Quantcast
Channel: SUFIANIMAFOTO
Viewing all articles
Browse latest Browse all 13053

*NHIF KUPELEKA MADAKTARI BINGWA MIKOANI

$
0
0
 Mkurugenzi wa Idara ya Masoko na Utafiti kutoka Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya Bw. Raphael Mwamoto (kushoto) akieleza kwa waandishi wa habari juu ya mpango wa mfuko huo kupeleka huduma za madaktari bingwa mikoani, kwenye mkutano uliofanyika leo katika ukumbi wa Idara ya Habari (MAELEZO)  jijini Dar es Salaam, kulia ni Mkurugenzi Msaidizi Idara ya Habari Bi. Zamaradi Kawawa.
Afisa Mwanadamizi kutoka Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya Bw. Daudi Bunyinyiga akifafanua jambo kwa waandishi wa habari kuhusu mpango wa kupeleka huduma za madaktari bingwa mikoani unaoratibiwa na mfuko huo, wakati wa mkutano na waandishi wa habari uliofanyika leo katika ukumbi wa Idara ya Habari(MAELEZO) Jijini Dar es Salaam.
*************************************
MPANGO WA KUPELEKA MADAKTARI BINGWA MIKOANI

1.0     UTANGULIZI
Pamoja na kutekeleza mpango wa kusogeza huduma karibu na wanachama na  wadau kwa maana ya kufungua ofisi mikoani, Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya umeanzisha mpango wa kupeleka huduma za Madaktari Bingwa mikoani.

Mpango huu unawahusisha Madaktari Bingwa kutoka Hospitali ya Taifa ya Muhimbili na Taasisi ya Mifupa MOI ambao wanafanya kazi katika hospitali za mikoa kwa kushirikiana na madaktari waliopo mikoani.

Madaktari hao ni mabingwa wa magonjwa ya wanawake, magonjwa ya kawaida, upasuaji na mabingwa wa magonjwa ya watoto.

2.0        LENGO LA KUANZISHA MPANGO HUO:
Lengo la kuanzisha mpango huo ni:-

Kuwapeleka Madaktari Bingwa katika mikoa yenye uhaba mkubwa wa      i.        madaktari bingwa na kuwatumia wataalamu hao wachache kitaifa;
    ii.        Kuwapunguzia wananchi gharama za usafiri kufuata huduma za madaktari bingwa katika miji mikubwa;
   iii.        Kurahisisha utaratibu wa kumwona daktari bingwa ambao wanaonwa kwa ahadi maalum;
   iv.        Kuwapa fursa ya kujifunza na kuwajengea uwezo wa kiutendaji madaktari walioko kwenye hospitali za mikoa hiyo.

3.0     GHARAMA ZA UTEKELEZAJI WA MPANGO HUO:
Katika kutekeleza mpango huu hadi sasa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya umeshatumia Shilingi 115,958,900.00 kwa ajili ya ununuzi wa dawa, vifaa tiba na gharama za madaktari bingwa.

4.0     MAFANIKIO YA MPANGO HUO:
Mpango wa kupeleka Madaktari Bingwa mikoani umekuwa na mafanikio makubwa kwa maana ya kuwafikia walengwa ambao wana mahitaji makubwa ya huduma za madaktari hao. Maisha ya watanzania yameokolewa kwa huduma zitolewazo na Madaktari Bingwa unaofadhiliwa na Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya.
Katika awamu ya kwanza ya mpango huo inayolenga kufikia mikoa saba, tayari mikoa ya Lindi, kigoma, Katavi na Rukwa imeshapata huduma hizo za madaktari bingwa. Mikoa iliyosalia ni Mara, Tabora na Pwani ambayo itafikiwa hivi karibuni.

5.0        WAGONJWA WALIOHUDUMIWA:
Takwimu zilizopatikana kutoka katika mikoa minne iliyofikiwa na Madaktari Bingwa hao ni kama ifuatavyo:

SN
MKOA
WAGONJWA WALIOONWA
WALIOFANYIWA OPERESHENI
1
Lindi
258
6
2
Kigoma
754
37
3
Katavi
1276
37
4
Rukwa
1410
18

Jumla
3,698
98

Mpango huu umepokelewa kwa mtizamo chanya na wadau wetu wakiwemo wanachama na wananchi wa mikoa husika kwa kuwa wengi wao hawana uwezo wa kufuata huduma hizo katika hospitali kubwa ambazo nyingi ziko mbali na maeneo wanayoishi.

Mikoa iliyobaki katika awamu ya kwanza ni Pwani, Mara na Tabora, na kwa sasa maandalizi ya awali yanafanyika katika mkoa wa Pwani.
 Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya unatarajia kuwa huduma za madaktari hao zitakuwa zinatolewa katika mikoa hiyo kadiri hali itakavyokuwa inaruhusu.

5.0        CHANGAMOTO ZA MPANGO WA KUPELEKA MADAKTARI BINGWA MIKOANI:
Pamoja na nia njema ya Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya kuwapeleka madaktari Bingwa karibu zaidi ya wananchi wengi wenye mahitaji ya huduma zao, bado zoezi hilo linakabiliwa na changamoto nyingi zikiwemo:

·         Idadi ndogo ya Madaktari Bingwa ikilinganishwa na wananchi wanaohitaji huduma hizo.
·         Uhaba wa vifaa tiba vya kisasa, kama vile vipimo katika hospitali za mikoa ya pembezoni na Uhaba wa vitendea kazi na madawa ili kufanikisha zoezi hili.
Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya unaamini kuwa mpango huu utaokoa maisha ya Watanzania wengi ambao walikwishakata tamaa ya kupata tiba kutokana na gharama kubwa za kufuata matibabu hayo katika hospitali walizopewa rufaa.

Viewing all articles
Browse latest Browse all 13053

Trending Articles