Quantcast
Channel: SUFIANIMAFOTO
Viewing all articles
Browse latest Browse all 13053

*RAMADHAN SINGANO 'MESSI' KUWAKOSA JKT RUVU JUMAPILI

$
0
0
Mshambuliaji wa Simba, Ramadhan Singano 'Messi' (kushoto) akiwa katika moja ya mchezo wa timu yake.
*************************************
WASHAMBULIAJI wa Simba, Ramadhani Singano ‘Messi’ na Betram Mwombeki watakosa mechi muhimu ya timu yao katika mchezo wa Ligi Kuu ya tanzania Bara dhidi ya JKT Ruvu itakayochezwa  keshokutwa kwenye Uwanja wa Taifa, jijini Dar es Salaam.

Messi atakosa mechi hiyo kwa sababu ya kutumikia kadi tatu za njano alizopewa katika mechi tofauti za Ligi Kuu Tanzania bara huku Mwombeki akiwa ni majeruhi kwa kuumia mguu wa kulia.
 
Akizungumza na Ripota wa Mtandao huu wa www.sufianimafoto.com, Kocha Mkuu wa timu hiyo, Zdravok Logarusic, alisema kuwa nafasi ya Messi itachukuliwa na Ali Badru huku Mwombeki atakuwa nje ya uwanja kwa muda wa siku tano zaidi.
 
“Mwombeki amepewa siku tano kwa ajili ya mapumziko, huku Said Nassor ‘Chollo’ akiwa amejiunga na wachezaji wenzake baada ya kuanza mazoezi mepesi,” alisema.
 
Aidha Zdravok, alisema kuwa kikosi chake kesho kitaingia kambini kwenye Hoteli ya Vinna maeneno ya Mabibo kujiandaa na mchezo huo.
 
“Timu ipo vizuri mpaka sasa na tuna imani ya kufanya vyema katika mechi zetu zilizosalia baada ya kupoteza michezo yetu ya mikoani,” alisema.

Viewing all articles
Browse latest Browse all 13053

Trending Articles



<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>