Timu ya Harambee Stars imejikatia tiketi ya kucheza fainali za michuano ya Chalenji na Sudan, baada ya kuiondosha Kilimanjaro Stars kwa bao 1-0 lililofungwa katika dakika ya tano kipindi cha kwanza bao lililodumu hadi mwisho wa mchezo.
Sudan nao wametinga fainali hizo baada ya kuichapa zambia mabao 2-1, ambapo sasa kwa mara nyingine tena Kilimanjaro Stars itakutana na Zambia katika mchezo wa kuwania nafasi ya mshindi wa tatu.