Wachezaji wa Yanga wakimpongeza Nahodha wao Nadir Haroub 'Canavaro', baada ya kuifungia timu yake bao pekee katika mchezo wa leo dhidi yao na Al-Ahly ya Misri uliomalizika jioni hii kwenye uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam. Canavaro amefunga bao hilo kufuatia mpira wa Kona iliyopigwa na Simon Msuva katika dakika ya 82.
Hongera Nahodha wetu.......
Hili ndilo bao la Canavaro, Kipa wa Al-Ahly akiwa hoi chini baada ya kuchambuliwa......
Kipa wa Al-Ahly akitafakari baada ya kufungwa bao hilo.....
Mashabiki wa Yanga wakishangilia bao hilo...
Uwanja ulijaa kama hivi......
Mashabiki wa Simba waliokuwa wakiishangilia timu ya Al-Ahly wakiendelea na zoezi la kung'oa viti kama kawaida yao.....KWA MATUKIO ZAIDI BOFYA REDA MORE
Mashabiki wa Al-Ahly wakiduwaa baada ya timu yao kufungwa....
Kwa mara ya kwanza leo mashabiki wa Yanga na wa Simba wataka kujaribu kuchanganyikana na hii ni kutokana na mashabiki wa Yanga kuwa wengi zaidi uwanjani, jambo ambalo lilizua mtafaruku baina ya mashabiki hao kabla ya mchezo kuanza ambapo mashabiki wa Simba waliokuwa wakiishangilia Al-Ahly walianza kung'oa viti na kuwarushia wa Yanga.
Mashabiki Orignal wa Al-Ahly wakishangilia timu yao kwa nguvu zote huku wakiwasha mafataki uwanjani hapo.
Ofisa Habari wa TFF, Boniface Wambura, akizuiliwa kuingia uwanjani hapo huku walinzi waliokuwapo eneo hilo wakimueleza kuwa utaratibu umebadilika hivyo hastahili kuingia kwa kutumia geti hilo. Baadaye aliweza kupita na kuingia baada ya mabishano marefu.
Mashabiki wa Yanga wakishangilia
Mmoja wa Wanakamati wa Yanga akizuiliwa kuingia uwanjani, askari wakimtaka kutoka nje
Benchi la Al-Ahly....
Benchi la akiba la Yanga....
Kikosi cha kwanza cha Yanga kilichoanza....
Kikosi cha kwanza cha Al-Ahly kilichoanza.....
Mshambuliaji wa Yanga, Emmanuel Okwi, akimgalagaza beki wa Al-Ahly....
Hamis Kiiza akijaribu kumtoka beki wa Al- Ahly...
Kutokana na mabeki wa Al-Ahly kumhofia zaidi Okwi, mara kadhaa walikuwa wakimkaba wawili wawili na kumchezea rafu kama hivi......
Haruna Niyonzima, akiangushwa....baada ya kumramba chenga beki wa Al-Ahly
Kipa wa Al-Ahly akiruka kuokoa mchomo wa Simon Msuva.....
Mrisho Ngassa, akimramba kanzu beki wa Al-Ahly.....
Simon Msuva, akitengeneza bao la wazi kwa Hamis Kiiza ambaye alikosa.....kutokana na kuchelewa.
Shabiki wa Yanga......
Mashabiki wa Al-AHly....
Emmanuel Okwi, akiwachachafya mabeki wa Al-Ahly..
Mrisho Ngassa akijaribu kuwatoka mabeki.....
Didier Kavumbagu, akiruka na kuukosa mpira wa kichwa.....
Mrisho Ngassa, akimtoka beki wa Al-Ahly....Timu ya Yanga leo imewashangaza waarabu wa Misri timu ya Al Ahly kwa kuwabanjua bao 1-0, lililofungwa Nahodha wa timu hiyo Nadir Haroub 'Canavaro' kwa kichwa katika kipindi cha pili, mpira uliopigwa na Simon Msuva kwa kona.