Quantcast
Channel: SUFIANIMAFOTO
Viewing all 13053 articles
Browse latest View live

*BancABC YAWAKARIBISHA WATEJA KUJIUNGA NA VISA CASH CARD AMBAYO SI LAZIMA UWE MTEJA WA BENKI HIYO

$
0
0
IMG_9016
Baadhi ya wafanyakazi wa BancABC wakisajili wateja wapya wa huduma ya VISA Cash Card ni Kadi ya malipo ya kabla ambayo hupunguza usumbufu wa kubeba fedha usio salama. Ambapo Mteja kuwa na kadi hii si lazima uwe na akaunti ya BancABC.
IMG_9032 
Afisa Mahusiano wa BancABC Sarah Pima akitoa maeleozo ya namna ya kutumia VISA Cash Card kwa mmoja wa wateja aliyetembelea banda la Bank hiyo lililopo karibu na Banda la Home Shopping Centre katika maonyesho ya 37 ya Biashara ya Kimataifa yanayoendelea katika uwanja wa Mwalimu Julius Nyerere jijini Dar es salaam. Wa pili kulia ni Afisa Mahusiano wa Bank hiyo Shamsa Aboud.
IMG_9038
Wananchi wakiendelea kupatiwa huduma na wafanyakazi wa Bank hiyo.
IMG_9045
Muonekano wa Banda la BancABC katika maonyesho ya 37 ya Biashara ya Kimataifa yanayoendelea katika uwanja wa Mwalimu Julius Nyerere jijini Dar es salaam.
IMG_9050
Moja ya Bango la Benki hiyo lililopo uwanjani hapo.
Zijue faida za VISA Cash Card kama ifuatavyo:-
- Una saa 24 siku 7 za juma kupata huduma kwenye akaunti yako popote, zaidi ya ATM 400 zenye nembo ya VISA ndani ya Tanzania na zaidi ya ATM milioni 1.3 duniani kote.
-Unaweza kufanya manunuzi kwenye sehemu za biashara zaidi ya 1000 zinazokubali VISA Tanzania na sehemu za biashara zaidi ya milioni 35 duniani.
-Rahisi kuipata.
-Inaweza kutumika papo hapo.
-Kuweka fedha na kuzitumia papo hapo.
-Rahisi kuweka fedha na kuzitumia haraka.
-Manunuzi ya moja kwa moja kupitia mtandao.
-Hudhibiti matumizi yako(unatumia ulichonacho kwenye kadi).
- Faraja na Usalama kupitia CHIP na namba za siri(PIN) hudhibiti udanganyifu na matumizi ya ulaghai.
-Fedha hurudishwa na kupata kadi nyingine pindi inapopotea/kuibiwa.
Ni nani anayeweza kutumia BancABC VISA Casha Card?
-Wateja na wasiokuwa wateja wa BancABC.
-Makampuni- kwa malipo ya posho na mishahara.
-Wazazi-fedha ya kujikimu kwa wanafunzi/gharama za maisha. Bora zaidi kwa usalama wa fedha.
-Mashirika ya Pensheni na Makampuni ya Bima- kwa malipo yenye faida.
-Wafanyabiashara ya Utalii- kwa malipo ya ada Utalii wa mbuga.
-Serikali- kwa malipo ya ruzuku na mikopo.
Na Unawezaje kupata BancABC VISA Cash Card?
Tembelea moja ya matawi yao ili uweze kujaza fomu fupi ya maombi ukiwa na viambatanishi vifuatavyo:
Raia- Kitambulisho cha Kura/Leseni ya Udereva/ Passport.
Sio Raia- Passport na Kibali cha makazi.
Kwa maelezo zaidi wasiliana nao kwa namba zifuatazo:
Upanga-Simu 255 22 2121537, 2121538, 2121539.
Kariakoo-Simu 255 22 2180212, 2180182, 2180108.
Quality Centre- Simu 255 22 2865904-910.
Arusha- Simu 255 27 2546390.

*MLEZI WA CCM MKOA WA DAR, MAKAMU WA RAIS DKT. BILAL AZUNGUMZA NA WAJUMBE WA HALMASHAURI KUU YA CCM MKOA WA DAR ES SALAAM LEO

$
0
0
 Mlezi wa CCM Mko wa Dar es Salaam, Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohamed Gharib Bilal, akizungumza na Wajumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Mkoa wa Dar es Salaam, wakati wa Kikao cha Halmashauri Kuu ya Mkoa kilichofanyika kwenye Ukumbi wa Karimjee jijini Dar es Salaam, leo.
 Mlezi wa CCM Mko wa Dar es Salaam, Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohamed Gharib Bilal, akizungumza na Wajumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Mkoa wa Dar es Salaam, wakati wa Kikao cha Halmashauri Kuu ya Mkoa kilichofanyika kwenye Ukumbi wa Karimjee jijini Dar es Salaam, leo.
 Baadhi ya wajumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Mkoa wa Dar es Salaam, wakiwa katika Ukumbi wa Karimjee wakimsikiliza Mlezi wao, Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, wakati alipozungumza nao leo.
 Baadhi ya wajumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Mkoa wa Dar es Salaam, wakisimama kumkaribisha Mlezi wao katika Ukumbi wa Karimjee, Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, wakati alipofika ukumbini hapo kuzungumza nao leo.
Mlezi wa CCM Mko wa Dar es Salaam, Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisalimiana na baadhi ya Wajumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Mkoa wa Dar es Salaam, Mbunge wa Temeke, Mhe. Abas Mtemvu, wakati alipowasili kwenye Ukumbi wa Karimjee jijini Dar es Salaam, leo kwa ajili ya kuzungumza na wajumbe hao.

*WAKAZI WA JIJI LA MWANZA WAFURIKA KUSHUHUDIA TAMASHA LA FILAMU LA GRAND MALT

$
0
0
Wananchi waliofurika katika Tamasha la Filamu la Grand Malt linalofanyika katika Uwanja wa Nyamagana, Mwanza wakifuatilia mambo yanavyoendelea.
********************************
 
Na Mwandishi Wetu, Mwanza
MWANZO MWISHO! Leo ni leo katika Uwanja wa Nyamagana jijini hapa, wakati kutakapofungwa rasmi Tamasha la Wazi la Filamu la Grand Malt Tanzania, maarufu kama ‘Grand Malt Tanzania Open Film Festival’ lililokuwa likifanyika kwa wiki nzima.

Huku wasanii wote mashuhuri wa filamu wakitarajiwa pia kufanya vitu vyao jukwaani, kazi kubwa itakuwa kwa burudani kali zitakazotolewa wakati wa kufunga tamasha hilo.


Mbali na hilo, pia kutakuwa na shindano kali hatua ya fainali ya kusaka wakali wa kurap pamoja na kukata nyonga, ambao nao watajiondokea na kitita kikubwa cha fedha.

Akizungumzia hilo, Mratibu wa Tamasha hilo, Musa Kissoky, alisema kutakuwa na mambo makubwa zaidi uwanjani hapo na kuwataka mashabiki wajitokeze kwa wingi kushuhudia kile kitakachoendelea.


 “Kila kitu kipo tayari na wasanii wote wakali wa filamu watakuwepo ili kutoa burudani kwa mashabiki waliofika hapa, huku kukiwa na filamu mbalimbali zitakazooneshwa,” alisema.

Baadhi ya wasanii wa filamu wanaotarajiwa kuwepo ni Irene Uwoya, Jacqueline Wolper, Vicent Kigosi ‘Ray’, Shamsa Ford, Ritchie Ritchie, Steven Jacob ‘JB’, Chuchu Hans, Steve Nyerere, Hashim Kambi na wengineo wengi.

 Akizungumzia hilo, Meneja wa Grand Malt, Consolata Adam alisema, amefurahi kuona tamasha hilo limefanikiwa kwa kiasi kikubwa, huku akitaka mashabiki kufurika Nyamagana leo kuona kile kinachoendelea.

“Hapa Mwanza tumeshuhudia vipaji vya kila aina, nimefurahi kwa kiasi kikubwa kuona mashabiki walivyolipokea tamasha hili, kwetu Grand Malt tunaamini lengo letu limefanikiwa kwa kiasi kikubwa,” alisema.

Katika mashindano ya kurap na kucheza katika kila eneo mshindi wa kwanza anatarajiwa kuondoka na Sh 200,000 wa pili Sh 100,000 na watatu Sh 50,000.

Tamasha la Filamu la Grand Malt lilianza rasmi mwishoni mwa wiki na linatarajiwa kumalizika leo, huku wakati wote wa tamasha hilo zikionyeshwa filamu mbalimbali za Tanzania.

Tamasha hilo la filamu limedhaminiwa na kinywaji cha Grand Malt kisicho na kilevi ambacho kinazalishwa na kusambazwa na Kampuni ya Bia Tanzania (TBL).

*PROFESA LIPUMBA AONGOZA MAZISHI YA MLINZI WA MAKAO MAKUU YA CUF MUHARAMI ABDALLAH SHAABAN TANGANYIKA

$
0
0
 Mwenyekiti wa CUF Profesa Ibrahim Lipumba akikabidhiwa daftari la michango wakati alipowasili Tabata, jijini Dar es salam, nyumbani kwa Marehemu Muharami Abdallah Shaaban Tanganyika aliyefariki juzi katika hospitali ya Amana. Marehemu alikuwa ni mfankazi ya ulinzi katika makao makuu ya CUF, Buguruni. Mwenye pama ni Naibu katibu Mkuu wa CUF Mhe. Julius Mtatiro
 Mwenyekiti wa CUF Profesa Ibrahim Lipumba akiandika kwenye daftari la michango. Mwenye pama ni Naibu katibu Mkuu wa CUF Mhe. Julius Mtatiro na kulia ni kaka wa marehemu Ismail
 Sehemu ya waombolezaji
 Mwenyekiti wa CUF Profesa Ibrahim Lipumba akipata chakula na waombolezaji wengine.

Mwenyekiti wa CUF Profesa Ibrahim Lipumba akiongea machache kabla ya safari ya kuelekea makaburini kuanza. Alimsifia marehemu Tanganyika kama mmoja wa wafanyakazi waaminifu na makini waliojituma sana. Pia alisema wamepoteza askari hodari ambaye alikuwa nguzo muhimu ya ulinzi katika makao makuu ya chama hicho cha ulinzi.
Mwenyekiti wa CUF Profesa Ibrahim Lipumba akiongoza mazishi hayo yaliyofanyika kwenye makaburi ya familia ya mama wa marehemu huko Segerea.

*WAMASAI WA MUNDULI MKOANI ARUSHA WATEMBELEA BANDA LA AICC LILILOPO KATIKA VIWANJA VYA MAONESHO YA 37 YA BIASHARA YA KIMATAIFA DAR ES SALAAM.

$
0
0
.Katibu Mhitasi wa Arusha Intarnational Confrerence Centre. Joyce Mollel (kushoto) akiwaonyesha baadhi ya akinamama wa kikundi cha Masai cha Munduli Arusha shughuli wanazotoa, wakati akimama hao walipotembelea katika banda lao lililopo katika maonesho ya 37 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam.

*NDEGE AINA YA BOING 777 YAUA WAWILI WAKATI IKITUA UWANJA WA SAN FRANCISCO CALFONIA

$
0
0
 Magari ya zimamoto yakijitahidi kumwaga maji kuzima moto uliokuwa ukiwaka kwenye Ndege aina ya 777, Namba 214 baada ya kukrash wakati ikitua kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa San Francisco Calfonia Nchini Marekani jana. Katika ajali hiyo watu wawili wamefariki dunia na wengine kibao.
 Baadhi ya abiria waliowahi kujiokoa wakishuka katika ndege hiyo, ambayo ilikuwa na abiria zaidi ya 300.
 SAN FRANCISCO (AP) — An Asiana Airlines flight packed with more than 300 people slammed into the runway while landing at San Francisco airport Saturday and caught fire, forcing many to escape by sliding down the emergency inflatable slides as flames tore through the plane.

At least two people died in the crash, while another 181 people were taken to hospitals, most with minor injuries, authorities said. Five people, including one child, remained in critical condition at San Francisco General Hospital, the region's main trauma center.

As the plane approached the runway from the waters of San Francisco Bay around noon, travelers in the terminals and others eyewitnesses could see that the aircraft was swaying unusually from side to side and that at one point the tail seemed to hit the ground.

Kate Belding, who was jogging a few miles away, said she thought: "Oh my God. That plane is crashing."

By the time the flames were out, the top of the Boeing 777's fuselage had burned away. The tail section was gone, with pieces of it scattered across the beginning of the runway. One engine appeared to have broken away. Emergency responders could be seen walking inside the burned-out wreckage.


This photo provided by Antonette Edwards shows what a federal aviation official says was an Asiana A …
News of the crash spread quickly on Twitter and the Internet in this wired city, with eyewitnesses tweeting their stories, posting images of the plumes of smoke rising above the bay and uploading video of passengers fleeing the burning plane.

"It just looked really bad," Belding said. "I've seen the pictures of it since then, and it's amazing anyone walked out of that plane."

The investigation has been turned over to the FBI and terrorism has been ruled out, said San Francisco Fire Chief Joanne Hayes-White said. Federal aviation and transportation investigators were heading to the scene. Asiana, Boeing and the engine manufacturer, Pratt & Whitney, pledged to work with them.

Vedpal Singh, who was sitting in the middle of the aircraft and survived the crash with his family, said there was no forewarning from the pilot or any crew members before the plane touched down hard and he heard a loud sound.

"We knew something was horrible wrong," said Singh, who suffered a fractured collarbone and had his arm was in a sling.
 This photo provided by Wei Yeh shows what a federal aviation official says was an Asiana Airlines fl …
"It's miraculous we survived," he said.

A visibly shaken Singh said the plane went silent before people tried to get out anyway they could. His 15-year-old son said luggage tumbled from the overhead bins The entire incident lasted about 10 seconds.

Based on witness accounts in the news and video of the wreckage, Mike Barr, a former military pilot and accident investigator who teaches aviation safety at the University of Southern California, said it appeared the plane approached the runway too low and something may have caught the runway lip — the seawall at the end of the runway.

San Francisco is one of several airports around the country that border bodies of water that have walls at the end of their runways to prevent planes that overrun a runway from ending up in the water.

Since the plane was about to land, its landing gear would have already been down, Barr said. It's possible the landing gear or the tail of the plane hit the seawall, he said. If that happened, it would effectively slam the plane into the runway, he said.
 Smokes rises from Asiana Flight 214 after it crashed at San Francisco International Airport in San F …
Noting that some witnesses reported hearing the plane's engines rev up just before the crash, Barr said that would be consistent with a pilot who realized at the last minute that the plane was too low and was increasing power to the engines to try to increase altitude. Barr said he could think of no reason why a plane would come in to land that low.

Belding was out jogging just before 11:30 a.m. on a path across the water from the airport when she noticed the plane approaching the runway in a way that "just didn't look like it was coming in quite right."

"Then all of a sudden I saw what looked like a cloud of dirt puffing up and then there was a big bang and it kind of looked like the plane maybe bounced (as it neared the ground)," she said. "I couldn't really tell what happened, but you saw the wings going up and (in) a weird angle."

"Not like it was cartwheeling," she said, but rather as though the wings were almost swaying from side to side.

The flight originated in Shanghai, China, and stopped over in Seoul, South Korea, before coming to San Francisco, airport officials said. The airline said there were 16 crew members aboard, and the 291 passengers included 77 South Koreans, 141 Chinese, 61 Americans and one Japanese citizen. The nationalities of the remaining passengers weren't immediately known.
 Smokes rises from Asiana Flight 214 after it crashed at San Francisco International Airport in San F …
Airport spokesman Doug Yakel said 49 people were in serious condition and 132 had less significant injuries.

The airport closed for several hours, and when it reopened, two of the four runways were operating.

Asiana is a South Korean airline, second in size to national carrier Korean Air. It has recently tried to expand its presence in the United States, and joined the Star Alliance, which is anchored in the U.S. by United Airlines.

The 777-200 is a long-range plane from Boeing. The twin-engine aircraft is one of the world's most popular long-distance planes, often used for flights of 12 hours or more, from one continent to another. The airline's website says its 777s can carry between 246 to 300 passengers.

The flight was 10 hours and 23 minutes, according to FlightAware, a flight tracking service. The 777 is a smaller, wide-body jet that can travel long distances without refueling and is typically used for long flights over water.
 The wreckage of Asiana Flight 214 is seen after it crashed at San Francisco International Airport in …
The last time a large U.S. airline lost a plane in a fatal crash was an American Airlines Airbus A300 taking off from John F. Kennedy International Airport in New York in 2001.

Asia remains one of the fastest-growing regions for aviation in the world. Even with slowing economies in Japan and China, airlines there saw 3.7 percent more passengers than a year ago, according to the International Air Transport Association.

Finding enough experienced pilots to meet a growing number of flights is becoming a problem. A 2012 report by aircraft manufacturer Boeing said the industry would need 460,000 new commercial airline pilots in the next two decades — with 185,000 of them needed in Asia alone.

"The Asia-Pacific region continues to present the largest projected growth in pilot demand," the report said.
In this photo provided by Scott Sobczak, smoke rises from of Asiana Flight 214 after it crashed at S …
The most notable accident involving a 777 occurred on Jan. 17, 2008 at Heathrow Airport in London. British Airways Flight 28 landed hard about 1,000 feet short of the runway and slid onto the start of the runway. The impact broke the 777-200's landing gear. There were 47 injuries, but no fatalities.

An investigation revealed ice pellets that had formed in the fuel were clogging the fuel-oil heat exchanger, blocking fuel from reaching the plane's engines. The Rolls-Royce Trent 800 series engines that were used on the plane were then redesigned.

Bill Waldock, an expert on aviation accident investigation, said he was reminded of the Heathrow accident as he watched video of Saturday's crash. "Of course, there is no indication directly that's what happened here," he said. "That's what the investigation is going to have to find out."

The Asiana 777 "was right at the landing phase and for whatever reason the landing went wrong," said Waldock, director of the Embry-Riddle Aeronautical University accident investigation laboratory in Prescott, Ariz.

"For whatever reason, they appeared to go low on approach and then the airplane pitched up suddenly to an extreme attitude, which could have been the pilots trying to keep it out of the ground," he said.

*NMB CHAPCHAP AKAUNTI YAWA KIVUTIO KIKUBWA KATIKA MAONYESHO YA SABASABA

$
0
0
 Maafisa Mauzo ya Nje wa Benki ya NMB wakiwahudumia wateja waliofika katika Banda la benki ya NMB lililopo katika viwanja vya sabasaba kwaajili ya kufungua akaunti ya Chapchap ambapo mteja ufunguliwa akaunti yake papo hapo na kupewa kadi ya kutolea pesa kwenye mashine muda huo huo.
 Baadhi ya Wateja waliofurika katika moja ya gazebo la NMB lililopo nje ya Banda la Benki ya NMB  katika Viwanja Vya Sabasaba wakifunguliwa akaunti ya ChapChap ambayo mteja ufunguliwa akaunti hiyo akiwa na kitambulisho cha kupigia kura na kupewa kadi yake ya kutolea pesa kwenye mashine za NMB papo hapo na kwa gharama ya Shilingi Elfu kumi tu
 Wateja waliofika katika Moja ya gazebo lililopo nje ya Banda la Benki ya NMB katika viwanja vya sabasaba wakipata maelezo mara baada ya kufungua akaunti zao za ChapChap na kukabidhiwa kadi zao za kutolea pesa kwenye mashine za NMB papo hapo kwa gharama nafuu ya shilingi Elfu Kumi tu.
 Afisa mauzo ya Nje wa Benki ya NMB Bw Respecious Denis akitoa maelezo ya akaunti ya Chapchap kwa Mteja aliyemaliza kufungua akaunti hiyo mara baada ya kufika kwenye moja ya gazebo la Benki ya NMB lililopo katika Viwanja Vya sabasaba mapema leo
 Maafisa Mauzo ya Nje wa Benki ya NMB wakiwahudumia wateja waliofika katika gazebo la Benki ya NMB lililopo nje ya Banda la Benki ya NMB kwaajili ya Kufungua akaunti ya Chapchap ambapo mteja akimaliza kufunguliwa akaunti ukabidhiwa kadi yake ya kutolea pesa kwenye mashine za NMB papo hapo
 Maafisa Mauzo ya Nje wa Benki ya NMB wakiendelea na zoezi la kuwafungulia akaunti ya Chapchap wateja waliofika katika moja ya gazebo la Benki ya NMB kwaajili ya kufungua akaunti  ya Chapchap Kulia Ni baadhi ya Maafisa Mauzo ya Nje wa Benki ya NMB wakijiandaa kwaajili ya kumpiga Picha mteja aliyefika kwaajili ya kufungua akaunti ya Chapchap.
 Afisa Mauzo ya Nje wa Benki ya NMB Maana Katuli akimpiga picha mteja aliyefika katika Banda la NMB kwaajili ya Kufungua Akaunti ya Chapchap ambapo mteja akimaliza kufunguliwa akaunti anakabidhiwa na kadi yake ya kutolea pesa papo hapo
 Wateja wakipata maelezo ya kutosha kutoka Kwa Maafisa Mauzo ya Nje wa Benki ya NMB
 Mteja akichukuliwa alama za vidole na mmoja kati ya maafisa mauzo ya nje wa benki ya NMB waliokuwa wakimuhudumia wakati mteja huyo alipofika kwaajili ya kufungua akaunti ya Chapchap
Afisa Mauzo ya Nje wa Benki ya NMB Batuli Suna akichukua alama za vidole vya mteja alifika katika banda la benki ya NMB kwaajili ya Kufungua akaunti ya Chapchap katika Maonyesho ya 37 ya Kibiashara ya Kimataifa. Picha Zote na Josephat Lukaza 

*WATU TISA WAPOTEZA MAISHA NA 53 WAJERUHIWA AJALI YA BASI LA SUMRI KATAVI

$
0
0
Basi la kampuni ya Sumry limetumbukia mtoni na kusabisha watu tisa kupoteza maisha na kujeruhi abiria wapatao 53 katika mto Iku uliopo katika kijiji cha Sitalike wilaya ya Mlele mkoani Katavi
 Tukio hilo la kusikitisha lilitokea saa sita usiku kuamkia Julai 5, 2013 wakati basi hilo lilipokuwa likitokea mjini Sumbawanga kuelekea Mpanda mkoani Katavi likiwa na abiri waliokuwa wametoka Mbeya.
 Kaimu Kamanda wa Polisi mkoani Katavi Emanuely Nnley alisema  kuwa ajali hiyo ilihusisha basi aina ya Nissan Diesel lenye namba T909 AZT mali ya kampuni ya Sumry lililokuwa likiendesha na dereva aliyetajwa kwa jina na Stephano Chimane maarufu kwa jina la Ntungu.
  Mganga mkuu wa wilaya ya Mpanda Mkoani Katavi, Dr Emanuely Kamgobe alisema basi hilo lilipofika katika daraja hilo lenye kona kali na mteremko dereva wake alishindwa kulenga daraja hali iliyosababisha tairi za nyuma kupanda juu ya ukingo na kudumbukia mtoni ambapo dereva huyo alitoka  na kukimbilia kusikojulikana.
 Alifafanua kuwa juhudi za uokoaji zilianza kufanyika usiku huo huo ambapo majeruhi 53 waliokolewa na maiti tisa za wanaume watatu na wanawake watano na 
mtoto mmoja wa kike ziliopolewa katika maji 
 Alisema hali ya majeruhi inaendelea vizuri isipokuwa majeruhi watatu walikimbizwa katika hospitali ya mkoa wa Rukwa kwa matibabu zaidi na kufafanua kuwa chanzo cha ajali hiyo ni uzembe wa dereva kushindwa kuliongoza gari, ubovu wa gari na wembamba wa daraja 
 Afisa Mwandamizi wa SUMATRA mikoa ya Rukwa na Katavi, David Chiragi alisema basi hilo lilikuwa limeiba njia kwani leseni yake inaliruhusu basi hilo kufanya safari za Sumbawanga Kirando na siyo Sumbawanga Mpanda kwa mujibu wa leseni iliyotolewa mwezi Juni mwaka huu 
 Alisema hata upana wa daraja ilipotkea ajali hiyo ni mdogo sana ambapo vipimo vinaonesha daraja hilo lina upana wa mita 3.5 (tatu na nusu) tu wakati basi lina upana wa mita nne na nusu hivyo kujenga mazingira ya ugumu wa dereva kulenga daraja inapotokea msukosuko wa aina yoyote hasa wakati wa usiku na hivyo kuwataka wakala wa barabara mkoani Katavi kuangalia namna ya kupanua daraja hilo na kuboresha eneo hilo 
 Alisema katika kipindi cha Januari hadi July 2013 zaidi ya ajali tisa zimetokea katika daraja hilo zikihusisha magari makubwa saba na madogo mawili kutokana na madereva kushindwa kumudu magari yao na kulenga daraja hilo 
 Alisema pia basi hilo lina makosa ya kutembea nje ya ratiba, kuiba njia na kuzidisha abiria hivyo ofisi yake imechukua hatua ya kuvunja safari za mabasi ya kampuni ya Sumry za mchana na badala yake mabasi yote yataondoka Sumbawanga na Mpanda majira ya asubuhi pekee.

*TAASISI LA STARKEY HEARING FOUNDATION YAWATIBU WALEMAVU WASIOSIKIA

$
0
0
 Nyota wa mchezo wa mpira wa miguu wa Marekani (American Football) Rays Lewis akimpa  Rais Dkt. Jakaya Kikwete zawadi ya kofia yenye nembo ya timu yake wakati nyota huyo alipomtembelea Rais Kikwete mjini Arusha. Nyota huyo yuko nchini ambapo ni mmoja wa wafadhili wakubwa wa huduma kwa wagonjwa wenye ulemavu wa kusikia inayotolewa na taasisi ya Starkey Hearing Foundation ya nchini Marekani.Wagonjwa zaidi ya 3500 wanatarajiwa kunufaika na huduma hiyo inayotolewa bure na taasisi hiyo.
 Muasisi wa Taasisi ya Strakey Hearing Foundation  Bwana Bill Austin Starkey akimhudumia mtoto Lissa Frank(9) ambaye alikuwa kiziwi tangu kuzaliwa na kuweza kusikia baada ya kupata tiba na huduma ya kuwekewa kifaa maalumu katika kliniki maalumu iliyofanyika katika hospitali ya Seliani mkoani Arusha leo.
Waasisi wa Taasisi ya Starkey Foundation Bwana Bill Austin Starkey(kulia aliyeinama) na Mkewe Tani Austin(Wapili kushoto) pamoja na mhudumu kutoka hospitali ya Seliani(kushoto) wakifurahi baada ya mtoto Lissa Frank(9) kuweza kusikia vyema baada ya kupatiwa matibabu katika kliniki maalumu iliyofanyika katika hospitali ya Seliani mjini Arusha leo. (Picha na Freddy Maro)

*RAIS KIKWETE ANOGESHA TAMASHA LA MATUMAINI UWANJA WA TAIFA DAR

$
0
0
Rais kikwete akifungua tamasha la matumaini hivi sasa uwanja wa Taifa,jijini Dar.Picha zaidi zitawajia hapo baadae kidooogo.
Waimba injili Ambwene Mwasongwe (kulia) na Edson (kushoto) wakiimba sambamba katika Tamasha la Matumaini 2013.
Edson akishambulia.
Ambwene Mwasongwe naye alikuwepo.
Sehemu ya mashabiki wakishangilia burudani.

*RAIS WA ZANZIBAR ATEMBELEA MAONYESHO YA SABASABA

$
0
0
 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa  Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,akipata maelezo kutoka kwa Mkurugenzi wa Kikundi cha ZAYDAT &BASMA GROUP cha Chukwani Zanzibar,TatuSuleiman,wakati alipokuwa  akiangalia bidhaa Mbali mbali za vikundi vya Ushirika kutoka Zanzibar vilivyoshiriki katika maonesho ya sabasaba ya kibiashara katika viwanja vya mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam jana.
 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa  Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,akipata maelezo kutoka kwa Mkurugenzi wa  Bana Enterprises Company Limited SAID OMAR SAID, kampuni ambayo inajishuhulisha na utengenezaji wa fanicha za Mti wa Mnazi,wakati alipotembelea maonesho ya sabasaba ya kibiashara katika viwanja vya
mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam jana.
  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa  Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,akisalimiana na Mke wa Rais Mstaafu Mama Anna Mkapa,wakati alipowasili katika Mabanda ya Taasisi yake (Mfuko wa Fursa sawa kwa Wote),alipotembelea maonesho ya sabasaba ya kibiashara yanayoendelea katikaviwanja vya mwalimu Nyerere Jijini Dar es Salaam.
 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa  Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,  akipata maelezo wakati alipokuwa
akiangalia Bidha mbali mbali za Akima mama kutoka Mkoani Kagera katika maonesho ya sabasaba ya kibiashara yanayoendelea katikaviwanja vya mwalimu Nyerere Jijini Dar es Salaam.

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa  Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein, akitoa ushauri kwa wasimamizi wa  kampuni ya Nguo ya Arusha chini ua usimamizi wa Mkurugenzi wake Anuj Shal,(kulia) wakati wa maonesho ya sabasaba ya kibiashara yanayoendelea katika viwanja vya mwalimu Nyerere Jijini Dar es Salaam. Picha na Ramadhan Othman,Ikulu.

*BALOZI SEIF AZUNGUMZA NA WAFANYABIASHARA

$
0
0
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibarf Balozi Seif Ali Iddi akizungumza na Wajumbe wa Kamati ya Wafanyabiashara ya kushajiisha ushiriki wa Sekta Binafsi katika maadhimisho ya Sherehe za kutimia miaka 50 ya Zanzibar  aliokutana nao Ofisini kwake Vuga Mjini Zanzibar. Picha na Hassan Issa wa – OMPR – ZNZ.
*************************************
Wazanzibari wote walioko ndani na nje ya Zanzibar wana fursa, haki na Uhuru wakati wowote kusaidia kwa njia mbali mbali maandalizi na hatimae  kufanikisha sherehe za Mapinduzi ya Zanzibar ya mwaka 1964 kutimia robo Karne ambayo ni  sawa na miaka 50 iliyopita.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibarf Balozi Seif Ali Iddi alisema hayo wakati akizungumza na Wajumbe wa Kamati ya Wafanyabiashara ya kushajiisha ushiriki wa Sekta Binafsi katika maadhimisho ya Sherehe za kutimia miaka 50 ya Zanzibar  aliokutana nao hapo Ofisini kwake Vuga Mjini Zanzibar.
Balozi Seif alisema Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar imelenga kuwaungalisha Wazanzibari wote popote pale walipo ili kuona wanashiriki kikamilifu kwenye maadhimisho hayo yanayotarajiwa kuwa ya aina yake na Kihistoria hapo mwakani.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar aliieleza Kamati hiyo baadhi ya mambo yaliyopangwa kufanya ndani ya vugu vugu la maadhimisho hayo ambayo yatasaidia kutoa taaluma kwa Jamii hasa kile kizazi kilichozaliwa baada ya mapinduzi ya mwaka 1964 ambacho bado hakijaelewa dhamira hasa ya kufanyika kwa Mapinduzi ya Zanzibar.
Balozi Seif ambae pia ni Mwenyekiti wa Sherehe na Maadhimisho ya Taifa aliyataja baadhi ya mambo yaliyolengwa kufanya katika kipindi hicho cha sherehe kuwa ni pamoja na warsha, makongamano kwa kushirikisha vyama vya Siasa,  matembezi ya kuashiria sherehe hizo pamoja na usiku maalum wa burdani na ngoma za asili.
Alifahamisha kwamba Mnara Maalum wa kumbu kumbu ya Mapinduzi utajengwa ili kupamba sherehe hizo za aina yake zitakazotoa pia fursa ya kualikwa kwa Viongozi wa nchi rafiki za mwanzo zilizojitokeza kuunga mkono mapinduzi ya mwaka 1964.
“ Katika kupamba sherehe zetu tumeandaa kutoa nishani maalum kwa watu waliotoa mchango mkubwa kwa Taifa tokea Mapinduzi ya Mwaka 64 wakiwemo askari wa Vikosi vya ulinzi na usalama, wana sanaa na Utamaduni “. Alisisitiza Mwenyekiti huyo wa Kamati ya sherehe na maadhimisho ya Taifa.
Balozi Seif aliwaomba wajumbe wa Kamati hiyo ya Wafanyabiashara ya kushajiisha ushiriki wa Sekta Binafsi katika maadhimisho ya Sherehe za kutimia miaka 50 ya Zanzibar  kuhakikisha  wanajitolea kwa nguvu zao zote katika kufanikisha vyema kazi waliyopewa na Taifa.
Naye mjumbe wa Kamati hiyo Mbunge wa Jimbo la Mpendae Salum Turky aliahidi akujitolea kugharamia ujenzi wa mnara huo wa kumbu kumbu ya Mapinduzi unaotarajiwa kujengwa katika eneo la Mzunguuko wa Bara bara za makutano ya Nyumba za Maendeleo Michezani.
Aliiomba Kamati ya Sekriterieti ya Sherehe na Maadhimisho ya Taifa Zanzibar kumpatia michoro ya ujenzi wa Mnara huo ili apate wasaa wakujiandaa kuitekeleza kazi hiyo ambayo anaamini kwamba atakuwa ametoa mchango na kuweka historia ndani ya maadhimisho ya sherehe za Mapinduzi ya Zanzibar.
“ Tunashukuru kuona kwamba Zanzibar inaingia kutimiza miaka hamsini ya Mapinduzi ya Zanzibar ya mwaka 1964 ikiwa katika hali ya amani na utulivu hali ambayo ni nadra kupatikana katika baadhi ya Nchi Duniani “. Alifafanua Mjumbe huyo wa Kamati hiyo Salum Turky.
Kwa upande wao wajumbe wengine Simai Mohd, Ahmada Abdullwakil, Sharifa Khamis na Meneja wa Kampuni ya Simu za Mkononi ya Zantel Zanzibar Mkweche wameipongeza Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kwa uamuzi wake wa kuanza kujiandaa mapema ya sherehe hizo kubwa.
Hata hivyo waliishauri Serikali kufikiria kutenga  maeneo ambayo wafanyabiashara wanaweza kuyatumia kutangaza biashara zao katika njia maalum itakayotoa fursa ya kuchangia maadhimisho hayo.
“ Sio mbaya kwa Serikali kutafuta njia ya kuwashirikisha pia Wafanyabiashara wa Tanzania Bara hasa wale waliowekeza vitega uchumi vyao hapa Zanzibar na pia wenye imani ya muelekeo wa kuunga mkono maadhimisho hayo “. Alisisitiza Simai Mohd.
“ Wakati tumejikubalisha na sisi kuingia katika ulimwengu wa sayansi na tenolojia na kwa vile wenzetu wamejiimarisha vyema katika masuala ya utambulisho wao itapendeza  nasisi kuelekea huko kwa kuwa na utambulisho wetu maalum ambao utawapa fursa wageni na watalii kuielewa vyema Zanzibar“. Alishauri pia Mjumbe mwengine wa kamati hiyo Ahmada Abdull wakil.
Katika kuanza rasmi jukumu zima walilopewa wana kamati hao walifikia uwamuzi  wa kuanza kikao cha dharura mara baada ya mkutano huo kupanga mikakati ya kufanikisha jukumu lao.
Ujumbe wa mwaka huu wa Maadhimisho ya sherehe za Mapinduzi ya Zanzibar kutimia robo Karne { sawa na miaka 50 } ni  Amani, Umoja na Maendeleo yetu ni Matunda ya Mapinduzi ya 1964. “ Mapinduzi Daima “.

*DKT SALMIN NA DKT SHEIN WAUNGURUMA KIBANDA MAITI ZANZIBAR LEO

$
0
0
 Makamu wa Mwenyekiti wa CCM Zanzibar na Rais Mstaafu wa  Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi (Komandoo) Dk.Salmin Amour Juma, alipokuwa akiwasalimia na kuwahutubia katika Mkutano wa hadhara

Kibandamaiti Mjini Zanzibar katika uwanja wa Demokrasia Kibanda maiti mjini Zanzibar.

Makamo wa Mwenyekiti wa CCM Zanzibar na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,akizungumza na wananchi na wanachama wa CCM wa Mikoa ya Unguja,katika Viwanja vya Demokrasia Kibanda maiti mjini Zanzibar,katika mkutano huo ulizungumzia uwepo wa Serikali mbili kwa Serikali ya mapinduzi Zanzibar na Serikali ya Muungano wa Tanzania.
Wanachama wa CCM wa maskani ya Kisonge wakishangilia katika Mkutano wa hadhara uliofanyika leo na kuhutubiwa na Makamo Mwenyekiti wa CCM Zanzibar na Rais wa Zanzibar  na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,Uwanja wa Kibandamaiti Mjini Zanzibar. Picha na Ramahan Othman,Ikulu.

*FULL MKANDA JK AKIFUNGUA TAMASHA LA MATUMAINI LEO UWANJA WA TAIFA

$
0
0
 Muziki wa Injili ulitawala. Hapa Solomon Mukubwa akitumbuiza
 MC wa Tamasha la Matumaini Godwin Gondwe a.k.a Double G akiwa kazini
 Bango lajieleza
 Uzalendo kwanza
 Nnape Nnauye akiwa na wadau
 JK akitete jambo na Eric Shigongo, mwandaaji wa Tamasha la Matumaini
 Wagunge wapenzi wa Simba wakipiga jalamba
 Profesa Maji Marefu akiongoza wabunge wapenzi wa Simba
 Wabunge wapenzi wa Simba
 Mwigulu Mchemba na skafu yake akiwa na  wabunge wapenzi wa Yanga
 Halima Mdee (kati mbele, bukta nyeusi) akiongoza kikosi cha wabunge wapenzi wa Yanga
 Kikosi kazi cha wabunge wapenzi wa Yanga
 Da' Asha Baraka akiwa na Mwenyekiti wa Baraza la Michezo (BMT) Dionis Malinzi
 Mwandaaji wa Tamasha la Matumaini akisema machache
 Millard Ayo wa Clouds FM akirusha vitu live
 Wapiganaji wakila mzigo
 Wapiganaji kazini
 Wapiganaji wakishuhudia
 Wapiganaji wakirekodi matukio
 JK akifungua rasmi Tamasha la Matumaini
 JK akiwaasa Watanzania wasidanganyike na watu wanaotaka kuwatenganisha
 Hatudanganyiki....
 JK akilisifia Tamasha la Matumaini kuwa ni moja ya majibu ya wanaotaka kutenganisha Watanzania kwa misingi ya kikabila ama kidini
 JK akijiandaa kupiga filimbi kuanzisha mechi ya wabunge wpenzi wa Yanga na Simba
 JK akiwa refarii akihesabu wachezaji kabla ya kuanzisha mechi
 JK akiaga baada ya kuanzisha mpambano huo 
 JK akikaribishwa na mwandaaji Eric Shigongo. Kati ni Waziri wa Habari,  Vijana, Utamaduni na Michezo Dkt Fenella Mukangara
 JK akiingia uwanja wa Taifa akiongozana na Waziri wa Habari,  Vijana, Utamaduni na Michezo Dkt Fenella Mukangara na Eric Shigongo
 JK akiwa meza kuu
 Meza kuu
 Mwandaaji wa tamasha Eric Shigongo akiongea machache
 JK akimpongeza Eric Shigongo kwa hotuba nzuri
 Waziri wa Habari,  Vijana, Utamaduni na Michezo Dkt Fenella Mukangara akimkaribisha JK kutoa hotuba yake
 Tamasha la Matumani Oye!
 JK akiongea na kadamnasi kwenye tamasha hilo katika hotuba iliyorushwa moja kwa moja na TBC
 TUSIDANGANYIKE...
 JK akiongea na kadamnasi
 "Tamasha hili ni majibu kwa wanaotutakia mabaya Tanzania...."
 JK akiongea na kadamnasi
 JK akisalimiana na wachezaji wa Bongo Movie
 JK akipeana mikono na kipa wa zamani  Yanga na Taifa Stars Peter Manyika ambaye sasa ni msanii wa Bongo Fleva na Bongo Movie
 Jk akisalimiana na Bongo Movie Stars
 JK akisalimiana na Katibu Mkuu wa FAT mstaafu Mwina Kaduguda
 JK akisalimiana na kipa (wa kweli)  wa Yanga Barthez
 JK akiingia uwanjani
 Kikosi cha wabunge wapenzi wa Simba
 Waamuzi na wabunge wapenzi wa Yanga
 JK akilakiwa na refa Othman Kazi
 JK akiweka saini katika mpira utaochezewa
JK akiweka saini 
 JK akitambulishwa waamuzi
 JK akikagua wabunge wapenzi wa Yanga
 JK akisalimiana na straika mkali wa Yanga kutoka DRC
 Hiki kifriji vipi.....
 JK akisalimiana na wabunge wa Yanga. Huyu ni Esther Bulaya
 JK akisalimiana na mwenyekiti wa kamati ya ufundi wa Yanga
JK akisalimiana na kiongozi-mchezaji wa Yanga
 JK akisalimiana na mshambuliaji hatari wa yanga Halima Mdee

 JK akisalimiana na nahodha wa Simba Amos Makala
 JK akisalimiana na Simba
 JK akisalimiana na mchezaji wa kulipwa wa wabunge toka Nzega, Dkt Hamisi Kigwangalla
 JK akisalimiana na Profesa Maji Marefu
 JK akisalimiana na wachezaji wabunge wa Simba
 JK akisalimiana na mshambukliaji hatari wa Simba William Ngeleja
 JK akiendelea kusalimia wabunge wana Simba
 JK akisalimiana na beki tatu wa wabunge wa Simba Joshua Nassari
 Haya waheshimiwa... mchezo mwema...
 Nyimbo ya Taifa ikipigwa, kila mtu mguu sawa
 Wimbo wa Taifa 
 JK akipungia umati unaomshangilia kwa nguvu
 JK akipena mkono na mashabiki
 JK akiteta jambo na JB huku Dkt Cheni akiwa pembeni
 Mashabiki wakiwa nje ya uwanja
 Nyomi ya nje inapita ya ndani
Mshabiki wa Yanga akielekea uwanjani.

*MADEREVA WA WEEKEND HATARI TUPU

$
0
0
 Gari dogo likitolewa mtaroni njia panda ya kutoka Tangbovu kuelekea Goba, jana mchana. Haikuweza kufahamika chanzo cha ajali hiyo iliyosababisha dereva huyo kuingia mtaroni mchana kweupe.
 Zoezi la kutoa gari hiyo likiendelea.....
Askari wa usalama barabarani akisimamia zoezi hilo.....

*MHE. ALI HASSAN MWINYI, MASANJA, SHILOLE WATIA FORA TAMASHA LA UTAMADAUNI WA KISWAHILI MAREKANI

$
0
0
Dj Luke akiambatana na mgeni wake Mhe. Ali Hassan Mwinyi kuelekea ukumbini kulikofanyika Tamasha la Utamaduni wa kiswahili na sherehe ya miaka 3 ya Vijimambo Jumamosi July 6, 2013 na kuwa tamasha la kihistoria lililohudhuriwa na Watanzania wakiwemo wadau wanaozungumuza Kiswahili wapatao 600 kutoka kila kona hapa Marekani, Ulaya na Tanzania.
Kutoka kushoto ni Dj Luke, Mhe, Ali Hassan Mwinyi, Mhe. Ramadhan Muombwa Mwinyi, Mama Lily Munanka, Idd Sandaly na Baraka Daudi katika picha ya pamoja wakati wakiingia ukumbini.
Watoto wa darasa la Kiswahili DMV wakiimba wimbo wa Taifa.
Mwenyekiti wa kamati ya maandalizi akiongea machache kabla ya kumkaribisha Dj Luke.
Dj Luke akisoma hotuba yake kabla ya kumkaribisha Kaimu Balozi wa Tanzania nchini Marekani, Mama Lily Munanka.
Kaimu Balozi Mama Lily Munanka akishukuru kamati ya maandalizi na kumkaribisha mgeni rasmi Rais Mstaafu Ali Hassan Mwinyi. ZAIDI BOFYA HAPO CHINI

Rais Mstaafu Ali Hassan Mwinyi akihutubia mamia ya Watanzania waliofika kwenye Tamasha la Utamaduni wa Kiswahili na sherehe ya miaka 3 ya Vijimambo na kulifungua rasmi.
Mwenyekiti wa Jumuiya ya Watanzania New York, Bwn. Haji akisoma shairi alilotunga maalum kwa ajili ya sherehe ya miaka 3 ya Vijimambo na tamasha la Utamaduni wa kiswahili Marekani.
Shilole na Masanja mkandamizaji wakikandamiza na kugaragaza kwenye Tamasha la Utamaduni wa Kiswahili na miaka 3 ya sherehe ya Vijimambo.
Shilole(mwenye gauni la punda milia) akimnyanyua Afisa Ubalozi Mindi Kasiga kwenye moja ya nyimbo zake alizotumbuiza kwenye tamasha hilo.
Mhe. Ali Hassan Mwnyi akiaga na kuelekea kwenye gari lililomleta tayari kwa kuondoka baada ya kumaliza sehemu ya kwanza ya tamasha hilo na sherehe ya miaka 3 ya Vijimambo.
Mhe. Ali Hassan Mwinyi akiwa tayari kuondoka.
kwa picha zaidi bofya read more.




*UMOJA WA MATAIFA YANYAKUA TUZO MAALUM KWA KUTAMBUA MCHANGO WAO WA KUHAMASISHA JAMII KATIKA MAONYESHO YA 37 YA KIMATAIFA YA BAISHARA JIJINI DAR.

$
0
0
photo (26)
Waziri Mkuu Mizengo Pinda akisaini kitabu cha wageni alipotembelea Banda la Shirika la Umoja wa Mataifa kwenye maonyesho ya 37 ya Biashara ya Kimataifa yaliyofikia tamati jana kwenye viwanja vya Mwl. Julius Nyerere jijini Dar. Waziri Mkuu aliambatana na Waziri wa Viwanda na Biashara Dk. Abdallah Kigoda pamoja na Mratibu Mkazi wa Umoja wa Mataifa nchini Dk. Alberic Kacou.
photo (29)
Waziri Mkuu Mizengo Pinda ( wa pili kushoto) akipata maelezo kutoka kwa mmoja wa Wajasiriamali wanaofadhiliwa na UNIDO kwenye banda la Shirika la Umoja wa Mataifa akiwa ameambatana na Waziri wa Viwanda na Biashara Dk. Abdallah Kigoda (kushoto) pamoja na Mratibu Mkazi wa Umoja wa Mataifa nchini Dk. Alberic Kacou (wa pili kulia) wakati wa sherehe za kufunga Maonesho ya 37 ya Biashara ya Kimataifa jijini kwenye viwanja vya Mwalimu Julius Nyerere leo.
photo (25)
Mratibu Mkazi wa Umoja wa Mataifa Dk. Alberic Kacou akipokea Tuzo ya Ngozi iliyotengenezwa kinyumbani kutoka kwa Wajasiriamali wanaodhaminiwa na UNIDO wakati alipotembelea Banda la Shirika hilo leo kwenye maonyesho ya 37 ya Kimataifa ya Biashara yalifungwa rasmi jana na Waziri Mkuu Mh. Mizengo Pinda. ZAIDI BOFYA HAPO CHINI

photo (31)
Mkufunzu wa Taasisi ya Teknolojia Dar es Salaam ( DIT) Marwa Wambura (kulia) akitoa maelezo kwa Mratibu Mkazi wa Umoja wa Mataifa nchini Dk. Alberic Kacou ya malighafi za ngozi zinazotumika kutengeneza bidhaa mbalimbali na wajasiamali wanaofadhiliwa na Shirika la Umoja wa Mataifa la kuendeleza viwanda Duniani (UNIDO).
photo (24)
Mratibu Mkazi wa Umoja wa Mataifa nchini Dk. Alberic Kacou akiwa kwenye picha ya pamoja na wafanyakazi wa vitengo mbalimbali vya Ofisi za Umoja wa Mataifa nchini. (UN-Tanzania Delivering as one).
photo (30)
Banda la Umoja wa Mataifa kwenye maonyesho ya Sabasaba likiwa limeandika ujumbe unaosema "Umoja wa Mataifa inafanya kazi kwa ajili yako-kuboresha maisha ya watoto, wakinamama na vijana".
photo (28)
Mratibu Mkazi wa Umoja wa Mataifa nchini Dk. Alberic Kacou alipotembelea banda la Wizara ya Fedha wakiwa ni wadau washirika wa Maendeleo nchini.
photo (27)
Mratibu Mkazi wa Umoja wa Mataifa nchini Dk. Alberic Kacou akibadilishana mawazo na mmoja wa wadau alipotembelea banda la Wizara ya Fedha ikiwa ni kudumisha ushirikiano na Serikali ya Tanzania.

*PAMBANO LA HALIMA MDEE NA JACQUELINE WOLPER HAKUNA MBABE

$
0
0
 Mbunge wa Kawe Halima Mdee (kushoto) akichana na Msanii wa Bongo Movie, Jacqueline Wolper, wakati wa Tamasha maalum la Usiku wa Matumaini, lililofanyika jana kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam. Katika pambano hilo Mabondia hao walitooka sare kwa pointi.
 Bondia Halima Mdee akiingia kwa mbwembwe.
Wolper akipanda ulingoni kwa mbwembwe.

*MAKAMU WA RAIS DKT. BILAL AFUNGUA MKUTANO WA 32 WA WADAU WA POSTA KWA NCHI ZA AFRIKA, JIJINI ARUSHA LEO

$
0
0
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akifungua Mkutano wa 32 wa Wadau wa Posta kwa Nchi za Afrika, ulioanza jijini Arusha leo, Mkutano huo umehudhuriwa na wadau wa Posta kutoka nchi za Afrika.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akifungua Mkutano wa 32 wa Wadau wa Posta kwa Nchi za Afrika, ulioanza jijini Arusha leo, Mkutano huo umehudhuriwa na wadau wa Posta kutoka nchi za Afrika.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiongozana na baadhi ya Viongozi, Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia, Prof. Makame Mbarawa (kushoto) Katibu Mkuu wa Shirikisho la Posta kwa Nchi za Afrika (PUPA) Younouss Djibrine (kulia) na Prof. John Nkoma, Mkurugenzi wa Mawasiliano Tanzania (wa pili kulia), wakati akiwasili kwenye Ukumbi wa AICC jijini Arusha leo kwa ajili ya kufungua Mkutano wa 32 wa Wadau wa Posta kwa Nchi za Afrika, ulioanza jijini Arusha leo.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akizungumza jambo na Katibu Mkuu wa Shirikisho la Posta kwa Nchi za Afrika (PUPA) Younouss Djibrine, wakati wa ufunguzi wa Mkutano wa 32 wa Wadau wa Posta kwa Nchi za Afrika, ulioanza jijini Arusha leo. Mkutano huo umehudhuriwa na wadau wa Posta kutoka nchi za Afrika.
 Baadhi ya washiriki wa mkutano huo wakimsikiliza Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, wakati akifungua rasmi mkutano huo leo kwenye Ukumbi wa AICC, jijini Arusha.
 Baadhi ya washiriki wa mkutano huo wakimsikiliza Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, wakati akifungua rasmi mkutano huo leo kwenye Ukumbi wa AICC, jijini Arusha.
 Kikundi cha Kwaya cha Jijini Arusha kikitoa burudani.
 Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia, Prof. Makame Mbarawa, akizungumza machache kabla ya kumkaribisha Mhe. Makamu wa Rais kufungua mkutano huo.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya washiriki baada ya kufungua mkutano huo.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya washiriki baada ya kufungua mkutano huo.

*ROTARY CLUB MZIZIMA DAR ES SALAAM, YAPATA RAIS WAKE BAADA YA KUCHAGULIWA TENA

$
0
0
 Rais wa klabu ya Rotary ya Mzizima Dar es salaam, Rotarian Ambrose Nshala (kulia), akimvisha pini rotarian mpya, Mhandisi Dennis, wakati wa hafla ya kumsimika rais mpya wa klabu hiyo jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki. Rais huyo amechaguliwa kwa mwaka wa pili kushika uongozi huo. 
  Rais wa klabu ya Rotary ya Mzizima Dar es Salaam, Rotarian Ambrose Nshala (kulia), akimpa nyaraka rotarian mpya wa klabu hiyo, Paul Mashauri katika hafla hiyo jijini Dar es Salaam.
 Rais mpya wa klabu ya Rotary ya Mzizima, Dar es Salaam, Rotarian Ambarose Nshala (kulia), akimvisha pini mmoja wa wajumbe wa bodi ya klabu ya Rotary ya Mzizima, Rotarian Edith Lyimo katika hafla hiyo jijini Dar es Salaam. Wengine kutoka kushoto ni wajumbe wa bodi hiyo, Emeria Mugonzibwa na Rotarian Ailinda Sawe. 
 Rais wa Rotary klabu ya Mzizima, Rotarian Ambrose Nshala (kushoto) akiwaongoza wanachama wengine wa klabu hiyo kuselebuka katika hafla ya kmsimika rais na viongozi wengine wa klabu hiyo jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki.
 Baadhi ya wanachama wa klabu ya Rotary ya Mzizima, Dar es Salaam wakijimwaga ukumbini katika hafla hiyo jijini humo mwishoni mwa wiki.
Wasanii wa kikundi cha Safi Theatre Group wakifanya vitu vyao katika hafla ya kumsimika rais na viongozi wengine wa klabu ya Rotary ya Mzizima jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki.
Viewing all 13053 articles
Browse latest View live


<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>