Timu ya Taifa 'Taifa Stars' jana imekubali kipigo cha mabao 4-2 kutoka kwa wenyeji wao Botswana katika mchezo wa kirafiki wa kujipima nguvu uliopigwa kwenye Uwanja wa Gaborone kabla ya kukutana na Msumbiji, jijini Dar es Salaam.
Mabao ya Stars yalifungwa na Khamis Mcha 'Vialli' na John Bocco 'Adebayor' kwa mkwaji wa penati.