Katika kusherehekea Siku ya Wanawake Dunia tarehe 8 Machi mwaka huu, kipindi pekee maalum cha Wanawake Tanzania Wanawake Live kilipata nafasi ya kuhudhuria kilele cha maadhimisho hayo katika mikoa ya Mwanza na Mara. Mada kuu katika mijadala ilikuwa kuhusu tafsiri ya mwanamke na mwanaume katika jamii na usawa wa majukumu ya kazi, huku kau7li mbiu ikiwa ni "Chochea Mabadiliko".
Je, unadhani nini kifanyike kuondoa kabisa dhana ya kazi za kike na kazi za kiume na kuleta usawa katika jamii?