Mgombea Ubunge wa Jimbo la Chalinze kwa tiketi ya CCM, Ridhiwani Jakaya Kikwete akiwahutubia wananchi wa kijiji cha Mindukene, Kata ya Talawanda Jimbo la Chalinze katika Mikutano yake ya kampeni kwenye Vijiji vya Mindukene, Msigi na Kisanga Jimbo hilo. Ridhiwani Kikwete ameahidi kuhakikisha vijiji vyote kwenye jimbo hilo vinakuwa na Matrekta ili kuboresha kilimo.
Mgombea Ubunge wa Jimbo la Chalinze kwa tiketi ya CCM, Ridhiwani Jakaya Kikwete akiwasalimiana na wananchi wa kijiji cha Msigi, Kata ya Talawanda Jimbo la Chalinze baada ya kuwahutubia wakati wa mkutano wake wa kampeni jana jioni.
Mgombea Ubunge wa Jimbo la Chalinze kwa tiketi ya CCM, Ridhiwani Jakaya Kikwete akifurahia jambo na Mzee Joseph January wa Kijiji cha Kisanda, Kata ya Talawanda Jimbo la Chalinze. Picha na Othman Michuzi