Quantcast
Channel: SUFIANIMAFOTO
Viewing all articles
Browse latest Browse all 13053

*BAADA YA KUPEWA TUZO YA BONDIA BORA WA 2013-014 KING CLASS MAWE SASA KUZICHAPA NA CHEKA FEB 8 PTA

$
0
0
BONDIA bora wa mwaka 2013,2014 katika uzito wa  KG 63  Ibrahimu Class 'King Class Mawe' amesaini mkataba wa kupambana na Cosmas Cheka Feb 8 mwaka huu katika ukumbi wa PTA Sabasaba Dar es salaam.

Mara baada ya kusaini mkataba huo wa kucheza raundi 10 za ubingwa waTaifa kg,60 amesema atafanya mazoezi ya kutosha kuhakikisha ana msambalatisha mpinzani wake raundi za awali kwa kuwa alikuwa anachonga sana juu yake.

Mpambano huo uliodhaminiwa na Promota Maarufu nchini Jay Msangi utakuwa na msisimko wa aina yake kutokana na mabondia hawo kuwa gumzo katika ulimwengu wa masumbwi ndani na nje ya nchi ya Tanzania.

King Class aliongeza kwa kusema kuwa nipo fiti nimejiandaa na ninasubili tu kuvishwa ubingwa huo wa taifa kwani Cheka ana ujanja kwangu mbinu zake zote nimesha zikamata.

King Class Mawe anae nolewa na jopo la makocha wanao ongozwa na Habibu Kinyogoli 'Masta' Rajabu Mhamila 'Super D' Kondo Nasoro.
Bondio huyo amewashukulu wadau wa mchezo wa ngumi kwa kumuwezesha kuchaguliwa kuwa bondia bora wa mwaka katika uzito wake kwa kuwapita mabondia wengine wanne na yeye kuibuka kidedea katika kin'yan'gan'yiro hicho.

Viewing all articles
Browse latest Browse all 13053

Trending Articles