Mfuko wa Maendeleo ya Jamii TASAF umeanza zoezi la kuwashirikisha walengwa wa Mpango wa kunusuru kaya masikini kuibua miradi ya Ujenzi PWP ambayo kwa mujibu wa taratibu walengwa watatumia fursa ya kufanya kazi katika miradi watakayoibua kwenye maeneo yao na kisha kulipwa ujira ambao utasaidia kuwaongezea kipato.Walengwa watafanya kazi hiyo kwa kipindi cha siku 15 katika mwezi na siku 60 kwa mwaka hususani wakati wa kipindi cha hari (kipindi kigumu).Chini ya utaratibu huo asilimia 75 ya fedha zitalipwa kwa walengwa na 25 zitatumika kununua vifaa vitakavyotumika kwenye mradi husika.
Na. 4428 Afisa kutoka TASAF makao makuu Bw. Geodfrey Nyamwihula akisisitiza jambo kwa walengwa wa Mpango wa kunusuru kaya masikini katika shehia ya Bandamaji wilaya ya Kaskazini B Unguja wakati walengwa wa mpango huo walipopewa mafunzo ya namna ya kuibua miradi ya ujenzi PWP ambayo ni moja ya jitihada za serikali kupitia TASAF kuongeza pato la kaya husika .
Na.4434 Baadhi ya walengwa wa Mpango wa kunusuru kaya Masikini wakisikiliza maelezo ya utaratibu wa kuibua miradi ya Ujenzi PWP katika shehia ya Bandamaji ,Unguja , kutoka kwa mwezeshaji wa Mpango huo (hayupo pichani).
Na. 4441 Mwezeshaji wa Mpango wa uibuaji miradi ya Ujenzi Issa Jabri akitoa maelezo ya namna ya kuibua miradi ya ujenzi PWP katika shehia ya Bandamaji wilaya ya Kaskazini B Unguja.
Na.4413 Mmoja wa wawezeshaji wa Mpango wa kuwawezesha walengwa wa mpango wa PSSN katika kuibua miradi ya Ujenzi PWP katika shehia ya Mpapa wilaya ya
Kati Unguja akisikiliza maelezo kutoka kwa walengwa wa mpango huo.
Na.4419 Hapa lazima ieleweke ndivyo anavyoelekea kusema Mwezeshaji wa PWP Rafii Fadhili Hasan alipotoa mafunzo kwa walengwa wa Mpango wa kunusuru kaya maskini katika kuibua miradi ya ujenzi katika shehia ya Bandamaji wilaya ya Kaskazini B.
Na.4486 Mwezeshaji wa PWP katika shehia ya Kipange,huko Unguja Bi. Hidaya Mussa akitoa maelezo ya namna ya kuibua Miradi ya Ujenzi PWP kwa walengwa wa mpango huo .