Mkurugenzi wa Bendi ya Extra Bongo, Ally Choki, akizungumza na waandishi wa habari hivi karibuni.
******************************************
Na Sufianimafoto, Reporter, Dar
MKURUGENZI wa bendi ya Extra Bongo, Ally Choki, ametangaza rasmi kuwatimua kazi wasanii wake watatu walioshiriki onyesho la Usiku wa Mwana Dar es Salaam, lililoandaliwa na Bendi Hasimu wake ya Twanga Pepeta.
Akizungumza na Sufianimafoto kwa njia ya simu, Chocki, alisema kuwa kamwe hawezi kuyumbishwa na wafanyakazi wake mweneye na kuongeza kuwa msimamo wake wa kuwatimua wasanii hao upo pale pale kutokana na wao kujifukuzisha kazi wenyewe kwa kukiuka taratibu na sheria ya bendi hiyo.
Pamoja na kwamba nimefanyanao kazi kwa muda mrefu miongoni mwa hao lakini inabidi waheshimu taratibu na agizo la uongozi.
“Mmoja wao tayari ameleta barua ya kuomba msamaha lakini hiyo bado haisaidii, kwani tayari alishaonyesha dharau kwa kutenda kosa wakati akifahamu kuwa ni kosa na akihisi kukutwa na suala hili’’. Alisema Choki
Wasanii hao walioshiriki Usiku wa Mwana Dar es Salaam uliofanyika katika ukumbi wa Mango Garden Kinondoni, Jumamosi iliyopita, ni Danger Boy, Sabrina na Maria Soloma.
‘’Miongoni mwao yupo mmoja ambaye amekuwa akitangaza kuwa Extra Bongo haina maslahi ya kutosha, na cha kushangaza zaidi yeye ndiye amekuwa wa kwanza kuandika barua ya kuomba msamaha’’. Alisema Choki
Ally Chocky amewataka wasanii na viongozi wa bendi wasitumie kigezo cha kutolipwa mshahara kama fimbo ya kuvunja taratibu na sheria za bendi hiyo.

“Sidhani kama kuna bendi hata moja inayofanya mambo yake kwa asilimia mia moja, ila zote ni sawa tu tunabadilisha mazingira tu, kwani najua hapa hapa Bongo pia zipi baadhi ya bendi ambazo zimeshindwa kabisa kulipa mishahara kwa wafanyakazi wake na badala yake zimekuwa zikifanya kazi na kulipana posho tu, “Ugumu wa bishara ya muziki wa dansi unajulikana, bendi nyingi zinashindwa kujiendesha kwa kipato kinachopatikana ukumbini, hivyo wakati mwingine suala la kuchelewa kwa mishahara halikwepeki, Kwa upande wangu naamini kuwa Tamasha hilo, liliandaliwa rasmi kwa ajili kuzalisha migogoro baina ya wamiliki wa bendi na wasanii ili watu wajizolee wasanii wa bure pale watakapotimuliwa na bendi zao na mimi nifanya hivyo ili wawachukue wasanii wanaowahitaji, kisha nitazalishwa wengine. ’’. alisema Chocki