Masoud Kipanya, Mkurugenzi Mtendaji wa Maisha Plus, akizungumza na wananchi waliofika kushuhudia uzinduzi wa Maisha Plus/Mama Shujaa wa Chakula 2013 Kingolwira Morogoro , pia kumkaribisha Mgeni rasmi Mkuu wa Wilaya ya Mvomero Mh. Anthony Mtaka kufanya uzinduzi huo.![]()
Mkuu wa Wilaya ya Mvomero Mh. Anthony Mtaka, Akizungumza na wakazi wa eneo la Kingolwira pamoja na wageni na kutoa tamko rasmi la kuzindua shindano la Maisha Plus/ Mama shujaa wa chakula 2013.
Mshindi wa Shindano la Maisha Plus, Bernick Kimiro, akizungumza na wageni waalikwa pamoja na wenyeji wa eneo la Kingolwira Morogoro, kwa kuwasisitiza vijana wajitokeze kuchukua fomu za ushiriki katika shindano la Maisha Plus/ Mama Shujaa wa Chakula 2013 ambazo sasa zimeanza kutolewa na kuwaeleza kuwa shindano hilo linatoa Fursa nyingi za kimaendeleo na kilimo kwa ujumla.![]()
Bwana Bonda ambaye ni mmoja wa wakurugenzi Maisha Plus.
Mgeni Rasmi katika uzinduzi wa Maisha Plus/ Mama shujaa wa Chakula 2013 Mkuu wa Wilaya ya Mvomero Mh. Anthony Mtaka akifanya uzinduzi wa aina yake wa Maisha Plus/ Mama Shujaa wa Chakula 2012/13 kwa kufukua fomu ambazo zilikuwa zimefukiwa ikiwa ni kielelezo cha kilimo kwanza.
Mgeni Rasmi Mkuu wa Wilaya ya Mvomero Mh. Anthony Mtaka akimkabidhi Fomu ya kwanza ya ushiriki kwa Bi. Nuru Saidi Mbonga kutoka Dakawa ikiwa ni fomu ya Mama shujaa wa Chakula 2013
Mheshimiwa Mkuu wa Wilaya ya Mvomero Mh. Anthony Mtaka Akimkabidhi fomu ya Ushiriki wa Maisha plus kwa vijana Bi. Shamimu Ramadhani
Mmoja ya Vijana wakiume nae akiwa anakabidhiwa fomu ya ushiriki na Mgeni rasmi Mkuu wa Wilaya ya Mvomero Mh. Anthony Mtaka
Wakiwa wanasoma fomu na kujiandaa kuzijaza
Burudani za Ngoma zikiendelea
Burudani za aina yake zikiendelea
Wazee kutoka eneo la Kingolwira wakiwa wamekuja kushuhudia uzinduzi huo
Wadau kutoka Sehemu mbalimbali wakiwa wamekuja shuhudia uzinduzi huo
Mkurugenzi Mtendaji wa Maisha Plus Ali Masoud 'Kipanya' akifunga sherehe fupi za uzinduzi wa Maisha Plus 2013.