Quantcast
Channel: SUFIANIMAFOTO
Viewing all 13053 articles
Browse latest View live

*USIKU WA SHEREHE YA MIAKA 3 YA VIJIMAMBO NA TAMASHA LA UTAMADUNI WA KISWAHILI MAREKANI ULIVYOBAMBA

$
0
0
Meza waliyokaa Kaimu Balozi Mama Lily Munanka baadhi ya wageni walikuja na masafara wa Rais Mstaafu Ali Hassan Mwinyi wakibadilishana mawazo huku wakicheka kwenye usiku wa sherehe ya miaka 3 ya Vijimambo na tamasha la Kiswahili Marekani lilofanyika Jumamosi July 6, 2013.
Afisa Ubalozi Suleiman Saleh pamoja na mkewe (kushoto) katika picha ya pamoja na Tina Magembe.
Afisa Ubalozi wa Tanzania nchini Marekani na mkwewe katika pivha ya pamoja na Kulwa (kati) kutoka North Carolina aliyekuja kwenye sherehe ya miaka 3 ya Vijimambo na tamasha la utamaduni wa Kiswahili kama muakilishi wa DICOTA.
Shilole na Masanja wakipagawisha wadau wa Kiswahili kwenye sherehe ya miaka 3 ya Vijimambo na tamasha la Kiswahili Marekani.
Shilole akicheza na Salha kwenye moja ya nyimbo zake alizopagawisha kwenye sherehe ya miaka 3 ya Vijimambo iliyofanyika Jumamosi July 6, 2013.
Shilole akizidi kuwasha moto.
Ulikuwa ni usiku wa Vijimambo kuandika historia mpya.
Dj Luke (kushoto) katika picha ya pamoja na Afisa Ubalozi wa Tanzania nchini Marekani, Mindi Kasiga (kati) na mwenyekiti wa kamati Baraka Daudi.
Vijana na wadau wakubwa wa kiswahili wakipata picha ya pamoja.
Hamprey mdau wa Kiswahili toka North Carolina.
kwa picha zaidi bofya read more. MATUKIO ZAIDI BOFYA HAPO CHINI






*TIMU YA MWACHA ALALE UTD YATWAA UBINGWA WA KOMBE LA ZAWEDA JIMBO LA KITOPE UNGUJA

$
0
0
 Mbunge wa Jimbo la Kitope ambae pia ni Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif akikabidhi Seti ya TV Flat Screen kwa Timu ya Soka ya Mwache  Alale United baada ya kuibuka na ushindi wa godi 5 – 3 dhidi ya African Boys ya Upenja kwenye mchezo wa Fainal ya Kombe wa Zaweda.
Nahodha wa Timu ya Soka ya Mwache Alale Abdullghani Gullan akipokea kikombe kutoka kwa Mbunge wa Jimbo la Kitope Balozi Seif Ali Iddi mara baada ya timu yake kuibuka na ushindi wa 5-3 dhidi ya African Boys ya Upenja. Pambano hilo lilichezwa katika uwanja wa Kitope na kushuhudiwa na Mbunge huyo Balozi Seif. Picha na Hassan Issa wa –OMPR – ZNZ.
************************
Hatimae Timu ya Soka ya Mwacha Alale United imeibuka na ubingwa wa mashindano ya Kombe la Zaweda ndani ya Jimbo la Kitope baada ya kuilaza Timu ya African Coast ya Upenja kwa mabao 5 – 3 yaliyopatikana kwa njia ya Penalti katika pambano la fainali lililochezwa kwenye uwanja wa Kitope.

Pambano hilo lililokuwa na ushindani mkali kwa timu zote mbili lilichezwa kwa dakika 90 bila ya mshindi lilishuhudiwa na wapenzi kadhaa wa mchezo wa soka wakiongozwa na Mbunge wa Jimbo la Kitope Balozi Seif Ali Iddi.

Mabingwa hao wapya wa Kombe la Zaweda Mwache Alale United  walifanikiwa kupata ushindi huo baada ya kufunga Penalti zote tano wakati wapinzani wao African Boys ya Upenja wakapata Penalti tatu na kupoteza moja.

Mgeni rasmi wa pambano hilo Mbunge wa Jimbo la Kitope Balozi Seif alikabidhi zawadi kwa bingwa wa mashindano hayo, mshindi wa pili pamoja  na zawadi kwa  timu zote zilizoshiriki katika mashindano hayo ambayo ni ya pili kufanyika tokea kuanzishwa kwake mwaka uliopita.

Balozi Seif aliwakabidhi mabingwa wa Kombe hilo Mwacha Alale United Seti moja ya TV, King’amuzi chake, shilingi 300,000/- taslimu, seti moja ya jezi, mpira pamoja na Kikombe cha ubingwa.

Mshindi wa Pili African Boys ya Upenja ikakabidhiwa shilingi  laki 150,000/- Taslimu, seti moja ya jezi, pamoja na mpira wakati mshindi wa Tatu Mahonda Kids wakaibuka na Seti moja ya jezi, shilingi 75,000/- taslim pamoja na Mpira.

Mchezaji bora na mdogo kuliko wote katika mashindano hayo alikuwa Said Khamis Kidagaa aliyepata zawadi ya shilingi 20,000/- taslimu na  Mfungaji bora wa mashindano hayo Abdull Nyafu wa African Coast ya Upenja alipata zawadi ya shilingi 20,000/-.

Mchezaji bora wa mashindano hayo Ali Alawi na Golkipa bora Siad Abdulla kutoka Timu ya Zaweda wamepata zawadi ya shilingi 20,000/- taslimu kila mmoja wakati zawadi ya shilingi 50,000/- Taslimu kwa timu bora katika mashindano hayo ilichukuliwa na timu ya soka ya Zaweda.

Muamuzi bora wa mashindano hayo aliibuka Haroun Kuchi aliyefanikiwa kupata zawadi ya shilingi 20,000/- taslim pamoja na mpira mmoja mmoja kwa kila timu ilizoshiriki katika mashindano hayo.

Timu zilizoshiriki mashindano hayo ya Zaweda Cup ni pamoja na Mbuyuni, Fujoni Boys, Mahonda Union, Kitope United,Zaweda, Mgambo F.C, Kilimani City, Kibweni Youth Organization, New Star, Mahonda Kids,washindi wa Pili African Boys ya Upenja na Mabingwa wa mashindano hayo Mwacha Alale United.

Mapema Mbunge huyo wa Jimbo la Kitope Balozi Seif alikabidhi zawadi kwa washindi wa mchezo wa Pete wanawake ambapo bingwa ni watanashati wa Kitope waliopata shilingi laki 100,000/- Taslimu, Mpira  pamoja na Seti ya Jezi.

Mshindi wa pili wa mchezo huo wa netball ni timu ya wanawake ya kiwengwa iliyozawadiwa shilingi laki 100,000/- Taslimu, Mpira na Seti ya Jezi.

Akizunguma mara baada ya pambano hilo la fainal na zawadi Mbunge huyo wa Jimbo la Kitope Balozi Seif aliwakumbusha wana michezo nchini kuendelea kushikamana katika michezo ili kuleta upendo michezoni na ndani ya Jamii.

Balozi Seif aliwatahadharisha wanamichezo hao kuvitumia viwanja vya michezo kwa mnasaba wa kiungwana na ustaarabu na kuacha tabia ya kuvifanya viwanja hivyo kuwa ni maeneo ya kuporomoshwa kwa matusi.

“ Haipendezi kuona maeneo ya viwanja vya michezo nchini yanakuwa sehemu ya kuporomoshwa matusi ambayo mara nyingi huelekezwa kuwakashifu viongozi wanaowaongoza wanamichezo hao “. Aliasa Balozi Seif.

Aliwapongeza Wanamichezo pamoja na uongozi wa Kamati ya mashindano hayo ya Zaweda Cup  kwa juhudi zao zilizosaidia kukamilisha mashindano hayo kwa amani na furaha.

Jumla ya shilingi Milioni 2,700,000/- zimetumika kugharamia vifaa mbali mbali vya mashindano hayo ya Zaweda Cup katika ununuzi wa TV, jezi mipira pamoja na kikombe.
 
Othman Khamis Ame
Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar

*WALIOMEREMETA MWISHONI MWA WIKI HII NI ANTHONY NA GEMA

$
0
0
 Harusi:Ndugu Antony David Mtavangu na Gema Nicholaus Temba wakila kiapo cha kuishi pamoja katika kanisa la Mtakatifu Peter ,siku ya Jumamosi tarehe 6 Julai 2013.
 Antony na mkewe Gema wakiwa wamependeza sana katika siku yao ya harusi.
 Antony Mtavangu na Bi. harusi Gema wakiwa kwenye picha ya pamoja na wasimamizi wao.
Saleh Saphy akizungumza kwa niaba ya wanafunzi waliosoma na Antony, chuo kikuu cha Mysore India, pamoja na kumtaka Antony maarufu kama 'Tony Yayo' kumtunza mkewe , vijana hao walimtakia maisha mema na kamwe kutomlisha mkewe 'Egg Puf '.

*TACAIDS WITH HAPPY FACES TO HAVE THEIR NEW BUILDING

$
0
0
By Immaculate Makilika - Maelezo
 
Tanzania Commissions for AIDS (TACAIDS)   is happy to welcome their partners to their new building which is located at Sokoine drive/ Luthuli road Dar es salaam .Chief Executive Officer  of TACAIDS  Mrs. Fatma Mrisho said “We wanted  to enjoy today  with you partners – let us  rejoice  together with this wonderful building “.
 
TACAIDS workers could not help themselves from smiling when welcoming their partners to their new building, some even said how much this building mean to them. So seeing this building it means more work, more challenges and still their gratitude for that.
 
The achievement of having new building shade happy tears to their faces since they worked under very difficult situation as they were in previous building. They faced a lot of challenges starting with enough space and comfortable environment.
 
Councilor of Embassy Denmark, Mr. Torben Larsew whose presence was very much appreciated, gave a word of congratulations to CEO Mrs. Mrisho for managing to have new building; he also said “enjoying building was long and tough fight for you” while Mrs Mrisho added “a fight worth fighting” and everybody laughed.
 
TACAIDS was first established by the President on 1 December 2000 by Act No. 22 of 2001. These steps were taken so as to ensure that, the Government of the United Republic of Tanzania has an institution which is legally mandated to provide strategic leadership and to coordinate as well as strengthen efforts of all stakeholders involved in the fight against HIV/AIDS.

*RAIS KIKWETE AKUTANA NA WAZIRI WA MAMBO YA NJE WA INDI, SPIKA WA BUNGE LA KOREA YA KUSINI NA KUAGANA NA BALOZI WA UHOLANZI

$
0
0
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akiagana na Balozi wa Uholanzi Mhe.Dkt.Ad Koekkoek anayemaliza muda wake wa uakilishi nchini. Balozi huyo baadaye alifanya mazungumzo na Rais Kikwete ikulu jijini Dar es Salaam leo asubuhi.
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akizungumza na Spika wa bunge la Korea ya Kusini Mhe.Hee Chang wakati  spika huyo na ujumbe wake walipomtembelea Rais ikulu jijini Dar es salaam leo.
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akiagana na Spika wa Bunge la korea ya Kusini Mhe.Hee Chang baada ya kufanya naye mazungumzo ikulu jijini Dar es Salaam leo.
Spika wa bunge la Korea Mhe.Hee Chang (kulia) akimfurahia  Simba aliyekaushwa na kupamba lango la  ikulu  leo asubuhi. Kushoto ni mwenyeji wake,Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete.
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akiwa katika mazungumzo na Waziri wa Mambo ya nje wa India Mhe.Preneet Kaur ikulu jijini Dar es Salaam  leo.
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akiwa katika picha ya pamoja na Waziri wa Mambo ya nje wa India Mhe.Preneet Kaur(wapili kushoto) na ujumbe wake ikulu jijini Dar es Salaam leo.kulia ni Waziri wa Mambo ya nje na Ushirikiano wa Kimataifa Mhe.Bernard Membe Picha na Freddy Maro

*RAIS TENGA KUFUNGUA KOZI YA BEACH SOCCER

$
0
0
Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Leodegar Tenga atakuwa mgeni rasmi kwenye ufunguzi wa kozi ya mpira wa miguu wa ufukweni (beach soccer) itakayoanza kesho (Julai 9 mwaka huu) jijini Dar es Salaam.

Kozi hiyo itafanyika kwa wiki nzima kwenye klabu ya Escape iliyoko karibu na Safari Carnival, Mikocheni karibu na makao makuu ya Jeshi la Kujenga Taifa (JKT)- JKT Mlalakuwa. Uzinduzi utafanyika saa 3 kamili asubuhi.

Washiriki wa kozi hiyo itakayokuwa chini ya wakufunzi kutoka Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu (FIFA) ni 60 ambapo 30 ni makocha wa mpira wa miguu na 30 wengine ni waamuzi wa mpira wa miguu.

Wakufunzi hao wa FIFA ni Angelo Schirinzi kutoka Uswisi kwa upande wa makocha wakati George Postmar kutoka Uholanzi ndiye atakayewanoa waamuzi.

*PROGRAMU YA MAZOEZI YA TAIFA STARS

$
0
0
Taifa Stars chini ya Kocha Kim Poulsen inaendelea kujinoa jijini Dar es Salaam tayari kuikabili Uganda (The Cranes) katika mechi ya kufuzu kwa Fainali za Afrika kwa Wazhezaji wa Ligi za Nyumbani (CHAN) itakayochezwa Jumamosi (Julai 13 mwaka huu) Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

*Ratiba ya mazoezi kwa Taifa Stars ni kama ifuatavyo;
Jumanne- Julai 9 mwaka huu      Saa 9 alasiri        Uwanja wa Taifa
Jumatano- Julai 10 mwaka huu   Saa 9 alasiri        Uwanja wa Taifa
Alhamisi- Julai 11 mwaka huu         Mapumziko
Ijumaa- Julai 12 mwaka huu       Saa 10 jioni         Uwanja wa Taifa

*UZINDUZI WA GATI MPYA YA ABIRIA MALINDI MJINI ZANZIBAR

$
0
0
 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein, akifungua pazia kama ishara ya uzinduzi wa Bandari mpya  ya Abiria katika bandari ya Malindi Zanzibar leo.mchana (kushoto) Sheikh  Said Salum  Bakhresa.
  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,akipta maelezo kutoka kwa mfadhili wa Kampuni ya ujenzi wa Bandari mpya ya Abiria,Sheikh Said Salum Bakhresa,wakati alipotembelea ukumbi wa VIP,na Business Class,katika sherehe za ufunguzi wa Bandari mpya  ya Abiria katika bandari ya Malindi Zanzibar leo.mchana.
 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,alitembelea sehemu mbali mbali katika ikiwemo IMMIGRATION DEPARTURES pamoja na Viongozi aliofuatana nao baada ya kugungua Bandari ya Abiria katika Bandari ya Malindi Mjini Zanzibar.
 
 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,akipata maelezo kutoka kwa  Injinia Mkuu wa Shirika la Bandari Mbarouk Hamad,(katikati) wakati alipotembelea sehumu ya Kuegeshea Meli ya Mizigo katika sherehe za  ufunguzi wa Bandari mpya  ya Abiria katika bandari ya Malindi Zanzibar leo mchana.
 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,alipokuwa akizungumza na wananchi na waalikwa katika sherehe za ufunguzi wa Bandari mpya  ya Abiria katika bandari ya Malindi Zanzibar leo.mchana,(kushoto) Naibu Waziri wa Mawasiliano na Miundimbinu Issa Haji Ussi (Gavu) Harison Mwakiembe Waziri wa Miundombinu Bara,na Sheikh Said Salum Bakhresa (kulia). Picha na Ramadhan Othman, Ikulu.

*KIJANA AJILIPUA KWA MAFUTA YA PETROLI MJINI DODOMA, KISA WIVU WA MAPENZI

$
0
0
Picha na Maktaba ya Sufianimafoto.
Na Mwandishi Wetu, DODOMA, Tanzania
Mwanafunzi wa Chuo cha Ufundi (VETA) cha mkoani Dodoma, aliyejulikana kwa jina la Taliki Juma (22), amedaiwa kujiua kwa staili ya kujilipua kwa mafuta ya Petroli hadi kufa kwa kisa cha mapenzi. 

Taarifa zilizoufikia mtandao huu, zinasema kuwa katika tukio hilo ulizuka moto mkali jambo lililosababisha watu wengine wanane kujeruhiwa na moto huo. 

Tukio hilo limethibibitishwa na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma, David Misime, aliyeeleza kuwa tukio hilo lilitokea jana majira ya saa 12:30 jioni katika Kitongoji cha Machaka Kata ya Nzughuni mkoani humo. 

Aidha Kamanda huyo alifafanua kwamba, awali mwanafunzi huyo, alionekana akitoka katika Kituo cha kuuzia mafuta cha Nane Nane, huku akiwa amenunua mafuta ya Petroli Lita tano, na kwenda nayo hadi katika Saluni moja ya Irene Mapunda, anayesadikiwa kuwa ndiye aliyekuwa mpenzi wake, na kisha kujimwagia na kujiwasha moto. 

Wakielezea tukio hilo baadhi ya mashuhuda waliokuwa karibu, walisema kuwa baadhi ya watu walipomuona akianza kujimwagia mafuta hayo walijaribu kumsihi na kumshika ili asijilipue lakini aliwashinda nguvu na kuingia ndani ya Saluni hiyo na kuwasha kiberiti na kusababisha moto mkubwa kuwaka na kuwajeruhi watu waliokuwamo na kuteketeza mali zote zilizokuwa katika Saluni hiyo. 

 ''Uchunguzi wa awali unaonyesha kuwa chanzo cha tukio hilo ni wivu wa kumapenzi, hata hivyo Jeshi la Polisi Mkoa wa Dodoma bado linaendelea na uchunguzi wa kina juu ya tukio hili'' alisema Kamanda Misime. 

*MEDIA ADVISORY LAUNCH OF WORLD INVESTMENT REPORT 10 July 2013 at ILO

$
0
0
The United Nations systems in Tanzania in collaboration with the Tanzania Investment Centre (TIC) ) cordially invites the media to the launch of 2013 World Investment Report (WIR)  subtitled : "Global Value Chains – Investment and Trade for Development". The launch will be held at ILO Conference Hall, along Maktaba Street on Wednesday, 10 July, 2013, at 1000-1130am. 


The WIR is the United Nations Conference on Trade and Development ( UNCTAD) annual flagship report, analysing trends in foreign direct investment (FDI) worldwide, at the regional and country levels, as well as emerging issues around the investment-development nexus. Each year, the Report selects a specific topic related to FDI and development. The report will be launched by the TIC Executive Director, Ms Juliet Kairuki and UNCTAD’s Chief of Technical Cooperation Ms. Manuela Tortora.


This year's theme, is important from a policy perspective since it goes to the heart of countries' sustainable development strategies in respect of global value chains (GVCs). In this context, the Report provides in-depth analysis of recent developments with regard to GVCs, their impact on trade, investment and sustainable development and – based on these findings – identify policy challenges and recommendations. The Report will therefore address questions such as:

·  How do international production networks of transnational corporations (TNCs) shape
value added trade?
·  In which countries and which industries are GVCs most significant?
· What is the impact of value added trade and GVCs on sustainable development?
· How should policymakers reflect the growing importance of GVCs in countries’
development strategies?
· How to maximize development benefits from integrating into GVCs and how to
minimize associated risks?
EVENT:           LAUNCH OF  2013 WORLD INVESTMENT REPORT    
                                     
DATE:             10 JULY, 2013

TIME:              1000 AM

VENUE:          ILO CONFERENCE HALL, ALONG MAKTABA STREET

CONTACT: 
Usia Nkhoma Ledama
National Information Officer
Mobile: 0762 871830 / 0784 228539

*DEREVA MWANAMAMA ASABABISHA AJALI, AMTELEKEZA MAJERUHI, AENDA SALUNI KUSETI NYWELE

$
0
0
Tukio lilikuwa kama hivi:- Dereva wa Pikipiki ya miguu mitatu, ambaye hakuweza kufahamika jina lake mapema, akiwa amelala chini huku akiugulia maumivu baada ya kugongwa na gari ndogo aina ya Pajero i0 Mitsubishi, yenye Namba za usajili T 179 BRU. 
Ajali hiyo imetokea mwishoni mwa wiki hii eneo la Samaki Mbezi Beach jijini Dar es Saalm, baada ya dereva huyo mwanamama kukata kona ghafla ya kuingia njia ndogo ili kuelekea Saluni kwa ajili ya kuseti Nywele. 
Jamaa mmoja (kulia) akianza kumuita mama huyo ili kufika eneo la tukio ili kumsaidia kijana huyo, mama akitoka Saluni....

Baada ya ajali hiyo mwanamama huyo hakuweza kuonyesha ushirikiano wala kusimama bali aliendelea na safari yake hadi katika Saluni moja iliyo karibu kabisa na eneo la tukio na kushuka garini na kisha kuingia saluni humo na kuanza kuendelea na utaratibu wa ratiba yake kuanza kusetiwa nywele. 

Jambo hilo liliwaudhi sana watu mashuhuda wa tukio hilo, ambao baada ya kuona kamera ya Sufianimafoto ikiwa kazini walianza kusema ya moyoni, ''Sasa wewe mwandishi unapiga picha na kuandika habari we unaona hivi ni sawa kweli wakati mgonjwa anaugulia maumivi bila hata huduma ya kwanza wala kupelekwa hospitali wakati mhusika aliyemgonga ameonekana na anaendelea na shughuli zake tu pale saluni, ameingia kuseti nywele''. alisema mama mmoja aliyeonekana kukerwa na jambo hilo.

Baada ya kusikia hivyo kamera ya Mafoto ilielekea hadi katika saluni hiyo pamoja na watu waliokuwapo eneo hilo huku wengi wao wakilalama kila mmoja akitukana kivyake, na kumkuta mama huyo akianza kuingia katika Draya kuanza kusetiwa nywele zake, na alipoitwa na mmoja wa watu hao, mama huyo alionyesha dharau na kuendelea na utaratibu wake.

Jambo hilo lilimkera kila aliyefika katika mlango wa saluni hiyo na watu kushikwa na hasira huku kila mmoja akianza kutukana na kuingia bila utaratibu katika chumba cha saluni hiyo jambo lililowafanya wafanyakazi wa saluni hiyo kuingilia kati na kumsihi mama huyo kutoka nje.

Mama huyo alipotoka nje na kuhojiwa kulikoni kugonga mtu na kumuacha kama alivyo na akaekea kuseti nywele, Mama huyo alijibu:- ''Tayari nimesha muita ndugu yangu anakuja na Tax kuja kumpeleka hospitali kwa hiyo asubiri, kwanza sikumgonga mimi, mimi nimemgusa tu baada ya kugongwa na gari ya GX 100 iliyokimbia, kwa hiyo asubiri'', alisema mama huyo

Baada ya watu hao kusikia kauli hiyo walikuja juu na kumzonga mama huyo wakitaka kumshushia kichapo, hatimaye mama huyo aliamua kukimbilia ndani ya Saluni hiyo na kufungiwa huku watu hao wakijadiliana kulichoma moto gari lake lililokuwa limeegeshwa mbele ya Saluni.

Ilielezwa kuwa baadaye alifika ndugu wa huyo mama akiwa na gari lakini tayari kijana huyo akawa tayari ameshapata msaada ya kuwahishwa hospitali. CHEKI TUKIO KAMILI CHINI 
 Kijana huyo akiwa amelala chini akiugulia maumivu huku mzigo wake wa Kreti za Bia na Soda zikiwa zimevunjika baada ya kutumbukia mtaroni.
 Raia wakimwangalia kijana huyo huku wakishindwa kumsaidia wakibaki kujadili kuhusu mama huyo aliyemgonga na kwenda kuingia Saluni huku watu wakishindwa kumchukulia hatua.
 Kijana mmoja akijaribu kusaidia kuokota baadhi ya vinywaji ambavyo vilikuwa havijavunjika.
 Mama akijielezea kujaribu kujitetea.....
 Mama akielekea kuonyesha sehemu ya nyuma ya gari lake anayodai kuwa ndipo alipojigonga dereva huyo wa Pikipiki.
 Ghafla alizongwa na watu, hapa akijaribu kuwaka 'eti' asisogelewe, lakini wapi watu hao walimzonga...
 Hapa wakiwa tayari wamemuweka mtu kati...huku kila mmoja akiwaka kivyake kuhusu dharau za mama huyo...
 Majadiliano yakiendelea...
Watu wakaiwa katika mlango wa Saluni hiyo wakimtaka mama huyo kutoka nje baada ya kukimbilia ndani.

*WALIOKAMATWA NA UNGA WA MABILIONI SAUZI NI AGNES HUYU HUYU WA MASOGANGE?

$
0
0
Wote ni Watanzania,walianzia safari Dar,washikiliwa Afrika Kusini

Wanawake wawili raia wa Tanzania wametambuliwa kuwa diyo wanaodaiwa kuingiza shehena ya dawa za kulevya zenye thamani ya zaidi ya Sh. bilioni 6.8 nchini Afrika Kusini wakitokea Tanzania.

Akizungumza na NIPASHE jana, Kamanda wa Polisi Kitengo cha Kuzuia na Kupambana na Dawa za Kulevya, Geofrey Nzoa, alisema haijafahamika wanawake hao wanatoka mikoa gani.

Kamanda Nzoa aliwataja wanawake hao kuwa ni Agnes Jerald ambaye alisema hajapiga hesabu ya umri wao, ila alizaliwa mwaka 1988 kwa maana hiyo ana umri wa miaka 25 na Melisa Edward ambaye alisema amezaliwa mwaka 1989 kwa maana hiyo atakuwa na umri wa miaka 24. Wawili hao bado wanaendelea kuhojiwa na polisi wa Afrika Kusini.

Alisema Jeshi la Polisi Nchini kwa upande wake linaendelea kufanya uchunguzi kubaini kama dawa hizo walitoka nazo wapi na pia linawasaka watu ambao watakuwa ndiyo wamiliki wa dawa hizo.

Jumapili iliyopita NIPASHE ilipata taarifa za kukamatwa kwa dawa za kulevya aina ya Crystal Methamphetamine zenye thamani hiyo nchini Afrika Kusini wakati zikisafirishwa kutoka Tanzania.

Taarifa hizo zilionyesha kuwa wanawake wawili walikamatwa katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Oriver Tambo uliopo eneo la Kempton Park siku ya Ijumaa wiki iliyopita wakitokea Tanzania.

Wanawake hao walikamatwa na maofisa wa Mamlaka ya Mapato ya Afrika Kusini wakiwa na masanduku sita ambayo yalipokaguliwa yalikutwa na takribani kilo 150 za dawa hizo ambazo pia zinajulikana kama ‘Tik’ zikiwa na thamani ya bei ya mtaani ya Randi milioni 42 sawa na Sh. bilioni 6.8.



Baada ya kukamatwa na dawa hizo wanawake hao walikabidhiwa polisi.
Tukio hilo linatoka takribani wiki moja baada ya Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, Juni 28, mwaka huu kutangaza kuwa tatizo la dawa za kulenya hivi sasa ni janga la kitaifa nchini.

Alisema kumekuwa na wimbi kubwa la Watanzania wanaojiingiza katika biashara haramu ya dawa za kulevya ndani na nje ya nchi na kwamba, katika kipindi cha miaka mitano iliyopita, watuhumiwa 10,799 walikamatwa kwa kujihusisha na dawa hizo.

Pia alisema katika kipindi hicho, Watanzania 240 walikamatwa katika nchi za Brazil, Pakistan na Afrika Kusini, na hivyo kuharibu taswira ya nchi na kusababisha Watanzania wasio na hatia kupata usumbufu na masharti magumu wanapotaka kusafiri kwenda nchi mbalimbali duniani.

Pinda alisema mwaka huu pekee kumekuwa na ukamataji mkubwa wa dawa za kulevya katika eneo la kimataifa la Bahari ya Hindi karibu na Tanzania.
Alisema hivi sasa mikate, maandazi na askrimu zinazouzwa kwenye shule za msingi, zinawekwa dawa za kulevya.

Alisema vitendo hivyo vinafanya vijana wengi wa shule za msingi na hata sekondari kuwa na tabia za ajabu, ikiwamo kuingia darasani wakiwa na kiatu kimoja mguuni, mkufu wenye nyembe na kidani chenye nyembe kifuani.
 CHANZO: NIPASHE

*UBALOZI WASHINGTON, DC WAMUAGA RAIS MSTAAFU ALI HASSAN MWINYI

$
0
0
Juu na chini ni Rais Mstaafu Mhe. Ali Hassan Mwinyi akiongea machache katika chakula cha jioni alichoandaliwa na Ubalozi wa Tanzania nchini Marekani katika kumuaga baada ya kumaliza ziara ya siku tano aliyofanya Washington, DC na kuwa mgeni rasmi kwenye sherehe ya miaka 3 ya Vijimambo na tamasha la utamaduni wa Kiswahili Marekani lililofanyika Jumamosi July 6, 2013 Capitol Heights, Maryland.
Rais mstaafu Ali Hassan Mwinyi akiingia Ubalozini kwenye chakula cha jioni alichoandaliwa na Ubalozi huo kwa ajili ya kumuaga rasmi baada ya kumaliza ziara yake ya siku tano.
Juu na chini ni Rais mstaafu Ali Hassan Mwinyi akisalimiana na maafisa na wafanyakazi wa Ubalozi wa Tanzania Washington, DC wakiwemo wanakamati wa miaka 3 ya Vijimambo na tamasha la utamaduni wa Kiswahili Marekani/
Rais mstaafu Ali Hassan Mwinyi pamoja na mkewe Sitti Mwinyi (watatu toka kulia) wachukua chakula walichoandaliwa na Ubalozi wa Tanzania nchini Marekani walipoandaliwa rasmi kwa ajili ya kuwaaga.
Afisa Ubalozi Suleiman Saleh akitambulisha wakati mbele ya mgeni rasmi na wageni waalikwa kwenye chakula hicho na kumtakia safari njema .
Mwenyekiti wa Kamati, Bwn. Baraka Daudi akijitambulisha kwa mgeni rasmi na kumtakia safari njema nyumbani.
Kaimu Balozi Mama Lily Munanka katika picha ya pamoja na Rais mstaafu Ali Hassan Mwinyi na mkewe mama Sitti Mwinyi.
Rais Mstaafu Ali Hassan Mwinyi pamoja na mkewe Mama Sitti Mwinyi katika picha ya pamoja na Maafisa wakiwemo wafanyakazi wa Ubalozi wa Tanzania nchini Marekani
Rais mstaafu Ali Hassan Mwinyi pamoja na mkewe Mama Sitti Mwinyi katika picha ya pamoja na kamati ya miaka 3 ya Vijimambo na tamasha la Utamaduni wa Kiswahili Marekani.

*TUME YA KATIBA YAFAFANUA KUHUSU TOLEO LA KIINGEREZA YA RASIMU YA KATIBA

$
0
0
Mwenyekiti-wa-Tume-ya-Mabadiliko-ya-Katiba-Jaji-Joseph-Warioba.
*********************************
Na Mwandishi Wetu
 Tume ya Mabadiliko ya Katiba imetoa ufafanuzi kuhusu Rasimu ya Katiba iliyotolewa hivi karibuni katika lugha Kiingereza na Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC) na kusema rasimu hiyo haitoi tafsiri sahihi ya maudhui ya Rasimu ya Katiba iliyozinduliwa na Makamu wa Rais, Dkt. Mohammed Gharib Bilal Juni 3 mwaka huu (2013).

Rasimu hiyo iliyotolewa na LHRC ambayo inasambazwa kupitia njia mbalimbali ikiwemo mitandao ya kijamii, pia inatumika katika mikutano na warsha mbalimbali zinazojadili kwa lengo la kutoa maoni kuhusu Rasimu iliyotolewa na Tume.

“Tume ya Mabadiliko ya Katiba inapenda kuwafahamisha wananchi na wadau wengine kuwa Rasimu hiyo ya Katiba katika lugha ya kiingereza iliyoandaliwa na LHRC haitoi tafsiri sahihi ya maudhui ya Rasimu ya Katiba iliyotolewa na Tume katika lugha ya Kiswahili na hivyo kupotosha umma kuhusu maudhui ya Rasimu ya Katiba iliyotolewa hivi karibuni,” amesema Katibu wa Tume hiyo, Bw. Assaa Rashid katika taarifa yake kwa Vyombo vya Habari leo (Julai 9, 2013).

Bw. Asaa amewataka wananchi kuendelea kusoma na kutoa maoni kuhusu Rasimu ya Katiba iliyotolewa na Tume ya Mabadiliko ya Katiba katika lugha ya Kiswahili ambayo amesema imesambazwa kwa wananchi, taasisi, jumuiya na taasisi mbalimbali. Rasimu hiyo pia inapatikana katika tovuti ya Tume (www.katiba.go.tz) na kutolewa bure katika Ofisi za Tume zilizopo Dar es Salaam na Zanzibar.

Aidha, Tume hiyo imesema iliandaa Rasimu ya Katiba katika lugha ya Kiswahili ili kuwawezesha wananchi ambao wengi wao wanajua kusoma na kuandika kwa lugha ya Kiswahili kuelewa maudhui ya Rasimu hiyo.

Katika taarifa yake, Tume imewataka wadau wote wanaotaka kutafsiri Rasimu ya Katiba iliyotolewa na Tume kuwasiliana na Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambayo ina Wataalamu wa Uandishi wa Sheria (Legislative Drafters).

* HAKUNA HILA KWENYE MAREKEBISHO YA KATIBA- TENGA

$
0
0
Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Leodegar Tenga amesema hakuna hila yoyote katika marekebisho ya Katiba kwa vile yametokana na maagizo ya Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu (FIFA).

Akizungumza na Wahariri wa Michezo kwenye ofisi za TFF, Dar es Salaam leo (Julai 9 mwaka huu), Rais Tenga amewahakikishia wajumbe wa Mkutano Mkuu wa Dharura kuwa dhamira ya marekebisho hayo ni nzuri, kwani lengo ni kila mtu apate haki yake.

Amesema Mkutano huo utakaofanyika Jumamosi (Julai 13 mwaka huu) utakuwa na ajenda moja tu ya kuingiza Kamati ya Maadili, na Kamati ya Rufani ya Maadili katika Katiba ya TFF kama ilivyoelekezwa na FIFA ili baadaye uanze mchakato wa uchaguzi.

“Katika kuunda Kamati ya Maadili tumeangalia ile ile ya FIFA, tusitengeneze kitu kipya, yaondolewe yale yanayotakiwa kuondolewa, na yaongezwe yale yanayotakiwa kuongozwa. Kwa sababu tumeangalia mazingira kwa Tanzania ni tofauti na Ujerumani au nchi za sehemu zingine,” amesema.

Rais Tenga amewataka wajumbe wafike kwenye Mkutano wakiwa na mtazamo wa kujenga, kwani kuna maagizo ya FIFA ambayo wanatakiwa kuyatekeleza ili wasonge mbele.

“Tutawaeleza kwanini hili limewekwa na lile limeondolewa. Mpira unataka unit (kitu kimoja), ni mchezo wa kila mtu. Baada ya hapa tunaanzisha mchakato wa uchaguzi. Watu wanaingia wakiwa wamoja, wanatoa hoja wanasikilizwa. 

Wanahukumiwa kwa hoja,” amesema na kuongeza utatolewa muda wa kutosha wajumbe ili wayaone na kuelewa marekebisho hayo.

Rais Tenga pia alizungumzia kipindi hiki cha usajili na kutaka klabu ziwaachie wataalamu wa mpira wa miguu kwani ndiyo wanaojua upungufu wa timu, hivyo wanaweza kusajili wachezaji sahihi.

Amesema tatizo kubwa la klabu za Tanzania ni kuwa timu zao hazina uwezo wa kuhimili dakika 90, hivyo watu wanapaswa pia kuzungumzia aina ya mazoezi ambayo timu zao zinafanya badala ya kubakia kutaja tu majina ya wachezaji wanaotaka kusajiliwa.

*KUWAONA TAIFA STARS v/s UGANDA JULAI 13 NI SH. 5000 TU

$
0
0
Kiingilio cha chini katika mechi ya mchujo ya Kombe la Afrika kwa Wachezaji wa Ligi za Ndani (CHAN) kati ya Tanzania (Taifa Stars) na Uganda (The Cranes) itakayochezwa Jumamosi (Julai 13 mwaka huu) kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam ni sh. 5,000 kwa viti vya rangi ya kijani.

Viti vya kijani katika uwanja huo wenye uwezo wa kuchukua watazamaji 60,000 viko 19,648. Kwa upande wa viti vya rangi ya bluu ambavyo viko 17,045 kiingilio ni sh. 7,000. Kiingilio kwa viti vya rangi ya chungwa ambavyo viko 11,897 ni sh. 10,000.

Viingilio vya daraja la juu ni kama ifuatavyo; VIP C yenye watazamaji 4,060 ni sh. 15,000 wakati sh. 20,000 ni kwa VIP B yenye watazamaji 4,160. VIP A yenye watazamaji 748 kiingilio chake ni sh. 30,000.

Mechi hiyo ya kwanza ya raundi ya mwisho kuwania tiketi ya kucheza fainali hizo zitakazofanyika mwakani nchini Afrika itachezeshwa na mwamuzi Thierry Nkurunziza kutoka Burundi. Mechi ya marudiano itachezwa jijini Kampala kati ya Julai 26 na 28 mwaka huu.

Tiketi kwa ajili ya mechi hiyo itakayoanza saa 9 kamili alasiri zitaanza kuuzwa siku moja kabla ya mchezo (Ijumaa) katika vituo vifuatavyo; Shule ya Sekondari Benjamin Mkapa, Sokoni Kariakoo, mgahawa wa Steers ulioko mtaa wa Ohio/Samora, Oilcom Ubungo, Kituo cha Mafuta Buguruni, Dar Live Mbagala na BMM Barbershop iliyoko Sinza Madukani.

Katika vituo hivyo tiketi zitauzwa katika magari maalumu. Magari hayo pia yatafanya mauzo ya tiketi uwanjani siku ya mechi.

Tunapenda kuwakumbusha watazamaji kutonunua tiketi mikononi mwa watu au katika maeneo yasiyohusika ili kuepuka kununua tiketi bandia, hivyo kukosa fursa ya kushuhudia mechi hiyo.

*RAIS KIKWETE AAGANA NA MABALOZI WAPYA LEO IKULU, DAR ES SALAAM

$
0
0
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akizungumza na mabalozi saba walioteuliwa hivi karibuni na kuagana nao kabla hawajaripoti kwenye vituo vyao katika nchi mbali mbali leo Ikulu jijini Dar es salaam. 
Mabalozi hao toka kushoto ni Mhe Modest Melo anayekwenda Umoja wa Mataifa, The Hague, Geneva, Mhe Mabrouk n. Mabrouk (Abu Dhabi – Umoja wa Falme za Kiarabu – UAE), Luteni Jenerali Mstaafu Abdulrahman Shimbo (Beijing, China), Mhe Anthony Cheche (Kinshasa - Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo – DRC), Mhe Chabaka Kilumanga (Visiwa vya Comoro), Mhe Wilson Masilingi (The Hague, Uholanzi) na Mhe Liberata Mulamula (Washington DC, Marekani).  PICHA NA IKULU

*TANZANIA FIRST & ONLY WEDDING TRADE FAIR & FASHION SHOW

$
0
0
Haika Lawere of Mbezi Garden hotel and catering as an Exhibitor
A fashion Must! photo opp at the Haruis Fashion Show!
Celebrity TV personality Deogratius Kithama, hosting the event.  
Models in a gown by designer An Nisaa Abayas 
Model wearing a wedding gown by Sintah Bridal Lounge  
Model wearing a suit from BRAND HOUSE.
Cakes by Cake Shop in display at the Harusi Fashion Show 
Famous Singer Christian Bella, is he Marrying soon? 
Baileys Brand Manager Azda Amani making a welcome note 
Designer Manju Msitta with his collection!
Designer Asia Idarous with two models in her designs!
Model wearing a gown by TWAIBA CLASSIC WEAR
Guest at the Harusi Fashion Show admiring products by Gogo Shop
Guest posing for the photographer at the Harusi Fashion Show
A lucky winner Daniella winning a Baileys Hamper
Model in a wedding gown by wedding Kingdom boutique!
Model in a Mustafa Hassanali Gown
361 DEGREES, EVENTLITES, CENTURY CINEMAX, PRIME ADVERTISING, CLOUDS FM , CLOUDS TV 

*MWEZI UMEANDAMA WAUNGWANA, RAMADHAN KAREEM

$
0
0
Mtandao wa Sufianimafoto, unawatakia mfungo mwema Waislam wote kokote Duniani, baada ya kuonekana muandamo wa mwezi mtukufu wa Ramadhani ambao ni kiashirio tosha cha kuwaongoza waumini wa dini ya Kiislam kuanza rasmi kufunga mwezi mtukufu wa ramadhan kuanzia kesho. Ramadhan Kareem.

*NHC YAMPIGA TAFU MISS TANZANIA 2012 KUJENGA BWENI LA ALBINO BUHANGIJA

$
0
0
Miss Tanzania 2012, Brigitte Alfred (kulia) akipokea hundi yenye thamani ya shilingi Milioni 4.1 kutoka kwa Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano na Huduma kwa Jamii wa Shirika la Nyumba la Taifa (NHC), Susan Omari jijini Dar es Salaam jana. Fedha hizo ni kwaajili ya ujenzi wa Bweni la wanafunzi wenye ulemavu wa ngozi (Albino) linalojengwa katika shule ya Msingi Buhangija mkoani Shinyanga. Fedha hizo ni maalum kwaajili ya kununulia mabati ya kuezekea bweni hilo.  Kwa mujibu wa Brigitte zaidi ya Shilingi milioni 60 zinahitajika kukamilisha ujenzi huo.
Viewing all 13053 articles
Browse latest View live


<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>