeti kwa kutambua michango yao kwa kipindi chote cha utumishi wao ambao ni Dkt. Oberlin Kisanga ,Dkt. Anna Nswila na Dkt. Didace Mutagwaba.
Viewing all 13053 articles
Browse latest View live


<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>