Wachezaji wa Simba na baadhi ya viongozi wao wakipozi na kombe lao kwa furaha baada ya kukabidhiwa kombe hilo kwa kuifunga Yanga katika mchezo wa Nani Mtani Jembe, uliochezwa kwenye uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam. Katika mchezo huo Simba wameibuka washindi kwa.kuichapa Yanga mabao 3-1, mabao ya Simba yalifungwa na Hamis Tambwe katika dakika ya 14 na 44 na Awadhi Juma, katika dakika ya 62, huku bao pekee la kufutia machozi la Yanga likifungwa na Emmanuel Okwi katika dakika ya 88.
Meneja wa Yanga, Afidh Ally akipokea mfano wa hundi ya zaidi sh. 98 milioni Kwa kuibuka washindi katika shindano la Nani Mtani Jembe kwa kupata kura nyingi katika unywaji wa bia ya Kilimanjaro.
Kiongozi wa Simba Hans Pope, akimpongeza Henry Joseph, baada ya mchezo huo. Kaa na ukurasa huu kwa matukio zaidi ya mchezo huu yatakayokujia hapo baadaye.