Quantcast
Channel: SUFIANIMAFOTO
Viewing all 13053 articles
Browse latest View live

BENKI YA NMB YAIKABIDHI SERIKALI GAWIWO LA SHILINGI BILIONI 10.1

$
0
0
Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Isdor. Mpango (Mb) (kushoto) na Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya NMB Bi. Ineke Bussemaker, wakiangalia hundi kifani yenye thamani ya shilingi bilioni 10.1, ambayo ni gawio lililotolewa na Benki ya NMB kwa Serikali, Jijini Dodoma.
Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Isdor. Mpango (Mb) (kushoto) na Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya NMB Bi. Ineke Bussemaker, wakipeana mkono wakati wa makabidhiano ya hundi kifani yenye thamani ya shilingi bilioni 10.1, ambayo ni gawio lililotolewa na Benki ya NMB kwa Serikali, Jijini Dodoma.
**************************************************************
Na Benny Mwaipaja, WFM, Dodoma

Benki ya NMB imetoa gawio la Sh. bilioni 10.1 kwa Serikali ambayo inamiliki asilimia 32 ya hisa za Benki hiyo baada ya kupata faida ya Sh. bilioni 94.8 baada ya kodi kwa mwaka 2017/2018.
Tukio hilo la kukabidhi hundi kifani ya gawio hilo limefanyika Makao Makuu ya Wizara ya Fedha na Mipango, Jijini Dodoma, kati ya Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Mpango, kwa niaba ya Serikali, na Mkurugenzi Mtendaji wa Benki hiyo Ineke Bussemaker. 
Dkt. Mpango amezipongeza juhudi za watendaji wa Benki hiyo waliofanikisha kupatikana kwa faida iliyowezesha Serikali kupata gawio licha ya changamoto zilizoikumba Sekta ya Benki likiwemo suala la mikopo chechefu.
“Mikopo chechefu imekua tatizo kwa Benki nyingi nchini hivyo ninatoa rai kwa Benki ya NMB kuhakikisha inafuata taratibu za kukopesha na kuendelea kusimamia vizuri wakopaji ili kuondoa tatizo la mikopo chechefu” alieleza Dkt. Mpango. 
Aidha ameipongeza Benki hiyo kwa kutoa huduma katika Sekta ya kilimo na kuitaka ipanue wigo zaidi na kuziwezesha sekta za uvuvi na ufugaji kutokana na umuhimu wake katika ukuaji wa uchumi wa taifa. 
Alisema kuwa anatarajia Benki hiyo itatoa gawio zaidi mwaka ujao wa fedha na amemwagiza Msajili wa Hazina, kuzihakiki taasisi zote ambazo Serikali imewekeza hisa zake ili zitoe gawio lasivyo ametishia Serikali kuondoa hisa zake kwakuwa uwekezaji huo hautakuwa na tija. 
Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Benki hiyo Ineke Bussemaker alieleza kuwa licha ya Benki yake kutoa gawio hilo la shilingi bilioni 10.1 kwa Serikali, pia inalipa kodi za Serikali vizuri ambapo katika kipindi cha mwaka 2017/18 imetoa kodi ya shilingi bilioni 127.
Aliongeza kuwa tangu mwaka 2014 hadi 2017 benki hiyo imetoa kodi zinazofikia zaidi ya shilingi bilioni 460 na kwamba itaendelea kuongeza ufanisi wa utoaji wa huduma za kibenki ili iweze kupata faida na kulipa gawio kubwa zaidi kwa wana hisa wake ikiwemo Serikali inayomiliki silimia 31.8 ya hisa 500.
Aidha, amesema kuwa Benki yake imeendelea kufanya kazi kwa karibu na Sekta ya Kilimo kwa kutoa huduma za kifedha kwa wakulima wakiwemo wakulima wa Tumbaku na Korosho katika mikoa ya Kusini ya Lindi na Mtwara, ambapo imefungua zaidi ya akaunti 300,000 na kuweza kukusanya zaidi ya shilingi bilioni 250 mwezi Novemba mwaka jana.
Bi. Bussemaker alisema kuwa Benki yake inajitahidi kuhakikisha kunakua na huduma jumuishi za kifedha kwa wananchi kote nchini kwa kuweka Mawakala na kuongeza Matawi ya Benki hiyo na pia kuhamasisha wananchi wafungue Akaunti ya Benki hiyo.
Alisema kuwa ili kufanikisha utoaji wa huduma hiyo ya kifedha kwa watanzania, Benki hiyo imejipanga kutumia teknolojia ya kisasa ya masuala ya fedha ambayo itarahisisha kuwafikia watu wengi ikiwemo huduma za fedha kwa njia ya simu za mkononi. 
Katika Mwaka wa Fedha 2016/2017, Benki hiyo ilitoa gawio la shilingi bilioni 16.5 kwa Serikali, huku kukiwa na pungufu ya shilingi bilioni 6 mwaka huu hatua iliyomlazimu Dkt. Mpango kuiagiza Benki hiyi ihakikishe inaboresha huduma zake ili Serikali ipate gawio kubwa zaidi kwa ajili ya kutumia fedha hizo kuwaletea wananchi maendeleo katika sekta za maji, afya, elimu, na miundombinu mingine muhimu.

SERIKALI: HAKUNA MFUKO MAALUM WA KUHIFADHI FEDHA ZA KULIPA DENI LA TAIFA

$
0
0
Na Benny Mwaipaja, Dodoma
Serikali imesema kuwa hakuna akiba ya fedha iliyowekwa katika mfuko maalum kwa ajili ya kulipia Deni la Taifa kwa sababu deni hilo linajumlisha Deni la Serikali na Deni la Sekta Binafsi, lakini Serikali inalipa deni lake pekee bila kuhusisha deni la Sekta Binafsi.
Hayo yameelezwa Bungeni Jijini Dodoma na Naibu Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji alipokuwa Akijibu maswali ya Mbunge wa Mtambile Mhe. Masoud Abdallah Salim aliyetaka kujua Deni la Taifa limefikia kiasi gani na namna mchanganuo wa fedha zilizowekwa akiba kwa ajili ya kulipa deni hilo ulivyo.
“Fedha kwa ajili ya malipo ya Deni la Serikali inatengwa kwa kuzingatia taratibu za kawaida za kibajeti kupitia Fungu 22, katika Mwaka wa Fedha 2017/18, Serikali ilitenga kiasi cha Sh. trilioni 1.262 kwa ajili ya malipo ya deni la ndani na Sh. bilioni 685.06 kwa deni la nje”, alisema Dkt. Kijaji.
Alisema hadi kufikia Aprili 30, mwaka huu Deni la Taifa limefikia Dola za Marekani milioni 26,161.02 sawa na zaidi ya Shilingi trilioni 59.4.
Akijibu swali la nyongeza la Mbunge huyo aliyetaka kujua mkakati wa Serikali kuhakikisha Deni la Taifa linahakikiwa ili kujua kama Serikali inakopesheka au la, Dkt. Kijaji alilihakikishia Bunge kuwa kuanzia mwaka ujao wa fedha, Deni la Taifa litahakikiwa kama nchi nyingine zinavyofanya kwani mkataba wa kuhakiki deni hilo upo kwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali katika hatua za mwisho.
Waziri huyo alisema kuwa Deni la Taifa ni himilivu na Serikali imekuwa makini katika ulipaji kwa kuhakikisha inalipa kila mwezi madeni katika Taasisi zote ilizokopa hali inayoifanya nchi kuaminika na Taasisi mbalimbali za kitaifa na kimataifa.
Aidha, Mhe. Kijaji alifafanua kuwa fedha zote zinazokopwa zinapelekwa katika shughuli za maendeleo ya kiuchumi ili kuendelea kuinua uchumi wa nchi hususani katika kipindi hiki cha uchumi wa viwanda.

SERIKALI: HAKUNA MFUKO MAALUM WA KUHIFADHI FEDHA ZA KULIPA DENI LA TAIFA

$
0
0
Na Benny Mwaipaja, Dodoma
Serikali imesema kuwa hakuna akiba ya fedha iliyowekwa katika mfuko maalum kwa ajili ya kulipia Deni la Taifa kwa sababu deni hilo linajumlisha Deni la Serikali na Deni la Sekta Binafsi, lakini Serikali inalipa deni lake pekee bila kuhusisha deni la Sekta Binafsi.
Hayo yameelezwa Bungeni Jijini Dodoma na Naibu Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji alipokuwa Akijibu maswali ya Mbunge wa Mtambile Mhe. Masoud Abdallah Salim aliyetaka kujua Deni la Taifa limefikia kiasi gani na namna mchanganuo wa fedha zilizowekwa akiba kwa ajili ya kulipa deni hilo ulivyo.
“Fedha kwa ajili ya malipo ya Deni la Serikali inatengwa kwa kuzingatia taratibu za kawaida za kibajeti kupitia Fungu 22, katika Mwaka wa Fedha 2017/18, Serikali ilitenga kiasi cha Sh. trilioni 1.262 kwa ajili ya malipo ya deni la ndani na Sh. bilioni 685.06 kwa deni la nje”, alisema Dkt. Kijaji.
Alisema hadi kufikia Aprili 30, mwaka huu Deni la Taifa limefikia Dola za Marekani milioni 26,161.02 sawa na zaidi ya Shilingi trilioni 59.4.
Akijibu swali la nyongeza la Mbunge huyo aliyetaka kujua mkakati wa Serikali kuhakikisha Deni la Taifa linahakikiwa ili kujua kama Serikali inakopesheka au la, Dkt. Kijaji alilihakikishia Bunge kuwa kuanzia mwaka ujao wa fedha, Deni la Taifa litahakikiwa kama nchi nyingine zinavyofanya kwani mkataba wa kuhakiki deni hilo upo kwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali katika hatua za mwisho.
Waziri huyo alisema kuwa Deni la Taifa ni himilivu na Serikali imekuwa makini katika ulipaji kwa kuhakikisha inalipa kila mwezi madeni katika Taasisi zote ilizokopa hali inayoifanya nchi kuaminika na Taasisi mbalimbali za kitaifa na kimataifa.
Aidha, Mhe. Kijaji alifafanua kuwa fedha zote zinazokopwa zinapelekwa katika shughuli za maendeleo ya kiuchumi ili kuendelea kuinua uchumi wa nchi hususani katika kipindi hiki cha uchumi wa viwanda.

MKUTANO WA KIMATAIFA WA MASUALA YA JINSIA NA MAHAKAMA WAFUNGULIWA LEO MJINI ARUSHA

$
0
0
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan amesema Licha ya changamoto kadhaa, Tanzania Imepiga hatua kubwa katika jitihada zake za kupunguza unyanyasaji na ubaguzi wa kijinsia.
Makamu wa Rais ameyasema hayo leo wakati wa Mkutano wa Kimataifa unaohusu masuala ya Jinsia na Mahakama Afrika ulioandaliwa na Mahakama ya Tanzania kwa kushirikiana na Benki ya Dunia na kuhudhuriwa na Majaji Wakuu kutoka nchi za Afrika.
Makamu wa Rais amesema Tanzania imepiga hatua kwa Marekebisho ya sheria kupitia makosa ya kijinsia ya mwaka 1998 ,pili Utekelezaji wa Sheria ya Ardhi na Sheria ya Ardhi ya Kijiji mwaka 1999 ilifanya mabadiliko makubwa katika kuzingatia haki za wanawake juu ya upatikanaji wa ardhi, Tatu Utekelezaji wa sheria ya sheria ya mtoto mwaka 2009, ambayo kati ya mambo mengine, imewekwa kwa namna sahihi ya haki za mtoto na kuanzishwa kwa madawati maalum kwenye vituo vya polisi ili kuboresha msaada kwa waathirika wa unyanyasaji wa kijinsia.
Makamu wa Rais aliwaambia Majaji Wakuu kutoka nchi za Afrika kuwa pamoja na uzoefu walionao, wana nafasi ya kufahamu umuhimu wa kuimarisha jinsia katika mfumo wa haki.
“Ni matumaini yangu kwamba mkutano huu utakuja na mapendekezo yenye manufaa ambayo yatafungua  njia ya kuwa na mifumo ya mahakama yenye uaminifu wa kijinsia na wajibu”
Akizungumzia Mkutano uliofanyika kwenye Kituo cha Kimataifa cha Mikutano cha Arusha (AICC), Jaji Mkuu wa Tanzania profesa Ibrahim Hamis Juma mkutano huo umejikita kuona namna gani kunakuwa na usawa katika kutoa haki, kusogeza huduma za kimahakama kuangalia sheria za mirathi ambapo bado mwanamke ameonekana kukandamizwa na sheria ya kujamiiana.
Mkutano huo ambao ulihudhuriwa na Makamu wa Rais wa Benki ya Dunia Bi. Sandie Okoro, Mkurugenzi Mkazi wa Benki ya Dunia Bi. Bella Bird, Majaji Wakuu kutoka nchi za Afrika na wadau mbali mbali wa sekta za kimahakama na sheria. 
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa kwenye picha ya pamoja na Majaji Wakuu kutoka nchi za Afrika waliohudhuria Mkutano wa Kimataifa unaohusu Jinsia na Mahakama Afrika ulioandaliwa na Mahakama ya Tanzania kwa kushirikiana na Benki ya Dunia na kufanyika kwenye Kituo cha Mikutano cha Kimataifa Arusha (AICC), Wengine pichani kulia ni Jaji Mkuu wa Ghana Sophia  Akuffo,Jaji Mkuu wa Zimbabwe Luke Malaba na Jaji Mkuu wa Zanzibar Omar Othman Makungu wengine kushoto ni Jaji Mkuu wa Kenya David Maraga, Jaji Mkuu wa Tanzania Profesa Ibrahim Hamis Juma, Jaji Mkuu na Jaji Mkuu wa Benin Batoko Ousmane.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza na Jaji Mkuu Mstaafu Augustino Ramadhan mara baada ya kufungua ​​Mkutano wa Kimataifa unaohusu Jinsia na Mahakama Afrika ulioandaliwa na Mahakama ya Tanzania kwa kushirikiana na Benki ya Dunia na kufanyika kwenye Kituo cha Mikutano cha Kimataifa Arusha (AICC). Picha na OMR

DKT.MNDOLWA AWAPA MAKAVU LIVE WANACHAMA WA CCM, MNASHINDWAJE KULIPA ADA YA MWAKA AMBAYO NI SAWA NA SODA MOJA?

$
0
0
Na Bashir Nkoromo, Tarime
Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi Tanzania Dk. Edmund Mndolwa ameshangazwa na baadhi ya wanachama wa CCM na Jumuiya zake kushindwa kulipa ada ya uanachama ya sh. 1200 kwa mwaka, ambayo ni sawa ya bei ya soda moja.
Dk. Mndolwa ameelezea kushangazwa huko, wakati akizungumza na viongozi wa CCM na Jumuiya za CCM kutoka Wilaya za mkoa wa Mara, katika ukumbi wa CMG mjini Tarime, leo, akiwa katika ziara ya kikazi mkoani humo.
Kufuatia hali hiyo Dk. Mndolwa ameagiza viongozi kusimamia ipasavyo ili kuhakikisha kila mwanachama wa CCM na Jumuiya ya Wazazi Tanzania analipa ada yake ya kila mwezi, akisisitiza kuwa watakaoshindwa kufanya hivyo itakuwa ni mfano unaoonyesha kuwa hawafai uongozi kutokana na kushindwa kusimamia uhai wa Jumuiya hiyo na Chama Cha Mapinduzi.
"Unamkuta mtu kila mara anajinasibu kuwa ni mwanachama wa CCM au Jumuiya ya Wazazi, lakini wakati huo huo halipi ada ya uanachama ya kila mwaka mbayo gharama yake kwa kila mwaka ni sawa na bei ya soda moja ambayo kila siku anamudu kuinunua", alisema Dk. Mndolwa.
Alisema, ni jambo la muhimu kwa kila mwanachama kuhakikisha analipa ada yake ya uanachama kwa sababu kufanya hivyo ndiyo ishara pekee inayodhihirisha uanachama wake kwa kuwa asipofanya hivyo anakuwa mwanachama mfu asiyeshiriki katika kuimarisha uhai wa Chama.
Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi Tanzania Dk. Edmund Mndolwa akizungumza na Viongozi wa Jumuiya hiyo, leo mjini Tarime mkoani Mara. Kushoto ni Katibu Mkuu wa Jumuiya hiyo Erasto Sima, Mwenyekiti wa Jumuiya hiyo mkoa wa Mara Samweli Kiboya na Makamu Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi Tanzania uoande wa Zanzibar Haidar haji Abdallah na kulia ni Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Mara Mrida Mshota.
***********************************************
Dk. Mndolwa amewasisitiza wanachama wa CCM kujiunga na Jumuiya za Chama akisema kwamba kufanya hivyo kunatoa fursa pana zaidi kwa mwanachama kuijenga CCM na pia hata kuwea kupata nafasi za uongozi kwa wepesi zaidi kuliko akiwa mwana CCM tu. KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA
"Tazameni, hivi sasa mimi ni Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM lakini ni kwa sababu nimekuwa mwanachama wa Jumuiya ya Wazazi na kisha nikagombea kupitia huko na kupata Uenyekiti wa Jumuiya hii ambapo sasa kwa nafasi niliyo nayo ya Uenyekiti nimekuwa pia Mjumbe wa Kamati Kuu", alisema Dk. Mndolwa.
Akizungumzia maadili katika jamii, Dk. Mndolwa aliwatupia lawama wazazi kuwa ndiyo chanzo kikubwa cha kumomonyoka kwa maadili katika jamii kutokana na kuwaacha watoto wao kufanya wapendavyo katika masuala ya tabia.
"Unakuta binti anatoka nyumbani amefaa nguo za kubaka maungo na zinazoacha wazi baadhi ya maungo yanayostahili kusitiriwa, mzazi anaona lakini anamuacha bila kumkemea, matokeo yake binti anakuwa mitaani katika namna ya kutokuwa na maadili bora, ikitokea hivyo jua lawama ni kwa mzazi", alisema Dk. Mndolwa.
Alisema, hali kadhalika ni kosa la mzazi pale mtoto wa kiume anapotoka nyumbani huku amevaa katula au suruali inayoporomoka matakoni, kwa sababu mzazi anapaswa kukemea uvaaji huo kwa kuwa unatia aibu katika jamii.
"Unakuta mzazi anampa hela nyingi mtoto wakati anakwenda shuleni huku akisema kuwa kwa kuwa yeye alisoma katika mazingira ya taabu hataki mwanae asome kwa taabu, kumbe hajui kuwa kwa kufanya hivyo anamjengea mtoto vishawishi vya kutumbukia katika utumiaji wa dawa za kulevya na uvutaji bangi", alisema Dk. Mndolwa.
Dk. Mndolwa aliwataka wazazi kuwa mstari wa mbele kuwahakikisha wanasaidia kujenga maadili ya jamii kwa kuwakanya na kuwachukulia hatua thabiti watoto wao kila wanapowagundua au kuwaona wanajaribu kuanza kuiga tabia zinazomomonyoa maadili.
Akizungumzia mshikamano ndani ya Chama, Dk. Mndolwa aliwataka wana CCM kuachana kabisa na mtindo wa kung'ang'ania makundi kila baada ya uchaguzi na pia kuachana na tabia ya kuthani mtu fulani ni maarufu kuliko chama.
Dk. Mndolwa alisema, ikiwa wanachama wataachana na mambo hayo CCM inakuwa imejihakikishia kupata ushindi kila uchaguzi kwa kuwa inao wanachama na wapenzi wengi na kinachohitajika ni mshikamano tu.
"Hadi sasa kuna baadhi ya majimbo au Kata walizoshinda wapinzani katika uchaguzi uliopita, lakini kwa maoni yangu wapinzani hawakushinda maeneo hayo eti kwa sababu ni weledi sana, hapana. ukweli ni kwamba walishinda kwa sababu ya uzembe wa wana CCM wenyewe kung'ang'ania makundi baada ya kura za maoni", alisema Dk. Mndolwa.
Lengo la ziara hiyo ya Dk. Mndolwa katika mikoa ya Kanda ya ziwa na mkoa wa Singida, ni kuwashukuru wananchama wa Jumuiya ya Wazazi kwa kumchagua kuwa Mwenyekiti wa Jumuiya hiyo na pia kuwatambulisha Makamu Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi Tanzania kwa upande wa Zanzibar Haidar Haji Abdallah na Katibu Mkuu wa Jumuiya hiyo Erasto Sima ambao ameambatana nao katika ziara hiyo.

MZEE MBIZO NA MWANAE H-MBIZO WAINGIA STUDIO KUREKODI KIBAO KIPYA

$
0
0

Inaweza kukuwia vigumu kuamini, lakini ndiyo hivyo tena, akiwa anatimiza umri wa miaka 68, miaka 39 ya kuwepo kwenye fani za michezo na burudani, hatimaye Mzee Juma Mbizo ameamua kuingia studio kwa mara kwanza na kufanya ‘kolabo’ na mwanae H-Mbizo.
Naam Mzee Mbizo amejitosa katika studio za Fire Music chini producer More Fire na kurekodi wimbo wa pamoja na H-Mbizo aliyepata kutamba na wimbo wa “Mchumba”.
H-Mbizo ambaye pia mwandishi mzuri wa nyimbo akiwa amewaandikia wasanii wengi akiwemo Snura kupitia wimbo “Majanga”, ameuambia mtandao huu kuwa kibao hicho alichoimba na baba yake kitaachiwa hewani mwezi huu.
Licha ya ukongwe wake kwenye game na utalaam wa kuandaa matamasha makubwa ya burudani, lakini Mzee Mbizo hakuwahi kuingia studio na kurekodi wimbo wowote ule na hii ndio hali itayofanya kazi hii alishoshirikishwa na mwanae iteke masikio ya mashabiki wengi wa muziki.

SPIKA NDUGAI MGENI RASMI MASHINDANO YA KUHIFADHI QURAN YALIYOFANYIKA PAHI WILAYANI KONDOA MKOANI DODOMA.

$
0
0
 Spika wa Bunge, Mhe. Job Ndugai akimkabidhi zawadi mmoja kati ya washindi wa mashindano ya Quran yaliyofanyika katika Kijiji cha Pahi kilichopo Wilayani Kondoa Jijini Dodoma. Kulia ni Sheikh Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Mustafa Shaban, Spika alikuwa Mgeni rasmi katika mashindano ya usomaji Quran yaliyoandaliwa na Mbunge wa Viti Maluum kutoka Kondoa na Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji
Spika wa Bunge, Mhe. Job Ndugai akizungumza na waumini wa dini ya kiislamu baada ya kumalizika kwa mashindano ya kuhifadhi Quran yaliyofanyika katika kijiji cha Pahi kilichopo Wilayani Kondoa Mkoani Dodoma. Spika alikuwa Mgeni rasmi katika mashindasno hayo. wa pili kulia ni Waziri wa Mambo ya Ndani ya nchi, Mhe. Mwigulu Nchemba, Mkuu wa Wilaya ya Chemba, Mhe. Simon Odunga (kulia) na Sheikh Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Mustafa Shaban (wa tatu kulia)

Spika wa Bunge, Mhe, Job Ndugai (kushoto) akikabidhiwa mifuko mia tatu (300) ya simenti kutoka kwa Meneja wa Shirika la Bima la Taifa (NIC) Tawi la Dodoma, Ndg. Halima Makange katika tukio lililofanyika jana katika Kijiji cha Pahi kilichopo Wilayani Kondoa Jijini Dodoma. Mifuko hiyo imetolewa kwa ajili ya maendeleo ya elimu kijijini hapo ikiwa ni pamoja na ujenzi wa Shule na zahanati. Katikati ni Waziri wa Mambo ya Ndani ya nchi, Mhe. Mwigulu Nchemba, wa pili kushoto ni Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Ashatu kijaji, Mbunge wa Mtwara Vijijini, Mhe. Hawa Ghasia (kushoto), Sheikh Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Mustafa Shaban na Mkuu wa Wilaya ya Chemba, Ndg. Simon Odunga aliemwakilisha Mkuu wa Mkoa wa Dodoma
Spika wa Bunge, Mhe. Job ndugai akizungumza na waumini wa dini ya kiislam na wakazi wa kijiji cha Pahi (hawapo pichani) Wilayani Kondoa Mkoani Dodoma, Baada ya hafla ya  futari iliyoandaliwa na Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Ashatu kijaji. Wa pili kushoto ni Waziri wa Mambo ya Ndani ya nchi, Mhe. Mwigulu Nchemba na kulia ni Sheikh Mkuu wa Mkoa  wa Dodoma, Mustafa Shaban. PICHA NA OFISI YA BUNGE

IJUE HISTORIA YA MUZIKI WA DISCO TANZANIA

$
0
0
Na Mwandishi wetu, Washington, DC
Nimeona nikae chini niipitie maandiko ya mhenga moja aliyeandika habari ya DISCO iliyokua na kichwa cha habari "WAHENGA TULITESA SANA ENZI ZETU DISCO LA MCHANA (BOOGIE) NA MA-DJ WAKALI!!!" mwandishi wa habari hiyo amejitahidi sana kuelezea kwa mapana ya ufahamu wake jinsi gani alivyoujua muziki wa Disco wa enzi zile waliwemo maDj wake.
Mimi nimeamua kuweka sawa baadhi ya mambo Dj Kalikali yeye alishapiga muziki YMCA wakishirikiana na Dj Niga Jay na kuna wakati pia walipiga pamoja na Dj John Peter Pantalakisi na muda mwingi John Peter Pantalakis walikua wakishirikiana na Dj Chogy Sly Dico la Born City na kuna kipindi fulani Dj Kalikali alikua Dj wa Disco la RSVP ambalo Mbowe walianzisha tawi la DICO katika hotel ya New Africa ghorofa ya saba.
Muziki wa Disco unasafari ndefu maDj wengi wa zamani walikua wanamuziki wa bendi na baadae kubadili mwelekeo na kuwa maDj kwa mfano Dj Sweet Francis na Dj Addy Sally chimbuko lao walitokea kwenye bendi na baadae miaka ya 1970 wakahamisha mawazo yao na kuwa maDj wakati huo kukiwa na Disco la Banda Beach, Sea View na madisco mengine Kilimanjaro Hotel Summit. KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA
Nataka nikupe historia ya musiki na disco theque.Africana Gogo Disco lilianza mwaka 1971 na aliyeanza kupiga disco hapo ni Bhoka Wilson (Mzimbabwe) wakati ule ikiitwa Southern Rhodesia naye alikuwa cabbaret singer Simba Grill Kilimanjaro hotel. August 1972 Dj Sweet Fransis akawa Dj hapo mpaka Nov.1973 kisha akawa Dj. Judy Kingui (Msouth Africa ambaye alikuwa mkewe Kingui aliyekuwa mwenye The Rifters Band. Judy alikuwa Dj.hapo Gogo Disco mpaka 1975.
Dj Sweet Francis jina kamaili ni Francis James Bundala,mwaka 1964 alianzisha bendi iliyoitwa The Screemers na Dj Sweet Francis akiwa mwimbaji(singer) hapo ndipo alipopewa jina la SWEET baada ya kusikia sauti yake na jinsi alivyokuwa akiimba iliwakuna sana na wakawa wanasema "YOUR VOICE IS SO SWEET " na ndiyo hapa akawa anaitwa Sweet. Hiyo ni hapa Dar.Bendi The Screamers ilidumu muda mfupi. Mwaka 1965 alianzish a bendi nyingine ya watu 5 wakaiita The Hot Five wakawa wanapiga bugi kila Jumapili mchana hapo Arnatoglo hall Mnazi mmoja. Wakawa wanashindana na bendi ilikuwa inaitwa The Flamming Star.
Mwaka 1967 June The Hot Five ikavunjika. 1967 Sept. Dj Sweet Francis na aliyekuwa Solo guitarist wakaanzisha bendi nyingine wakapata watu wengine 3 ambao walianza kuwafundisha ambao walikuwa mpiga bass, mpiga rythym na drummer. Bendi wakaiita The TONICS. Mwimbaji- Sweet, Solo- Michael Jackson, Rythym- Green Jackson. Bass- John Morand na Drums- Charles Alowasa. 
Baada ya mazoezi makali mwezi November1967 wakaapata mkataba wa kupiga muziki kila siku hapo Splendid Hotel iliyokuwa inamilikiwa na mtaliano aliyeitwa MOSKA mtaa wa Samora zamani ukiitwa Independence Ave.
Siku moja wakati wanapiga muziki jamaa mmoja ambaye hawakuwa na mazoea naye akaja kwenye stage akaomba apige bongos wakamruhusu, wakati Dj Sweet Francis anaimba na yule jamaa akawa amapiga bongos vizuri sana Dj Sweet Francis akawaambia wenzake kuwa anafaa kuwa drummer lakini wenzake walimkatalia na baada ya kuwasihi sana walikubali kwa sharti kuwa amfundishe kupiga drums mpaka ajue. 
Baada ya kumfundisha kwa muda mfupi akaona ameelewa na baada ya kumpa nafasi kwenye stage alipiga drums na wenzangu wakamfurahia, huyo alikuwa anaitwa Adam Salehe Mwambile (R.I.P.) na tangu siku hiyo Dj Swett Francis akamwambia kuazia leo utaitwa ADDY SALLY, ilikuwa mwezi April 1968, hilo ndiyo lilikuwa chimbuko la ADDY SALLY. 
May 1968 mkataba ulimalizika hapo Splendid wakaamua kwenda mikoani.Wakati wote huo Dj Sweet Francis alikuwa mfanyakazi wa NPF sasa ni NSSF.
Dj Sweet Franacis aliamua kuacha kazi maana alivutiwa sana na muziki. July 1968 walifika Arusha wakiwa wanamuziki 5 na fundi mitambo aliyejulikana kwa jina Joseph Magali. 
Yule drummer wa kwanza .walimwacha baada ya kumwona Dj Addy Sally anafaa zaidi. March 1970 Dj Sweet Francis walirudi Dar. May1970 Dj Sweet Francis na Addy waliacha bendi kwa kutoelewana na Michael Jackson ambaye ndiye aliyekuwa kiongozi wa Bendi.
July 1970 Dj Sweet Francis alienda Mombasa na kuanza kuimba na Sunshine club. Mwezi Sept.1970 Dj Sweet Francis alimwita Dj Addy Sally Mombas akawa anapiga drums Central night club, May 1971 wakarudi wote Dar. 
Wakati huo The Tonics wakiwa Nairobi waliwaita Dj Sweet Francis na Addy Sally huko, Dj Sweet Francis alikataa ila Dj Addy Sally akaenda.
Dj Sweet Francis akawa anaimba mara moja moja Simba grill Kilimanjaro Hotel wakiwa na bendi kutoka Spain iliyoitwa Los Valdos na hotel ikiwa ya chini ya raia kutoka Israel aliyejulikana kwa jina la LEVY na meneja mkuu wa hotel akiitwa FERGUSON raia wa Canada.
Kwa vile Africana hotel ilijengwa kutokana na faida ya pesa za Kilimanjaro hotel hivyo mmiliki alikuwa mmoja na mwaka 1971 ilianzishwa Gogo Disco baada ya kuhamisha disco kutoka Summit, Kilimanjaro hotel kwenda Afrikana. Bokha Wilson alikuwa msanii wa Cabaret Simba grill pia kuwa Dj. Summit akahamishiwa Gogo disco hotel Africana. August 1972 Bokha Wilson akarudishwa Simba grill na Dj Sweet Francis akapelekwa Africana Hotel kuwa Disc Jockey Gogo Disco Theque.
Wote waliotajwa hapo mwanzo wameshatangulia mbele ya haki isipokuwa Dj Sweet Francis na Bhoka Wilson hatuna taarifa zake, miaka ya 80 alikuwa Ujerumani. baada ya kuwa Dj wa Gogo disco.
Mwisho wa mwaka wa 1972 alikuja Dj. Mactwist akaanza kupiga disco Sea view hotel, nalo likaitwa Sansui disco,
Dj Mactwist hakudumu sana na badala yake Dj.Addy Sally akawa Dj hapo Sansui disco. Mwezi Nov.1973 Dj Sweet Frncis akapata mkataba mwingine wa kupiga disco Lusaka Zambia katika Club Lagondol.
Baada ya muda fulani Dec.1974 Di Sweet Francis alirudi Dar kwa lilizo na alipotembelea Kilimanjaro Hotel wakampa kazi ya kutafuta bendi wafanye mazoezi kisha tarehe 25 Dec 1974 wakapige kwenye sherehe ya Ubalozi wa Marekani, Dj Sweet Francis aliichukua bendi ya The Rifters wakaenda kupiga na wote wa Ubalozi walifurahia sana mpaka Kilimanjaro Hotel wakawapa nafasi ya kupiga Simba grill mkesha wa mwaka mpya tarehe 31, Dec 1974 na cha ajabu siku hiyo wote wafanyakazi na Maafisa wa Ubalozi wa Marekani nchini Tanzania walikuja Simba grill.
Baada ya hapo Dj Sweet Francis alirudi Lusaka. Wakati ule karibu wote kwenye Ubalozi wa Marekani walikua Wamarekani weusi.
Mwaka 1975 July Dj Sweet Francis alirudi tena Dar kwa likizo ndipo alimkuta Dj Addy Sally akipiga disco Mlimani Park huo ulikuwa wakati wa BUMPING. Baada ya mwezi mmoja alirudi Lusaka. 
Mwezi June 1976 Dj Sweet Francis aliitwa Arusha kufungua The Cave Disco Safari hotel, alifika Arusha tar.28 June 1976 kutoka Lusaka, alifungua The Cave Disco tar. 17June.1976, pia alimkuta Arusha Dj Addy Sally na disco la ARUSHA BY NIGHT. January 1977 Dj Addy Sally akaagiza wacheza show Nairobi na Dj Sweet Francis akaleta wacheza show watatu kutoka Dar nao walikuwa Dj Choggy Sly (R.I.P.), Anna Simba na Mwanahamisi hata hivyo Dj Sweet Francis na Dj Addy Sally walikuwa wanashirikiana sana hapo Arusha. March 1977 Dj Addy Sally akurudi Dar. na baadae nae Dj Sweet Francis July 1977 akarudi Dar na kumwachia Dj Choggy Sly akiwa Dj wa Cave Disco Safari Hotel- Arusha. 
Mwaka 1977 Dec. Dj Sweet Francis alienda Durban Afrika Kusini alienda kuimba Cosmo night club, Febr 1978 alienda Brazil, kwa vile kule wanatumia lugha ya kireno ilibidi ajifunze nyimbo za kiportugese, alirudi Dar. May 1978 na Aug. 1978 akaaenda kuwa mwimbaji wa Cabaret Simba Grill, alikuta bendi ya vijana Watanzania wakipiga Simba Grill baada ya muda wakamaliza mkataba wao, akaingia mzee Makassy ikabidi wajifunze nyimbo zake za show na mzee Makassy aliipenda sana nyimbo moja ya kireno.
Dj Sweet Francis nae mkataba wake ukaisha. Cabaret singer au cabaret artist ni kuwa bendi ikiwa inapiga musiki Wateja huwa wanacheza lakini wakati wa cabaret huwa ni muziki maalum wa muda wa dakika 30 au 45, watu wanakuwa wamekaa na musiki huwa umesimama, cabaret singer unatangazwa kwa kishindo kisha anaingia kwa mbwembwe ukumbini watu wanampigia makofi kisha unaanza kuimba kisha anazungumza nao kwenye kipaza sauti au unatoa matani kisha anaendelea kuimba kwa mpangilio aliouweka baada ya muda wake wa show kuisha anawaaga na wakati anatoka anapigiwa makofi na muda wake unakuwa umeisha na musiki wa bendi unaendelea kama kawaida. 
Na wakati anafanya cabaret hasimami kwenye jukwaa Bali anaimba huku akizungukia wateja. Hii ndiyo CABARET.
Sept.1978 Dj Addy Sally alienda Lusaka kuwa Dj Club 2000 disco, huko Dj. Addy Sally alipata umaarufu sana kutokana na ujio wa James Brown, kwa kuwa mipigo ya drums nyimbo za James Brown Addy alikuwa anapatia sana. James Brown alifanya show Intercontinental Hotel na Addy Sally akampigia drums. 
James Brown alimfurahia sana Addy Sally na siku ya pili James Brown akaamua kutembelea Disco la Addy Sally na ndipo Addy Sally alipopata umaarufu sana Lusaka. Dj Sweet Francis alienda Lusaka Jan.1979 kumtembelea Addy na kukutana na hizo sifa na Addy Sally akampa picha aliyopiga na James Brown ambayo Dj Sweet Francis anayo mpaka leo na mwisho wa Jan.1979 Dj Sweet Francis akarudi Dar. na Addy Sally akaendelea kupiga Disco hapo Club 2000, Lusaka. 
Mwezi May 1979 Dj Sweet Francis alienda Bandari Grill ghorofa ya 6 New Africa Hotel, Makassy Orchestra walikuwa wanapiga hapo , Dj Sweet Francis akawa amekaa kwenye meza wakiwa wanne ila mmoja walikuwa hawafahamiani, baada ya bendi kupata mapumziko, Mzee Makasy alipita karibu ya meza waliyokuwa wamekaa Dj Sweet Francis na wenzake alipomuonana akamuomba wakirudi kwenye stage Dj Sweet Francis akaimbe wimbo wa kireno aliokua akiuimba Simba Grill. 
Dj Sweet Francis alipanda kwenye stage na kuanza kuimba, cha ajabu kila mtu aliufurahia sana huo wimbo na walimshangilia sana na aliporudi mezani kwake, yule jamaa ambaye hakumjua alisimama akampa mkono akasema " Kumbe hapa tumekaa na mwanamuziki mzuri hivi, (akaendelea) Sikia kijana mimi najenga hotel hapo mtaa wa Uhuru na karibu kumalizika, hivyo ikiwa tayari wewe nataka uanze muziki hapo. Dj Sweet Francis akamkubalia, Hotel ikawa tayari Nov.1979 na kabla ya Dj Sweet Francis hajajiunga na Keys Hotel alipiga Disco kwa muda mfupi Mbowe Hotel na hapo ndipo alipomfundisha Dj.Jerry Kotto na Dj Sweet Francis akaanza kupiga Disco Keys Hotel Dec.1979.
Baada ya Addy Sally kurudi toka Lusaka, mwezi April 1980 wakawa pamoja hapo Keys Hotel akiwa vyombo vya Disco vipya kabisa vikiitwa M3. waliendelea pamoja hapo Keys Hotel lakini kufika Dec.1980 Dj Sweet Francis walishindwa kuelewana na Addy, ikabidi Addy aondoke.
Jan.1981 Dj Sweet Francis akawa na Dj. Seydou na baada ya muda kidogo Dj.Seydou akaondoka baada ya mzee Ndesamburo (R.I.P) kununua vyombo vya Disco na baada ya hapo Dj Sweet Francis akapiga Disco na Dj Johnson Pantaleo (R.I.P) na ndiye Dj Sweet Francis aliyemuacha Keys hotel,
June 1981 ndio ukawa mwisho Dj Sweet Francis wa kupiga disco.
Mwezi Sept.1981 Dj Sweet Francis alienda Ujerumani na nchi zingine za Ulaya, alirudi Dar. Sept.1983 baada ya mapumziko 1993 Oct. akaanza tena kuwa Cabaret singer hapo International Pub, Kijitonyama nyuma ya Sayansi na Teknolojia mpaka June-August 1994. Sept 1994 Simba Grill Kilimanjaro Hotel. Nov.2003--June 2004 Cine Club. Hii ndiyo historia yake katika tasnia ya muziki. Mwanamuziki na Disc Jockey "SWEET FRANCIS."
Baada ya kumalizana na hiyo historia ndefu na nzuri ya Dj Sweet Francis sasa turudi tena kwenye historia ya Disco wakiwemo maDj wake.
Disco la Motel Villa pamoja na madj wengi kupitia hapa lakini dj maarufu wa hapo alikua Kim and The Boys ambaye pia kuna wakati alikua maarufu katika kupromoti madansa.
Paul Mc Ghee alianzia Morogoro akiwa na disco la Biribi likiwa chini ya usimamizi wa kaka yake Joseph Kusaga anayeitwa Justine Kusaga. Baadae Disco lilikua chini ya usimamizi wa Joe Kusaga nakubadilika jina na kua Mawingu Dj alikua Paul Mc Ghee na baadae Disco lilihamia Dar likiwa linapiga muziki wake Salender Bridge na ndio ukawa mwanzo wa kukua kwa Disco hilo na kuendelea kupiga Motel Agip, Pool side hotel ya Kilianjaro kila Jumapili, New Africa ghorofa ya Saba, Twiga na baadae wakaanzisha Disco la Bolingo Tazara, na kuendelea kupanua wigo wao mpaka Arusha. Clouds walikua na maDj wengi na Disco hili lilikuza vipaji, vijana wengi wa enzi hizo wakiwemo Boni Luv, Stev B (R.I.P.), Rankim Ramadhani (R.I.P.) na wengine wengi wakiwasaidia maDj Jesse Malongo, Dj Young Ray akiwemo Joseph Kusaga mwenyewe.
Disco la Space 1900 wakati huo likiwa chini ya usimamizi Sudi Ally Salehe lilianzia Mbowe chini ya maDJ Saydou na Gerry Kotto na Sudi Ally Salehe walikua washirika na Dj Saydou walichangia vyombo vya muziki disco pamoja.
Baada ya Sudi Salehe kuwa kushirikiana na Dj Saydou kwa muda, siku moja maelewano hayakua mazuri wakafarakana na Dj Saydou kuondoka space 1900 na ndio ukawa mwanzo wa kuingia maDj Chris Phaby, Ebony woo Jack na wengineo.
Mwaka 1987 Disco la Space 1900 liliingia mkataba na Ushirika Club (Magoti) kufanyia matengenezo jengo na wao kufunga vyombo vipya vya muziki kwa muda wa makubaliano yao mpaka watakapo maliza deni Disco lao lilikua likiitwa Vision 1900 na baadae walianzisha Disco lingine hotel Continental lililokua maarufu kwa jina la Valentino na huo ndio ukawa mwanzo wa kuingia kwa Dj Danny Star ambaye alitokea Zambia wakishirikiana na Dj Lawrence Kadri, Richie Dillon na baadae space 1900 walianzisha Dico toto YMCA, na Vision 1900 na pia Space 1900 walishapiga muziki wao Msasani Beach Club kabla ya Jetset ya Dj Russell kukamata Club hiyo ya jeshi la JWTZ.
MaDj wengine waliofanya kazi na Space 1900 walikua ni Joe Holela, Paul Mc Ghee, Super Deo, Young Millionaire, John Kitambi, Mr A na Dj Luke Joe.
Dj Richie Dillon ndie Dj alikuwa kati ya maDj wa kwanza kwanza kuingiza mixing ya beat to beat Tanzania miaka ya 1990 huko Mwanza yeye alianzia muziki wake 1984-85 Disco la Alshars Tikkha Disco na baadae akajiunga na Golden Gates Discotheque Mwanza hotel, baadae alijiunga na Disco la Magnum kabla hajahamia Nairobi mwaka 1987-88 alipokwenda kupata ujuzi wa kumix beat to beat mixing katika club ya Boomerang chini ya marehemu Majid Fundikirs(Dj Tubbs) na boss wake Dj Pacco Perez kabla ya kurudi tena na kujiunga na Disco la Magnum 1990 na baadae aliingia Dar kwa kupiga Disco la Valentino, Club Mix (cassanova Masaki) na kurudi tena Continental wakati huo akiwa na Dico la Club Mix, pia alishapiga ghorofa ya saba Clouds, Twiga Hotel na Clouds na kuhamia Club ya Bilicanas upande wa Casino.
Madisco mengine aliyopiga ni - Masuka Motel - Morogoro- Butiama Hotel - Shinyanga.
- Pamba Roof Hotel Mwanza- Oysterbay Hotel - Club Mix- XTC - Oysterbay Hotel- La Dolce Vita.
- Dar Institute- Kilimanjaro Hotel - Swimming Pool (Clouds)- Bahari Beach Hotel (Clouds)
Disco lingine lililotamba miaka hiyo ni Disco Parliament chini ya maDj Big Joe na Dj Piopose katika miaka 1986-1990 waporomosha muziki wao Kunduchi Beach hotel, Dj Big Joe ambaye jina halisi ni Joseph Shawa na Dj Piopose akijulikana kama Pius Ntare walipiga muziki pia katika sherehe mbalimbali.
Disco la Parliament lilipiga muziki wake kwenye club ya Princes chini ya Dj Joe na Dj Edo Cool.
Dj Eddie Grant uDj wake ulianzia mtaani enzi hizo alipokua akiishi Kurasini mwaka 1988 na baadae akajiunga na Biashara Club akiwa kama dj wa Silver Town Disco Sound maisha yake ya uDj ndio yakawa yameanzia hapo na baadae alijiunga na Studio 35 pale High Way wakiwa pamojana Dj Cool Joe (R.I.P) hii ilikua ni 1989 wakati huo akiwa mwanafunzi NVTC Chang'ombe na baada ya kumaliza chuo alijiunga na FM55 Disco Iringa Club, mkoani Iringa 1989-1989 na baadae 1991 alihamia jijini Mwanza na kujiunga na Disco lililokua likiendesha shughuli zake Nata Hotel na kwa umahiri wake wa kupiga muziki alifanikiwa kuwakamata wadau na wapenzi wa muziki wa Disco wa jiji hilo.
Mwaka 1993 alirudi Dar na kuanza kupiga Disco Imasco Club ambako alidumu kwa miezi 7 tu kabla hajanunuliwa na tajiri kurudishwa Mwanza na yeye kuambatana na Dj Young Millionaire wakati huo Dj Young Millionaire akiwa anapiga muziki Vision 1900 wakati huo Disco hilo la Vision likiwa halifanyi vizuri. Dj Eddie Garant na Dj Young Millionare wakaelekea Mwanza na kuwa waajiriwa wa na KAM Disco ndani ya hotel ya Deluxe. Dj Eddie Grant alipiga muziki hapo kwa miaka 8 na kupata mafanikio makubwa na kuweza kununua sound yake mwenyewe na kuanza kupiga muziki wa party na matamasha mbalimbali na mwaka 1999 wakaanzisha yeye na Clouds Disco la Bolingo Yatch Club na mwaka 2000 mpaka 2003 akaanzisha Disco Club Capri Cabana , mwaka 2005 akapiga Rumours Pab muziki wa Old school na katika ufunguzi huo aliwaalikamaDj Saydou, JP Pantalakis, Kim and The Boys na Dj Coll Joe.
Dj mwingine aliyetamba ni Dj Habib ambaye kwa sasa anaendesha maisha yake nchini Uingereza, Dj Huyu mahiri alianza muziki wa Disco Club ya Bilicanas 1994 wakati huo akiwa na Dj 45 na Dj Luke Joe na baadae alijiunga na Mambo Club 2000-2001. Kwa sasa Dj Habib yupo Uingereza anapiga Club ya Tiger Tige ambayo alianzia kupiga kuanzia 2010.
Dj Luke Joe alianza safari yake ya uDj mwaka 1978 wakati huo akiwa sekondari baada meneja wa Disco la Stereo II Michael Kisaka kufuata na kumwomba ajiunge na Disco hilo baada ya Dj Agib Show kuwazengua kwa kudai kulipwa zaidi. Dj Luke Joe alijiunga rasmi na Stereo II ambayo ilikua chini ya mmiliki Kessy Sakapala (R.I.P.) meneja akiwa Michael Kisaka na baada ya muda Disco lilihamia Kunduchi beach hotel.
Mwaka 1981 Disco liliingia mkataba na Ushirika Club (Magoti) na Dj Luke Joe akipiga Disco peke yake na wakati huo kulikua na bendi ya Ushirika wana njatanjata iliyokua ikipiga muziki wa dansi siku ya Jumatatu hadi alhamisi na Disco likianzia Ijumaa hadi Juamapili. Dj Franco Kabigi (R.I.P.) alijiunga baadae mwaka 1982 na kuendelea kusumbua kwenye jiji la Dar enzi hizo huku wakichuana vikali na Mbowe Hotel iliyokuwa chini ya madj wake Saydou na Jerry Kotto na YMCA kukiwa na DJ Kalikali (R.I.P.) na Niga Jay.
Enzi hizo madisco hayo yalikua yakishindana na nyimbo mpya kila Disco utakuta madj kupiga nyimbo kali huku baadhi yao wakiwa na baadhi ya nyimbo zisizo fanana.
Mwaka 1987 Kessy Sakapala aliumuuzia Disco shemeji yake Mvungi wakati huo akiwa meneja wa Tanesco Iringa na Stereo II ikaendeleo kutesa Railway Club Iringa na DJ Sweet Coffee alijiunga kumwongezea nguvu Dj Luke Joe na mwaka 1989 ulikuja ujio wa Disco la XTC na kupiga muziki wake Iringa Club na ndio ikawa chanzo cha Disco la Stereo II kuporomoka na kupiga sabasaba Iringa na baadae Makambako na mwaka 1990 Dj Luke Joe alifiwa na baba yake na yeye kuelekea Tarime kwa mazishi, wakati Dj Luke Joe akirudi kutoka tarime alikutana na Dj Richie Dillon Mwanza na kukubaliana amwonyeshe jinsi ya kumix beat na beat kwani Dj Richie Dillon alikua dj wa kwanza Tanzania kujua kupandishia muziki kwa beat zinazofanana.
Dj Luke aliporudi Iringa alihamia Disco la Ruaha International wakati huo likiwa chini ya Hussein Kipara aliyekua amekuja na vyombo vya Disco pale na baadae Disco lilihamia kwenye uwanja Samora kabla halijamaliza muda wake. na Dj Luke Joe kurudi Dar na kujiunga na Space 1900 na kuanza kupiga Disco Vision 1900 pale ushirika Club (Magoti).
Dj Luke Joe aliendelea kuwa chini ya Disco la space 1900 kwa kupiga madisco ya Space 1900 kama vile Lang'ata, Valentino, Boogie YMCA na baadae kuwa mshindi wa mashindano ya madj yaliyofanyika Lang'ata chini ya marehemu Shaban Sato.
Mwaka 1994 Dj Luke Joe alijiunga na Bilicanas akiwana Madj wengine Dj Habib na Dj 45, hapo alipiga Disco kwa mwaka mmoja kabla hajahamia Mambo Club mwaka 1995 na baada ya miaka miwili Mambo Club ilifungwa kwa kufanyiwa marekebisho na maDj wengine aliopiga nao hapo Mambo Club walikua ni Dj MacKay, Dj Vumi, Dj Rico (R.I.P) na Dj Ommy.
Mwaka 1997 Dj Luke Joe alipiga Disco la Bolingo FM Club (Lang'ata) likiwa chini ya Felician Mutta akiwa na Dj Kishoka na baadae akajiunga Dj Venture na FM wakaanzisha Dico lingine IMASCO Temeke na Dj Luke Joe na Dj Kishoka wakahamishiwa huko wakimwacha Dj Venture FM Club akishirikiana na bendi ya FM Academia.
Mwishoni mwa 1998 Dj Luke Joe alirejea Mambo Club na kupiga Disco hapo mpaka mwaka 1999 na baadae kuondoka kuelekea Marekani na kupiga muziki wa Disco katika club mbalimbali na majimbo tofauti.
Hii ni historia ya baadhi ya madj waliotamba Tanzania shukrani kwa madj waliokubali kushirikiana kuandika historia hii wakishiirikiana na Dj Luke Joe.
Luke Joe Jun 9 (2 days ago) to issa, Mubelwa, Cassius, pamojapure, me Translate message Turn off for: Swahili naomba mtumie hii asante 
Baada ya kumfundisha kwa muda mfupi akaona ameelewa na baada ya kumpa nafasi kwenye stage alipiga drums na wenzangu wakamfurahia, huyo alikuwa anaitwa Adam Salehe Mwambile (R.I.P.) na tangu siku hiyo Dj Swett Francis akamwambia kuazia leo utaitwa ADDY SALLY, ilikuwa mwezi April 1968, hilo ndiyo lilikuwa chimbuko la ADDY SALLY. 
May 1968 mkataba ulimalizika hapo Splendid wakaamua kwenda mikoani.Wakati wote huo Dj Sweet Francis alikuwa mfanyakazi wa NPF sasa ni NSSF.
Dj Sweet Franacis aliamua kuacha kazi maana alivutiwa sana na muziki. July 1968 walifika Arusha wakiwa wanamuziki 5 na fundi mitambo aliyejulikana kwa jina Joseph Magali. 
Yule drummer wa kwanza .walimwacha baada ya kumwona Dj Addy Sally anafaa zaidi. March 1970 Dj Sweet Francis walirudi Dar. May1970 Dj Sweet Francis na Addy waliacha bendi kwa kutoelewana na Michael Jackson ambaye ndiye aliyekuwa kiongozi wa Bendi.
July 1970 Dj Sweet Francis alienda Mombasa na kuanza kuimba na Sunshine club. Mwezi Sept.1970 Dj Sweet Francis alimwita Dj Addy Sally Mombas akawa anapiga drums Central night club, May 1971 wakarudi wote Dar. 
Wakati huo The Tonics wakiwa Nairobi waliwaita Dj Sweet Francis na Addy Sally huko, Dj Sweet Francis alikataa ila Dj Addy Sally akaenda.
Dj Sweet Francis akawa anaimba mara moja moja Simba grill Kilimanjaro Hotel wakiwa na bendi kutoka Spain iliyoitwa Los Valdos na hotel ikiwa ya chini ya raia kutoka Israel aliyejulikana kwa jina la LEVY na meneja mkuu wa hotel akiitwa FERGUSON raia wa Canada.
Kwa vile Africana hotel ilijengwa kutokana na faida ya pesa za Kilimanjaro hotel hivyo mmiliki alikuwa mmoja na mwaka 1971 ilianzishwa Gogo Disco baada ya kuhamisha disco kutoka Summit, Kilimanjaro hotel kwenda Afrikana. Bokha Wilson alikuwa msanii wa Cabaret Simba grill pia kuwa Dj. Summit akahamishiwa Gogo disco hotel Africana. August 1972 Bokha Wilson akarudishwa Simba grill na Dj Sweet Francis akapelekwa Africana Hotel kuwa Disc Jockey Gogo Disco Theque.
Wote waliotajwa hapo mwanzo wameshatangulia mbele ya haki isipokuwa Dj Sweet Francis na Bhoka Wilson hatuna taarifa zake, miaka ya 80 alikuwa Ujerumani. baada ya kuwa Dj wa Gogo disco.
Mwisho wa mwaka wa 1972 alikuja Dj. Mactwist akaanza kupiga disco Sea view hotel, nalo likaitwa Sansui disco,
Dj Mactwist hakudumu sana na badala yake Dj.Addy Sally akawa Dj hapo Sansui disco. Mwezi Nov.1973 Dj Sweet Frncis akapata mkataba mwingine wa kupiga disco Lusaka Zambia katika Club Lagondol.
Baada ya muda fulani Dec.1974 Di Sweet Francis alirudi Dar kwa lilizo na alipotembelea Kilimanjaro Hotel wakampa kazi ya kutafuta bendi wafanye mazoezi kisha tarehe 25 Dec 1974 wakapige kwenye sherehe ya Ubalozi wa Marekani, Dj Sweet Francis aliichukua bendi ya The Rifters wakaenda kupiga na wote wa Ubalozi walifurahia sana mpaka Kilimanjaro Hotel wakawapa nafasi ya kupiga Simba grill mkesha wa mwaka mpya tarehe 31, Dec 1974 na cha ajabu siku hiyo wote wafanyakazi na Maafisa wa Ubalozi wa Marekani nchini Tanzania walikuja Simba grill.
Baada ya hapo Dj Sweet Francis alirudi Lusaka. Wakati ule karibu wote kwenye Ubalozi wa Marekani walikua Wamarekani weusi.
Mwaka 1975 July Dj Sweet Francis alirudi tena Dar kwa likizo ndipo alimkuta Dj Addy Sally akipiga disco Mlimani Park huo ulikuwa wakati wa BUMPING. Baada ya mwezi mmoja alirudi Lusaka. 
Mwezi June 1976 Dj Sweet Francis aliitwa Arusha kufungua The Cave Disco Safari hotel, alifika Arusha tar.28 June 1976 kutoka Lusaka, alifungua The Cave Disco tar. 17June.1976, pia alimkuta Arusha Dj Addy Sally na disco la ARUSHA BY NIGHT. January 1977 Dj Addy Sally akaagiza wacheza show Nairobi na Dj Sweet Francis akaleta wacheza show watatu kutoka Dar nao walikuwa Dj Choggy Sly (R.I.P.), Anna Simba na Mwanahamisi hata hivyo Dj Sweet Francis na Dj Addy Sally walikuwa wanashirikiana sana hapo Arusha. March 1977 Dj Addy Sally akurudi Dar. na baadae nae Dj Sweet Francis July 1977 akarudi Dar na kumwachia Dj Choggy Sly akiwa Dj wa Cave Disco Safari Hotel- Arusha. 
Mwaka 1977 Dec. Dj Sweet Francis alienda Durban Afrika Kusini alienda kuimba Cosmo night club, Febr 1978 alienda Brazil, kwa vile kule wanatumia lugha ya kireno ilibidi ajifunze nyimbo za kiportugese, alirudi Dar. May 1978 na Aug. 1978 akaaenda kuwa mwimbaji wa Cabaret Simba Grill, alikuta bendi ya vijana Watanzania wakipiga Simba Grill baada ya muda wakamaliza mkataba wao, akaingia mzee Makassy ikabidi wajifunze nyimbo zake za show na mzee Makassy aliipenda sana nyimbo moja ya kireno.
Dj Sweet Francis nae mkataba wake ukaisha. Cabaret singer au cabaret artist ni kuwa bendi ikiwa inapiga musiki Wateja huwa wanacheza lakini wakati wa cabaret huwa ni muziki maalum wa muda wa dakika 30 au 45, watu wanakuwa wamekaa na musiki huwa umesimama, cabaret singer unatangazwa kwa kishindo kisha anaingia kwa mbwembwe ukumbini watu wanampigia makofi kisha unaanza kuimba kisha anazungumza nao kwenye kipaza sauti au unatoa matani kisha anaendelea kuimba kwa mpangilio aliouweka baada ya muda wake wa show kuisha anawaaga na wakati anatoka anapigiwa makofi na muda wake unakuwa umeisha na musiki wa bendi unaendelea kama kawaida.
Luke Joe Jun 9 (2 days ago) to issa, Mubelwa, Cassius, pamojapure, me Translate message Turn off for: Swahili samahani naomba mtumie hii .
Mwaka 1967 June The Hot Five ikavunjika. 1967 Sept. Dj Sweet Francis na aliyekuwa Solo guitarist wakaanzisha bendi nyingine wakapata watu wengine 3 ambao walianza kuwafundisha ambao walikuwa mpiga bass, mpiga rythym na drummer. Bendi wakaiita The TONICS. Mwimbaji- Sweet, Solo- Michael Jackson, Rythym- Green Jackson. Bass- John Morand na Drums- Charles Alowasa. 
Baada ya mazoezi makali mwezi November1967 wakaapata mkataba wa kupiga muziki kila siku hapo Splendid Hotel iliyokuwa inamilikiwa na mtaliano aliyeitwa MOSKA mtaa wa Samora zamani ukiitwa Independence Ave.
Siku moja wakati wanapiga muziki jamaa mmoja ambaye hawakuwa na mazoea naye akaja kwenye stage akaomba apige bongos wakamruhusu, wakati Dj Sweet Francis anaimba na yule jamaa akawa amapiga bongos vizuri sana Dj Sweet Francis akawaambia wenzake kuwa anafaa kuwa drummer lakini wenzake walimkatalia na baada ya kuwasihi sana walikubali kwa sharti kuwa amfundishe kupiga drums mpaka ajue. 
Baada ya kumfundisha kwa muda mfupi akaona ameelewa na baada ya kumpa nafasi kwenye stage alipiga drums na wenzangu wakamfurahia, huyo alikuwa anaitwa Adam Salehe Mwambile (R.I.P.) na tangu siku hiyo Dj Swett Francis akamwambia kuazia leo utaitwa ADDY SALLY, ilikuwa mwezi April 1968, hilo ndiyo lilikuwa chimbuko la ADDY SALLY. 
May 1968 mkataba ulimalizika hapo Splendid wakaamua kwenda mikoani.Wakati wote huo Dj Sweet Francis alikuwa mfanyakazi wa NPF sasa ni NSSF.
Dj Sweet Franacis aliamua kuacha kazi maana alivutiwa sana na muziki. July 1968 walifika Arusha wakiwa wanamuziki 5 na fundi mitambo aliyejulikana kwa jina Joseph Magali. 
Yule drummer wa kwanza .walimwacha baada ya kumwona Dj Addy Sally anafaa zaidi. March 1970 Dj Sweet Francis walirudi Dar. May1970 Dj Sweet Francis na Addy waliacha bendi kwa kutoelewana na Michael Jackson ambaye ndiye aliyekuwa kiongozi wa Bendi.
July 1970 Dj Sweet Francis alienda Mombasa na kuanza kuimba na Sunshine club. Mwezi Sept.1970 Dj Sweet Francis alimwita Dj Addy Sally Mombas akawa anapiga drums Central night club, May 1971 wakarudi wote Dar. 
Dj Sweet Francis alipanda kwenye stage na kuanza kuimba, cha ajabu kila mtu aliufurahia sana huo wimbo na walimshangilia sana na aliporudi mezani kwake, yule jamaa ambaye hakumjua alisimama akampa mkono akasema " Kumbe hapa tumekaa na mwanamuziki mzuri hivi, (akaendelea) Sikia kijana mimi najenga hotel hapo mtaa wa Uhuru na karibu kumalizika, hivyo ikiwa tayari wewe nataka uanze muziki hapo. Dj Sweet Francis akamkubalia, Hotel ikawa tayari Nov.1979 na kabla ya Dj Sweet Francis hajajiunga na Keys Hotel alipiga Disco kwa muda mfupi Mbowe Hotel na hapo ndipo alipomfundisha Dj.Jerry Kotto na Dj Sweet Francis akaanza kupiga Disco Keys Hotel Dec.1979.
Baada ya Addy Sally kurudi toka Lusaka, mwezi April 1980 wakawa pamoja hapo Keys Hotel akiwa vyombo vya Disco vipya kabisa vikiitwa M3. waliendelea pamoja hapo Keys Hotel lakini kufika Dec.1980 Dj Sweet Francis walishindwa kuelewana na Addy, ikabidi Addy aondoke.
Jan.1981 Dj Sweet Francis akawa na Dj. Seydou na baada ya muda kidogo Dj.Seydou akaondoka baada ya mzee Ndesamburo (R.I.P) kununua vyombo vya Disco na baada ya hapo Dj Sweet Francis akapiga Disco na Dj Johnson Pantaleo (R.I.P) na ndiye Dj Sweet Francis aliyemuacha Keys hotel,
June 1981 ndio ukawa mwisho Dj Sweet Francis wa kupiga disco.
Mwezi Sept.1981 Dj Sweet Francis alienda Ujerumani na nchi zingine za Ulaya, alirudi Dar. Sept.1983 baada ya mapumziko 1993 Oct. akaanza tena kuwa Cabaret singer hapo International Pub, Kijitonyama nyuma ya Sayansi na Teknolojia mpaka June-August 1994. Sept 1994 Simba Grill Kilimanjaro Hotel. Nov.2003--June 2004 Cine Club. Hii ndiyo historia yake katika tasnia ya muziki. Mwanamuziki na Disc Jockey "SWEET FRANCIS."
Baada ya kumalizana na hiyo historia ndefu na nzuri ya Dj Sweet Francis sasa turudi tena kwenye historia ya Disco wakiwemo maDj wake.
Disco la Motel Villa pamoja na madj wengi kupitia hapa lakini dj maarufu wa hapo alikua Kim and The Boys ambaye pia kuna wakati alikua maarufu katika kupromoti madansa.
Paul Mc Ghee alianzia Morogoro akiwa na disco la Biribi likiwa chini ya usimamizi wa kaka yake Joseph Kusaga anayeitwa Justine Kusaga. Baadae Disco lilikua chini ya usimamizi wa Joe Kusaga nakubadilika jina na kua Mawingu Dj alikua Paul Mc Ghee na baadae Disco lilihamia Dar likiwa linapiga muziki wake Salender Bridge na ndio ukawa mwanzo wa kukua kwa Disco hilo na kuendelea kupiga Motel Agip, Pool side hotel ya Kilianjaro kila Jumapili, New Africa ghorofa ya Saba, Twiga na baadae wakaanzisha Disco la Bolingo Tazara, na kuendelea kupanua wigo wao mpaka Arusha. Clouds walikua na maDj wengi na Disco hili lilikuza vipaji, vijana wengi wa enzi hizo wakiwemo Boni Luv, Stev B (R.I.P.), Rankim Ramadhani (R.I.P.) na wengine wengi wakiwasaidia maDj Jesse Malongo, Dj Young Ray akiwemo Joseph Kusaga mwenyewe.
Hapa ni baadhi ya maDj waliokua chini ya Joe Kusaga Dj Jesse Malongo, Sterwat Chiduo (Dj Young Ray), Elliud Pemba, Dj Louis, Ebonite Who jack, Julius Tandau, Julius Kagaruki, Boni. Luv, Stev B (R.I.P.), Clouds Ma Dj tulikuwa Elliude Pemba (Elliwood), Jesse Malongo (Babyface), Joseph Kussaga (Emperor), Stuart Chiduo (Young Ray), Julius Tandau (Jet), Richard Mazula (Ebonite woo Jack)
Elliud Pemba (Dj Elliwood) safari yake ya muziki imeanzia Clouds pale Motel Agip Snack Bar, Kilimanjaro Pool Side, Seventh Floor New Africa Hotel, Dar es Salaam Institute na Twiga.
Dj Ellud Pemba ndio niliyemwachia Dj Boni luv U Dj mwaka 1992 baada ya kwenda Shule na 1994 Kuanza kazi nyingine ITV.
Disco la Space 1900 wakati huo likiwa chini ya usimamizi Sudi Ally Salehe lilianzia Mbowe chini ya maDJ Saydou na Gerry Kotto na Sudi Ally Salehe walikua washirika na Dj Saydou walichangia vyombo vya muziki disco pamoja.

RC MAKONDA AKABIDHI KADI 220 ZA BIMA YA AFYA KWA WATOTO YATIMA NA WAISHIO KATKA MAZINGIRA MAGUMU

$
0
0
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda akiwapatia kadi za bima ya Afya (Toto Afya Kadi) watoto wanaoishi kwenye mazingira magumu zilizotolewa na hospitali ya Regency na TMJ leo Jijini Dar es Salaam.
***************************************************
MKUU wa Mkoa wa Dar es salaam Paul Makonda amekabidhi kadi 220 za Bima ya Afya (Toto Afya Card) zenye thamani ya zaidi ya Sh. milioni 11 kwa watoto yatima na waishio kwenye mazingira magumu ili wapate uhakika wa matibabu mwaka mzima ikiwa ni sehemu ya Mwezi mtukufu wa Ramadhan. 
Makonda amekabidhi kadi hizo leo jijini Dar es Salaam ambapo amesema kwa kawaida Mwezi wa Ramadhan watu wamekuwa wakifuturisha watoto yatima lakini inakuwa ni chakula cha siku moja kwa hiyo katika mwendelezo wa mwezi mtukufu ameona ni vyema aguse maisha ya watoto yatima kwa kuwapatia Bima ya Afya.
Moja ya watoto wanaoishi katika mazingira magumu akifurahi baada ya kupatiwa kadi yake ya Bima ya Afya leo Jijini Dar es Salaam.
*******************************************
Aidha Makonda amesema kadi hizo zitawawezesha watoto kupatiwa matibabu Bure kwa kipindi cha mwaka mmoja katika Hospital yoyote hapa nchini.
Makonda amesema watoto waliopatiwa kadi hizo hawahusiani na wale waliojitokeza kwenye mchakato wa kutafuta haki ya mtoto ambapo ameshukuru Hospital ya Regency na TMJ kwa kujitolea kutoa kadi hizo.
Pia Makonda amesema atakabidhi pia mabegi 400 yaliyosheheni vifaa vyote vya Shule kwa vituo vya watoto yatima na waishio kwenye mazingira magumu ili wawe na uhakika wa kupata masomo mwaka mzima na kuweza kutumia vyema fursa ya elimu bure.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa Hospital ya Regency Dk. Kanabar Rajni na Mkurugenzi wa Hospital ya TMJ Parul Chhaya wamesema wameguswa kutoa msaada huo Kama sehemu ya kuunga mkono hamasa anayoitoa RC Makonda kwa wazazi kuwa na kadi za bima za afya (Toto Afya Card).
Meneja Masoko na Elimu kwa Umma wa Mfuko wa Bima ya Afya Nchini Angela Mziray amesema kuwa ugonjwa hauna muda kwahiyo kupatikana kwa kadi hizi kutasaidia sana waotot hawa kuwa na uhakika wa tiba pindi pale wanapopata maradhi na watatibiwa katika hospitali yoyote nchini.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda akizungumza na waandishi wa habari wakati wa utoaji wa kadi za bima ya Afya ( Toto Afya Kadi) kwa watoto wanaoishi kwenye mazingira magumu katika vituo vya kulelea watoto yatima Jijini Dar es Salaam.
Meneja Masoko na Elimu kwa umma NHIF Angela Mziray akizungumza na waandishi wa habari na kuwashukuru hospitali ya Regency na TMJ kuweza kulipia kadi za bima ya Afya kwa watoto 220 wanaoishi kwenye mazingira magumu Jijini Dar es Salaam.

RAIS DKT MAGUFULI AKAGUA UJENZI WA MSIKITI WA BAKWATA KINONDONI DAR, AKUTANA NA BALOZI WA VATICAN NCHINI IKULU,

$
0
0
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akilakiwa na Mfuti wa Tanzania Sheikh Aboubakary Zubeiry Ally na Balozi wa Mororcco nchini Mhe. Abdellah Benyryane wakati akiwasili kukagua maendeleo ya ujenzi wa msikiti mkuu wa Baraza Kuu la Waisalmu Tanzania (BAKWATA) unaojengwa kwa ufadhili wa Mfalme Mohamed wa Sita wa Morocco Kinondoni jijini Dar es salaam leo.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na wakandarasi wa ujenzi wakati akiwasili kukagua maendeleo ya ujenzi wa msikiti mkuu wa Baraza Kuu la Waisalmu Tanzania (BAKWATA) unaojengwa kwa ufadhili wa Mfalme Mohamed wa Sita wa Morocco Kinondoni jijini Dar es salaam leo Juni 12, 2018.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa ameongozana na Mfuti wa Tanzania Sheikh Aboubakary Zubeiry Ally na Balozi wa Mororcco nchini Mhe. Abdellah Benyryane akikagua maendeleo ya ujenzi wa msikiti mkuu wa Baraza Kuu la Waisalmu Tanzania (BAKWATA) unaojengwa kwa ufadhili wa Mfalme Mohamed wa Sita wa Morocco Kinondoni jijini Dar es salaam leo Juni 12, 2018 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akipata maelezo toka kwa Mfuti wa Tanzania Sheikh Aboubakary Zubeiry Ally na Balozi wa Mororcco nchini Mhe. Abdellah Benyryane alipokagua maendeleo ya ujenzi wa msikiti mkuu wa Baraza Kuu la Waisalmu Tanzania (BAKWATA) unaojengwa kwa ufadhili wa Mfalme Mohamed wa Sita wa Morocco Kinondoni jijini Dar es salaam leo Juni 12, 2018
Sehemu ya msikiti mkuu wa Baraza Kuu la Waisalmu Tanzania (BAKWATA) unaojengwa kwa ufadhili wa Mfalme Mohamed wa Sita wa Morocco Kinondoni jijini Dar es salaam leo Juni 12, 2018
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na Mfuti wa Tanzania Sheikh Aboubakary Zubeiry Ally akimshukuru Balozi wa Mororcco nchini Mhe. Abdellah Benyryane baada ya kukagua maendeleo ya ujenzi wa msikiti mkuu wa Baraza Kuu la Waisalmu Tanzania (BAKWATA) unaojengwa kwa ufadhili wa Mfalme Mohamed wa Sita wa Morocco Kinondoni jijini Dar es salaam leo Juni 12, 2018
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiongea na wananchi baada ya kukagua maendeleo ya ujenzi wa msikiti mkuu wa Baraza Kuu la Waisalmu Tanzania (BAKWATA) unaojengwa kwa ufadhili wa Mfalme Mohamed wa Sita wa Morocco Kinondoni jijini Dar es salaam leo Juni 12, 2018
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na Mfuti wa Tanzania Sheikh Aboubakary Zubeiry Ally na Balozi wa Mororcco nchini Mhe. Abdellah Benyryane na Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Paul Makonda akimsikiliza mjumbe wa Nyumba Kumi wa Konondoni Shamba Bw. Rashidi Mohamed Mashaushi anayeeelezea kuhusu changamoto ya barabara na mfereji wa maji eneo lao baada ya kukagua maendeleo ya ujenzi wa msikiti mkuu wa Baraza Kuu la Waisalmu Tanzania (BAKWATA) unaojengwa kwa ufadhili wa Mfalme Mohamed wa Sita wa Morocco Kinondoni jijini Dar es salaam leo Juni 12, 2018.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiaga wananchi baada ya kukagua maendeleo ya ujenzi wa msikiti mkuu wa Baraza Kuu la Waisalmu Tanzania (BAKWATA) unaojengwa kwa ufadhili wa Mfalme Mohamed wa Sita wa Morocco Kinondoni jijini Dar es salaam leo Juni 12, 2018
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na Mfuti wa Tanzania Sheikh Aboubakary Zubeiry Ally aliye na Balozi wa Mororcco nchini Mhe. Abdellah Benyryane na Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Paul Makonda baada ya kukagua maendeleo ya ujenzi wa msikiti mkuu wa Baraza Kuu la Waisalmu Tanzania (BAKWATA) unaojengwa kwa ufadhili wa Mfalme Mohamed wa Sita wa Morocco Kinondoni jijini Dar es salaam leo Juni 12, 2018
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na Balozi wa Mororcco nchini Mhe. Abdellah Benyryane aliye na Mfuti wa Tanzania Sheikh Aboubakary Zubeiry Ally na Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam baada ya kukagua maendeleo ya ujenzi wa msikiti mkuu wa Baraza Kuu la Waisalmu Tanzania (BAKWATA) unaojengwa kwa ufadhili wa Mfalme Mohamed wa Sita wa Morocco Kinondoni jijini Dar es salaam leo Juni 12, 2018.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akikutana na kufanya mazungumzo na Balozi wa Vatican Nchini Mhashama Askofu Mkuu Mrek Solezyriski Ikulu jijini Dar es salaam leo Juni 12, 2018
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimsindikiza Balozi wa Vatican Nchini Mhashama Askofu Mkuu Mrek Solezyriski baada ya kukutana na kufanya naye mazungumzo Ikulu jijini Dar es salaam leo Juni 12, 2018
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na Balozi wa Vatican Nchini Mhashama Askofu Mkuu Mrek Solezyriski baada ya kukutana na kufanya naye mazungumzo Ikulu jijini Dar es salaam leo Juni 12, 2018. PICHA NA IKULU

MATUKIO MBALIMBALI YA WAZIRI MKUU KUTOKA BUNGENI JIJINI DODOMA LEO

$
0
0
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na Naibu Waziri wa Kilimo Mary Mwanjelwa, Bungeni jijini Dodoma , leo.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akimsikiliza Makamu wa Rais wa Bunge la Afrika, Stephen Masele ambaye ni Mbunge wa Shinyanga Mjini, Bungeni jijini Dodoma. 
Waziri wa Mambo ya Ndani Mwigulu Nchemba, akizungumza Bungeni jijini Dodoma. 
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, akiteta jambo na Mbunge wa Katavi, Inj. Gerson Lwenge Bungeni jijini Dodoma. 
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa, akisalimiana na Mbunge wa Kilindi, Omari Kigua kwenye viwanja vya Bunge jijini Dodoma.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na Mwanafunzi Isack Chidodolo wa shule Chinangali Sekondari Dodoma, kwenye viwanja vya Bunge jijini Dodoma. 
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, akimsikiliza Mbunge wa Moshi vijijini,Anthony Komu, kwenye viwanja vya Bunge jijini Dodoma, katikati ni Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na Mazingira Kangi Lugola.
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, akizungumza na Mbunge wa Kasulu mjini, Daniel Nsanzugwanko, nje ya jengo la utawala Bungeni jijini Dodoma leo. Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu

CAF YATAJA WAAMUZI WATAKAOCHEZESHA YOUNG AFRICANS NA GOR MAHIA KOMBE LA SHIRIKISHO

$
0
0
SHIRIKISHO la Mpira wa Miguu Barani Africa CAF limetaja waamuzi kutoka nchini Somalia kuchezesha mchezo wa Kombe la Shirikisho hatua ya makundi kati ya Gor Mahia ya Kenya na Young Africans ya Tanzania utakaochezwa Uwanja wa Moi Kasarani Julai 18,2018.
Kwenye mchezo huo Mwamuzi wa katikati atakua Hassan Mohamed Hagi akisaidiwa na Mwamuzi namba 1 Hamza Hagi Abdi, Mwamuzi msaidizi namba 2 Suleiman Bashir Sh.Abdi na Mwamuzi wa akiba Nur Muhidin Mohamed.
Mtathmini waamuzi anatokea Gabon Jan Olivier Mbera na Kamishna wa mchezo anatokea Africa Kusini Simphiwe Brian Xaba sambamba na mratibu wa mchezo huo Nomsa Jacobeth Mahlangu.
Aidha mchezo wa marudiano kwa timu hizo utakaochezwa July 29,2018 Kwenye Uwanja wa Taifa wenyewe utachezeshwa na Waamuzi kutoka Mauritius. 
Mwamuzi wa katikati atakuwa Ahmed Imtehaz Heeralall akisaidiwa na Mwamuzi msaidizi namba 1 Cauvelet Louis Ralph Fabian,Mwamuzi msaidizi namba 2 Akhtar Nawaz Rossaye na Mwamuzi wa akiba Ganesh Chutooree.
Kamishna wa mchezo anatokea Zambia Patrick Kangwa, Mtathmini waamuzi anatokea Congo Louzaye Rene Daniel wakati Mratibu anatokea Nigeria Nasiru Sarkintudu Jibril.

KAMATI YA TUZO ZA LIGI KUU YAKAMILISHA UTEUZI WA WACHEZAJI 3 WA MCHEZAJI BORA

$
0
0
Kamati ya Tuzo za Ligi Kuu ya Vodacom (VPL), imekamilisha uteuzi wa wachezaji 3 watakaowania tuzo ya mchezaji bora wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara msimu wa 2017/2018.
Wachezaji watatu waliobaki katika kinyang'anyiro hicho ni Emmanuel Okwi, John Bocco na Erasto Nyoni wote wa Simba, ambapo kamati ya Tuzo hiyo ya Mchezaji Bora imeandaa utaratibu wa kupiga kura kuwashirikisha Wahariri wa Habari za Michezo, manahodha wa timu za Ligi Kuu ya Vodacom na makocha wa timu za Ligi Kuu. 
Pia kamati imekamilisha uteuzi wa wachezaji watakaowania tuzo katika kategori mbalimbali kwenye sherehe hizo za Tuzo ya Mchezaji Bora wa VPL itakayofanyika ukumbi wa Mlimani, City Dares Salaam Juni 23 mwaka huu.
Tuzo 16 zinatarajiwa kutolewa siku hiyo, ambapo baadhi ni za kikanuni za Ligi Kuu Tanzania Bara, ambazo tayari washindi wake wamefahamika, ambazo ni bingwa, mshindi wa pili, mshindi wa tatu, mshindi wa nne na mfungaji bora.Ukiacha hizo tano za kikanuni, zipo tuzo 10 ambazo zimefanyiwa kazi na Kamati ya Tuzo kulingana na takwimu mbalimbali za ligi hiyo, ambapo tuzo moja nyingine ya Mchezaji Bora chini ya umri wa miaka 20 (Tuzo ya Ismail Khalfan), inayohusisha vikosi vya vijana vya timu za Ligi Kuu yenyewe inaendelea kufanyiwa kazi kwa vile mashindano yanaendelea mkoani Dodoma na itakapokamilika watatangazwa wateule watatu.
Tuzo nyingine zitakazotolewa siku hiyo ni Timu yenye Nidhamu inayowaniwa na Kagera Sugar, Simba na Mtibwa Sugar, wakati Mchezaji Bora Chipukizi inawaniwa na Shaaban Idd Chilunda, Yahya Zayd (Azam) na Habibu Kiyombo (Mbao).
Mwamuzi Msaidizi Bora inawaniwa na Helen Mduma, Mohammed Mkono na Ferdinand Chacha, wakati Mwamuzi Bora wateule ni Elly Sasii, Jonesia Rukyaa na Hans Mabena.
Tuzo ya Kipa Bora wanaowania ni Aron Kalambo (Prisons), Aishi Manula (Simba) na Razack Abalora (Azam), huku Kocha Bora wateule ni Abdallah Mohamed (Prisons), Zuberi Katwila (Mtibwa) na Pierre Lechantre (Simba).
Goli Bora ni Seif Karihe (Lipuli) na Shaaban Idd Chilunda (Azam) ambaye ameingiza mabao mawili.
Tuzo nyingine ambazo zitatolewa Juni 23 ni Mchezaji wa Heshima ambayo licha ya kuwa kamati ina majina ya wachezaji mbalimbali inaoona wanastahili tuzo kwa mwaka husika, lakini haitangazi majina hayo, isipokuwa hutaja jina la aliyepewa tuzo siku ya sherehe. 
Pia kutakuwa na kikosi bora (VPL Best Eleven), ambacho kitatangazwa siku ya sherehe.

WANAFUNZI WATEMBELEA BUNGE KUJIFUNZA SHUGHULI ZA BUNGE

$
0
0

 Wanafunzi kutoka Shule ya Msingi Mount Kibo ya Jijini Dar es salaam wakiongozwa na Walimu wao wakiwa katika Majukwaa ya Wageni Bungeni kufuatilia Shughuli za Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania namna linavyoendeshwa.
 Wanafunzi kutoka Shule ya Msingi Angelico Lipani ya Jijini Arusha wakiongozwa na Walimu wao wakiwa katika Majukwaa ya Wageni Bungeni kufuatilia Shughuli za Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania namna linavyoendeshwa.
Wanafunzi kutoka Shule ya Msingi Martin Luther ya Jijini Dodoma wakiongozwa na Walimu wao wakiwa katika Majukwaa ya Wageni Bungeni kufuatilia Shughuli za Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania namna linavyoendeshwa. PICHA NA BUNGE

SPIKA NDUGAI AONGOZA KIKAO CHA KAMATI YA UONGOZI CHA KUPOKEA TAARIFA YA MAJUMUISHO KATI YA KAMATI YA BAJETI NA SERIKALI.

$
0
0
Spika wa Bunge, Mheshimiwa Job Ndugai (katikati) akizungumza na Mawaziri, Wenyekiti wa kamati za kudumu za Bunge na Watendaji wakuu kutoka Serikalini (hawapo pichani) wakati wa kikao cha Kamati ya uongozi kilicholenga kupokea Taarifa ya majumuisho yaliyofanyika kati ya kamati ya Bajeti na Serikali, kilichofanyika leo tarehe 13 Juni, 2018 katika Ukumbi wa Pius Msekwa Bungeni Jijini Dodoma.
Spika wa Bunge, Mheshimiwa Job Ndugai (katikati) akiongoza kikao cha Kamati ya uongozi kilicholenga kupokea Taarifa ya majumuisho yaliyofanyika kati ya kamati ya Bajeti na Serikali, kilichofanyika leo tarehe 13 Juni, 2018 katika Ukumbi wa Pius Msekwa Bungeni Jijini Dodoma. kushoto ni Naibu Spika wa Bunge, Mhe. Dkt. Tulia Ackson na kulia ni Mwenyekiti wa kamati ya Kudumu ya Bunge ya Bajeti na Mbunge wa Mtwara Vijijini, Mhe. Hawa Ghasia
Mwenyekiti wa kamati ya Kudumu ya Bunge ya Bajeti na Mbunge wa Mtwara Vijijini, Mhe. Hawa Ghasia (wa pili kulia) akizungumza na Mawaziri, Wenyeviti wa kamati za kudumu za Bunge na Watendaji wakuu kutoka Serikalini (hawapo pichani) wakati wa kikao cha Kamati ya uongozi kilicholenga kupokea Taarifa ya majumuisho yaliyofanyika kati ya kamati ya Bajeti na Serikali, kilichofanyika leo tarehe 13 Juni, 2018 katika Ukumbi wa Pius Msekwa Bungeni Jijini Dodoma. Katikati ni Spika wa Bunge, Mhe. Job Ndugai, Naibu Spika wa Bunge, Mhe. Dkt. Tulia Ackson (wa pili kushoto), Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Phillip Mpango (kushoto) na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, kazi, Vijana, Ajira na Wenye U​lemavu.

KAMISHNA MKUU WA TRA AWASHUKURU WAFANYABIASHARA JIJINI DODOMA

$
0
0
 Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Bw. Charles Kichere akitoa hotuba fupi kwa Wafanyabiashara wa Jijini Dodoma wakati wa hafla fupi ya Iftar aliyowaandalia wafanyabiashara hao ikiwa ni sehemu ya kuwathamini walipakodi  nchini.
 Kamishna wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Bw. Charles Kichere (aliyevaa miwani) akiwekewa futari wakati wa hafla fupi ya Iftar aliyowaandalia wafanyabiashara wa Jijini Dodoma ikiwa ni sehemu ya kuwathamini walipakodi  nchini.
 Baadhi ya Wafanyabiashara wa Jijini Dodoma wakichukua futari wakati wa hafla fupi ya Iftar iliyoandaliwa na Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Bw. Charles Kichere kwa wafanyabiashara hao ikiwa ni sehemu ya kuwathamini walipakodi nchini.
*******************************************************
Na Veronica Kazimoto, Dodoma
Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Charles Kichere amewashukuru wafanyabiashara jijini Dodoma kwa mchango wao wa kulipa kodi na kuiwezesha Serikali kutekeleza wajibu wake wa kukuza uchumi na kutoa huduma mbalimbali za jamii hapa nchini.
Akizungumza wakati akifuturisha wafanyabiashara na wafanyakazi wa TRA katika ukumbi wa LAPF jijini hapa, Kichere alisifia uhusiano mzuri uliopo kati ya wafanyabiashara hao na ofisi ya TRA Mkoa wa Dodoma.
"Nachukua nafasi hii kuwashukuru wafanyabiashara wa Dodoma kwa kuwa walipakodi wazuri na kuonyesha ushirikiano wa hali ya juu na ofisi yetu ya TRA hapa mkoani Dodoma ambapo kutokana na uhusiano huu uliopo, tunapata urahisi wa kutekeleza jukumu letu la kukusanya mapato ya Serikali kwa manufaa ya watanzania wote," alisema Kichere.
Kichere amewaahidi wafanyabiashara hao kuwa, TRA itaendelea kudumisha ushirikiano huo na kukaribisha mazungumzo ya pamoja na viongozi wa TRA mkoani hapa ili kufikia muafaka wa masuala mbalimbali yanayohusu kodi badala ya kulalamika mitaani bila kupata suluhisho.
Aidha, Kamishna Mkuu Kichere amewahimiza wafanyabiashara hao kuendelea kulipa kodi mbalimbali kwa wakati kwani kodi hizo hutumika katika kujenga uchumi wa nchi na kutoa huduma mbalimbali za jamii ikiwa ni pamoja na huduma za afya, maji safi na salama, elimu, kulipa mishahara ya watumishi wa Umma, miundombinu ya barabara na umeme.
"Nachukua fursa hii kutoa rai kwenu wafanyabiashara kuendelea kulipa kodi zote kwa wakati ikiwa ni pamoja na Kodi ya Majengo na  Kodi ya Mapato awamu ya pili ambapo mwisho wa kulipa kodi hizi ni tarehe 30 Juni, mwaka huu. Kodi nyingine ni Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT) ambayo hulipwa tarehe 20 ya kila mwezi.  Hivyo, uhiari wenu wa kulipa kodi hizi kwa wakati ndio chachu ya kujenga uchumi wetu na kuharakisha kutoa huduma za jamii kwa watanzania wote", alisema Kichere.
Naye Katibu Mtendaji wa Chemba ya Biashara, Viwanda na Kilimo (TCCIA) mkoani Dodoma ambaye pia ni Katibu wa Sekta Binafsi mkoani hapa Idd Senge amesema kwamba, sekta binafsi itaendelea kushirikiana na TRA kwa ajili ya kuhakikisha kuwa wafanyabiashara wanalipa kodi kwa wakati ili kuepuka faini ambazo zinarudisha nyuma maendeleo ya biashara zao.
"Sisi kama wafanyabiashara wa hapa mkoani Dodoma tutaendelea kushirikiana na Mamlaka ya Mapato Tanzania na pale patakapotokea sintofahamu yoyote tutafanya mawasiliano na viongozi wa TRA ili kupata muafaka wa pamoja," alieleza Senge.
Mamlaka ya Mapato Tanzania imejiwekea utaratibu wa kufuturisha wafanyabiashara na wafanyakazi wake kila ifikapo Mwezi Mtukufu wa Ramadhani kwa lengo la kumshukuru Mwenyezi Mungu katika shughuli mbalimbali wanazozifanya hususani za ukusanyaji mapato ya Serikali.
 Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Bw. Charles Kichere (aliyevaa kofia kulia) akiwa na baadhi ya wafanyabiashara na watumishi wa TRA wakifuturu wakati wa hafla fupi ya Iftar iliyoandaliwa na Kamishna Mkuu huyo ikiwa ni sehemu ya kuwathamini walipakodi  nchini.
 Baadhi ya watumishi wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), wakiwa katika hafla fupi ya Iftar jijini Dododma aliyoiandaa Kamishna Mkuu wa Mamlaka hiyo Bw. Charles Kichere ikiwa ni sehemu ya kuwathamini walipakodi  nchini.
 Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Bw. Charles Kichere (wa nne kulia) akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya wafanyabiashara na watoto yatima wa Kituo cha kulelea watoto yatima cha  Rahman kilichopo jijini Dodoma wakati wa hafla fupi ya Iftar aliyowaandalia wafanyabiashara na watumishi wa TRA ikiwa ni sehemu ya kuwathamini walipakodi  nchini. Hafla hiyo ilifanyika katika Ukumbi la LAPF jijini Dodoma.
Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Bw. Charles Kichere (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya wafanyabiashara na watumishi wa TRA mara baada ya hafla ya Iftar aliyowaandalia wafanyabiashara hao ikiwa ni sehemu ya kuwathamini walipakodi  nchini. Hafla hiyo ilifanyika katika Ukumbi la LAPF jijini Dodoma. PICHA ZOTE NA TRA

KUPATA SIMU BORA NA WARRANT YA MIAKA 2 BOFYA LINKI HII: https://www.jumia.co.tz/mobile-phones/

KUPATA SIMU OG AINA YA INFINIX HADI NOTE 5: BOFYA LINK HII CHINI IKIWA NA WARRANT YA MIAKA 2

DKT. MPANGO AWASILISHA BAJETI KUU YA MAPATO NA MATUMIZI YA SERIKALI 2018/19

$
0
0
 Waziri wa Fedha na MipangoMhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb) akiwasilisha Taarifa ya Hali ya Uchumi wa Taifa katika mwaka 2017 na Mpango wa Maendeleo wa Taifa  wa mwaka 2018/19 Bungeni Jijini Dodoma ambapo kwa mwaka 2017 uchumi wa Tanzania ulikua kwa asilimia 7.1. 
Baadhi ya viongozi na Maafisa Waandamizi wa Wizara ya Fedha na Mipango wakifuatilia kwa makini Taarifa ya Hali ya Uchumi wa Taifa katika mwaka 2017 na Mpango wa Maendeleo wa Taifa  wa mwaka 2018/19 iliyokuwa ikiwasilishwa na Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb) (hayupo pichani), Jijini Dodoma. 
Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (kushoto) na Naibu wake Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji (Mb), wakifurahia jambo Bungeni Dodoma baada ya  kuwasilishwa kwa Taarifa ya Hali ya Uchumi wa Taifa katika mwaka 2017 na Mpango wa Maendeleo wa Taifa  wa mwaka 2018/19 ambapo vipaumbele  vya sasa ni pamoja na mazingira wezeshi ya ufanyaji wa biashara, viwanda vya kukuza uchumi na kufungamanisha ukuaji wa uchumi na Maendeleo ya watu. 
Kamishna wa Bajeti wa Wizara ya Fedha na Mipango Bi. Mary Maganga (kulia), Mkurugenzi Mtendaji wa Bodi ya Taifa ya Wahasibu na Wakaguzi wa Hesabu (NBAA) Bw. Pius Maneno (wa pili kulia) na Mkaguzi Mkuu wa Ndani Bw. Mohamed Mtonga, wakiwa katika viwanja vya Bunge Jijini Dodoma baada ya Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango, kuwasilisha Taarifa ya Hali ya Uchumi wa Taifa katika mwaka 2017 na Mpango wa Maendeleo wa Taifa  wa mwaka 2018/19. 
 Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango, Bi. Susana Mkapa, (kushoto) na Kamishna Msaidizi wa Sera wa Wizara ya Fedha na Mipango Bw. William  Mhoja wakipeana mikono  katika viwanja vya Bunge Jijini Dodoma baada ya Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango(Mb), kuwasilisha Taarifa ya Hali ya Uchumi wa Taifa katika mwaka 2017 na Mpango wa Maendeleo wa Taifa  wa mwaka 2018/19 ambapo Tanzania kwa mwaka 2017 mfumuko wa bei ulikua kwa wastani wa asilimia 5.1.
 Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT) Prof. Florens Luoga, akizungumza jambo na Balozi wa Uingereza nchini Tanzania Bi. Sarah Cooke  baada ya Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango kuwasilisha Taarifa ya Hali ya Uchumi wa Taifa katika mwaka 2017 na Mpango wa Maendeleo wa Taifa wa mwaka 2018/19. ambapo moja ya vipaumbele vya sasa ni Kuimarisha utekelezaji wa Mpango wa Maendeleo.
Baadhi ya Maafisa Waandamizi wa Wizara ya Fedha na Mipango  wakibadilishana mawazo katika viwanja vya Bunge  Jijini Dodoma baada ya  Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango,  kuwasilisha Taarifa ya Hali ya Uchumi wa Taifa katika mwaka 2017 na Mpango wa Maendeleo wa Taifa  wa mwaka 2018/19 ambapo Serikali imetenga takribani Sh. trilioni 12 kwa ajili ya kutekeleza miradi ya Maendeleo. Picha na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini Wizara ya Fedha na Mipango
***************************************

HOTUBA YA WAZIRI WA FEDHA NA MIPANGO,
  MHESHIMIWA DKT.  PHILIP I. MPANGO (MB),
AKIWASILISHA BUNGENI MAPENDEKEZO
 YA SERIKALI KUHUSU MAKADIRIO
YA MAPATO NA MATUMIZI KWA
 MWAKA 2018/19 

I.      UTANGULIZI
1.         Mheshimiwa Spika, naomba kutoa hoja kwamba Bunge lako Tukufu lipokee, lijadili na kupitisha Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa mwaka 2018/19. Bajeti hii inawasilishwa kwa kuzingatia matakwa ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977, Ibara ya 137 ikisomwa pamoja na Sheria ya Bajeti namba 11 ya mwaka 2015 kifungu cha 26. 
2.         Mheshimiwa Spika, pamoja na hotuba hii, ninawasilisha vitabu vinne vya bajeti. Kitabu cha Kwanza ni Makadirio ya Mapato; Kitabu cha Pili ni Makadirio ya Matumizi ya Kawaida kwa Wizara, Idara zinazojitegemea, Taasisi na Wakala za Serikali; Kitabu cha Tatu ni Makadirio ya Matumizi ya Kawaida kwa Sekretarieti za Mikoa na Mamlaka za Serikali za Mitaa; na Kitabu cha Nne ni Makadirio ya Matumizi ya Maendeleo kwa Wizara, Idara Zinazojitegemea, Wakala za Serikali, Sekretarieti za Mikoa na Mamlaka za Serikali za Mitaa. Aidha, upo Muswada wa Sheria ya Fedha wa mwaka 2018 pamoja na Muswada wa Sheria ya Matumizi ya Serikali wa mwaka 2018 ambayo ni sehemu ya bajeti hii. KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

3.         Mheshimiwa Spika, ni heshima kubwa na upendeleo wa hali ya juu kusimama mbele ya Bunge lako Tukufu kuwasilisha bajeti ya tatu ya Serikali ya awamu ya tano. Hivyo, namshukuru kwanza Mwenyezi Mungu kwa kuendelea kuijalia nchi yetu neema nyingi, utulivu na amani na kwa kuniwezesha kuwasilisha bajeti kuu ya Serikali kwa wananchi wa Tanzania kwa mara ya tatu. Pili napenda kumpongeza kwa dhati Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. John Pombe Joseph Magufuli, kiongozi wetu shupavu; kiongozi anayeaminiwa na kutumainiwa na wananchi, hasa wanyonge; kiongozi anayechukia na kupiga vita rushwa, ufisadi na ubadhirifu wa mali za umma kwa vitendo; na Rais anayejipambanua kwa kufanya maamuzi magumu ya kulinda rasilimali za Taifa. Ninampongeza kwa kazi kubwa ambazo ameendelea kuzifanya tangu aliposhika hatamu za uongozi wa Taifa letu, ambazo zimepelekea kupatikana kwa mafanikio makubwa sana katika kipindi kifupi cha miaka miwili na nusu tu ya utawala wake. Napenda niyataje mambo kumi tu aliyothubutu kutenda na kuiletea nchi mafanikio makubwa: 
(i)         Kuhamishia makao makuu ya Serikali Dodoma: Ametekeleza ndoto ya Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere na uamuzi wa Chama Tawala wa mwaka 1972 wa kuhamishia makao makuu ya Serikali Dodoma. Aidha, kwa mamlaka aliyo nayo amepandisha hadhi ya iliyokuwa Manispaa ya Dodoma kuwa Jiji kuanzia tarehe 26/4/2018;
(ii)       Kujenga ukuta kuzunguka mgodi wa Tanzanite Mirerani: Amejenga ukuta wenye mzingo wa kilomita 24.5 kuzunguka machimbo ya madini ya Tanzanite Mirerani, Wilaya ya Simanjiro uliogharimu shilingi bilioni 5.42. Lengo likiwa ni kudhibiti uchimbaji na uuzaji holela wa madini hayo yanayopatikana Tanzania pekee na kuliingizia Taifa mapato. Katika kipindi cha miezi mitatu kuanzia Januari hadi Machi, 2018 Serikali imefanikiwa kukusanya mrabaha wa shilingi milioni 714.6. Kati ya kiasi hicho, shilingi milioni 614.6 kilitokana na makusanyo kutoka kwa wachimbaji wadogo. Kiasi hicho kilichokusanywa kutoka kwa wachimbaji wadogo kinazidi jumla ya makusanyo ya mrabaha wa miaka mitatu iliyopita. Kiasi kilichokusanywa na Serikali kilikuwa shilingi milioni 116.8 (2015), shilingi milioni 71.8 (2016), na shilingi milioni 147.1  (2017);
(iii)     Kudhibiti uuzaji wa makinikia nje ya nchi na kutunga sheria kuwezesha nchi kunufaika na rasilimali zake:Amezuia usafirishaji wa makontena 277 ya makinikia nje ya nchi yenye thamani ya kati ya shilingi bilioni 829.4 na shilingi bilioni 1,438.8 na kuagiza kutungwa kwa sheria mpya za mfano katika Afrika kuwezesha nchi zenye maliasili kunufaika na rasilimali hizo. Sheria hizo ambazo zilipitishwa na Bunge lako Tukufu ni:
(a)       Sheria ya Mamlaka ya nchi kuhusu Umiliki wa Maliasili ya mwaka 2017 (The Natural Wealth and Resources - Permanent Sovereignity Act, 2017);
(b)       Sheria ya Mapitio na Majadiliano kuhusu Masharti Hasi katika Mikataba ya Maliasili za Nchi ya Mwaka 2017 (The Natural Wealth and Resources Contracts(Review and Re- Negotiation of Unconscionable Terms) Act, 2017; na
(c)       Sheria ya Marekebisho ya Sheria mbalimbali ya mwaka 2017 (The Written Laws - Miscellaneous Ammendments ) Act, 2017.
(iv)     Kutoa elimu msingi bila ada na kuongeza bajeti ya dawa, vifaa tiba na vitendanishi kwa zaidi ya mara nane: Ametoa elimu msingi bila ada ambapo kila mwezi Serikali inalipa shilingi bilioni 20.8. Kutokana na hatua hiyo, uandikishwaji wanafunzi wa darasa la kwanza umeongezeka kutoka watoto 1,568,378 mwaka 2015 hadi watoto 2,078,379 mwaka 2018. Aidha,  uandikishaji wa wanafunzi wa kidato cha kwanza nao umeongezeka kutoka wanafunzi 448,826 mwaka 2015 hadi wanafunzi 562,695 mwaka 2017. Kadhalika, ameongeza fedha za mikopo ya wanafunzi wa elimu ya juu ambapo mgao uliotolewa mwaka 2017/18 ni shilingi bilioni 409.9 ikilinganishwa na matumizi halisi ya shilingi bilioni 367.4 mwaka 2015/16. Idadi ya wanafunzi wanaopata mikopo hiyo imeongeza kutoka wanafunzi 96,589 mwaka 2015 hadi 122,623 mwaka 2017. Katika sekta ya afya, amethubutu kuongeza bajeti kwa ajili ya kugharamia ununuzi wa dawa, chanjo, vifaa, vifaa tiba na vitendanishi kufikia shilingi bilioni  269 mwaka 2017/18  kutoka shilingi bilioni 31 mwaka 2015/16, hivyo kuimarisha huduma za afya;
(v)       Ununuzi wa ndege mpya kufufua Shirika la Ndege Tanzania (ATCL): Amefufua Shirika la Ndege la Tanzania kwa kufanya maamuzi magumu ya kununua ndege mpya tatu aina ya Bombardier Q400 zenye uwezo wa kubeba abiria 76 kila moja ambazo tayari ziko nchini na zinafanya safari za ndani. Aidha, ndege kubwa nyingine tatu (3), moja aina ya Boeing 787-8 Dreamliner yenye uwezo wa kubeba abiria 262 na ndege mbili  aina ya Bombardier CS 300 zenye uwezo wa kubeba abiria 132 kila moja zitawasili nchini baadae mwaka huu. Kadhalika, Serikali imekamilisha taratibu za kupata ndege ya pili kubwa aina ya Boeing 787-8 Dreamliner yenye uwezo wa kubeba abiria 262 na malipo ya awali yamekamilika;
(vi)     Kudhibiti matumizi yasiyo ya lazima, kuondoa watumishi hewa na wenye vyeti vya kughushi: Amedhibiti matumizi yasiyo ya lazima hususan safari za watumishi wa Serikali nje ya nchi, kuondoa watumishi hewa 19,708 waliokuwa wanalipwa mshahara wa jumla ya shilingi bilioni 19.8 kwa mwezi, na watumishi 14,404 wenye vyeti vya kughushi waliokuwa wanalipwa mshahara wa jumla ya shilingi bilioni 15.5 kwa mwezi, ambazo zote hizo zimeokolewa. Aidha, chini ya utawala wake, nidhamu katika utumishi wa umma imeimarika na ameanzisha Mahakama ya mafisadi ili kupambana na mafisadi wanaonyonya uchumi wa nchi;
(vii)   Ujenzi wa reli ya kati ya kisasa kwa kiwango cha kimataifa (Standard Gauge Railway – SGR): Ameanza ujenzi wa reli ya kati ya kisasa kwa kiwango cha kimataifa (Standard Gauge Railway – SGR). Awamu ya kwanza kutoka Dar es Salaam hadi Morogoro (km 205) na awamu ya pili kutoka Morogoro hadi Makutupora Dodoma (km 422) tayari zinatekelezwa. Awamu zote mbili zitagharimu takriban Dola za Marekani bilioni 3.14;
(viii)  Ujenzi wa mradi wa umeme katika bonde la mto Rufiji: Amefanya uamuzi wa kuanza ujenzi wa mradi mkubwa wa umeme katika mto Rufiji (Stiegler’s Gorge) ambao nao ulikuwa ndoto ya Baba wa Taifa utakaozalisha MW 2,100 utakapokamilika nao umeanza katika hatua za awali;
(ix)     Kuimarisha usimamizi wa mapato ya ndani: Ametekeleza ahadi yake kwa Watanzania kuimarisha ukusanyaji wa mapato na kudhibiti ukwepaji kodi, hatua ambazo zimewezesha Serikali kuongeza ukusanyaji wa mapato kutoka wastani wa shilingi bilioni 850 kwa mwezi hadi wastani wa shilingi tirioni 1.3 kwa mwezi;
(x)       Kuendeleza umeme vijijini na kusitisha miradi ya wazalishaji binafsi wa umeme (IPPs): Ameendeleza utekelezaji wa mradi kabambe wa kupeleka umeme vijijini kupitia REA Awamu ya Tatu kwa ufanisi mkubwa, ambapo ndani ya miaka miwili na nusu ya utawala wake jumla ya vijiji 557 vimeunganishwa umeme. Vijiji hivyo vimetokana na utekelezaji wa miradi ya REA II na REA III ya kuongeza msongamano (densification), mkongo (backbone) na ule wa kusafirisha umeme Makambako - Songea. Aidha, amesitisha miradi ya wazalishaji binafsi wa umeme (Independent Power Producers – IPPs) ambayo ilikuwa inaigharimu Serikali fedha nyingi. Vile vile, bila yeye mradi wa Bomba la Mafuta kutoka Hoima (Uganda) hadi bandari ya Tanga usingepatikana na tayari ujenzi unaendelea;

4.         Mheshimiwa Spika, yapo mambo mengi sana makubwa (barabara, meli, madaraja, maji, usimamizi wa sekta ya fedha n.k.) ambayo Jemadari huyu ametekeleza, lakini kwa uchache wa muda siwezi kuyataja yote. Haya yote ni ushahidi usio na mashaka kwamba Tanzania chini ya Rais Magufuli imeshika kasi ya maendeleo. Hivyo ni wajibu wa kila Mtanzania kuchangia katika jitihada hizi za Mheshimiwa Rais kujenga Tanzania mpya. Maeneo matatu ya msingi sana kwa kila mwananchi kuwajibika ni: (i) uzalendo kwa nchi yetu; (ii) kupiga vita wizi, ubadhirifu na ufisadi; na (iii) kufanya kazi kwa bidii na kulipa kodi.

5.         Mheshimiwa Spika, pamoja na pongezi hizo za dhati kwa Rais wetu, napenda kumshukuru kwa moyo wangu wote kwa kuendelea kuniamini na kuniongoza katika kazi zangu za Waziri wa Fedha na Mipango. Hata pale nilipoelemewa na kazi na kulaumiwa kwamba waziri huyu ni bahili mno katika kutoa fedha na baadhi wakinipaka tope la kiburi, alinitia moyo. Niliwahi kumuuliza Mheshimiwa Rais kwa nini alinitwika mimi kazi hii nzito kama msalaba wa zege, tena bila matumaini ya kutokea mtu mfano wa Simon wa Kirene katika Biblia wa kuja kunipokea mzigo huu!. Yeye alinijibu kwamba “Mungu atawatuma malaika wake watakusaidia!” na akaongeza kwamba “lazima watu wachache tuwe tayari kuumia kwa faida ya Watanzania wengi maskini”. Naomba nikiri kuwa, majibu hayo yalinichoma na kunikumbusha sala ya wana “Opus Dei” katika mateso isemayo “Mapenzi ya Mungu, yenye haki na yanayopendeza sana, yafanyike, yatimizwe, yasifiwe na kutukuzwa kuliko vitu vyote milele. Amina. Amina.” Baada ya hapo, nilipata amani ya kuendelea katika utumishi huu. Asante sana Mheshimiwa Rais. Najua unasikiliza!.

6.         Mheshimiwa Spika, napenda pia kumpongeza Mheshimiwa Mama Samia Suluhu Hassan Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, kwa kumsaidia Rais kuongoza Taifa letu kwa hekima na uadilifu. Kadhalika, ninatoa pongezi kwa Mheshimiwa Dkt. Ali Mohamed Shein, Rais wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi kwa kuiongoza Zanzibar kwa busara, jambo ambalo limepelekea wananchi wa Zanzibar kuishi katika hali ya amani na utulivu mkubwa kwa kipindi cha miaka saba na nusu sasa. Aidha, ninampongeza sana Mheshimiwa Kassim M. Majaliwa, Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Ruangwa, kwa kuwa kapteni hodari wa timu ya Serikali hapa Bungeni na kwa kumsaidia Rais kufuatilia utekelezaji wa Ilani ya Chama Tawala CCM ya mwaka 2015 – 2020. Vile vile, ninawapongeza wakuu wa mihimili mingine ya dola, nikianza na wewe Mheshimiwa Job Yustino Ndugai, Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mbunge wa Kongwa kwa kuliongoza Bunge kwa umahiri; na MheshimiwaProfesa Ibrahim Hamis Juma,  Jaji Mkuu wa Tanzania kwa kazi nzuri ya kuongoza chombo cha utoaji haki. Napenda vile vile kumpongeza Mheshimiwa Balozi Mhandisi John Kijazi, Katibu Mkuu Kiongozi ambaye pia ni mkuu wa Utumishi wa Umma na Katibu wa Baraza la Mawaziri kwa utumishi uliotukuka.

7.         Mheshimiwa Spika, ni vema pia niwapongeze waheshimiwa wenza wa viongozi wakuu wa kitaifa kwa umuhimu wao wa kipekee. Niruhusu niwataje kwa majina yao Mwalimu Janet Magufuli, Bwana Ameir Hafidh Ameir, Mama Mwanamwema Shein, Mwalimu Mary Majaliwa, Dkt. Fatuma Ramadhani Mganga, na Mama Marina Papadopoulos Juma. Tunawapongeza na kuwashukuru kwa kuwawezesha viongozi wetu wakuu wa kitaifa kutekeleza vizuri majukumu yao kwa utulivu, hamasa na tabasamu kutokana na mapenzi makubwa wanayopata nyumbani.

8.         Mheshimiwa Spika,napenda niwapongeze na kuwashukuru wakuu wote wa vyombo vya ulinzi na usalama ambao ni Mkuu wa Majeshi, Jenerali Venance Mabeyo; Inspekta Jenerali wa Polisi, Simon Sirro; Kamishna Jenerali wa Magereza, Dkt. Juma Ali Malewa; Kamishna Jenerali wa Uhamiaji Dkt. Anna Makakala; Mkurugenzi wa Usalama wa Taifa, Dkt. Modestus Kipilimba; Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa, Kamishna wa Polisi, Valentino Mlowola; Kamishna Jenerali wa Mamlaka ya Kuzuia na Kupambana na Madawa ya Kulevya Bw. Rogers William Sianga; na Kamishna Jenerali wa Zimamoto na Uokoaji Bw. Thobias Andengenye. Mimi na Watanzania wenzangu tunawapongeza kwa dhati kabisa viongozi hawa, pamoja na makamanda, askari na watumishi wote wa vyombo hivi nyeti kwa kuendelea kuilinda nchi yetu kwa ushupavu, kudumisha amani na usalama na kuwawezesha wananchi wote wa Tanzania kufanya shughuli za maendeleo kwa utulivu. Aidha, ninampongeza Mheshimiwa Dkt Adelardus Lubango Kilangi kwa kuteuliwa na Rais kuwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali, na ninamshukuru kwa kutayarisha kwa wakati Muswada wa Sheria ya Fedha wa mwaka 2018 na Muswada wa Sheria ya Matumizi wa mwaka 2018.

9.         Mheshimiwa Spika, naomba kutumia fursa hii pia kutoa shukrani mahsusi kwa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Bajeti inayoongozwa na Mheshimwa Hawa Abdulrahman Ghasia, Mbunge wa Mtwara Vijijini na Makamu wake Mheshimiwa Jitu V. Soni, Mbunge wa Babati Vijijini. Maoni na ushauri uliotolewa na Kamati ya Bajeti wakati wa kuchambua mapendekezo ya bajeti ninayoiwasilisha mbele ya Bunge lako Tukufu, ulikuwa wa kizalendo na wenye tija. Aidha, ninawapongeza Wenyeviti, Makamu wenyeviti na wajumbe wa Kamati zote za Kudumu za Bunge kwa michango yao waliyoitoa kupitia vikao vya kamati za kisekta katika kuboresha Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa mwaka 2018/19 ili kuwapatia wananchi wa Tanzania huduma bora zaidi.

10.    Mheshimiwa Spika, kama ilivyokuwa mwaka 2017/18, dhima ya bajeti ya mwaka 2018/19 kwa nchi zote wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki itakuwa ni “kujenga uchumi wa viwanda utakao chochea ajira na ustawi endelevu wa jamii”. Bajeti hii imeandaliwa kwa kuzingatia uhalisia wa nchi yetu ambao sisi wote tunaufahamu, kwa maana ya changamoto kuu za kiuchumi na kijamii zinazotukabili, fursa tulizo nazo, mafanikio hadi sasa na malengo yetu kama Taifa. Naomba nifafanue haya kwa kifupi:


a) Changamoto
(i)         Bado tuna kiwango kikubwa cha umaskini ambapo taarifa kutoka Ofisi ya Taifa ya Takwimu zinaonesha kiwango cha umaskini kimepungua kidogo kutoka asilimia 28.2 (2011/12) hadi asilimia 26.4 (2015/16). Matarajio ni kuwa Utafiti wa Matumizi ya Kaya unaoendelea hivi sasa utatupatia taarifa nzuri zaidi ya kuendelea kupungua kwa umaskini kwa kuzingatia kuwa uchumi wa Taifa umeendelea kukua kwa kasi ya wastani wa asilimia 7.0 kwa mwaka katika miongo miwili sasa;
(ii)       Ukosefu wa fursa za ajira hasa kwa vijana, ambapo takwimu zinaonesha kuwa asilimia 10.4 ya Watanzania hawana ajira. Vile vile kati ya vijana wanaohitimu masomo yao wapatao 800,000 kila mwaka, uwezo wa Serikali kuajiri ni wastani wa watu 40,000 tu;
(iii)     Sekta ya kilimo (inayojumuisha mazao, mifugo na uvuvi) ambayo inaajiri asilimia 66 ya Watanzania na inachangia asilimia 30 ya Pato la Taifa inaendelea kukua kwa kasi ndogo ya wastani wa asilimia 3.7 kwa mwaka kwa kipindi cha miaka kumi iliyopita kutokana na uwekezaji mdogo, tija ndogo na kutegemea mvua, sambamba na mchango mdogo wa sekta ya viwanda katika Pato la Taifa wa asilimia 5.5;
(iv)     Mahitaji makubwa ya upatikanaji wa huduma muhimu za jamii (hasa maji, afya na elimu bora) na yanaongezeka kutokana na kuongezeka kwa idadi ya watu (asilimia 3.1 kwa mwaka). Aidha, hali ya miundombinu ya umeme, usafiri na usafirishaji (barabara, reli, usafiri wa anga na majini) bado haikidhi mahitaji ya uchumi kukua kwa kasi zaidi na kugusa wananchi wengi. Mathalani, mtandao wa barabara nchini ni kilomita 86,472 ambapo ni asilimia 9.7 tu ndiyo za kiwango cha lami. Aidha, mahitaji ya umeme kwa ajili ya matumizi ya nyumbani na viwandani bado ni makubwa ikilinganishwa na uwezo wa uzalishaji. Mitambo iliyopo kwa sasa ina uwezo wa kuzalisha Megawati 1,424.6 ikilinganishwa na mahitaji ya zaidi ya Megawati 3,000 ili kuweza kuhimili mahitaji ya uchumi wa viwanda; na
(v)       Wigo mdogo wa ukusanyaji wa mapato ya ndani ambapo uwiano wa mapato ya ndani na Pato la Taifa ni takriban asilimia 15.0 ikilinganishwa na wastani wa asilimia 17.0 kwa nchi za Afrika Kusini mwa Jangwa la Sahara.
b)Fursa
11.    Mheshimiwa Spika, maandalizi ya bajeti hii pia yamezingatia fursa mbalimbali tulizo nazo katika Taifa letu hususan nguvukazi kubwa ya Taifa ambao ni vijana; rasilimali na fursa nyingi tulizonazo katika kilimo (mazao, mifugo, na uvuvi); madini; gesi; vivutio vya utalii; viwanda vya huduma za kilimo (agri-business); vyanzo mbalimbali vya uzalishaji wa umeme; biashara na huduma za usafirishaji wa mizigo kwenda nchi jirani.

c)Mafanikio
12.    Mheshimiwa Spika, bajeti hii pia imezingatia mafanikio tuliyopata hadi hivi sasa ambayo hatuna budi tuyaimarishe na nitayaeleza kwa muhtasari katika sehemu ya mapitio ya utekelezaji wa bajeti.
d)Malengo
13.    Mheshimiwa Spika, bajeti hii vile vile imeandaliwa kwa kuzingatia malengo ya Dira ya Taifa ya Maendeleo 2025; Mpango wa Pili wa Maendeleo wa Taifa wa Miaka Mitano (2016/17 – 2020/21) na Ilani ya CCM ya mwaka 2015 – 2020. Malengo makuu ni kuondokana na umaskini na kuibadilisha Tanzania kuwa nchi ya uchumi wa viwanda na kuingia kwenye kundi la nchi zenye kipato cha kati (Middle Income Countries) ifikapo mwaka 2025.

14.    Mheshimiwa Spika, changamoto, fursa mafanikio na malengo niliyoyaeleza sasa hivi lazima yaende pamoja na wajibu upande wa Serikali, sekta binafsi, wadau wengine na mwananchi mmoja mmoja, wa kuzipatia majibu changamoto hizo na kuchangia ipasavyo katika jitihada za kulipeleka Taifa letu mbele. Tutafanya hivyo ikiwa kila mwananchi atafanya kazi na kutumia uwezo wake wote kwa ajili ya maendeleo yake na ya Taifa. Aidha, ni muhimu pia tuendelee kujenga na kutumia ubia wa kimkakati (harness strategic partnerships). Ujumbe wangu kwa Watanzania kupitia bajeti hii ni kuwa, lazima tuendelee kufanya chaguo gumu (tough choices) katika kuelekeza rasilimali kidogo tunazokusanya ili tuweze kuzishinda changamoto hizo zilizoko mbele yetu. Ukweli ni kuwa, mabadiliko ni magumu na mara nyingi yanapingwa!. Hivyo, lazima tuwe imara, tukusudie kufanikiwa na tutumie vizuri fursa na uwezo wa Watanzania, sekta binafsi na Serikali ili kufikia azma yetu.

15.    Mheshimiwa Spika, katika hotuba niliyosoma leo asubuhi, nilieleza kwa kirefu hali ya uchumi wetu ilivyokuwa katika mwaka 2017, utekelezaji wa Mpango wa Maendeleo wa Taifa wa mwaka 2017/18, mafanikio yetu na changamoto tulizokumbana nazo na niliainisha pia maeneo ya vipaumbele kwa mwaka 2018/19. Katika hotuba hii nitajikita zaidi katika masuala ya kibajeti, nikianza na utekelezaji wa bajeti ya mwaka 2017/18, hatua muhimu zitakazopewa msukumo zaidi upande wa matumizi katika mwaka ujao wa fedha, maboresho ya mfumo wa kodi na tozo mbalimbali na mapendekezo ya bajeti ya mwaka 2018/19.


II.      TATHMINI YA UTEKELEZAJI WA BAJETI YA MWAKA 2017/18
Mwenendo wa Mapato
16.    Mheshimiwa Spika, Katika kipindi cha Julai, 2017 hadi Aprili, 2018 mapato kutoka vyanzo vyote yalifikia shilingi trilioni 21.89 sawa na asilimia 69 ya lengo la mwaka la kukusanya shilingi trilioni 31.71 Mchanganuo wa mapato hayo ni kama ifuatavyo:

A.                Mapato ya Ndani
17.    Mheshimiwa Spika, Mapato ya ndani yakijumuisha mapato ya Halmashauri yalifikia shilingi trilioni 14.84 ikilinganishwa na lengo la kukusanya shilingi trilioni 19.98 kwa mwaka sawa na asilimia 74.3. Kati ya kiasi hicho, makusanyo ya kodi yalikuwa shilingi trilioni 12.61; makusanyo yasiyo ya kodi ni shilingi trilioni 1.79; na makusanyo ya Halmashauri ni shilingi bilioni 437.6. Kutofikiwa kwa malengo ya ukusanyaji  kumetokana na changamoto mbalimbali ikiwa ni pamoja na:
(i)         Ukwepaji wa kodi;
(ii)       Ugumu wa kutoza kodi wafanya biashara walioko katika sekta isiyo rasmi kwa vile hawana sehemu rasmi na za kudumu za kufanyia biashara na hawatunzi kumbukumbu;
(iii)     Mazingira yasiyo rafiki ya ulipaji kodi na mlolongo wa kodi na tozo, hasa  huduma zinazotolewa na mamlaka za udhibiti na usimamizi (zikiwemo TBS, TFDA, EWURA, TCRA, OSHA, Zimamoto), viwango vikubwa vya kodi; urasimu katika taratibu za kulipa kodi, na ugumu na gharama kubwa za kulipa kodi;
(iv)     Matumizi hafifu ya mashine za kielektroniki za kutolea risiti (EFD);
(v)       Udhaifu katika usimamizi wa uvunaji wa rasilimali za nchi hasa madini, gesi asilia, misitu, rasilimali bahari, utalii na ardhi; na
(vi)     Mchango mdogo na utegemezi wa mashirika ya umma katika bajeti ya Serikali.

B.                Mikopo ya Ndani na Nje yenye Masharti ya Kibiashara
18.    Mheshimiwa Spika,Serikali ilikopa jumla ya shilingi trilioni 4.96 kutoka soko la ndani sawa na asilimia 80 ya shilingi trilioni 6.17 zilizotarajiwa kukopwa kwa mwaka 2017/18. Kati ya kiasi hicho, shilingi trilioni 4.13 zilikopwa kwa ajili ya kulipia dhamana na hati fungani za Serikali zilizoiva (rollover), na shilingi bilioni 832.3 zilikopwa ili kugharamia miradi mbalimbali ya maendeleo. Aidha, Serikali ilikopa kutoka soko la nje shilingi bilioni 224 sawa na asilimia 14 ya lengo la kukopa shilingi trilioni 1.6. Fedha hizi zimeelekezwa kwenye utekelekelezaji wa miradi mbalimbali ya kimkakati. Aidha, mwezi Mei, 2018, Serikali ilipokea mkopo wa kibiashara kiasi cha shilingi trilioni 1.13.

C.                Misaada na Mikopo Nafuu kutoka kwa Washirika wa Maendeleo
19.    Mheshimiwa Spika, misaada na mikopo nafuu iliyopokelewa kutoka kwa Washirika wa Maendeleo ilikuwa shilingi trilioni 1.87 sawa na asilimia 47 ya makadirio ya mwaka ya shilingi trilioni3.97. Kati ya kiasi hicho, shilingi bilioni 70.2 ni misaada na mikopo nafuu ya kibajeti sawa na asilimia 7.5 ya makadirio ya shilingi bilioni 941.3, shilingi bilioni 182.9 ni misaada na mikopo nafuu ya Mifuko ya Kisekta sawa na asilimia 33 ya makadirio ya shilingi bilioni 556.1, na shilingi trilioni1.61 ni misaada na mikopo nafuu ya Miradi ya Maendeleo sawa na asilimia 65 ya makadirio ya shilingi trilioni 2.47.

Mwenendo wa Matumizi
20.    Mheshimiwa Spika, katika kipindi cha Julai, 2017 hadi Aprili 2018, Serikali imetoa jumla shilingi trilioni 21.68 sawa na asilimia 68.4 ya lengo la mwaka la shilingi trilioni 31.71. Kati ya kiasi hicho, shilingi trilioni 16.56 zilikuwa kwa ajili ya matumizi ya kawaida ambazo zinajumuisha shilingi trilioni 5.63 kwa ajili ya mishahara ya watumishi wa umma na shilingi trilioni 8.42 kwa ajili ya kugharamia Deni la Serikali na mahitaji mengine ya Mfuko Mkuu.

21.    Mheshimiwa Spika, hadi kufikia Aprili, 2018 Serikali imetoa jumla   ya shilingi trilioni 5.12 kwa ajili utekelezaji wa miradi ya maendeleo ambapo shilingi trilioni 4.35 ni fedha za ndani na shilingi bilioni 775.8 ni fedha za nje. Hata hivyo, kiasi hiki hakijumuishi fedha kutoka kwa Washirika wa Maendeleo zilizopelekwa moja kwa moja kwenye utekelezaji wa miradi ambazo hazikupita kwenye mfumo wa malipo wa Serikali. Fedha hizi zitajumuishwa pindi taratibu ya kiuhasibu zitakapokamilika.

22.    Mheshimiwa Spika, naomba nieleze mafanikio yaliyopatikana katika utekelezaji wa bajeti ya mwaka 2017/18 katika kipindi cha Julai 2017 hadi Aprili 2018 kama ifuatavyo:
(i)         Jumla ya shilingi bilioni 59.0 zimetolewa katika Halmashauri za Wilaya 110 kwa ajili ya ujenzi na ukarabati wa vituo vya afya, na shilingi bilioni 24.1 kwa ajili ya ukarabati wa hospitali za mikoa 24. Aidha, jumla ya shilingi bilioni 125.7 zimetolewa kwa ajili ya ununuzi wa dawa, vifaa tiba na vitendanishi;
(ii)       Kiasi cha shilingi bilioni 156.1 kimetolewa kwa ajili ya utekelezaji wa miradi ya maji mijini na vijijini;
(iii)     Kiasi cha shilingi bilioni 409.9 kimetolewa kwa ajili ya miradi ya nishati vijijini, umeme wa jotoardhi, uzalishaji wa umeme katika vyanzo mbalimbali na usambazaji wa gesi asilia;
(iv)     Katika kutekeleza azma ya kutoa elimumsingi bila ada na kugharamia mikopo ya wanafunzi wa elimu ya juu, Serikali imetoa shilingi bilioni 618.0;
(v)       Serikali imeendelea kutekeleza ujenzi wa miundombinu ili kupanua fursa za uchumi, kilimo, biashara na viwanda ikiwemo barabara zinazounganisha mikoa na nchi jirani, barabara zinazopunguza msongamano katika majiji, barabara za vijijini, reli, viwanja vya ndege, na bandari. Katika eneo hili kiasi cha shilingi trilioni 1.87 kimetolewa; na
(vi)     Serikali imeendelea kulipa malimbikizo ya madai ya watumishi umma, wazabuni, wakandarasi na watoa huduma ambapo kiasi cha shilingi trilioni 1.17 kimelipwa.

23.    Mheshimiwa Spika, Serikali pia imeendelea kuchukua hatua nyingine zenye lengo la kuimarisha usimamizi wa bajeti ya Serikali kama ifuatavyo:

a)Deni la Serikali
24.    Mheshimiwa Spika, katika kuhakikisha Deni la Serikali linadhibitiwa na linaendelea kuwa himilivu, Serikali inaendelea kuzingatia Sheria ya Mikopo, Dhamana, na Misaada SURA 134. Aidha, Serikali inatekeleza Mkakati wa Muda wa Kati wa Kusimamia Deni unaotoa dira ya namna bora ya ukopaji ili kuepuka gharama na athari mbalimbali zinazoweza kujitokeza katika kusimamia deni la Serikali. Katika kudhibiti kuongezeka kwa gharama za mikopo, Serikali ilijikita zaidi kukopa kwenye mikopo yenye masharti ya kati (Semi Concessional Loans) hasa mikopo inayowezesha uagizaji wa vifaa na mitambo kutoka nchi inayokopesha (Export Credit Agency - ECA) na pale ilipolazimu, mikopo ya masharti ya kibiashara ilikopwa kwa uangalifu mkubwa ikiwemo kuhakikisha kwamba mikopo hiyo inatumika kwenye maeneo ambayo yanachochea ukuaji wa uchumi.

25.    Mheshimiwa Spika, hadi kufikia Aprili 2018, deni la Serikali lilifikia shilingi trilioni 49.65 ikiwa ni sawa na ongezeko la asilimia 13.4 ikilinganishwa na shilingi trilioni 43.79 Aprili 2017.  Kati ya kiasi hicho, deni la ndani lilikuwa shilingi trilioni 14.05 na deni la nje shilingi trilioni 35.60 sawa na asilimia 71.71 ya deni lote.  Ongezeko la deni hilo limetokana na mikopo ya zamani na inayoendelea kupokelewa yenye masharti nafuu au kibiashara na malimbikizo ya riba ya Deni la Nje  hasa kwenye nchi zisizo wanachama wa kundi la Paris ambazo Serikali bado inajadiliana nazo kuhusu msamaha wa madeni  kulingana na makubaliano na kundi hilo.

26.    Mheshimiwa Spika, Mikopo nafuu kutoka Mashirika ya Fedha ya Kimataifa imeendelea kuwa chanzo kikubwa cha mikopo kutoka nje ambayo imechangia asilimia 59.6 ya deni lote la nje. Mikopo yenye masharti ya kibiashara imechangia asilimia 28.5, wakati mikopo kutoka nchi wahisani imechangia asilimia 11.9. Mikopo hii imetumika kugharamia miradi mbalimbali ya maendeleo.

27.    Mheshimiwa Spika, Deni la Serikali limekuwa likiongezeka. Hata hivyo deni hilo limeendelea kuwa himilivu na ukuaji wake unawiana na kasi ya ukuaji wa uchumi wetu. Tathmini ya uhimilivu wa deni iliyofanyika Novemba 2017 inaonesha kuwa deni ni himilivu kwa kipindi cha muda wa kati na muda mrefu. Uwiano wa deni kwa thamani ya sasa (present value) kwa Pato la Taifa ni asilimia 34.4 ikilinganishwa na ukomo wa asilimia 56; thamani ya deni la nje kwa mauzo ya nje ilikuwa asilimia 81.8 ikilinganishwa na ukomo wa asilimia 150; thamani ya deni la nje kwa mapato ya ndani asilimia 117.1 ikilinganishwa na ukomo wa asilimia 250; ulipaji wa deni la nje kwa mapato yatokanayo na mauzo nje asilimia 9.3 ikilinganishwa na ukomo wa asilimia 20; na ulipaji wa deni la nje kwa kutumia mapato ya ndani ulifikia asilimia 13.3  ikilinganishwa na ukomo wa asilimia 20. Napenda kusisitiza tena kwamba hakuna dhambi kwa nchi kukopa kwa busara (prudently). Mambo ya muhimu ya kujiridhisha nayo ni kuwa mikopo hiyo inatumika kujenga uwezo zaidi wa kuzalisha mali (productive capacity) na kurejesha mikopo hiyo kwa kuzingatia uwezo wa uchumi kuhimili mzigo wa madeni (debt sustainability).

b)Kudhibiti Malimbikizo ya Madai ya Serikali
28.    Mheshimiwa Spika, Serikali imekuwa ikifanya juhudi mbalimbali za kupunguza malimbikizo ya madai ikiwa ni pamoja na kutenga fedha kila mwaka kwenye bajeti kwa ajili ya kulipa madai yaliyohakikiwa; kuhimiza uzingatiaji wa sheria na kanuni zake kama vile, Sheria ya Bajeti Na. 11 ya mwaka 2015; Sheria ya Ununuzi wa Umma SURA 410; Sheria ya Fedha za Umma SURA 348 na kanuni zake na kutoa miongozo na maelekezo mbalimbali yakiwemo Waraka Na. 1 wa Mlipaji Mkuu wa Serikali unaotolewa kila mwaka kuhusu utekelezaji wa bajeti na Mwongozo wa Mpango na Bajeti unaotolewa kila mwaka.
 
29.    Mheshimiwa Spika, Katika kukabiliana na changamoto hiyo ya malimbikizo ya madai, Serikali imeandaa Mkakati wa Kulipa Madeni na Kuzuia ulimbikizaji wa Madeni. Madai yanayohusika kwenye Mkakati huo ni yale yaliyozalishwa na Wizara, Idara Zinazojitegemea (MDAs) na Sekretarieti za Mikoa (RSs) yakiwemo madeni ya Watumishi, Wazabuni na Watoa Huduma, pamoja na madai ya Wakandarasi. Serikali itaendelea kutenga bajeti kwa ajili ya kulipa madai yaliyohakikiwa kwa kuzingatia mpango (roadmap) ulioandaliwa kulipa madeni hayo hadi yatakapofikia kiwango himilivu. Katika ulipaji wa madeni, kipaumbele kitatolewa kwa madeni yanayogusa watoa huduma wengi na yale ambayo yanaongezeka kutokana na riba.
30.    Mheshimiwa Spika, Mkakati huo unamtaka kila Afisa Masuuli kushiriki kikamilifu katika utekelezaji wake ili kuiwezesha Serikali kufikia malengo yake ya kudhibiti malimbikizo ya madai na kutoa huduma kwa wananchi kwa wakati. Hivyo, katika kuhakikisha kwamba hakuna madeni mapya yanayozalishwa, kila Afisa Masuuli atapaswa kuzingatia yafuatayo:
(i)         Mikataba yote ya ujenzi wa miundombinu inazingatia viwango vya bajeti vilivyowekwa katika kila Fungu. Aidha, Fungu husika lisiingie mikataba nje ya viwango hivyo bila kibali cha Mlipaji Mkuu wa Serikali; vile vile Kifungu cha 51(1) na (2) cha Sheria ya Bajeti ya 2015 kinaelekeza kwamba miadi yote ya miaka zaidi ya mmoja (Multi-year Commitments) lazima ipate idhini ya Waziri wa Fedha ikiwa imezingatia viwango vya bajeti, malipo ya miadi hii isizidi viwango/bajeti iliyoidhinishwa na Bunge, pamoja na kulipa madai baada ya uhakiki;
(ii)       Kutoa kipaumbele kwa ukamilishaji wa miradi inayoendelea kabla ya kuanzisha miradi mipya, sambamba na kuhakikisha kwamba miradi inayoanzishwa inatengewa fedha katika bajeti;
(iii)     Maafisa Masuuli kutoingia makubaliano ya kupatiwa huduma au bidhaa bila ya kuwa na fedha au kibali cha maandishi kutoka kwa Mlipaji Mkuu wa Serikali; na miadi yoyote ni lazima iingizwe kwenye mtandao wa IFMS;
(iv)     Madai ya watoa huduma wote na Wakandarasi lazima yafanyike baada ya kupata hati za ununuzi (LPO) kutoka kwenye mfumo wa IFMS iliyozingatia bajeti iliyoidhinishwa na Bunge, pamoja na kuwepo kwa ridhaa ya matumizi (Exchequer Issue Notification) kwa vifungu husika vya matumizi. Hivyo, Serikali inasisitiza kwamba, LPO zilizotoka kwenye mfumo wa Malipo ya Serikali (IFMIS) ndiyo zitumike kama msingi wa malipo kwa Watoa Huduma; na
(v)       Kuzingatia matumizi ya Sheria ya Bajeti Na. 11 ya mwaka 2015 na  Sheria ya Fedha za Umma SURA 348 na waraka wa Mlipaji Mkuu wa Serikali kuhusu utekelezaji wa bajeti.



III.      SERA ZA BAJETI  KWA MWAKA 2018/19
Shabaha za Uchumi Jumla na Bajeti
31.    Mheshimiwa Spika, Shabaha za uchumi jumla na bajeti katika kipindi cha mwaka 2018/19 ni kama ifuatavyo:-
(i)         Pato la Taifa kukua kwa asilimia 7.2 mwaka 2018 kutoka ukuaji halisi wa asilimia 7.1 mwaka 2017;
(ii)       Mfumuko wa bei kuendelea kubaki katika wigo wa tarakimu moja;
(iii)     Mapato ya ndani kufikia asilimia 15.8 ya Pato la Taifa mwaka 2018/19 kutoka matarajio ya asilimia 15.3 mwaka 2017/18 na uwiano halisi wa asilimia 15.6 mwaka 2016/17;
(iv)     Mapato ya kodi kufikia asilimia 13.6 ya Pato la Taifa mwaka 2018/19 kutoka matarajio ya asilimia 13.0 mwaka 2017/18 na uwiano halisi wa asilimia 13.3 mwaka 2016/17;
(v)       Matumizi ya Serikali kufikia asilimia 24.5 ya Pato la Taifa  mwaka 2018/19 kutoka matarajio ya asilimia 23.0 mwaka 2017/18  na matumizi halisi ya asilimia 22.2 mwaka 2016/17; na
(vi)     Nakisi ya bajeti kufikia asilimia 3.2 ya Pato la Taifa mwaka 2018/19 kutoka matarajio ya asilimia 2.1 mwaka 2017/18 na uwiano halisi wa asilimia 1.5 mwaka 2016/17.

Sera na Mikakati ya Kuongeza Mapato
32.    Mheshimiwa Spika, ili kuongeza na kuimarisha ukusanyaji wa mapato ya ndani, sera za mapato kwa mwaka 2018/19 zitalenga katika kuongeza wigo wa kodi, kuimarisha usimamizi wa vyanzo vilivyopo hususan katika matumizi ya mifumo ya kielektroniki na hatua nyingine za kiutawala.

33.    Mheshimiwa Spika, katika kuongeza wigo wa kodi, yapo maeneo makuu mawili yatakayozingatiwa na Serikali ambayo ni kurasimisha sekta isiyo rasmi na kuboresha mazingira ya uwekezaji ili kupata vyanzo vipya vya mapato vitokanavyo na uwekezaji huo. Zipo hatua za urasimishaji zilizoanza kufanyika mfano uthaminishaji wa majengo, na upimaji wa viwanja, zoezi ambalo linaendelea nchi nzima. Serikali itaongeza kasi ya urasimishaji ikiwa ni pamoja na kuwepo na mbinu bunifu, rafiki, shirikishi na za kimkakati.

34.    Mheshimiwa Spika, mazingira bora ndio msingi mkuu wa kuvutia biashara na uwekezaji ikiwemo kuboresha miundombinu msingi, vivutio vya kikodi, sera zisizobadilika (policy consistency and predictability), upatikanaji wa ardhi na taratibu za kisheria na usimamizi. Pale mazingira yanapokuwa mazuri, uwekezaji, uzalishaji, ajira na miamala ya kibiashara inaongezeka na hivyo kupelekea kuongezeka kwa vyanzo vipya vya mapato.

35.    Mheshimiwa Spika, uchambuzi uliofanywa na Serikali mwaka 2017/18 ulibaini changamoto zifuatazo kuhusiana na mazingira ya biashara na uwekezaji :
(i)         Migongano ya sheria, kanuni na taratibu zinazotumiwa na mamlaka mbalimbali;
(ii)       Gharama kubwa za kuanzisha  na kuendesha biashara kutokana na wingi wa kodi, ada na tozo zinazoambatana na taratibu ngumu na nyingi zenye urasimu  usio na tija  na hivyo kutoa mianya na mazingira ya rushwa; na
(iii)     Muingiliano wa majukumu na wingi wa mamlaka za udhibiti katika kuidhinisha na kutoa hati, vibali na vyeti kwenye shughuli za uwekezaji na biashara.

36.    Mheshimiwa Spika, kutokana na uchambuzi huo, Serikali imeandaa Mpango wa Kuboresha Mfumo wa Udhibiti wa Biashara (Blueprint for Regulatory Reforms to Improve Business Environment for Tanzania). Miongoni mwa mapendekezo ya Mpango huo ambayo yatatekelezwa kwa nguvu zaidi kuanzia mwaka ujao wa fedha  (2018/19) ni kurahisisha taratibu za kulipa kodi, tozo na ada mbalimbali, na kupunguza muda na mlolongo mrefu wa kusajili makampuni na biashara. Serikali ya Awamu ya Tano inaamini kuwa maendeleo endelevu yatapatikana kwa haraka zaidi katika mazingira yenye ushirikiano wa kweli na wa dhati kati ya sekta ya umma na sekta binafsi.

37.    Mheshimiwa Spika, katika kuimarisha usimamizi wa vyanzo vya mapato vilivyopo, Serikali itaendelea na zoezi la uunganishaji wa Wizara, Idara, Wakala, taasisi na mashirika ya umma kwenye Mfumo wa Serikali wa Kielektroniki wa ukusanyaji wa mapato (Government electronic Payment Gateway -GePG) ili kuboresha ukusanyaji na kudhibiti upotevu wa mapato ya Serikali. Mfumo huu ulianzishwa mwaka 2017 na kupitishwa na Bunge kupitia marekebisho ya Sheria ya Fedha za Umma SURA 348 ambayo iliziagiza taasisi zote za Serikali kukusanya mapato kwa kutumia Mfumo wa GePG. Hadi mwezi Mei, 2018, jumla ya taasisi 234 zinazokusanya maduhuli zikijumuisha Halmashauri zote 185 zimeunganishwa kwenye Mfumo huu. Nachukua fursa hii kuagiza Mikoa, Mamlaka za Serikali za Mitaa, Wizara, Idara na Taasisi zote za Serikali zilizobaki zihakikishe kwamba zimeunganishwa na kuanza kutumia mfumo wa GePGkabla ya Juni, 2019. Mbali na Mfumo huu, ninawakumbusha Maafisa Masuuli wote kuhakikisha kuwa ukusanyaji wa maduhuli unafanyika kwa kutumia mashine za kielektroniki (EFDs) pamoja na benki na siyo risiti za kuandikwa kwa mkono.

38.    Mheshimiwa Spika, kuhusu hatua nyingine za kiutawala za kuongeza mapato ya Serikali, ninaelekeza yafuatayo:
(i)         Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA)  ichukue hatua za makusudi za kuboresha mahusiano kati yake na walipa kodi kwa lengo la kuondoa dhana  iliojengeka miongoni mwa walipa kodi kuwa TRA inatumia nguvu na vitisho kudai kodi;
(ii)       Ofisi ya Msajili wa Hazina iimarishe  usimamizi na ukaguzi  kwenye kampuni ambazo Serikali ina hisa ili kuhakikisha kuwa Serikali inapata gawio stahiki katika uwekezaji wake; na
(iii)     Mamlaka za Serikali za Mitaa zijielekeze kwenye miradi itakayochochea upatikanaji wa mapato katika mamlaka hizo hususan viwanda, masoko na machinjio ya kisasa, stendi za mabasi, stendi za maegesho ya malori kwenye mipaka na nchi jirani na maghala ya kuhifadhi nafaka.

Kuimarisha Ushirikiano na Washirika wa Maendeleo
39.    Mheshimiwa Spika, misaada na mikopo nafuu imekuwa ikipungua kutoka wastani wa asilimia 26.3 ya bajeti halisi ya mwaka 2010/11 hadi asilimia 10.4 mwaka 2016/17. Kutokana na umuhimu wa kuwa na maendeleo endelevu na kuhakikisha kuwa misaada na mikopo nafuu inapatikana  kama ilivyoahidiwa na kwa wakati, Serikali kwa kushirikiana na Washirika wa Maendelo na wadau wengine imekamilisha Mwongozo wa Ushirikiano wa Maendeleo (Development Cooperation Framework - DCF). Mwongozo huo uliidhinishwa na Serikali mwezi Agosti 2017 na umebainisha:
(i)         Misingi ya jumla ya kuongoza ushirikiano ambayo ni pamoja na Serikali kuongoza michakato ya kuibua vipaumbele vya miradi ya maendeleo; na
(ii)       Mfumo wa majadiliano ambao uko katika ngazi tatu; Majadiliano ya Kitaifa ya Kimkakati, Majadiliano ya Kisekta na Majadiliano yenye Mwelekeo wa Kisiasa.


Sera za Matumizi
40.    Mheshimiwa Spika, sera za matumizi katika mwaka 2018/19 zitajumuisha:
(i)         Kudhibiti nakisi ya bajeti isizidi asilimia 3.2 ya Pato la Taifa;
(ii)       Kuelekeza fedha kwenye maeneo ya kipaumbele na yenye tija ili kuchochea ukuaji wa kilimo na viwanda, kupanua fursa za ajira, kujenga na kuboresha miundombnu ya uchumi na kuimarisha upatikanaji wa huduma bora za jamii;
(iii)     Kusimamia nidhamu ya matumizi ya fedha za umma na kuendelea kupunguza matumizi yasiyo ya lazima; na
(iv)     Kudhibiti ulimbikizaji wa madai.

41.    Mheshimiwa Spika, Katika kusimamia sera hizi, Serikali itachukua hatua zifuatazo:
(i)         Kuwachukulia hatua za kisheria, kinidhamu na kiutawala wote watakaothibitika kwenda kinyume na sheria na kanuni zinazoongoza utendaji katika nafasi zao. Napenda niwakumbushe tena kuwa kula fedha za miradi ya wananchi ni sawa na kula sumu – wasijaribu!!
(ii)       Kuhakikisha kuwa Maafisa Masuuli hawaingii mikataba bila kuwa na uhakika wa upatikanaji wa fedha au ridhaa ya Mlipaji Mkuu wa Serikali na kuzuia matumizi na ahadi (commitments) za matumizi nje ya mfumo wa “IFMS”. Lengo ni kudhibiti ulimbikizaji wa madai;
(iii)     Kuwianisha matumizi na mapato halisi yatakayopatikana kwa kila mwezi;
(iv)     Kulipa madai mbalimbali yaliyohakikiwa;
(v)       Kuhakikisha kuwa ununuzi wa umma unawiana na thamani ya fedha itakayotumika; na
(vi)     Kuimarisha ufuatiliaji wa matumizi ya fedha za umma ili zitumike kama ilivyokusudiwa.

 Maeneo ya vipaumbele kwa mwaka 2018/19
42.    Mheshimiwa Spika, kama ilivyoainishwa katika Mpango wa Maendeleo wa Taifa wa Mwaka 2018/19 ambao niliuwasilisha leo asubuhi, bajeti ya matumizi katika mwaka 2018/19 itaweka mkazo zaidi katika uendelezaji wa miradi ya kielelezo; kufungamanisha maendeleo ya watu; na ujenzi wa mazingira wezeshi kwa ajili ya uwekezaji na uendeshaji biashara.
43.    Mheshimiwa Spika, maeneo ya kipaumbele katika bajeti hii ni yafuatayo:
(i)         Kilimo:Fedha zitaelekezwa zaidi kuboresha miundombinu ya umwagiliaji, maghala na masoko, kuimarisha upatikanaji wa  pembejeo na zana za kilimo, kupanua huduma za ugani, kuboresha mfumo wa utafiti na utoaji wa matokeo ya utafiti kwa wananchi, na uendelezaji wa sekta ndogo za uvuvi na mifugo. Mkazo umewekwa katika sekta hii kwa kuzingatia kuwa inategemewa na wananchi wengi na ndiyo itakayotupatia malighafi kwa ajili ya viwanda, kutuhakikishia usalama wa chakula na kuongezeka kwa kipato cha wananchi;
(ii)       Viwanda: Katika kuchochea ukuaji wa viwanda nchini, Serikali itaelekeza nguvu zake kwa kutekeleza Mpango wa Kuboresha Mfumo wa Udhibiti wa Biashara ili kuvutia uwekezaji wa sekta binafsi hususan viwanda vya nguo, ngozi na nyama, samaki, mafuta ya kula, madawa na vifaa tiba, vyakula vya binadamu na mifugo, na katika sekta ya madini. Aidha, uendelezaji wa viwanda na kilimo utapaswa kuzingatia uendelevu wa mazingira;
(iii)     Huduma za Jamii: Maji:Eneo lingine muhimu ni kuongeza upatikanaji na usambazaji wa maji safi hasa vijijini na uondoshaji wa majitaka, uchimbaji wa visima katika maeneo kame nchini na ujenzi wa mabwawa makubwa ya kimkakati. Elimu:Serikali itaendelea kugharamia elimu msingi bila ada, kuongeza idadi ya wataalam katika fani adimu kwenye maeneo ya madini, mafuta na gesi, madaktari bingwa (moyo na figo) pamoja na utoaji wa mikopo kwa wanafunzi wa elimu ya juu. Afya: rasilimali fedha zitaelekezwakuongeza usambazaji wa dawa, vifaa tiba, vitendanishi nauboreshaji wahuduma katika vituo vya afya, zahanati na hospitali za rufaa. Vile vile katika mwaka ujao wa fedha, Serikali itaelekeza fedha zaidi za LGCD kwenye miradi ya maendeleo inayotekelezwa na Halmashauri hususan miradi ya elimu na afya. Aidha, Serikali itaweka msukumo kuimarisha upatikanaji wa lishe bora kwa mama na mtoto hususan katika siku 1,000 za mtoto tangu kutungwa kwa mimba ili kuondokana na changamoto ya kuwa na watoto wenye udumavu na hivyo kukua vema kimwili na kiakili. Aidha, mahitaji ya makundi maalum katika jamii yetu (wanawake, vijana, watoto, watu wenye ulemavu na wazee) yataendelea kuangaliwa kipekee;
(iv)     Kujenga na kukarabati miundombinu wezeshihususan kuongeza uzalishaji wa umeme kwa kutumia vyanzo mbalimbali, kuendelea na ujenzi wa reli mpya ya kati kwa kiwango cha kimataifa (standard gauge), ujenzi wa barabara za kuunganisha mikoa na zile za vijijini, na kuimarisha usafiri wa anga na majini; na
(v)       Maeneo mengine ya kipaumbele ni: kurahisisha umiliki wa ardhi,  kuimarisha huduma za mawasiliano,  kifedha na utalii na kuimarisha ulinzi, usalama, utawala bora, na utoaji haki.

IV.      HATUA ZA MAPATO NA MABORESHO YA MFUMO WA KODI, ADA NA TOZO MBALIMBALI

Maboresho ya Mfumo wa Kodi, Ada na Tozo Mbalimbali

44.    Mheshimiwa Spika, napenda kuwasilisha mapendekezo ya kufanya marekebisho ya mfumo wa kodi ikiwemo kurekebisha baadhi ya viwango vya kodi, tozo na ada zinazotozwa chini ya Sheria mbalimbali na pia taratibu za ukusanyaji na usimamiaji wa mapato ya Serikali. Marekebisho haya yanalenga pamoja na mambo mengine, kuchochea kasi ya ukuaji wa uchumi hususan katika sekta ya Viwanda, Utalii, kukuza ajira, na kuongeza mapato ya Serikali. Aidha, marekebisho haya yamezingatia dhamira ya Serikali ya kuwa na mfumo wa kodi ambao ni tulivu na wenye kutabirika. Marekebisho hayo yanahusu Sheria zifuatazo:-

a.   Sheria ya Kodi ya Ongezeko la Thamani, SURA 148;
b.   Sheria ya Kodi ya Mapato, SURA 332;
c.   Sheria ya Ushuru wa Bidhaa, SURA 147;
d.   Sheria ya Fedha za Serikali za Mitaa, SURA 290;
e.   Sheria ya Usimamizi wa Kodi, SURA 438;
f.     Sheria ya Fedha za Serikali za Mitaa, SURA 290; Sheria ya Fedha za Umma, Sura 348; na Sheria ya Benki Kuu, SURA 197;
g.   Sheria ya Forodha ya Jumuiya ya Afrika Mashariki ya mwaka 2004;
h.  Sheria zinazosimamia Bodi za Mazao;
i.     Sheria ya Michezo ya Kubahatisha SURA 41;
j.     Marekebisho madogo madogo katika baadhi ya Sheria za Kodi na Sheria nyingine mbalimbali; na
k.   Marekebisho ya Ada na Tozo mbalimbali zinazotozwa na Wizara, Mikoa na Idara zinazojitegemea.


a)       Sheria ya Kodi ya Ongezeko la Thamani, SURA 148
45.    Mheshimiwa Spika, napendekeza kufanya marekebisho kwenye Sheria ya Kodi ya Ongezeko la Thamani,Sura 148 kama ifuatavyo:-

(i)         Kusamehe Kodi ya Ongezeko la Thamani kwenye vifungashio vya madawa ya binadamu vitakavyotengenezwa mahsusi kwa ajili ya viwanda vinavyozalisha dawa hapa nchini. Aidha, vifungashio hivyo vitakuwa na machapisho ya majina ya kiwanda husika cha utengenezaji madawa ili kuhakikisha kwamba vinatumiwa na viwanda hivyo na siyo vinginevyo. Lengo la hatua hii nikupunguza gharama za uzalishaji na kuvilinda viwanda vinavyotengeneza madawa hapa nchini ili viweze kumudu ushindani na kuongeza uzalishaji;
(ii)       Kusamehe Kodi ya Ongezeko la Thamani kwenye virutubisho vinavyotumika kutengenezea vyakula vya mifugo (animal and poultry feeds additives) vinavyoagizwa kutoka nje. Lengo la hatua hii ni kupunguza gharama kwa wafugaji na kuhamasisha ufugaji bora ili kuongeza mchango wa Sekta hiyo katika Uchumi;
(iii)     Kufanya marekebisho kwenye kifungu cha 6(2)(a) cha Sheria ya Kodi ya Ongezeko la Thamani ili kumpa mamlaka Waziri mwenye dhamana na maswala ya fedha  kutoa msamaha wa kodi kwa miradi ya Serikali inayotekelezwa kwa mikopo ya kibiashara. Hivi sasa Sheria ya Kodi ya Ongezeko la Thamani inakataza kusamehe kodi kwenye mikopo ya kibiashara hali ambayo imesababisha kukwama kwa utekelezaji wa miradi muhimu ya Serikali kama vile miradi ya Maji, barabara n.k. Hivyo, marekebisho yanayopendekezwa yatawezesha utekelezaji wa miradi ya Serikali kwa wakati uliopangwa;
(iv)     Kufanya marekebisho kwenye kifungu cha 6(2)(a) cha Sheria ya Kodi ya Ongezeko la Thamani ili kumpa mamlaka Waziri mwenye dhamana na masuala ya fedha kusamehe kodi hiyo pale ambapo kuna mkataba uliosainiwa baina ya Serikali ya Tanzania na Taasisi ya Fedha au Benki ambayo ni “mwakilishi” wa Serikali nyingine aliyepewa dhamana na Serikali hiyo kuingia mikataba na kusimamia utekelezaji wa miradi husika. Hivi sasa Sheria ya Kodi ya Ongezeko la Thamani inampa mamlaka Waziri huyo kusamehe kodi pale ambapo kuna mkataba baina ya Serikali ya Tanzania na Serikali ya nchi nyingine unaotoa msamaha wa kodi. Hivyo miradi mingi inayohusisha mikataba ya misaada au mikopo kupitia mabenki na Taasisi za fedha imekwama utekelezaji wake. Kwa msingi huo, marekebisho haya yanalenga katika kuondoa ukwamishaji na ucheleweshaji wa utekelezaji wa miradi mingi ya Serikali inayotekelezwa kwa fedha za Washirika wa Maendeleo kupitia mikataba inayosainiwa na Serikali yetu na Benki au Taasisi za Fedha za Serikali za nchi nyingine; na
(v)       Kusamehe Kodi ya Ongezeko la Thamani kwenye taulo za kike (sanitary pads) HS Code 9619.00.10. Lengo la hatua hii ni kuwezesha upatikanaji wa bidhaa hii muhimu kwa bei nafuu kwa ajili ya kulinda afya ya mama na mtoto wa kike hasa watoto walio shuleni na vijijini. Ni matarajio ya Serikali kuwa wazalishaji na wauzaji wa taulo za kike wataziuza kwa bei nafuu baada ya kusamehewa kodi hii.

Hatua hizi zote za Kodi ya Ongezeko la Thamani kwa ujumla wake zinatarajiwa kupunguza mapato ya Serikali kwa kiasi cha shilingi milioni 219.1

b)       Sheria ya Kodi ya Mapato, SURA 332
46.    Mheshimiwa Spika, napendekeza kufanya marekebisho kwenye Sheria ya   Kodi ya Mapato, Sura 332 kama ifuatavyo:-

(i)         Kufanya marekebisho kwenye Sheria ya Kodi ya Mapato ili kupunguza kiwango cha Kodi ya Mapato ya Makampuni (Corporate Income Tax) kutoka asilimia 30 mpaka asilimia 20 kwa miaka mitano kuanzia mwaka 2018/19 hadi mwaka 2022/23 kwa wawekezaji wapya wa viwanda vya madawa ya binadamu na viwanda vinavyotengeneza bidhaa za  ngozi. Aidha, Serikali itaingia mkataba wa makubaliano (performance agreement) na kila mwekezaji ambao utaainisha wajibu wa kila upande. Lengo la hatua hii ni kuongeza uwekezaji katika sekta ya madawa ya binadamu na usindikaji wa ngozi ambao kwa sasa haufanyiki nchini na pia kuongeza ajira na mapato ya Serikali. Aidha, hatua hii itapunguza matumizi ya fedha za kigeni zinazotumika kuagiza dawa hizo kutoka nje na kuhamasisha uzalishaji wa madawa mengi zaidi hapa nchini;
(ii)       Kufuta kifungu cha 10A cha Sheria ya Kodi ya Mapato kinachomkataza Waziri mwenye dhamana ya masuala ya fedha kutoa msamaha wa kodi kwenye miradi ya Serikali inayotekelezwa kwa fedha za mikopo ya kibiashara (non concessional loans). Lengo la hatua hii ni kumpa mamlaka Waziri huyo kutoa msamaha wa kodi ya mapato kwa miradi hiyo ambayo imekuwa na changamoto katika utekelezaji wakati Serikali inapopata mikopo ya aina hiyo; na
(iii)     Kurekebisha Sheria ya Kodi ya Mapato ili kutoa msamaha wa Kodi ya zuio inayotozwa kwenye riba kwa mikopo inayotolewa kwa Serikali na Benki, Taasisi za Fedha na wahisani kwa ajili ya utekelezaji wa miradi ya Serikali.

Hatua hizi za Kodi ya Mapato kwa ujumla wake zinatarajiwa kuongeza mapato ya Serikali kwa kiasi cha shilingi milioni 220.5.

c)       Sheria ya Ushuru wa Bidhaa,  SURA 147
47.    Mheshimiwa Spika, kwa mujibu wa Sheria ya Ushuru wa Bidhaa Kifungu cha 124(2), marekebisho ya viwango maalum vya Ushuru wa Bidhaa (specific duty rates)zisizo za petroli yanaweza kufanyika kila mwaka ili kuviwianisha na mfumuko wa bei na viashiria vingine vya uchumi jumla. Hata hivyo, ili kutekeleza azma ya Serikali ya awamu ya tano ya kujenga uchumi wa viwanda, napendekeza kutofanya mabadiliko ya viwango maalum vya Ushuru wa Bidhaa zisizo za petroli zinazozalishwa hapa nchini na kuongeza viwango vya Ushuru wa Bidhaa zisizo za petroli zinazoagizwa kutoka nje ya nchi kama ifuatavyo:- 

(i)         Ushuru wa Bidhaa kwenye vinywaji baridi utaendelea kutozwa kwa kiwango cha shilingi 61 kwa lita;
(ii)       Ushuru wa Bidhaa kwenye maji ya kunywa yaliyosindikwa kwenye chupa yaliyoagizwa kutoka nje utaongezeka kutoka shilingi 61 kwa lita hadi shilingi 64.05 kwa lita ikiwa ni ongezeko la shilingi 3.05 kwa lita. Aidha, Ushuru wa Bidhaa kwenye maji yanayozalishwa hapa nchini utaendelea kutozwa kwa kiwango cha  sasa cha shilingi 58 kwa lita;
(iii)     Ushuru wa Bidhaa kwenye maji ya matunda (juisi) iliyotengenezwa kwa matunda yanayozalishwa hapa nchini (local juices)hautaongezeka na utaendelea kutozwa kwa kiwango cha shilingi 9 kwa lita;
(iv)     Ushuru wa Bidhaa kwenye maji ya matunda (juisi) iliyotengenezwa kwa matunda ambayo hayazalishwi hapa nchini (imported juices) utaongezeka kutoka shilingi 221 kwa lita hadi shilingi 232 kwa lita ikiwa ni ongezeko la shilingi 11 kwa lita;
(v)       Ushuru wa Bidhaa kwenye bia inayotengenezwa kwa nafaka ya hapa nchini na ambayo haijaoteshwa (Beer from Local Unmalted Cereals) hautaongezeka na utaendelea kutozwa kwa kiwango cha shilingi 450 kwa lita;
(vi)     Ushuru wa Bidhaa kwenye bia zinazoagizwa kutoka nje ya nchi utaongezeka kutoka shilingi 765 kwa lita hadi shilingi 803.25 kwa lita ikiwa ni ongezeko la shilingi 38.25 kwa lita;
(vii)   Ushuru wa Bidhaa kwenye bia zisizo za kilevi, ikijumuisha vinywaji vya kuongeza nguvu vinavyoagizwa kutoka nje ya nchi utaongezeka kutoka shilingi 561 kwa lita hadi shilingi 589.05 kwa lita ikiwa ni ongezeko la shilingi 28.05 kwa lita. Aidha, Ushuru wa Bidhaa kwenye bia zisizo za kilevi, ikijumuisha vinywaji vya kuongeza nguvu vinavyozalishwa hapa nchini utaendelea kutozwa kwa kiwango cha sasa cha shilingi 561 kwa lita;
(viii)Kuanzisha Ushuru wa Bidhaa wa shilingi 200 kwa lita kwenye mvinyo uliotengenezwa kutokana na usindikaji wa matunda (kama ndizi, rozela/choya, nyanya, nk) yanayozalishwa hapa nchini tofauti na zabibu kwa kiwango kinachozidi asilimia 75;
(ix)     Ushuru wa Bidhaa kwenye mvinyo uliotengenezwa kwa zabibu inayozalishwa ndani ya nchi kwa kiwango kinachozidi asilimia 75 hautaongezeka na utaendelea kutozwa kwa kiwango cha shilingi 200 kwa lita;
(x)       Ushuru wa Bidhaa kwenye mvinyo uliotengenezwa kwa zabibu inayozalishwa nje ya nchi kwa kiwango kinachozidi asilimia 25, utaongezeka kutoka shilingi 2,349 kwa lita hadi shilingi 2,466 kwa lita, ikiwa ni ongezeko la shilingi 117 kwa lita;
(xi)     Ushuru wa Bidhaa kwenye vinywaji vikali vinavyoagizwa kutoka nje utaongezeka kutoka shilingi 3,481 kwa lita hadi shilingi 3,655.05 kwa lita, ikiwa ni ongezeko la shilingi 174.05 kwa lita. Aidha, Ushuru wa Bidhaa kwenye vinywaji vikali vinavyozalishwa nchini hautaongezeka na utaendelea kutozwa kwa kiwango cha shilingi 3,315 kwa lita;
(xii)   Ushuru wa Bidhaa kwenye sigara zisizo na kichungi zinazotengenezwa kutokana na tumbaku inayozalishwa hapa nchini kwa kiwango cha angalau asilimia 75, hautaongezeka na utaendelea kutozwa kwa kiwango cha shilingi 12,447 kwa kila sigara elfu moja;
(xiii)Ushuru wa Bidhaa kwenye sigara zenye kichungi zinazotengenezwa kutokana na tumbaku inayozalishwa hapa nchini kwa kiwango cha angalau asilimia 75, hautaongezeka na utaendelea kutozwa kwa kiwango cha shilingi 29,425 kwa kila sigara elfu moja;
(xiv)Ushuru wa Bidhaa kwenye sigara zenye sifa tofauti na (xii) na (xiii) utaongezeka kutoka shilingi 53,235 hadi shilingi 55,896.75 kwa kila sigara elfu moja ikiwa ni ongezeko la shilingi 2,661.75 kwa kila sigara elfu moja;
(xv)   Ushuru wa Bidhaa kwenye tumbaku ambayo iko tayari kutengeneza sigara (cut filler) inayoagizwa kutoka nje utaongezeka kutoka shilingi 26,888 hadi shilingi 28,232.4 kwa kilo, ikiwa ni ongezeko la shilingi 1,344.4 kwa kilo; na
(xvi)Ushuru wa Bidhaa wa ‘cigar’ unabaki kuwa asilimia 30.

48.    Mheshimiwa Spika, napendekeza kuanzisha Mfumo Mpya wa Stempu za Kodi za kielektroniki utakaoanza kutumika tarehe 1 Septemba 2018. Mfumo mpya wa Stempu za Kodi za kielektroniki utaiwezesha Serikali kutumia teknolojia ya kisasa kupata taarifa sahihi za uzalishaji viwandani na kwa wakati (real time) zinazotumika kupanga mipango ya maendeleo ya Taifa. Pia mfumo huu mpya utaiwezesha Serikali kudhibiti uvujaji wa mapato na kutambua mapema kiasi cha Kodi ya Ushuru wa Bidhaa, Kodi ya Mapato na ile ya Ongezeko la Thamani itakayolipwa. Aidha, mfumo wa Stempu za Kodi za kielektroniki utadhibiti tatizo la uwepo wa stempu za karatasi za kugushi ambalo linachangia uwepo wa bidhaa zisizokidhi viwango vya ubora na zinazoweza kuathiri afya za binadamu. Mfumo huu mpya unatumika katika nchi nyingine ikiwa pamoja na Kenya, Morocco, Uturuki, Malaysia na Switzerland na umekuwa na mafanikio makubwa.

Hatua za Ushuru wa Bidhaa kwenye bidhaa zisizo za petroli kwa ujumla wake zinatarajiwa kuongeza mapato ya Serikali kwa kiasi cha shilingi milioni 119,456.6

d)       Sheria ya Fedha za Serikali za Mitaa, SURA 290.
49.    MheshimiwaSpika napendekeza kufanya marekebisho ya Sheria ya Fedha za Serikali za Mitaa Sura 290 kama ifutavyo:-

(i)         Kuongeza kifungu cha 37A kwenye Sheria ya Serikali za Mitaa ili kumpa Mamlaka Waziri mwenye dhamana na Serikali za Mitaa Kuzitaka Serikali za Mitaa kutenga asilimia 10 ya fedha wanazokusanya kutoka kwenye vyanzo vyao vya mapato kwa ajili ya kuwezesha vikundi vya vijana na wanawake. Aidha asilimia 50 ya fedha hizo zitatengwa kwa ajili ya vikundi vya vijana na asilimia 50 kwa vikundi vya wanawake. Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais- TAMISEMI ataandaa Kanuni ambazo zitaweka utaratibu wa kusimamia utoaji wa fedha hizo kwa vikundi vya vijana na wanawake vilivyosajiliwa. Pia, fedha zitatolewa kwa kuwakopesha bila kutoza riba yoyote; na
(ii)       Kurekebisha kifungu cha 16(6) cha Sheria ya Fedha za Serikali za Mitaa Sura 290, ambacho kinatoa mwanya kwa Taasisi/Makampuni yanayolipa Ushuru wa Huduma kutolipa Ushuru wa Mazao. Mfano, Makampuni mengi yanayochakata zao la mkonge ili kuzalisha nyuzi za katani yanamiliki pia mashamba ya mkonge. Hivyo siyo busara kuwalipisha ushuru wa mazao na ushuru wa huduma. Hata hivyo, yapo makampuni yenye mashamba ya mkonge ambayo hayachakati mkonge, haya yanapaswa kulipa ushuru wa mazao badala ya ushuru wa huduma. Napendekeza kiongezwe kifungu cha 16(7) kwenye Sheria hiyo kuyataka Makampuni yanayozalisha mazao na hayachakati kwa ajili ya kuyaongezea thamani yawajibike kulipa Ushuru wa Mazao.

e)       Sheria ya Usimamizi wa Kodi, SURA 438
50.    Mheshimiwa Spika, napendekeza Kurekebisha Sheria ya Usimamizi wa Kodi SURA 438, ili kuanzisha utaratibu maalum wa kusamehe kodi (Tax Amnesty) ambao unalenga kusamehe malimbikizo ya nyuma ya riba na adhabu (Interest and Penalties) kwa kiwango cha asilimia 100. Msamaha huo utatolewa kwa kipindi cha miezi sita (6) kinachoanzia tarehe 1 Julai 2018 mpaka tarehe 31 Desemba 2018. Aidha kwa kufanya hivyo, Serikali inatarajia kukusanya malimbikizo ya madeni ya nyuma ya kodi (Principal Tax) pamoja na kuinua kiwango cha ulipaji kodi kwa hiyari kwa zaidi ya asilimia 10.

Hatua hiyo ya marekebisho ya Sheria ya Usimamizi wa Kodi inatarajiwa kuongeza mapato ya Serikali kwa kiasi cha shilingi milioni 500,000.





f)         Sheria ya Fedha za Serikali za Mitaa, SURA 290, Sheria ya Fedha za Umma, SURA 348 na Sheria ya Benki Kuu, SURA 197.

51.    Mheshimiwa Spika, napendekeza kurekebisha Sheria ya Fedha ya Serikali za Mitaa, Sura 290, Sheria ya Fedha za Umma Sura 348, na Sheria ya Benki Kuu, Sura 197 ili kuanzisha Akaunti Jumuifu ya Hazina (Treasury Single Account) ambapo akaunti hii itatumika kupokea fedha zote za Serikali na kufanya malipo yote ya Serikali. Msingi wa kuanzishwa kwa akaunti hii ni kutekeleza makubaliano ya nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki yaliyozitaka nchi wanachama kuanzisha akaunti jumuifu ili kuimarisha usimamizi wa fedha za Serikali. Uwepo wa akaunti hii pamoja na mambo mengine utarahisisha usimamizi wa fedha za Serikali kwa kupunguza idadi ya akaunti kwenye benki za biashara na Benki Kuu, kupunguza gharama za kibenki zinazolipwa hivi sasa na Serikali kufuatia huduma zinazotolewa kwa Serikali na Benki za Biashara, kupunguza nakisi kwenye mfuko Mkuu wa Serikali ambapo akaunti maalum zitajumuishwa kwenye ukokotoaji wa bakaa katika Mfuko Mkuu wa Serikali tofauti na utaratibu wa hivi sasa ambapo akaunti hizi hazijumuishwi katika ukokotoaji huo.

g)       Sheria ya Forodha ya Jumuiya ya Afrika Mashariki ya  mwaka 2004

52.    Mheshimiwa Spika, kikao cha Mawaziri wa Fedha wa Jumuiya ya Afrika Mashariki cha Maandalizi ya Bajeti (Pre-Budget consultations of Ministers of Finance) kilichofanyika tarehe 4 Mei, 2018 mjini Arusha, Tanzania kilipendekeza kufanya marekebisho ya Viwango vya Ushuru wa Pamoja wa Forodha (EAC – Common External Tariff “CET”) na Sheria ya Forodha ya Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC Customs Management Act, 2004) kwa Mwaka 2018/19. Mapendekezo hayo yanalenga kwa kiwango kikubwa katika kuchochea maendeleo ya viwanda ili kukuza ajira na ustawi wa jamii (Industrialization for Job Creation and Shared Prosperity).


53.    Mheshimiwa Spika, mapendekezo ya kufanya marekebisho kwenye Viwango vya Pamoja Ushuru wa Forodha ni kama ifuatavyo:-

(i)         Kuendelea kutoza Ushuru wa Forodha wa asilimia 10 badala ya asilimia 35 kwenye ngano (HS Code 1001.99.00 na HS Code 1001.99.90) kwa mwaka mmoja. Lengo la hatua hii ni kuendelea kutoa unafuu kwa viwanda vya wazalishaji wa bidhaa na vyakula vinavyotumia ngano na kuimarisha utulivu wa bei kwa bidhaa zinazozalishwa kwa kutumia ngano hiyo. Aidha, hatua hii inazingatia kwamba bado kiwango cha uzalishaji wa bidhaa hiyo muhimu ni kidogo katika nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki na hivyo hautoshelezi mahitaji. Ili kudhibiti uagizaji wa bidhaa hii, utaratibu wa “Duty Remission”utatumika ambapo viwanda vinavyotumia ngano ya aina hii katika uzalishaji ndivyo vitakavyohusika na kutumia kiwango hicho cha msamaha wa Ushuru wa Forodha;
(ii)       Kuendelea kutoza Ushuru wa Forodha kwa kiwango cha asilimia 0 badala ya asilimia 10 kwenye mashine za Kielektroniki zinazotumika kukusanya mapato ya Serikali (Electronic Fiscal Devices) zinazotambulika katika HS Code 8470.50.00 kwa mwaka mmoja. Hatua hii inatarajiwa kuendelea kutoa unafuu na kuhamasisha wafanyabiashara na walipa kodi kutumia mashine hizo katika kufanya mauzo na kuongeza ufanisi katika Usimamizi na Udhibiti wa kodi;
(iii)     Kutoza Ushuru wa Forodha wa asilimia 15  badala ya asilimia 25 kwenye karatasi zinazotambulika katika HS Codes 4804.11.00; 4804.21.00; 4804.31.00; na 4804.41.00. Utaratibu wa “Duty Remission” utatumika ambapo wazalishaji wanaotumia karatasi hizo katika kutengeneza madaftari na vitabu ndio watakaofaidika. Lengo la hatua hii ni kupunguza gharama kwa wazalishaji hao. Ni matarajio ya Serikali kwamba wazalishaji watauza bidhaa hizi kwa bei nafuu na hivyo kuwezesha watumiaji, hususan wanafunzi, kuzipata kwa gharama nafuu;
(iv)     Kutoza Ushuru wa forodha wa asilimia 0 badala ya asilimia 10 kwa mwaka mmoja kwenye karatasi zinazoingizwa kutoka nje kwa ajili ya utengenezaji wa gypsum board (Gypsum paper for manufacturing of gypsum board) zinazotambulika katika HS Code 4805.92.00;
(v)       Kutoza Ushuru wa forodha wa asilimia 35 badala ya asilimia 100 kwenye sukari ya matumizi ya kawaida (consumption sugar) inayoagizwa kutoka nje ya nchi kwa vibali maalum kwa lengo la kuziba pengo (gap sugar) la uzalishaji hapa nchini. Hivi sasa sukari hiyo inatozwa Ushuru wa Forodha wa asilimia 25 badala ya asilimia 100;
(vi)     Kuendelea kutoza Ushuru wa Forodha wa asilimia 10 badala ya asilimia 0 kwenye "Gypsum Powder" inayotambuliwa kwa HS Code 2520.20.00 kwa mwaka mmoja. Marekebisho haya yanalenga katika kulinda viwanda vinavyozalisha bidhaa hiyo hapa nchini na kuhamasisha wawekezaji watumie "gypsum"inayopatikana hapa nchini kuzalisha "gypsum"powder. Aidha, hatua hii inatarajiwa kuongeza ajira na mapato ya Serikali;
(vii)   Kutoza Ushuru wa Forodha wa asilimia 10 badala ya asilimia 25 kwa mwaka mmoja kwenye bidhaa ijulikanayo kama "Self-adhesive label" (HS Code 4821.10.90) ambayo hutumika kama alama ya kutambulisha aina ya bidhaa kwa watengenezaji wa dawa za meno. Hatua hii inalenga katika kupunguza gharama ya uzalishaji kwenye viwanda vya dawa za meno kwa kuwa self-adhesive labels hazizalishwi hapa nchini;
(viii)Kutoza Ushuru wa Forodha wa asilimia 0 badala ya asilimia 25 kwenye bidhaa ijulikanayo kama “Printed Alluminium Barrier Laminates"(ABL) HS Code 3920.10.90 kwa mwaka mmoja. Aidha utaratibu wa “duty remission” utatumika ambapo hatua hii itawahusu wenye viwanda vinavyoagiza bidhaa hiyo kwa matumizi ya kiwandani. Lengo la hatua hii ni kupunguza gharama ya uzalishaji kwa viwanda vya dawa za meno. Aidha, ina lengo la kuvilinda viwanda hivi kutokana na ushindani na ajira;
(ix)     Kutoza Ushuru wa Forodha wa asilimia 25 badala ya asilimia 0 kwa mwaka mmoja kwenye mafuta ghafi ya kula ya mawese (Crude Palm Oil) yanayotambulika katika HS Code 1511.10.00 kwa mwaka mmoja. Hatua hii inalenga katika kulinda na kuhamasisha uzalishaji wa mbegu za mafuta na mafuta ya kula hapa nchini kwa kuzingatia kuwa nchi yetu ina fursa kubwa ya kuongeza uzalishaji wa bidhaa hiyo.    Aidha, lengo ni kuhamasisha uwekezaji katika viwanda vya kuchakata mafuta ghafi kwa kutumia mbegu zinazozalishwa hapa nchini. Pia inatarajiwa kwamba uzalishaji wa mbegu utaongezeka na kuongeza ajira viwandani na mashambani pamoja na kuongeza kipato cha wakulima;
(x)       Kutoza Ushuru wa Forodha wa asilimia 25 badala ya asilimia 0 au asilimia 10 kwa mwaka mmoja kwenye mafuta ghafi ya kula (mfano alizeti, mawese, soya, mzaituni, nazi, karanga, mahindi n.k). Lengo la hatua hii ni kuhamasisha uzalishaji wa mbegu na mafuta ya kula hapa nchini kwa kutumia mbegu zinazozalishwa nchini. Aidha, inatarajiwa kwamba hatua hii italinda viwanda na ajira katika sekta ndogo ya mafuta ya kula, na kuongeza mapato ya serikali na wakulima;
(xi)     Kutoza Ushuru wa Forodha wa asilimia 35 badala ya asilimia 25 kwa mwaka mmoja kwenye mafuta ya kula yaliyochakatwa kwa kiwango cha kati na cha mwisho (semi-refined, refined/double refined oil) mfano alizeti, mawese, soya, mzaituni, nazi, karanga, mahindi n.k. Ongezeko hilo la Ushuru wa Forodha linatarajiwa kulinda uzalishaji wa mafuta ya kula na kuhamasisha uchakataji wa mbegu za mafuta zinazozalishwa nchini badala ya kuagiza mafuta ya kula kutoka nje ya nchi. Aidha, hatua hii inatarajiwa kupunguza fedha za kigeni zinazotumika kuagiza mafuta kutoka nje ya nchi;
(xii)   Kutoza Ushuru wa Forodha wa asilimia 25 au dola za Kimarekani 350 kwa kila tani moja ya ujazo (Metric ton) kwa mwaka mmoja kutegemea kiwango kipi ni kikubwa kwenye bidhaa za chuma za misumari zinazotambulika katika HS Code 7317.00.00 (nails, tacks, drawing pins, corrugated nails, staples other than those of heading 83.05). Hatua ya kuweka kiwango hicho cha Ushuru wa Forodha inalenga katika kulinda viwanda vya bidhaa hizo hapa nchini kutokana na uingizaji wa bidhaa kama hizo kutoka nje ya nchi;
(xiii)  Kutoza Ushuru wa Forodha wa asilimia 25 au dola za kimarekani 1.35 kwa kilo moja ya viberiti (safety matches) vinavyotambuliwa kwenye HS Code 3605.00.00 kutegemea kiwango kipi ni kikubwa. Hatua hii inazingatia kuwa nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki zina uwezo wa kuzalisha viberiti na kutosheleza mahitaji katika soko hivyo kuwepo na umuhimu wa kulinda viwanda vinavyozalisha bidhaa hiyo;
(xiv)Nchi za Jumuiya zimekubaliana kupunguza Ushuru wa Forodha kutoka asilimia 10 hadi asilimia 0 kwenye malighafi ya kutengeneza bidhaa za rangi za kupaka nyumba ijulikanayo kama “polyvinyl Alcohol” (HS Code 3905.30.00). Lengo la hatua hii ni kuhamasisha uwekezaji katika uzalishaji wa bidhaa hizo;
(xv)   Kutoza Ushuru wa Forodha wa asilimia 0 kwa utaratibu wa “duty remission” kwenye malighafi (inputs) zinazotumika katika kutengeneza dawa za kuua wadudu (pesticides, fungicides, insecticides na acaricides). Hatua hii itahusisha viwanda vinavyotumia malighafi hizo kutengeneza dawa za kuua wadudu. Aidha, viwanda vitakavyoagiza malighafi hizo vitatakiwa kupata kibali cha Wizara ya Kilimo. Lengo la hatua hii ni kupunguza gharama za uzalishaji na kuhamasisha uwekezaji kwenye viwanda hivyo;
(xvi)Kutoza Ushuru wa Forodha wa asilimia 0 badala ya asilimia 10 kwa utaratibu wa duty remission kwenye bidhaa ya kutengeneza sabuni ijulikanayo kama “RBD Palm Stearin” inayotambulika katika HS Code 1511.90.40. Hatua hii inahusisha viwanda vinavyotumia bidhaa hiyo katika kutengeneza sabuni. Aidha, hatua ya kupunguza ushuru huo imezingatia kwamba Serikali imeongeza ushuru wa forodha katika mafuta ghafi ya mawese;
(xvii)Kutoza Ushuru wa Forodha wa asilimia 35 badala ya asilimia 25 kwenye viazi (potatoes fresh or chilled, other than seeds) vinavyotambulika katika HS Code 0701.90.00. Lengo la hatua hii ni kulinda uzalishaji wa viazi hapa nchini;
(xviii)    Kutoza Ushuru wa Forodha wa asilimia 35 badala ya asilimia 25 kwenye Chingamu (Chewing Gum) zinazotambulilka katika HS Code 1704.10.00. Lengo la hatua hii ni kulinda viwanda vya ndani kwa kuwa kuna uwezo wa kuzalisha chewing gum katika nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki;
(xix)Kutoza Ushuru wa Forodha wa asilimia 35 badala ya asilimia 25 kwenye peremende HS Code 1704.90.00. Hatua hii inachukuliwa kwa lengo la kulinda viwanda vya ndani na ajira;
(xx)   Kutoza Ushuru wa Forodha wa asilimia 35 badala ya asilimia 25 kwenye Chokoleti (chocolates) HS Code 18.06. Nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki zinazalisha bidhaa hizi na zina uwezo wa kutosheleza mahitaji ya soko;
(xxi)Kutoza Ushuru wa Forodha wa asilimia 35 badala ya asilimia 25 kwenye Biskuti (Biscuits) zinazotambullika kwa HS Code 1905. Hatua hii inazingatia kuwa nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki zina uwezo wa kuzalisha bidhaa hiyo na kutosheleza mahitaji ya soko;
(xxii)    Kutoza Ushuru wa Forodha wa asilimia 35 badala ya asilimia 25 kwenye nyanya zilizosindikwa (tomato sauce) zinazotambulika katika HS Code 2103.20.00. Lengo la hatua hii ni kulinda uzalishaji wa bidhaa hiyo katika viwanda vya ndani na mashambani. Aidha, imezingatia kwamba nchi yetu inazalisha nyanya za kukidhi mahitaji na pia kuna umuhimu wa kusindika nyanya hizo hapa nchini ili kuongeza thamani na kuongeza ajira katika kilimo cha nyanya;
(xxiii)  Kutoza Ushuru wa Forodha wa asilimia 60 badala ya asilimia 25 kwenye maji (mineral water) yanayotambulika katika HS Code 2201.10.00. Hatua hii ni muhimu katika kuhamasisha uzalishaji na kulinda viwanda vya hapa nchini vinavyozalisha bidhaa hiyo;
(xxiv)  Kutoza Ushuru wa Forodha wa asilimia 35 badala ya asilimia 25 kwenye nyama (meat and edible meat offal in chapter 12) kwa mwaka mmoja. Lengo la hatua hii ni kuhamasisha uanzishaji wa viwanda vya uchakataji wa nyama hapa nchini na hivyo kuongeza thamani yake. Aidha, itaongeza fursa za ajira na kipato katika sekta ya ufugaji na viwandani; na
(xxv)Kutoza Ushuru wa Forodha wa asilimia 35 badala ya asilimia 25 kwenye Soseji (sausages) na bidhaa za aina hiyo (HS Code 1601.00.00). Hatua hii ina lengo la kulinda na kuhamasisha Viwanda vinavyozalisha bidhaa hiyo katika Nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki.

54.    Mheshimiwa Spika, Mawaziri wa Fedha wa Nchi Wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki walifanya pia marekebisho kwenye Sheria ya Forodha ya Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC Customs Management Act, 2004) kama ifuatavyo:-

(i)         Kufanya marekebisho katika Jedwali la Tano la Sheria ya Forodha ya Jumuiya ya Afrika Mashariki linalotoa msamaha wa Ushuru wa Forodha kwenye magari yanayotumika kwenye mashindano ya mbio za magari (rally cars) na kuingiza pikipiki (motorcycles) ili nazo ziweze kupata msamaha huo. Aidha, magari na pikipiki husika hutengenezwa mahsusi kwa ajili ya mashindano hayo. Hatua hiyo inatarajiwa kuhamasisha mashindano hayo na kukuza sekta ya utalii;
(ii)       Kufanya marekebisho kwenye Jedwali la Tano la Sheria ya Forodha ya Jumuiya ya Afrika Mashariki ili kutoa msamaha kwa boti inayotumika mahsusi kwa ajili ya kutoa huduma kwa wagonjwa kwenye maji (Motor Boat Ambulance) inayotambulika katika HS Code 8903.99.10 kama vile yanavyosamehewa magari ya kutoa huduma kwa wagonjwa (Motor Vehicle Ambulance). Hatua hii ina lengo la kupunguza gharama na kuwezesha utoaji wa huduma za matibabu katika usafiri wa majini; na
(iii)     Kufanya Marekebisho katika Jedwali la Tano la Sheria ya Forodha ya Jumuiya ya Afrika Mashariki ili kutoa msamaha wa Ushuru wa Forodha kwenye magari ya kubebea watalii (Motor vehicle for Transport of Tourists). Magari haya yanajumuisha magari ya aina mbalimbali ambayo yametengenezwa mahsusi kwa ajili ya kubebea watalii (Motor sightseeing buses, overland trucks). Lengo la kutoa msamaha huo ni kuhamasisha uwekezaji katika sekta ya utalii, kuboresha huduma ya usafiri kwa watalii na kuongeza ajira na mapato ya Serikali.

55.    Mheshimiwa Spika, Mawaziri wa Fedha wa Jumuiya ya Afrika Mashariki tumekubaliana kupunguza Viwango vya Ushuru wa Forodha (duty remission) kwenye malighafi na vipuri vinavyohitajika katika kutengeneza nguo na viatu katika Jumuiya ya Afrika Mashariki. Aidha, tayari nchi hizi zimewasilisha orodha ya malighafi na vifaa vitakavyopunguziwa Ushuru wa Forodha. Uamuzi huo utaanza kutekelezwa mwaka 2018/19.

Hatua hizi za Ushuru wa Forodha kwa pamoja zinatarajiwa kupunguza mapato ya Serikali kwa kiasi cha shilingi milioni 1,630.2

h)      Sheria zinazosimamia Bodi za Mazao.

56.    Mheshimiwa Spika, napendekeza kufanya marekebisho kwenye sheria zote zinazosimamia Bodi za mazao mbalimbali kwa lengo la kuwezesha ushuru wote unaokusanywa na bodi hizo kuingizwa kwenye Mfuko Mkuu wa Serikali. Lengo la hatua hii ni kuhakikisha kwamba mapato yatokanayo na ushuru unaotozwa kwenye mazao mbalimbali yanasimamiwa ipasavyo na kutumika kwa ajili ya shughuli zilizokusudiwa. Aidha,  shughuli za kuendeleza mazao pamoja na gharama za uendeshaji wa Bodi zitagharamiwa kupitia Bajeti ya Serikali.


i)         Sheria ya Michezo ya kubahatisha, SURA 41

57.    Mheshimiwa Spika, napendekeza kufanya mabadiliko ya kiwango cha kodi katika michezo ya kubahatisha ya ubashiri wa matokeo ya michezo (sports betting) kutoka asilimia 6 ya mauzo ghafi hadi asilimia 10. Lengo ni kuongeza mapato ya Serikali kutoka kwenye sekta ndogo ya michezo hiyo ya kubahatisha.

58.    Mheshimiwa Spika, napendekeza kufanya marekebisho ya kiwango cha kodi kinachotozwa kwenye mashine za michezo ya kubahatisha (slot machines) kutoka shilingi 32,000 hadi shilingi 100,000 kwa kila mashine kwa mwezi. Lengo ni kuongeza mapato ya Serikali.

59.    Mheshimiwa Spika, napendekeza kuongeza kiwango cha kodi kinachotozwa kwenye michezo ya kubahatisha (Casino) kutoka asilimia 15 hadi asilimia 18 ya mapato halisi ambayo hupatikana baada ya kutoa zawadi (Gross Gaming Revenue -GGR). Lengo ni kuongeza mapato ya Serikali kwa sababu kiwango cha asilimia 15 kimedumu kwa muda mrefu kuanzia mwaka 2012.

60.    Mheshimiwa Spika, napendekeza kufanya marekebisho ya kiwango cha kodi kinachotozwa kwenye mashine arubaini (Forty Machines Site) za michezo ya kubahatisha kutoka asilimia 15 hadi asilimia 20 ya mapato halisi ambayo hupatikana baada ya kutoa zawadi (Gross Gaming Revenue -GGR). Lengo ni kuongeza mapato ya Serikali.

Hatua hizi za marekebisho ya michezo ya kubahatisha zinatarajiwa kuongeza mapato ya Serikali kwa kiasi cha shilingi milioni 21,198.8.

j)         Marekebisho madogo madogo katika baadhi ya Sheria za Kodi na   Sheria nyingine mbalimbali.

61.    Mheshimiwa Spika, napendekeza kufanya marekebisho mengine madogo madogo yasiyo ya kisera katika sheria mbalimbali za kodi pamoja na sheria nyingine mbalimbali ili ziwe sanjari na azma ya kurahisisha utekelezaji wake. Marekebisho hayo yataainishwa katika Muswada wa Sheria ya Fedha ya mwaka 2018 na Matangazo ya Serikali (Government Notices).


k)      Marekebisho ya Ada na Tozo mbalimbali zinazotozwa na Wizara, Mikoa na Idara zinazojitegemea.

62.    Mheshimiwa Spika, napendekeza kufanya marekebisho ya viwango vya ada na tozo mbalimbali zinazotozwa na Wizara, Mikoa na Idara zinazojitegemea ili kuvihuisha kulingana na hali halisi ya ukuaji wa uchumi. Aidha, marekebisho hayo yataainishwa katika Muswada wa Sheria ya Fedha ya mwaka 2018 na Matangazo ya Serikali (Government Notices). Marekebisho hayo yatajumuisha:-

(i)         Kusamehe Kodi ya Ardhi kwa Taasisi za Serikali kwa sababu taasisi hizi ni za umma hazitengenezi faida. Aidha, marekebisho mengine ya ada na tozo mbalimbali yanayohusu sekta ya ardhi yalitangazwa na Waziri mwenye dhamana ya ardhi kwenye hotuba yake;
(ii)       Kufuta na kupunguza baadhi ya viwango vya tozo na ada zinazotozwa kwenye sekta ya uzalishaji wa Chumvi. Hatua hii imetokana na kuwepo kwa utitiri wa tozo na ada zinazotozwa kwenye Madini ya Chumvi hali ambayo inasababisha gharama za uzalishaji kuwa juu na kuwakatisha tamaa wazalishaji kuendelea na uzalishaji wa chumvi. Hivyo napendekeza kufanya marekebisho ya tozo na ada kwenye sekta ya uzalishaji chumvi kama ifuatavyo:-
a)Kufuta ushuru wa mazao ya chumvi unaotozwa na Halmashauri;
b)Kufuta ada ya ukaguzi wa madini ya chumvi (Inspection and Clearance fee) inayotozwa kwa kiwango cha asilimia moja (1%) ya thamani ya madini;
c)  Kufuta ushuru wa Mikoko (Mangrove Levy) unaotozwa kwenye maeneo ya uzalishaji wa chumvi kwa kiwango cha shillingi 100,000 kwa eka moja kwa mwaka;
d)Kufuta ada ya kupitia andiko la mradi kwenye sekta ya uzalishaji chumvi inayotozwa na Baraza la Taifa la Usimamizi wa Mazingira;
e)  Kufuta ada ya usajili wa Jangwa la Chumvi (Solar Salt Panel);
f)   Kufuta ada ya Usimamizi kwenye eneo la Chumvi (Supervision fee)  inayotozwa na Wakala wa Misitu Tanzania;
g)  Kufuta ada ya usajili wa mradi wa uzalishaji chumvi inayotozwa na Baraza la Taifa la Usimamizi wa Mazingira;
h)Kufuta ada ya Ukaguzi wa Mazingira (Environmental Impact Assesment) inayotozwa na Baraza la Taifa la Usimamizi wa Mazingira kwenye sekta ya uzalishaji chumvi;
i)    Kupunguza ada ya gharama za ukaguzi wa usalama mahala pa kazi inayotozwa kwenye sekta ya uzalishaji chumvi kutoka shilingi millioni 2 hadi shilingi millioni 1 kwa mwaka; na
j)    Kupunguza ada ya kibali cha kusafirisha madini ya chumvi nje ya nchi kutoka Dola za Kimarekani 100 hadi shilingi 20,000 kwa mwaka.
(iii)     Napendekeza kufanya marekebisho ya ada na tozo zinazotozwa na Mamlaka ya Afya na Usalama (OSHA) mahali pa kazi kama ifuatavyo:-
a)         Kufuta ada inayotozwa kwenye fomu ya usajili sehemu za kazi;
b)         Kufuta tozo ya usajili sehemu za kazi;
c)          Kufuta faini zinazohusiana na vifaa vya kuzimia moto inayotozwa kwa kiwango cha shilingi 500,000;
d)         Kufuta Leseni ya kukidhi matakwa ya Sheria ya afya na usalama; na
e)          Kufuta tozo ya ushauri wa kitaalam ya usalama wa afya.

63.    Mheshimiwa Spika, Serikali itaendelea kufanya uchambuzi na tathmini ya tozo na ada zinazotozwa na mashirika, taasisi na wakala mbalimbali ili kuendelea kuweka mazingira bora ya kufanya biashara na kuwekeza na kuondoa kero kwa wananchi. Hii itajumuisha kupitia upya na kuvisawazisha viwango vya tozo na ada hizo na pia kuondoa tozo na ada za usumbufu.

l)         Tarehe ya Kuanza Kutekeleza Hatua Mpya za Kodi
64.    Mheshimiwa Spika, hatua hizi za kodi zinazopendekezwa zitaanza kutekelezwa tarehe 1 Julai, 2018, isipokuwa pale ilipoelezwa vinginevyo.



V.      SURA YA  BAJETI KWA MWAKA 2018/19
65.    Mheshimiwa Spika, kwa kuzingatia shabaha na sera za bajeti kwa mwaka 2018/19, Sura ya Bajeti inaonesha kuwa jumla ya shilingi trilioni 32.48 zinatarajiwa kukusanywa na kutumika katika kipindi hicho. Jumla ya mapato ya ndani (ikijumuisha mapato ya Halmashauri) yanatarajiwa kuwa shilingi trilioni 20.89, sawa na asilimia 64.3 ya bajeti yote. Kati ya mapato hayo, Serikali inalenga kukusanya mapato ya kodi ya jumla ya shilingi trilioni 18.0 sawa na asilimia 13.6 ya Pato la Taifa. Aidha, mapato yasiyo ya kodi yanakadiriwa kuwa shilingi trilioni 2.16 na mapato kutoka vyanzo vya Halmashauri shilingi bilioni 735.6.

66.    Mheshimiwa Spika, Washirika wa Maendeleo wanatarajiwa kuchangia shilingi trilioni 2.68 ambayo ni asilimia 8.2 ya bajeti yote. Misaada na mikopo hii inajumuisha misaada na mikopo nafuu ya miradi ya maendeleo shilingi trilioni 2.0; mifuko ya pamoja ya kisekta shilingi bilioni 125.9; na misaada na mikopo nafuu ya kibajeti (GBS) shilingi bilioni 545.8.

67.    Mheshimiwa Spika, Serikali inatarajia kukopa shilingi trilioni 8.90 kutoka soko la ndani na nje kwa masharti ya kibiashara. Mikopo ya ndani inatarajiwa kuwa shilingi trilioni 5.79, ambapo shilingi trilioni 4.6 ni kwa ajili ya kulipia dhamana za Serikali zinazoiva (rollover) na shilingi trilioni 1.19 ni mikopo mipya kwa ajili ya kugharamia miradi ya maendeleo. Ili kuongeza kasi katika ujenzi wa miundombinu, Serikali inatarajia kukopa shilingi trilioni 3.11 kutoka soko la nje.

68.    Mheshimiwa Spika, katika mwaka 2018/19, Serikali inapanga kutumia jumla ya shilingi trilioni 32.48. Kati ya fedha hizo, shilingi bilioni 20.47 zimetengwa kwa ajili ya matumizi ya kawaida, ikijumuisha shilingi trilioni 7.41 za mishahara na shilingi trilioni 10.00 kwa ajili ya kulipia deni la Serikali, michango ya Serikali kwenye Mifuko ya Hifadhi ya Jamii na huduma nyinginezo. Aidha, matumizi ya maendeleo yatakuwa shilingi trilioni 12.01 sawa na asilimia 37 ya bajeti yote, ambapo shilingi trilioni 9.88 ni fedha za ndani na shilingi trilioni 2.13 ni fedha za nje. Kiwango hiki cha bajeti ya maendeleo kimezingatia matakwa ya Mpango wa Maendeleo wa Miaka Mitano 2016/17 – 2020/21 wa kutenga bajeti ya maendeleo kati ya asilimia 30 na 40 ya bajeti yote.

69.    Mheshimiwa Spika, kwa kuzingatia mfumo wa bajeti kama nilivyoeleza, sura ya bajeti kwa mwaka 2018/19 ni kama inavyooneshwa katika Jedwali A.
Jedwali A: Mfumo wa Bajeti ya Mwaka 2018/19
Chanzo: Wizara ya Fedha na Mipango


VI.      HITIMISHO
70.    Mheshimiwa Spika, kama nilivyotangulia kusema hapo awali, dhima ya bajeti ya mwaka 2018/19 ni kuendelea “kujenga uchumi wa viwanda utakaochochea ajira na ustawi endelevu wa jamii”. Mageuzi haya ya uchumi wa viwanda yatajengwa kupitia ushiriki wetu katika shughuli za kiuchumi, ubia na kuunganisha juhudi zetu pamoja. Ili kufikia malengo tunayoyakusudia, maamuzi magumu ni lazima yafanyike katika kuelekeza rasilimali chache tulizonazo katika maeneo ya kimkakati. Mabadiliko yoyote ni vigumu kuyakubali na mara nyingi mabadiliko hupingwa. Naomba Waheshimiwa Wabunge na wananchi kwa ujumla tuunganishe nguvu zetu, vipaji vya wananchi wetu na biashara zetu ili kufikia malengo tunayoyakusudia. Hivyo, tunahitaji uzalendo na nidhamu ya kazi ya hali ya juu tukikusudia kuondoa umasikini, kuongeza ajira na kuwa na uchumi jumuishi.

71.    Mheshimiwa Spika, ili kufikia malengo hayo, Serikali itaendelea kuchukua hatua zaidi kuongeza uzalishaji katika sekta za viwanda na kilimo na ukusanyaji wa mapato ya ndani yatakayowezesha ugharamiaji wa miradi ya maendeleo na matumizi ya kawaida na hivyo kupunguza utegemezi. Hatua hizo ni pamoja na: kuvutia uwekezaji; kuelekeza rasilimali kwenye maeneo machache yenye tija; kusimamia utekelezaji wa sheria za kodi; kurasimisha sekta isiyo rasmi ikiwemo usajili wa wamiliki wa ardhi na majengo katika mfumo wa walipa kodi; na kuhimiza matumizi ya mifumo ya kielektroniki katika miamala mbalimbali ikiwemo matumizi ya EFD na kadi za kielectroniki za benki (Debt/credit cards) katika maeneo yanayotoa huduma kama vile katika maduka makubwa, hoteli na vituo vya mafuta. Hivyo, napenda kuwahimiza Watanzania tuwajibike kulipa kodi na kuhakikisha tunatoa na kudai risiti  kulingana na muamala uliofanyika. Aidha, Serikali inawashukuru kwa dhati wananchi wote ambao wameonesha uzalendo kwa kuendelea kulipa kodi kwa hiari.

72.    Mheshimiwa Spika, kipaumbele kikuu cha Serikali ni kujenga uchumi wa viwanda vinavyotumia malighafi zinazopatikana nchini hususan zinazotokana na kilimo, mifugo na uvuvi ili kupanua fursa za ajira, kuboresha upatikanaji na ubora wa huduma za jamii (maji, afya, elimu) na kupunguza umaskini. Aidha, Serikali itaendeleza mapambano dhidi ya rushwa, kuimarisha ulinzi wa rasilimali za umma na kudhibiti matumizi ya fedha za umma. Serikali pia itaongeza msukumo katika kuboresha mazingira ya biashara na uwekezaji kwa kutekeleza Mpango wa Kuboresha Mfumo wa Udhibiti wa Biashara (Blueprint for Regulatory Reforms to Improve the Business Environment). Mpango huu, pamoja na mambo mengine unakusudia kuhuisha na kurahisisha taratibu za kulipa kodi, tozo na ada mbalimbali.

73.    Mheshimiwa Spika, Serikali ya awamu ya tano inalenga kujenga utamaduni  na nidhamu ya kukubali maoteo halisia ya ukusanyaji wa mapato ambayo yanapaswa kuwa  ukomo wa  matumizi (expenditure ceiling) badala ya utarabu uliozoeleka wa kuanza kupanga au kuorodhesha mahitaji kwanza. Hivyo, Serikali itajielekeza katika utekelezaji wa miradi michache ya kimkakati kwa namna ambayo itashirikisha sekta zote zinazotegemeana na kuhakikisha kuwa miradi hiyo inakamilika kabla ya kuanza miradi mipya.

74.    Mheshimiwa Spika, mimi ni mpenzi sana wa kujisomea kuhusu maisha na sifa za viongozi mashuhuri, viongozi bora na wa kipekee wa nchi mbalimbali waliofanikiwa kuongoza mabadiliko makubwa ya kijamii, kisiasa na kiuchumi katika nchi zao kama vile Deng Tsiaoping –Jamhuri ya Watu wa China; Dkt. Mahithir Mohamed – Malaysia; Lee Kuan Yew – Singapore; Park Chung Hee – Korea, Nelson Mandela –Afrika ya Kusini, Baba wa Taifa Mwl. Julius Nyerere, Quett Masire – Botswana nk. Nilichojifunza na nilieleza katika hotuba ya bajeti kuu ya Serikali  mwaka jana kuwa viongozi wa aina hiyo wana sifa muhimu zifuatazo:
(i)         Dira au maono dhahiri kuhusu maendeleo ya nchi zao;
(ii)       Hawasiti kutekeleza dira hizo kwa dhamira kubwa tena bila kusita au kubadili msimamo;
(iii)     Ni jasiri, shupavu na wenye kuthubutu kutekeleza jambo wanaloliamini bila kigugumizi;
(iv)     Wana kipaji cha kujali maumivu ya wanyonge;
(v)       Ni waadilifu, wanachukia rushwa na ufisadi na ni wenye nidhamu ya kazi ya hali ya juu;
(vi)     Wanaongoza kwa vitendo; na
(vii)   Huvumilia magumu ili kuiletea nchi mabadiliko chanya.

75.    Mheshimiwa Spika, ninapenda niwaambie tena Watanzania kwamba Mwenyezi Mungu ametutunukia kiongozi Mkuu wa nchi Mheshimiwa Dkt. John Pombe Joseph Magufuli mwenye sifa hizo zote nilizotaja. Nilieleza  mwanzoni mambo machache ambayo amethubutu kutenda kwa kipindi kifupi kuthibitisha sifa hizo. Rai yangu kwa Watanzania wenzangu ni kuwa tutumie fursa hii adimu kwa kufanya kazi kama njia bora ya kumuunga mkono Rais wetu katika jitihada zake za kuijenga Tanzania mpya, Tanzania ya Viwanda. Jambo hili ni muhimu kwa sababu kama Baba wa Taifa Mwalimu Julius Nyerere alivyotabiri, katika safari ya maendeleo – ya kuelekea kujenga uchumi wa viwanda – kiongozi wetu atakumbana na vikwazo na kelele nyingi za kuzomea kutoka kwa wale wasiotutakia mema ili kutukatisha tamaa tusifikie malengo. Hivyo, Watanzania wote tunao wajibu wa kumtia nguvu Rais wetu ili asirudi nyuma katika safari aliyoianza na aweze kutuvusha kuifikia Tanzania ya viwanda. Niruhusu nimalizie rai yangu kwa nukuu ya mazungumzo ya Mwalimu Nyerere kwa “TANU study Group” tarehe 13 Juni, 1967:

Maendeleo na kazini kitu kile kile, hakuna namna nyingine sisi ya kuendelea, hatukupewa namna nyingine sisi ya kuendelea….. Huwezi kutenganisha vitu viwili hivi, kuendelea na kazi, kwani kazi ndiyo shughuli ya …..  kuondoa matatizo yanayomzuia binadamu hali yake kukamilika…. Hakuna njia nyingine lazima kufanya kazi…… na kila unavyozidi kufanya kazi kwa akili zaidi ndivyo mnavyozidi kwenda, ndivyo mnavyozidi kuendelea,….. Kazi ndio utu …kazi ndio maendeleo…kazi ndio maisha, ni uhai, kazi ndio civilization, ndio uungwana, ndio kula vizuri, ndio kuvaa vizuri, ndio kuishi katika nyumba nzuri,…. ndio kushinda matatizo yote tuliyo nayo duniani – namna ya kuyashinda ni kazi….”[1]

76.    Mheshimiwa Spika, ninapoelekea mwisho wa hotuba hii, napenda kuwashukuru Washirika wa Maendeleo kwa misaada na mikopo wanayoendelea kutupatia katika kutekeleza miradi na programu mbalimbali za maendeleo nchini.  Wahisani hao wanatarajiwa kuchangia jumla ya shilingi bilioni 2,676.6 katika bajeti ya mwaka 2018/19 kama ifuatavyo: Benki ya Dunia/IDA shilingi bilioni 863.13; Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) shilingi bilioni 358.63; Global Fund shilingi bilioni 313.90; Sweden shilingi bilioni 179.80; Jumuiya ya Umoja wa Ulaya shilingi bilioni 158.40; India shilingi bilioni 104.57; Ujerumani (Kfw & GIZ) shilingi bilioni 81.31; Japan/JICA shilingi bilioni 76.96; Uingereza/DFID shilingi bilioni 71.21; Denmark shilingi bilioni 69.57; French/AFD shilingi bilioni 61.06; Canada shilingi bilioni 48.84; BADEA shilingi bilioni 40.01; Korea ya Kusini/EDCH shilingi bilioni 39.05; UNICEF shilingi bilioni 36.53; Finland shilingi bilioni 28.08; IFAD shilingi bilioni 26.82; Italy shilingi bilioni 22.05; Norway shilingi bilioni 20.04; Benki ya Uwekezaji ya Ulaya shilingi bilioni 17.88; Uswisi shilingi bilioni 15.74; UNDP shilingi bilioni 12.34 ; Ubelgiji shilingi bilioni 11.08; Saudi Arabia/Saud Fund shilingi bilioni 4.81; USAID shilingi bilioni 4.20; OPEC/OFID shilingi bilioni 2.75; na UNFPA shilingi bilioni 2.56. Ni matarajio yetu kuwa fedha zilizoahidiwa na marafiki zetu hawa zitatolewa kama nilivyozisoma na kwa wakati muafaka. Sisi kama Serikali tunaahidi kuwa fedha watakazotupatia zitatumika kama ilivyokusudiwa.

77.    Mheshimiwa Spika, ninakiri kuwa bajeti niliyowasilisha isingekuwa hivi ilivyo bila kupata michango mizuri ya kuboresha kutoka kwa Waheshimiwa Mawaziri, Naibu Mawaziri, Makatibu Wakuu, Naibu Makatibu Wakuu, Sekretariaeti ya Baraza la Mawaziri na wataalam wa wizara zote na taasisi za Serikali. Ninatoa shukrani kwa kila mmoja wenu kwa michango mliyotoa katika mchakato mzima wa maandalizi ya bajeti hii.

78.    Mheshimiwa Spika, napenda pia kuwashukuru viongozi wenzangu wa Wizara ya Fedha na Mipango, nikianza na Mheshimiwa Dkt. Ashatu K. Kijaji, Mbunge wa Kondoa na Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, pia Bwana Doto M. James, Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango na Mlipaji Mkuu wa Serikali, na Naibu Makatibu Wakuu, Bibi Amina Kh. Shaaban, Dkt. Khatibu M. Kazungu, na Bibi Susan B. Mkapa. Wote hawa kwa pamoja wamenipatia ushirikiano na msaada wa hali ya juu katika kusimamia utekelezaji wa majukumu ya Wizara na wameratibu vizuri maandalizi ya bajeti hii. Aidha, ninampongeza Profesa Florens Dominick Makinyika Luoga kwa kuteuliwa na Rais kuwa Gavana mpya wa Benki Kuu ya Tanzania na kwa kusimamia vema majukumu makubwa ya mhimili huo wa sekta ya fedha akisaidiwa na Naibu Gavana watatu, Wakurugenzi na watumishi wote wa Benki Kuu ya Tanzania. Vivyo hivyo, napenda kutambua kazi nzuri ya viongozi na watumishi wa Mamlaka ya Mapato Tanzania katika kukusanya mapato ya Serikali wakiongozwa na Bw. Charles E. Kichere, Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania, Profesa Musa Assad, Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali na Dkt. Albina Chuwa, Mkurugenzi Mkuu wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu. Aidha, nampongeza Bwana Athumani Selemani Mbuttuka aliyeteuliwa na Mheshimiwa Rais hivi karibuni kuwa Msajili wa Hazina (Treasury Registrar).

79.    Mheshimiwa Spika, vile vile, ninawashukuru Wakuu wengine wa taasisi zilizo chini ya Wizara ya Fedha na Mipango ikijumuisha Mabenki (TADB, TIB-DFI, TIB-CBL,TPB Bank); Mifuko ya hifadhi ya jamii (PSPF, GEPF, PPF); Rufani za kodi (TRAB, TRAT); Huduma za bima (TIRA,NIC); Mitaji na dhamana (CMSA, TCEM, DSE); Dhamana za uwekezaji (UTT-MFI, UTT-AMIS,UTT-PID); Bodi ya michezo ya kubahatisha; Taasisi za mafunzo (IFM, IRDP, IAA, TIA, EASTC); na Mfuko wa huduma ndogo za fedha (SELF Microfinance Fund). Nawashukuru pia Wakuu wa Idara na Vitengo, bila kuwasahau wataalam, makatibu muhtasi, watunza kumbukumbu, madereva, wahudumu na walinzi wa Wizara yetu na taasisi zake kwa kazi kubwa walizofanya katika mwaka 2017/18 na katika kukamilisha Bajeti hii.

80.    Mheshimiwa Spika, nashindwa kumaliza hotuba hii bila kumtaja mke wangu na rafiki yangu mpenzi Mbonimpaye. Moyo wake wa ibada kwa Mungu na uaminifu wake vimekuwa ndiyo nguzo yangu kuu katika utumishi wangu. Ninamshukuru sana yeye pamoja na watoto na wajukuu wetu wote tuliopewa na Mungu na familia nzima. Aidha, ninawiwa kuwashukuru wananchi wote wa Tanzania (wakulima, wafanyakazi, na wafanyabiashara). Ninawashukuru sana kwa uzalendo wao wa kufanya kazi kwa bidii na kulipa kodi kwa mujibu wa sheria kwa ajili ya maendeleo ya nchi yetu. Ninawashukuru pia wanafunzi wote wa shule za awali, msingi, sekondari na vyuo wanaosoma kwa bidii maana miongoni mwao tutapata viongozi na nguvukazi bora ya Taifa. Ninawashukuru pia Wazee wetu ambao walitoa mchango mkubwa kwa Taifa letu katika umri wao wa kufanya kazi. Aidha, siwezi kuwasahau wananchi wa wilaya za Buhigwe na Kasulu, na mkoa wetu wa Kigoma kwa ujumla. Ninyi ni fahari yangu maana mlinikuza. Ninawapenda! Vile vile ninawashukuru wananchi wenzangu wa Nzinje hapa Dodoma (Zuzu kwa jina la zamani), kwa kunipokea vizuri mimi na familia yangu.

81.    Mheshimiwa Spika, kwa kuwa inatarajiwa leo itakuwa siku ya mwisho wa mwezi Mtukufu wa Ramadhan, naomba nihitimishe hotuba hii kwa kuwatakia Waislamu wote Eid Mubarak.

82.    Mheshimiwa Spika, nimalizie kwa kusema ASANTE SANA MUNGU” kwa baraka zako zilizoniwezesha kukamilisha kusoma hotuba hii. Na kwenu Waheshimiwa Wabunge na Watanzania wote …….
(i)         “SANDENYI SANA”!
(ii)       “NGW’ABHEJA SANA”
(iii)     “WAITU MWAKORA”
(iv)     “OKORREE BHUYA”
(v)       “HAIKENI SANA”
(vi)     “MSENGWILE”
(vii)   “NDAGHA FIJO”
(viii)  “HEWELA”
(ix)     “KAJEKAJE”
(x)       “MURAKOZE CHANE”
(xi)     “ASANTENI SANA”

83.       Mheshimiwa Spika, naomba kutoa hoja

Jedwali Na 1: Mwenendo wa Makusanyo ya Mapato ya Serikali: 2011/12 -2018/19        Shilingi  Milioni

2012/13
2013/14
2014/15
2015/16
2016/17
2017/18
2017/18
2018/19

Halisi
Halisi
Halisi
Halisi
Halisi
Bajeti
Matarajio
Bajeti
Jumla ya Mapato (Yakijumuisha Halmashauri)
8,442,611
11,537,523
10,957,765
14,139,230
16,639,933
19,977,001
18,692,251
20,894,578


A. Mapato yanayotokana na Kodi
7,729,986
10,395,440
9,908,996
12,525,378
14,126,590
17,106,336
15,312,632
18,000,219

 1.  Ushuru wa Forodha
584,137
852,199
748,961
880,296
998,164
1,231,135
1,077,034
1,204,090

 2.   Ushuru wa Bidhaa
1,258,242
1,908,857
1,742,721
2,144,395
2,106,442
2,776,302
2,248,954
2,541,287

 3.   Kodi ya Ongezeko la Thamani
2,146,337
2,590,291
2,488,066
2,992,835
3,912,674
4,767,853
4,390,218
5,463,990

 4.   Kodi ya Mapato
3,034,360
3,656,506
3,716,685
4,594,971
5,117,862
5,997,039
5,556,523
6,540,038

 5.   Kodi Nyingine
706,910
1,387,587
1,212,563
1,912,880
1,991,449
2,334,006
2,039,904
2,250,814


B. Mapato yasiyotokana na Kodi
683,362
869,936
1,048,769
1,613,852
2,513,343
2,870,665
3,379,619
2,894,358

 1.   Michango na Gawio la Mashirika
47,602
110,014
161,234
388,551
893,935
529,583
646,415
597,770

 2.   Wizara Nyingine na Mikoa
414,925
444,694
527,451
799,449
1,107,690
1,653,776
2,183,359
1,561,000

 3.   Mapato ya Halmasahuri
220,835
315,228
360,084
425,852
511,718
687,306
549,845
735,589

Chanzo: Wizara ya Fedha na Mipango





Jedwali 2a: Mfumo wa Bajeti 2011/12-2018/19                                                                                   Shilingi  Milioni


2010/11
2011/12
2012/13
2013/14
2014/15
2015/16
2016/17
2017/18
2017/18
2018/19

Halisi
Halisi
Halisi
Halisi
Halisi
Halisi
Halisi
Bajeti
Matarajio
Matarajio
I. Mapato Yote
10,202,603
12,171,877
15,404,216
15,667,535
17,488,626
22,543,664
25,417,791
31,711,986
28,619,612
32,475,949
Mapato ya Ndani
5,577,986
7,025,884
8,221,776
9,867,227
10,597,681
13,622,182
16,128,215
19,289,695
17,639,052
20,158,989
Mapato ya Halmashauri
158,280
195,525
220,835
315,228
360,084
425,852
511,718
687,306
549,845
735,589
Misaada na Mikopo ya Bajeti
900,825
967,163
894,955
1,040,659
757,016
291,381
342,785
941,258
684,227
545,765
Misaada na Mikopo ya Miradi
1,013,078
1,207,445
1,423,579
1,194,930
1,154,909
1,186,982
1,857,399
2,473,770
1,804,663
2,005,016
Mikopo ya Kisekta (Basket Loans)
220,681
172,212
186,336
207,665
163,177
161,842
104,991
355,454
355,454
33,701
Misaada ya Kisekta (Basket Grants)
334,609
301,152
280,936
188,623
127,637
86,199
168,984
200,621
177,799
92,163
MCA (T) USA
196,114
221,601
220,350
213,612
0
0
0
0
0
0
Mikopo ya Ndani (Rollover)
720,249
1,326,852
1,734,535
1,528,153
2,064,756
3,005,789
4,615,670
4,948,229
4,835,199
4,600,000
Mikopo  ya Ndani (Financing)
1,244,330
334,864
1,069,321
976,712
799,776
2,299,151
1,300,000
1,220,668
1,199,373
1,193,669
Marekebisho
-317,498
-382,101
88,588
-1,059,790
408,786
1,010,781
-838,731
0
0
0
Mikopo ya kibiashara
153,948
801,282
1,063,006
1,194,516
1,054,803
453,504
1,226,760
1,594,985
1,374,000
3,111,058











II. Matumizi Yote
10,202,602
12,171,877
15,404,216
15,667,535
17,488,626
22,543,664
25,417,791
31,711,986
28,619,612
32,475,950
Matumizi ya Kawaida
7,453,565
8,397,155
10,904,521
11,741,493
13,778,397
18,204,111
18,144,967
19,712,394
19,302,746
20,468,676
CFS
1,625,883
2,518,207
3,383,124
3,666,799
4,724,910
6,480,906
8,643,560
9,461,433
9,892,197
10,004,480
Kulipa Madeni
1,116,572
1,843,666
2,627,946
2,686,455
3,552,426
5,047,764
7,234,530
7,829,918
8,260,682
8,372,951
Malipo Mengine
509,311
674,541
755,178
980,344
1,172,484
1,433,142
1,409,030
1,631,515
1,631,515
1,631,529
Matumizi ya Kawaida (Bila CFS)
5,827,682
5,878,949
7,521,397
8,074,693
9,053,487
11,723,205
9,501,407
10,250,961
9,410,549
10,464,196
o/w   Malipo ya Mishahara
2,346,378
2,722,084
3,349,959
3,969,108
4,617,648
5,627,497
5,599,246
6,276,267
5,962,454
6,386,265
 Mishahara ya Mashirika
457,665
455,006
518,755
568,708
637,711
925,760
767,901
929,501
883,026
1,023,687
 Fedha ya Halmashauri
158,280
195,525
362,206
315,228
170,627
170,340
251,484
274,922
274,922
389,862
 Matumizi Mengine
3,628,554
2,506,333
3,290,477
3,221,649
3,627,501
4,999,607
2,882,775
2,770,270
2,290,147
2,664,382
Matumizi ya Maendeleo
2,749,037
3,774,722
4,499,695
3,926,042
3,710,228
4,339,553
7,272,824
11,999,592
9,316,866
12,007,273
Fedha za Ndani
984,555
1,872,312
2,314,718
2,121,212
2,264,506
2,904,530
5,141,451
8,969,747
6,978,950
9,876,393
Fedha za Nje
1,764,482
1,902,410
2,184,977
1,804,831
1,445,722
1,435,023
2,131,374
3,029,845
2,337,916
2,130,880
Pato la Taifa
48,607,221
57,098,397
66,193,721
75,197,863
85,153,090
97,304,216
106,589,234
120,866,799
118,737,328
132,629,849

Chanzo:Wizara ya Fedha na Mipango
Jedwali 2b: Mfumo wa Bajeti 2010/11 - 2018/19
Asilimia ya Pato la Taifa

2011/12
2012/13
2013/14
2014/15
2015/16
2016/17
2017/18
2017/18
2018/19

Halisi
Halisi
Halisi
Halisi
Halisi
Halisi
Bajeti
Matarajio
Bajeti
Mapato Yote
21.3%
23.3%
20.8%
20.5%
23.2%
23.8%
26.2%
24.1%
24.5%
Mapato ya Ndani
12.3%
12.4%
13.1%
12.4%
14.0%
15.1%
16.0%
14.9%
15.2%
LGAs own source
0.3%
0.3%
0.4%
0.4%
0.4%
0.5%
0.6%
0.5%
0.6%
Misaada na Mikopo ya Bajeti
1.7%
1.4%
1.4%
0.9%
0.3%
0.3%
0.8%
0.6%
0.4%
Misaada na Mikopo ya Miradi
2.1%
2.2%
1.6%
1.4%
1.2%
1.7%
2.0%
1.5%
1.5%
Mikopo ya Kisekta (Basket Loans)
0.3%
0.3%
0.3%
0.2%
0.2%
0.1%
0.3%
0.3%
0.0%
Misaada ya Kisekta (Basket Grants)
0.5%
0.4%
0.3%
0.1%
0.1%
0.2%
0.2%
0.1%
0.1%
MCA (T) USA
0.4%
0.3%
0.3%
0.0%
0.0%
0.0%
0.0%
0.0%
0.0%
Mikopo ya Ndani (Rollover)
2.3%
2.6%
2.0%
2.4%
3.1%
4.3%
4.1%
4.1%
3.5%
Mikopo  ya Ndani (Financing)
0.6%
1.6%
1.3%
0.9%
2.4%
1.2%
1.0%
1.0%
0.9%
Marekebisho
-0.7%
0.1%
-1.4%
0.5%
1.0%
-0.8%
0.0%
0.0%
0.0%
    Mikopo yenye masharti ya kibiashara
1.4%
1.6%
1.6%
1.2%
0.5%
1.2%
1.3%
1.2%
2.3%










II. Matumizi Yote
21.3%
23.3%
20.8%
20.5%
23.2%
23.8%
26.2%
24.1%
24.5%
Matumizi ya Kawaida
14.7%
16.5%
15.6%
16.2%
18.7%
17.0%
16.3%
16.3%
15.4%
CFS
4.4%
5.1%
4.9%
5.5%
6.7%
8.1%
7.8%
8.3%
7.5%
Kulipa Madeni
3.2%
4.0%
3.6%
4.2%
5.2%
6.8%
6.5%
7.0%
6.3%
Malipo Mengine
1.2%
1.1%
1.3%
1.4%
1.5%
1.3%
1.3%
1.4%
1.2%
Matumizi ya Kawaida (Bila CFS)
10.3%
11.4%
10.7%
10.6%
12.0%
8.9%
8.5%
7.9%
7.9%
o/w Malipo ya Mishahara
4.8%
5.1%
5.3%
5.4%
5.8%
5.3%
5.2%
5.0%
4.8%
Mishahara ya Mashirika
0.8%
0.8%
0.8%
0.7%
1.0%
0.7%
0.8%
0.7%
0.8%
Fedha za Halmashauri
0.3%
0.5%
0.4%
0.2%
0.2%
0.2%
0.2%
0.2%
0.3%
Matumizi Mengine
4.4%
5.0%
4.3%
4.3%
5.1%
2.7%
2.3%
1.9%
2.0%
Matumizi ya Maendeleo
6.6%
6.8%
5.2%
4.4%
4.5%
6.8%
9.9%
7.8%
9.1%
Fedha za Ndani
3.3%
3.5%
2.8%
2.7%
3.0%
4.8%
7.4%
5.9%
7.4%
Fedha za Nje
3.3%
3.3%
2.4%
1.7%
1.5%
2.0%
2.5%
2.0%
1.6%










Chanzo: Wizara ya Fedha na Mipango

Jedwali Na. 3 Misaada na Mikopo Nafuu kutoka Nje 2014/15 - 2018/19
Shilingi Milioni

2014/15
2015/16
2016/17
2017/18
2017/18
2018/19

Halisi
Halisi
Halisi
Bajeti
Matarajio
Bajeti








Misaada ya Kibajeti
Misaada
546,709
0
190,303
190,023
190,613
236,264
Mikopo yenye Masharti Nafuu
375,459
291,381
152,482
751,235
493,614
309,501

Jumla
922,168
291,381
342,785
941,258
684,227
545,765


Mifuko ya Kisekta
Misaada
       189,112
        86,199
       168,984
       200,621
       177,799
        92,163
Mikopo yenye Masharti Nafuu
84,975
161,842
104,991
355,454
355,454
33,701

Jumla
274,087
248,041
273,975
556,075
533,253
125,864


Miradi ya Maendeleo
Misaada
       745,344
       409,157
       733,208
       853,815
       607,101
          752,982
Mikopo yenye Masharti Nafuu
    1,000,000
       777,825
    1,124,190
    1,820,576
    1,197,563
    1,252,035

Jumla
  1,745,344
  1,186,982
  1,857,399
  2,674,391
  1,804,663
  2,005,016

Jumla Kuu
2,941,599
1,726,404
2,474,159
4,171,723
3,022,143
2,676,645






Chanzo: Wizara ya Fedha na Mipango


Chanzo: Wizara ya Fedha na Mipango
















[1] Insha Tatu za Kifalsafa, Julius Nyerere, Kivazi Occassional Papers, No. 3, 2016

DKT. NDUGULILE AHIMIZA UTUNZAJI MZURI WA DAWA.

$
0
0
Naibu Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile akiongea na Wafamasia hawapo pichani wakati wa maadhimisho ya wiki ya Famasia yaliyofanyika leo jijini Dar es salaam.
Naibu Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile wa kwanza kushoto akipata maelezo juu ya dawa aliyoishika kutoka kwa Mkurugenzi wa kiwanda cha kutengeneza dawa Gullin Bw. Ashok Pandey kulia wakati wa maadhimisho ya wiki ya Famasia yaliyofanyika leo jijini Dar es salaam.
Naibu Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile kushoto akionesha juu Bango Kitita la famasia baada ya kulizindua wakati  wa maadhimisho ya wiki ya Famasia yaliyofanyika leo jijini Dar es salaam. Kulia ni Msajili wa Baraza la Famasia Bi. Elizabeth Shekirego .
Naibu Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile akiwakabidhi zawadi baadhi ya wadau wa Famasi kwa mchango wao katika sekta hiyo wakati wa maadhimisho ya wiki ya Famasia yaliyofanyika leo jijini Dar es salaam.
Naibu Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile akiwakabidhi zawadi baadhi ya wadau wa Famasi kwa mchango wao katika sekta hiyo wakati wa maadhimisho ya wiki ya Famasia yaliyofanyika leo jijini Dar es salaam.

Naibu Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile akiwakabidhi zawadi baadhi ya wadau wa Famasi kwa mchango wao katika sekta hiyo wakati wa maadhimisho ya wiki ya Famasia yaliyofanyika leo jijini Dar es salaam.
PICHA NA WIZARA YA AFYA.
*************************************************

NA WAMJW-DAR ES SALAAM.
NAIBU Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile amewaagiza wafamasia wa Hospitali za serikali kutunza dawa vizuri na mahali panapostahili ili kuweza kuepuka uharibifu wa dawa hizo.
Hayo ameyazungumza wakati wa maadhimisho ya wiki ya Famasia duniani yaliyofanyika leo jijini Dar es salaam yakiwa na lengo la kuimarisha na kuboresha fani hiyo nchini.
“Licha ya kutunza dawa  mahali salama wafamasia wanapaswa kutunza kumbukumbu za dawa hizo zinapoingia,zinapopokelewa ,zinapotolewa kwa wagonjwa na matumizi ili kuondoa uhaba wa dawa na kuthibitisha matumizi yake” alisema Dkt. Ndugulile.
Aidha Dkt. Ndugulile amesema kuwa wafamasia wanatakiwa kuwa waaminifu kazini kwani kuna badhi ya wafamasia wana tabia ya kuiba dawa  kwenye  vituo vyao vya kazi na kwenda kuuza nje ya kituo cha kutolea huduma za afya.
Mbali na hayo Dkt. Ndugulile amewaagiza Mganga Mkuu wa Serikali na Mfamasia Mkuu wa serikali kukaa pamoja na kujadili na kuwatengenezea mazingira wezeshi wazalishaji wa Dawa nchini ili waweze kutengeneza dawa kwa kuzingatia ubora na usalama wa mtumiaji .
“Asilimia 90 ya dawa zinanunuliwa nje ya nchi hivyo lazima tukae na kutengeneza mazingira wezeshi kwa wazalishaji wa ndani ili kuweza kutengeneza dawa hapa nchini na tuweze kuokoa fedha nyingi zinazokwenda nje ya nchi” alisema dkt. Ndugulile.
Kwa upande wake Msajili wa Baraza la wafamasia Bi. Elizabeth Shekirego amewasisitiza wanawake kujiunga na fani hiyo kwani wapo wachache ambapo ni asilimia 30 kuliko wanaume.
Aidha Bi. Shekirego amesema Baraza la wafamasia wamejidhatiti kuleta matokeo chanya kwa kuhakikisha dawa zinazotengenezwa nchini zinaboreshwa kwa mahitaji ya watanzania.
Wiki ya Famasia nchini imeadhimishwa leo jijini Dar es salaam ambapo imebeba kauli mbiu isemayo “TAALUMA YA FAMASI KUELEKEA TANZANIA YA UCHUMI WA VIWANDA” ambapo ulienda na uzinduzi wa bango kitita kitakachotumika kutoa elimu na wajibu wa mfamasia.
Viewing all 13053 articles
Browse latest View live


<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>